KUFIKIA DISEMBA 2022 RASIMU YA MITAALA MIPYA NA RASIMU YA MAPITIO YA SERA KUKAMILIKA-PROF MKENDA

Na Mathias Canal

Serikali imesema kuwa ina mpango kabambe wa kukimbiza na kuyafanyia haraka mageuzi ya elimu ambapo kufikia mwezi Disemba 2022 rasimu ya Mitaala mipya pamoja na rasimu ya mapitio ya sera itakuwa imekamilika.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda ameyasema hayo leo tarehe 18 Mei 2022 Ofisini kwake Jijini Dodoma wakati alipokutana na kuzungumza na Mwakilishi Mkazi wa Taasisi ya Umoja wa Mataifa Bw Zlatan Milisic.

Waziri Mkenda amemuhakikishia mgeni wake kuwa serikali ya Tanzania imejipanga vyema na kufikia Mwezi Januari mwaka 2023 inatarajia kuanza mchakato wa kufanya maamuzi baada ya Rasimu hiyo kuwa imekamilika.

Waziri Mkenda ameeleza kuwa Umoja wa Taifa umeandaa mkutano maalumu unaotarajiwa kufanyika mwezi Septemba mwaka huu Mjini New York nchini Marekani kujadili mageuzi makubwa ya elimu Duniani.

Waziri Mkenda ameeleza kuwa Mkutano wa wakuu wa nchi utaanzisha mchakato katika nchi nyingi Duniani lakini wakati zinaanza mageuzi hayo ya elimu tayari Tanzania itakuwa imefikia hatua nzuri za maamuzi hivyo kwenda mbele kwa haraka Zaidi.

Prof Mkenda amesema kuwa mchakato huo wa magezi hayo nchini Tanzania umetokana na maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan aliyotoa wakati akilihutubia Bunge la Tanzania tarehe 22 Aprili 2021 kuhusu mabadiliko ya Mitaala ya elimu na muelekeo mpya katika sekta ya elimu aitakayo.

“Na mimi niwahakikishie tu kuwa Kupitia umoja wa Mataifa ni rahisi kujua nchi zingine zinafanya nini kwenye sekta ya elimu ili kuweza kuboresha sekta yetu” Amekaririwa Prof Mkenda na kuongeza kuwa

Amemuahidi Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda kuendeleza ushirikiano ili kuhakikisha kuwa malengo ya maboresho kwenye elimu yanatimia ili elimu itolewayo iendelee kuwa bora.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *