BASHUNGWA ATOA SIKU 30 TARURA KUFANYA USANIFU WA BARABARA YA SUCA – GOLANI ILI IWEKEWE LAMI.

OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa ametoa mwezi mmoja kwa Meneja wa TARURA Mkoa wa Dar es salaam kufanya upembuzi yakinifu wa barabara Suca – Golani katika halmashauri ya Manspaa ya Ubungo yenye urefu wa kilometa 7.5 ili itengewe bajeti na kujengwa kwa kiwango cha lami.

Bashungwa ametoa maagizo hayo kwa Meneja huyo Mhandisi Geofrey Mkinga wakati wa ziara katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kukagua barabara ya Suca – Gorani inayohudumia kata mbili ya Saranga (Jimbo la Kibamba) na Kata ya Kimara (Jimbo la Ubungo).

Amesema baada ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hasaan kusikia kilio cha muda mrefu cha mawasiliano barabara hiyo amemuagiza kufika katika eneo hilo na kuhakikisha anatatua kero hiyo ya wananchi.

Bashungwa amemuagia Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo kupitia asilimi 60 ya mapato ya ndani inayotengwa kutekeleza miradi ya maendeleo na asilimi 10 kati ya hiyo inayotengwa kwa ajili ya barabara kulingana na Mwongozo wa Ofisi ya Rais TAMISEMI atenge fedha ambazo atashirikiana na TARURA ili kujenga barabara hiyo.

Aidha, Bashungwa amesema Serikali ya awamu ya sita itahakisha inatatua kero za Wananchi wote bila kujali mijini au vijijini ikiwa ni Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapindunzi.

Vile vile, Ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikao kwa timu itayokuwa inafanya upembuzi yakinifu ili kwakamilishe kazi hiyo kwa wakati ya kupata BOQ ili Serikali iweze kuleta fedha za kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *