CCM YAWASILISHA MAONI NA MAPENDEKEZO YA CHAMA KUHUSU MASUALA YANAYOHUSU DEMOKRASIA YA VYAMA VINGI VYA SIASA.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo amewasilisha maoni na mapendekezo ya Chama Cha Mapinduzi kwa Kikosi Kazi Cha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kinachofanyia kazi masuala yanayohusu Demokrasia ya Vyama Vingi vy Siasa leo tarehe 24, Mei 2022 katika ukimbi wa ofisi ndogo ya Bunge jijini Dar es Salaam.

Katika kikao hicho cha kuwakilisha maoni na mapendekezo ya Chama Cha Mapinduzi, Katibu Mkuu Chongolo aliongozana na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Unenezi Ndugu Shaka Hamdu Shaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *