MTANGAZAJI APIGWA RISASI NA KUFARIKI DUNIA

Mtangazaji wa kituo cha Al jazeera Shireen Abu Akleh, amepigwa risasi na kuuwawa na majeshi ya Israel katika eneo la West Bank, kwa mujibu wa Waziri wa Afya wa Palestina.



Shireen aliuwawa kwa risasi siku ya Jumatano wakati akiripoti uvamizi wa jeshi la Israel katika jiji la Jenin ambapo alikimbizwa hospitali akiwa mahututi na kuthibitishwa kufariki baada ya kufika hospitali.

Jeshi la Israel limesema lililazimika kujihami baada ya kushambuliwa kwa risasi na milipuko wakati likiendesha oparesheni Jenin na kwamba limeanzisha uchunguzi.

Katika tukio hilo mwandishi mwingine wa habari alipigwa risasi ya mgongoni, kwa mujibu wa Waziri wa Afya wa Palestina mwandishi huyo anaendelea kupatiwa matibabu.

Giles Trendle, Mkurugenzi Mtendaji wa Al Jazeera amesema wameshtushwa na kusikitishwa kwa kifo cha Shireen Abu Akleh na kuomba uchunguzi wa kina ufanyike.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *