BIASHARA UNITED KUACHANA NA MPAPI

Joto linazidi kupanda kuelekea mwishoni mwa msimu huu ambao utafikia tamati mwezi juni, wakati huu bado dirisha kubwa la usajili halijafunguliwa rasmi timu mbali mbali za ligi kuu NBC PL zinaendelea kusuka vikosi vyao kuelekea msimu mpya wa 2022/23

Moja ya taarifa kutoka Biashara United ya mara ni kukosekana kwa beki wao tegemezi Mpapi Nasibu katika msimu ujao wa 2022/23

Beki huyo aliyeitumikia Biashara United kwa muda wa miaka 4 sasa ataondoka rasmi katika klabu hiyo ifikapo mwishoni mwa msimu huu.

“Ni kweli nitaondoka Biashara United mwishoni mwa Msimu Baada ya mkataba wangu kuisha na sitoweza kuongeza mkataba mpya kwa sababu tayari tushakubaliana kila kitu na klabu yangu”

alisema Mpapi Nasibu baada ya kutafutwa na Uhondo Tv kuthibitisha kuwa ni kweli ataachana na Biashara United mwishoni mwa Msimu huu pindi mkataba wake utakapotamatika mwezi juni.

Biashara United ipo nafasi ya 15 Katika msimamo wa ligi kuu ya NBC PL ikiwa imekusanya point 24 katika michezo 25 iliyokwisha cheza msimu huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *