MORRISON AONGEA KWA UCHUNGU BAADA YA SIMBA KUMUONDOA” NINA MOYO MZITO SANA”

Baada ya Simba Sc Kutangaza kumpumzisha Mchezaji wao Bernad Morrison, Hatimaye Mchezaji huyo ameeleza kuhusu Hatua hiyo

Morrison ameeleza kupitia Ukurasa wake wa Instagram ambapo amesema kuwa

“Nina moyo mzito kutangaza kwamba sitakuwepo kwa muda uliosalia wa msimu huu kwa sababu ya masuala ya kifamilia ambayo ni nje ya uwezo wangu na huenda yakaathiri utendaji wangu wa kazi ikiwa nitaendelea kuitumikia klabu.

Mengi yanahitajika kusemwa kuhusu hilo lakini naitakia klabu kila la kheri katika michezo yetu iliyosalia. Ni matumaini yangu kuwa nitatatue hili haraka iwezekanavyo ili nijiunge na timu tena”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *