Na Emmanuel Charles

- Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe ameliomba Bunge kuidhinisha Jumla ya Shilingi Wizara ya Kilimo inaliomba Bunge lako Tukufu liidhinishe jumla ya Shilingi 751,123,280,000
Waziri Bashe ametoa Ombi hilo leo Mei 17, 2022 Bungeni, Dodoma Wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Bajeti Wizara ya Kilimo kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023
- “Wizara inatarajia kukusanya Shilingi 126,117,732,000 kutokana na vyanzo mbalimbali. Kati ya fedha hizo, Shilingi 17,732,000 zitakusanywa kupitia Fungu 43 na Shilingi 126,100,000,000 zitakusanywa kupitia Fungu Na.05. “
- Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2022/2023, Bajeti ya Wizara ya Kilimo imeongezeka kwa mafungu yote matatu kutoka Shilingi 294,162,071,000 hadi Shilingi 751,123,280,000 sawa na ongezeko la asilimia
Amesema Sehemu kubwa ya fedha hizo zimetengwa kwa ajili ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji, miundombinu ya uhifadhi wa mazao, kuimarisha upatikanaji wa masoko ya mazao, kuimarisha utafiti wa kilimo, uzalishaji wa mbegu na utoaji wa ruzuku.

“Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2022/2023, Wizara ya Kilimo inaliomba Bunge lako Tukufu liidhinishe jumla ya Shilingi 751,123,280,000 kupitia Fungu 43, Fungu 05 na
Fungu 24 kama ifuatavyo;
Fedha kwa Fungu 43
” Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2022/2023, Wizara inaomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi 368,561,661,000 kupitia Fungu 43 kwa ajili ya matumizi ya Kawaida na Maendeleo. Kati ya fedha hizo, Shilingi 268,906,114,000 ni kwa ajili ya kutekeleza miradi ya Maendeleo ambapo Shilingi 185,978,709,000 ni fedha za ndani na Shilingi 82,927,405,000 ni fedha za nje. Aidha, Shilingi 99,655,547,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida, ambapo Shilingi 49,403,470,000 ni kwa ajili ya mishahara na Shilingi 50,252,077,000 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo.”
Fedha kwa Fungu 05
Amefafanua kuwa jumla ya Shilingi 366,768,352,000 zinaombwa. Kati ya fedha hizo, Shilingi 361,500,000,000 ni kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya Maendeleo ambapo Shilingi 350,000,000,000 ni fedha za Ndani na Shilingi 11,500,000,000 ni fedha za nje. Aidha, kati ya fedha zinazoombwa, Shilingi 5,268,352,000 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida ambapo Shilingi 3,630,168,000 ni kwa ajili ya Mishahara ya Watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na Shilingi 1,638,184,000 ni kwa ajili ya Matumizi mengineyo.
Fedha kwa Fungu 24
- “Mheshimiwa Spika, jumla ya Shilingi 15,793,267,000 zinaombwa. Kati ya fedha hizo, Shilingi 1,100,000,000 ni kwa ajili kutekeleza Miradi ya Maendeleo ambapo Shilingi:”
550,000,000 ni kwa ajili ya Tume na Shilingi 550,000,000 ni kwa ajili ya COASCO.
Aidha, kati ya fedha zinazoombwa Shilingi 14,693,267,000 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida ambapo Shilingi 5,549,009,000 ni fedha za matumizi mengineyo ya Tume na Shilingi 5,115,312,000 ni kwa ajili ya Mishahara ya Watumishi wa Tume. Aidha, Shilingi 2,380,000,000 ni kwa ajili ya Matumizi mengineyo ya COASCO na Shilingi 1,648,946,000 ni kwa ajili ya mishahara ya COASCO.