Waziri Bashungwa awakabidhi vitendea kazi Kailima & Dkt. Msonde amuaga Mweli& Mkama

Asila Twaha – TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa amewakabidhi vitendea kazi Naibu Katibu Mkuu – TAMISEMI Ramadhan Kailima na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Elimu Dkt. Charles Msonde.

Makabidhiano hayo yamefanyika leo tarehe 23 Mei 2022 katika Ofisi ya Rais -TAMISEMI yakishuhudiwa na Menejiment ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Ofisi hiyo.

Waziri Bashungwa amewakaribisha viongozi hao na kusema wamekuja kwenye Treni iliyoko kwenye mwendokasi hivyo wanapaswa kudandia na kuendelea na safari.

Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Ramadhan Kailima amesema kuziimarisha Sekretarieti za Mikoa kutasaidia kuimarisha usimamizi wa majukumu ya Halmashauri hivyo ameahidi kusimamia eneo hilo kikamifu ili waweze kufanyaka kazi kwa kufuata miongozo, sheria na taratibu za Serikali.

Naye Naibu Katibu Mkuu Elimu Dkt.Charles Msonde amewataka watumishi wa Ofisi ya Rais Tamisemi kufanyakazi kwa ushirikiano ilikuleta matokeo chanya katika Sekta ya Elimu hasa elimumsingi na kuaihidi kuendelea kuimarisha elimu nchini.

“Nimefurahi kuletwa sehemu ambayo viongozi wake wote tunafahamiana na tumefanya kazi kwa muda mrefu kwa umoja huu naamini tutaleta mabadiliko katika sekta ya elimu nchini” amesema Dkt. Msonde

Kwa upande wa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Elimu Gerald Mweli ambaye sasa amehamishiwa Wizara ya Kilimo ameushukuru uongozi wa TAMISEMI na watendaji wake kwa kufanya kazi kwa ushirikiano kwa wakati wote aliokuwepo Ofisi ya Rais – TAMISEMI.

“Mafanikio yoyote yale huletwa kwa ushirikiano ninawashukuru sana viongozi na watendaji wote katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, Maafisa Elimu Mikoa na Halmashauri nchini na niwaombe tuendelee kufanya kazi kwa bidii kwa maendeleo ya nchi” amesema Mweli

Katika Mabadiliko yaliyofanywa hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanAzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alimhamishia Bw. Ramadhan Kailima kuwa Naibu Katibu Mkuu-TAMISEMI kuchukua nafasi ya Dkt.Switbert Mkama ambaye alihamishiwa Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira.

Pia alimteua Dkt. Charles Msonde kuwa Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia (Elimu) kuchukua nafasi ya Gerald Mweli ambaye amehamishiwa Wizara ya Kilimo kuwa Naibu Katibu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *