TAARIFA YA ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA MADINI WA ZIMBABWE HAPA NCHINI.

Leo Mei 23, 2022 Naibu Waziri wa Madini hapa nchini Dkt. Steven Kiruswa atampokea Naibu Waziri wa Madini wa Zimbabwe Mhe. Dkt. Polite Kambamura na ujumbe wake kwa ziara ya siku tano.

Lengo la ziara hiyo ni kujifunza masuala mbalimbali ya usimamizi wa Sekta ya Madini kama utafutaji, uchimbaji, uongezaji thamani na biashara ya madini.

Aidha, ujumbe kutoka Zimbabwe utajifunza kuhusu fursa ya madini yaliyopo Tanzania, mfumo wa usimamizi wa leseni Tanzania na usimamizi wa wachimbaji wadogo.

Pia, watatembelea mtambo wa kusafisha dhahabu wa Mwanza, mgodi wa dhahabu wa GGM, wachimbaji wadogo wa Nyarugusu , na wachimbaji wadogo wa madini ya almasi Shinyanga.

Taarifa zaidi itawasilishwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *