
Mbunge wa Mbinga Vijijini, Mhe. Benaya Kapinga ameipongeza Serikali ya inayoongozwa kupitia kwa Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa maamuzi ya kumrudisha katika nafasi yake Mkurugenzi wa Shirika la nyumba la Taifa (NHC), Ndg. Nehemia Mchechu kwakuwa amewezesha mafanikio makubwa katika shirika hilo.

Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Mei 26, 2022 wakati akichangia Bajeti ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa mwaka wa fedha 2022/23 iliyowasilishwa Bungeni.