LATRA NA WADAU KUJADILI NAULI MWENDOKASI

Serikali kupitia Mamlaka ya uthibi na Usafiri Ardhini LATRA imeandaa mkutano na wadau wa mabasi yaendayo haraka kujadili nauli za mabasi hayo.

Akifuangua mkutano huo Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Charles Msonde Amesema kuwa mkutano huo na wadau ni mkutano muhimu wa majadiliano katika kufikia malengo ya nchi, huku akitoa wito kwa wadau kuwa mabalozi wa dhati kwa kutoa Maoni yenye tija pasipo kutumia mabavu.

Dkt. Charles Msonde

“Kila mmoja aliyefanikiwa kufika hapa ajuwe kuwa kuna watu wengi anaowawakilisha, hivyo kila mmoja wetu ajitahidi kuwawakilisha ipasavyo”, amesema Dkt Msonde.

Aidha Naibu Waziri Dkt Mkonde amesema sekta ya usafiri wa umma ninsekta muhimu inayochangia mapato kwa kiasi kikubwa

Naye Mkurugenzi Mkuu LATRA, Gilliard Ngewe ametoa wito kwa wadau kuendelea kutuma Maoni Yao lakini pia amesisitiza kwa wadau ambao wangependa kuwasilisha maoni yao kwa maandishi wanayo nafasi ya kuyawasilisha katika Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu iliyopo katika Jengo la Mamlaka, Barabara ya Nkrumah kabla ya tarehe 07 Juni, 2022.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *