NAIBU WAZIRI KHAMISI ATOA WITO UHAMASISHAJI UHIFADHI WA MAZINGIRA

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis ametoa wito kwa Shirika la Action Aid kusaidia kampeni ya uhamasishaji wa mazingira kupitia mpango wake wa haki ya mazingira na mpango wa green solutions uliobuniwa na vijana.

Ametoa wito huo leo tarehe 27 Mei, 2022 jijini Dar es Salaam wakati akifungua Maadhimisho ya Siku ya Ukombozi wa Afrika yenye mada ya Mabadiliko ya Tabianchi na Haki ya Mazingira”.

Mhe. Khamis alisema haki ya mazingira ni kutengeneza mfumo wa kuhakikisha kuwa binadamu na mifumo ikolojia inatendewa haki kwa njia ambazo zitanapunguza mabadiliko ya tabianchi na changamoto zingine za mazingira.

“Watu wanapaswa kufahamishwa na kushiriki katika kufanya maamuzi kuhusu maliasili zao na zaidi ya hayo, ni lazima wawe na uhakika wa kupata taarifa za mazingira na wanapaswa kufahamishwa vyema haki zao na wajibu wao katika masuala ya mazingira,” alisema.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akifungua akifungua Maadhimisho ya Siku ya Ukombozi wa Afrika yenye mada ya Mabadiliko ya Tabianchi na Haki ya Mazingira” leo tarehe 27, 2022 jiji Dar es Salaam.

Aidha, naibu waziri huyo aliongeza kuwa ili kufikia haki ya mazingira, Tanzania iliunda mfumo wa kisheria unaozingatia haki ya mazingira ambayo inawataka watu wapate hewa safi, maji, ardhi bora na jamii yenye afya salama.

Alifafanua kuwa Sera ya Taifa ya Mazingira ya 2021 inabainisha jukumu la wadau mbalimbali kuhakikisha suala la mazingira linakuwa kipaumbele wakati wa kufanya maamuzi ya utekelezaji wa shughuli za kiuchumi. Aidha, EMA, 2004 ina kipengele kinachowezesha kushughulikia masuala ya Mabadiliko ya Tabianchi, na haki za watu kutafuta haki ya mazingira.

“Kwa mfano, Kifungu cha 172  kinazungumzia haki ya kupata haki ya mazingira, Kifungu cha 178 kinatoa matakwa ya lazima kwamba umma unapaswa kushiriki katika maamuzi ya mazingira na zaidi, kifungu cha 202(e) kinatoa haki kwa mtu binafsi kushtaki kwa maslahi ya mazingira,” alisema.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa mazingira mara baada ya kufungua Maadhimisho ya Siku ya Ukombozi wa Afrika yenye mada ya Mabadiliko ya Tabianchi na Haki ya Mazingira” leo tarehe 27, 2022 jiji Dar es Salaam.
 
 

Hata hivyo, Naibu Waziri Khamis alisema ongezeko la joto katika angahewa  kumesababisha mabadiliko makubwa na ya haraka katika mifumo ya hali ya hewa na ikilojia.

Hivyo alisema madahara ya mabadiliko  yake huathiri maisha ya binadamu na mifumo yetu  ikolojia akitolea mfano Ripoti ya Tatu ya Hali ya Mazingira Nchini imeonyesha kuwa asilimia 61 ya ardhi yetu imeharibika kutokana na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *