WAZIRI BASHE ASHIRIKI MKUTANO MAALUM WA KAHAWA

WAZIRI wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe, leo tarehe Mei 25  amehudhuria mkutano maalum wa kwanza wa Kahawa wa nchi 25 zinazolima Kahawa barani Afrika.
Mkutano huo unaoendelea jijini Nairobi nchini Kenya utafanyika kwa siku tatu kuanzia Mei 25 hadi Mei 27, 2022.
Aidha Waziri Bashe ameshuhudia utiaji saini wa hati ya makubaliano ya pamoja ya nchi mwanachama (Nairobi Declaration the adaptation of Coffee as a strategic Agricultural Commodity in the AU Agenda 2063).
Kati ya hoja ambazo Waziri Bashe ametoa ni pamoja na namna Afrika inavyoweza kunufaika na zao la Kahawa huku akifafanua kuwa Afrika inatumia Dola 20 kuagiza kilo moja ya kahawa iliyoongezewa thamani kutoka nje ya bara huku ikiuza Kahawa ghafi kwa Dola 4 kwa kilo moja, na kutaka kuwepo kwa mabadiliko yatakayowezesha kilimo cha kahawa kukua na kuongeza ajira.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *