TAKUKURU TEMEKE YAJIPANGA KUFUATLIA MIRADI YA MAENDELEO

NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.

Taasisi ya Kuzui na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Temeke imejipanga kuendelea kuongeza kasi ya ufatiliaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo ili kuziba mianya ya rushwa hasa katika sekta ya ujenzi ambapo serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi.

Akizumgumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu utekelezaji wa majukumu yake kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia January hadi March 2022, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Temeke, Bw. Holle Makungu amesema kuwa wamefanikiwa kufatilia utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa barabara zenye thamani ya zaidi ya bilioni moja.

Bw. Makungu amesema kuwa wamefatilia utekelezaji wa ujenzi wa barabara ya Mvomero, Ngomano na Keko Machungwa zenye gharama ya Tsh. 447,052, 367 ambazo zipo katika Jimbo la Temete.

Amesema wamefatilia ujenzi wa barabara ya Jeshini – Kizuiani yenye gharama ya Tsh. 165, 704, 740, barabara ya Machinjio za Jimbo la Mbagala zenye gharama ya Tsh. 307, 588, 300.

Barabara za Tungi, Mjimwema na Upendoyeye zenye gharama ya Tsh. 467, 752, 466. 40 pamoja na ujenzi wa Bweni katika Shule ya Msingi ya Chekenimwasonga yenye gharama ya Tsh 80,000, 000.

”Baadhi ya miradi iliyofanyiwa ufatiliaji imebainika kuwa na mapungufu ya ucheleweshaji wa utekelezaji, ucheleweshaji wa malipo ya mkandarasi, hivyo tumewashauri watendaji kutekeleza na kukamilisha miradi hiyo kwa wakati ili kufikia lengo lililokusudiwa” amesema Bw. Makungu.

Bw. Makunga amesema kuna jumla ya mashauri 19 yanaendelea kusikilizwa katika Mahakama ya Mkoa wa Temeke, huku akibainisha kuwa wamepokea malalamiko 75 katika ya hayo 49 yanahusu rushwa na 26 malalamiko yasiyohusu rushwa.

Amebainisha kuwa malalamiko 49 yaliyohusu rushwa uchunguzi wake umekamilika, na majalada 10 yamefungwa kwa kukosa ushaidi huku mjalada 30 uchunguzi wake bado unaendelea.

“Ili kuhakikisha elimu ya mapambano dhidi ya rushwa inawafikia watu wengi, tumeendelea kuelimisha jamii kupitia njia mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari, semina, mikutano ya hadhara pamoja na kushiriki maonesho mbalimbali” amesema Bw. Makungu.

Ametoa wito kwa wananch kuwajibika kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya rushwa kwa kuunganisha nguvu kwa pamoja, kuwa mstari wa mbele katika kutoa taarifa ya vitendo vya rushwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *