
Mke mdogo wa Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso Bi. Zainabu Abdallah ameamua kufunguka mambo mbalimbali kwa kumwelezea Mmewe ambaye ni Aweso
Kupitia Kurasa zake za Mitandao ya Kijamii Bi. Zainabu amefunguka kwa kuandika kuwa
“Pamoja na mapito mazito niliyopitia kwenye ndoa ya kwanza, hukujali ulinipokea kama nilivyo na ukanipa heshma ya kuwa mke wako halali. Nikushkuru sana kwa utu, uvumilivu na mapenzi yako ya dhati kwangu kwa kipindi chote hiki cha miaka 4 ya ndoa yetu.”
_
“Leo nakushkuru Mume wangu kwa kunipa zawadi ya watoto 3 alhamdulillah. Uke wenza sio jambo rahisi, nimevumilia kwa miaka 3 ya ndoa bila ya kutambulika rasmi popote, leo hii mwaka 4 namshukuru M/Mungu kwa kupata heshma ya kutambulishwa mbele ya umma wa watanzania.”

_
“Siku zote umekuwa ukiniunga mkono kwenye safari yangu ya siasa na uongozi, nami naahidi katika safari yako ya siasa na uongozi sitakuacha peke yako.”
_
“Nitaendelea kumuheshimu Dada yangu Mke Mkubwa-Bi Kauthar kama ilivyo siku zote, na nitaendelea kuwalea na kuwatunza watoto wetu wote kama ilivyo siku zote. Zaidi, kuwaenzi wazazi, ndugu, jamaa, rafiki na wote waliotuzunguka. Mwenyezi Mungu atujaalie mwisho mwema inshaaAllah.”
Maneno ya Bi. Zainab Abdallah ambaye ni Mke Mdogo wa Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Aweso

