WAZIRI DKT MABULA ASHIRIKI MKUTANO WA MAJIJI KISUMU KENYA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameshiriki mkutano wa tisa wa viongozi wa majiji huko Kusumu nchini Kenya.
 
Mkutano huo uliwakutanisha maelfu ya wadau ulijadili maendeleo ya miji Barani Afrika na ulifunguliwa kwenye mji wa Kisumu, Magharibi mwa Kenya.


Mbali na maelfu ya Wadau, Watalaam na Viongozi wa Miji waliokutana kwenye mkutano huo, viongozi kadhaa wa mataifa ya Afrika, pamoja na wale waliostaafu nao walihudhuria mkutano huo.
 
Aidha, kupitia mkutano huo Waziri wa Ardhi Dkt Angeline Mabula alikabidhiwa Tuzo ya Heshima (Commitment in Fevour of the African Movement of the Territorial Government) kwa niaba ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete iliyotolewa na Taasisi ya United Cities and Local Government of Africa (UCLG Africa).
 
Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa kwenye mkutano huo wa kimataifa maarufu kwa jina la Africities ni kuhusu hali ya miundo mbinu kwenye miji mbalimbali na namna bora ya kuimarisha maisha ya wakazi wa miji hiyo.
 
Mameya wa miji mbalimbali, Mawaziri wa serikali za mitaa walihudhuria mkutano huo na kutafuta suluhu ya changamoto zinazowasumbua wakazi wa miji yao kama vile mipangilio mibaya ya majengo, mitaa pamoja na changamoto za  upatikanaji wa umeme.


Huo ni mkutano wa kwanza kufanyika katika jiji ambalo lina wakazi kati ya Elfu 50 na Laki tano ambapo kwa mujibu wa Sensa ya mwaka 2009 lina watu 409,000.
 
Kauli mbiu ya mkutano huu ni mchango wa miji inavyoweza kuchangia utekelezwaji wa dira ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2030 na Umoja wa Afrika mwaka 2063.
 
Majiji mengine ambao yamewahi kuandaa mkutano huu unaofanyika kila baada ya miaka mitatu tangu1998 jijini Abidjan, umewahi pia kufanyika jijini Johannersburg, Dakar Kule Senegal na Marakesh Nchini Morocco

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *