DIAMOND NA ZUCHU WASHANGAA VIDEO YAO KUFUNGIWA

Baada ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) Kutangaza kuzuia Kuoneshwa kwa Video ya Mwanamziki na Mkurugenzi wa WCB, Naseeb Abdul “Diamond Platnumz” aliomshirikisha Msanii wake ambaye yuko kwenye Lebo hiyo Zuhura Othman Soud”Zuchu” ya wimbo unaoitwa Mtasubiri

Leo hii Msanii Zuchu ameweka Chapisho kwenye Ukurasa wake wa Instagram akionesha kushangazwa na Maamuzi hayo ambapo Zuchu ameandika

“Huu ndio umauti wa Tasnia hii unapoanzia .Sijui nileleze vipi hisia zangu zipokelewe kwa heshima ya kutosha na utii bila ya kuchukuliwa kama mjeuri ila kwa hili mumetuonea .Sisi ni vijana tunaotafuta rizki bila ya kuchoka lakini pengine Wazazi wetu @basata.tanzania mmekua mstari wa mbele kutuvunja nguvu mbele ya jamii bila kujali hisia muda vipaji na uwekezaji unaofanyika .Hapo awali mlitoa mirabaha Wasanii wa Wcb Hatukunusa Top List Wakati kitwakwimu za namba ,MAUZO na ufanyaji vizuri Katika Chati zote Kasoro yenu nyinyi @basata.tanzania @cosotatanzania Nini shida wazazi wetu .Inawezekana vipi . Kisha hapo Tunalaumiwa kwa kutoshiriki Tuzo .Ni wazi kua Hii imekua wazi sasa kama mamlaka ya kisanaa inafanya kazi Kupinga juhudi za WCB lakini pengine hii hasira mnayoipandikiza juu yetu tunaihitaji kwa mafanikio chanya yetu na mashabiki zetu wanaotupigania .mwisho niseme kazi iendelee Mashabiki zetu ,Maboss zetu mtusamahe sana kwa kero mnayokutana nayo haiko mikononi mwetu Wenye mamlaka washasema sisi ni nani? tuwe na subra na msituache mana nyinyi ndo kimbilio letu la mwisho Nawapenda sana .Sikukuu njema KAZI IENDELEE”

Kwenye Chapisho hilo Diamond Platnumz ni Miongoni mwa walioandika maoni yao ambapo ameandika kuwa

“Najiuliza kuna baya lolote limefanyika kwenye hio scene? Mlivaa vimini? hapana!… Nlitwerk ama Mliimba matusi humo kanisani? Hapana!.. Mlivuta sigara au bangi humo? Hapana!… Mlikiss ama Kunywa Pombe humo Hapana!… Simu iliita, ulipokelea ndani? Hapana…je kushoot kanisani ni sisi wa kwanza? hapana! Kuna wengine walishoot Videos na Movie tena wao walifanya kwa kulidhalilisha kabisa kanisa… Nyimbo zao Zili fungiwa??? hapana! …. Halaf kesho utaniuliza kwanini Nilikataa kushiriki Tuzo za Basata…NCHI ya Wenyewe hii Zuuh… Kikubwa Mungu na Mashabiki wanatupenda hio inatosha…tuendelee kuwawakilishia Taifa lao, leo bendera inapeperukia Ethiopia InshaAllah 🇹🇿”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *