“BASHUNGWA KASIMAMIE WALIOPEWA ZABUNI ZA UNUNUZI WA VIFAA KWA FEDHA ZA UVIKO-19” RAIS SAMIA

Angela Msimbira TABORA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassani amemuagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Mhe. Innocent Bashungwa kusimamia tenda za ununuzi wa vifaa tiba na kazi zingine kupitia fedha za uviko 19.

Akiongea na wananchi wa Uyui Mkoani Tabora leo tarehe 17 Mei, 2022 kwenye ufunguzi wa barabara ya Nyahua –Chanya- Uyui-Tabara; Rais Samia amesema kuna zabuni za ununuzi wa vifaa vya afya bado zinasuasua kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Mhe Samia anafafanua kuwa mwisho wa matumizi ya fedha za UVICO 19 ni mwezi Juni, 2022 hivyo fedha zote zinahitajika kutumiwa kwa wakati ili kukidhi vigezo vya kuoata fedha zaidi, amemuagiza Waziri Bashungwa kuhakikisha zabuni hizo zinafanyiwa kazi kwa wakati ili kazi hizo zikamilike kwa wakati.

“Ucheleweshaji wa zabuni hizo utasababisha fedha nyingi kutotumika kwa wakati na kusababisha ukiukwaji wa malengo ya fedha hizo, suala hilo litapelekea fedha kurudishwa na kukosa fedha nyingine za maendeleo, nakuagiza Waziri wa TAMISEMI kalisimamie hili” amesema Rais. Samia

Kuhusu matumizi ya fedha kwenye Halmashauri Rais Samia ameziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanatumia fedha zinazotolewa na Serikali kwa kazi zilizokusudiwa za kutatua kero za wananchi

Amesema Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi kwenye ngazi ya Halmashauri lengo likiwa ni kutatua kero za wananchi katika Sekta ya Afya, Elimu, Maji hivyo zisimamie na kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa na Serikali.

Aidha ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Uyui kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya elimu ikiwemo ujenzi wa matundu ya vyoo, meza, ujenzi wa maabara, ununuzi wa viti na ujenzi wa nyumba za waalimu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *