HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA MHE. UMMY ALLY MWALIMU (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA YA WIZARA YA AFYA KWA MWAKA 2022/23

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel akisalimiana na wateja waliofika katika Hospitali ya Wilaya ya Makete kwa ajili ya kupata huduma za matibabu.  Machi 1, 2022.

HOTUBA YA WAZIRI WA AFYA MHE. UMMY ALLY

MWALIMU (MB), KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA YA WIZARA YA 

AFYA KWA MWAKA 2022/23 

A.       UTANGULIZI

  1. Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ndani ya Bunge lako Tukufu, ambayo imechambua Bajeti ya Wizara ya Afya,ninaomba kutoa hoja kwamba sasa Bunge lako likubali kupokea na kujadili Taarifa ya utekelezaji wa kazi za Wizara ya Afya kwa mwaka 2021/22 na vipaumbele vya Wizara kwa mwaka 2022/23. Aidha, ninaliomba Bunge lako Tukufu likubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Kawaida pamoja na Miradi ya Maendeleo ya Wizara kwa mwaka 2022/23. 
  • Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kuniwezesha kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu na kuwasilisha Hotuba yangu siku ya leo. Aidha, ninapenda kutumia fursa hii kwa heshima na unyenyekevu mkubwa kumshukuru kwa dhati Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuniamini kwa kuniteua kuwa Waziri wa Afya. Ninamuahidi Mheshimiwa Rais na Watanzania kuwa nitaifanya kazi hii kwa weledi, uaminifu na ubunifu mkubwa ili kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora za Afya. Kipekee nimpongeze Rais Samia kwa uongozi wake imara na pia kwa dhamira yake, maono yake na uthubutu wake ambao umekuwa dira sahihi inayoongoza utendaji wangu katika kuimarisha utoaji wa huduma za Afya nchini. Aidha, ni dhahiri kuwa katika kipindi cha Uongozi wake Watanzania wameshuhudia kasi kubwa ya uimarishaji na utoaji wa huduma bora za afya nchini ikiwa ni pamoja ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya afya katika Halmashauri na Mikoa yote nchini, kuimarisha upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba na huduma za matibabu ya Kibingwa na ubingwa Bobezi katika Hospitali za Rufaa za Mikoa, Kanda na Taifa. Ninamuahidi Mheshimiwa Rais kuwa, Wizara itaendelea kubuni na kutekeleza mikakati mbalimbali ili kuhakikisha huduma za afya nchini zinawafikia watanzania walio wengi na hususan wenye kipato cha chini.
  • Mheshimiwa Spika, ninapenda kutoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha Serikali inatimiza wajibu wake wa kuboresha huduma za afya nchini hususani kwa wananchi wa maeneo ya Vijijini. 
  • Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii pia kumshukuru Mheshimiwa Kassim Majaliwa

Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa utendaji wake mahiri ikiwemo kusimamia vyema utekelezaji wa vipaumbele vya Afya nchini. Aidha, ninampongeza kwa Hotuba yake aliyoiwasilisha kwenye Bunge lako Tukufu tarehe 6 Aprili 2022 ambayo imetoa mwelekeo wa majukumu yatakayotekelezwa na Serikali katika mwaka 2022/23. 

  • Mheshimiwa Spika, ninapenda kukupongeza wewe binafsi kwa kuchaguliwa kwa kishindo kuliongoza Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tunapenda kukuhakikishia kuwa Uongozi na Watumishi wa Sekta ya Afya nchini tutakeleza wajibu wetu wa kutoa huduma za afya kwa kuzingatia Sheria na Kanuni mbalimbali zinazopitishwa na Bunge lako tukufu. Aidha, ninampongeza Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu kwa kuchaguliwa kuwa Naibu

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Vilevile, nitumie fursa hii kuwapongeza Wenyeviti wa Bunge kwa kusimamia vyema mijadala ndani ya Bunge.

  • Mheshimiwa Spika, ninapenda kuwashukuru Mawaziri wenzangu kwa ushirikiano walionipatia ambao umeiwezesha Wizara yangu kuendelea kuimarisha na kuboresha utoaji wa huduma za Afya. Wizara yangu itaendelea kushirikiana nao na kuhakikisha tunatimiza dhamira ya Mheshimiwa Rais ya kuhakikisha kuwa watanzania wana afya bora ili washiriki kikamilifu katika kujenga uchumi wa viwanda, na hivyo kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye uchumi wa kati.
  • Mheshimiwa Spika, kipekee ninapenda kuishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Stanslaus Haroon Nyongo (Mb), na Makamu wake, Aloyce John Kamamba (Mb) kwa ushauri na maelekezo waliyoyatoa katika kuboresha utendaji wa Wizara hususani katika kipindi cha maandalizi ya Bajeti hii. Aidha, ninawashukuru Waheshimiwa Wabunge wote kwa ushirikiano mzuri wanaonipatia ikiwemo kutoa ushauri na maoni mbalimbali yenye lengo la kuboresha huduma za Afya. Ninawaahidi waheshimiwa Wabunge wote kwamba, Wizara yangu itazingatia ushauri wenu na kuendelea kuwapa ushirikiano katika kutekeleza majukumu na kazi zetu za kuwatumikia Wananchi ndani na nje ya Bunge. 
  • Mheshimiwa Spika, napenda kutoa pongezi kwa Mheshimiwa Emmanuel Lekishon Shangai kwa kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro na Mheshimiwa Shamsi Vuai Nahodha aliyeteuliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 
  • Mheshimiwa Spika, naomba kutoa pole kwako, Bunge lako Tukufu, kwa Familia na Wananchi wa Jimbo la Ngorongoro kwa kifo cha Mheshimiwa Wiliam Ole Nasha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro. Aidha, naomba kutoa pole kwa familia na wananchi wa Mkoa wa Rukwa kwa kifo cha Mheshimiwa Irene Alex Ndyamkama aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalam mkoa wa Rukwa. Vilevile, natoa pole kwa Watanzania wote, waliopoteza ndugu, Jamaa na marafiki zao kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na magonjwa, ajali na majanga mbalimbali. Napenda kutumia fursa hii kutoa pole kwa wagonjwa na majeruhi wa ajali waliopo Hospitalini na majumbani. Namuomba Mwenyezi Mungu awaponye haraka ili waweze kuendelea na ujenzi wa Taifa.
  1. Mheshimiwa Spika, baada ya kutoa maelezo ya awali, ninapenda sasa kutoa maelezo kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Afya kwa mwaka 2021/22, Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi pamoja na maombi ya fedha ya kutekeleza vipaumbele vya Wizara kwa mwaka 2022/23.

B. MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2021/22

  1. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza majukumu yake, Wizara imeendelea kuzingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo (2025), Sera ya Afya ya mwaka 2007, Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya 2020-2025, Mpango Mkakati wa Tano wa Sekta ya Afya (Health Sector Strategic Plan (HSSP) V 2021/22 – 2025/26)pamoja na makubaliano ya Kimataifa na kikanda yenye lengo la kuimarisha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi.
  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/22, Wizara yangu kwa kushirikiana na Wizara nyingine, Idara na Taasisi za Serikali, Wakala wa Serikali na Wadau wa Maendeleo ilipanga kutekeleza afua mbalimbali zenye lengo la kuboresha utoaji huduma za afya katika maeneo yafuatayo: –
  2. Kuimarisha huduma za kinga dhidi ya magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza nchini kwa kuboresha upatikanaji wa huduma za chanjo, lishe na afya ya uzazi, mama na mtoto;
  3. Kuimarisha huduma za tiba nchini ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi kulingana na mahitaji halisi katika ngazi zote za utoaji wa huduma za afya nchini;
  4. Kuweka mazingira wezeshi ya ukusanyaji wa damu salama na mazao yake katika mikoa mitano ya Dodoma, Mbeya, Kigoma, Mtwara na Mwanza ili kukidhi mahitaji;
  5. Kuimarisha huduma za matibabu ya Kibingwa na ubingwa Bobezi katika Hospitali ya Taifa

Muhimbili, Taasisi ya Mifupa Muhimbili, Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete, Taasisi ya Saratani Ocean Road, Hospitali ya Benjamini Mkapa kufikia viwango vya Kimataifa ili kukidhi mahitaji ya hapa nchini na kuhudumia wagonjwa kutoka nje ya nchi;

  • Kuimarisha mfumo wa bima ya afya nchini ili kufikia lengo la Serikali la kuwa na bima ya afya

kwa wananchi wote;

  • Kuongeza udahili wa wanafunzi wa kada mbalimbali za afya kwa kuimarisha miundombinu katika vyuo vya afya nchini;
  • Kuimarisha utoaji wa mafunzo ya wataalam bingwa na bobezi katika Sekta ya Afya ikiwa ni pamoja na kutumia utaratibu wa mafunzo ya kibingwa na bobezi wakiwa kazini (Fellowship Training Programme);
  • Kuimarisha huduma za dharura katika Hospitali za Kanda ikiwemo Hospitali ya Benjamini Mkapa ili iweze kumudu ongezeko la mahitaji ya huduma za dharura kutokana na Serikali kuhamishia Makao Makuu ya nchi Dodoma;
  • Kuimarisha mpango wa Taifa wa utayari wa kukabiliana na magonjwa ya mlipuko, ajali na majanga kwa kuboresha huduma za dharura na uokoaji ikiwemo miundombinu na vitendea kazi;
  • Kusimamia ubora, usalama na ufanisi pamoja na kufanya tafiti mbalimbali zinazohusiana na Tiba Asili na Tiba Mbadala Nchini;
  • Kuimarisha utoaji wa huduma za afya kuanzia ngazi ya Afya ya Msingi, hospitali za rufaa ngazi ya Mkoa, Kanda na Taifa kwa kukamilisha ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya kutolea huduma za afya;

Mapato na Matumizi ya Fedha 

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Fungu 52, inalo jukumu la kusimamia upatikanaji na utoaji wa Huduma za Afya nchini. Wizara hukusanya mapato kutokana na Huduma za Tiba zitolewazo na Hospitali zilizo chini yake, tozo za huduma katika Taasisi mbalimbali, ada za Vyuo na uuzaji wa zabuni. 
  1. Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2021/22

Wizara na Taasisi zilizo chini yake ilikadiria kukusanya kiasi cha shilingi 507,218,152,321.00 ambapokati ya fedha hizo, shilingi 81,717,635,624.00 zilitarajiwa kukusanywa kutokana na vyanzo vya ndani vya Makao Makuu ya Wizara na shilingi 92,044,336,376.00 kutoka Hospitali za Rufaa za Mikoa. Aidha, Mashirika yaliyo chini ya Wizara yalikadiriwa kukusanya shilingi 333,456,180,321.00. Hadi kufikia mwezi Machi, 2022, jumla ya shilingi 403,030,966,255.18 zilikuwa zimekusanywa, sawa na asilimia 79 ya lengo. Kati ya fedha hizo kiasi cha shilingi 84,812,539,861.00 kimekusanywa kutoka Makao Makuu ya Wizara, sawa na asilimia 104 ya makadirio, kiasi cha shilingi 48,102,720,587 sawa na asilimia 52 kimekusanywa kutoka Hospitali za Rufaa za Mikoa na kiasi cha shilingi 270,115,705,806.88 sawa na asilimia 81 kimekusanywa kutoka katika Taasisi zilizo chini ya Wizara. 

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/22 Wizara ilipitishiwa na Bunge lako tufuku bajeti ya jumla ya shilingi 1,034,134,295,000.00. Kati ya fedha hizo, kiasi cha shilingi 557,303,059,000.00 ilikuwa kwa ajili ya matumizi ya Kawaida ikijumuisha shilingi 252,523,260,000.00 kwa ajili ya matumizi mengineyo na shilingi 304,779,799,000.00 kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa Wizara na Taasisi zilizo chini yake. Vilevile, Wizara ilipata nyongeza ya bajeti (supplimentary Budget) ya kiasi cha shilingi 263,728,066,998.00 kwa ajili ya kutekeleza Mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO 19.
  1. Mheshimiwa Spika, fedha zilizopitishwa kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ni shilingi 476,830,236,000.00, kati ya fedha hizo shilingi

351,700,000,000.00 ni fedha za ndani na shilingi 125,130,236,000.00 ni fedha za njekutoka kwa Wadau wa Maendeleo wanaochangia Sekta ya Afya.  Aidha, fedha kiasi cha shilingi 263,728,066,998.00 ambazo ziliongezwa kwenye bajeti ya Wizara pia zililenga kutumika kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

  1. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi, 2022, Wizara ilipokea jumla ya shilingi 700,158,699,597.02 sawa na asilimia 68 ya bajeti iliyoidhinishwa ya shilingi 1,034,133,295,000.00 kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu yake.  Fedha zilizopokelewa kwa ajili ya matumizi ya kawaida hadi Machi, 2022 ni shilingi 441,433,858,257.14 sawa na asilimia 79 ya fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida kwa mwaka 2021/22. Kati ya fedha hizo shilingi 212,174,499,103.19 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo, sawa na asilimia 84 na shilingi 229,259,359,153.95 sawa na asilimia 75 ni kwa ajili ya Mishahara ya Watumishi wa Afya. 
  1. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa miradi ya maendeleo kiasi cha shilingi 258,724,841,339.88 sawa na asilimia 54 kimepokelewa. Kati ya fedha hizo, fedha za ndani ni shilingi 241,351,889,683.77 sawa asilimia 69 na fedha za nje ni shilingi

17,372,951,656.11. Vilevile, Wizara imepokea kiasi cha shilingi 230,667,862,267.28 sawa na asilimia 87 ya shilingi 263,728,066,998.00 ya bajeti ya nyongeza (Supplimentary budget) kupitia Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO 19. Aidha, Wizara imepokea shilingi 258,127,631,886.17 nje ya mfumo wa malipo wa Hazina (Exchequer system)kutoka kwa Wadau wa maendeleo kwenda moja kwa moja kutekeleza Miradi Misonge ya afya ikiwemo ugharamiaji wa dawa na vifaa tiba.Vilevile, Wizara ilipokea kiasi cha shilingi 41,195,716,045.96 kutoka Mfuko wa Afya wa Pamoja na kukipeleka moja kwa moja OR – TAMISEMI kwa ajili ya kuimarisha upatikanaji na utoaji wa huduma za afya katika ngazi ya msingi. 

C. UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA WIZARA 

HUDUMA ZA KINGA Chanjo

  1. Mheshimiwa Spika, kwa kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022, Wizara ilihakikisha chanjo na vifaa vya kutolea chanjo vinapatikana kulingana na mahitaji ya Mikoa yote nchini. Lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa watoto 2,061,343 wenye umri wa chini ya mwaka mmoja, wajawazito 2,229,015 na Wasichana 685,580 wenye umri wa miaka 14 ambao ni walengwa wa huduma za chanjo kwa mwaka 2021/22 wanapata huduma za chanjo kwa wakati.
  • Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuratibu upatikanaji wa chanjo mbalimbali kama ifuatavyo: sindano ya kukinga polio (IPV) dozi 612,900 kwa ajili ya kuzuia ugonjwa wa kupooza kwa Watoto; chanjo ya Pentavalent Pneumococcal Conjugate Vacine(PCV) dozi 3,167,400 kwa ajili ya kuwakinga watoto dhidi ya magonjwa ya Nimonia na homa ya uti wa mgongo; chanjo ya Rota dozi 630,000 za kuwakinga watoto dhidi ya ugonjwa wa kuhara; chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi Human Papilloma-virus (HPV) dozi 641,400; chanjo ya Measle and Rubella (MR) dozi 2,500,000 dozi ya surua na rubella ; chanjo ya Bivalent Oral Polio Vaccine (BOPV) dozi 6,000,000 kwa ajili ya kuzuia virusi mbalimbali vinavyosababisha ugonjwa wa kupooza kwa watoto; chanjo ya Tetanus Diphtheria (Td) dozi 2,000,000 kwa ajili ya  kuzuia ugonjwa wa Pepopunda kwa mama wajawazito; chanjo ya Bacillus Calmette-Guerin(BCG) dozi 4,000,000 kwa ajili ya kuwakinga watoto wachanga na ugonjwa wa Kifua; na chanjo ya Pentavalent dozi 4,800,500 kwa ajili ya kuzuia magonjwa ya Dondakoo, Kifaduro, Kupooza, homa ya ini na homa ya uti wa mgongo. Chanjo zilizopokelewa zilisambazwa kwenye mikoa yote kulingana na idadi ya walengwa na uhitaji. 

Hadi kufikia Machi 2022, hali ya utoaji wa chanjo nchini imeendelea kuimarika, ambapo chanjo kwa Watoto wa chini ya umri wa mwaka mmoja kwa chanjo ya Penta kwa ajili ya kuzuia magonjwa ya Dondakoo, Kifaduro, Kupooza, homa ya ini na homa ya uti wa mgongo ambayo hutumika kama kipimo kikuu cha Shirika la Afya Duniani (WHO) cha kupima utoaji wa Chanjo katika nchi ilifikia asilimia 96 kati ya 1,060,726 ya lengo. Chanjo za kukinga ugonjwa wa Polio ya matone (OPV3) ilifikiwa kwa asilimia 79, sindano ya kukinga polio (IPV) kwa asilimia 95, Surua rubella dozi ya 1 asilimia 92, Surua Rubella dozi ya 2 asilimia 78, chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana dozi ya kwanza (HPV 1) asilimia 78 na dozi ya pili (HPV 2) asilimia 61.

  • Mheshimiwa Spika, katika kipindi hiki pia, Wizara iliratibu upatikanaji wa chanjo dhidi ya UVIKO19 ambapo jumla ya dozi 9,845,774 zilipatikana kama ifuatavyo: – aina ya Janssen dozi 1,679,550, Sinopharm dozi 4,066,964, Pfizer dozi 3,722,940 na moderna dozi 376,320. Hadi kufikia mwisho wa mwezi Machi, 2022 dozi 6,375,456 sawa na asilimia 62 zilizopokelewa zilikuwa zimesambazwa mikoani kwa matumizi. Dozi zilizotumika ni 5,547,743.  
  • Mheshimiwa Spika, Takwimu zinaonesha kuwa, tangu ugonjwa huu wa UVIKO-19 uliporipotiwa hapa nchini Machi 2020, hadi kufikia Machi, 2022, jumla ya watu 14,198 wamethibitika kuwa na maambukizi ya UVIKO – 19 na Watu 403 wamepoteza maisha sawa na asilimia 2.8 ya waliougua. Wizara, inaendelea kuratibu utoaji wa chanjo ya UVIKO -19 kupitia vituo vya kutolea huduma za Afya vya umma na binafsi vilivyoidhinishwa hapa nchini. Zoezi la utoaji chanjo hapa nchini lilianza rasmi mwezi Julai, 2021. Hadi kufikia 31 Machi, 2022 jumla ya watu 3,067,877 kati ya watu 30,740,928 ikiwa ni asilimia 10 ya Watanzania wenye umri wa miaka 18 na kuendelea, wamepata chanjo kamili dhidi ya ugonjwa huu. Lengo ni kufika asilimia 70 ya watanzania wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea.

Wizara pia ilifanya mafunzo ya utoaji chanjo za UVIKO-19 kwa wakufunzi ngazi ya Taifa na baadaye kufuatiwa na mafunzo ya utoaji chanjo kwa wasimamizi wa chanjo katika ngazi za Mikoa 26 na Wilaya 184 na watoa huduma wawili kutoka kila kituo kinachotoa chanjo. Wizara iliratibu mikutano mbalimbali ya uhamasishaji ikiwemo mkutano wa kuhamasisha wadau wa chanjo kwa Sekta binafsi, Asasi za Kiraia na Viongozi wa dini. 

  • Mheshimiwa Spika, Wizara iliendelea na kazi ya udhibiti wa magonjwa yanayozuilika kwa chanjo ambapo sampuli 539 za ulemavu wa ghafla ulio tepetepe (AFP), sampuli 24 za ufuatiliaji wa ugonjwa wa polio katika mazingira (Environmental surveillance for polio) na sampuli 1,506 za Wagonjwa waliokuwa na dalili za homa na vipele (FRI) zilichukuliwa na kupelekwa maabara. Majibu ya vipimo vya AFP yalikuwa salama ikithibitisha kuwa hapakuwa na ugonjwa wa Polio nchini. 

Afya na Usafi wa Mazingira

  • Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kusimamia afua za kuimarisha hali ya afya na usafi wa mazingira. Kazi zilizotekelezwa ni pamoja na kuendesha mafunzo kwa Waganga Wakuu, Wahandisi na Maafisa Afya katika ngazi ya Mikoa na Halmashauri kutoka Mikoa 17 ya Tanzania Bara juu ya matumizi ya Mwongozo wa Maji na Usafi wa Mazingira kwenye Vituo vya Kutolea Huduma za Afya yaani “Water, Sanitation and Hygiene in Healthcare Facilities – 2017”.  

Aidha, katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022 Wizara kwa kushirikiana na WHO ilifanya tathmini ya udhibiti wa taka zitokanazo na huduma za Afya katika Mikoa 26 ya Tanzania bara, kazi hii imefanyika kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza ilifanyika mwezi Septemba 2021 ikihusisha Mikoa 13 ambayo ni Kigoma, Tabora, Iringa, Mbeya, Manyara, Arusha, Sumbawanga, Dodoma, Morogoro, Mtwara, Pwani, Mwanza na Shinyanga na Awamu ya pili ilifanyika mwezi Oktoba 2021 katika Mikoa iliyofanyiwa tathmini awamu ya pili ambayo ni Songwe, Njombe, Katavi, Lindi, Tanga, Dar es salaam, Simiyu, Geita, Kilimanjaro, Mara, Singida, Kagera na Ruvuma. Matokeo yalibainisha kuwa katika Vituo vya kutolea huduma za afya asilimia 65 ya vituo vyote vina uelewa wa mfumo wa udhibiti taka hatarishi kwa kutenganisha taka kwa kutumia “3 clour coded bin system”. Aidha, imebainika kuwa katika Hospitali za rufaa za mikoa asilimia 75 zina viteketezi vinavyokubalika na miongozo ya wizara ya afya na asilimia 40 kwa hospitali za wilaya na asilimia 38 kwa vituo vya afya na zahanati. Hivyo Wizara itaendelea kuimarisha Mifumo ya udhibiti wa taka nchini.

  • Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuratibu na kusimamia utekelezaji wa awamu ya pili ya Kampeni ya Taifa ya Usafi wa Mazingira yenye kaulimbiu isemayo “USICHUKULIE POA NYUMBA NI CHOO” yenye lengo la kuhimiza ujenzi na matumizi ya vyoo bora na vifaa vya kunawia mikono vyenye maji tiririka na sabuni katika ngazi ya kaya na Taasisi. Kupitia kampeni hii, idadi ya kaya zenye vyoo bora imeongezeka kutoka asilimia 64 mwaka 2020 hadi kufikia asilimia 72 mwezi Machi, 2022. Vilevile, kaya zenye vifaa vya kunawia mikono vyenye maji tiririka na sabuni zimeongezeka kutoka asilimia 40 Mwaka 2020 kufikia asilimia 41 mwezi Machi, 2022. Nitumie Bunge lako tukufu kuendelea kuwahimiza watanzania kuzingatia kanuni za usafi binafsi na usafi wa mazingira ili kujikinga na magonjwa mbalimbali kwani Kinga ni Bora kuliko Tiba.
  • Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha huduma za Afya ya jamii mipakani, katika kipindi cha mwaka 2021/22, Wizara imetekeleza afua mbalimbali ikiwemo: 

i. Kukamilisha uandaaji wa Mwongozo wa Wasafiri (Travel advisory) Namba 10 ambao umeanza kutekelezwa katika Viwanja vyote vya Ndege,

Bandari zote na Mipakani   ii. Upimaji wa wasafiri umeendelea kufanyika katika mipaka yote nchini, ambapo katika kipindi hiki jumla ya Wasafiri 784,822 wameweza kupimwa hali ya maambukizi ya UVIKO-19

  1. Kufanya Mafunzo ya kuwajengea uwezo wahudumu wa afya ya msingi na Kamati za Ulinzi na Usalama ngazi ya Wilaya, mafunzo hayo yalihusu kujikita zaidi katika kukabiliana na changamoto ya wasafiri wanaotumia njia zisizo rasmi kuingia nchini katika Mikoa ya Pwani, Tanga, Arusha, Rukwa, Kagera na Kigoma. Mafunzo hayo pia yalijikita katika mbinu za kumtambua na utoaji wa taarifa za msafiri mwenye dalili za magojwa na njia za kujikinga ili kuzuia maambukizi wakati wa kumhudumia msafiri huyo. 
  2. Kuongeza vituo vya kupimia UVIKO-19 kutoka kituo 1 hadi vituo 9 ambavyo ni Maabara ya Taifa, hospitali ya Mount Meru (Arusha), Ngorongoro (Arusha), Hospitali Bugando (Mwanza), Hospitali

ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Hospitali ya Kanda ya Mbeya, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Bukoba (Kagera), Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni (Kigoma), Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga. Pia Vituo viwili vitaanza kutoa huduma hivi karibu ambavyo ni Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Musoma (Mara) na Hospitali ya Mji wa Kahama

  • Wizara pia imeendesha mafunzo kwa watalaam 20 wanaofanya kazi mipakani kuhusu namna ya kuingiza taarifa kwenye ramani yaani

(Geographical Information System). 

Huduma za Lishe

  • Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuimarisha lishe na afya ya watoto wachanga na wadogo kwa kuendelea kutekeleza Kampeni ya Kitaifa ya utoaji wa matone ya Vitamini A kwa watoto walio chini ya miaka mitano. Malengo ya kampeni ya mwaka 2021/22 yalikuwa ni kutoa matone ya Vitamin A kwa watoto 8,248,450, kati ya umri wa miezi (6 – 59).  Zoezi hili lilikamilika kwa kuweza kuwafikia walengwa 8,015,463 sawa na asilimia 97.2 ikilinganishwa na asilimia 95 ya mwaka 2020. Vilevile, Wizara imeendelea kuimarisha huduma za matibabu ya utapiamlo mkali kwa watoto kwa kuimarisha upatikanaji wa chakula dawa, upatikanaji wa vifaa vya kufanyia tathmini ya hali ya lishe pamoja na kuboresha miundombinu ya kufanyia matibabu ya utapiamlo mkali kwa watoto. Pia vituo vinavyotoa matibabu ya utapiamlo mkali kwa kulaza vimeongezeka kutoka vituo 365 mwaka 2020 kufikia vituo 385 vya kutolea huduma za afya hadi kufikia Machi, 2022.
  • Mheshimiwa Spika, Wizara imefanya utafiti wa hali ya lishe kwa wanafunzi wa shule za msingi za Serikali nchi nzima, ambapo jumla ya wanafunzi 63,000 kutoka shule 650 wamefanyiwa tathmini ya hali ya lishe na kudodoswa masuala ya ulaji na wanafunzi 21,000 wamepimwa kiasi cha damu. Utafiti huu umefanyika mwezi Agosti na Oktoba, 2021, uchakataji wa takwimu unaendelea. Ni matumaini ya Wizara kuwa matokeo ya utafiti huu yatachangia katika kuboresha hali ya lishe kwa vijana hususani walioko mashuleni.
  • Mheshimiwa Spika, Lishe bora ni muhimu kwa uhai, ukuaji na maendeleo ya binadamu kiakili na kimwili na hivyo kuchangia katika kuongeza tija katika uzalishaji mali kwa kaya na kuimarisha uchumi wa jamii na Taifa kwa ujumla. Katika kuhakikisha hilo linafanikiwa, Wizara imeandaa na kuratibu Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Maziwa ya Mama ambayo yalifanyika mwezi Agosti, 2021 Mkoani Songwe. Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka 2021 ilikuwa ni; “Kulinda unyonyeshaji wa maziwa ya mama ni jukumu letu sote”.  Pia Wizara ilifanya warsha kwa wanahabari Mkoani Dodoma na Iringa mwezi Agosti, 2021 ambapo jumla ya waandishi wa habari 60 (magazeti, radio, luninga, blogs, social media) walijengewa uwezo kuhusu masuala mbalimbali ya Lishe ili kuweza kuibua changamoto za Lishe katika jamii zetu pamoja na kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa Lishe-bora kwa maendeleo ya mtu na Taifa kwa ujumla.
  • Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na wadau wa lishe nchini imefanya maadhimisho ya Siku ya Lishe Kitaifa tarehe 18 – 23 Oktoba, 2021. Uzinduzi na Kilele cha Maadhimisho hayo umefanyika Mkoani Tabora. Aidha, Wizara ilifanya uraghibishi na mafunzo kwa timu za uendeshaji wa huduma za afya za Mikoa na Halmashauri (RHMT na CHMT) pamoja na watoa huduma za Afya kuhusu uanzishwaji wa vitengo vya kuratibu huduma za Lishe kwenye Vituo vya kutolea huduma za Afya katika Mikoa ya Tabora, Manyara na Dodoma, ambapo jumla ya watoa huduma 150 wamejengewa uwezo.

Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto

  • Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma za Afya ya Uzazi, ikiwa ni pamoja huduma kabla ya kujifungua, Wakati wa ujauzito, Wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua. Katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi 2022, kwa upande wa huduma kabla ya ujauzito ambapo Wizara kupitia Bohari ya Dawa (MSD) ilinunua na kusambaza vidonge vya uzazi wa mpango dozi 1,755,349 sawa na asilimia 82 ya lengo, sindano za uzazi wa mpango aina ya depo-provera dozi 2,125,625 sawa na asilimia 93 ya lengo na vipandikizi 206,000 sawa na asilimia 78 ya lengo.  Dawa hizi zilisambazwa katika Halmshauri zote nchini. Katika kipindi hicho, wateja waliotumia njia za uzazi wa mpango walikuwa 4,189,787 ukilinganisha na wateja 4,357,151 wa mwaka 2020. Njia hizo za uzazi wa mpango zilizotolewa katika vituo mbalimbali vya huduma za afya nchini ni pamoja na vipandikizi asilimia 57.1, sindano asilimia 18.5, vidonge asilimia 10.1, kondomu asilimia 5.3, kufunga kizazi mama asilimia 0.4, Kitanzi asilimia 7.2 na njia zingine asilimia 1.4
  • Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya wakati wa ujauzito (Antenatal Care) ambapo inakadiriwa kuwa kila mwaka akinamama wapatao milioni 2.3 hutarajiwa kupata ujauzito nchini Tanzania. Katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi 2022, jumla ya Wanawake wajawazito 1,784,809 walihudhuria Kliniki na kupatiwa huduma za Afya na kati yao, asilimia 99.7 ya akinamama wajawazito walifanya mahudhurio manne au zaidi ikilinganishwa na asilimia 85 mwaka 2020. Hata hivyo changamoto iliyopo ni wanawake wajawazito kuchelewa kuhudhuria klinik wapatapo ujauzito. Takwimu zinaonesha kuwa kati ya wajawazito 1,784,809 ni wajawazito 656,040 sawa na asilimia 37.6 walianza kupata huduma za wajawazito chini ya wiki 12 za mwanzo wa ujauzito, ikilinganishwa na asilimia 36 ya kipindi kama hiki mwaka 2020. Aidha, katika kipindi Julai 2021 hadi Machi 2022, asilimia 99.7 ya akinamama wajawazito walifanya mahudhurio manne au zaidi ikilinganishwa na asilimia 85 mwaka 2020. Ongezeko hili kubwa la matumizi ya huduma za kliniki wakati wa ujauzito limetokana na kubadilika kwa mwongozo wa huduma muhimu wakati wa ujauzito kutoka mahudhurio ya kila baada ya miezi mitatu na kuwa mahudhurio ya kila mwezi (Jumla mahudhurio 8 au zaidi kwa kipindi chote cha ujauzito) pamoja na kuongezeka kwa uhamasishaji juu uhumimu wa wajawazito kuhudhuria kliniki ngazi ya jamii. Nitumie Bunge lako Tukufu kuhimiza wajawazito kuhudhuria kliniki mapema ndani ya wiki 12 za mwanzo wa ujauzito na kukamilisha mahudhurio yote 8 ili kuepuka kupata changamoto mbalimbali zinazoweza kusababisha vifo vyao na vichanga vyao wakati wa kujifungua.
  • Mheshimiwa Spika, kwa upande wa huduma ya afya wakati wa kujifungua, Serikali imeendelea kutoa elimu ya umuhimu wa akina mama wajawazito kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za afya. Katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi 2022, wajawazito 1,398,778walijifungulia katika vituo vya kutolea huduma za afya sawa na asilimia 79.5 ikilinganishwa na wajawazito 890,909 sawa na asilimia 80 ya waliojifungulia kliniki kipindi kama hicho mwaka 2020. Aidha, katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi 2022, wajawazito 1,340,239walihudumiwa na watoa huduma wenye ujuzi, ikilinganishwa na wajawazito 851,040 waliohudhuria kliniki kipindi kama hicho mwaka 2020. Takwimu zinazokusanywa katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini zinaonesha vifo vitokanavyo na uzazi vimeendelea kupungua kutoka vifo 1,640 mwaka 2020 hadi vifo 1,580 mwaka 2021. Takwimu hizi hazijumuishi vifo vinavyotokea kwenye ngazi ya jamii, hata hivyo zinatuonyesha mwenendo wa kupungua vifo vitokanavyo na uzazi. Kupitia tafiti mbalimbali zinazoendelea kufanyika ikiwa ni pamoja na Tanzania Demographic Health Survey (iliyoanza kufanyika Septemba 2021, matokeo ya utafiti huu yanatarajiwa kutoka mwezi Septemba 2022) zitaonesha hali iliyofikiwa katika jitihaza za nchi yetu za kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.
  • Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI   imeratibu ujenzi na ukarabati mkubwa wa vituo vya Afya 304 ili kuviwezesha kutoa huduma kwa wajawazito wanaopata uzazi pingamizi wakati wa kujifungua (CEmONC), huduma ambayo imesaidia kuokoa maisha ya mama na mtoto. Hadi kufikia Machi, 2022 jumla ya vituo vya Afya 250 sawa na asilimia 82.2 vilikuwa vimeanza kutoa huduma kamili ya CEmONC ikiwa ni pamoja na upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni. Wizara inaendelea kuhakikisha vituo vyote vya afya vilivyojengwa ambavyo havijaanza kutoa huduma vinapata watumishi wenye ujuzi hasa Madaktari, watoa dawa za usingizi na wakunga pamoja na vifaa tiba kwa lengo la ykuharakisha kuanza utoaji wa huduma. Vilevile, Wizara kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wametoa mafunzo ya huduma muhimu za dharura kwa matatizo yatokanayo na uzazi na watoto wachanga pamoja na utoaji wa dawa za usingizi na ganzi kwa watoa huduma za afya 598 kutoka Mikoa ya Dodoma, Kigoma, Simiyu, Mtwara, Lindi, Mwanza na Morogoro. 
  • Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuboresha huduma za Watoto wachanga ambapo katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi 2022 jumla ya Vyumba/Wodi za Watoto Wachanga Mahututi (Neonatal Intensive Care Unit – NICU) 30 zimeanzishwa katika hospitali za Halmashauri na hivyo kuwa kuwezesha kuwepo kwa jumla ya NICU 165. Aidha, katika kipindi hicho Wizara imeziwezesha hospitali zote za Rufaa za Mikoa kuwa na NIC. Vilevile maboresho yamefanyika katika NICU ya Hospitali ya Taifa Muhimbili. Wizara pia imeendelea kufanya ufuatiliaji wa watoto wanaozaliwa na ulemavu katika Halmashauri za Ifakara TC, Mlimba DC, Kahama TC, Mbulu DC na Mbeya CC.  Takwimu zilizokusanywa zinaonyesha kuwa jumla ya watoto wenye ulemavu 32,586 walizaliwa katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi 2022, na kati yao Watoto 31,640 sawa na asilimia 97 walizaliwa katika vituo vya kutolea huduma za afya. Kati ya watoto waliozaliwa, 54 walibainika kuwa na ulemavu wa kuzaliwa ambapo 14 walizaliwa wafu na 40 walikuwa hai na walipatiwa rufaa kwa matibabu zaidi ya kitaalamu. Huu ni wastani wa watoto 2 kuzaliwa na ulemavu kwa kila vizazi 1,000. Vilevile, Wizara imeendelea kuhakikisha upatikanaji wa dawa muhimu za kutibu na kuzuia magonjwa kwa Watoto ikiwemo Dawa ya kidonge myeyuko cha

Amoxicillin kwa ajili ya Kichomi kwa Watoto (bacterial pneumonia)dozi 25,646,700 zilinunuliwa na kusambazwa sawa na asilimia 84 ya lengo. Aidha dawa ya zinki na ORS kwa ajili ya kutibu kuharisha zilizofungashwa kwa pamoja dozi 439,760 sawa na asilimia 86.5 ya lengo zilinunuliwa na kusambazwa.

  • Mheshimiwa Spika, Kulingana na takwimu zinazokusanywa kutoka katika vituo vya kutolea huduma zinaonesha kuwa vifo vya Watoto vimeendelea kupungua mwaka hadi mwaka ambapo vifo vya Watoto wachanga vimepungua kutoka vifo 8,190 mwaka 2020 hadi vifo 6,741 mwaka 2021; vifo vya Watoto wa chini ya mwaka mmoja vimepungua kutoka vifo 2,657 mwaka 2020 hadi vifo 1,092 mwaka 2021 na vifo vya Watoto umri chini ya miaka mitano vimepungua kutoka vifo 3,482 mwaka 2020 hadi vifo 1,512 mwaka 2021. Takwimu hizi hazijumuishi vifo vinavyotokea kwenye ngazi ya jamii, hata hivyo zinatuonyesha mwenendo wa kupungua vifo vya Watoto wa umri chini ya miaka mitano nchini. Kupitia tafiti mbalimbali zinazoendelea kufanyika ikiwa ni pamoja Tanzania Demographic Health Survey (iliyoanza kufanyika Septemba 2021, matokeo ya utafiti huu yanatarajiwa kutoka mwezi Septemba 2022) zitaonesha hali iliyofikiwa katika vifo vya watoto.
  • Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022 huduma kwa waliopatwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia na Ukatili Dhidi ya watoto ziliendelea kutolewa ambapo jumla ya wateja 97,479 walitoa taarifa katika vituo vya kutolea huduma za afya, kati yao waliotoa taarifa ndani ya masaa sabini na mbili (72) walikuwa 26,364 sawa na asilimia 27. Ili kupanua wigo wa huduma kwa waliofanyiwa vitendo vya Ukatili wa kijinsia na Ukatili Dhidi ya Watoto, vituo vya kutolea huduma jumuishi kwa waliofanyiwa vitendo vya ukatili vimeendelea kuongezeka ambapo kwa sasa vimefikia 18 kutoka vituo 13 mwaka 2020. Aidha, Watoa huduma wa afya 745 na watoa huduma wa ngazi ya jamii 155 wamejengewa uwezo wa namna ya kutoa huduma za kitabibu na kisaikolojia pamoja na utoaji wa elimu kwenye ngazi ya jamii. Wizara pia iliboresha huduma za kitabibu na kisaikolojia ambapo Mwongozo wa Kuzuia na Kupambana na Vitendo vya Ukatili wa Kijinsia umehuishwa na kuongeza afua ya huduma kwa wanawake na wasichana waliofanyiwa ukeketaji ili kuweza kutoa huduma stahiki kwa wahanga ikiwemo wakati wa kujifungua. Nitoe wito kwa wahanga wa ukatili kwenda katika vituo vya kutolea huduma za afya ndani ya saa 72 baada ya tukio. Aidha, ninawataka watoa huduma za afya kutowanyanyapaa wahanga wa vitendo hivyo bali wawapatie huduma haraka kwa kuzingatia miongozo mbalimbali iliyowekwa.
  • Mheshimiwa Spika, Katika kupambana na changamoto za afya wanazokutana nazo vijana jumla ya Watoa huduma za afya 650 kutoka Mikoa ya Njombe, Dodoma, Morogoro, Kigoma, Tanga, Geita, Singida, Shinyanga, Iringa na Arusha walijengewa uwezo kuhusu kutoa huduma za afya rafiki kwa vijana. Vilevile,  jumla ya Waelimishaji rika 350 kutoka Mikoa ya Iringa, Dodoma, Morogoro, Dar es Salaam, Tanga, Singida, Geita, Kigoma na Rukwa wamejengewa uwezo ili wawe na ujuzi wa stadi za maisha na elimu ya afya. Aidha, jumla ya vijana 397,613 sawa na asilimia 32 ya vijana balehe walipatiwa elimu na matumizi ya njia za kisasa za uzazi wa mpango. Vilevile, ili kupunguza changamoto za afya ambazo vijana wanakumbana nazo, Mwongozo umeandaliwa wa namna ya kuanzisha program za kuwafikia vijana walioko kwenye taasisi za elimu ya juu na kati ili kutoa elimu na huduma za kujikinga na maambukuzi ya Virusi vya UKIMWI, Ukatili wa Kijinsia na elimu ya afya ya uzazi. Kamati za afya ya Mkoa na Wilaya zote za Mkoa wa Rukwa wamefanyiwa uraghibishi wa agenda ya Kitaifa ya kuwekeza katika afya na ustawi wa vijana ili afua zilizoainishwa zianze kutekelezwa.
  • Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha huduma za saratani ya mlango wa kizazi Wizara iliweka malengo ya kufanya uchunguzi wa saratani ya Mlango wa Kizazi kwa wanawake 459,822 sawa na asilimia 12 ya wanawake walio kati ya miaka 30 hadi 50 kwa mwaka. Katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022, jumla ya wanawake 162,773 sawa na asilimia 71 walifanyiwa uchunguzi. Kati ya hao, wanawake 3,847 walipatiwa matibabu ya awali ya saratani ya mlango wa kizazi. Vilevile, jumla ya vituo vya kutolea huduma za saratani ya Mlango wa Kizazi viliongezeka kutoka 794 mwezi Juni, 2021 hadi kufikia vituo 801 mwezi Machi, 2022. Mpango wa Wizara ni kuhakikisha kuwa huduma za kupima saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti zinapatikana kwa urahisi katika ngazi za chini hususani kwenye Zahanati na Vituo vya Afya lengo likiwa ni kupunguza mzigo wa kutiba magonjwa ya saratani na kuwaepusha wananchi na vifo kwani saratani inatibika ikigundulika mapema.

Udhibiti wa VVU/UKIMWI

  • Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuboresha afua mbalimbali ambazo zinahamasisha wananchi kwenda kupima na kutambua hali zao za maambukizi ya VVU/UKIMWI, ili waweze kupatiwa huduma za ushauri, upimaji, matunzo na huduma za dawa kwa haraka pale inapoonekana kuwa wameambukizwa. Hadi kufikia Desemba 2021 Jumla ya wateja 1,519,013 sawa na asilimia 84.6 ya watu 1,795,905 wanaokadiriwa kuishi na virusi vya UKIMWI nchini walikuwa wanatambua hali zao za maambukizi (95 ya kwanza). Kati yao, wateja 1,507,686 sawa na asilimia 99.3 walikuwa wameanza kutumia dawa za kufubaza Virusi vya UKIMWI (95 ya pili). Aidha, hadi sasa asilimia 95.8 ya wateja waliokuwa wanatumia dawa za ARV nchini walikuwa wamefubaza wingi wa virusi vya UKIMWI ambayo ni sawa na chini ya nakala 1,000 (95 ya tatu).
  • Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Machi, 2022 Idadi ya vituo vinavyotoa huduma ya Tiba ya UKIMWI (CTC) vimefikia 6,759 kutoka vituo 5,555 mwaka 2015 na kati ya hivyo CTC kamili ni 3,075 na vituo vya huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto (RCHS) vinavyotoa huduma ya kutoa dawa ya kufubaza Virusi vya UKIMWI vipo 3,684. Aidha, Wizara ilisaini mwongozo wa utekelezaji wa utoaji dawa kinga na kuanza kwa huduma hiyo, ambapo hadi sasa jumla ya walengwa 13,285 walianza huduma hiyo katika Mikoa yote nchini.
  • Mheshimiwa Spika, huduma ya Kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT) zinatolewa katika vituo 6,996 sawa na asilimia 98 kati ya vituo 7,138 vinavyotoa huduma za afya ya uzazi na Mtoto. Aidha, Wizara imeweza kupanua huduma ya upimaji wa pamoja wa VVU na kaswende kwa wajawazito ambapo jumla ya vituo 3,497 kati ya 7,138 sawa na asilimia 49 vinavyotoa huduma za afya ya uzazi na mtoto vimeanza kupima VVU na kaswende kwa kutumia kitepe kimoja, lengo ni vituo vyote viweze kutoa huduma ya upimaji huo. Vilevile, katika kipindi cha 2021/22 wajawazito waliopatiwa huduma za upimaji wa VVU walifikia asilimia 99. Wizara imeendelea kupanua huduma za upimaji wa Watoto wachanga waliozaliwa na akina mama wenye VVU kutoka Idadi ya vituo vinavyotoa huduma hizi kutoka vituo 50 mwaka 2020 hadi vituo 141 mwaka 2021. Upimaji huo hufanyika kwa kutumia vinasaba vya VVU mahali zitolewapo huduma (EID Point of Care). Katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi 2022, jumla ya watoto 54,134 waliozaliwa na akina mama wanaoishi na VVU walipimwa vinasaba vya VVU na kati yao watoto 1,299 sawa na asilimia 2 walikutwa na maambukizi ya VVU na wote waliunganishwa na huduma ya matibabu lengo ni kuzuia kabisa maambukizi ya mama kwenda kwa mtoto. Kwa ujumla maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto yameendelea kuwa asilimia 11 kwa kipindi cha mwaka 2020 hadi 2021. 
  • Mheshimiwa Spika, Wizara imeanzisha afua mpya ya Mama Kinara katika ngazi ya Jamii kwa ajili ya kuwezesha ufuatiliaji wa wajawazito na akina mama wanaonyonyesha ambao wamekwisha thibitika kuwa na maambukizi ya VVU. Kitendea kazi cha “Mama Kinara” kimetengenezwa na jumla ya Mama Kinara 818 na Wakufunzi 40 walipata mafunzo yaliyofanyika katika mikoa ya Morogoro, Pwani, Tanga, Dodoma, Manyara, Arusha, Mwanza, Shinyanga, Geita na Tabora. Hadi sasa jumla ya akinamama 68,028 wanaonyonyesha walio na VVU wamefikiwa kati ya akinamama 73,935. Lengo la hatua hii ni kuhakikisha wanawake wenye maambukizi ya VVU/UKIMWI wananyonyesha Watoto wao ili kuweza kuwafanya wawe na afya bora.

Udhibiti wa Kifua Kikuu na Ukoma

  • Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kusimamia utoaji wa huduma za Kifua Kikuu na Ukoma sanjari na Mpango Mkakati wa Sita wa mapambano dhidi ya Kifua Kikuu na Ukoma. Lengo kuu katika mpango huu ni Kuongeza kasi ya uibuaji wa wagonjwa, kupunguza vifo vitokanavyo na Kifua Kikuu na kutokomeza Ukoma katika Halmashauri zenye wagonjwa wa Ukoma. Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022, Wizara ilipanga kuibua wagonjwa 44,993 ambapo wagonjwa 46,104 waliibuliwa, sawa na asilimia 102. Aidha, hadi kufikia Machi, 2022 asilimia 96 ya wagonjwa waliopatiwa matibabu ya Kifua Kikuu walipona ambapo ni juu ya lengo la Shirika la Afya Duniani (WHO) la kuponyesha asilimia 90 ya wagonjwa wanaoanza matibabu. Mafanikio haya ni matokeo ya ufuatiliaji wa kimkakati wa karibu wa wagonjwa vituoni na ushirikishwaji wa watoa huduma katika ngazi ya jamii na ushiriki mzuri wa Jumuia ya Mwitikio wa Kudhibiti Kifua Kikuu na UKIMWI Tanzania (MKUTA). Vilevile, katika kipindi hicho, jumla ya wagonjwa 275 wa Kifua Kikuu Sugu waligundulika ikilinganishwa na wagonjwa 214 waliogundulikwa katika kipindi cha mwaka 2021. Wagonjwa waliogunduliwa kuwa na Kifua Kikuu Sugu walianzishiwa matibabu kikamilifu.
  • Mheshimiwa Spika, Katika kuimarisha huduma za upimaji wa Kifua Kikuu, Serikali imeongeza mashine za kisasa za GeneXpert zinazopima Kifua Kikuu kwa ufanisi na muda mfupi kutoka 268 mwaka 2020/21 hadi mashine 336mwezi Machi, 2022. Mashine hizo hupima na kutoa majibu ndani ya masaa 2 ikilinganishwa na darubini ambazo hutoa majibu baada ya masaa 48. Pia katika kipindi hiki, Wizara imenunua na kusambaza mashine 179 za ECG kwa ajili ya ufuatiliaji wa wagonjwa wa Kifua Kikuu Sugu. 
  • Mheshimiwa Spika, Wizara imeanzisha huduma mkoba za kliniki tembezi (Mobile vans outreach services) zenye uwezo wa kutoa huduma za uchunguzi na ugunduzi kwa magonjwa ya Kifua Kikuu na magonjwa mengine ya mfumo wa njia ya hewa katika maeneo yenye makundi hatarishi ya ugonjwa wa Kifua Kikuu. Katika kipindi cha kuanzia Julai, 2021 hadi Machi, 2022 jumla ya watu 14,000 walio katika maeneo hayo walichunguzwa na kupimwa Kifua Kikuu. Kati ya waliopimwa 1,076 sawa na asilimia 8 waligundulika kuwa na ugonjwa wa Kifua Kikuu na kuanzishiwa matibabu.
  • Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuboresha njia za uibuaji wa wagonjwa wapya wa Ukoma na utoaji wa tiba kinga kwa makundi hatarishi. Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022 jumla ya Kaya 110 zilifikiwa na kufanyiwa uchunguzi. Katika zoezi hili, wagonjwa wapya wa Ukoma 15 waliibuliwa na kuanzishiwa matibabu. Pia katika kipindi hiki watu 2,131 waliokuwa katika makundi hatarishi walipewa tiba kinga na watu 1,050 waligundulika kuwa na magonjwa mengine ya ngozi walianzishiwa matibabu. Sanjari na utoaji wa huduma za Ukoma, Wizara imeendelea kutoa vifaa tiba kwa  waathirika wa Ukoma kwa kugawa jozi za viatu 1,800 ili kupunguza athari za ulemavu kwa waathirika wa Ukoma. Aidha, Wizara imeendelea kutekeleza tafiti kubwa tatu za Ukoma; (i) Tafiti inayolenga kubainisha maeneo hatarishi ya maambukizi ya Ukoma “Geo Spatial Methods of clustering Leprosy cases”, (ii) Tafiti ya kubaini njia ya ufuasi ya utoaji tiba kinga “PEP4LEP study” na (iii) Tafiti ya kubaini njia bora ya kuanza ufuatiliaji wa mwenendo wa usugu wa dawa za Ukoma

“Antimicrobial resistance study”. 

Udhibiti wa Malaria

  • Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kutekeleza shughuli mbalimbali katika jitihada za kupunguza na kutokomeza ugonjwa wa malaria nchini kama ilivyo ainishwa kwenye Mpango Mkakati wa Malaria wa mwaka 2021-2025. Shughuli zilizotekelezwa kwa kipindi cha Julai hadi Machi 2022 ni pamoja na; Kufuatilia wingi (density), tabia (Behavior), aina (Species) na uwepo wa vimelea vya malaria (sporozoites) kwenye miili ya mbu waenezao malaria katika Halmashauri zenye vituo maalumu (sentinel sites) vinavyotumika katika ufuatiliaji huo. Katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi 2022, ufuatiliaji na usimamizi shirikishi ulifanyika katika Halmashauri 24 zenye vituo maalumu ambavyo ni; Uvinza DC, Kigoma Ujiji, Kasulu DC, Uyui DC, Igunga DC, Sikonge DC, Tanganyika DC, Mlele DC, Muleba DC, Missenyi DC, Ngara DC, Geita DC, Bukombe DC, Bagamoyo DC, Rufiji DC, Mtwara MC, Tandahimba DC, Ruangwa DC, Kilwa DC, Ilala MC, Kinondoni MC, Kilosa DC, Mvomero DC na Ulanga DC. Kazi nyingine zilizotekelezwa ni pamoja na ununuzi wa vifaa vya entomolojia kwa ajili ya kazi ya utegaji wa mbu wapevu kwenye vituo maalumu 32 pamoja na uchunguzi wa kimaabara kwa sampuli kwa njia ya PCR/ELISA ili kuweza kutambua aina ya mbu na uwepo wa vimelea wa malaria katika vituo maalumu 32 kutoka Mikoa yote ya Tanzania bara. 

Aidha,katika kipindi hicho jumla ya vyandarua vyenye dawa ya kuzuia mbu 2,514,276 vimesambazwa katika Mikoa 5 ya Mwanza, Geita, Kigoma, Kagera na Mara kwa lengo la kupambana na maambukizo ya ugonjwa wa malaria.

  • Mheshimiwa Spika, katika kupambana na maambukizo ya ugonjwa wa malaria, Wizara pia imeendelea kutekeleza afua ya upuliziaji dawa ukoko katika kuta za nyumba katika mikoa yenye kiwango kikubwa cha maambukizo ya ugonjwa wa malaria. Katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022, upuliziaji wa dawa umefanyika katika Halmashauri 6 za Kasulu, Kakonko, Kibondo, Biharamulo, Bukombe na Ukerewe ambapo jumla ya nyumba 592,444 zimepuliziwa na wananchi 2,665,998 wamekingwa dhidi ya maambukizi ya malaria katika maeneo hayo. 
  • Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na Serikali ya Uswisi, inatekeleza Mradi wa Kuelekea Utokomezaji wa Malaria (Towards Elimination of Malaria in Tanzania-TEMT) unaotekelezwa kwenye Mikoa 5 na Halmashauri 15 za Tanzania Bara ambayo ni Kilimanjaro (Rombo DC, Same DC na Moshi DC), Dodoma (Kondoa DC, Chamwino DC na Mpwapwa DC), Tanga (Handeni DC, Lushoto DC na Tanga Jiji), Kigoma (Kibondo DC, Kigoma-Ujiji MC na Uvinza) na Ruvuma (Tunduru DC, Nyasa DC na Songea MC). Kazi zilizotekelezwa katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi 2022 ni pamoja na; kutoa mafunzo kwa washiriki 969 katika mkoa wa Tanga ambapo washiriki hao walitoka ngazi ya Mkoa, Halmashauri, Kata na vijiji kuhusu upuliziaji dawa ukoko, ununuzi wa pampu 532 pamoja na viuadudu (lita 342 aina ya Bactivec na lita 147 aina ya Griselesf).
  • Mheshimiwa spika, Katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022 Wizara kupitia Bohari ya Dawa (MSD) ilipokea kutoka kwa Wadau wa Maendeleo Dawa mseto ya kutibu Malaria (ALu) dozi 14,977,710, Vipimo vya haraka vya malaria (mRDT) jumla ya vitepe 20,991,875 na dawa ya sindano ya kutibu Malaria kali (Inj. Artesunate) vichupa 2,356,930. Dawa na vitendanishi hivi vinaendelea kusambazwa katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini kupitia Bohari ya Dawa (MSD), kulingana na mahitaji ya vituo husika. Huduma za uchunguzi wa malaria kwa kutimia vipimo vya haraka na matibabu ya Malaria zinatolewa bila malipo. Nitumie Fursa hii kuwataka watoa huduma za afya nchini kuzingatia Mwongozo wa Serikali wa kutoa huduma bure za uchunguzi na matibabu ya malaria.

Udhibiti wa Magonjwa ya Mlipuko yanayotolewa Taarifa kimataifa

  • Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022 Wizara imeendelea kupambana na maambukizi ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo Kipindupindu, Kimeta, Ebola, UVIKO-19, ambapo jitihada mbalimbali zimeendelea kuchukuliwa ikiwemo kutoa Elimu ya Afya kwa Umma na kuandaa miongozo kuhusu kujikinga na magonjwa. Mafunzo ya Epidemiolojia na Usimamizi wa Maabara kwa ngazi zote za utoaji mafunzo (mafunzo ya awali, ya kati na ya muda mrefu) yanaendelea kutolewa. Jumla ya Wanafunzi 44wa mafunzo ya Shahada ya Uzamili ya Epidemiolojia na Udhibiti wa Magonjwa pamoja na Epidemiolojia na usimamizi wa Maabara wameendelea na mafunzo yao ya darasani na ya vitendo ambapo wameweza kufanya tafiti mbalimbali za magonjwa, kutathmini mifumo mbalimbali ya ufuatiliaji wa magonjwa na matukio yenye athari kiafya, kufanya uchunguzi wa milipuko ya magonjwa (Kimeta na Kipindupindu) pamoja na kusaidia mapambano dhidi ya UVIKO-19.
  • Mheshimiwa Spika,katika kipindi cha kuanzia Julai 2021 hadi Machi 2022, ugonjwa wa kipindupindu uliripotiwa katika Halmashauri za Nkasi, Kigoma Manispaa, Kigoma DC, Tanganyika na Uvinza ambapo jumla ya wagonjwa 390 na vifo 4 viliripotiwa. Aidha ugonjwa wa UVIKO19 umeendelea kuripotiwa hapa Nchini ambapo katika kipindi cha kuanzia Julai hadi Novemba 2021 ugonjwa umeripotiwa kwa wastani wa visa 55 kwa siku na vifo 2 kwa wiki moja. Hali ya ugonjwa iliongezeka katika kipindi cha Disemba 2021 hadi Januari 2022, ambapo viliripotiwa wastani wa visa 121 kwa siku na vifo 7 kwa wiki moja. Hali ya ugonjwa huu iliendelea kupungua kwa wastani wa visa 7 kwa siku na kifo 1 kwa wiki kuanzia mwezi Februari 2022 hadi Mei, 2022 
  • Mheshimiwa Spika, Wizara inaendelea na Ufuatiliaji wa magonjwa ya njia ya hewa yanayofanana na influenza katika vituo maalum (Sentinel sites) vilivyopo katika Mikoa 15 ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara, Manyara, Arusha, Dodoma, Mwanza, Tabora, Rukwa, Mbeya, Ruvuma, Iringa na Kigoma. Vituo vinavyo toa huduma ya upimaji vimeendelea kuongezeka kutoka 9 mwaka 2020 hadi vituo 18 Machi, 2022 Lengo ni kuwa na angalau na kituo kimoja katika kila Mkoa ili kuendelea na ufuatiliaji wa mwenendo wa magonjwa ya njia ya hewa yaliyopo na mapya. 
  • Mheshimiwa Spika, Wizara inakamilisha mfumo wa ki-elekroniki wa ufuatiliaji wa tetesi za Magonjwa na matukio yenye athari za kiafya unaotegemewa kukamilika mwezi Mei, 2022. Pia Madawati ya ufuatiliaji wa tetesi za magonjwa ngazi ya Mkoa yamehuishwa katika Mikoa 6 (Kagera, Dar es

Salaam, Mwanza, Kigoma, Tanga na Arusha) na Watumishi 640 na Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii 800 katika Mikoa ya Mwanza, Kigoma na Dar es Salaam wamepatiwa mafunzo ya ufuatiliaji wa Taarifa za tetesi za Magonjwa na Matukio yenye athari kiafya.

Udhibiti wa Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi

Kipaumbele 

  • Mheshimiwa Spika, katika kupambana na magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ikiwa ni pamoja na Usubi, matende na mabusha, kichocho na trakoma, Wizara imehakikisha kuwa wataalam, dawa, vifaa na vifaa tiba vya  kutosha vinapelekwa katika maeneo ambayo yameonekana yanasumbuliwa zaidi na magonjwa hayo. Wizara kupitia Bohari ya Dawa (MSD) ilisambaza dawa aina ya Ivermectin (Mectizan) vidonge 26,620,500 na Albendazole vidonge 7,817,400 vya kudhibiti na kukinga magonjwa ya Usubi, Matende na Mabusha. Aidha, Wizara ilisambaza dawa aina ya Praziquantel vidonge 7,966,000 kudhibiti na kukinga ugonjwa wa Kichocho; Zithromax vidonge 1,944,500 na Zithromax ya maji, chupa 16,088 kwa ajili ya kudhibiti ugonjwa wa Trakoma katika halmashauri za Ngorongoro, Longido, Kiteto na Simanjiro.
  • Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022, Wizara ilitoa Kingatiba za kutokomeza ugonjwa wa Matende na Mabusha kwa Wananchi wa Wilaya za Kilwa, Pangani Temeke, Ilala na Kinondoni. Wananchi  wengi walijitokeza kumeza kinga  tiba dhidi ya ugonjwa wa matende ikilinganishwa na lengo lililopangwa katika maeneo husika kama ifuatavyo; Kilwa asilimia 80 ya lengo, Pangani asilimia 83. Temeke asilimia 80, Jiji la Dar es Salaam asilimia 70, Kinondoni asilimia 76, Mtwara DC asilimia 79, Mtama asilimia 82 na Mafia asilimia 71.  Jumla ya watu 4,055,719 walimeza kingatiba hiyo ambayo ni sawa na asilimia 77.6 ya walengwa wote. Mafanikio haya yametokana na upatikanaji wa madawa kwa wakati, rasilimali fedha, uhamasishaji na mwitikio mzuri wa Jamii.
  • Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022 jumla ya Wagonjwa 2,473 wa vikope walifanyiwa usawazishaji wa kope katika Mikoa ya Pwani, Mtwara, Lindi, Ruvuma, Singida, Rukwa na Dodoma. Mafanikio haya yametokana na mwitikio chanya wa jamii katika kupokea huduma hii ya usawazishaji wa kope. Aidha ugawaji wa kingatiba ya kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa trakoma ulifanyika katika Halmashauri za Chamwino, Kongwa na Kiteto. Wananchi wengi walijitokeza kumeza dawa hizi kwa asilimia kubwa dhidi ya malengo yaliyokuwa yamewekwa katika maeneo husika kama ifuatavyo; Ngorongoro asilimia 88, Chamwino asilimia 83, Kongwa asilimia 96, na Kiteto asilimia 93. Jumla ya watu 714,273 walimeza Kingatiba hiyo. Vilevile, Wizara iliendelea na shughuli za kudhibiti ugonjwa wa usubi, ambapo ugawaji wa dawa za kingatiba kwa jamii ulifanyika katika Mikoa 7 na Halmashauri 28 ambapo mafanikio dhidi ya malengo yaliyokuwa yamewekwa katika maeneo husika ni kama ifuatavyo; Iringa asilimia 86, Mbeya asilimia 82, Morogoro asilimia 86, Njombe asilimia 85, Ruvuma asilimia 83, Songwe asilimia 84, Tanga asilimia 86. Jumla ya watu 5,730,442 walimeza kingatiba hiyo ambayo ni sawa na asilimia 85 ya walengwa wote.

Elimu ya Afya kwa Umma

  • Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu masuala ya lishe, huduma za mama na mtoto, afya ya mazingira, magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza na namna ya kujikinga na majanga mbalimbali. Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022, Wizara iliandaa na kusambaza vielelezo vya kutoa elimu kwa jamiii kama ifuatavyo; Mabango 693,000, Vipeperushi 500,050 pamoja na kurusha matangazo ya Runinga 12,734 na 21,572 ya Redio.  Aidha Wizara imeratibu Vipindi 618 vya Redio, vya Runinga 308 na kurusha kupitia mitandao ya kijamii vipeperushi 5,690, picha za sauti 286 na kusambaza USB flash 621 zenye ujumbe wa elimu ya afya. 
  • Mheshimiwa Spika, katika kuhamasisha na kushirikisha jamii kuchukua hatua dhidi ya magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza pamoja na kupata uelewa wa masuala mbalimbali ya afya, Wizara ilitoa mafunzo na uelimishaji kwa makundi mbalimbali ya kijamii ambapo Viongozi wa Dini 1,230, Wanahabari na Wahariri wa vyombo vya habari 230, Wazee Mashuhuri 1,560 na Wasanii 45. Mafunzo haya yalilenga kuhamasisha masuala mbalimbali ya kiafya hususan kinga dhidi ya UVIKO-19 na matumizi ya chanjo. Wizara imefanya mafunzo na kampeni ya Mpango Harakishi na Shirikishi wa Kinga dhidi ya UVIKO-19 pamoja na matumizi ya chanjo awamu ya pili. Mafunzo yalihudhuriwa na washiriki 249 kutoka Wizara ya Afya, OR-TAMISEMI, Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu wa Bunge, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Wizara nyingine, Wadau wa maendeleo, Wawakilishi wa viongozi wa Kidini, viongozi wa Serikali za Mitaa na Viongozi wa Kimila.

HUDUMA ZA TIBA

Usimamizi wa Vituo vya kutolea huduma za Afya

  • Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kusimamia upatikanaji wa huduma za afya nchini zinazotolewa kupitia Vituo vya kutolea huduma vya Serikali, binafsi na mashirika ya dini. Katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022, vituo vya kutolea huduma za afya nchini vilivyosajiliwa vimeongezeka kufikia 8,549 ikilinganishwa na vituo 8,458 mwaka 2020. Kati ya hivyo, Hospitali ni 404, Vituo vya Afya 956 and Zahanati 7,189.

Idadi ya vituo vya kutolea huduma za afya vilivyosajiliwa, 2021/22

Aina ya VituoJulai 2020-Juni 2021 Julai 2021 – Machi, 2022 Idadi ya vituo Vilivyo ongezeka (Julai 2021 – Machi, 2022
SerikaliMashirika ya Dini Binafsi  Jumla Serikali   Mashirika      ya Diniu Binafsi   JumlaJumla
Hospitali185117673692071128540435
Vituo vya Afya645124157  92667915012795630
Zahanati5,3956761,0927,1635,4916221,0767,1 8926
Jumla ndogo6,2259171,3168,4586,3778841,288 91

  Chanzo: HFR

  • Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022, Wizara kupitia Bodi ya Usajili wa Hospitali za Watu Binafsi imesajili vituo vya kutolea huduma katika ngazi mbalimbali ambavyo ni;

Hospitali ngazi ya Wilaya 12, Hospitali ngazi ya Mkoa mbili (2), Hospitali za Kibingwa 1, Vituo vya Afya 7, Zahanati 89, Polyclinic 57 na kliniki za kawaida 47. Kwa ujumla vituo vilivyosajiliwa na bodi hadi kufikia Machi 2022 ni 3,198. Aidha, Wizara imetengeneza Mfumo wa Usajili wa Kielektroniki, ambao utatumiwa na wamiliki wa Hospitali Binafsi na Umma kutuma maombi yao ya usajili na kulipia ada mbalimbali kupitia mfumo huu ambao umeunganishwa na Mfumo wa Mfuko Mkuu wa Serikali (GePG). Kwa kufanya hivi, Mfumo huo utarahisisha upatikanaji wa haraka wa huduma ya usajili wa vituo na kupokea malipo mbalimbali ili kupunguza gharama za usafiri badala ya kufuata huduma hii Dodoma na hivyo kuepuka usumbufu usio wa lazima. 

  • Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kutekeleza afua mbalimbali za tiba nchini ambapo katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022 jumla ya Wagonjwa 21,230,469 walipatiwa huduma, ambapo Wagonjwa 20,428,932 ni wa nje na Wagonjwa 801,537 walilazwa. Wagonjwa hao walipatiwa huduma katika Hospitali za ngazi ya Taifa, Kanda, Mikoa, Halmashauri, Vituo vya Afya na Zahanati zote nchini kama ilivyoainishwa katika jedwali hapo chini.

Idadi ya Wagonjwa waliohudhuria katika Vituo vya kutolea huduma za afya kwa kipindi Julai 2020 hadi Machi, 2021.  

AINA YA VITUO Mahudhurio katika Vituo 
 Julai, 2020 hadi Machi, 2021 
OPD  (wagonjwa wa nje)AsilimiaIPD (wagonjwa wa kulazwa)AsilimiaJUMLAAsilimia
Hospital i5,372,49526566,853665,939,34828
Vituo vya Afya4,614,19322275,185324,889,37823
Zahanat i10,297,155500010,297,15548
Kliniki447,894312,4421460,3363
 Jumla20,731,73 7 854,480 21,586,21 7 

 Chanzo: DHIS2

  • Mheshimiwa Spika, kulinganisha na takwimu zilizoainishwa katika jedwali hapo juu, idadi kubwa ya Wagonjwa wa Nje walipatiwa huduma katika ngazi ya Zahanati kwa kipindi cha Julai 2020 hadi Machi 2021 na asilimia kubwa ya Wagonjwa wa kulaza walipata huduma katika Hospitali. Hali hii imejidhihirisha pia katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi 2022 kama ilivyoainishwa katika jedwali hapo chini.

Idadi ya Wagonjwa waliohudhuria katika Vituo vya kutolea huduma za afya kwa kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022.

AINA YA VITUOMahudhurio ya Vituo  
Julai 2021 hadi machi 2022  
OPD (wagonjwa wa Nje)Asilimi aIPD (wagonjwa  wa kulazwa)asilimi aJUMLAAsilimi a
Hospitali8,693,15328.4823,97367.669,517,12630
Vituo vya Afya6,565,69621.5380,02431.206,945,72022
Zahanati14,101,02046.113,3051.0914,114,32 544
Kliniki 1,222,22746000.051,222,8274
 Jumla30,582,096 1,217,902 31,799,99 8 

 Chanzo: DHIS2

Magonjwa yaliyoongoza kuwaathiri wananchi

(Top ten Diseases)

  • Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi 2022, magonjwa yaliyoongoza kwa wagonjwa wa nje (OPD) wenye umri chini ya miaka mitano yalikuwa ni maambukizi katika mfumo wa hewa, Malaria na maambukizi katika njia ya mkojo; na kwa umri wa miaka mitano na zaidi magonjwa yalikuwa ni maambukizi katika mfumo wa hewa, Maambukizi katika njia ya mkojo na Malaria

(Kiambatisho Na.1) 

  • Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi 2022, magonjwa yaliyoongoza kwa wagonjwa wa kulazwa (IPD) kwa wenye umri chini ya miaka mitano yalikuwa ni Kichomi (Severe and nonSevere), Malaria na kuharisha sana (Acute diarhoea), ambapo kwa watu walio na umri wa miaka mitano na zaidi, magonjwa yalioongoza yalikuwa ni Malaria, Kichomi (Severe and non-Severe) na maambukizi katika njia ya mkojo (UTI) (Kiambatisho Na.2). Katika kundi hili la wagonjwa, magonjwa yasiyoambukiza yalikuwa ni moja ya chanzo cha watu kwenda kulazwa katika vituo vya kutolea huduma za afya; hali inayoashiria kukua kwa kiwango cha tatizo la magonjwa ya aina hiyo hapa nchini. 

Upatikanaji wa Dawa, Vifaa, Vifaa Tiba na Vitendanishi

  • Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuhakikisha kuwa upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi katika vituo vya kutolea huduma za afya unakuwa wa kuridhisha. Wizara kupitia Bohari ya Dawa hununua, hutunza na husambaza zaidi ya aina 2,976 za dawa, vifaa tiba na vitendanishi. Kati ya hizo aina 290 zimeainishwa kuwa ni dawa muhimu na za kipaumbele cha Wizara ya Afya kwa lengo la kuhakikisha kuwa zinapatikana nyakati zote katika Bohari ya Dawa (MSD). Aidha hadi sasa, Wizara ya Afya kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imeshapeleka MSD kiasi cha shilingi 129,851,510,000.00 kwa ajili ya ugharamiaji wa mnyororo mzima wa upatikanaji wa dawa. Kupatikana kwa fedha hizi kumewezesha upatikanaji wa aina 290 za dawa, vifaa tiba na vitendanishi muhimu kufikia asilimia 51 katika ngazi ya MSD na asilimia 43 ngazi ya Zahanati, asilimia 42 kwa ngazi ya Vituo vya Afya, asilimia 50 kwa ngazi ya hospitali za Wilaya, asilimia 76 kwa Hospitali za Rufaa za Mikoa na asilimia 51 katika Hospitali za Kanda, Maalum na Taifa. Wizara itaendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha MSD wananunua na kusambaza dawa, vifaa na vifaatiba vyenye ubora na kwa gharama nafuu. Aidha Wizara kwa kushirikiana na OR – TAMISEMI itaendelea kusimamia na kufuatilia kwa karibu upatikanaji wa dawa katika Vituo vya kutolewa huduma za afya vinavyomilikiwa na Serikali.
  • Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha uzalishaji wa bidhaa za afya nchini, MSD imeendelea kusimamia uzalishaji wa barakoa ambapo hadi Machi, 2022 kiwanda cha KEKO Phamaceautical kimezalisha barakoa 1,988,200 zenye thamani ya shilingi 1,361,985,200. Aidha, Ujenzi wa Kiwanda cha Mipira ya kuvaa mikononi (Gloves) umekamilika kwa asilimia 90 na uzalishaji wa majaribio tayari umeanza.  Ujenzi wa kiwanda hicho umeenda sanjari na ujenzi wa nyumba tatu za wafanyakazi ambazo tayari zimekamilika. Vilevile, MSD imenunua mitambo ya kutengeneza na kufungasha dawa rojorojo (ointment and cream) ambayo imekwishawasili nchini, ambapo ujenzi kwa ajili ya kiwanda hicho umeendelea kukamilishwa na baadhi ya malighafi zimekwishawasili nchini na mkandarasi wa kusimika mitambo ya kiwanda tayari amepatikana. Ni matarajio ya Wizara kuwa viwanda hivi vitawezesha upatikanaji wa dawa na bidhaa za afya kwa wakati na kwa gharama nafuu.  

Upatikanaji wa Damu Salama

  • Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Mpango wa Taifa wa Damu Salama ilipanga kukusanya chupa za Damu Salama 375,000 ili kukidhi mahitaji ya Damu Salama nchini katika kipindi cha mwaka mzima wa 2020/21. Hadi kufikia mwezi Machi 2021, Wizara ilifanikiwa kukusanya chupa za damu 252,372 sawa na asilimia 67 ya lengo la mwaka, ikilinganishwa na idadi ya chupa za damu salama 250,933 zilizokusanywa katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2010/21. Damu zote zilizokusanywa zilipimwa makundi ya damu, pamoja na magonjwa makuu manne ambayo ni UKIMWI (HIV), Homa ya ini B na C (HBV & HCV) na Kaswende (Syphilis). Jumla ya chupa za damu 222,444 sawa na asilimia 88 ya chupa zilizokusanywa zilikuwa salama na kusambazwa hospitalini kwa ajili ya matumizi. Wizara imepanga kukusanya jumla ya chupa za damu 550,000 ikiwa ni ongezeko la chupa 175,000 sawa na ongezeko la asilimia 46.  Na katika kuimarisha upatikanaji wa damu salamu, Wizara imeamua kutoa bure mifuko ya kukusanyia damu kwa Halmashauri zote nchini. Hii ni kutokana na kuwa Damu salama ni bidhaa ya afya ambayo haiuzwi au kupatikana katika maduka au benki binafsi isipokuwa Serikalini tu. Hivyo Wizara imeona ni vyema kuondoa vikwazo vilivyopo vya upatikanaji wa damu salama ili kuokoa Maisha. Kutokana na uamuzi huu wa Wizara wa kugawa bure mifuko ya damu, Halmashauri na Mikoa sasa watawajibika kugharamia shughuli za kuelimisha na kuhamasisha wananchi kuchagia damu pamoja na kuandaa kampeni za kuchangia damu katika maeneo yao.

Aidha katika kipindi hicho Jumla ya chupa za Damu Salama 27,616 sawa na asilimia 11 ya chupa zote zilizokusanywa zilitengenezwa mazao ya damu, ambapo jumla ya mazao 48,079 (Chembe sahani 4,887, Plasma mgando ni 15,566 na Chembe hai nyekundu ni 27,626). yalitengenezwa 

  • Mheshimiwa Spika Wizara imeendelea kuhakikisha huduma za damu salama zinaimarika na kusogea karibu na wananchi kupitia ujenzi unaoendelea wa Kituo cha Kanda ya Kati Dodoma, pamoja na vituo vitano (5) vya Mikoa kwenye Mikoa ya Njombe, Rukwa, Tanga, Kigoma na Manyara. Vilevile, mpango utawezesha Hospitali za Mikoa kutengeneza mazao ya damu kwa mwaka 2022/2023 ili kuongeza vituo vinavyotengeneza mazao ya damu vya sasa ambavyo ni Vituo saba vya Kanda, Hospitali za Rufaa za kanda, Pamoja na Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza

71. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kutekeleza afua mbalimbali zilizolenga katika kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza ambayo yameendelea kuwa changamoto katika Sekta ya Afya. Afua zilizotekelezwa kwa kipindi cha Julai 2021 hadi Machi 2022 ni pamoja na;

  • Ukarabati wa Kliniki zinazotoa huduma za Selimundu na Hemofilia katika Hospitali ya KCMC, Muhimbili, Benjamin Mkapa, Bugando, Mbeya ZRH na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro umefanyika.
  • Kuendelea na upanuzi wa huduma za usafishaji wa damu (dialysis) katika Hospitali za Rufaa za Mikoa kwa kuongeza Hospitali nyingine 12 za awamu ya pili zitakazotoa huduma hizo ambapo awamu ya kwanza ilihusu Hospitali 7. Mkakati huo unatekelezwa kwa kushirikisha MSD na NHIF, ambao utawezesha huduma za usafishaji wa damu kuongezeka kutoka asilimia 47, yaani watu 2,749 wanaopata huduma za dialysis sasa kati ya 5,800 wanaokadiriwa kuhitaji huduma hiyo kufikia asilimia 60 ifikapo Juni 2023. Mkakati wa Wizara ni kuziwezesha Hospitali zote za Rufaa za Mikoa kutoa huduma ya kusafisha damu.
  • Kuandaa Sheria ya uvunaji na upandikizwaji wa Viungo ambayo mchakato wake umefikia hatua ya kukusanya maoni ya Wadau wa Sheria hiyo. 
  • Kuandaa na kuzindua Mpango Mkakati Jumuishi wa Kitaifa wa Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa Yasiyoambukiza wa mwaka 2021-2026 unaotoa dira ya mapambano dhidi ya Magonjwa yasiyoambukiza nchini.
  • Kufanya uchambuzi wa Sera na Sheria mbalimbali zinazohusu afua za lishe na mazoezi ili kuweza kurekebisha Sheria na Sera katika kuongeza kasi ya mapambano ya vihatarishi (risk factors) vya magonjywa yasiyoambukiza. Uchambuzi huu umekamilika na ushawishi na uraghibishi kwa makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Waheshimiwa Wabunge unaendelea. 
  • Kuandaa na kuzindua Mwongozo wa mazoezi ya kuushughulisha mwili na kuepuka tabia bwete ambao pia umeainisha aina ya mazoezi kwa makundi mbalimbali.
  • Kuandaa vipindi mbalimbali na machapisho ya utoaji wa elimu ya afya dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza. Hii ikiwa ni pamoja na kuadhimisha wiki ya Magonjwa yasiyoambukiza iliyoadhimishwa tarehe 07 hadi 13 Novemba 2021, ambapo machapisho zaidi ya 250 yaliwasilishwa katika Kongamano la Kisayansi, na Wananchi zaidi ya 300,000 walifikiwa na huduma mbalimbali za upimaji wa Magonjwa yasiyoambukiza zilizotolewa.
  • Kuandaa mtaala wa mafunzo ya Magonjwa yasiyoambukiza kwa watoa huduma za afya katika ngazi ya Afya ya Msingi. Hadi sasa, Wizara imeweza kufanya mafunzo kwa watoa huduma 159 kutoka katika vituo vya afya 57 vya Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam. 
  • Kukamilisha  Mkakati wa Kifaifa wa Kudhibiti Matumizi ya Tumbaku nchini kwa miaka (5 ) kuanzia  mwaka 2021/22 hadi 2025/26.
  • Kufanya mafunzo ya utoaji huduma za kisukari na diabetic foot kwa Hospitali zote za Rufaa za Mikoa.
  • Wizara kwa kushirikiana na wadau imekamilisha tathmini ya hali ya huduma za utengamao ambayo ilitumika kuandaa mkakati wa uimarishaji wa huduma za utengamao wa mwaka 2021-2026. Sambamba na mkakati huo serikali imeendelea kuimarisha karakana za tiba mtengamao katika Hospitali za Rufaa za Mikoa ya Iringa na Mtwara ili kuziwesha kuwa na vifaa vya kisasa katika utoaji wa huduma hizo.  

Uimarishaji wa huduma za Matibabu ya Kibingwa nchini

  • Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuboresha na kuimarisha huduma za matibabu ya kibingwa nchini, ili kuokoa maisha ya wananchi wengi sambamba na kupunguza idadi ya wagonjwa wanaopewa rufaa ya Matibabu nje ya nchi. Katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022 Hospitali za Rufaa za Kanda na Taifa ziliwasilisha Wizarani idadi ya wagonjwa 49 waliokuwa na mahitaji ya kupatiwa matibabu nje ya nchi, ambapo wagonjwa 37 walipatiwa kibali cha kwenda kutibiwa nje ya nchi.
  • Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022, Hospitali ngazi ya Taifa, Kanda na Maalum zimehudumia jumla ya wagonjwa 1,782,264. Kati ya hao, wagonjwa wa nje (OPD) walikuwa 1,566,536 na wagonjwa wa kulazwa (IPD) walikuwa 215,728 ikilingalinishwa na wagonjwa 1,686,395 waliohudumiwa katika kipindi kama hicho mwaka 2020/21 kama inavyoonesha katika kiambatisho Na.3. Aidha, kati ya wagonjwa 1,782,264 waliohudumiwa katika Hospitali hizo, wagonjwa 84,109 walikuwa ni wagonjwa wa msamaha, na walizigharimu Hospitali hizo za Rufaa za Taifa, Kanda na Maalum jumla ya shilingi 35,469,895,902.19 kama inavyoonesha katika kiambatisho Na.4.

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)

  • Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imehudumia jumla ya wagonjwa 367,213. Kati ya hao, wagonjwa wa nje (OPD) walikuwa 328,938 na wagonjwa wa kulazwa (IPD) walikuwa 38,275. Aidha, wagonjwa wa misamaha walikuwa 46,591 ambao waliigharimu Hospitali kiasi cha shilingi bilioni 14.1 katika kipindi hicho.
  • Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022, Hospitali imetoa huduma ya upandikizaji figo (renal transplant) kwa wagonjwa 6 ambapo gharama ya huduma hiyo ni shilingi milioni 30kwa mgonjwa mmoja ambapo huduma hiyo hugharimu shilingi milioni 120 nchini India. Wagonjwa waliopandikizwa figo tangu huduma hiyo ilipoanzishwa hapa nchini mwaka 2017, wamefikia wagonjwa 70. Hivyo wagonjwa 70 waliopata huduma hii katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wangegharimu shilingi 8,400,000,000 iwapo wangepata huduma hiyo nchini India.  Kwa kuanzisha huduma hii hapa nchini Serikali imeokoa jumla ya shilingi 6,300,000,000.
  • Mheshimiwa spika, Katika kipindi cha Julai 2021 mpaka Machi, 2022, Hospitali imetoa huduma ya upandikizaji vifaa vya usikivu (cochlea implant) kwa watoto 14 ambapo gharama ya huduma hiyo ni shilingi milioni 36 kwa mgonjwa mmoja ambapo huduma hiyo hugharimu shilingi milioni 100 nchini India. Wagonjwa waliopandikizwa vifaa vya usikivu tangu huduma hiyo ilipoanzishwa hapa nchini mwaka 2017, wamefikia 49 kwa gharama ya shilingi bilioni 1.764. Hivyo watoto 49 waliopata huduma hii katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wangegharimu shilingi bilioni 4.9 Kwa kuanzisha huduma hii hapa nchini Serikali imeokoa jumla ya shilingi bilioni 3.136.   
  • Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022, Hospitali ya Taifa Muhimbili imetoa huduma za Matibabu ya Radiolojia kwa njia ndogo (Intervertional Radiology)kwa wagonjwa 1,692 na kufanya jumla ya wagonjwa waliopata huduma hii kufikia 2,343 tangu huduma hii ilipoanzishwa Novemba, 2018. Gharama ya kumpeleka mgonjwa mmoja nje ya nchi kwa huduma hii ni shilingi milioni 96 ambapo Hospitali ya Taifa Muhimbili inatoa huduma hiyo kwa gharama ya shilingi milioni 8 tu. Kwa wagonjwa 2,343 Hospitali imetumia shilingi bilioni 18.7, na endapo wangeenda nje Serikali ingetumia shilingi bilioni 224.9. Hivyo jumla ya shilingi bilioni 206.2 zimeweza kuokolewa.

Hospitali ya Mloganzila

  • Mheshimiwa Spika, kwa kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022 Hospitali ya Mloganzila imehudumia jumla ya Wagonjwa 91,744 ukilinganisha na Wagonjwa 82,339 waliohudumiwa kipindi kama hiki kwa mwaka 2020/21. Kati ya wagonjwa hao, Wagonjwa 82,804 walikuwa ni wa nje (OPD) na wagonjwa 8,940 walikuwa ni wa ndani (IPD). Aidha, wagonjwa wa misamaha walikuwa 2,928 ambao waliigharimu Hospitali kiasi cha Shilingi bilioni 1.9 katika kipindi hicho. Hali ya upatikanaji wa damu katika Hospitali imefikia wastani wa asilimia 94 ya mahitaji. 
  • Mheshimiwa Spika, Hospitali imefanikiwa kusimika mtambo wa kuzalisha hewa tiba (Oxygen generating plant) wenye uwezo wa kuzalisha mitungi 200 yenye ujazo wa 8.5 M³ kwa siku, ambapo mitungi ya ziada takribani 100 itauzwa na hivyo kuongeza mapato ya ndani. Aidha, mtambo huu umegharimu Dola za Marekani 300,000. Vilevile, Hospitali imefanya ukarabati wa wodi ya watoto wachanga mahututi (Neonatal Intensive Care Unit -NICU) ambapo ukarabati huu umeongeza vitanda vya NICU kutoka vitanda 30 mwaka 2020 hadi hadi kufikia vitanda 60 kwa mwaka 2021. Pia, mradi huu unahusisha uanzishwaji wa Wodi ya Watoto wachanga, na wodi ya wajawazito mahututi (Maternal ICU) yenye uwezo wa vitanda 4 pamoja na wodi ya wajawazito wanaohitaji uangalizi maalum (HDU) yenye uwezo wa vitanda 6. Ukarabati huu umegharimu jumla shilingi milioni 168.2.
  • Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022, Hospitali ya Mloganzila kwa kushirikiana na Hospitali ya Taifa Muhimbili ilifanikiwa kutoa huduma ya upandikizaji wa uloto

(bone marrow transplant) ambapo jumla ya wagonjwa 11 walifanyiwa upandikizaji huo. Huduma hii ni mara ya kwanza kufanyika nchini na katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Gharama za kumpeleka mgonjwa mmoja nje ya nchi ni shilingi milioni 250 wakati katika Hospitali ya Mloganzila ni shilingi milioni 70 tu. Hivyo Hospitali imetumia shillingi milioni 770 na kama wagonjwa hao wangeenda nje ya nchi, Serikali ingetumia shillingi bilioni 2.75 na hiyo jumla ya shilingi bilioni 1.98 zimeweza kuokolewa.

  • Mheshimiwa Spika, Katika kuimarisha utendaji wa hospitali ya Mloganzila ambayo ipo chini ya usimamizi wa hospitali ya Taifa Muhimbili naomba kuchukua fursa hii kulijulisha Bunge lako Tukufu na wananchi kwa ujumla kuwa kuanzia tarehe 1 Julai

2022, hospitali hii itaanza kujiendesha yenyewe. Wizara inaendelea na uchambuzi wa huduma mahususi za ubingwa bobezi ambazo Hospitali hii itajikita katika kuzitoa kwa wananchi. Tunaamini kuwa hatua hii itaiwezesha Hospitali kutoa huduma bora na kwa haraka sambamba na kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI)

  • Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanzia Julai 2021 hadi Machi, 2022 Taasisi ya Mifupa (MOI) iliendelea kutoa huduma ambapo jumla ya Wagonjwa 154,260 walihudumiwa. Kati yao, Wagonjwa wa nje (OPD) ni 147,847 na Wagonjwa wa kulazwa (IPD) ni 6,413 ikilinganishwa na Wagonjwa 155,843 waliohudumiwa kipindi kama hicho kwa mwaka 2020/2021. 
  • Mheshimiwa Spika, Hospitali ilifanya upasuaji kwa Wagonjwa 5,098 ambapo upasuaji wa Mifupa mbalimbali Wagonjwa 1,765; upasuaji wa kubadilisha nyonga Wagonjwa 121; upasuaji wa goti Wagonjwa 90; upasuaji wa goti kwa kutumia matundu Wagonjwa 131; upasuaji wa mfupa wa kiuno Wagonjwa 59; upasuaji wa uti wa mgongo Wagonjwa 142; upasuaji wa ubongo Wagonjwa 157; upasuaji wa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi Wagonjwa 288; upasuaji wa mfupa wa paja (femur) Wagonjwa 345; na upasuaji kwa wagonjwa wa dharura 1,793. Vilevile Taasisi imefanya upasuaji wa kunyoosha vibyongo (Scoliosis Surgery) kwa Watoto 22 na upasuaji wa kuondoa uvimbe ulio kwenye sakafu ya ubongo kupitia tundu la pua (transphenadial hypophysectomy) Wagonjwa 23, na upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye mshipa wa damu kwenye ubongo (Aneurysm clipping) ilikuwa Wagonjwa 162. 
  • Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi 2022, Taasisi kwa kutumia maabara maalum ya upasuaji wa ubongo bila kufungua fuvu (Angio – Suite) imefanya upasuaji kwa  kutumia maabara hii kwa wagonjwa 161. Aidha, kwa mara ya kwanza Taasisi imeweza kutoa matibabu ya kifafa (Epilepsy) kwa njia ya upasuaji.
  • Mheshimiwa Spika, Taasisi iliendelea kutoa huduma za Mkoba ikiwa ni pamoja na upasuaji wa mifupa kwa lengo la kusogeza huduma kwa Wananchi. Katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022 Madaktari Bingwa wa MOI wamewahudumia

Wagonjwa 1,465 katika Hospitali ya Nyangao (Lindi); Hospitali ya Misheni Ndanda (Lindi) wamehudumiwa Wagonjwa 1,051; Hospitali ya Mkoa wa Geita wamehudumiwa Wagonjwa 315; Hospitali ya Arusha HDC wamehudumiwa Wagonjwa 60 na Hospitali ya Benjamini Mkapa (Dodoma) wamehudumiwa

Wagonjwa 32. 

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)

  • Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022, Taasisi ilihudumia jumla ya Wagonjwa 87,332 ikilinganishwa na Wagonjwa 75,716 waliohudumiwa katika kipindi cha mwaka 2020/21. Kati yao, Wagonjwa 84,045 walikuwa wa nje (OPD) na Wagonjwa wakulazwa (IPD) walikuwa 3,287. Miongoni mwa waliopata huduma ni pamoja na Wagonjwa 58 kutoka nchi za Visiwa vya Comoro, Zambia, DRC, Kenya, Botswana na Burundi. Aidha, wagonjwa wa misamaha walikuwa 2,135 ambao waliigharimu

Hospitali kiasi cha shilingi milioni 814.8.

  • Mheshimiwa Spika, Taasisi imeweza kufanya upasuaji wa moyo kwa Wagonjwa 439, kati ya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji, Wagonjwa 311 walifanyiwa upasuaji mkubwa wa kufungua kifua bila kusimamisha Moyo, kati yao Watu wazima walikuwa 113 na Watoto walikuwa 198. Aidha, Wagonjwa wengine 128 ambao ni Watu wazima wenye matatizo ya mishipa ya damu walifanyiwa upasuaji kwa njia ya kisasa (Vascular surgery), upasuaji huu umefanywa na Wataalam wa ndani. 

Aidha, jumla ya Wagonjwa 1,425 walipata huduma za upasuaji wa Moyo kwa kutumia mtambo maalum (Catheterization Laboratory) ikiwa ni ongezeko la asilimia 12 ikilinganishwa na Wagonjwa 1,262 waliofanyiwa huduma hiyo kwa kipindi kama hicho kwa mwaka 2020/21, kati yao Watu wazima walikuwa 1,288 na Watoto 137.

Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI)

  • Mheshimiwa Spika, Taasisi ya Saratani ya Ocean Road ilihudumia jumla ya wagonjwa 37,882 kati ya Wagonjwa hao, wagonjwa wa nje (OPD) walikuwa 33,621 na Wagonjwa wa kulazwa walikuwa 4,261. Kati ya wagonjwa waliohudumiwa katika kipindi hiki, wagonjwa 15,153 walipatiwa huduma za tiba mionzi, wagonjwa 9,849 walipatiwa huduma ya tiba kemia na wagonjwa 12,880 walipata tiba ya kemia na mionzi. Baada ya huduma za uchunguzi na tiba ya Saratani kuimarishwa, wagonjwa kutoka nje ya nchi wameendelea kufika katika Taasisi ambapo katika kipindi hicho wagonjwa wapya 59 walipatiwa huduma za uchunguzi na tiba ya Saratani.
  • Mheshimiwa Spika, aidha huduma za uchunguzi wa Saratani umeendelea kufanywa na Taasisi kwa njia ya Mkoba. Uchunguzi huo ulifanyika katika Mikoa ya Dar es Salaam, Geita, Lindi, Ruvuma, Dodoma, Arusha, na Mtwara. Katika kipindi hiki, jumla ya wanawake 9,219 walifanyiwa uchunguzi wa Saratani ya Matiti na Saratani ya mlango wa kizazi; kati yao wanawake 2,977 walifanyiwa uchunguzi katika Taasisi na wanawake 6,242 walifanyiwa uchunguzi kupitia huduma za Mkoba. Kati ya Wanawake waliofanyiwa uchunguzi wa Saratani ya Matiti na Saratani ya mlango wa kizazi, wanawake 364 walionekana kuwa na dalili za awali za Saratani na wanawake 26 waligundulika kuwa na Saratani. Pia, jumla ya wanaume 686 walifanyiwa uchunguzi wa Saratani ya tezi dume; kati yao wanaume 165 walifanyiwa uchunguzi katika Taasisi na wanaume 521 walifanyiwa uchunguzi kupitia huduma za Mkoba. Katika uchunguzi huo, wanaume 21 sawa na asilimia 3 waligundulika kuwa na Saratani ya tezi dume. Pia, uchunguzi wa Saratani ya ngozi (kaposi sarcoma) na utumbo mpana ulifanyika kwa watu 302 ambapo watu 33 sawa na asilimia 10 waligundulika kuwa na

Saratani. 

Katika kuhakikisha kwamba wananchi wanapata elimu kuhusu ugonjwa wa Saratani, Taasisi iliendelea kutoa elimu kwa umma kwa njia mbalimbali zikiwepo vipindi 34 vya runinga, redio vipindi 51 na machapisho 46 ya magazeti kuhusu namna ya kujikinga na Saratani. Utoaji wa elimu kwa umma ulitekelezwa kwa asilimia 90 ya lengo. Aidha, elimu imeendelea kutolewa kwa          njia   ya        mitandao   ya      kijamii        kupitia

(@oceanroadcancerinstitute, @wizara_afya). Vilevile, jumla ya wanafunzi 262 kutoka shule za Sekondari walipatiwa elimu kuhusu Saratani.

  • Mheshimiwa Spika, Upatikanaji wa dawa za Saratani kwa Wagonjwa ilikuwa ni asilimia 99 ikilinganishwa na asilimia 98 mwaka 2020/21. Taasisi imeendelea kusimamia utoaji wa dawa za Saratani kwa mgonjwa kuchangia kadiri anavyomudu ambapo wagonjwa wasiomudu gharama walipatiwa msamaha wa kupata dawa za tiba ya Saratani kupitia dawati la Afisa Ustawi wa Jamii ambapo jumla ya wagonjwa 2,792 walipatiwa misamaha mbalimbali ya gharama za uchunguzi wa Kimaabara, Radiolojia na tiba. Huduma zilizotolewa kwa msamaha katika kipindi hicho zina thamani ya shilingi bilioni 13.9 Taasisi iliendelea kuimarisha upatikanaji wa dawa za saratani katika Duka la Dawa la Jamii. Upatikanaji wa dawa za Saratani katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022 uliendelea kuwa asilimia 100 na imesaidia kuongeza mapato kwa Taasisi. Vilevile, bei ya dawa katika duka la dawa la Jamii la Taasisi ni nafuu kwa wastani wa asilimia 30 ikilinganishwa na bei ya dawa hizo katika maduka binafsi nje ya Taasisi.
  • Mheshimiwa Spika, Kutokana na uboreshaji mkubwa wa miundombinu uliofanywa na Serikali katika eneo la matibabu na uchunguzi wa Kibingwa na ubingwa Bobezi kwa wagonjwa wa saratani, Rufaa za matibabu nje ya nchi zimepungua. Kutokana na maboresho hayo, Taasisi ilitoa rufaa ya matibabu nje ya nchi kwa mgonjwa mmoja (1) tu katika kipindi cha miaka miwili mfululizo.
  • Mheshimiwa Spika, Taasisi ilitoa tiba Shufaa (palliative care) kwa jumla ya wagonjwa 25,224 na wagonjwa 2,013 walipatiwa oral morphine kwa ajili ya kupunguza maumivu. Pia huduma za Maabara zimezidi kuimarika ambapo katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi 2022, jumla ya vipimo vya Maabara 148,676 vilifanyika, ambapo kati yake, vipimo 147,339 vilikuwa vipimo vya kawaida na vipimo 1,337 ni vya patholojia. Vipimo mahsusi vya Saratani vya histopathology, cytology, Immunoassay (tumor markers), haematology, clinical chemistry, immunology, parasitology, na blood transfusion vinafanyika na kusaidia kutoa tiba mahsusi kwa wagonjwa wa

Saratani.

  • Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha taarifa hii, Taasisi ilitoa jumla ya tiba mionzi 168,255 kwa wagonjwa kwa kutumia mashine 5 za mionzi ya nje (2 za Cobalt-60, 1 ya Caesium na 2 za LINAC) na mashine 2 mionzi ya ndani (brachytherapy). Taasisi ilifanikiwa kutoa jumla ya vipimo 18,633 vya radiolojia, kati ya vipimo hivyo, vipimo 7,192 ni vya X-ray, 7,535 vya ultrasound, 3,759 vya CT Scan na 147 vya mammograph ikiwa ni sawa na asilimia 105 ya lengo. 
  • Mheshimiwa Spika, Taasisi iliendelea kutoa huduma za uchunguzi na tiba za dawa nyuklia ambapo katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022, jumla ya wagonjwa 1,082 walipatiwa huduma sawa na asilimia 95 ya lengo. Wagonjwa 369 walifanyiwa uchunguzi (diagnostic scans) katika Mifupa, Figo, Ubongo, na Tezi ya shingoni na wagonjwa 36 walipatiwa tiba ya nyuklia. Aidha, Maabara ya Taasisi ilifanyiwa tathmini kwa ajili ya ithibati ya Kimataifa (International accreditation) na kupewa ithibati katika vipimo vya aina tano. Cheti cha ithibati cha ubora kimetolewa kutoka Shirika la Viwango la Ukaguzi la Kimataifa SADCAS na hivyo Maabara ya Taasisi imeingizwa katika orodha ya maabara bora inayotoa huduma za vipimo Duniani. 
  • Mheshimiwa Spika, Taasisi kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili iliendelea kutoa mafunzo kwa Wanafunzi 67 wa Shahada ya Kwanza ya Tiba ya Mionzi (Bachelor of Science in Radiation Therapy Technology), wanafunzi 34 wa Shahada ya Uzamili ya Onkolojia (Masters of Medicine in Clinical Oncology) na wanafunzi 10 wa Shahada ya Uzamili ya Uuguzi katika Onkolojia (Masters of Science in Nursing Oncology). Mafunzo haya yameongeza uwepo wa Wataalamu wa huduma za Saratani hapa nchini; kwa sasa Taasisi ina Madaktari Bingwa 37.
  • Mheshimiwa Spika, Taasisi iliendelea kutekeleza mradi wa kusimika mashine ya PET/CT Scan ambapo unahusisha ujenzi wa Bunkers na ununuzi na usimikaji wa mashine za PET/CT Scan na Cyclotron, kwa gharama ya shilingi bilioni 18.2. Ujenzi wa jengo ulianza Mei, 2021, na unategemewa kukamilika Juni, 2022 ambapo hadi sasa umefikia asilimia 80 ya utekelezaji. 

Hospitali ya Benjamin Mkapa 

  • Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022, Hospitali ya Benjamin Mkapa imeendelea kutoa huduma ambapo jumla ya Wagonjwa 168,479 walihudhuria na kupata matibabu, ikilinganishwa na Wagonjwa 126,196 waliopata huduma kwa kipindi kama hiki mwaka 2020/21. Kati ya hao, Wagonjwa 160,942 walikuwa wa nje (OPD) na wagonjwa waliolazwa (IPD) Walikuwa 7,537. Wagonjwa wanaopatiwa huduma katika Hospitali wameendelea kuongezeka sawa na ongezeko la asilimia 34 ikilinganishwa na mwaka 2020/21. Ongezeko hilo limetokana na uboreshwaji wa huduma zinazotolewa kutokana na uwepo wa vifaa vya kisasa na wataalam wenye ujuzi. Aidha, wagonjwa wa msamaha walikuwa 2,228 ambao waliigharimu Hospitali kiasi cha shilingi milioni 281 katika kipindi hicho.
  • Mheshimiwa Spika, Jumla ya vipimo vya moyo 9,270 vimefanyika kwa kipindi cha mwaka 2021/22, ikilinganisha na vipimo 7,104 vilivyofanyika kipindi kama hiki mwaka 2020/21 ikiwa ni ongezeko la asilimia 31. Vilevile Katika kipindi cha Julai hadi Machi, 2022, jumla ya wagonjwa 4,872 walipata huduma ya upasuaji, ikilinganishwa na wagonjwa 3,188 waliopewa huduma hiyo kwa kipindi kama hicho mwaka 2020/21, ambapo kumekuwa na ongezeko la asilimia 53. Wagonjwa waliofanyiwa huduma za upasuaji kwa kutumia matundu madogo walikuwa 846 ikilinganishwa na 509 waliofanyiwa kipindi kama hiki mwaka 2021 ambalo ni ongezeko la asilimia 66.
  • Mheshimiwa Spika, kwa kipindi cha Julai hadi Machi 2022, jumla ya Wagonjwa nane (8) walipata huduma ya Upandikizwaji wa Figo na kufikisha jumla ya wagonjwa 29 waliopata huduma hii toka Hospitali ilipoanza kutoa huduma za kupandikiza figo mwezi Machi, 2018. Gharama ya upandikizaji figo katika Hospitali ya Benjamin Mkapa ni kati ya Shilingi milioni 27 hadi Milioni 35 kwa mgonjwa mmoja ikilinganishwa na Shilingi milioni 75 hadi Milioni 100 mgonjwa mmoja akitibiwa nje ya nchi. Upatikanaji wa huduma hizo hapa nchini kumeiwezesha Serikali kuokoa jumla ya Shilingi bilioni 2.1   

Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe

100. Mheshimiwa Spika, Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi 2022 ilihudumia jumla ya wagonjwa 28,325 kati yao 26,761 ni wagonjwa wa akili wa nje (OPD) na wagonjwa wa akili wa ndani (IPD) 1,564. Aidha, wagonjwa wa msamaha waliopewa huduma walikuwa 3,985 ambao waliigharimu Hospitali kiasi cha shilingi 60,217,746 katika kipindi hicho. Jumla ya Wagonjwa 123, walipata huduma za kibingwa za Saikolojia na wagonjwa 443 wa Neuro-psychiatry na wagonjwa wapatao 123 walifanyiwa uchunguzi na kuandikiwa taarifa za Kisheria. Vilevile, katika kliniki ya afya ya akili kwa Watoto na vijana wagonjwa 1,121 walihudumiwa. Taasisi pia, ilipokea wagonjwa wapya 225 wenye matatizo ya utumiaji wa madawa ya kulevya na hivyo kufanya jumla ya waraibu wanaohudumiwa na kituo cha Itega kufikia 548 toka kilipoanza kutoa huduma mwaka 2020.

Hospitali ya Taifa ya Magonjwa Ambukizi

Kibong’oto

  1. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022 Hospitali ilihudumia jumla ya Wagonjwa 26,884 ambapo wagonjwa wa nje walikuwa 13,953 na wagonjwa waliolazwa walikuwa 636 na wagonjwa waliohudumiwa katika Jamii (community outreach) walikuwa 12,295. Kati ya Wagonjwa waliolazwa wagonjwa wa kifua kikuu sugu walikuwa 104. Aidha, Wagonjwa wa kifua kikuu sugu waliomaliza matibabu ni asilimia 75 na kati yao asilimia 70 walithibitishwa kupona kifua kikuu sugu. 
  1. Mheshimiwa Spika, Hospitali imeweza kufanya ubainishaji wa vinasaba vya UVIKO-19 katika sampuli 69 ambapo sampuli 29 ziliweza kuleta majibu kati ya sampuli hizo zilizoleta majibu, sampuli 19 zilikuwa na vinasaba vya delta and Beta. Hospitali imeendelea pia kutoa huduma kwa wagonjwa wa msamaha, ambapo jumla yao walikuwa 497 ambao waliigharimu Hospitali kiasi cha Shilingi 114,541,967 katika kipindi hicho.

Hospitali ya Rufaa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mbeya

  1. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi 2022, Hospitali imehudumia jumla ya Wagonjwa 237,186, ikilinganishwa na Wagonjwa 330,947 waliopatiwa huduma mwaka 2020/21. Kati yao, Wagonjwa 205,329 walikuwa wa nje na Wagonjwa 31,857 walilazwa. Hospitali imeendelea pia kutoa huduma kwa Wagonjwa wa msamaha, ambapo jumla ya Wagonjwa 18,547 walihudumiwa na waliigharimu Hospitali kiasi cha Shilingi 185,478,000 katika kipindi hicho. Hospitali imeendelea kuboresha huduma za kibingwa kwa kuendelea kuongeza Wataalam wa kada mbalimbali. Hadi kufikia Machi 2022 huduma zilizoongezeka ni za upasuaji wa mishipa ya fahamu na ubongo. Huduma ya tiba ya Saratani imeendelea kutolewa ambapo Hospitali imehudumia jumla ya Wagonjwa 820 waliopata matibabu ya Saratani kwa kutumia dawa (chemotherapy) na upasuaji. 
  1. Mheshimiwa Spika, Hospitali imeendelea kuboresha miundombinu ya kutolea huduma ambapo jengo la huduma za daraja la kwanza lilikarabatiwa na kuongeza vitanda 50, na kufanya Hospitali kuwa na jumla ya vitanda 603. Aidha, Serikali imetoa kiasi cha Shilingi bilioni 9.2 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la ghorofa sita (6) la kutolea huduma za afya ya uzazi na Mtoto lililopo eneo la Meta. Jengo hili linajengwa kwa utaratibu wa “Force Account” na ujenzi umefikia asilimia 95. Kukamilika kwa jengo hili kutaongeza vitanda 220 na kufikia jumla ya vitanda 823.

      Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando

  1. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022 Hospitali ilihudumia jumla ya Wagonjwa 291,837 ikilinganishwa na Wagonjwa 311,610 katika kipindi kama hicho mwaka 2020/21. Wagonjwa wa nje (OPD) walikuwa 269,019 na Wagonjwa wa kulazwa (IPD) walikuwa 22,818. Aidha, Hospitali imeendelea kutoa huduma kwa wagonjwa wa msamaha, ambapo Wagonjwa 548 walihudumiwa na waliigharimu Hospitali kiasi cha Shilingi 308,651,412. Vilevile, Hospitali imeendelea kuboresha huduma za kibingwa kwa kuanza kutoa uchunguzi wa Saratani ya matiti baada ya kununua mashine iitwayo mammogram kwa Shilingi million 800.

Taasisi ilihudumia jumla ya Wagonjwa 9,542 wa matibabu ya Saratani ikilinganishwa na Wagonjwa 12,320 waliopata huduma hiyo mwaka 2020/21. Kati yao, Wagonjwa 2,765 walipatiwa tiba ya Saratani kwa kutumia dawa (Chemotherapy) na Wagonjwa 598 walipatiwa tiba ya mionzi (Radiotherapy). Upatikanaji wa huduma hii umepunguza Rufaa za Wagonjwa wa Saratani wa Kanda ya Ziwa kwenda Taasisi ya Saratani Ocean Road. 

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Kaskazini (KCMC)

  1. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022 Hospitali ya KCMC ilipokea jumla ya Wagonjwa 297,810. Kati yao Wagonjwa wa nje (OPD) walikuwa 208,467 na Wagonjwa wa ndani (IPD) ni 89,343, ambapo asilimia 87 ya wagonjwa wote wanatoka katika Mikoa iliyopo ndani ya maeneo yanayohudumiwa na Hospitali kwa Kanda ya

Kaskazini. 

  1. Mheshimiwa Spika, Hospitali pia imeendelea kuboresha huduma za uchunguzi wa magonjwa kwa kununua na kufunga mitambo mipya ya MRI, CT na Digital X- ray.  Maboresho hayo yamewezesha wagonjwa kuendelea kufanyiwa kipimo cha MRI Wagonjwa 735, vipimo vya CT Scan wagonjwa 5,678, vipimo vya Ultrasound Wagonjwa 6,213 na Wagonjwa 9,873 vipimo vya X-ray. Huduma za upasuaji zimefanyika kwa Wagonjwa 4,674. 
  1. Mheshimiwa Spika, Hospitali pia imeendelea kutoa huduma katika idara ya Saratani, ambapo katika kipindi tajwa jumla ya wagonjwa 6,806 wa Saratani, kati yao Wagonjwa 4,878 walikuwa ni Watu wazima na Wagonjwa 1,928 walikuwa ni watoto. Hospitali kupitia idara ya Urolojia iliweza kufanya upasuaji kwa Wagonjwa 761 waliokuwa na changamoto mbalimbali katika njia ya Mikojo, kati yao Wanaume walikuwa 695 na wanawake ni 66. Idara ya ngozi, imeendelea kutoa huduma za matibabu na upasuaji, ambapo katika kipindi cha mwezi Julai 2021 hadi Machi 2022 jumla ya Wagonjwa 11,893 walifikiwa. Hospitali pia imeendelea kutoa huduma za Mkoba (outreach services) katika maeneo mbalimbali nje ya Hospitali ambapo katika kipindi tajwa jumla ya Wagonjwa 5,254 wamepatiwa huduma mbalimbali. 109. Mheshimiwa Spika, Katika kuadhimisha miaka 50 ya Hospitali ya KCMC tangu kuanzishwa kwake mwaka 1971, Hospitali ilitoa huduma ya upimaji kwa Wananchi bure, ambapo jumla ya Watu 1,930 walipimwa magonjwa mbalimbali ikiwemo utoaji wa chanjo ya UVIKO – 19.  Hospitali pia imetoa huduma ya macho ambapo jumla ya wagonjwa 17,281 kati yao wagonjwa wapya walikuwa ni 15,989 na Wagonjwa wakujirudia ni 1,292. Katika kipindi tajwa Hospitali imetoa msamaha kwa wagonjwa 703 ambapo jumla ya Shilingi bilioni 3.5 zimetumika, kati ya hizo Shilingi bilioni 2.9 zimetumika kwa Wagonjwa wa Saratani.  

110. Mheshimiwa Spika, Hospitali imeendelea kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za kibingwa ambapo, ujenzi wa wodi maalumu ya wagonjwa wa Saratani imekamilika kwa asilimia 100 na inaendelea kutoa huduma. Katika kipindi tajwa Hospitali pia inaendelea na ujenzi wa jengo la mionzi (Bunker) ambapo jumla ya gharama ya ujenzi ni Shilingi Bilioni 4.7, kati ya hizo Shilingi Bilioni 2 zimetolewa. Mradi huu umetekelezwa kwa asilimia 48. Hospitali pia imeendelea na ujenzi wa mabweni ya kulala Wagonjwa wa Saratani na ndugu wa Wagonjwa ambao watakuwa wanatokea maeneo ya nje ya Mkoa wa Kilimanjaro, malazi yatakuwa kwa gharama nafuu sana, ujenzi huu umefikia asilimia 52 na unategemewa kugharimu Shilingi bilioni 2 hadi kukamilika kwake.  111. Mheshimiwa Spika, Hospitali inaendelea kutoa huduma ya uzalishaji wa hewa ya Oksijeni kupitia kinu chake chenye uwezo wa kuzalisha mitungi 400 kwa siku hivyo kuokoa zaidi ya shilingi 150,000,000 kwa mwezi. Upatikanaji wa hewa hii katika hospitali umekuwa msaada mkubwa hasa kipindi cha mfumuko wa UVIKO- 19 na hivyo kuokoa zaidi ya shilingi bilioni

3. 

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato

  1. Mheshimiwa Spika, Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato ilianza kutoa huduma Julai, 2021 ambapo hadi kufikia Machi 2022, Hospitali imeweza kuhudumia jumla ya wagonjwa 5,607 ambapo Wagonjwa wa nje (OPD) walikuwa 4,810 na wagonjwa wa ndani (IPD) walikuwa 797. Huduma za kibingwa zilizoanza kutolewa ni pamoja na upasuaji kwa Wanawake (obstretics & Gyanocology) kama vile Hysterectomy intravaginal & Abdominal, Laparatomy, VVF Repair, Colporhaphy Anterior & posterior, Vulvectomy + Biopsy taking.  
  1. Mheshimiwa Spika, Hospitali imeendelea na ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya utoaji huduma ambapo kwa kipindi cha mwezi Julai, 2021 hadi Machi 2022, Hospitali imeendelea na ujenzi wa majengo 6 na nyumba 20 za Watumishi, ambayo yanajengwa kwa awamu. Katika Awamu ya kwanza ilihusu Ujenzi wa jengo la Wagonjwa wa nje (OPD), jengo la Famasi na uchunguzi (Maabara), Jengo la huduma za dharura (EMD) na Jengo la Wagonjwa wanaohitaji Uangalizi maalumu (ICU) na utekelezaji wake umefikia asilimia 98. Ujenzi wa awamu ya pili unahusisha Majengo yafuatayo, Wodi yenye ghorofa mbili (2) na likikamilika litakuwa na uwezo wa kuwa na vitanda 201 ambalo ujenzi wake umefikia asilimia 45, jengo la Mionzi limefikia asilimia 95, kazi za nyongeza za ujenzi wa Jengo la kuhifadhia maiti (Mortuary), jengo la kutakasisha vifaa (CSSD) na jengo la kufulia nguo. 
  1. Mheshimiwa Spika, Katika kuboresha huduma, Hospitali imeanzisha utengenezaji wa mifuko ya kuwekea taka mbalimbali (Bin liners) na kuuza kwa vituo vya kutoa huduma za afya vya karibu, pia Hospitali imeshaanza kutoa huduma kwa wagonjwa wa dharura (EMD). Aidha, hospitali ipo katika taratibu za kuanzisha Kitengo cha kuchanganya Dawa (compounding na infusion unit), kuanzisha huduma ya kitengo cha ICU, kitengo cha Mionzi ambapo kutakuwa na huduma ya CT Scan na MRI, na kuanzisha Huduma ya kuchuja Damu kwa Wagonjwa ambao Figo zao zimeshindwa kufanya kazi (Dialysis).

Hospitali za Rufaa za Mikoa 

  1. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022, Hospitali 28 za Rufaa za Mikoa zilihudumia jumla ya wagonjwa 2,636,890 ikilinganishwa na wagonjwa 2,814,390 waliohudumiwa katika kipindi kama hicho mwaka 2020/21. Kati ya wagonjwa waliohudumiwa katika kipindi cha 2021/22 wagonjwa wa nje (OPD) walikuwa 2,415,431 na wagonjwa waliolazwa (IPD) walikuwa 221,459. Mchanganuo wa wagonjwa waliohudumiwa upo katika kiambatisho Na.5. Aidha, kati ya wagonjwa hao waliohudumiwa katika Hospitali za Rufaa za Mikoa, jumla ya wagonjwa 145,797 walikuwa ni wagonjwa wa msamaha, na walizigharimu Hospital hizo jumla ya shilingi 3,473,134,105 ikilinganishwa na Wagonjwa 353,139 wa msamaha mwaka 2020/21 waliozigharimu Hospitali hizo kiasi cha shilingi 4,286,784,135 kama ilivyofafanuliwa katika kiambatisho Na.6
  1. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Huduma za Kujifungua katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022 jumla ya akinamama65,616 walijifungua katika Hospitali za Rufaa za Mikoa ukilinganisha na akinamama 77,563 waliojifungua mwaka 2020/21 kama inavyoonekana katika kiambatisho Na.7. Aidha, katika kipindi hicho vilitokea vifo 231 vinavyohusiana na uzazi ukilinganisha na vifo 272 vilivyoredokiwa mwaka 2020/21. Kupungua kwa idadi hii ni kutokana na jitihada za Serikali za kuboresha Vituo vya Afya katika Halmashauri mbalimbali nchini, ambavyo vimewezeshwa kutoa huduma bora za uzazi za dharura ikiwemo upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni (CEmONC).  
  1. Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma za kibingwa katika ngazi ya mikoa ambapo huduma mbalimbali za kibingwa zimeendelea kutolewa ikiwemo huduma ya usafishaji wa damu (dialysis) kwa wagonjwa wenye magonjwa ya figo. Jumla ya wagonjwa 62 wameendelea kupata huduma za kusafisha damu katika Hospitali za Rufaa za Mikoa 7 ambazo ni Bombo (Tanga), Bukoba

(Kagera), Mount Meru (Arusha), Ligula (Mtwara),

Maweni (Kigoma), Musoma (Mara) na Sekou-Toure (Mwanza). Wagonjwa hawa wanapata huduma za kusafisha damu mara tatu kwa wiki. Aidha, Serikali inaendelea kuzijengea uwezo hospitali zote za rufaa za Mikoa ziweze kutoa huduma za kusafisha damu. 

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuimarisha upatikanaji wa huduma za kibingwa kwenye mazingira ya karibu na wananchi, ambapo katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022 Hospitali za Rufaa za Mikoa 18 zilitoa huduma za mkoba (outreach services) katika fani za ubingwa zifuatazo; magonjwa ya macho, magonjwa ya watoto, dawa za usingizi, upasuaji wa mifupa, magonjwa ya ndani, upasuaji wa kawaida, afya ya uzazi na magonjwa ya wanawake, magonjwa ya sikio, pua na koo, afya ya akili, radiolojia, afya ya kinywa na meno, magonjwa ya damu, magonjwa ya ngozi na huduma za tiba kwa mazoezi (physiotherapy). Katika kliniki hizo, jumla ya wagonjwa 23,976 walihudumiwa, kati yao 2,934 walifanyiwa upasuaji.  

HUDUMA ZA DHARURA NA MAAFA

119. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuimarisha huduma za dharura na kutekeleza afua mbalimbali za kukabiliana na maafa yanayotokea nchini ambayo huathiri afya za Wananchi. Katika kipindi cha taarifa hii nchi yetu imeendelea kukabiliana na janga la ugonjwa wa UVIKO-19 ambalo limeathiri nchi nyingi Duniani. Katika kukabiliana na janga hilo, Wizara imetekeleza afua zifuatazo;

  1. Kuratibu kuanzishwa kwa vituo vinne (4) vya Operesheni ya matukio ya dharura (PHEOCs) na kutoa mafunzo kwa wataalamu wa vituo hivyo katika Mikoa ya Kagera, Kigoma, Mwanza na Dar es Salaam. Aidha, kwa sasa Wizara inaratibu maandalizi ya uanzishaji wa vituo vitano (5) vya Operesheni ya matukio ya Dharura katika mikoa ya Songwe, Dodoma, Katavi, Mtwara na Iringa ili kuimarisha ufanisi wa kukabiliana na dharura katika Mikoa hiyo.
  2. Kuratibu utekekelezaji wa ununuzi na ufuatiliaji wa usimikaji wa Mitambo saba (7) ya kuzalisha na kujaza hewa tiba ya oksijeni chini ya fedha za Benki ya Dunia. Mitambo hiyo imesimikwa katika Hospitali za rufaa za Mikoa ya Amana (DSM), Ligula (Mtwara), Mbeya, Dodoma, Geita, Manyara na Songea (Ruvuma). Mitambo mingine 12 imeshanunuliwa na Serikali na inaendelea kufungwa katika Hospitali za Rufaa za Mikoa ya Sekou Toure (Mwanza), Maweni (Kigoma), Katavi, Songwe, Sokoine (Lindi), Morogoro, Njombe, Simiyu, Musoma (Mara), Kitete (Tabora), Sumbawanga (Rukwa) na Shinyanga. Lengo la Wizara  ni kuhakikisha hospitali zote za Rufaa za

Mikoa, Taifa, Maalumu, Kanda na baadhi ya Hospitali za Wilaya zinakuwa na mitambo ya kuzalisha hewa tiba ya oksijeni ili kuondoa changamoto ya uhaba wa hewa tiba hiyo na kuimarisha huduma za Dharura na Maafa, ambapo jumla ya Mitambo 55 inatarajiwa kununuliwa na kusimikwa ifikapo Desemba, 2022 na,

  1. Kuratibu utekelezaji wa mradi wa mwendelezo wa huduma za msingi wakati wa dharura na majanga “Continued Essential Health services” unaotekelezwa kwa kushirikiana na OR – TAMISEMI pamoja na Shirika la Amref katika Mikoa 11 ya Dar es salaam, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Dodoma, Mwanza, Iringa, Njombe, Songwe na Mbeya. Zaidi ya Watumishi wa afya 8,600 wamepata mafunzo ya tiba na kuzuia maambukizo ya ugonjwa wa UVIKO-19, Nakala 6000 za Miongozo ya Matibabu imesambazwa kwenye Vituo vya kutolea huduma za afya na Vituo 8 vimefanyiwa ukarabati wa majengo ya triage na kuwekewa vifaa. Vituo hivyo ni; Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Iringa, Kituo cha Afya cha Magugu (Manyara), Hospitali ya Mji ya Mafinga (Iringa), Hospitali ya Mji ya Kibena (Njombe), Hospitali ya Wilaya ya Makete (Njombe), Kituo cha Afya cha Ruanda (Mbeya) na Kituo cha Afya cha Tunduma (Songwe).

UDHIBITI WA UBORA WA HUDUMA ZA TIBA

  1. Mheshimiwa Spika, Katika kuimarisha  ubora wa huduma za Afya katika vituo vya kutolea huduma za Afya nchini, Wizara ilifanya uhakiki wa ubora wa huduma za matibabu (Clinical Audit) katika Hospitali 28 za Rufaa za Mikoa. Lengo ilikuwa ni kupata hali halisi (baseline) ya ubora wa huduma kwa kulinganisha na kiwango cha ubora cha utoaji wa huduma za Afya. Uhakiki huu ulionyesha wastani wa utoaji wa huduma bora ni sawa na asilimia 45 ambayo ni chini ya kiwango cha ubora kinachotakiwa. Wizara imeweka mikakati ya kuboresha maeneo yote yenye mapungufu na kuendelea kufanya uhakiki katika vituo vyote vya huduma. Sambamba na ubora wa huduma kwa ujumla, ubora wa huduma za Maabara umeendelea kuimarika ambapo jumla ya Maabara 48 zimepata ithibati ya Kimataifa na Maabara zingine 47 zipo katika hatua mbalimbali za mchakato wa kupata ithibati ya Kimatifa katika utoaji wa huduma bora za Maabara. 
  1. Mheshimiwa Spika, Tathmini ya kutoa nyota (Star Rating Assessment) kwenye Vituo vya Kutolea Huduma za Afya ya Msingi imefanyika kwenye Mikoa mitano (5) ya Kilimanjaro, Mtwara, Shinyanga, Singida na Songwe. Tathmini hiyo ilifanyika Novemba 2021 na imeonesha kuwa ubora wa huduma kwenye Mikoa hiyo unaendelea kuimarika ambapo vituo ambavyo vimepata nyota 0 viko chini ya asilimia 4 (isipokuwa kwa mkoa wa Njombe ambapo ni asilimia 8). Mkoa wa Kilimanjaro umefanya vizuri ukilinganisha na Mikoa mingine minne ambapo kwa Kilimanjaro Vituo vilivyopata nyota 3 au zaidi ni asilimia 27. Aidha, tathmini inaendelea kwenye Mikoa mingine mitano ya Katavi, Kigoma, Mara, Njombe na Rukwa. 
  1. Mheshimiwa Spika, katika  kuimarisha usalama wa  wagonjwa na watoa huduma katika vituo vya kutolea huduma za afya,  Wizara imeendelea kutekeleza afua mbalimbali zenye lengo la  kukinga na kudhibiti Maambukizo (Infection Prevention and Control). Katika kipindi cha kuanzia Julai, 2021 hadi Machi, 2022, tathmini na mafunzo maalumu

(mentorship) yalifanyika katika Hospitali 37 za rufaa, ikijumuisha Hospitali za Rufaa za Mikoa 28, Hospitali 4 za Rufaa za Kanda na Hospitali Maalum tano (5).  

RASILIMALI WATU KATIKA SEKTA YA AFYA

  1. Mheshimiwa Spika, uwepo wa watoa huduma za Afya ni moja ya nguzo muhimu inayohitajika kwa ajili ya kuwa na mfumo imara na fanisi kwa ajili ya utoaji wa huduma za Afya. Upatikanaji wa Rasilimali watu katika Sekta ya Afya upo katika kiwango cha asilimia 47 ya mahitaji yote na hivyo kuwepo kwa upungufu kwa kiwango cha asilimia 53. Moja ya sababu inayosababisha kuwepo na upungufu wa Watumishi ni pamoja na kasi kubwa ya ongezeko la vituo vya kutolea huduma za Afya ikilinganishwa na kasi ya ukuaji wa uchumi isiyoruhusu kuajiriwa kwa Watumishi wanaokidhi mahitaji halisi.
  1. Mheshimiwa Spika, pamoja na changamoto zinazoikabili Sekta ya Afya kutokana na upungufu wa rasilimaliwatu, Wizara imeendelea kuchukua hatua mbalimbali zenye lengo la kupunguza pengo kati ya upatikanaji wa Watumishi ikilinganishwa na mahitaji halisi. Katika kufikia azma hiyo, Wizara imeendelea

kuwasiliana na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na tunamshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kibali  cha ajira mpya kwa wataalam wa afya ambapokwa

mwaka   2022/23    jumla   ya   nafasi  za  ajira  10,285 zimetengwa. Hatua nyingine zinazoendelea kuchukuliwa ni pamoja na: kuandaliwa kwa mwongozo utakaotumika na vituo vya kutolea huduma za Afya kutoa ajira za mikataba ya muda mfupi kwa kutumia mapato ya ndani; kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika Sekta ya Afya kwa kuwashawishi kutumia sehemu ya rasilimali fedha zinazotumika katika kutekeleza program mbalimbali kugharamia ajira za muda mfupi kwa wataalam wa afya; na kuendelea kufanya upembuzi wa uzito wa majukumu katika kila kituo cha kutoa huduma za afya dhidi ya idadi ya watumishi kwa kila kituo na hatimaye kuwa na uwiano sahihi katika ngazi zote za utoaji huduma za afya. 

  1. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha uzalishaji wa wataalam wa afya wenye ujuzi na weledi unaotakiwa, Wizara imeendelea kuratibu uendeshaji wa Vyuo 44 vya Kada za Afya ngazi ya Kati pamoja na kushirikiana na Taasisi zinazosimamia uzalishaji wa wataalam katika ngazi ya vyuo vikuu. Aidha katika kusimamia uendeshaji wa Vyuo ngazi ya Kati, Wizara kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ilifanya uchaguzi wa wanafunzi 37,941 sawa na asilimia 62 ya wanafunzi 61,276 waliotuma maombi kujiunga na vyuo vya Afya ngazi ya kati katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022. Kati yao wanafunzi 4,768 sawa na asilimia 12.6 walichaguliwa kwenye vyuo vya Serikali vya afya na wanafunzi 33,173 sawa na asilimia 87 walichaguliwa kwenye vyuo binafsi na taasisi za dini katika program za Uuguzi na Ukunga na Sayansi Shirikishi za Afya. 
  1. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea na utaratibu wa kuwajengea uwezo watumishi katika Sekta ya Afya, ili kuimarisha na kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini. Katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022, Wizara kwa kushirikiana na wadau wa Maendeleo imefanikiwa kutoa fursa za mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu katika nyanja mbalimbali za ubingwa na ubobezi, ambapo jumla ya watumishi 783 wameendelea kulipiwa gharama za masomo ya uzamili (postgraduate studies) katika vyuo vikuu vya ndani watumishi 756 na nje ya nchi watumishi 27. Katika kipindi hicho, jumla ya wataalam bingwa 124 walihitimu mafunzo ya shahada ya uzamili kwa ufadhili wa Serikali ikilinganishwa na wataalam bingwa 137 ambao walihitimu mafunzo hayo mwaka 2020/21.

UGHARAMIAJI WA HUDUMA ZA  AFYA

  1. Mheshimiwa Spika, Upatikanaji na utoaji wa huduma za Afya nchini umeendelea kugharamiwa na fedha za ndani pamoja na wadau wa maendeleo wanaochangia katika Sekta ya Afya. Mwenendo wa ugharamiaji wa huduma katika Wizara umeonesha kuwepo kwa ongezeko la fedha za ndani kutoka shilingi 406,122,271,000.00 mwaka 2015/16 hadi shilingi 909,003,059,000.00 mwaka 2021/22 ambapo fedha za nje zimeendelea kupungua kutoka shilingi 374,618,452,000.00 mwaka 2015/16 hadi shilingi 125,130,236,000.00 mwaka 2021/22. Ni dhahiri kuwa mwenendo huo unaonyesha kutekeleza kwa vitendo dhamira ya Serikali inayolenga katika kugharamia afya za wananchi kwa kutumia vyanzo vya ndani.
  1. Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Sera ya Afya ya Mwaka 2007, wananchi wote wenye uwezo wa kiuchumi hutakiwa kuchangia gharama za huduma za afya pindi wanapozihitaji. Utaratibu wa uchangiaji unaotumika hivi sasa ni kwa kutoa fedha taslimu papo kwa papo au kulipa kabla ya kuugua na kupatiwa kadi ya bima ya afya ambayo hutumika pindi muhusika anapohitaji huduma za afya. Hata hivyo uzoefu umeonesha kuwa wananchi wanaotumia utaratibu wa malipo ya papo kwa papo wapo katika hatari ya kutopata huduma pindi wanapohitaji na wakiwa hawana fedha za kuchangia. Hadi Desemba 2021 jumla ya watanzania 9,094,624 sawa na asilimia 15 ya Watanzania wote ndiyo wanaonufaika na mfumo wa bima ya afya ambapo asilimia 85 wapo nje ya mfumo wa Bima ya Afya. Katika kutatua changamoto ya Watanzania wengi kuwa nje ya mfumo wa bima ya afya, Wizara inaendelea na maandalizi ya Muswada wenye lengo la kutunga sheria itakayowataka watanzania wote kujiunga na Bima ya Afya na hivyo kuwa na uhakika wa kupata huduma za afya pindi wanapozihitaji bila ya kikwazo cha fedha.   

MIRADI YA MAENDELEO

129. Mheshimiwa Spika, Wizara iliendelea na ujenzi na ukarabati wa vituo vya kutolea huduma za afya katika maeneo mbambali nchini. Jumla ya Miradi 22 ilikuwa inasimamiwa na Wizara katika maeneo mbalimbali hadi kufikia Machi, 2022. Miradi mitatu (3) imekamilika, miradi 12 inatarajiwa kukamilika ifikapo Juni, 2022 na miradi saba (7) itakamilika ifikapo

Desemba, 2022. Kwa upande wa Miradi inayogharamiwa na fedha za UVIKO-19 yote inatarajiwa kukamilika kati ya Mwezi Mei na Juni, 2022. Kwa Wastani utekelezaji wa miradi yote ya uboreshaji wa miundombinu ya kutolea huduma za Afya imefikia wastani wa asilimia 75. Taarifa ya kina ya utekelezaji wa miradi hiyo imeambatishwa katika taarifa hii (kiambatisho Na. 8)

D. UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA TAASISI ZILIZO CHINI YA WIZARA 

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)

  1. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai hadi Machi, 2022, Mfuko Taifa wa Bima ya Afya ulikuwa na lengo la kusajili wanachama wapya 489,058. Mfuko ulifanikiwa kusajili wanachama wapya 453,294 sawa na asilimia 93 ya lengo ikilinganishwa na wanachama 418,972 waliosajiliwa  katika kipindi  kama hiki mwaka 2021. Idadi hiyo ya wanachama waliosajiliwa, imewezesha Mfuko kuwa na wanachama wachangiaji 1,548,958 na wanufaika 4,826,978 sawa na asilimia 8 ya Watanzania wote hadi kufikia Machi, 2022. Serikali inaendelea na juhudi za kutoa elimu ya dhana ya bima ya afya na umuhimu wa kujiunga na bima ya afya kabla ya kuugua, ikiwa ni pamoja na kuimarisha mfumo wa bima ya afya nchini (NHIF na CHF) ili kuwawezesha Wananchi wengi kuwa na bima ya afya. 
  1. Mheshimiwa Spika, Vyanzo vikuu vya mapato ya Mfuko ni pamoja na michango ya wanachama, mapato yatokanayo na uwekezaji na mapato mengineyo. Katika kipindi cha Julai hadi Machi 2022, Mfuko ulikuwa na lengo la kukusanya fedha zitokanazo na michango ya wanachama shilingi bilioni  419.12. Mfuko ulifanikiwa kukusanya fedha za michango shilingi bilioni 356.75 sawa na asilimia 85 ya lengo.
  1. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha uboreshaji wa huduma za matibabu nchini, mfuko unatoa mikopo nafuu ya vifaa tiba, dawa na ukarabati wa vituo. Tangu kuanzishwa kwa mpango huu, jumla ya vituo 367 vimefaidika na utaratibu huu ambapo kiasi cha shilingi bilioni  35.33 zilitolewa kwa vituo vilivyokidhi vigezo. Katika kipindi cha kuanzia Julai hadi Machi 2022, shilingi bilioni 1.8 zilitolewa kwa vituo 21 vilivyokidhi vigezo. Utaratibu huu umesaidia kujenga uwezo wa vituo katika kutoa huduma za afya kwa wanachama na wananchi kwa ujumla. Mfuko unaendelea kuwahamasisha watoa huduma kutumia fursa hii ya mikopo katika kuboresha upatikanaji wa huduma za matibabu kwa wananchi. Aidha, majadiliano baina ya Mfuko na Bohari ya Dawa (MSD) yamefanyika kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma za afya nchini ambapo Mfuko utakuwa na jukumu la kutoa fedha za mikopo kwa vituo vya matibabu vitakavyoomba na MSD itakuwa na jukumu la kutoa vifaa tiba.
  1. Mheshimiwa Spika Mfuko umeendelea kuongeza mtandao zaidi wa vituo vya kutolea huduma za afya ambapo hadi Machi 2022, ulikuwa umesajili vituo 9,025 vya matibabu vya ngazi na umiliki wa watoa huduma mbalimbali mijini na vijijini ili kutoa huduma za matibabu kwa wanachama na wanufaika wa huduma zake nchi nzima ikilinganishwa na vituo 8,482 mwaka 2021. Kati ya vituo hivi, vituo vya Serikali ni  6,361 sawa na  asilimia 71, vituo vya Mashirika ya Dini ni  854 sawa na asilimia 9, na vituo vya watu binafsi ni  1,810 sawa na asilimia 20. 
  1. Mheshimiwa Spika, maeneo makubwa ya matumizi ya Mfuko ni malipo ya madai kwa watoa huduma na gharama za uendeshaji wa shughuli za Mfuko na Maendeleo. Mfuko umeendelea kutoa mchango katika uchangiaji wa gharama za matibabu katika Sekta ya afya ambapo kwa mwaka 2020/21 shilingi bilioni 540.55 zililipwa kwa watoa huduma. Katika kipindi cha kuanzia Julai hadi Machi 2022, jumla ya Shilingi bilioni 371.03 zililipwa kwa vituo vya kutolea huduma ikilinganishwa na shilingi bilioni 365.68 zilizolipwa mwaka 2021. Takwimu zinaonesha kuwa, fedha za NHIF kwa sasa zinachangia wastani wa asilimia 80 ya mapato ya vituo vya kutolea huduma za afya nchini. Katika kipindi husika, Mfuko umelipa madai kwa wastani wa siku 57 ambazo ni ndani ya matakwa ya Sheria, lengo ni kufikia wastani wa siku 45. Mfuko umeanzisha mfumo wa uwasilishaji na uchakataji wa madai kwa njia ya Kielekitroniki kwa lengo la kuhakikisha madai ya watoa huduma yanalipwa kwa wakati. Hadi Machi 2022, jumla ya watoa huduma 81 kati ya 9,025 waliosajiliwa na Mfuko walikuwa wamejiunga katika mfumo huu.
  1. Mheshimiwa Spika, Mfuko unaendelea kufanya kaguzi za mara kwa mara katika vituo vya kutolea huduma kwa lengo la kusimamia ubora wa huduma na kutoa elimu ya miongozo mbalimbali ya tiba inayotolewa na Serikali. Vilevile, ili kuhakikisha Mfuko unakuwa endelevu, utaendelea kufuata mapendekezo yanayotolewa na taarifa ya Tathmini ya uhai na uendelevu wa Mfuko (actuarial valuation).

Mamlaka ya  Dawa na Vifaa Tiba  (TMDA)

  1. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022, Mamlaka ilifanya tathmini ya maombi 714 ya usajili wa dawa za binadamu kati ya 868 sawa na asilimia 82 ya yaliyokuwepo katika kipindi husika. Maombi 421 kati ya maombi yaliyofanyiwa tathmini yaliidhinishwa na hivyo kusajiliwa. Aidha, maombi 293 ambayo hayakukidhi vigezo, wahusika walishauriwa kurekebisha maeneo yaliyokuwa na upungufu. Vilevile, Mamlaka ilipokea maombi 79 ya usajili wa dawa za mifugo ambapo maombi 71 yalifanyiwa tathmini na kati ya hayo maombi 58 sawa na asilimia 82 yalikidhi vigezo na hivyo kusajiliwa. Maombi 206 ya usajili wa vifaa tiba na vitendanishi yalipokelewa ambapo maombi 192 yalifanyiwa tathimini na kati ya hayo,  maombi 164 sawa na asilimia 85 yalikidhi vigezo vya usajili.  
  1. Mheshimiwa Spika, Mamlaka ilifanyia kazi maombi 496 ya usajili wa maeneo ya biashara ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi kati ya maombi 497 yaliyopokelewa. Maombi 467  sawa na asilimia 94 yaliyofanyiwa kazi yalikidhi vigezo na hivyo maeneo husika kusajiliwa na kupewa vibali vya kuanza biashara za bidhaa hizo. Aidha, Mamlaka ilifanya ukaguzi wa viwanda vipya vitatu (3) vya uzalishaji dawa ndani ya nchi ambapo viwanda vyote vilikidhi vigezo vya uzalishaji. Vilevile, Mamlaka ilifanya ukaguzi wa viwanda tisa (9) vya uzalishaji  wa vifaa aina ya barakoa na vyote vilikidhi vigezo na kupewa usajili. Maeneo 7,291 yanayojihusisha na biashara ya dawa, vifaa tiba na vitendanishi yalifanyiwa ukaguzi ambapo maeneo 6,351 sawa na asilimia 87 yalikidhi vigezo. Maeneo ambayo hayakukidhi vigezo yalipewa maelekezo ya kufanya marekebisho stahiki.
  1. Mheshimiwa Spika, jumla ya Sampuli 2,930 kati ya Sampuli 3,272 sawa na asilimia 90 za bidhaa za dawa, vifaa tiba na vitendanishi zilichunguzwa ambapo Sampuli 2,862 sawa na asilimia 98 zilikidhi vigezo. Bidhaa ambazo Sampuli zake hazikukidhi vigezo hazikusajiliwa na nyingine kuondolewa kwenye Soko kwa njia ya ukaguzi. Kiwango cha asilimia 98 cha bidhaa za dawa, vifaa tiba na vitendanishi zilizokidhi vigezo kwa kipindi hiki, kinaashiria uhakika wa uwepo wa bidhaa bora na salama kwenye soko kwa watumiaji. Katika kulinda afya za watumiaji wa bidhaa za dawa, Mamlaka ilisimamia uteketezaji wa tani 1,234.15 za bidhaa za dawa na vifaa tiba zenye thamani ya takriban shilingi bilioni 5.33 kutokana na kutokidhi vigezo vya ubora na usalama hivyo kutofaa kwa matumizi ya binadamu. 
  2. Mheshimiwa Spika, Mamlaka iliendelea kudhibiti ubora wa bidhaa za dawa, vifaa na vifaa tiba vinavyoingizwa au kusafirishwa nje ya nchi. Katika kipindi hicho, jumla ya maombi 7,573 ya kuingiza nchini bidhaa za dawa, vifaa na vifaa tiba, vitendanishi na malighafi ya kutengeneza dawa nchini yalipokelewa na kufanyiwa tathmini ambapo maombi 6,837 sawa na asilimia 90 yalikidhi vigezo na kuidhinishwa. Aidha, Mamlaka ilipokea na kufanyia kazi jumla ya maombi 732 ya kusafirisha nje ya nchi bidhaa za dawa na vifaa tiba ambapo maombi 674 sawa na asilimia 92 yalikidhi vigezo na hivyo kuidhinishwa. 

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa

Serikali (GCLA)

  1. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi 2022, jumla ya sampuli  mbalimbali 70,981 zilizopokelewa sawa na asilimia 115 ya lengo. Sampuli zilizochunguzwa ni 64,685 sawa na asilimia 91 ya sampuli zilizopokelewa. Ongezeko la sampuli zilizopokelewa limetokana na kuwepo kwa kazi maalum zilizotekelezwa na vikosi kazi vya vyombo vya ulinzi na usalama. Matokeo ya uchunguzi wa Kimaabara yameendelea kuchangia katika utoaji wa haki na ulinzi wa Afya za Wananchi na mazingira.

Aidha, katika kipindi husika ukaguzi wa Maghala, usajili wa Wadau wa Kemikali na utoaji wa vibali ulifanyika, ambapo jumla ya kampuni 438 zinazojihusiha na kemikali zilisajiliwa sawa na asilimia 82 ya lengo na jumla ya vibali 31,333 vya kemikali vilitolewa sawa na asilimia 180 ya lengo. Maghala yaliyokaguliwa yalikuwa 1,000 sawa na asilimia 114 ya lengo. Ukaguzi umeimarisha utekelezaji wa sheria na kuchangia kulinda usalama wa Afya ya binadamu na mazingira.

  1. Mheshimiwa Spika, katika kipindi hiki, Mamlaka imeendelea na ujenzi wa jengo lenye ghorofa nne (4) la Ofisi ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Makao Makuu ya nchi Dodoma. Ujenzi huu unagharimu shilingi bilioni 8.14 na ulianza mwezi Julai 2021 na unategemewa kukamilika mwezi Julai 2022. Hadi kufikia mwezi Machi, 2022 ujenzi ulikuwa umefikia asilimia 45. Pia, Mamlaka imeendelea kutoa elimu kwa wadau ambapo jumla ya Wadau 9,360 walielimishwa juu ya majukumu ya Mamlaka na wajibu wa Wadau katika kutekeleza Sheria, taratibu na kanuni zinazosimamiwa na Mamlaka.
  1. Mheshimiwa Spika, katika kipindi hiki Mamlaka iliweza kufanya tafsiri ya Sheria tatu zinazotekelezwa chini ya Mamlaka kutoka lugha ya Kiingereza kwenda lugha ya Kiswahili ili kuweza kutoa uelewa mpana wa sheria hizo na kurahisisha utekelezaji wake. Sheria hizo ni: Sheria ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Sheria Na.8 ya Mwaka 2016; Sheria ya udhibiti wa Vinasaba vya Binadamu, Sheria Na.8 ya Mwaka 2009; na Sheria ya usimamizi na udhibiti wa Kemikali za Viwandani na

Majumbani, Sheria Na.3 ya Mwaka 2003.`

Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR)

  1. Mheshimiwa Spika, Taasisi ya Utafiki wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) imeendelea kufanya tafiti mbalimbali zinazolenga kupambana na magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza, pamoja na kuimarisha mifumo ya afya. Katika kipindi hiki miradi 120 iliendelea kutekelezwa ikilinganishwa na lengo la mwaka la kutekeleza miradi 135. Taasisi ilikamilisha utafiti wa usalama na ufanisi wa dawa za tiba asili za NIMRCAF, Covidol, Convotanxa, Bingwa, Planet ++,

Uzima na Bupiji kwa wagonjwa wa UVIKO-19.  Matokeo yalionesha kuwa, hakukuwa na matatizo kwenye figo au ini kwa wagonjwa wa UVIKO-19 waliotumia dawa hizi; Utafiti mwingine uliangalia uwezo na utayari wa wananchi kulipia bima ya afya ili kufikia malengo ya upatikanaji wa afya kwa wote. Matokeo yalionesha kuwa asilimia 73 ya Wananchi walioshiriki katika utafiti huu walionesha utayari wa kujiunga na mifuko ya bima ya afya. 

  1. Mheshimiwa Spika, Taasisi iliendelea kutekeleza tafiti zingine ikiwa ni pamoja na; Utafiti wa usalama na ufanisi wa chanjo ya TANCoV 1.3.20 ya UVIKO-19 iliyotengenezwa hapa nchini; Utafiti wa kufuatilia hali ya maambukizi ya malaria nchini kwa kutumia mbinu za vinasaba katika Mikoa 13 ya Tanzania bara; Utafiti unaolinganisha utoaji huduma wa pamoja kwa magonjwa ya VVU, kisukari na shinikizo la damu na mfumo wa utoaji huduma unaotumika sasa (Integrated diabetes, hypertension and HIV care); Utafiti wa majaribio ya chanjo ya VVU ulienda sambamba na utafiti wa dawa kinga za TAF/FTC na TDF/FTC kwa watu walio katika hatari ya kupata maambukizi ya VVU ( PrEPVacc TRIAL). Kwa ujumla, muda wa kukamilika kwa tafiti zinazoendelea ni kati ya mwaka mmoja hadi miaka mitano ambapo Taasisi imejipanga kutoa matokeo pindi hizo tafiti zitakapokamilika.
  1. Mheshimiwa Spika, Taasisi ilipokea na kuratibu tathmini za maadili na usalama kwa maombi ya tafiti 213 ikilinganishwa na lengo la mwaka la tafiti 275 sawa na asilimia 77. Katika maombi haya, zaidi ya asilimia 21 ya tafiti hizi zililenga kwenye Mifumo ya afya, asilimia 12 magonjwa yasiyoambukiza, asilimia 9 UKIMWI, asilimia 10 Malaria, asilimia 8.5 UVIKO-19, na asilimia 10 Kifua Kikuu. Miradi hii imelenga kutoa majibu na takwimu zinazohusu magonjwa ya Malaria, Virusi vya Ukimwi (VVU), Kifua kikuu, Magonjwa ya kitropiki yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, na magonjwa yasiyoambukiza. 
  1. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa uzalishaji wa dawa za tiba asili, Taasisi imeendelea na utekelezaji wa ujenzi wa jengo la uzalishaji wa dawa za tiba asili katika eneo la Mabibo Dar es Salaam, ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 95. Kwa sasa Taasisi inaendelea na taratibu za usimikaji wa Mitambo ya Uzalishaji.

 Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC)

  1. Mheshimiwa Spika,Taasisi ya Chakula na Lishe inajukumu la kuratibu na kuishauri Serikali kuhusu namna bora ya kuimarisha huduma za lishe nchini. Katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi 2022,Taasisi imetekeleza miradi Mitano (5) ya kiutafiti inayolenga kutatua changamoto za hali duni ya lishe (utapiamlo) katika Jamii. Miradi hiyo ni pamoja na “Food Intake Survey Among Non-Pregnant Lactating

Women Of Reproductive Age In Mbeya Region”, “Barriers of Health-Seeking Behaviours Among Parents or Caregivers of Children Who Suffer From Severe Acute Malnutrition In Tanzania”, “Assessment of Food Taboos and Preferences in Mainland Tanzania and Zanzibar”,  “Definining the Optimal Standards for Iodized Salts” na “The Efficacy of a developed Ready to Use (RUTF) Therapeutic Food for Children aged 6 – 59 months in Dodoma and Singida Regions.

  1. Mheshimiwa Spika, Pamoja na miradi hii ya utafiti iliyoorodheshwa hapa juu Maabara ya Taasisi imeteuliwa na imeanza kufanya uchambuzi na kuchakata Sampuli zinazohusu viashiria vya chakula na lishe katika Utafiti wa Taifa wa Afya na Demografia (Tanzania Demographic and Health Survey 2021/22) ambao unaendelea nchi nzima. Uamuzi huu umetokana na Taasisi kujiimarisha zaidi katika eneo la uchambuzi wa Kimaabara kwa kununua mashine mpya ya kisasa ijulikanayo kama “Cobas Integra+”  ambayo ina uwezo mkubwa wa kuchakata Sampuli za aina tofauti na kutoa matokeo ya viashiria vingi kwa usahihi na kwa muda mfupi.
  1. Mheshimiwa Spika, ili kuimarisha afua za kukabiliana na  tatizo la upungufu wa vitamini na madini, katika kipindi hiki Taasisi kwa kushirikiana na

Wadau wa maendeleo, kupitia VETA imenunua mashine tano (5) za kuchanganya madini joto katika chumvi zenye thamani ya Shilingi Milioni 55 ambazo zimesambazwa katika Mikoa mitatu (3) na

Halmashauri Tano (5); Tanga (Halmashauri za Tanga Jiji na Mkinga), Pwani (Halmashauri za Bagamoyo na Mkuranga) na Mtwara (Halmashauri ya Mtwara

Vijijini). Aidha, kwa kutengeneza mashine hizi ndani ya nchi, Serikali imeweza kuokoa takribani Shillingi Millioni 80.

  1. Mheshimiwa Spika, Taasisi kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu imeratibu uandaaji na uzinduzi wa Mpango Jumuishi wa Pili wa Taifa wa masuala ya lishe (2nd National Multisectoral Nutrition Action Plan 2021-2025) ambao unatoa Mwongozo kwa Wadau wote kuhusu vipaumbele katika utekelezaji wa afua za lishe katika kipindi cha miaka mitano (5) ijayo. Uzinduzi wa mpango huu ulifanyika sambamba na uzinduzi wa Mkakati wake wa kutafuta Rasilimali fedha (Resouce Mobilization Stratergy). Pia, katika kipindi hiki Taasisi imeendelea kuratibu maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Lishe ambapo kwa mwaka huu wa fedha hafla ya kilele cha maadhimisho ilifanyika Mkoani Tabora.  

E. MABARAZA YA WANATAALUMA NA BODI ZA   USHAURI ZA AFYA 

151. Mheshimiwa Spika, Wizara ina jukumu la kusimamia utendaji wa wataalam wa Sekta ya Afya. Katika kutekeleza hilo mabaraza na bodi mbalimbali za kitaaluma ziliundwa kisheria kwa ajili ya kusimamia majukumu hayo. Mabaraza na bodi za kitaaluma ni pamoja na; Baraza la Madaktari Tanganyika, Baraza la Afya Mazingira, Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Baraza la Uuguzi na Ukunga, Baraza la Famasia, Baraza la Wataalam wa Macho, Baraza la Radiologia, Baraza la Wataalam wa Maabara, Bodi ya Maabara Binafsi za Afya (PHLB) na Bodi ya Ushauri ya Hospitali Binafsi. Katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022 Mabaraza na bodi hizi zimetekeleza majukumu yafuatayo:-

Baraza la Madaktari Tanganyika

  1. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022, Baraza limesajili wanataaluma wa kada mbalimbali kama ifuatavyo; Madaktari na

Madaktari        wa     Kinywa     Watarajali       (Provisional

Registration) 1,494;Uhuishaji wa Usajili (Retention) ya Madaktari na Madaktari wa Kinywa 15; na Usajili wa Kudumu (Full registration) Madaktari na Madaktari wa kinywa 2,395. Hadi kufikia Machi, 2022, Jumla ya madaktari 26,090 wamesajiliwa na Baraza.  

  1. Mheshimiwa Spika, Baraza liliendesha na kusimamia Mitihani ya kabla ya utarajali (Preinternship examinations) iliyofanyika katika Vituo vitano ambavyo ni Dodoma, Kilimanjaro, Mbeya, Dar es Salaam na Mwanza. Mitihani hii ilihusisha Watahiniwa 1,198 kutoka katika Vyuo tisa (09) nchini, ambapo Madaktari walikua 1,153 na Madaktari wa Meno walikua 36.
  1. Mheshimiwa Spika, katika kipindi hicho, Baraza liliendesha na kusimamia mtihani wa baada ya utarajali (post-internship examination) iliyofanyika katika vituo 6 ambavyo ni Dodoma, Mbeya, Kilimanjaro, Mwanza, Dar es Salaam na Pwani. Mitihani hii ilihusisha watahiniwa 2,186 kutoka katika vyuo 9 Nchini kwa mchanganuo ufuatao; Madaktari walikuwa 2,084, Madaktari wa meno walikuwa 43, Physiotherapist walikuwa 26, Prosthetics and Orthotics walikuwa 12 na Clinical Psychiatrists 21 
  1. Mheshimiwa Spika, Baraza limefanya uhamasishaji wa mafunzo endelevu ya kitaaluma kuanza kutekelezwa na wanataaluma ambapo kwa kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022, Baraza kupitia Kamati ya Mafunzo Endelevu ya kitaaluma (CPD Committee) imefanya uhamasishaji kwa wanataaluma mbalimbali katika ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam, Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Mkoa wa Mbeya,

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Mwanza, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora-Kitete, Arusha Lutheran Medical Centre na Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru – Arusha. Lengo la vikao hivi ni kuhamasisha wataalamu juu ya usajili na utoaji wa Mafunzo Endelevu ambapo Baraza limeweza kusajili jumla ya Taasisi 21 zitakazotoa kozi mbalimbali za

Mafunzo Endelevu

  1. Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022, Baraza limesikiliza jumla ya Mashauri 34 ya uvunjifu wa maadili ya kitaaluma. Baada ya kusikiliza mashauri hayo, Baraza limefanya maamuzi ya Mashauri hayo kwa kuzingatia Sheria ya Madaktari wa Meno na Wataalamu wa Afya Shirikishi Sura Na. 152 ya mwaka 2017 pamoja na kanuni zake, ambapo mashauri 11 yameshafanyiwa maamuzi, na mashauri 23 uchunguzi bado unaendelea.

Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania

  1. Mheshimiwa Spika, Baraza limeendelea kutekeleza majukumu yake kufuatana na mpango kazi ambapo katika kipindi cha Julai 2021 mpaka Machi 2022 Baraza limefanikiwa kusajili jumla ya Wauguzi na Wakunga wapya 4,567 wenye sifa ambao ni sawa na asilimia 82 ya wote waliyotarajiwa kusajiliwa. Aidha Wauguzi na Wakunga wanaendelea kuhuisha leseni zao, ambapo kati ya Julai 2021 hadi Machi 2022, Jumla ya Wauguzi na Wakunga 1,148 wamehuisha leseni zao kwa wakati na jumla ya Watarajali 571 wanaendelea na mafunzo yao katika vituo mbalimbali. Hivyo hadi Machi 2022 baraza lina jumla ya wauguzi na wakunga waliosajiliwa 47,973.
  1. Mheshimiwa Spika, Baraza limeendelea kuratibu, kuhamasisha na kufuatilia mafunzo ya kujiendeleza kazini (CPD) kwa Wauguzi na Wakunga kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na njia ya mtandao na masomo yanayoandaliwa katika Taasisi za mafunzo. Katika kipindi cha Julai, 2021 mpaka Machi,

2022 jumla ya wauguzi na wakunga 4,695 wamehudhuria mafunzo mbalimbali yakiwemo ya huduma bora kwa mteja (customer care), weledi wa kuhudumia wagonjwa mbalimbali, uwekaji wa kumbukumbu sahihi (documentation) na maadili ya wanataaluma. 

159. Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi 2022, Baraza lilipokea tuhuma mbalimbali za ukiukwaji wa maadili kutoka katika Mikoa wa Dar es Salaam, Arusha, Dodoma na Ruvuma. Baraza lilichunguza na kusikiliza tuhuma hizo na kufanya maamuzi kama ifuatavyo: Tuhuma 10 zilifanyiwa maamuzi ambapo Muuguzi mmoja (1) alikutwa na hatia na alisimamishwa kazi kwa muda wa miaka mitatu (3), Muuguzi mmoja (1) alipewa onyo la maandishi, Wauguzi wawili (2) walipewa karipio, Wauguzi wanne (4) mashauri yao yatasikilizwa tena, Muuguzi mmoja (1) aliachiwa huru na Muuguzi mmoja (1) shauri lake lipo kwa Afisa Ustawi wa Jamii. Mashauri mapya manne (4) yaliyopokelewa katika kipindi hiki, bado yapo katika hatua mbalimbali za kushughulikiwa. 

Baraza la Famasia

  1. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022, Baraza lilisajili jumla ya wanataaluma 1724 ambapo kati yao Wanataaluma 1359 (wafamasia 397, fundi dawa sanifu 918 na fundi dawa wasaidizi 44) walipatiwa usajili wa kudumu, na Wafamasia 365 walipatiwa Usajili wa muda

(Provisional Registration). Hivyo hadi Machi 2022, Baraza lina jumla ya wanataaluma 8,580 (8,215 wamepata usajili wa kudumu na 365 wana usajili wa muda). Kati ya 8,215 wenye usajili wa kudumu, wafamasia ni 2998, Fundi dawa 4432 na fundi dawa Wasaidizi 785).  

  1. Mheshimiwa Spika, Vilevile, katika kipindi hiki, Baraza lilifanya ukaguzi katika majengo 2,199. Kati ya hayo, 960 ni majengo mapya, na 1,239 ni maduka ya dawa muhimu yanayotoa huduma. Kati ya maeneo mapya yaliyokaguliwa maeneo 533 yalikidhi vigezo na kuruhusiwa kuendelea na biashara. Maeneo ambayo hayakukidhi vigezo wamiliki walishauriwa kurekebisha upungufu ulioonekana. Vilevile, Baraza lilihuisha vibali 2,082 na hakuna vibali vya maduka ya famasi vilivyofutwa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo ukiukwaji wa utaratibu wa uendeshaji wa maduka hayo. Vilevile, ilani za kufunga famasi (closure order) ziliandikwa kwa famasi 196.
  1. Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi 2022, Baraza limeratibu mitihani ya usajili kwa waombaji 4,029 wakiwemo Wafamasia 694, Fundi dawa sanifu 3,000, Fundi dawa wasaidizi 292 na

Watoa dawa 43 wa mwaka mmoja. Kati yao, watahiniwa 1782 (Wafamasia 491, Fundi dawa sanifu 1,136, Fundi dawa wasaidizi 134 na Watoa dawa 21) waliofanya mitihani katika Mwezi oktoba 2021, jumla ya watahiniwa 847 (47.5%) walifaulu na kupatiwa Leseni za utendaji kazi za taaluma, wakiwemo wafamasia 350, Fundi dawa Sanifu 487, Fundi dawa wasaidizi 6 watoa dawa 4 na hivi sasa wanatoa huduma katika maeneo mbalimbali nchini. Watahiniwa 2,245 wakiwemo wafamasia 203 Fundi dawa sanifu 1,864, Fundi dawa wasaidizi 158 Watoa dawa 22 walifanya mitihani yao mwezi Februari 2022, na matokeo ya watahiniwa hawa yanasubili kuidhinishwa na Bodi. Katika kuimarisha usimamizi wa dawa nchini naomba kuujulisha umma wa Tanzania kuwa Wizara inasitisha kwa muda Mafunzo ya ADDO kuanzia tarehe 1 Julai 2022.  

Baraza la Wataalam wa Maabara

  1. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022, Baraza limetoa usajili na leseni kwa Wataalam 5,111 na hivyo kuwa na jumla ya Wataalam wa Maabara 22,348 waliosajiliwa. Kati ya Wataalam waliopewa usajili kati ya kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi 2022, Wataalamu 1,303 walipewa usajili wa awali, na Wataalamu 748 walipewa usajili wa kudumu. Vilevile, Baraza liliandikisha Wataalamu 217 katika ngazi ya Cheti, na Wataalamu 2,843 wa kada ya afya ambao wanatoa huduma za Kimaabara, lakini sio Wataalamu waliosomea Maabara, kwa ajili ya kutoa huduma za upimaji wa vipimo vya haraka walipewa leseni za upimaji.
  1. Mheshimiwa Spika, Baraza limefanya ukaguzi katika Vyuo vitatu (3) ambavyo ni Kibaha College of Health and Allied Sciences, Mwanza City College na Arusha City College kwa ajili ya kuanzisha kozi ya Maabara kwa ngazi ya Astashahada na Stashahada. Kati ya Vyuo hivyo, Vyuo viwili (2) ambavyo ni Kibaha College of Health and Allied Sciences na Mwanza City College havikukidhi vigezo vya kupewa kibali cha kutoa mafunzo hayo kutokana na mapungufu makubwa yaliyobainika. Chuo cha Arusha City College kilikidhi vigezo vya kupewa kibali cha kuanzisha kozi ya Maabara na hivyo sasa kuwepo kwa jumla ya Vyuo 46 vinavyotoa mafunzo hayo. 
  1. Mheshimiwa Spika, Jumla ya Vyuo 7 vilifanyiwa ukaguzi shirikishi wa kufuatilia ubora wa utoaji wa mafunzo. Vilevile, Baraza limewatahini Wataalamu wa Maabara kwa ngazi ya Astashahada Wataalam 256, Stashahada Wataalamu 1,468 na Shahada Wataalamu 387 kwa ajili ya usajili wa leseni za kudumu.

Baraza la Wataalamu wa Radiolojia

  1. Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi 2022, jumla ya maombi 321 yalipokelewa kwa ajili ya usajili, uandikishaji na uorodheshaji wa Wataalamu wa Radiolojia. Maombi 312 yalipitishwa na kupata usajili, na maombi 9 hayakukidhi vigezo. Aidha, jumla ya Wataalamu 1,000 kati ya 1,647 wamehuisha leseni zao. Vilevile, Watarajali 59 walisajiliwa na kupangiwa vituo vya kufanyia mazoezi kwa vitendo (Watarajali 28 kwa mwaka wa fedha 2020/2021 na Watarajali 31 kwa mwaka wa fedha 2021/2022). Kundi la kwanza lilimaliza mwezi Oktoba 2021 na kundi la pili lilianza Novemba 2021 na ukaguzi wa Watarajali umekuwa ukifanyika kila baada ya miezi mitatu. 
  1. Mheshimiwa Spika, katika kusimamia maadili na miiko ya taaluma ya Radiolojia, jumla ya Mashauri matatu ya uvunjifu wa Miiko na Maadili ya Taaluma yaliripotiwa. Mashauri mawili yalijadiliwa kwenye kikao cha Kamati ya nidhamu ya Baraza na kutolewa maamuzi. Aidha, shauri la tatu lipo katika ngazi ya Mahakama.  Baraza limekuwa likifuatilia Wataalamu wake kupitia ukaguzi shirikishi katika maeneo mbalimbali. Katika kipindi hiki Baraza liliweza kutembelea Vyuo vyote vinavyotoa mafunzo ya Radiolojia kwa Kada mbalimbali na kutoa elimu juu ya Miiko na Maadili. Baraza limekamilisha mfumo wa usajili wa Wataalamu (Health Practioners Registration System) ambapo Wataalamu wameanza kupata mafunzo ya namna ya kuutumia mfumo huo.

Baraza la Afya Mazingira

  1. Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi 2022 Baraza limesajili Wataalamu wapya 132, Waliohuisha leseni 1,183, na Usajili wa awali (provisional registration) 99. Aidha Baraza limefanya usimamizi elekezi na shirikishi katika Vyuo vitano (5) vinavyotoa mafunzo ya Sayansi ya Afya Mazingira kwa lengo la kutoa elimu ya masuala ya usajili na leseni kwa Wanafunzi wanaoelekea kuhitimu, wafanyakazi (Wakufunzi) wa vyuo husika na kufanya ufuatiliaji wa Watarajali 63 waliokuwa wakifundisha katika Vyuo hivyo ili kujua maendeleo, changamoto na kuzitafutia ufumbuzi. Hivyo hadi

Machi 2022 Baraza lina jumla ya wanataaluma 4,002 waliosajiliwa.

  1. Mheshimiwa Spika, Baraza limetengeneza Mtaala unaojitegemea wa elimu ya kujiendeleza (CPD) na nyenzo za kufanyia tathimini. Aidha, majukumu mengine yaliyotekelezwa na Baraza ni pamoja na: kufanya majaribio ya mfumo mpya wa usajili wa kieletroniki na kuanza zoezi la kuingiza taarifa za wataalamu 1,627 waliosajiliwa ili waanze kutambuliwa na mfumo huo; Kushiriki katika utekelezaji wa Kampeni ya usafi wa mazingira; na kuandaa Mwongozo wa ufundishaji wa masuala ya afya na mabadiliko ya tabia ya nchi ambao utatumika na Vyuo vya Afya Mazingira nchini.
  1. Mheshimiwa Spika, Baraza limefanya ufuatiliaji na usimamizi elekezi katika Mikoa ya Ruvuma, Songwe, Mtwara, Singida, Arusha, Tabora, Manyara na Kilimanjaro kwa lengo la kufuatilia tuhuma za uvunjifu wa maadili, kusimamia watarajali waliopo katika mikoa tajwa na kuhimiza masuala ya Usajili wa wataalamu, vikundi na taasisi zinazotoa huduma za afya Mazingira na uhuishaji wa leseni za wataalamu wa Mikoa husika na kutoa elimu kwa Maafisa Afya wa Mikoa tajwa juu ya mfumo mpya wa kujisajili kwa njia ya kielektroniki.  
  1. Mheshimiwa Spika, Baraza limeendelea kutoa elimu ya masuala ya kuzingatia maadili na miiko ya kada kama sheria inavyosisitiza, kazi hii inafanyika kwa ushirikiano kati ya Baraza, Chama cha Maafisa Afya (CHAMATA) na Maafisa Afya wa Mikoa na Halmashauri kwa kusisitiza Wataalamu kufanya kazi kwa weledi na uaminifu pasipo kuvunja miiko na maadili ya kada. Ambapo kwa kipindi cha Mwezi Julai, 2021 hadi Machi, 2022 mashauri ya uvunjifu wa maadili yaliyoshughulikiwa ni matatu (3).

Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala

  1. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi 2022, Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala limesajili jumla ya Waganga wa tiba asili na tiba mbadala pamoja na wasaidizi wao 3,271, vituo vya kutolea huduma za tiba asili 91, dawa za asili 8 na uhuishaji wa leseni kwa Waganga wa tiba asili 707. Aidha, katika kipindi hicho Baraza limeendelea kusimamia, kuratibu na kuendeleza huduma za tiba asili na tiba mbadala ambazo ni miongoni mwa huduma za afya zinazotolewa hapa nchini. Hivyo hadi Machi 2022 baraza lina jumla ya waganga wa

Tiba Asili na Tiba Mbadala 31,064 waliosajiliwa

  1. Mheshimiwa Spika, Baraza liliendesha zoezi maalumu la uhamasishaji na utengenezaji wa leseni za Waganga wa tiba asili kwa papo hapo, zoezi hili lilifanyika katika mikoa ya Simiyu na Shinyanga ili kupunguza changamoto ya Waganga wengi kufanya kazi bila kuwa na leseni. Katika zoezi hili lililofanyika katika Halmashauri zote za mikoa ya Simiyu na Shinyanga jumla ya Waganga 2,742 walisajiliwa.
  1. Mheshimiwa Spika, Baraza lilifanya ukaguzi katika vituo vya kutolea huduma za Tiba Mbadala mkoa wa Dar es Salaam ambapo watoa huduma 105 na vituo 82 vya kutolea huduma za tiba mbadala (Masaji) walifikiwa na kuelimishwa juu ya sheria na taratibu za usajili wa vituo na watoa huduma. Katika zoezi hili ilibainika kuwa watoa huduma za tiba mbadala (masaji) hawakuwa na uelewa juu ya mamlaka inayowasimamia na taratibu wanazopaswa kuzifuata kwa mujibu wa sheria ili kuendesha huduma zao kama sehemu za tiba mbadala zilizorasimishwa.
  2. Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022 Baraza kupitia kamati ya maadili imefanyia kazi mashauri matatu ya uvunjifu wa maadili ambayo yamewasilishwa kwenye kikao cha kisheria cha Baraza kwa ajili ya kufanyiwa maamuzi. Mashauri hayo yanahusika na; Uchakachuaji wa dawa asili zinazoombewa usajili (Adulteration) na dhuluma ya haki miliki ya ugunduzi wa dawa asili.
  1. Mheshimiwa Spika, Katika kuhakikisha taaluma ya tiba asili na tiba mbadala inasimamiwa na kukuwa, Baraza limeendelea kutoa mafunzo kwa waratibu wa tiba asili na tiba mbadala ngazi ya halmashauri na mikoa juu ya sheria, kanuni, miongozo na taratibu mbalimbali ili waratibu hao ambao ndiyo wasimamizi wa shughuli za tiba asili katika maeneo yao wakawe chachu ya usimamizi na uendelezaji wa tiba asili.

Bodi ya Ushauri ya Hospitali Binafsi

  1. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022, Bodi ya Ushauri ya Hospitali binafsi imesajili Hospitali Binafsi 250, kati ya Vituo hivyo, Vituo 230 viliomba usajili mpya, viliomba kupandishwa hadhi na vituo 3 viliomba kuongeza huduma. Katika Vituo vilivyoomba kusajiliwa, Vituo 5 viliomba kusajiliwa katika Hospitali ngazi ya mkoa, 4 ngazi ya Wilaya, 6 huduma ya kuchuja damu, 115 usajili wa Clinic aina mbalimbali, 10 ngazi ya Vituo vya

Afya na 104 ngazi ya Zahanati. Aidha, Bodi imeidhinisha Mashirika 95 kati ya 98 yaliyoomba kusimamia na kuendesha Vituo vya kutolea huduma za afya. 

  1. Mheshimiwa Spika, katika kusimamia utoaji wa huduma bora kulingana na Sheria, Kanuni, Miongozo na taratibu Bodi ya Ushauri ya Hospitali binafsi ilifanya ukaguzi wa Hospitali Binafsi 366 katika mikoa ya Arusha, Tanga na Mbeya. Kati ya Vituo vilivyokaguliwa Vituo 39 vilisitishiwa huduma kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kutokuwa na usajili, kutokuwa na watumishi na miundombinu mibovu. 
  1. Mheshimiwa Spika, Bodi ilipokea tuhuma moja (1) ya ukiukwaji wa miongozo na sheria za usajili wa hospitali binafsi kutoka mkoa wa Iringa. Tuhuma hii ilifanyiwa kazi kwa pamoja na Bodi ya Hospitali Binafsi (PHAB), Bodi ya Vituo vya Maabara Binafsi (PHLB) na Kurugenzi ya Tiba na Kituo kilikutwa na makosa na hivyo kupewa adhabu. Mmiliki wa Kituo cha Afya ambaye pia ndiye mmiliki wa Chuo aliagizwa kutenganisha eneo la Chuo na kituo cha Afya. Mmiliki alipokea maagizo na kuahidi kuhamisha chuo kutoka kwenye Kituo cha Afya kwenda eneo jingine ndani ya miezi sita (6). 

Bodi ya Maabara Binafsi za Afya (PHLB) 

180. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022, Bodi ya Maabara Binafsi za Afya imesajili jumla ya Maabara Binafsi za Afya 346 na kufikia jumla kuu ya Maabara Binafsi za Afya 2,839 zilizosajiliwa kote nchini hadi mwezi Machi 2022. Aidha, katika kuhakikisha kuwa wamiliki wa maabara binafsi za Afya nchini wanazingatia sheria, kanuni na miongozo, Bodi imefanya ukaguzi shirikishi wa maabara za Mikoa ya Dodoma, Morogoro, Tanga, Mbeya na Iringa na jumla ya maabara 562 zilifikiwa.  181. Mheshimiwa Spika, Bodi ya Maabara Binafsi ya Afya pia ilitoa elimu ya ubora wa huduma za maabara, sheria, kanuni za maabara kwa wamiliki na watendaji wa maabara ili kuondoa mazingira hatarishi kwa mgonjwa, kuhakikisha wamiliki wanasajili maabara zao kwa mujibu wa Sheria Na. 10 ya 1997 na kanuni zake kuboresha huduma za maabara na pia kuhuisha leseni zao pindi zinapoisha muda wake. Bodi ya Maabara Binafsi za Afya imeweza kufanya mafunzo kwa waratibu wa huduma za maabara nchini katika Wilaya 49 za Mikoa 8. Katika mafunzo hayo  jumla ya Waratibu wa huduma za Maabara ngazi ya Wilaya 49 walipata nafasi ya kujengewa uwezo kuhusu sheria, kanuni na miongozo ya Bodi ya Maabara Binafsi za Afya.  Aidha, walielimishwa juu ya mbinu za ukaguzi, malipo ya tozo mbalimbali za Bodi kupitia mfumo wa malipo ya Serikali “GePG”, maadili ikiwa ni pamoja na kuepuka Rushwa na kutumia lugha nzuri kwa wateja kwa lengo la kuboresha huduma za maabara na vipimo kwa ustawi wa umma wa watanzania. 

F. VIPAUMBELE VYA WIZARA NA BAJETI YA

MAPATO, MATUMIZI YA KAWAIDA NA MIRADI YA

MAENDELEO      KWA         MWAKA    WA   FEDHA 2022/2023

182. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/23 Wizara ya Afya imejiwekea vipaumbele vifuatavyo ili kuboresha huduma za afya nchini: – 

  1. Kuimarisha utoaji wa huduma za chanjo kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano;
  1. Kusimamia viwango vya ubora wa huduma za kinga na tiba katika ngazi zote za utoaji huduma za afya nchini;
  2. Kuimarisha huduma za afya ya uzazi, mama na mtoto ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi, vifo vya watoto wachanga pamoja na mimba za utotoni, 
  3. Kuimarisha upatikanaji wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi katika ngazi zote za utoaji wa huduma za afya
  4. Kuimarisha huduma za lishe hususani kwa watoto wa umri wa chini ya miaka 5, vijana balehe na wanawake wa umri wa kuzaa; 
  5. Kuimarisha huduma za afya na usafi wa mazingira ili kudhibiti magonjwa ya kuambukizi na hivyo kupunguza idadi ya wagonjwa katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini;
  6. Kuimarisha miundombinu ya kutolea huduma za afya ikiwemo katika Hospitali za Rufaa za Mikoa,

Kanda, Maalum na Taifa; viii. Kuimarisha huduma za matibabu ya ubingwa na ubingwa bobezi;

  1. Kudhibiti magonjwa ya mlipuko, magonjwa ya kuambukiza na magonjwa yasiyo ya kuambukiza; 
  2. Kuimarisha utoaji wa mafunzo ya wataalamu katika Sekta ya Afya;
  3. Kuimarisha mifumo ya ugharamiaji wa huduma za afya nchini;
  4. Kuimarisha utawala bora na uwajibikaji katika utoaji huduma za afya; na
  5. Kuimarisha mifumo ya TEHAMA na matumizi ya takwimu katika utoaji wa huduma za afya nchini. 183.Mheshimiwa Spika, ili kutekeleza vipaumbele vilivyoanishwa katika mwaka 2022/23, Wizara imekadiria kutumia kiasi cha shilingi 1,109,421,722,000 zitakazotumika kutekeleza majukumu ya Wizara ikiwa ni pamoja na uendeshaji wa Ofisi na miradi wa maendeleo. Baadhi ya miradi ya maendeleo iliyotengewa fedha kwa mwaka 2022/23 ni pamoja na: –
  1. Kununua, kutunza, kusambaza na kutoa Chanjo kwa watoto nchini ambapo kiasi cha Shilingi 74,473,286,354 zimetengwa. 
  2. Kujenga Hospitali Maalum ya Mama na Mtoto Jijini Dodoma ili kuimarisha huduma za tiba kwa magonjwa ya wanawake na watoto ambapo kiasi cha shilingi bilioni 10 kimetengwa. Aidha kiasi cha shilingi bilioni 23.36 kimetengwa kwa ajili ya kujenga vyumba vya huduma za Watoto wachanga katika hospitali 100 za wilaya, kuwajengea uwezo watoa huduma kuwa na stadi, weledi na tabia bora katika kutoa huduma za mama na mtoto, kujenga, kuweka vifaa na watumishi wenye weledi kwenye ICU za Wazazi katika hospitali za Kanda  na mikoa 
  3. Kuwezesha Ununuzi wa dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi na kuzisambaza katika ngazi zote za utoaji wa huduma za afya ambapo kiasi cha shilingi bilioni 200 zimetengwa.
  4. Kukamilisha ujenzi wa Hospitali (5) za Rufaa za Mikoa katika Mikoa mipya ya Katavi, Geita, Njombe, Songwe na Simiyu ambapo jumla ya shilingi bilioni 18.6 kimetengwa.
  5. Kukamilisha ujenzi wa Hospitali mpya tatu (3) za Rufaa za Mikoa katika mikoa ya Shinyanga, Singida na Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere – Mara ambapo kiasi cha Shilingi bilioni 26 kimetengwa.
  6. Kuendelea kukamilisha upanuzi wa miundombinu ya kutolea huduma za afya katika hospitali nane (8) za Rufaa za Mikoa ambayo mikataba yake bado inaendelea. Hospitali hizo ni pamoja na Ligula (Mtwara) Tumbi (Pwani), Bombo (Tanga), Kagera, Maweni (Kigoma), Kitete

(Tabora), Sekou – Toure (Mwanza) na Mawenzi

(Kilimanjaro) ambapo kiasi cha Shilingi 13,698,000,000 kimetengwa.

  • Kuboresha huduma za matibabu ya ubingwa bobezi katika Hospitali ya Taifa na Kanda kwa kuimarisha miundombinu na ununuzi wa vifaa katika Taasisi ya JKCI, Hospitali za Rufaa za Kanda za Chato, Mtwara, KCMC, Bugando, Mbeya na kuanza ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Magharibi. Vilevile, Hospitali Teule ya Ukerewe itaimarishwa katika eneo hili ambapo jumla ya Shilingi 16,900,000,000 zimetengwa.
  • Kuendelea na ujenzi wa wodi ya wagonjwa binafsi (Private word katika hospitali ya Taifa Muhimbili) ambapo kiasi cha shilingi bilioni 4 kimetengwa
  • Kuanza ujenzi wa jengo la kutolea huduma za uchunguzi na tiba ya saratani ikiwemo huduma ya Mionzi katika hospitali ya Benjamini Mkapa- Dodoma, kiasi cha shilingi bilioni 10 kimetengwa
  • Kuendelea na ujenzi wa Hospitali mbili (2) mpya za Mikoa ya Ruvuma na Sokoine (Lindi) ambapo kiasi cha Shilingi 2,000,000,000 zimetengwa. xi. Kuwezesha Mafunzo ya Ubingwa Bobezi Nje ya Nchi ambapo kiasi cha Shilingi 3,000,000,000 kimetengwa.
  • Kugharamia mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi tarajali (Interns) ambapo kiasi cha shilingi 65,000,000,000 zimetengwa.
  • Kuimarisha udhibiti wa Magonjwa ya Kuambukiza ambapo kiasi cha Shilingi 12,609,396,973 zimetengwa.
  • Kusimamia utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI nchini ambapo kiasi cha Shilingi 26,608,315,374 zimetengwa.
  • Kusimamia utekelezaji wa Mpango wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma nchini ambapo kiasi cha Shilingi 14,833,845,612 zimetengwa.
  • Kutekeleza afua nyingine mbalimbali za afya ambapo kiasi cha Shilingi 57,409,211,687 zimetengwa. 

G. SHUKRANI

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara imekuwa ikipata ushirikiano mkubwa kutoka kwa nchi rafiki, Mashirika ya Kimataifa na Sekta nyingine zinazosaidia na kuchangia katika huduma za Afya na Ustawi wa Jamii. 
  1. Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua nafasi hii ya kipekee kuzishukuru nchi za Canada (DFATD), Denmark (DANIDA), Ireland (Irish Aid), Uswisi (SDC), Korea Kusini (KOICA) na Mashirika ya Maendeleo ya Kimataifa yakiwemo Benki ya Dunia, UNICEF, kwa kuchangia katika Mfuko wa Afya wa Pamoja (Health Basket Fund), ambao umesaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma za afya nchini hususani afya ya msingi. Aidha, napenda kuzishukuru nchi za China, Cuba, India, Italia, Japan, Marekani, Misri, Sweden, Uingereza, Ujerumani na Ufaransa na nchi nyingine ambazo zimeendelea kuisaidia Wizara kwa njia mbalimbali ikiwemo kufadhili miradi mbalimbali  inayotekelelezwa na Serikali kwa kushirikia na Mashirika yasiyo ya kiserikali ili kuboresha huduma za afya nchini.
  1. Mheshimiwa Spika, nayashukuru pia mashirika mengine ya Kimataifa kwa ushirikiano wao waliotoa kwa Wizara. Mashirika hayo ni pamoja na: Mashirika yaliyo chini ya Umoja wa Mataifa (UNAIDS, UNDP, UNFPA, UN-Women, WHO na IAEA); Jumuiya ya Nchi za Ulaya (EU); IMF, Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB); GAVI; PEPFAR; CDC; USAID; PMI; Abbott Fund; DFID; EED; Elizabeth Glaser Paediatric Aids Foundation (EGPAF); GIZ; Global Fund (for HIV, TB na Malaria); Bill and Melinda Gates Foundation; Good Samaritan Foundation (GSF);

HelpAge International; John Snow Incorporation (JSI); JICA;  KfW; Save the Children; World Vision; Benki ya

STANBIC; Walter REED; Jhpiego na Delloite

  1. Mheshimiwa Spika, niwashukuru watu binafsi, vyama vya hiari na mashirika yasiyo ya Kiserikali ya ndani ya nchi kwa kuwa mstari wa mbele katika kuchangia uimarishaji wa huduma za afya. Mashirika hayo ni pamoja na Benjamin Mkapa Foundation, AGOTA, Aga Khan Foundation, APHFTA, AMREF, AGPAHI, APT, BAKWATA, CSSC, CCT, Counsenuth, ELCT, Ifakara Health Institute, Lions Club, MAT, AFRICARE, Msalaba Mwekundu, MEHATA, TAMWA, TAWLA, TGNP, MDH, MeLSAT, PASADA, PAT, PSI, PRINMAT, Rotary Club International, SIKIKA, Shree Hindu Mandal, TANNA, TPHA, TPRI, Tanzania Surgical Assosciation (TSA), Tanzania Diabetic Association, TANESA, THPS, TUNAJALI, Tanzania Midwife Association, TDA, TAYOA, TISS, TEC, UMATI, USADEFU, White Ribbon Alliance, LSF, Kivulini, WiLDAF, TCRF na FSDT.
  1. Mheshimiwa Spika, navishukuru Vyuo Vikuu vya Dar es Salaam, Muhimbili, Sokoine, Ardhi, Mzumbe, Dodoma, Chuo Kikuu Huria, Kumbukumbu ya Hurbert Kairuki, IMTU, Tumaini, St. Agustino, CUHAS, Sebastian Kolowa, St. John, Aga Khan, Morogoro Muslim, Taasisi ya Teknolojia ya Nelson Mandela, Arusha pamoja na Vyuo vyote vilivyo chini ya Wizara ya Afya kwa kuwa mstari wa mbele katika kuchangia uimarishaji wa huduma za afya. 
  1. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha utendaji wangu wa kazi nikiwa Waziri, nimepata ushirikiano mkubwa kutoka kwa viongozi na wafanyakazi wa Wizara ya Afya. Napenda kumshukuru Mheshimiwa Dkt. Godwin Mollel (Mb.), Naibu Waziri wa Afya.

Aidha, naomba kuwashukuru Prof. Abel N. Makubi  Katibu Mkuu na Dkt  Seif A. Shekalaghe, Naibu  Katibu Mkuu. Vilevile, nawashukuru Dkt Alfello W. Sichalwe, Mganga Mkuu wa Serikali, Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo vya Wizara. Nawashukuru pia Wakurugenzi Wakuu wa Hospitali za Taifa na Kanda ambao ni  Prof. Lawrence M.  Museru (Hospitali ya Taifa Muhimbili), Dkt. Respicious L. Boniface (Taasisi ya Mifupa MOI), Prof. Mohamed Janabi (Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete), Dkt. Julius Mwaiselage, (Taasisi ya Saratani ya Ocean Road), Dkt. Leonard Subi (Hospitali yaKibong’oto), Dkt. Paul S. Lawala (Hospitali ya Mirembe) na Wakurugenzi wa Hospitali  za Rufaa za Kanda Dkt. Godlove Mbwanji (Hospitali ya Rufaa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mbeya), Dkt. Alphonce Chandika (Hospitali ya Benjamin Mkapa), Dkt. Brian Mawala (Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato), Dkt. Fabian A. Massaga(Hospitali ya Bugando) na Dkt. Geleard Masenga (Hospitali ya Rufaa ya Kanda KCMC). 

  1. Mheshimiwa Spika, kipekee naomba kuwashukuru wakurugenzi na wakuu wa Taasisi zote zilizo chini ya Wizara ambazo ni MSD, NHIF, TMDA, NIMR, Mamlaka ya Mkemia Mkuu wa Serikali, TFNC pamoja na Mabaraza ya Kitaaluma na Bodi za Usajili. Vilevile ninawashukuru Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Waganga Wafawidhi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa, Hospitali za Halmashauri, Vituo vya Afya, Zahanati, Wakuu wa Vyuo vya Mafunzo vilivyo chini ya Wizara na Wafanyakazi wote wa Wizara na Mashirika ya Dini, Mashirika ya Kujitolea na Mashirika Binafsi. Natoa shukrani kwa Sekta zote ambazo tunashirikiana nazo katika kutoa huduma za afya pamoja na wananchi wote kwa ushirikiano wao. Nawaasa watanzania kujali na kulinda afya zao ikiwemo kwa kuzingatia ulaji wa vyakula unaofaa, kufanya mazoezi ya viungo mara kwa mara na kujiepusha na unywaji wa pombe kupita kiasi. Ni muhimu watanzania wakatambua kuwa Afya ni Mtaji. 
  1. Mheshimiwa Spika, nichukue fursa hii pia kuishukuru Familia yangu, kwa uvumilivu wao na pia kwa kunitia moyo katika kutekeleza majukumu yangu ya Kitaifa. Kwa wananchi wa Jimbo la Tanga Mjini  nawashukuru kwa ushirikiano wanaoendelea kunipatia katika kutekeleza majukumu yangu. Naahidi kuwa nitaendelea kuwaenzi na kuwatumikia kwa nguvu zangu zote ili kuleta mabadiliko ya haraka ya kimaendeleo katika Jimbo letu la  Tanga Mjini.

H. MAOMBI YA FEDHA KWA KAZI ZILIZOPANGWA KUTEKELEZWA KATIKA MWAKA 2022/23

Makadirio ya Makusanyo ya Maduhuli kwa Mwaka 2022/23

192. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/23 Wizara na Taasisi zilizo chini yake imekadiria kukusanya kiasi cha shilingi  619,538,808,257. Kati ya fedha hizo, shilingi 140,813,114,464.00 zinatarajiwa kukusanywa kutoka vyanzo vya ndani Makao Makuu ya Wizara, shilingi 85,739,668,813.00 zinatarajiwa kukusanywa kutoka Hospitali za Rufaa za Mikoa, shilingi 392,986,024,980.00 zinatarajiwa kukusanywa kutoka katika Mashirika yaliyo chini ya Wizara. Makusanyo hayo ni sawa na ongezeko la asilimia 22 ikilinganishwa na makadirio ya mwaka 2021/22 ambayo yalikuwa ni kukusanya shilingi 507,218,152,321.00.

Matumizi ya Kawaida

193. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2022/23,

Wizara imepanga kutumia kiasi cha shilingi 554,289,666,000.00 kwa ajili ya Matumizi ya kawaida sawa na asilimia 50 ya bajeti tengwa, ambapo kiasi cha shilingi 331,566,406,000.00 ni kwa ajili ya Mishahara ya Wizara na Taasisi zilizo chini yake, na kiasi cha shilingi 222,723,260,000.00 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo.

Miradi ya Maendeleo

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara inakadiria kutumia shilingi 555,132,056,000.00 kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo sawa na asilimia 50 ya bajeti tengwa. Kati ya hizo, fedha za ndani ni shilingi 410,298,000,000.00 na fedha za nje ni shilingi 144,834,056,000.00
  1. Mheshimiwa Spika, jumla ya fedha zote zinazoombwa na     Wizara        ni     shilingi 1,109,421,722,000.00 ili kuweza kutekeleza malengo iliyojiwekea. 
Na.FunguMatumizi                 ya KawaidaMiradi ya MaendeleoJumla
1Fungu 52554,289,666,000.00555,132,056,000.001,109,421,722,000.00
 Jumla554,289,666,000.00555,132,056,000.001,109,421,722,000.00
  1. Mheshimiwa Spika, Hotuba hii inapatikana pia   katika        tovuti        za      Wizara        ya      Afya www.moh.go.tz
  1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.  

VIAMBATISHO

Kiambatisho Na.1. Magonjwa 10 yaliyoongoza kwa wagonjwa wa nje (OPD) 2021/22

 Umri chini ya Miaka 5Umri miaka mitano na zaidi
Na.Aina ya UgonjwaIdadi ya WagonjwaAsilimia/ (wagonjwa wote)Aina ya UgonjwaIdadi ya wagonjwaAsilimia/ (Wagonjwa wote)
1Maambukizi katika mfumo wa hewa3,270,32933.3Maambukizi katika mfumo wa hewa3,675,50618.6
2Malaria1,183,96512.0Maambukizi katika njia ya mkojo3,059,48715.5
3Maambukizi katika njia ya mkojo828,2058.4Malaria1,356,8656.9
4Kuharisha (With No Dehydration)750,9407.6Shinikizo la juu la moyo1,017,1065.2
5Kichomi, (Non- Severe & Severe)695,8617.0kichomi (severe & Non severe)636,4223.2
6Magonjwa ya mfumo wa chakula323,0723.3Vidonda vya tumbo610,2643.1
7Minyoo ya tumboni284,6422.9Magonjwa ya mfumo wa chakula560,3302.8
8Magonjwa ya ngozi207,3142.1Minyoo yatumboni488,2092.5
9Kuharisha (With Dehydration)206,9272.1Kisukari488,0542.5
10Magonjwa ya ngozi143,5081.5Upasuaji400,2562.0

Kiambatisho Na 2: Magonjwa 10 yaliyoongoza kwa Wagonjwa wa Kulazwa (IPD) 2021/22

 Umri chini ya Miaka 5Umri miaka mitano na zaidi
Na. Aina ya UgonjwaIdadi ya WagonjwaAsilimia/ (Wagonjwa wote)Aina ya UgonjwaIdadi ya wagonjwaAsilimia/ (Wagonjw a wote)
1Kichomi (Severe & Non severe)64,59918.9Malaria76,8349.8
2Malaria52,55415.4Kichomi (severe & non severe)65,9048.4
3Kuharisha sana (<siku 14)36,05210.6Magonjwa ya mfumo wa mkojo50,7236.5
4Upungufu wa damu25,9377.6Upungufu wa damu45,9975.9
5Kuzaliwa na uzito mdogo (<2.5kg)13,2823.9Shinikizo la juu la moyo43,9745.6
6Maambukizi katika damu13,0403.8Vidonda vya tumbo30,3163.9
7Maambukizi ya mfumo wa upumuaji12,9393.8Magonjwa ya kina mama29,4453.8
8Maambukizi ya mfumo wa mkojo11,5083.4Mimba kutoka (Abortion)26,7203.4
9Magonjwa ya mfumo wa chakula10,3963.1Kisukari25,7773.3
1 0Kukosa hewa (Birth Asphyxia)9,3292.7Magonjwa ya mfumo wa chakula23,9903.1

Chanzo: DHIS2

Kiambatisho Na.3. Idadi ya Wagonjwa waliohudumiwa katika Hospitali ngazi ya Taifa, Kanda na                                  Maalum kwa kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022

NA.HOSPITALIWAGONJWA WALIOHUDUMIWA 2021/22JUMLA
Nje (OPD)Wakulazwa (IPD) 
1HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI(UPANGA)328,93838,275367,213
2HOSPITALI YA MUHIMBILI (MLOGANZILA)82,8048,94091,744
3TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE (JKCI)84,0453,28787,332
4TAASISI YA MIFUPA MUHIMBILI (MOI)147,8476,413154,260
5TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD33,6214,26137,882
6HOSPITALI YA MIREMBE26,7611,56428,325
7HOSPITALI YA RUFAA KANDA MBEYA205,32931,857237,186
8HOSPITALI YA     MAGONJWA           AMBUKIZI KIBONG’OTO13,95363614,589
9HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA160,9427,537168,479
10HOSPITALI YA BUGANDO269,01922,818291,837
11HOSPITALI YA KCMC208,46789,343297,810
12HOSPITALI YA KANDA YA CHATO4,8107975,607
 JUMLA 1,566,536215,7281,782,264

Kiambatisho Na.4. Idadi ya Wagonjwa wa Msamaha katika Hospitali ngazi ya Taifa, Kanda na 

                                Maalum kwa kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022

NA.HOSPITALIWAGONJWA WALIOPATA MISAMAHA (Julai 2021 hadi Machi, 2022)
MISAMAHATHAMANI
1HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI UPANGA46,59114,100,000,000
2HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI MLOGANZILA2,9281,900,000,000.00
3TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE (JKCI)2,135814,848,257.29
4TAASISI YA MIFUPA MUHIMBILI (MOI)3,152318,307,889.90
5TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD2,79213,885,950,630
6HOSPITALI YA RUFAA KANDA MBEYA18,547185,478,000.00
7HOSPITALI YA MAGONJWA AMBUKIZI KIBONG’OTO497114,541,967.00
8HOSPITALI YA MIREMBE3,98560,217,746.00
9HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA          2,228 281,000,000.00
10HOSPITALI YA BUGANDO548308,651,412.00
11HOSPITALI YA KCMC7033,500,000,000.00
12HOSPITALI YA KANDA YA CHATO3900,000.00
 JUMLA84,10935,469,895,902.19

Kiambatisho Na.5.  Wagonjwa waliohudumiwa katika Hospitali za Rufaa za Mikoa kwa kipindi cha

                                 Julai 2021 hadi Machi, 2022

Na.Hospitali  Mkoa  Idadi ya VitandaWagonjwa Julai 2021 hadi Machi, 2022Jumla  
NJE (OPD)WAKULAZWA (IPD) 
1Amana DSM 341123,90514,115138,020
2BomboTanga45758,0908,70066,790
3Bukoba   Kagera31264,2344,69968,933
4Dodoma Dodoma423148,78520,927169,712
5Geita   Geita22739,4944,48843,982
6Iringa   Iringa37758,6758,99067,665
7Katavi Katavi14947,5276,19953,726
8KiteteTabora24037,9986,91744,915
9Ligula  Mtwara22240,8233,79444,617
10Manyara Manyara11121,4902,98724,477
11Maweni Kigoma 17838,1524,57242,724
12Mawenzi Kilimanjaro 21075,5416,59482,135
13Mbeya Mbeya 18031,1281,54832,676
14Morogoro   Morogoro   37588,81013,193102,003
15Mt. Meru   Arusha42086,89610,71097,606
16Musoma  Mara  26939,0025,13944,141
17Mwananyamala  DSM 309453,83311,976465,809
18Njombe*  Njombe549,71895310,671

 

Na.Hospitali  Mkoa  Idadi ya VitandaWagonjwa Julai 2021 hadi Machi, 2022Jumla  
NJE (OPD)WAKULAZWA (IPD) 
19Sekou Toure Mwanza 33186,04826,278112,326
20Shinyanga  Shinyanga27645,0416,88051,921
21Simiyu*Simiyu2413,36793514,302
22Singida Singida30066,8294,33871,167
23Sokoine Lindi17623,0323,92726,959
24Songea Ruvuma32180,9329,08790,019
25Songwe Songwe15681,9794,14786,126
26Sumbawanga Rukwa21729,16113,31842,479
27Temeke DSM370443,91010,354454,264
28Tumbi Pwani 23681,0315,69486,725
 Jumla 7,2612,415,431221,4592,636,890

Chanzo:  

Kiambatisho Na.6.   Idadi ya Wagonjwa wa Msamaha waliohudumiwa pamoja na gharama zao katika Hospitali za Rufaa za Mikoa kwa kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022

 NaHospitaliIdadi ya Wagonjwa WaliosamehewaGharama za Msamaha 
 1Amana-DSM          9,020 128,615,836 
 2Bombo-Tanga         12,055 270,908,988 
 3Bukoba-Kagera          4,672 112,184,704 
 4Dodoma         16,687 596,349,500 
 5Geita          7,891 178,820,171 
 6Iringa          2,005 35,909,420 
 7Katavi          1,968 80,224,870 
 8Kitete-Tabora          7,387 185,995,965 
 9Ligula-Mtwara             716 3,945,350 
 10Manyara          1,902 129,779,354 
 11Maweni-Kigoma          1,457 42,880,210 
 12Mawenzi-Kilimanjaro         11,175 104,686,389 
 13Mbeya               52 1,731,470 
 14Morogoro          2,357 39,275,516 
 15Mount Meru-Arusha          5,543 102,011,830 
 16Musoma-Mara          4,061 109,244,396 
 17Mwananyamala -DSM          5,422 238,127,590 
 18Njombe             175 6,039,390 
 19Sekou Toure-Mwanza         21,640 351,342,118 
 20Shinyanga          2,242 49,093,830 
 21Simiyu               81 3,235,810 
 22Singida          3,499 244,439,034 
NaHospitaliIdadi ya Wagonjwa WaliosamehewaGharama za Msamaha
23Sokoine-Lindi          1,146 5,488,820
24Songea-Ruvuma          7,375 86,132,940
25Songwe          5,717 235,668,860
26Sumbawanga-Rukwa          1,827 23,466,903
27Temeke-DSM          6,024 65,401,000
28Tumbi-Pwani          1,701 42,133,841
 Jumla       145,797             3,473,134,105

Chanzo: MOH.

Kiambatisho Na.7: Idadi ya akina mama waliojifungua na vifo vilivyotokana na uzazi katika Hospitali za Rufaa za Mikoa, kwa kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi,2022.

NaHospitaliWaliojifunguaVifo Vilivyotokana na Uzazi
1Amana-DSM5,29310
2Bombo-Tanga2,80213
3Bukoba-Kagera1,1759
4Dodoma5,82818
5Geita3,66816
6Iringa1,7547
7Katavi1,1296
8Kitete-Tabora1,77228
9Ligula-Mtwara94610
10Manyara2,2948
11Maweni- Kigoma7737
12Mawenzi-Kilimanjaro1,2900
13Mbeya2,1796
14Morogoro3,75917
15Mount Meru-Arusha3,6028
16Musoma-Mara1,5667
17Mwananyamala-DSM4,3527
18Njombe2726
19Sekou Toure- Mwanza4,4187
20Shinyanga1,5244
21Simiyu0
22Singida1,9154

 Kiambatisho Na.8. Jedwali linaloonesha hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo

Na.Hospitali HusikaLengo la MradiGharama za MradiChanzo cha FedhaKiasi kilichotolewaHatua ya utekelezaji
1: Ujenzi na Upanuzi wa Majengo mbalimbali ya kutolea huduma katika Hospitali Ngazi ya   Taifa
Na.Hospitali HusikaLengo la MradiGharama za MradiChanzo cha FedhaKiasi kilichotolewaHatua ya utekelezaji (%)
1Hospitali ya Taifa MuhimbiliUjenzi wa Jengo la Wodi Maalum (Private wards)  Ujenzi unatekelezwa kwa awamu ambapo awamu ya kwanza (hadi hatua ya jamvi) iligharimu 1.2bil. Awamu26,000,000,000.00GOT4,000,000,000.00 Asilimia 26
Na.Hospitali HusikaLengo la MradiGharama za MradiChanzo cha FedhaKiasi kilichotolewaHatua ya utekelezaji
  ya pili (Framed Structure) itagharimu 4.36 Bil.     
Ukarabati wa vyumba vya ICU 5 1,000,000,000.00IMF900,000,000.00Asilimia 80
Ukarabati wa vyumba vya Radiologjia (MRI 1, CT SCAN 1 na Xray 240,000,000.00IMF40,000,000.00Asilimia 90
JUMLA KUU HOSPITALI NGAZI YA TAIFA        27,040,000,000.00                   4,940,000,000.00  
2: Ujenzi na Upanuzi wa Majengo mbalimbali ya kutolea huduma katika Hospitali za Rufaa za Kanda
Na.Hospitali HusikaLengo la Mradi Gharama za Mradi   Chanzo cha Fedha   Kiasi kilichotolewa   Hatua ya utekelezaji (%)
1ChatoAwamu ya kwanza OPD,16,072,813,776.31GOT16,072,813,776.31 Asilimia 98 
Na.Hospitali HusikaLengo la MradiGharama za MradiChanzo cha FedhaKiasi kilichotolewaHatua ya utekelezaji
  Maabara, Pharmasia, EMD Upasuaji na ICU    
Awamu ya pili: Radiologia na wodi za wagonjwa 17,705,497,182.27GOT9,756,138,647.49Asilimia 70
Awamu ya tatu ujenzi wa Nyumba 20 za watumishi1,143,582,899.00GOT1,092,842,899.00Asilimia 99
Uzio (Fence)1,125,666,900.00GOT933,202,033.00Asilimia 85
Njia za kupita wagonjwa (Walk ways) na Barabara za ndani ya eneo la  Hospitali 2,010,000,000GOT1,970,000,000.00Asilimia 86
Na.Hospitali HusikaLengo la MradiGharama za MradiChanzo cha FedhaKiasi kilichotolewaHatua ya utekelezaji
  Ukarabati Mdogo kuwezesha usimikaji wa vifaa vya radilogia (MRI1, CT scan 1 na Xray 1) IMF Vyumba viko tayari maboresho madogo yatakamilish wa wakati wa ufungaji mashine. 
2Kanda ya kusini MtwaraUjenzi wa jengo la OPD Complex kwa ajili ya huduma mbalimbali kwa ngazi ya Kanda. Upanuzi wa huduma utaendelea kwa kujenga majengo mengine kadri master plan ya hospitali16,488,012,643.02 GOT&WB  15,111,404,882.65 Asilimia 98 
Na.Hospitali HusikaLengo la MradiGharama za MradiChanzo cha FedhaKiasi kilichotolewaHatua ya utekelezaji
  na upatikanaji wa fedha.     
Ukarabati Mdogo kuwezesha usimikaji wa vifaa vya radilogia (MRI1, CT scan 1 na Xray 1)40,000,000MFI Vyumba vipo katika jengo Jipya. Maboresho madogo yatafanyika wakati wa ufungaji mashine
3Kanda ya Nyanda za juu – Mbeya Ujenzi wa jengo la pekee kwa ajili ya Huduma za uzazi (Maternity Complex) unafanyika katika Hospitali ya Rufaa, Kanda ya Nyanda za          9,392,191,914.99 GOT  9,392,191,914.99 Asilimia 94
Na.Hospitali HusikaLengo la MradiGharama za MradiChanzo cha FedhaKiasi kilichotolewaHatua ya utekelezaji
  juu Kusini Mbeya tawi la Meta. Jengo lina Ghorofa Sita    
Ukarabati Mkubwa wa eneo la ICU 500,000,000.00  497,920,186.71 Asilimia 60
Ukarabati wa EMD    Asilimia 25
4Kanda ya ziwa – BugandoUjenzi wajengo la ghorofa nne la wodi maalumu ya Saratani   5,400,000,000.00 GOT&BM C1,990,000,000.00 Asilimia 85
Ukarabati Mkubwa wa ICU516,000,000.00 IMF500,000,000.00 Asilimia 30
Ukarabati kwa ajili chumba cha X-Ray IMF Chumba kipo tayari 
5Kanda ya KaskaziniUjenzi wa Jengo la4,700,000,000.00 GOT2,000,000,000.00 Asilimia 60
Na.Hospitali HusikaLengo la MradiGharama za MradiChanzo cha FedhaKiasi kilichotolewaHatua ya utekelezaji
 (KCMC)huduma za tiba – Mionzi kwa matibu ya magonjwa ya cancer (Radiotherapy)      
Ukarabti Mkubwa wa jengo la ICU499,318,800.00 IMF499,318,800.00 Asilimia 70
6Kanda ya Kati, Hospitali ya Benjamini MkapaJengo la Tiba Mionzi (Radiotherapy) 32,000,000,000.00 GOT Asilimia 0
Ukarabati Mkubwa wa eneo la ICU100,000,000.00 IMF100,000,000.00 Asilimia 90
Ukarabati kwa ajili chumba cha X-Ray IMF Asilimia 90
JUMLA KUU HOSPITALI ZA KANDA  107,693,084,115.59    59,915,833,140.15  
3: Ujenzi na Upanuzi wa Majengo mbalimbali ya kutolea huduma  katika Hospitali Maalumu 
1Kibong’otoUjenzi wa Maabara ya Kisasa (BSL 3)13,732,409,704.50GOT, WB & GF7,773,061,071.97Asilimia 96
Ujenzi na ukarabati Mkubwa wa jengo la Radiologia kwa ajili ya kusimika CT Scan  262,000,000.00ORIO262,000,000.00Asilimia 10
Ukarabati Mkubwa na upanuzi wa  wa jengo kwa ajili ya huduma za wagonjwa mahututi ( ICU)350,000,000.00IMF350,000,000.00Asilimia 60
2Taasisi ya Moyo,Ukarabati Mkubwa wa509,466,480IMF500,000,000.00Asilimia 60
 Jakaya Kikwete ( JKCI)Jengo la ICU    
3Ocean RoadUkarabati Mkubwa wa Jengo la ICU  714,649,507IMF714,649,507.00Asilimia 60
Ukarabati Mkubwa kwa ajili ya chumba cha kufunga MRI  280,000,000IMF280,000,000.00Asilimia 60
4MirembeUkarabati kwa ajili ya chumba cha X-ray na Ultrasound    ORIO Asilimia 60
Ujenzi na ukarabati mkubwa wa wodi na majengo mbalimbali ya Hospitali  3,000,000,000IMF3,000,000,000.00Asilimia 40
Ujenzi wa Jengo la EMD1,200,667,641IMF750,000,000.00Asilimia 40
  na ICU      
5Ukerewe Ujenzi wa jengo la OPD, RCH, Mortuary na Pharmacy  3,000,000,000IMF3,000,000,000.00Asilimia 10
JUMLA KUU HOSPITALI MAAL UM        23,049,193,332.65                   16,629,710,578.97  
 4.0 UJENZI NA UKARABATI HOSPITALI ZA RUFAA ZA MIKOA   4.1 : Ujenzi wa Hospitali Mpya tano (Njombe, Simiyu, Geita, Songwe na Katavi)
Na.Hospitali HusikaLengo la Mradi Gharama za Mradi   Chanzo cha Fedha   Kiasi kilichotolewa  Hatua ya Utekelezaji (%)
1NjombeUjenzi unatekelezwa kwa awamu ambapo awamu ya kwanza ilihusu ujenzi wa OPD ambalo kwa sasa linatumika, ujenzi wa awamu ya pili        27,478,274,300.00 GOT&GF  22,192,716,800.00 Asilimia 96 
  umehusisha majengo yafuatayo, Jengo la Afya ya uzazi (Maternity), EMD&ICU, Upasuaji & Mifupa na wodi, laundry, Damu Salama na Incinerator  na nyumba tano za watumishi    
Ujenzi wa jengo la CT Scan na nyumba 1 ya Mtumishi             390,000,000.00 IMF  Asilimia 40
2SimiyuUjenzi wa Maternity Block          5,774,992,393.00 GOT&GF  3,250,745,328.86 Asilimia 80  
Ujenzi wa jengo la EMD na ICU          1,210,000,000.00 IMF  1,210,000,000.00 Asilimia 55
  Ukarabati mdogo Chumba cha CT Scan na nyumba 1 ya Mtumishi IMF Vyumba vipo, ukarabati mdogo utafanyika wakati wa kufunga mashine 
3GeitaUjenzi unatekelezwa kwa awamu ambapo awamu ya kwanza ulianza ujezi wa OPD block (Ghorofa 1) Theatre &Radiology Block (Ghorofa 1) Laundry Building na jengo la Mgahawa (Cafeteria)                  8,612,994,260.00 GOT  8,612,994,260.00 Asilimia 95
Ujenzi wa Jengo la             998,628,336.00 GF  998,628,336.00 Asilimia 99
  Maabara    
Ujenzi wa Jengo la Afya ya Uzazi (Maternity Wing)          6,999,848,824.00 GOT & Global Fund   3,865,986,022.39 Baada ya Mradi kusimama hatua za kuendeleza mradi kupitia Mkandarasi mwingine ziko hatua ya kusainiwa Mkataba zinakamilishw a 
Ujenzi wa jengo la EMD na ICU          1,210,000,000.00 IMF  1,210,000,000.00 Asilimia 40
Ukarabati mdogo Chumba cha CT Scan na nyumba 1 ya Mtumishi                          90,000,000.00 IMF  90,000,000.00 Asilimia 55
4Songwe Ujenzi wa Jengo la OPD        6,246,443,640.00 GOT  6,246,443,640.00 Asilimia 99.
Ujenzi wa Jengo la           999,448,336.00 GF  999,448,336.00 Asilimia 99
  Maabara    
Ujenzi wa jengo la wazazi (maternity)        9,745,114,617.81 GOT  2,668,663,229.77 Asilimia 22
Ujenzi wa jengo la EMD na ICU        1,210,000,000.00 IMF  1,210,000,000.00 Asilimia 20
Ujenzi wa Nyumba 1 ya Mtumishi na ukamilishaji wa chumba cha CT Scan na X    -ray           120,000,000.00 IMF Bado  
5KataviUjenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa          9,915,512,420.00 GOT  9,915,512,420.00 Asilimia 72
Ujenzi wa Maabara           998,628,336.00 GF  998,628,336.00 Mradi umekamilika na kukabidhiwa 
Ujenzi wa Jengo la EMD           1,188,849,798.00 IMF  860,000,000.00 Asilimia 28
Ujenzi wa Jengo la ICUIMF Asilimia 7
  Ujenzi wa nyumba ya Mtumishi               90,000,000.00 IMF  90,000,000.00  Asilimia 40
 Vyumba vya CT Scan na Xray             178,518,660.00 IMF  178,518,660.00 Vyumba viko ndani ya jengo la Hospitali
JUMLA KUU KUNDI LA 4.1        83,457,253,920.81                   64,598,285,369.02  
4.2: Ukarabati na upanuzi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa iliyopokelewa kutoka OR-TAMISEMI mwaka 2017. ikijumuisha Singida, Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (Mara – Kwangwa), Shinyanga, Manyara, Mawenzi (Kilimanjaro), Mbeya RRH 
Na.Hospitali HusikaLengo la Mradi Gharama za Mradi   Chanzo cha Fedha   Kiasi kilichotolewa  Hatua ya utekelezaji (%)
1SingidaUjenzi unatekelezwa kwa awamu ambapo awamu ya sasa ni kujenga sakafu ya chini jengo lenye ghorofa   3 kwa ajili ya wodi za kulaza wagonjwa  19,525,525,130.75 GOT & GF  6,021,614,224.19 Asilimia 70
  (Wards), vyumba vya upasuaji (Theatres), huduma za famasi (Pharmacy), huduma za maabara (Laboratory) na huduma za wagonjwa mahututi (ICU)     
Ujenzi wa Jengo la EMD na ICU          1,426,254,074.86 IMF  1,426,254,074.86 Asilimia 45
Ujenzi wa Nyumba ya Mtumishi               90,000,000.00 IMF  90,000,000.00 Asilimia 40
Ukarabati Mkubwa kwa ajili vyumba vya radiologia (CT Scan na X-ray)                66,696,678.00 IMF  66,696,678.00 Asilimia 80
2Kwangwa- MaraUjenzi wa Hospitali ya Kumbukumbu ya Mwal. Nyerere Kwangwa – Mara ni jengo moja lenye sehemu ya kutolea huduma za wagonjwa wa nje, wagonjwa wa kulazwa, maabara, radiolojia, upasuaji, famasia na dharura. Ujenzi unaendelea vizuri ambapo tayari upande wa kitalu C umekabidhiw a na unatoa huduma. upande wa        22,959,162,959.26 GOT  14,321,021,916.48 Asilimia 95 
  kitalu A na B bado vinaendelea kukamilishwa kwa ujumla, hatua ya awali ya mradi iko katika    
Ujenzi wa Nyumba 1 ya Mtumishi               90,000,000.00 IMF Asilimia 40
3ShinyangaJengo la huduma za kupambana na ugonjwa wa UVIKO (Covid 19) linaendelea pamoja na maandalizi ya Jengo la Afya ya Uzazi           2,071,850,094.32 GOT&GF 1,941,058,554,56 Asilimia 97.5
Ujenzi wa Jengo la EMD na ICU          1,210,000,000.00 IMF  1,210,000,000.00 Asilimia 65
Ujenzi wa Jengo la Radiologia (CT   Asilimia 10
  Scan na XRay)    
 Nyumba 1 ya Mtumishi             400,000,000.00 IMF Asilimia 10
4ManyaraUkamilishaji wa Jengo la wagonjwa wa Nje (OPD)          1,499,000,000.00 GF  1,499,000,000.00 Asilimia 98
Ujenzi wa Jengo la Damu Salama        1,133,059,693.50 GOT  647,770,207.00 Asilimia 45
Ujenzi wa Jengo la EMD na ICU        1,210,000,000.00 IMF  1,210,000,000.00 Asilimia 45
Ujenzi wa Jengo la CTScan na Nyumba 1 ya Mtumishi IMF Asilimia 40
5Mawenzi – KilimanjaroUjenzi wa EMD           764,995,975.00 GF  764,995,974.62 Asilimia 99
Ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto        6,434,028,320.00 GOT & GF  4,778,059,098.00 Asilimia 70 
Ukarabati Mkubwa wa Jengo la ICU           149,067,895.00 IMF  149,067,895.00  Asilimia 55
  Ujenzi wa nyumba ya Mtumishi             90,000,000.00 IMF   90,000,000.00 Asilimia 25
Ukarabati wa vyumba vya radiologia (CT scan na Nyumba 1 ya Mtumishi) IMF Vyumba vipo na ukamilishwaj i unafanyika na Mkandarasi aliyeko site
6Mbeya RRHUjenzi wa Jengo la EMD           683,664,745.00 GF  683,664,745.00 Asilimia 100 
Ujenzi wa jengo la upasuaji (theatre, ICU & CSSD)         5,339,493,180.24 GOT & GF  5,339,493,180.24 Asilimia 90 
Ukarabati Mkubwa wa Jengo la ICU           150,000,000.00 IMF  150,000,000.00 Asilimia 80
Ujenzi wa Nyumba ya Mtumishi             90,000,000.00 IMF  90,000,000.00 Asilimia 35
Ujenzi wa Jengo la CTScan  IMF Asilimia 10
JUMLA KUU KUNDI LA 4.2        65,382,798,745.93    38,537,637,993.39  
4.3:  Upanuzi wa majengo katika Hospitali ya Sekou Toure – Mwanza, Mwananyamala – Dar es Salaam, Ruvuma, Tanga, Maweni- Kigoma, Sumbawanga (Rukwa), Iringa, Kitete -Tabora, Dodoma, Sokoine Lindi, Mount Meru – Arusha, Temeke na Amana
Na.Hospitali HusikaLengo la Mradi Gharama za Mradi   Chanzo cha Fedha   Kiasi kilichotolewa   Hatua ya utekelezaji 
1SekouToure (Mwanza)Ujenzi wa Jengo la Afya ya Uzazi Ni ujenzi wa jengo la sakafu 5         10,106,468,902.31 GOT  9,876,453,413.53 Asilimia 96
Ujenzi wa nyumba ya Mtumishi               90,000,000.00 IMF  90,000,000.00 Asilimia 40
Ukarabati wa chumba cha X-ray pamoja na ujenzi wa Nyumba 1 ya Mtumishi               12,770,080.00 IMF  12,770,080.00 Asilimia 60
2Mwananya malaUkamilishaji wa Jengo la Afya ya Uzazi lenye ghorofa 4 kutoa huduma zote mama na mtoto          2,604,937,502.91 GOT & GF  2,604,937,502.91 Asilimia 98
  Ujenzi wa Jengo la EMD na ICU          1,050,000,000.00 IMF  1,050,000,000.00 Asilimia 40
Ukarabati wa chumba cha X-ray                35,256,000.00 IMF Asilimia 40
3RuvumaUjenzi wa Jengo la huduma za Dharura (EMD)           630,340,507.00 GF  630,340,507.00 Umekamilika na kuanza kutumika
Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Nje (OPD) awamu ya kwanza katika eneo jipya la Hospitali ya mkoa        3,000,000,000.00 GOT & IMF  3,000,000,000.00 Asilimia 30
Ukarabati mkubwa wa jengo kwa ajili ya ICU Hospitali ya mkoa ya sasa           169,246,500.00 IMF  152,000,000.00 Asilimia 94
Ujenzi wa Nyumba ya             90,000,000.00 IMF  90,000,000.00 Asilimia 30
  Mtumishi     
Ujenzi wa jengo la CT Scan            271,079,500.20 IMF  271,079,500.20 Asilimia 10 
4BOMBO – TangaUjenzi wa Jengo la Methadone           736,705,586.00  GF  736,705,586.00 Awamu ya kwanza imekamilika 
Ujenzi wa Jengo la Damu Salama        1,133,059,693.50 GOT  647,770,207.00 Kusafishaji eneo la kufanya ujenzi
Ukarabati Mkubwa wa jengo la EMD na ICU           250,000,000.00 IMF  250,000,000.00 ICU asilimia 99  EMD asilimia 90
Nyumba ya Mtumishi             90,000,000.00 IMF  90,000,000.00 Bado (Changamoto ya upatikanaji wa eneo)
ujenzi wa jengo la CT Scan  IMF Asilimia 10 
5Maweni – KigomaUjenzi wa Jengo la Upasuaji           619,255,321.00 GF  619,255,321.00 Asilimia 100 
  Ujenzi wa Jengo la Damu Salama        1,271,033,725.50 GOT  647,770,207.00 Asilimia 60.
Ujenzi wa jengo la Mortuary na Upanuzi wa jengo la OPD na Maternity        3,520,000,000.00 GOT& IMF  3,000,000,000.00 Asilimia 30
Ujenzi wa Jengo la EMD na ICU        1,335,348,000.00 IMF  1,210,000,000.00 Asilimia 45
Ujenzi wa nyumba ya Mtumishi             90,000,000.00 IMF  90,000,000.00 Asilimia 50
Ukarabati wa jengo la CT Scan  IMF bado
6Sumbawang a – RukwaUjenzi wa Jengo la Damu Salama        1,099,993,610.00 GF  1,099,993,610.00 Asilimia 40
Ukarabati mkubwa wa jengo la ICU           247,141,173.00 IMF                  247,141,173.00 Asilimia 65
Ujenzi wa Nyumba              90,000,000.00 IMF                  90,000,000.00 Asilimia 40
Upanuzi wa jengo kwa ajili           205,386,339.60 IMF Asilimia 10
  ya CTScan     
7IringaUjenzi wa Jengo la huduma za Dharura (EMD)621,993,845GF                  621,993,845.00 Asilimia 100 
Ukarabati Mkubwa wa Jengo la ICU150,000,000IMF                  150,000,000.00 Asilimia 90 
Ujenzi wa nyumba ya Mtumishi 90,000,000IMF                  90,000,000.00 Bado kuanza 
Ujenzi wa Jengo la CT Scan 271,079,500IMF                  271,079,500.20 Asilimia 10 
8Kitete – TaboraUjenzi wa Jengo la huduma za Dharura (EMD)604,870,350GF                  604,870,350.00 Asilimia 98
Ujenzi wa Jengo la Afya ya Uzazi (Maternity Block) awamu ya Kwanza6,735,155,134GOT & IMF                  3,000,000,000.00 Asilimia 35
Ujenzi wa560,000,000IMF                  130,000,000.00 Asilimia 45
  Jengo la ICU    
Ujenzi wa nyumba ya mtumishi90,000,000IMF                  90,000,000.00 Asilimia 38
Ujenzi wa jengo la CT Scan  IMF Asilimia 7
9Ligula MtwaraUkamilishaji wa Jengo la Upasuaji na Miundombinu ya majengo mengine ndani ya Hospitali1,000,000,000GOT Bado
Ujenzi wa Jengo la EMD na ICU1,177,489,386IMF                  860,000,000.00 Asilimia 45
Ujenzi wa Jengo la OPD3,000,000,000IMF                  3,000,000,000.00 Asilimia 5
Ujenzi wa nyumba 1 ya Mtumishi90,000,000IMF                  90,000,000.00 Asilimia 25
10DodomaUkarabati wa jengo la EMD             103,235,987.00 IMF                  100,000,000.00 Asilimia 95
Ujenzi wa Jengo la ICU             725,006,257.00 IMF                  560,000,000.00 Asilimia 80
Ujenzi wa              IMF                 Asilimia 20
  nyumba ya Mtumishi90,000,000.00  90,000,000.00  
ujenzi wa jengo la CT Scan              300,169,628.00 IMF                  300,169,628.00 Asilimia 7
Ujenzi wa Kituo cha Kanda ya kati cha Damu Salama Dodoma           1,702,065,625.00 UNICEF                  1,157,404,625.00 Asilimia 90
11AmanaUkarabati wa ICU150,331,260.00 IMF150,000,000.00 Asilimia 98
Ukarabati wa EMD             457,204,904.00 IMF & GOT                  120,000,000.00 Asilimia 95
Upanuzi wa jengo kwa ajili ya CT Scan na X-ray             405,000,000.00 IMF Asilimia 10 
12Bukoba – KageraUjenzi wa ICU             561,000,000.00 IMF                  560,000,000.00 Asilimia 45
Ujenzi wa EMD             660,000,000.00 IMF                   650,000,000.00 Asilimia 45
Ujenzi wa nyumba ya Mtumishi na jengo la CT Scan  IMF Bado kuanza 
  Ujenzi wa Nyumba ya Mtumishi               90,000,000.00 IMF                  90,000,000.00 Asilimia 10
13MorogoroUjenzi wa ICU             560,000,000.00 IMF                  560,000,000.00 Asilimia 65 
Ujenzi wa EMD             650,000,000.00 IMF                   650,000,000.00 Asilimia 85
Ujenzi wa nyumba ya Mtumishi na                90,000,000.00 IMF                  90,000,000.00 Asilimia 60
Jengo la XRay  IMF Asilimia 80
14Mount Meru ArushaUkarabati wa ICU             194,831,505.00 IMF                  194,831,505.00 Asilimia 90
Ukarabati wa EMD             364,000,000.00 IMF                   335,168,495.00 Asilimia 80
Ujenzi wa nyumba ya mtumishi                90,000,000.00 IMF                  90,000,000.00 Asilimia 50
Ukarabati wa chumba cha CT Scan na XRay              177,375,086.40 IMF                  177,375,086.40 Asilimia 80
15Sokoine – LindiUjenzi wa ICU             560,000,000.00 IMF                  560,000,000.00 Asilimia 30
Ujenzi wa EMD             650,000,000.00 IMF                   650,000,000.00 Asilimia 30
Ujenzi wa               90,000,000.00 IMF                  90,000,000.00 Asilimia 20
  nyumba ya Mtumishi     
Jengo la CT Scan              231,280,000.00 IMF                  231,280,000.00 Ujenzi bado hujaanza 
Ujenzi wa Jengo OPD          3,000,000,000.00 IMF                  3,000,000,000.00  Asilimia 7
16TemekeUkarabati wa ICU             180,000,000.00 IMF                  180,000,000.00 Asilimia 85
Ukarabati wa EMD             130,000,000.00 IMF                   130,000,000.00 Asilimia 97
Upanuzi wa jengo kwa ajili ya CT Scan na X-ray             338,495,909.50 IMF                  338,495,909.50  Asilimia 20
17Tumbi RRHUjenzi wa Jengo la Hospital kwa ajili ya huduma za EMD, Surgical Ward na OPD GOT3,900,000,000.00 bado
Ukarabatai wa EMD              360,666,416.00 IMF                  360,666,416.00 Asilimia 90
Ukarabati wa ICU             326,819,148.00 IMF                  326,819,148.00 Asilimia 98
Ujenzi wa Nyumba ya Mtumishi               90,000,000.00 IMF                  90,000,000.00 Asilimia 35
  Ukarabati wa chumba cha CT Scan             163,022,664.00 IMF                  163,022,664.00 Asilimia 55
JUMLA KUU KUNDI LA 4.3        56,629,115,045.75                   51,309,394,279.74  
5: Ujenzi na Upanuzi wa Majengo mbalimbali ya kutolea huduma  katika Vituo Maalumu
Na.Kituo HusikaLengo la Mradi Gharama za Mradi   Chanzo cha Fedha   Kiasi kilichotolewa   Hatua ya utekelezaji (%)
1Chanjo, IVD MabiboUkarabati, Upanuzi na ujenzi wa miundombinu ya kuhifahia Chanjo – IVD Mabibo1,388,682,288.50CHAI /GAV374,485,879.56Asilimia 52 
2Elimu ya Afya kwa UmmaUjenzi wa kituo cha Kisasa (Health Promotion services) ambapo jengo linaloanza kujengwa ni Jengo la Uchapishaji (Printing and Press2,184,000,000IMF2,184,000,000.00Hatua za awali, maandalizi ya Ujenzi
  Building)    
3Kituo cha Umahiri kwa Magonjwa hatarishi na Milipuko – Kisopwa          Dar es Salaam        Ujenzi wa Kituo cha Umahiri kwa ajili ya matibabu ya magonjwa hatarishi na Milipuko 7,776,000,000GOT & IMF2,900,000,000.00Asilimia 25
JUMLA KUU 5          11,348,682,288.50                                    5,458,485,879.56  
6: Ujenzi na Upanuzi wa Majengo mbalimbali ya kutolea huduma za Mafunzo, Vyuo vya Afya 
Na.Hospitali HusikaLengo la Mradi Gharama za Mradi   Chanzo cha Fedha   Kiasi kilichotolewa   Hatua ya utekelezaji (%)
1Tabora Clinical Officers Training CentreUjenzi wa Jengo la Wodi Maalum (Private wards)261,651,078.35BSF261,651,078.35Asilimia 75
2Ngudu Environmen tal Health SchoolUkarabati Mkubwa wa majengo mbalimbali ndani ya chuo419,538,606.28BSF419,538,606.28Asilimia 90

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *