NAIBU WAZIRI NDEJEMBI AWAPA RUNGU WAKAGUZI

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deo Ndejembi amewataka Wakaguzi wa Ndani kusimamia kwa weledi ukaguzi wanaoufanya ili kuweza kuisaidia Serikali kuepukana na hasara ambazo imekua inapata au kusubiri kuvumbuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Ndejembi ameyasema hayo alipokua akizungumza na Wakaguzi wa Ndani wakati akifungua mkutano wao jijini Tanga ambapo amewaahidi kuwa Serikali itahakikisha inafanyia kazi maboresho waliyoomba wapatiwe ili kuwafanya kuwa miongoni mwa idara rasmi za Serikali.

“Wakati tunapohitaji kutambulika rasmi kama Idara yenye nguvu kwenye Taasisi za Umma basi tusisahau wajibu wetu kama wakaguzi wa ndani, mna wajibu mkubwa sana wa kuisaidia Serikali. Haya yote mnayoyaona kwenye ripoti za CAG ni kufeli kwa kitengo cha wakaguzi wa ndani kuyaona hayo, hivyo niwaombe muisaidie Nchi yenu,” Amesema Ndejembi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *