PILIPILI KICHAA KUENDELEZWA NCHINI

Na Emmanuel Charles

Wizara ya Kilimo imesema itaendeleza zao la pilipili kichaa ambapo bei yake katika soko la dunia imefikia Dola za Marekani 9,324 kwa tani mwaka 2021/2022. Kutokana na fursa hiyo, Wizara itahamasisha uzalishaji wa zao la pilipili kichaa kutoka tani 7,270 mwaka 2018/2019 hadi tani 7,561 mwaka 2022/2023 kwa kuongeza eneo la uzalishaji kutoka hekta 4,038.9 hadi hekta 4,846.7.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Kilimo Nchini Mhe. Hussein Bashe akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023

Ameeleza kuwa itahamasisha kilimo cha mashamba ya pamoja (block farming) kwa zao la pilipili kichaa kwa kuainisha mashamba na kujenga miundombinu ya kukausha na kuhifadhi katika mashamba hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *