SPIKA DKT. TULIA ATOA UFAFANUZI MBELE YA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU WABUNGE WA CHADEMA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Tulia Ackson kama alivyozungumza ndani ya Bunge kwamba yeyote mwenye swali kuhusu Wabunge 19 wa Chadema amuulize yeye

Wabunge hao ambao Chama chao kimetangaza kuwafutia Uanachama na hivyo kukosa sifa ya Kuwa Wabunge, Wamekata rufaa Mahakamani ili kupinga Hukumu hiyo

Spika Dkt. Tulia amesisitiza kuwa bado anasubiri uamuzi wa Mahakama

Amesema, kesi ikishafunguliwa Mahakamani ni jitihada za Mtu kutafuta taarifa na sio kazi ya Mahakama kukuandikia, hivyo alipojulishwa na Wabunge wa waliofukuzwa na CHADEMA kuwa wamefungua kesi Spika amejiridhisha kwa kufuatilia kama kesi namba ngapi na imefunguliwa Mahakama gani.

Hivyo Mhe. Spika Dkt. Tulia, anasubiria maamuzi ya Mahakama kama Mahakama itasema wanachama hao wamepoteza sifa ya kuwa wanachama kwa sababu chama chao kimewakufukuza yeye atakuwa na kazi moja tu ya kutangaza nafasi kuwa wazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *