AZAM FC KUMENYANA NA COASTAL UNION BILA UWEPO WA AJIBU, DUBE, NADO NA WENGINE

Na, Fabian Patrick Simbagone

Dakika 90 za mchezo wa nusu fainali ya kombe la Azam Sport Federation Cup {ASFC} zinasubiriwa kwa hamu na wapenzi, mashabiki na wafuatiliaji wa soka nchini nje ya mipaka ya Tanzania.

Mchezo huo kati ya Coastal Union na Azam Fc ni mchezo ambao mashabiki wengi wa Azam FC pamoja na timu nzima wameonyesha kuhitaji zaidi matokeokatika mchezo huo hali inayoibua ushindani mkubwa kutoka Coastal Union na timu zote hasipo katika mbio za ubingwa wa NBC PL.

Kuelekea mchezo huo utakaochezwa tarehe 29 /5/ 2022 wako wachezaji wa Azam watakaokosekana katikamchezo huo, huku msafara wa wachezaji 23 wa Azam FC ukiwa umeshandoka kwenda Arusha tayari kuvaana na Coastal Union Jumapili hii.

Kocha wa Azam FC, Abdihamid Moallin amesema; “Wachezaji watakaoukosa mchezo huo ni pamoja na Ibrahim Ajib, Mathias Kigonya, Nicholaus Wadada, Abdul Haji Omar, Khlefin Hamdoun,, Yahya Zayd, Frank Domayo na Emmanuel Kaberege, wote wameachwa Dar kutokana na sababu za kiufundi, wengine ambao wameshindwa kusafiri na timu ni Prince Dube, Ayoub Lyanga na Idd Seleman ‘Nado’ ambao wote wanasumbuliwa na majeraha”.

Kukosekana kwa nyota hao kutaifanya Azam FC kutokuwa salama zaidi katika baadhi ya maeneo. Azam imekuwa haina matokeo mazuri sana katika michezo yao ya hivi karibuni, huku coastal unioni wakiwa hawajapoteza mchezo wowote katika mechi tano zilizopita, wakishinda mechi 4 na sare 1, huku wakifunga mabao 5 na kuruhusu wavu wao kuguswa mara moja tu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *