
Mahakama kuu Kanda ya Arusha imemuachia huru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili baada ya kubaini kulikuwa na mapungufu katika mwenendo mzima wa kesi.
Sabaya na wenzake walikata rufaa kupinga hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela iliyotolewa Oktoba 2021 na Mahakama hiyo ambapo Mrufani namba mbili Silvester Nyegu na namba tatu Daniel Mbura hawakupewa haki ya kumhoji Shahidi namba mbili wa Jamhuri na kutokufanya hivyo kunawanyima haki yao msingi.
Jaji aliyekuwa akisikiliza rufaa hiyo, Ezedekia Kisanya amesema kulikuwa na mkanganyiko kwenye mwenendo wa usikilizwaji wa kesi hiyo ikiwemo kutofautiana kwa mashahidi na kuufanya ushahidi kuwa batili.
Jaji amesema watakuwa huru endapo watakuwa hawana kesi nyingine kwenye Mahakama yoyote.
