MAHAKAMA KUU YATOA TAMKO WABUNGE 19 WA CHADEMA

Mahakama Kuu Tanzania leo imesema Wabunge 19 waliovuliwa uanachama na Chadema, wataendelea kufanya shughuli zao za kibunge hadi pale Mahakama itakaposikiliza maombi yao ya zuio la muda kuhusu ubunge wa wao.

Uamuzi huo umetolewa na Jaji John Mgeta baada ya kusikiliza kesi hiyo kwa ajili ya kutoa uamuzi kama Wabunge hao waendelee kuwa Bungeni ama laah, ambapo June 13, 2022 ndio atasikiliza zuio hilo.
Halima Mdee na wenzake wanapinga uamuzi wa kuvuliwa uanachama wa Chadema.

Awali Akizungumza Bungeni mapema leo Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson amesema Suala hilo liko chini ya Mahakama hivyo Wanasubiri uamuzi wa Mahakama kwa kuzingatia misingi ya Katiba

“Bunge haliwezi kuingilia mchakato wa mahakama na badala yake linalazimika kusubiri hadi hapo mahakama itakapotoa uamuzi wake kuhusu jambo hilo”Amesema Spika

“Ninalazimika kutotangaza kwamba nafasi 19 za Wabunge wa Viti maalum wa Chadema hazitabaki wazi mpaka pale mahakama itakapotoa maamuzi, Kama kutakuwa na swali lolote Msemaji wa Mwisho wa jambo hii ni Spika wa Bunge na si yeyote” Spika Dkt. Tulia

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *