MEWAKA KUONGEZA UJUZI WA WALIMU WETU NCHINI

Asila Twaha, Kigoma

Mratibu wa Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini(MEWAKA) Tezra Mkama amesema, somo la TEHAMA kwa walimu limekuwa na mtazamo chanya ambapo walimu wamewezeshwa kutumia simu janja kwa kutafuta maudhui ya kufundishia na mbinu za kujifunzia.

Tezra amesema hayo tarehe 10 Mei, 2022 wakati muendelezo wa mafunzo ya MEWAKA yanayoendelea Mkoani Kigoma.

Amesema mafunzo yamekuwa na tija na manufaa kwa walimu katika kuendelea kujifunza pale wanapoenda kutekeleza majukumu yao kazini.

Kupitia mafunzo haya sasa walimu wanaweza kutumia simu zao kutafuta maudhui Ya kufundishia na pia wamepitishwa kwenye miongozo inayowezesha kufundisha kwa kutumia maktaba mtandao (ELMS) na mafunzo haya yatawezesha walimu kutekeleza mtaala mpya wa masomo kwa wanafunzi.

‘’Utekelezaji wa mtaala mpya una lengo la kuwajengea uwezo wanafunzi kupata mbinu za zaidi za ujifunzaji kwenye mazingira tofauti tofauti.

Pia amesema walimu wanaweza kuendelea kujifunza kupitia vituo vya walimu vilivyopo kwenye maeneo yao, wakakutana na wakabadilishana uzoefu na kutatua changamoto zao kitu ambacho kitaongeza tija katika kutekeleza majukumu yao.

Kwa upande wake mshiriki wa mafunzo ya MEWAKA Mwl. Pamela Aidan(Shule ya Msingi Nyete) ameishukuru Serikali kuwepo kwa mfunzo amesema, hapo awali mbinu walizokuwa wanatumia zimekuwa ni za zamani tofauti na sasa ambapo kumekua na mabadiliko ya teknolojia.

Kupitia mafunzo haya tumejifunza mbinu mpya za kuweza kuzitumia kwa manufaa ya wanafunzi na kuweza kufanya vizuri katika masomo yao.

Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini (MEWAKA) katika Mkoa wa Kigoma ina jumla ya washiriki 770 na mfunzo hayo yanaendela katika Halmashuri ya Uvinza, Kigomaa Dc, Kibondo na Kasulu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *