HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT. ASHATU K. KIJAJI (MB.),AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2022/2023

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA

HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT. ASHATU K. KIJAJI (MB.),
WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA
AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2022/2023

Dodoma Mei, 2022

VIFUPISHO

BICO – Bureau for Industrial Cooperation
BRELA – Business Registrations and Licensing Agency
CAMARTEC – Centre for Agricultural Mechanization and Rural Technology
AfCFTA – Africa Continental Free Trade Area
CNC – Computer Numerical Control Machine
COMESA – Common Market for Eastern and Southern Africa
COSTECH – Commission for Science and Technology
CPB – Cereals and Other Produce Board of Tanzania
DITF – Dar es Salaam International Trade Fair
EAC – East African Community
EPZ – Export Processing Zones
EPZA – Export Processing Zones Authority
EU – European Union
FCC – Fair Competition Commission
FCT – Fair Competition Tribunal
FDI – Foreign Direct Investment
ICDs – Inland Container Depots
ICT – Information and Communications Technology
ITC – International Trade Centre
JBCs – Joint Border Committees
KMTC – Kilimanjaro Machine Tools Manufacturing Company
MMA – Mechandized Marks Act
MoU – Memorandum of Understanding
MSMEs – Micro, Small and Medium Enterprises

MSY – Magonjwa Sugu Yasiyoambikiza
NBM – National Brand Mark
NDC – National Development Corporation
NEDF – National Entrepreneurship Development Fund
NIDS – National Investment Development Strategy
OPRAS – Open Performance Review and Appraisal System
PCP – Programme for Country Partnership
PhD – Doctor of Philosophy
PSSSF – Public Service Social Security Fund
REPOA – Research on Poverty Alleviation
RITA – Registration, Insolvency and Trusteeship Agency
SACCOS – Savings and Credit Co-Operative Society
SADC – Southern African Development Community
SEA – Strategic Environmental Assessment
SEZ – Special Economic Zone
SIDO – Small Industries Development Organization
SIDP – Sustainable Industrial Development Policy
SMEs – Small and Medium Enterprises
TAHA – Tanzania Horticultural Association
TAMCO – Tanzania Automobiles Manufacturing Company
TAMISEMI – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
TANePS – Tanzanian National e-Procurement System

TANESCO – Tanzania Electric Supply Company Limited
TANTRADE – Tanzania Trade Development Authority
TARURA – Tanzania Rural and Urban Road Agency
TASPA – Tanzania Spices Association
TASUPA – Tanzania Sunflower Processors Association
TBPL – Tanzania Biotech Products Limited
TBS – Tanzania Bureau of Standards
TDCs – Technology Development Centres
TEHAMA – Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
TEMDO – Tanzania Engineering and
Manufacturing Design Organisation
TIC – Tanzania Investment Centre
TIRDO – Tanzania Industrial Research and Development Organization
TMDA – Tanzania Medicines and Medical Devices Authority
TMEA – Trade Mark East Africa
TPC – Training Cum Production Centres
UKIMWI – Upungufu wa Kinga Mwilini
UNCTAD – United Nations Conference on Trade and Development
VICOBA – Village Community Banks
VVU – Virusi Vya Ukimwi
WCF – Workers Compensation Fund
WMA – Weights and Measures Agency
WRRB – Warehouse Receipts Regulatory Board
WTO – World Trade Organization
ZaSCI – Zanzibar Seaweed Cluster Initiative
ZSTC – Zanzibar State Trading Corporation

YALIYOMO

1 UTANGULIZI …………………………………………………. 1

2 HALI NA MWENENDO WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA NCHINI ……………………………………. 9

2.1 Uwekezaji……………………………………………………9

2.2 Uwekezaji katika Viwanda ……………………………10

2.3 Biashara …………………………………………………..13

2.4 Mwenendo wa Bei za Bidhaa Muhimu Nchini ….18

3 UBORESHAJI WA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA NCHINI ……………………. 24

3.1 Sera …………………………………………………………24

3.2 Sheria ………………………………………………………24

3.3 Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara
Nchini………………………………………………………26

4 UMUHIMU NA MCHANGO WA SEKTA YA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA NCHINI….. 28

5 UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI KATIKA MWAKA 2021/2022……………………………………… 30

5.1 Utekelezaji wa Bajeti kwa Mwaka 2021/2022 ….30

5.1.1 Bajeti iliyoidhinishwa na Fedha iliyopokelewa kwa Mwaka 2021/2022 ………………………………..30

5.1.2 Fedha za Matumizi ya Kawaida ……………………..31

5.1.3 Fedha za Matumizi ya Miradi ya Maendeleo …….32

5.2 Utekelezaji wa Mipango ……………………………….33

5.2.1 Sekta ya Uwekezaji ……………………………………….33

5.2.2 Sekta ya Uwezeshaji Kiuchumi na Maendeleo ya
Sekta Binafsi ………………………………………………..43

5.2.3 Sekta ya Viwanda …………………………………………50

5.2.4 Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo ….75

5.2.5 Sekta ya Mtangamano wa Biashara ………………..79

5.2.6 Sekta ya Maendeleo ya Biashara ……………………88

5.2.7 Masuala Mtambuka……………………………………. 124

5.2.8 Mawasiliano Serikalini ……………………………….. 126

5.2.9 Usimamizi wa Fedha na Ununuzi ………………… 127

5.2.10  TEHAMA na Takwimu ................................. 129 

6 MWELEKEO WA SEKTA YA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA …………………………………………… 130

7 VIPAUMBELE KWA BAJETI YA MWAKA 2022/2023……………………………………………….. 139

8 MALENGO YA MWAKA 2022/2023………………… 142
8.1 Idara na vitengo vya Wizara……………………….. 142

8.1.1 Maendeleo ya Uwekezaji …………………………….. 142

8.1.2 Uwezeshaji Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta
Binafsi ……………………………………………………… 143

8.1.3 Maendeleo ya Viwanda ………………………………. 144

8.1.4 Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo…………….. 145

8.1.5 Mtangamano wa Biashara ………………………….. 146

8.1.6 Maendeleo ya Biashara………………………………. 147

8.1.7 Maendeleo ya Rasilimali Watu na Utoaji wa
Huduma ……………………………………………………. 148

8.2 Taasisi zilizopo chini ya Wizara ………………….. 149

8.2.1 Kituo cha Uwekezaji Tanzania …………………….. 149

8.2.2 Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi…………………………………………………… 150

8.2.3 Shirika la Taifa la Maendeleo ………………………. 151

8.2.4 Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji
kwa Mauzo Nje ya Nchi ………………………………. 152

8.2.5 Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda
Tanzania…………………………………………………… 153

8.2.6 Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini . 155

8.3 Shirika la Uhandisi na Usanifu wa Mitambo
Tanzania………………………………………………… 156

8.3.1 Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo ………… 158

8.3.2 Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ………………. 159

8.3.3 Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni
(BRELA)…………………………………………………….. 161

8.3.4 Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala…. 162

8.3.5 Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara
Tanzania…………………………………………………… 164

8.3.6 Wakala wa Vipimo……………………………………… 164

8.3.7 Tume ya Ushindani ……………………………………. 165

8.3.8 Baraza la Ushindani………………………………… 166

8.3.9 Chuo cha Elimu ya Biashara……………………. 166

9 MAOMBI YA FEDHA KWA MWAKA 2022/2023….168
9.1 Makisio ya Maduhuli kwa Mwaka
2022/2023 …………………………………………….. 168

9.2 Maombi ya Fedha kwa Mwaka 2022/2023 … 168

9.3 HITIMISHO ……………………………………………… 169  

ORODHA YA MAJEDWALI

Jedwali Na. 1: Biashara kati ya Tanzania na China kwa
Mwaka 2013 – 2021 (Dola za Marekani „000,000‟) .. 171

Jedwali Na. 2: Biashara kati ya Tanzania na India kwa
Mwaka 2010-2021 (Dola za Marekani „000,000‟)…171

Jedwali Na. 3: Biashara kati ya Tanzania na Japani kwa
Mwaka 2010-2021 (Dola za Marekani „000,000‟)..172

Jedwali Na. 4: Biashara kati ya Tanzania na Jumuiya ya Ulaya kwa Mwaka 2010-2021 (Dola za Marekani
„000,000‟) ……………………………………………………173

Jedwali Na. 5: Biashara ya Bidhaa kati ya Tanzania na
Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Mwaka 2010 – 2021 (Dola za Marekani “000,000”) ………..173

Jedwali Na. 6: Biashara kati ya Tanzania na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kwa Mwaka 2010 – 2021 (Dola za Marekani
„000,000‟) ……………………………………………………174

Jedwali Na. 7: Mwenendo wa Bei ya Nondo…………….175

Jedwali Na.8: Mwenendo wa Bei Mabati…………………176

Jedwali Na. 9: Mwenendo wa Bei ya Saruji …………….177

Jedwali Na.10: Uwezo wa Uzalishaji wa Viwanda vya
Saruji………………………………………………………….178 Jedwali Na. 11: Mwenendo wa Bei za Mafuta ya Kula .. 180

Jedwali Na. 12: Wastani wa Bei za Mazao Makuu ya
Chakula Mwezi Machi, 2021……………………………181

Jedwali Na. 13: Mwenendo wa Mchango wa Sekta ya
Viwanda katika Pato la Taifa…………………………..182
Jedwali Na. 14: Ukuaji wa Sekta ya Viwanda …………182

Jedwali Na. 15: Ajira katika Sekta ya Viwanda 2013 –
2021…………………………………………………………..182

Jedwali Na. 16: Usajili wa Miradi ya Uwekezaji katika
Kituo cha Uwekezaji Tanzania kwa Kipindi cha Julai 2021 hadi Machi 2022…………………………………….183

Jedwali Na. 17: Usajili wa Miradi ya Uwekezaji EPZA
Julai 2021 hadi Machi, 2022 …………………………..184

Jedwali Na. 18: Mchanganuo wa Mikopo iliyotolewa kupitia Mfuko wa NEDF Kimkoa kwa Kipindi cha
Julai, 2021 hadi Machi, 2022…………………………… 187

  1. UTANGULIZI
  2. Mheshimiwa Spika, Kutokana na taarifa iliyowasilishwa leo hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira ambayo ilichambua Bajeti ya Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara tarehe 24, 25 na 28 Machi, 2022, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako sasa likubali kupokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Mwaka 2021/2022. Aidha, ninaliomba Bunge lako Tukufu likubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Kawaida na Miradi ya Maendeleo ya Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kwa Mwaka 2022/2023.
  3. Mheshimiwa Spika, Napenda kuanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema kwa kutujalia waja wake baraka na afya tele na hivyo kutuwezesha kuwa pamoja leo kutekeleza wajibu wetu kwa Taifa. Naomba tuungane sote kumuomba Mwenyezi Mungu aendelee kutujaza yaliyo mema na kuyapa kibali chake masuala tuliyoyapanga ili yampendeze na yafanikiwe.
  4. Mheshimiwa Spika, Napenda nitumie fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuliongoza Taifa letu kwa ujasiri na uzalendo wa hali ya juu. Mwenyezi Mungu azidi, kumpa afya njema, hekima na busara. Aidha, nitumie fursa hii pia ikiwa nawasilisha Hotuba yangu ya kwanza ya Bajeti nikiwa Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara kumshukuru kwa dhati Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuniamini na kuniteua kuongoza Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara. Hakika ni dhamana kubwa kwangu na nimeipokea kwa moyo mkunjufu. Napenda kumhakikishia Mheshimiwa Rais kuwa, kwa kushirikiana na Naibu Waziri wangu, Viongozi na Watumishi wa Wizara na Taasisi zake nitayatekeleza majukumu aliyonikabidhi na kufuata miongozo anayonipatia kwa moyo, uwezo, juhudi na ujuzi wangu wote kwa kushirikiana na Baraza la Mawaziri, Waheshimiwa Wabunge na Watanzania wote.
  5. Mheshimiwa Spika, Napenda kumshukuru Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kuchochea maendeleo ya uwekezaji, viwanda na biashara. Pia, namshukuru Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miongozo yake yenye kutia chachu na hamasa katika kuimarisha Sekta ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara nchini. Aidha, ninampongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Hotuba yake ya Bajeti iliyowasilishwa kwenye Bunge lako Tukufu tarehe 6 Aprili, 2022. Hotuba hiyo imetoa mwelekeo na dira ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa Mwaka 2022/2023 ambapo Wizara yangu itaizingatia katika utekelezaji wake.
  6. Mheshimiwa Spika, Napenda pia kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi; Mheshimiwa Othman Masoud Othman, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar; na Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar kwa kuendelea kuelekeza na kusimamia masuala yanayoimarisha Muungano wetu na kuwaletea Watanzania maendeleo. Aidha, namshukuru Mheshimiwa Omar Said Shaban, Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda (SMZ) na Mheshimiwa Mudrick Soraga, Waziri wa Uwekezaji (SMZ) kwa ushirikiano wanaonipatia katika kutekeleza masuala ya Sekta ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara.
  7. Mheshimiwa Spika, Ninapenda kukupongeza wewe binafsi na Naibu Spika kwa kuchaguliwa kwa kura za kishindo kuliongoza Bunge la Kumi na Mbili (12) la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hiyo inadhihirisha namna Waheshimiwa Wabunge walivyo na imani kubwa kwenu katika kuliendesha Bunge hili kwa umahiri mkubwa na kuweza kusimamia na kuishauri Serikali ipasavyo.
  8. Mheshimiwa Spika, Napenda pia kuipongeza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa David Mwakiposa Kihenzile, Mbunge wa Mufindi Kusini, na Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Eric James Shigongo, Mbunge wa Buchosa na Waheshimiwa Wajumbe wote wa Kamati hiyo kwa ushauri na umakini wao wakati wa kujadili Mpango na Makadirio ya Matumizi ya Wizara kwa Mwaka 2022/2023. Ushauri na maelekezo yao yamekuwa msingi muhimu katika kuandaa Hotuba hii ninayoiwasilisha leo. Vilevile, nampongeza Mheshimiwa Emmanuel Lekishon Shangai, kwa kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro na Mheshimiwa Shamsi Vuai Nahodha, kwa kuteuliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia, nichukue fursa hii kumpongeza, Mheshimiwa Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi (Mb.), kwa kuteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Nawaahidi kuwapa ushirikiano unaohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya ujenzi wa Taifa letu.
  9. Mheshimiwa Spika, Niwapongeze pia Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge, Katibu wa Bunge na Watendaji wote wa Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushirikiano mzuri ambao Wizara na wadau wetu wameendelea kupata.
    Niwahakikishie kuwa tutaendeleza na kuudumisha ushirikiano huo ili Watanzania wanufaike na matokeo chanya ya utekelezaji wa majukumu ya kisekta.
  10. Mheshimiwa Spika, Napenda kutumia fursa hii kuwashukuru kwa dhati wapiga kura wote wa Jimbo la Kondoa kwa imani yao kwangu, kwa kunipa moyo na ushirikiano mzuri ulioniwezesha kuchaguliwa kuwa Mbunge wao na pia katika kutekeleza majukumu yangu kama mwakilishi wao katika Bunge hili. Naishukuru pia familia yangu, ndugu na jamaa kwa dua zao na ushirikiano wao mzuri unaoniwezesha kuwatumikia Watanzania na hususan wawekezaji, wanaviwanda na wafanyabishara bila ya kuchoka. Nawaombeni tuendelee kushikamana ili tufikie malengo tuliyokusudia.
  11. Mheshimiwa Spika, Ninaomba kutumia fursa hii kuwashukuru viongozi na watendaji wote wa Sekta Binafsi. Kwa uchache, napenda kuwatambua: Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania -TPSF; Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania – CTI; Chama cha Wafanyabiashara,
    Viwanda na Kilimo Tanzania – TCCIA; Baraza la Kilimo
    Tanzania – ACT; Chama cha Wadau wa Ngozi Tanzania – LAT; Chama cha Wafanyabiashara Wanawake – TWCC; na Vikundi vya Biashara Ndogo (VIBINDO) kwa michango yao katika kuendeleza uwekezaji, viwanda, biashara, masoko, viwanda vidogo na biashara ndogo.
  12. Mheshimiwa Spika, Nawashukuru pia wamiliki na waandishi wa vyombo vya habari kwa mchango wao mkubwa katika kuelimisha umma wa Watanzania kuhusiana na utendaji wa Wizara, taasisi na uendelezaji wa Sekta zake, kuvutia wawekezaji na kuhimiza uzalishaji viwandani. Nawaomba tuendeleze ari hiyo kwa lengo la kukuza uelewa kwa umma ili washiriki kikamilifu katika kutekeleza masuala ya kuendeleza sekta hii na kutia chachu zaidi katika mafanikio tuliyoyapata.
  13. Mheshimiwa Spika, Hotuba hii ya Bajeti ninayoiwasilisha leo ni matokeo ya uratibu na ushirikiano mzuri wa Viongozi wenzangu katika Wizara, akiwemo Mheshimiwa Exaud S. Kigahe – Mbunge wa Mufindi Kaskazini Naibu Waziri; Prof. Godius W. Kahyarara, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara; Dkt. Islam S. Salum, Katibu Mkuu wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda (SMZ); Dkt. Habiba Hassan Omar, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji (SMZ); Dkt. Hashil T. Abdallah, Naibu Katibu Mkuu – Viwanda na Biashara; Bw. Ally S. Gugu, Naibu Katibu Mkuu – Uwekezaji, Wakurugenzi; Wakuu wa Vitengo na Taasisi na Wafanyakazi wote wa Wizara. Napenda kuwapongeza sana na kuwasihi kuendeleza moyo huo wa kujituma katika kuwatumikia Watanzania. Aidha, namshukuru Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali na Wachapishaji wengine kwa kuchapisha machapisho mbalimbali ya Wizara kwa wakati.
  14. Mheshimiwa Spika, Wizara inafanya kazi kwa kushirikiana kwa karibu na wadau mbalimbali katika kuendeleza Sekta ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara. Hivyo, ninapenda kutumia nafasi hii kuwashukuru wadau wote wakiwemo Washirika wetu wa Maendeleo (Development Partners) na pia wadau wa ndani.
  15. Mheshimiwa Spika, Ninapenda kuungana na Viongozi wenzangu kutoa pole kwa Watanzania wote waliokumbwa na kadhia ya kuondokewa na wapendwa wao. Kwa namna ya pekee natoa pole kwa familia na wapiga kura wa Jimbo la Ngorongoro kwa kuondokewa na aliyekuwa Mbunge wao Mheshimiwa William Tate Olenasha na Mheshimiwa Irene Alex Ndyamkama, Mbunge wa Viti Maalum Rukwa. Aidha, nawapa pole wananchi mbalimbali waliokumbwa na kadhia ya mafuriko na ajali nchini katika Mwaka huu na kusababisha majeruhi, ulemavu na uharibifu mkubwa wa mali. Mwenyezi Mungu awatie nguvu na kuwapa ahueni waathirika wote ili warejee katika hali njema na hivyo kuendelea kulijenga Taifa letu.
  16. Mheshimiwa Spika, Ninawapongeza Mawaziri wote walionitangulia kuwasilisha na kupitishiwa Bajeti zao za Mwaka 2022/2023 hapa Bungeni. Ni matumaini yangu kuwa mipango na bajeti zilizopitishwa zitaendelea kuwa chachu na kuleta ufungamanisho wenye tija na Sekta ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara.
  17. Mheshimiwa Spika, Taarifa ya utekelezaji ninayoiwasilisha inabainisha mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo, Hotuba hii imeainisha Hali na Mwenendo wa Sekta; Uboreshaji wa Mazingira ya uwekezaji, viwanda na ufanyaji biashara nchini; Mchango wa Sekta; Utekelezaji wa Mpango na Bajeti 2021/2022; Changamoto na jitihada za kutatua changamoto hizo; Malengo na Vipaumbele vya Sekta kwa Mwaka 2022/2023; Mwelekeo wa Sekta; na Maombi ya Bajeti ya
    Mwaka 2022/2023.
  18. Mheshimiwa Spika, Baada ya maelezo hayo ya utangulizi, naomba kutoa Taarifa ya Utekelezaji wa kazi za Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kwa kipindi cha Mwaka 2021/2022 na Malengo ya Mwaka 2022/2023.

2 HALI NA MWENENDO WA UWEKEZAJI,
VIWANDA NA BIASHARA NCHINI

2.1 Uwekezaji

  1. Mheshimiwa Spika, Tanzania ni eneo la kimkakati kijiografia na lenye rasilimali nyingi zenye kuvutia uwekezaji katika sekta mbalimbali za uchumi zikiwemo viwanda, madini, utalii, kilimo na biashara. Uwekezaji huo ambao hufanywa kwa kiwango kikubwa na Sekta Binafsi umechochewa na uwepo wa mazingira rafiki ya uwekezaji na mfumo wa kitaasisi na kisheria wa kusimamia uwekezaji nchini. Mifumo hiyo, pamoja na mambo mengine, inatoa vivutio vya uwekezaji kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kupitia TIC, EPZA na Wizara za kisekta. Sheria ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji (SEZ/EPZ) ya Mwaka 2002 pamoja na Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 pamoja na Marekebisho yake ya Mwaka 2017, Tanzania imeendelea kuvutia na kuchochea uwekezaji wa ndani na mitaji kutoka nje (Foreign Direct Investment – FDI).
  2. Mheshimiwa Spika, Serikali imejielekeza katika uwekezaji mkubwa wa ujenzi wa miundombinu ya msingi na saidizi ikiwemo ya umeme, mawasiliano, maji na usafirishaji kwa njia ya barabara, maji, reli na anga ambayo ni kichocheo kikubwa cha uwekezaji. Vilevile, maboresho ya mazingira ya uwekezaji na biashara nchini kupitia utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara Nchini unatoa fursa zaidi kwa ushiriki wa Sekta Binafsi katika shughuli za uzalishaji nchini. Kutokana na jitihada mbalimbali, Tanzania imeweza kusajili na kuvutia uwekezaji mkubwa zaidi katika sekta mbalimbali za kiuchumi ambao utaleta fursa nyingi za ajira, mapato ya kodi na yasiyo ya kodi kwa Serikali, kuongezeka kipato cha mtu mmoja mmoja na hivyo kuchangia katika kupunguza umaskini.

2.2 Uwekezaji katika Viwanda

  1. Mheshimiwa Spika, Uwekezaji katika Sekta ya Viwanda umeendelea kukua na kumilikiwa kwa sehemu kubwa na Sekta Binafsi. Uwekezaji huo wa viwanda uko katika Maeneo Maalum ya Uwekezaji (EPZ na SEZ) na maeneo binafsi. Viwanda vimesambaa nchi nzima na sehemu kubwa ya viwanda hivyo ni vidogo sana ambavyo ni 62,400 sawa na asilimia 77.07, wakati vidogo ni 17,267 sawa na asilimia 21.33, vya kati ni 684 sawa na asilimia 0.84 na vikubwa ni 618 sawa na asilimia 0.76. Kati ya Viwanda Vikubwa 618 (Vinavyoajiri kuanzia watu 100), Viwanda 41 pekee vinaajiri zaidi ya watu 500.Viwanda vingi vinajishughulisha na uongezaji thamani ya mazao ya kilimo na vinajielekeza katika kutumia malighafi za ndani kuzalisha bidhaa hizo.
  2. Mheshimiwa Spika, Kutokana na usajili wa viwanda chini ya TIC na EPZA, inategemewa kuwa viwanda vipya vikubwa 500 vitajengwa kufikia mwaka 2025 na kufanya idadi ya sasa ya viwanda vikubwa vinavyoajiri wafanyakazi zaidi ya 500 kuongezeka kutoka 41 hadi kufikia 541. Tayari Serikali ya Awamu ya Sita imekwishaanza utekelezaji wa Kongani kubwa ya Viwanda ya Kwala ambayo itakuwa na viwanda 200 vikubwa kwa ajili ya kutengeneza nguo, vifaa vya umeme, vifaa vya ujenzi, dawa na aina nyingine. Mradi huo umekwishaanza na awamu ya kwanza itakamilika ifikapo mwaka 2024 na viwanda vitatoa ajira za moja kwa moja 100,000 na zisizo za moja kwa moja 300,000. Aidha, uwekezaji katika eneo hilo unakadiriwa kugharimu Dola za Marekani Bilioni 3 na unalenga kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha bidhaa za viwanda katika Soko la Pamoja la Afrika.
  3. Mheshimiwa Spika, Viwanda vingine vitatokana na uwekezaji katika Maeneo Maalum ya Nala – Dodoma ambapo tayari Serikali imeanzisha Eneo Maalum la Uwekezaji, pamoja na kongani nyingine kubwa itakayojengwa katika Mkoa wa Mwanza. Uwekezaji huo utafanywa na Serikali ikishirikiana na Sekta Binafsi. Ni matarajio yetu kuwa, uwekezaji huo utachochea matumizi ya kiuchumi ya miundombinu ya ndani ya nchi hasa Reli ya Kisasa ya SGR, Bandari za Maziwa Makuu, Bahari pamoja na barabara. Matokeo makubwa yanatarajiwa kupatikana katika kuongeza wigo wa kodi, kukuza teknolojia na kwa Taifa letu kujitosheleza kwa bidhaa ambazo zimekuwa zikiagizwa kutoka nje ya nchi.
    Aidha, uwekezaji huo utaifanya Tanzania kuwa nguzo ya uchumi ya Bara la Afrika (Africa Economic Power House) ikitumia fursa yake iliyopewa na Mwenyezi Mungu ya kuwa kiunganishi kupitia Bahari – GateWay.
  4. Mheshimiwa Spika, Kwa upande wa Viwanda Vidogo na vya Kati, Serikali itaendelea kushirikiana na wadau kuendeleza mkakati wake wa ujenzi wa viwanda vidogo vya kisasa vinavyotumia teknolojia ya hali ya juu ili kuzalisha bidhaa ambazo zinaagizwa kwa wingi kutoka nje ilhali zinaweza kutengenezwa hapa nchini. Bidhaa hizo ni pamoja na toothpicks, cotton-buds, sukari, mafuta ya kula, tomato source na nyinginezo. Viwanda hivyo vitatengewa Kongani maalum na kwa kuanzia kuna Kongani ya Dumila – Morogoro na Kitaraka – Singida. Utekelezaji wa miradi hiyo unafanywa kwa pamoja baina ya Sekta Binafsi na Serikali kupitia Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) na Mpango wa Maendeleo ya Viwanda Vidogo chini ya NSSF, Benki ya Azania na SIDO. Matokeo ya Mpango huo ni kukuza teknolojia, kuwezesha nchi kujitosheleza kimahitaji kupitia viwanda vidogo ambavyo uwekezaji wake hautumii mitaji mikubwa, kuongeza fursa za masoko ya mazao na kuondoa utegemezi wa bidhaa za nje ambazo zinaweza kuzalishwa nchini.
    2.3 Biashara
  5. Mheshimiwa Spika, Tanzania ina fursa mbalimbali za masoko ya kuuza mazao na bidhaa inayozalisha. Uwezo wa nchi kuuza nje mazao na bidhaa unaongezeka na hususan uuzaji wa bidhaa zilizoongezwa thamani katika masoko ya ndani, kikanda na kimataifa. Matumizi ya bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi umeongezeka na hivyo kuchochea kupunguza uagizaji nje wa baadhi ya bidhaa na malighafi na hivyo kuiwezesha nchi kupunguza matumizi ya fedha za kigeni. Pamoja na kuwepo kwa uagizaji wa bidhaa za mwisho (final products), kumekuwa na ongezeko la uagizaji nje wa bidhaa za kati na za mitaji (intermediate input and capital goods) zinazotokana na mahitaji ya viwanda vinavyowekeza hapa nchini.
  6. Mheshimiwa Spika, Kutokana na athari za UVIKO-19 na vita inayoendelea kati ya nchi ya Urusi na Ukraine, ugavi wa mazao na bidhaa unaendelea kuathiri bei za bidhaa mbalimbali za viwandani hususan zile zinazotegemea malighafi kutoka nje au kuagizwa kutoka nje zikiwemo mafuta ya kula, mafuta ya petroli na ngano. Hii inatokana na utegemezi wa biashara ya malighafi na bidhaa hizo ambazo uzalishaji na usambazaji wake unaguswa na uchumi wa Urusi na Ukraine. Hali hiyo itaathiri urari wa biashara kutokana na kuyumba kwa biashara katika masoko hayo ikiwianishwa na uwezo wa kulipia bidhaa kutoka nje.
  7. Mheshimiwa Spika, Katika kukabiliana na changamoto hizo, Serikali imechukua hatua zenye matokeo ya muda mfupi na muda mrefu. Kwa upande wa masuala ya mafuta ya kula ya alizeti, katika Mkataba wa Makubaliano (MoU) ya uwekezaji yaliyofikiwa mwaka 2022 huko Marekani, kuna Mkataba wa Mradi wa kuongeza uzalishaji wa mafuta ya kula (Kitaraka – Manyoni) ambao utachochea jitihada za Serikali kuhakikisha kuwa inaimarisha uzalishaji wa bidhaa hizo ambazo tunategemea soko la nje. Pia kuna Mkataba wa mradi unaolenga kuongeza uzalishaji wa ngano. Aidha, Waziri Mkuu aliagiza TARI kugawa miche ya kisasa ya michikichi huko Kigoma ili kuongeza uzalishaji wake. Vilevile, mikoa ya Singida, Dodoma na Simiyu ni mikoa ya kimkakati ya kuzalisha alizeti ili kuongeza upatikanaji wa mafuta ya kula nchini. Jitihada hizo pia zinachochewa na Mradi wa Kuwajengea Uwezo Wazalishaji na Wachakataji Wadogo na wa Kati walio kwenye Mnyororo wa Thamani (Strengthening MSMES Capacity to Improve Competitiveness in Domestic, Regional and International Markets for Selected Value Chains Project – EIF Tier 2) wa zao la Chikichi ili waweze kuyafikia Masoko ya Ndani, Kikanda na Kimataifa. Pia, Wizara kupitia SIDO itajenga Viwanda Viwili (2) vidogo vya kuzalisha mafuta ya Mawese katika Kijiji cha Nyamuhoza kilichoko kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma (DC) na Kijiji cha Sunura kilichoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Ujiji. Vilevile, Wizara kupitia SIDO ilitoa mafunzo ya Kilimo Biashara (Farming as a Business) kwa vikundi 50 vya wanawake na vijana wa vijiji vya Nyamuhoza na Sunura ambapo Viwanda viwili
    (2) Vidogo vitajengwa katika maeneo hayo.
  8. Mheshimiwa Spika, Mauzo ya bidhaa kwenye soko la China yaliongezeka kutoka Dola za Marekani Milioni 238.9 mwaka 2020 hadi Dola za Marekani Milioni 273.1 mwaka 2021, sawa na ongezeko la asilimia 14.31. Ongezeko hilo linatokana na uzalishaji na uuzaji kwa wingi mbegu za ufuta. Bidhaa zingine zilizouzwa kwa wingi ni pamoja na tumbaku, pamba, jute, manila (coconut, abaca) na nguo na mavazi. Manunuzi ya Tanzania kutoka China yalikuwa Dola za Marekani Milioni 1,940.3 mwaka 2020 ikilinganishwa na Dola za Marekani Milioni 2,696.2 mwaka 2021, ikiwa ni pungufu kwa asilimia 38.94 (Jedwali Na. 1).
  9. Mheshimiwa Spika, Mauzo katika Soko la India yaliongezeka kutoka Dola za Marekani Milioni 528.7 mwaka 2020 hadi Dola za Marekani Milioni 1,008.7 mwaka 2021, sawa na ongezeko la asilimia 90.79. Ongezeko hilo lilitokana na mauzo ya bidhaa mbalimbali zikiwemo Madini, Korosho, Mbaazi na Maharage ya Soya. Aidha, Manunuzi ya Tanzania kutokaIndia yaliongezeka kutoka Dola za Marekani Milioni 1,940.3 mwaka 2020 hadi Dola za Marekani Milioni 2,696.2 mwaka 2021, ikiwa ni ongezeko la asilimia 38.96 (Jedwali Na. 2).
  10. Mheshimiwa Spika, Mauzo katika soko la Japan yaliongezeka kutoka Dola za Marekani Milioni 55.8 mwaka 2020 hadi Dola za Marekani Milioni 67.5 mwaka 2021, sawa na ongezeko la asilimia 20.97. Manunuzi ya bidhaa kutoka Japan yalikuwa na thamani ya Dola za Marekani Milioni 338.4 mwaka 2020 ikilinganiswa na Dola za Marekani Milioni 469 mwaka 2021, sawa na ongezeko la asilimia 38.59. Bidhaa zilizoagizwa kwa wingi ni zile zinazotumika kwenye uzalishaji viwandani kama vile mashine, mitambo na kemikali (Jedwali Na. 3).
  11. Mheshimiwa Spika, Bidhaa zilizonunuliwa na Tanzania kutoka Jumuiya ya Ulaya zilikuwa na thamani ya Dola za Marekani milioni 1,072 mwaka 2020 ikilinganishwa na Dola za Marekani milioni 1,003.7 kwa mwaka 2021, sawa na upungufu wa asilimia 6.37. Bidhaa zilizoagizwa kwa wingi ni pamoja na; vifaa vya mitambo, mashine mbalimbali, vipuri vya magari, magari, nguo, vyombo vya majini (marine vessels), gesi na mafuta, vifaa vya madawa (medical apparatus), paper board, fittings, gas tubes, mineral/chemical fertilizers, data processing machines, vifaa vya mawasiliano na vifaa vya uchunguzi wa kimaabara. Pia, mauzo ya bidhaa za Tanzania kwenda Jumuiya ya Ulaya yalipungua kutoka Dola za Marekani Milioni 1,475. kwa mwaka 2020 hadi kufikia Dola za Marekani Milioni 857.1 mwaka 2021, ambayo ni sawa na upungufu wa asilimia 41.89. Bidhaa zilizouzwa kwa wingi ni bidhaa za tumbaku, madini, kahawa, maharage ya soya, alizeti, pamba na maua (Jedwali Na. 4).
  12. Mheshimiwa Spika, Mauzo ya Tanzania katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 2021 yalikuwa Dola za Marekani Milioni 1,161.2 ikilinganishwa na Dola za Marekani Milioni 807.9 mwaka 2020 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 43.73. Ongezeko hilo limetokana na mauzo ya bidhaa za chai, mahindi, ngano, alizeti, mchele, bidhaa za karatasi, mabati, vigae, vyandarua, kemikali (methyl bromide), saruji na mafuta ya kupaka. Aidha, bidhaa za Tanzania zilizouzwa kwa wingi katika soko hilo ni pamoja na mbogamboga, chai, matunda, magunia, mifuko ya plastiki, wanyama hai, viazi, samaki, udongo asilia, kahawa, mahindi, mchele, unga wa nafaka, karanga, mawese, ufuta, pamba na makaa ya mawe. Kwa upande mwingine, uagizaji wa Tanzania kutoka nchi za Jumuiya hiyo uliongezeka kutoka Dola za Marekani Milioni 324.3 mwaka 2020 ikilinganishwa na Dola za Marekani Milioni 523.4 mwaka 2021, sawa na ongezeko la asilimia 61.39. Kutokana na hali hiyo, urari wa biashara ni chanya kwa Dola za Marekani Milioni 637.8 (Jedwali Na. 5).
  13. Mheshimiwa Spika, Mauzo ya Tanzania kwenda katika soko la nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika, mwaka 2020 yalikuwa Dola za Marekani Milioni 1,458.3 ikilinganishwa na Dola za Marekani Milioni 1,311.5 mwaka 2021, sawa na upungufu wa asilimia 10.06. Uagizaji wa Tanzania kutoka katika soko hilo ulipungua kutoka Dola za Marekani Milioni 492.4 mwaka 2020 hadi Dola za Marekani Milioni 232.5 mwaka 2021, sawa na upungufu wa asilimia 52.78 (Jedwali Na. 6).

2.4 Mwenendo wa Bei za Bidhaa Muhimu Nchini

  1. Mheshimiwa Spika, Mwenendo wa kupanda bei kusikoendana na uhalisia wa soko ni kati ya changamoto zinazokabili sekta yetu ya biashara. Licha ya kuwepo sababu za msingi za kupanda kwa bei kwa baadhi ya bidhaa hasa zinazoagizwa kutoka nje, katika kipindi cha kuanzia mwezi Desemba, 2021, kulikuwa na taarifa za uhaba na upandaji wa bei usioendana na uhalisia wa soko kwenye bidhaa za ujenzi, vyakula, nishati na pembejeo za kilimo. Kwa upande wa vifaa vya ujenzi, wastani wa bei ya Nondo moja ya mm 12 imepanda kutoka Shilingi 20,393 kipindi cha mwezi Machi, 2021 na kufikia Shilingi 26,875 mwezi Machi, 2022 sawa na ongezeko la asilimia 31.8; Nondo moja ya mm 16 imepanda kutoka Shilingi 36,036 na kufikia Shilingi 46,607 sawa na ongezeko la bei la asilimia 29.3; Nondo moja ya mm10 imepanda kutoka Shilingi 15,857 na kufikia Shilingi 19,157 sawa na ongezeko la asilimia 20.8. Vilevile, bei ya Nondo moja ya mm 8 imepanda kutoka Shilingi 12,161 na kufikia Shilingi 15,750 sawa na ongezeko la bei la asilimia 29.5 (Jedwali Na. 7).
  2. Mheshimiwa Spika, Wastani wa bei ya Bati la geji 30 imepanda kufikia Shilingi 27,714 mwezi Machi 2022, kutoka Shilingi 20,786 mwezi Machi, 2021, sawa na ongezeko la asilimia 33.3; Bei ya Bati la geji 32 imepanda kwa asilimia 15.5 na kufikia Shilingi 18,679 kutoka bei ya Shilingi 16,179 mwezi Machi, 2021; na Bati la geji 28 imepanda kufikia wastani wa Shilingi 37,500, sawa na ongezeko la bei la asilimia 36.2 kutoka Shilingi 27,536. Aidha, Wastani wa bei ya rejareja ya Saruji kwa mfuko wa kilo 50 ni Shilingi 18,283, sawa na ongezeko la bei kwa asilimia 3.5 ukilinganisha na wastani wa bei ya Shilingi 17,662 ya mwezi Machi, 2021 (Jedwali Na.
    8-10).
  3. Mheshimiwa Spika, Kwa ujumla wake bei za vifaa vya ujenzi ikiwemo mabati na nondo zimeendelea kuwa juu kutokana na kuongezeka kwa bei za malighafi za vifaa vya ujenzi katika soko la dunia. Tathmini iliyofanyika ilibaini kuwa upandaji wa bei ya saruji unatokana na uhaba unaosababishwa na mahitaji makubwa ya saruji katika miradi ya kitaifa; usambazaji hafifu wa bidhaa hiyo kuwafikia watumiaji wa mwisho na ucheleweshaji wa upatikanaji wa saruji kutoka kiwandani. Wizara imeendelea kukusanya taarifa za bidhaa sokoni ikiwa ni pamoja na bei za mazao makuu ya chakula na mafuta ya kula katika masoko mbalimbali hapa nchini ili kuwafahamisha wananchi na wadau wengine kuhusu mwenendo wa bei za bidhaa mbalimbali.
  4. Mheshimiwa Spika, Mwenendo wa bei ya mafuta ya kula katika soko la dunia imeendelea kupanda kutokana na Janga la UVIKO -19 na athari ya vita ya Urusi na Ukraine ambapo kufikia mwezi Machi, 2022 wastani wa bei ya mafuta ya alizeti kwa tani moja ilikuwa ni Dola za Marekani 1,491.30 na mafuta asili ya mawese ilikuwa Dola za Marekani 1,776.96 kutoka Dola za Marekani 711.71 na 573.02 kwa tani moja mtawalia kipindi cha mwezi Machi, 2019, sawa na ongezeko la asilimia 149.67 (Jedwali Na. 11).
  5. Mheshimiwa Spika, Sambamba na kupanda kwa bei za vifaa vya ujenzi, kumekuwa pia na ongezeko la bei za mazao ya chakula Nchini. Wastani wa bei ya Maharage imepanda kutoka Shilingi 177,340 kwa gunia la kilo 100 kwa mwezi Machi, 2021 hadi Shilingi 188,294 Mwezi Machi, 2022 sawa na ongezeko la asilimia 6.2. Wastani wa bei ya Mahindi kwa gunia la kilo 100 imeongezeka kutoka Shilingi 48,341 Mwezi Machi, 2021 hadi 59,861 Mwezi Machi, 2022 sawa na ongezeko la asilimia 23. Vilevile, wastani wa bei ya Mchele imeongezeka kutoka
    Shilingi 139,212 mwezi Machi, 2021 hadi Shilingi
    185,278 mwezi Machi, 2022 sawa na ongezeko la asilimia
    33.1 (Jedwali Na. 12).
  6. Mheshimiwa Spika, Kwa kuzingatia unyeti wa suala hilo, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliiagiza Wizara yangu kuratibu na kufanya tathmini ya kina ya suala hilo ili kulitafutia ufumbuzi. Kwa kuzingatia tathmini iliyofanywa, hatua zifuatazo zinachukuliwa katika kudhibiti ongezeko la bei za bidhaa muhimu:-

i. Serikali inaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa bei za bidhaa muhimu hususan zile zilizoonekana kuathiriwa na UVIKO-19 sambamba na vita kati ya Ukraine na Urusi. Hivyo, Wizara kwa kushirikiana na wadau wengine inaendelea kutumia mbinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutafuta vyanzo mbadala vya upatikanaji wa bidhaa hizo ili kukidhi mahitaji;

ii. Serikali imeendelea kuwaagiza wazalishaji na wasambazaji wa bidhaa muhimu kushusha mara moja bei za bidhaa walizopandisha pasipo kuendana na uhalisia wa bei ya soko;

iii. Serikali inawaelekeza wazalishaji na wafanyabiashara wa bidhaa muhimu kuuza bidhaa husika kwa kuzingatia gharama halisi za uingizaji, uzalishaji na usambazaji;

iv. Serikali inawaelekeza wazalishaji wa bidhaa muhimu kuzalisha na kusambaza bidhaa husika kulingana na uwezo wa viwanda uliosimikwa ili kukidhi mahitaji ya soko;

v. Serikali inawaelekeza wauzaji na wasambazaji wa mbolea zenye bei elekezi wahakikishe wanazingatia bei zilizopangwa na Serikali na wale wote watakaokiuka watachukuliwa hatua kali za kisheria, ikiwa ni pamoja na kufutiwa leseni za biashara; na

vi. Tume ya Ushindani (FCC) inaelekezwa ifuatilie kwa karibu mwenendo wa biashara wa bidhaa muhimu ambazo katika tathmini iliyofanyika zimeonesha kuathirika zaidi na upandaji wa bei na kuchukua hatua za kisheria kwa watakaobainika kukiuka Sheria ya Ushindani ya Mwaka 2003.

vii. Serikali imeendelea kushawishi na kuvutia Wawekezaji wa ndani na nje kwenye uzalishaji wa mazao ambayo tumekuwa tegemezi kwa kiwango kikubwa kutoka nje ya nchi ikiwa ni pamoja na mafuta ya kula, sukari na ngano. Lengo likiwa ni kupata uzalishaji unaotosheleza mahitaji ya soko letu la ndani na hatimaye kuuza nje kwa sababu hiyo tunayo kama Taifa.

  1. Mheshimiwa Spika, Upandaji bei holela ambao kamwe haukubaliki, ni jinai na Serikali itachukua hatua. Sheria zipo za kusimamia biashara na kitendo cha kupandisha bei kiholela bila sababu za msingi ni kosa la jinai chini ya Kifungu cha 9 (1) cha Sheria ya Ushindani Na. 8 ya 2003 (Fair Competition Act, No.8 of 2003 Kwa mujibu wa Kifungu hicho, makubaliano ambayo malengo au matokeo tarajiwa ni washindani: kupanga bei; kufanya mgomo; kukubaliana katika manunuzi; na kuzuia uzalishaji ni makosa yanayostahili adhabu hiyo. Hivyo, kwa maeneo ambayo wafanyabiashara hawana sababu ya kupandisha bei, tutatumia sheria na kanuni zilizopo kudhibiti mwenendo batili wa bei.
  2. Mheshimiwa Spika, Ninapenda kusisitiza maelekezo ya Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya kote nchini kuwasimamia ipasavyo Maafisa Biashara kwenye maeneo yao ili watekeleze wajibu wao wa kufuatilia mwenendo wa bei za bidhaa muhimu na kuwasilisha taarifa hizo Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kwa wakati.
    3 UBORESHAJI WA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI,
    VIWANDA NA BIASHARA NCHINI

3.1 Sera

  1. Mheshimiwa Spika, ili kuhakikisha kuwa kunakuwa na mazingira wezeshi ya uwekezaji na ufanyaji biashara nchini, Wizara inafanya mapitio ya Sera, Sheria na Kanuni mbalimbali inayozisimamia na zipo kwenye hatua mbalimbali za kukamilishwa. Sera zinazofanyiwa mapitio ni Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996, Sera ya Maendeleo ya Viwanda (1996-2020), Sera ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo (2003), Sera ya Taifa ya Biashara (2003) na Sera ya Masoko ya Mazao ya Kilimo (2003). Sera hizo zinafanyiwa mapitio ili ziendane na mazingira ya sasa ya uwekezaji na biashara ikiwa ni pamoja na kujumuisha vipaumbele vilivyoainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa. Zoezi hilo la kupitia Sera litasaidia kukidhi mahitaji yanayotokana na mabadiliko mbalimbali yakiwemo ya kiuchumi na kiteknolojia.

3.2 Sheria

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara inafanya marekebisho ya sheria mbalimbali ili kuweka mazingira rafiki katika uwekezaji, viwanda na biashara. Kwa sasa, Wizara inaendelea kufanya Marekebisho ya Sheria ya Ushindani ya Mwaka 2003; Sheria ya Uwekezaji ya Mwaka
    1997; Sheria ya Viwango ya Mwaka 2009; Sheria ya Leseni za Biashara Sura 208; na Sheria ya Vipimo Sura na 340 na mapitio yake ya mwaka 2002. Sambamba na hilo, Wizara inaendelea na maandalizi ya Kutunga Sheria ya Ahueni ya Athari za Biashara ya Mwaka 2022 (Trade Remedies Act, 2022). Lengo la Marekebisho hayo ni kufanyia kazi upungufu uliopo katika Sheria hizo ili ziendane na hitaji la Serikali la kuweka mazingira wezeshi ya ufanyaji wa biashara na uwekezaji nchini.
  2. Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2021/2022, Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, imekamilisha marekebisho ya Sheria tatu (3) zinazosimamiwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA). Sheria hizo ni: Sheria ya Makampuni, Sura 212; Sheria ya Majina ya Biashara, Sura 213; na Sheria ya Alama za Biashara na Huduma, Sura 326. Marekebisho yake yamefanyika na kupitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali Na.3 ya Mwaka 2021 iliyochapishwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 5 la tarehe 11 Oktoba, 2021. Lengo la Marekebisho hayo ni kuweka mazingira mazuri na wezeshi ya ufanyaji wa biashara nchini.
  3. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imefanya marekebisho ya Sheria ya Kuratibu Ajira za Wageni Na.1 ya Mwaka 2015 ambapo kwa sasa Sheria hiyo inaruhusu Mwekezaji kuingiza Wataalam hadi 10 kwa masharti nafuu kutoka watano (5) ilivyokuwa kabla ya Mwezi Oktoba, 2021 na kuondoa sharti la kupata ithibati ya vyeti vya elimu kutoka TCU na NACTE kwa wanaoomba vibali vya kazi. Halikadhalika, Serikali imeunganisha Mifumo ya Kielektroniki ya Utoaji wa Vibali vya Kazi kwa Wageni na Wawekezaji (Online Work Permit Application and Issuance System-OWAIS). Mfumo huo umepunguza muda wa kushughulikia maombi ya Vibali vya Kazi kutoka siku za kazi 14 hadi saba (7) na kupunguza hatua za uchakataji wa kibali kutoka hatua 33 hadi saba (7). Pia, Mfumo huo umefungamanishwa (integrated) na Mfumo wa Kielektroniki wa Maombi ya Vibali vya Ukaazi (Online System for Application of Residence Permit – e-Permit).

3.3 Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara
Nchini

  1. Mheshimiwa Spika, Katika jitihada za kuweka mazingira rafiki na wezeshi ya kufanya uwekezaji na biashara nchini. Maboresho ya mazingira ya uwekezaji na biashara yamejikita katika kupunguza gharama, muda na taratibu za kufanya biashara nchini. Utekelezaji wa maboresho hayo yanajumuisha: Kufanya marejeo ya Sheria, Kanuni na Taratibu, Leseni, Tozo na Faini; Kuimarisha utoaji wa huduma za leseni na vibali na malipo kwa njia ya mtandao; Kuondoa baadhi ya tozo, faini na gharama za leseni na vibali; Kuondoa muingiliano wa majukumu kwenye baadhi ya mamlaka za udhibiti; Kuimarisha mifumo ya ukaguzi; na Kuanzisha na kuimarisha Vituo vya Pamoja vya Kutoa Huduma (OSBC). Wizara imeendelea kuratibu utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara Nchini. Wizara imeandaa Mpango Kazi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara ambao unatekelezwa kwa kushirikisha wadau mbalimbali nchini chini ya uratibu wa Wizara yangu. Kutokana na utekelezaji wa Mpango huo, Serikali imewezesha kufutwa kwa tozo kero na faini na kuunganisha majukumu yanayofanana katika mamlaka za udhibiti ili kupunguza gharama za kufanya biashara nchini.
  2. Mheshimiwa Spika; Tayari maboresho hayo yameanza kuonesha matokeo chanya katika kuchochea uwekezaji na biashara katika Sekta Binafsi. Ni dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita kuendelea kuboresha mazingira ya biashara ambayo yatachochea na kuongeza kasi ya uwekezaji nchini.

4 MCHANGO WA SEKTA YA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA NCHINI

  1. Mheshimiwa Spika, Mchango wa Sekta ya Viwanda katika Pato la Taifa kwa mwaka 2021 ulikuwa asilimia 8.0 ikilinganishwa na asilimia 8.4 mwaka 2020, sawa na upungufu wa asilimia 0.4 (Jedwali Na.13). Vilevile, Kasi ya ukuaji wa Sekta ya Viwanda ilikuwa asilimia 5.1 mwaka 2021 ikilinganishwa na asilimia 4.5 mwaka 2020 (Jedwali Na. 14). Ongezeko hilo la ukuaji lilitokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa baadhi ya bidhaa za viwandani kama vile uzalishaji wa biskuti na tambi uliongezeka kwa asilimia 35.5 kila moja, rangi (asilimia 33.9), nguo (asilimia 23.2), chibuku (asilimia 7.2), dawa za pareto (asilimia 6.5), bati (asilimia 6.1), chuma (asilimia 4.9), kamba za katani (asilimia 4.8), nyavu za uvuvi (asilimia 4.6) na saruji (asilimia 0.5) Kwa upande mwingine, Sekta ya Viwanda imetoa ajira 345,615 mwaka 2021 ikilinganishwa na ajira 370,485 mwaka 2020 (Jedwali Na. 15).
  2. Mheshimiwa Spika, Mchango wa Sekta ya Biashara katika Pato la Taifa kwa mwaka 2021 ulikuwa asilimia 8.9 ikilinganishwa na asilimia 8.7 mwaka 2020 sawa na ongezeko la asilimia 0.2. Vilevile, Kasi ya Ukuaji wa Sekta ya Biashara ilikuwa asilimia 4.0 mwaka 2021 ikilinganishwa na asilimia 2.1 mwaka 2020. Ongezeko hilo linatokana na kuongezeka kwa bidhaa zilizouzwa zikiwa ni pamoja na bidhaa za kilimo na bidhaa zilizozalishwa viwandani. Sekta ya Biashara imewezesha uuzaji nje wa bidhaa zenye thamani ya Dola za Marekani 6,755.6 kwa mwaka 2021 ikilinganishwa na Dola za Marekani 6,371.7 kwa mwaka 2020 sawa na ongezeko la asilimia sita (6) Ongezeko hilo limetokana na kuongezeka kwa mauzo ya bidhaa zisizo asilia hususan bidhaa za viwandani, mazao ya mbogamboga na bidhaa nyinginezo zikijumuisha mahindi na mpunga.  
    5 UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI KATIKA
    MWAKA 2021/2022

5.1 Utekelezaji wa Bajeti kwa Mwaka 2021/2022

5.1.1 Bajeti iliyoidhinishwa na Fedha iliyopokelewa
kwa Mwaka 2021/2022

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara ni Wizara mpya ambayo imeundwa kwa Tamko la Serikali Namba 384 la mwaka 2022. Kwa Mwaka wa fedha 2021/2022, Wizara inaendeshwa kwa Bajeti za Fungu 11, 44 na
    60 zilizopitishwa mwaka 2021/2022 chini ya iliyokuwa Ofisi ya Waziri Mkuu – Uwekezaji (Fungu 11); na iliyokuwa Wizara ya Viwanda na Biashara (Fungu 44 na 60). Jumla ya Shilingi 112,688,672,000.00 ziliidhinishwa kutumiwa katika mafungu hayo ambapo Fungu 11 ni Shilingi 7,018,213,000.00; Fungu 44 ni
    Shilingi 81,398,833,000.00; na Fungu 60 ni Shilingi
    24,271,626,000.00.
  2. Mheshimiwa Spika, Hadi kufikia Mwezi Machi, 2022, Wizara ilikuwa haijakusanya maduhuli yoyote ikilinganishwa na lengo la kukusanya Shilingi 15,000,000. Pia, katika kipindi hicho, Wizara imepokea jumla ya Shilingi 55,157,194,610.17 sawa na asilimia 48 ya jumla ya Bajeti iliyotengwa. Kiasi hicho kinajumuisha Shilingi 4,872,606,782.92 kutoka Fungu 11 (sawa na asilimia 69); Shilingi 31,821,858,869.34 kutoka Fungu 44 (sawa na asilimia 39) na Shilingi 18,462,728,957.91 kutoka Fungu 60 (sawa na asilimia
    76) ya Bajeti zilizotengwa.

5.1.2 Fedha za Matumizi ya Kawaida

  1. Mheshimiwa Spika, Katika Mwaka 2021/2022,
    Wizara kupitia Fungu 11 ilitengewa jumla ya Shilingi 7,018,213,000.00 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Kati ya hizo, Shilingi 3,229,915,000.00 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo (OC) na Shilingi 3,818,298,000.00 kwa ajili ya Mishahara. Hadi kufikia mwezi Machi, 2022, Wizara ilikuwa imepokea jumla ya Shilingi 2,310,164,437.38 kwa ajili ya Matumizi Mengineyo (OC) sawa na asilimia 71 ya fedha zilizotengwa na Shilingi 2,562,442,345.54 kwa ajili ya Mishahara sawa na asilimia 67 ya fedha iliyotengwa. Katika Mwaka 2021/2022, Wizara katika Fungu 44 ilitengewa jumla ya Shilingi 28,310,947,000 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida.
  2. Mheshimiwa Spika, Kati ya hizo, Shilingi 5,119,373,000 kwa ajili ya Matumizi Mengineyo (OC) na Shilingi 23,191,574,000 kwa ajili ya Mishahara. Hadi kufikia Mwezi Machi, 2022, Wizara ilipokea jumla ya Shilingi 4,308,198,554.12 kwa ajili ya Matumizi Mengineyo (OC), sawa na asilimia 84 ya fedha zilizotengwa na Shilingi 17,028,147,001.51 kwa ajili ya Mishahara sawa na asilimia 73 ya fedha iliyotengwa. Katika Mwaka 2021/2022, Wizara kupitia Fungu 60 ilitengewa jumla ya Shilingi 24,271,626,000.00 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Kati ya kiasi hicho, Shilingi 1,470,091,000 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo (OC) na Shilingi 22,801,535,000.00 kwa ajili ya Mishahara. Hadi kufikia Mwezi Machi, 2022, Wizara ilikuwa imepokea jumla ya Shilingi 1,189,507,846.46 kwa ajili ya Matumizi Mengineyo (OC) sawa na asilimia 80 ya fedha zilizotengwa na Shilingi 17,273,221,111.45 kwa ajili ya Mishahara sawa na asilimia 76 ya fedha iliyotengwa.

5.1.3 Fedha za Matumizi ya Miradi ya Maendeleo

  1. Mheshimiwa Spika, Katika Mwaka 2021/2022, Wizara kupitia Fungu 44
    ilitengewa Shilingi 53,087,886,000 kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo. Kiasi hicho kinajumuisha Shilingi 52,687,886,000 fedha za ndani na Shilingi 400,000,000 fedha za nje. Hadi kufikia Mwezi Machi, 2022, Wizara ilipokea jumla ya Shilingi 15,870,545,473.13 ya fedha za ndani kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo sawa na asilimia 30 ya fedha zilizotengwa. Wizara haijapokea fedha za nje kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.
    Aidha, Fungu 11 na 60 hazikutengewa fedha kwa ajili ya kutekeleza Miradi ya Maendeleo.

5.2 Utekelezaji wa Mipango

5.2.1 Sekta ya Uwekezaji

A. Kuboresha Mazingira ya Uwekezaji

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na Taasisi ya Trademark East Africa (TMEA) inatengeneza
    Mfumo wa Dirisha Moja la Kutoa Huduma kwa
    Wawekezaji kwa Njia ya Kielektroniki (Tanzania Electronic Investment Single Window – TeIW) ambapo hadi kufikia Mwezi Machi, 2022, ujenzi ulikuwa umefikia asilimia 90. Katika awamu ya kwanza, mfumo unaunganisha mifumo ya taasisi saba (7) ambazo ni Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA); Idara ya Uhamiaji, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu; Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Wakala wa Usajili na Leseni (BRELA); Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA); na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC). Mfumo huo utasaidia kupunguza gharama za ufanyaji biashara pamoja na urasimu ikiwemo kuondoa taratibu za mwekezaji kujaza fomu mbalimbali zenye taarifa zinazojirudia na kuwasilisha viambatisho vinavyofanana kwenye taasisi mbalimbali.
  2. Mheshimiwa Spika, Wizara ilihamasisha wawekezaji nchini kuwasilisha changamoto wanazokabiliana nazo ambapo hadi Mwezi Machi, 2022 jumla ya changamoto 112 zilipokelewa. Changamoto hizo zinahusu kunyang’anywa au kucheleweshwa utoaji wa leseni za udhibiti, kuchelewa kwa umilikishwaji ardhi, kuchelewa kwa marejesho ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), makadirio makubwa ya kodi, kuchelewa kutolewa kwa zabuni za kuzalisha umeme na kutolipwa mauzo ya umeme kwenye mikataba ya mauziano ya umeme (PPA). Nyingine ni kuchelewa kwa vibali vya NEMC, kuchelewa kwa vibali vya ujenzi, taratibu za malipo ya tozo za mazao, kuchelewa kwa vibali vya kazi, migogoro ya mikataba ya kuchimba madini, ukiukwaji wa kilimo cha mkataba na kuchelewa kulipwa deni kwa vifaa vya mabomba vilivyouzwa kwa wakandarasi waliopewa kazi na Halmashauri mbalimbali. Hata hivyo, Wizara imefanikiwa kuratibu utatuzi wa changamoto 75 na changamoto nyingine zinaendelea kufanyiwa kazi katika sekta husika chini ya uratibu wa Wizara yangu.
  3. Mheshimiwa Spika, Wizara imeandaa Kanzidata ya Benki ya Ardhi kwa ajili ya uwekezaji ili kurahisisha upatikanaji wa ardhi ya uwekezaji. Hadi kufikia Mwezi Machi, 2022 Kanzidata hiyo ilikuwa na jumla ya maeneo yenye ukubwa wa hekta milioni 1.6 kwa ajili ya uwekezaji. Wizara inaendelea na jitihada za kutafuta ardhi kwa ajili ya uwekezaji kutoka katika Sekta ya Umma na Binafsi.
  4. Mheshimiwa Spika, Napenda kuchukua nafasi hii kuhamasisha wamiliki wa maeneo yanayofaa kwa uwekezaji wa aina mbalimbali kuwasilisha taarifa hizo kwenye Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) pamoja na Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa Mauzo Nje (EPZA) kwa ajili ya kutangazwa kwa wawekezaji wa ndani na nje wanaohitaji maeneo ya uwekezaji. Wizara kupitia TIC na EPZA zitahakikisha taratibu za makubaliano zinafikiwa kwa mujibu wa Sheria za nchi.

B. Kuratibu Uwekezaji wa Miradi ya Kimkakati yenye

Manufaa Makubwa

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuratibu uwekezaji katika Kongani Maalum za Viwanda katika sekta zenye manufaa makubwa kwa nchi zinazowezesha kupunguza utegemezi wa uagizaji wa bidhaa kutoka nje, kuzalisha ajira kwa wingi na kukuza uchumi. Katika Sekta Ndogo ya Mafuta ya Kula, Wizara inaratibu uwekezaji wa Kongani ya Viwanda vya Mafuta ya Kula yanayotokana na mbegu za Alizeti katika eneo la Kitaraka, Wilaya ya Manyoni, Mkoa wa Singida. Tayari ardhi yenye ukubwa wa ekari 45,000 imepatikana kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi huo. Vilevile, katika Sekta Ndogo ya Sukari, Wizara inaratibu uwekezaji wa Kongani ya Sukari eneo la Dakawa Magole, Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro. Mradi utahusisha wawekezaji wadogo wanaotumia mashine zenye uwezo wa kuchakata tani 200 hadi 500 za miwa kwa siku. Mradi huo utawanufaisha wananchi katika mnyororo wa thamani wa Zao la Miwa na shughuli nyingine zinazoambatana na kilimo na usindikaji wa miwa.
  2. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuratibu uwekezaji wa kongani kubwa zitakazovutia uwekezaji wa viwanda katika eneo moja na hivyo kupunguza gharama za miundombinu na kuimarisha ushindani wa uzalishaji. Katika eneo la Kwala Mkoa wa Pwani, Kampuni ya Sino Tan Kibaha Industrial Park Limited inaendeleza uwekezaji katika kongani lenye ukubwa wa ekari 2,500 ambapo viwanda 400 vinatarajiwa kujengwa na kuwekeza kiasi cha Dola za Marekani Bilioni 3, kuzalisha ajira za moja kwa moja 100,000, ajira zisizo za moja kwa moja 300,000 na kuzalisha bidhaa za takriban Dola za Marekani bilioni 6 kwa mwaka.
  3. Mheshimiwa Spika,Wizara inaratibu uendelezaji wa Mradi wa Eneo Maalum la Kiuchumi la Mkulazi ambalo linajumuisha ujenzi wa Bwawa la Maji la Kidunda. Eneo hilo lenye ukubwa wa hekta 60,103 limepangwa kwa uwekezaji wa kilimo cha mazao mbalimbali ambapo hekta 28,000 kwa ajili ya kilimo cha miwa na hekta 32,103 kwa ajili ya kilimo cha mazao mengine yakiwemo alizeti, mtama na mpunga. Mradi huo utajumuisha Kanda Maalum za Viwanda vya Kuchakata Mazao ya Kilimo ikiwa ni pamoja na yale yatakayozalishwa katika eneo hilo na mikoa ya jirani. Uendelezaji wa eneo hilo, unakwenda sambamba na ujenzi wa Bwawa la Maji la Kidunda kwa ajili ya kuimarisha upatikanaji wa maji, kilimo cha umwagiliaji na matumizi ya Jiji la Dar es Salaam na Mikoa ya Morogoro na Pwani. Aidha, Wizara imesaini Hati ya Makubaliano (MoU) na Kampuni ya Symphomy Investment Ltd iliyoonesha nia ya uendelezaji wa Mradi huo wakati wa Maonesho ya Biashara ya Expo
    2020 Dubai.
  4. Mheshimiwa Spika, Wizara inaratibu uendelezaji wa Mradi wa Bandari na Kanda Maalum ya Kiuchumi Bagamoyo (Bagamoyo Special Economic Zone – BSEZ) unaolenga kuwezesha nchi kuendana na ushindani wa biashara za usafiri wa majini (marine transport services) na muunganisho na shughuli nyingine za kiuchumi ikiwemo viwanda na utalii.
  5. Mheshimiwa Spika, Katika Mwaka 2021/2022, Wizara imefufua majadiliano na wawekezaji wa Kampuni za China Merchants Holdings (International) Co. Ltd (CMHI) na Oman Investment Authority (OIA) ambayo awali ilikuwa inaitwa Mfuko wa Uwekezaji wa Serikali ya Oman (State General Reserve Fund – SGRF). Majadiliano hayo yanahusu eneo dogo la Mradi wa BSEZ kwa kuendeleza eneo la hekta 3,087 kati ya hekta 9,887 ambapo unahusishaujenzi wa Bandari (Sea Port) na Kituo cha Usafirishaji (logistics Park) kwenye eneo la hekta 887 na uendelezaji wa Eneo Maalum la Viwanda (Portside Industrial City) kwenye eneo la hekta 2,200. Msingi wa marejeo ya majadiliano hayo ambayo yalisimama mwaka 2018 ni kuhakikisha kuwa Serikali inatekeleza maeneo ambayo ni wajibu wake kama vile ujenzi wa miundombinu wezeshi (barabara, reli, umeme, maji, gesi na mifumo ya mawasiliano) na lango la kuingilia bandarini (dredging) kwa maslahi mapana ya Taifa. Uwekezaji katika maeneo ya Mradi yatafanywa kwa kuvutia wabia wa Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) au kufanywa na mwekezaji binafsi.

C. Kuhamasisha na Kuvutia Uwekezaji

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara iliratibu maandalizi ya Maonesho ya Wafanyabiashara na Kongamano la Uwekezaji lililofanyika Zanzibar ikiwa ni moja ya shughuli za kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Kongamano hilo lilikuwa na lengo la kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo nchini katika Sekta ya Uchumi wa Buluu, Utalii, Uzalishaji, Usafirishaji, Madini na Sekta ya Huduma za Jamii (afya na elimu). Kupitia Kongamano hilo, Kampuni mbalimbali zilizoonesha nia ya kuwekeza nchini katika viwanda vya dawa, chakula, bidhaa za nyumbani, kilimo, vifaa vya nyumbani, hoteli za kitalii (Resorts), uwekezaji katika majengo (Real Estate) na uzalishaji wa nyaya za umeme
    (Power Cables).
  2. Mheshimiwa Spika, Wizara imeshiriki kwenye makongamano mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Burundi, Kongamano la Wadau wa Sekta ya Alizeti, Kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Uingereza na Makongamano ya Uwekezaji katika Maonesho ya Kibiashara Dubai (Dubai EXPO 2020). Katika Maonesho hayo Mikataba ya Makubaliano (MoU) 37 yenye thamani ya Shilingi trilioni 18.5 ilisainiwa na ipo katika hatua mbalimbai za utekelezaji. Aidha, Wizara kupitia TIC ilishiriki katika makongamano na mikutano ya uwekezaji nje ya nchi ikiwemo Afrika Kusini, Algeria, Misri, Italia, Kenya, Uturuki, Oman, Qatar, Ufaransa na Ubelgiji ambapo ilikutana na wawekezaji mbalimbali. Kati ya wawekezaji hao, wawekezaji sita (6) waliotoka Ubelgiji na wawekezaji 11 waliotoka Ufaransa wameonesha nia ya kuwekeza nchini. Vilevile, Wizara kupitia TIC imeendelea kuwasiliana na wawekezaji hao ili kuwasaidia na kuhakikisha wanawekeza hapa nchini.
  3. Mheshimiwa Spika, Katika jitihada za kuendelea kuvutia wawekezaji nchini, Serikali iliamua kuandaa Filamu Maalum ya Ziara ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika maeneo ya vivutio vya uwekezaji vikiwemo Utalii, Madini, Usafirishaji na Kilimo. Ziara hiyo ambayo inajulikana kama Royal Tour ilizinduliwa rasmi na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huko Marekani katika Jimbo la New York katika Jengo la Makumbusho la Guggerheim tarehe 18 Aprili 2022 na baadaye huko Los Angels, Jimbo la California tarehe 21 Aprili, 2022. Aidha, uzinduzi huo hapa nchini umefanyika Jijini Arusha tarehe 28 Aprili, 2022 na unategemewa pia kufanyika Zanzibar tarehe
    7 Mei, 2022.
  4. Mheshimiwa Spika, Kutokana na ziara iliyofanyika Marekani, Mikataba yenye thamani ya
    Shilingi trilioni 11.7 ilisainiwa na inatarajiwa kutengeneza jumla ya ajira 301,110. Mikataba hiyo inahusisha Sekta za Kilimo na Biashara za Sekta nyingine za uchumi Miradi mingine iliyosainiwa inalenga kuwekeza kwenye mnyororo wa thamani katika Kanda ya Kaskazini ya Sekta ya Utalii wa Tanzania, ikiwemo kwenye maeneo ya kutangaza utalii na kuongeza idadi na ubora wa huduma zinazotolewa.
  5. Mheshimiwa Spika, Wizara imeandaa na kusimamia uhamasishaji wa matumizi ya Mwongozo wa Uwekezaji (Investment Guide) ambao umeainisha miradi mbalimbali katika Sekta ya Madini, Afya, Usafirishaji (Anga na Reli ya Kisasa – SGR), Mafuta na Gesi Asilia,
    Nguo na Mavazi, Uchumi wa Buluu, Utalii, Uvuvi, Kongani za Viwanda pamoja na fursa za uwekezaji katika maeneo mbalimbali nchini. Aidha, Mwongozo huo unapatikana katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, tovuti ya Kituo cha Uwekezaji nchini na Ofisi za Balozi zetu nje ya nchi.
  6. Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha Julai,
    2021 hadi Machi, 2022, miradi 221 ilisajiliwa kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa Mauzo Nje (EPZA). Miradi hiyo inatarajiwa kuwekeza mitaji yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 1,922.2 na kuzalisha ajira 45,369. Pia, miradi 77 sawa na asilimia 34.8 inamilikiwa na wawekezaji kutoka nje, miradi 75 sawa na asilimia
    33.9 ni ya Watanzania na miradi 69 sawa na asilimia 31.2 ni ya ubia. Aidha, kati ya miradi 221, TIC ilisajili miradi 206 yenye thamani ya Dola za Marekani 1,859.4 ambayo inatarajiwa kutoa ajira 37,451. Kati ya hiyo Miradi 72 sawa na asilimia 35 ni ya wawekezaji kutoka nje, miradi 70 sawa na asilimia 34 ni ya Watanzania na miradi 64 sawa na asilimia 31 ni ya ubia. Vilevile, EPZA ilisajili miradi 15 yenye thamani ya Dola za Marekani Milioni 62.8 na inayotarajiwa kutoa ajira 7,918 (Jedwali Na. 16).
  7. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TIC imeendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara kupitia Kituo cha Huduma za Mahala Pamoja (One Stop Facilitation Centre) Kituo hicho kwa sasa kinaweza kuchakata maombi ya vibali na leseni mbalimbali kwa wawekezaji wakiwa TIC. Hadi Mwezi Machi, 2022 jumla ya vibali, vyeti na hati mbadala za ardhi 7,734 zilitolewa kwa wawekezaji mbalimbali kupitia Kituo cha Huduma za Mahala Pamoja. Wizara kupitia TIC imeanzisha Kituo cha Mawasiliano kwa Wawekezaji (Tanzania Investment Call Centre) ambapo katika kipindi cha Julai, 2021 mpaka Machi, 2022, jumla ya wateja 916 walifanya mawasiliano kupitia kituo hicho, ili kupata huduma mbalimbali zikiwemo taarifa kuhusu taratibu na upatikanaji wa vibali, usajili, vyeti, taratibu na fursa mbalimbali za uwekezaji.
  8. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TIC ilitembelea jumla ya miradi 1,672 kati ya miradi 1,500 iliyokuwa imepangwa na kupatiwa huduma (After-Care Services and Project Verification Visit – PVV). pia Wizara iliweza kuwafikia na kuwahudumia wawekezaji 1,402 kwa njia ya simu. Miradi hiyo iliweza kufikiwa na kupita lengo kutokana na zoezi rasmi liliofanyika TIC katika kipindi husika kwa kushirikiana na Maafisa Biashara kutoka katika Halmashauri za Mkoa wa Dar es Salaam.
  9. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TIC kwa kutumia wataalam wa ndani ilifanya utafiti wa kuibua na kuchambua fursa za uwekezaji zinazotokana na Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) katika eneo la Dar es
    Salaam hadi Morogoro. Jumla ya miradi ya uwekezaji
    30 imeibuliwa, kati ya hiyo, miradi tisa (9) imefanyiwa upembuzi yakinifu.

5.2.2 Sekta ya Uwezeshaji Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi

A. Kukuza Maendeleo ya Sekta Binafsi

  1. Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Sita imeonesha nia ya dhati ya kukuza na kuimarisha majadiliano na ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi. Kwa kutambua hilo, Serikali imejenga uwezo wa uendeshaji wa majadiliano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika ngazi ya mikoa na wilaya ambapo mafunzo ya uendeshaji majadiliano yamefanyika katika Mikoa saba (7) ya Dodoma, Iringa, Manyara, Njombe, Rukwa, Ruvuma na Singida. Jumla ya washiriki
    217 walipatiwa mafunzo ambapo kati yao, 129 walitoka Sekta ya Umma na 88 walitoka Sekta Binafsi. Lengo la mafunzo hayo ilikuwa ni kuongeza tija na ufanisi wa majadiliano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi ili kuwa endelevu kwa lengo la kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji. Mafunzo hayo yamewezesha Mikoa ya Rukwa, Singida na Ruvuma ambayo ilikuwa haifanyi Mikutano ya Mabaraza ya Biashara na Sekta Binafsi kuanza kufanya mikutano hiyo.
  2. Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imeratibu ushiriki wa Sekta Binafsikatika ziara za Serikali (Kenya, BurundinaMarekani)naziarazakikazi(Malawi,Msumbiji na Uganda). Katika ziara hizo, Sekta Binafsi ilishiriki majadiliano ya kutatua changamoto zinazoikabili Sekta hiyo katika kufanya biashara katika masoko ya nchi mbalimbali. Aidha, kupitia ushirikishwaji huo, Vikwazo Visivyo vya Kikodi (NTBs) 42 kati ya 64 vilijadiliwa na kupatiwa ufumbuzi na hivyo kuwezesha ustawi wa biashara baina ya Tanzania na Kenya.
  3. Mheshimiwa Spika, Vilevile, Sekta Binafsi ilishiriki katika Maonesho ya Dubai Expo 2020 yaliyofanyika Jijini Dubai. Kutokana na Maonesho hayo, Sekta Binafsi iliweza kutangaza bidhaa zao na kupata fursa za masoko na kuingia mikataba 23 ya ushirikiano baina ya Sekta Binafsi ya Tanzania na kampuni kubwa za nchi za nje.
  4. Mheshimiwa Spika, Matokeo ya ziara hiyo ni kuimarishwa kwa ushirikiano wa taasisi za Sekta Binafsi na Vyama vya Biashara baina ya Tanzania na Malawi na Tanzania na Burundi. Pia, kuongezeka kwa fursa za biashara na uwekezaji katika nchi za Burundi, Dubai, Kenya, Malawi na Uganda kwa wafanyabiashara wa Tanzania. Mfano Kampuni ya Taifa Gas kutoka Tanzania kupata soko la Kenya.
  5. Mheshimiwa Spika, Serikali imefanya tathmini ya matumizi ya Ushoroba wa Dar es Salaam na miundombinu mingine inayotumika na Nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini Mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Lengo la tathmini ilikuwa ni kuangalia kinachosababisha kudorora kwa matumizi ya Ushoroba wa Dar es Salaam na miundombinu mingine ya Tanzania inayotumiwa na nchi za SADC na EAC. Tathmini hiyo inaonesha kuwa, Ushoroba wa Dar es Salaam una ufanisi mdogo kutokana na changamoto mbalimbali zikiwemo za miundombinu na za uendeshaji. Tathmini hiyo imewezesha Serikali kuandaa Mpango na Mkakati wa Pamoja wa Kukuza Biashara na Uwekezaji kwa ajili ya masoko ya nchi jirani.

B. Kukuza Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati na Uwekezaji

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia NEEC imeendelea kuratibu ushiriki wa Watanzania katika miradi ya kimkakati na uwekezaji unaofanyika hapa nchini (Local Content). Katika suala hilo, tunasisitiza maslahi ya Watanzania kwenye maeneo ya ajira, matumizi ya bidhaa za Tanzania, ushiriki wa kampuni za Kitanzania, uhaulishaji wa teknolojia, mafunzo na ushiriki wa jamii kiuchumi. Kwa msingi huo umefanyika ufuatiliaji katika miradi yote ya kimkakati ikiwemo Reli ya Kisasa (SGR), Ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda kwenda Chongoleani Tanga nchini
    Tanzania, uchimbaji wa madini kwenye migodi yote, miradi ya umeme na maji vijijini, ujenzi wa barabara na madaraja na viwanda vyote vyenye uwekezaji wa kutoka nje.
  2. Mheshimiwa Spika, Matokeo ya ufuatiliaji huo unaonesha kuwa, Mwaka 2021, jumla ya ajira 72,395 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja zilizalishwa katika miradi ya kimkakati na uwekezaji nchini. Kati ya ajira hizo, ajira 68,305 sawa na asilimia 94.35 zilitolewa kwa wazawa na ajira 4,090 zilitolewa kwa wageni sawa na asilimia 5.65. Aidha, Miradi ya Kimkakati ilitoa kandarasi ndogo ndogo kwa kuingia mikataba na Kampuni 2,019 za Watanzania kwa huduma za chakula, ulinzi, biashara, bidhaa za ujenzi kama vile saruji, nondo, kokoto, mchanga, kampuni za usafiri, kampuni za bima na kampuni za mafuta.

C. Mifuko na Programu za Uwezeshaji

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia NEEC imeendelea kuimarisha uratibu wa mifuko na programu za uwezeshaji 62 ili iweze kutoa huduma kwa wananchi ikiwemo huduma za mikopo, dhamana na ruzuku. Kati ya mifuko na programu hizo, mifuko na programu
    52 zinamilikiwa na Serikali na mifuko na programu
    10 zinamilikiwa na taasisi binafsi. Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022 jumla ya mikopo yenye thamani ya Shilingi bilioni 903 ilitolewa kwa wanufaika 5,932,668 kutoka katika mikoa 26 wakiwemo wanawake
    3,737,581 na wanaume 2,195,087.
  2. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia NEEC imeendelea na mkakati wa kuanzisha Vituo vya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi katika mikoa yote ya
    Tanzania Bara. Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi,
    2022, Vituo tisa (9) vimeanzishwa katika Mikoa ya
    Dodoma, Geita na Rukwa na hivyo kufikia jumla Vituo
    17 vilivyoanzishwa katika mikoa sita (6) ya Shinyanga (Kahama), Geita, Singida, Rukwa (Sumbawanga), Kigoma (Vituo 6) na Dodoma (Vituo 7). Nia ya Serikali ni kuhakikisha huduma za kuwawezesha wananchi kiuchumi zikiwemo za mikopo, mafunzo, urasimishaji wa biashara, ujuzi wa wafanyabiashara, uongezaji thamani ya mazao, elimu ya kodi na upatikanaji wa masoko, zinapelekwa karibu na walengwa.
  3. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia NEEC inasimamia utekelezaji wa Mwongozo wa Taifa wa Mafunzo ya Ujasiriamali (National Entrepreneurship Training Framework, 2015) ili kuendeleza ujasiriamali hapa nchini. Katika Mwaka 2021/2022, jumla ya Watanzania 78,908 walipatiwa mafunzo ya ujasiriamali kwa kushirikiana na Shule, Vyuo vya Ualimu, Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu, Wizara na Taasisi za Serikali na Binafsi. Aidha, Serikali inatekeleza Mpango wa Maendeleo ya Biashara (Geita Entrepreneurship Development Program – GEDP) katika Mkoa wa Geita, ambapo jumla ya wafanyabiashara 365 kutoka Mkoa wa Geita wamenufaika na mafunzo ya kukuza biashara zao. Utekelezaji wa Mpango huo umeleta matokeo chanya ya uanzishaji wa Kituo cha Uwezeshaji katika Mji wa Geita ambapo taasisi za Mfuko wa SELF MicroFinance, Tanzania Women Chamber of Commerce, Tanzania Bureau of Standards na GSI Tanzania zinatoa huduma kwenye kituo hicho.
  4. Mheshimiwa Spika, Serikali pia imetekeleza Programu ya Vijana 2JIAJIRI (2JIAJIRI Youth Entrepreneurship Training Program) kwa ushirikiano na Benki ya KCB. Programu hiyo inawawezesha vijana wahitimu wa Vyuo Vikuu na Vyuo vya Ufundi kupata mafunzo ya ujasiriamali ili waweze kujiendeleza kwenye biashara zao. Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022 jumla ya vijana 303 wakiwemo wanawake 172 na wanaume 131 wamenufaika na programu hiyo Zanzibar na katika mikoa mitano (5) ya Arusha, Dar es Salaam, Kilimanjaro, Morogoro na Mwanza.
  5. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia NEEC ilihamasisha uanzishwaji wa vikundi vya kijamii vya kiuchumi kama inavyoelekezwa na Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018. Katika kipindi cha Julai, 2021hadiMachi,2022jumlayavikundi13,711vilisajiliwa katika ngazi ya Halmashauri. Wizara imeendelea na jukumu lake la msingi la kuhamasisha vikundi hivyo kuanzishwa na kuendelezwa kwa kuviunganisha na fursa mbalimbali za kiuchumi.
  6. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia NEEC inaratibu Programu ya Majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi katika Mikoa, Wilaya, Kata, Vijiji na Mitaa. Hadi kufikia Mwezi Machi, 2022 kuna jumla ya Majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi 991 yakiwemo majukwaa 23 katika ngazi ya Mkoa, 144 katika ngazi ya Halmashauri za Wilaya, 302 katika ngazi ya Kata, na majukwaa 522 katika ngazi ya Kijiji. Majukwaa hayo yanahusika katika kujadili kwa pamoja changamoto zinazowakwamisha wanawake kushiriki katika shughuli za kiuchumi na kuweka mipango ya utatuzi. Katika kuimarisha Majukwaa hayo, Mwaka 2021, Serikali imefufua Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (Presidential Trust Fund) ili utumike katika kuimarisha majukwaa kwa kuwawezesha wanawake kupata mafunzo ya ujasiriamali na mikopo.
  7. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia NEEC inatekeleza Mpango wa Kuendeleza Viwanda Vidogo na vya Kati (SANVN Viwanda Scheme) ambao ulizinduliwa tarehe 10 Julai, 2020 kwa lengo la kutoa fursa kwa Watanzania kupata mikopo yenye riba nafuu kwa ajili ya kuanzisha na kuendeleza viwanda vidogo na vya kati hususan vinavyochakata mazao ya kilimo na mifugo. Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022 Mpango huo umewezesha kutolewa mikopo yenye jumla ya thamani ya Shilingi 1,746,557,651.29 kwa miradi 32 katika mikoa nane (8). Mikoa hiyo ni pamoja na: Mwanza iliyowezeshwa kupata miradi sita (6) yenye thamani ya Shilingi 296,000,000; Arusha miradi 10 yenye thamani ya Shilingi 465,460,000; Dar es Salaam miradi mitatu (3) yenye thamani ya Shilingi 274,250,000; Kilimanjaro miradi mitatu (3) yenye thamani ya Shilingi 482,847,651.29; Mbeya miradi sita (6) yenye thamani ya Shilingi 108,000,000; Geita miradi miwili (2) yenye thamani ya Shilingi 35,000,000; Dodoma mradi mmoja (1) wenye thamani ya Shilingi 15,000,000; na Shinyanga mradi mmoja (1) wenye thamani ya Shilingi 70,000,000. Kipekee napenda kutoa wito kwa wananchi wenye viwanda vidogo na vya kati na wanaotaka kuanzisha viwanda kutumia fursa ya uwepo wa Mpango huo kupata mitaji yenye masharti nafuu.

5.2.3 Sekta ya Viwanda

A. Kuendeleza Miradi ya Kimkakati

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia NDC imepanga kurudia zoezi la uthamini wa fidia katika mradi wa Mchuchuma na Liganga katika Mwaka 2022/2023 kutokana na uthamini uliofanyika mwaka 2015 kuwa wa muda mrefu kulingana na Sheria ya Uthaminishaji ya Mwaka 2016 Kipengele cha 52:2. Kwa mujibu wa Kipengele hicho, mara baada ya uthamini kufanyika, malipo ya fidia yanapaswa kufanywa ndani ya kipindi cha miezi sita (6), na isipolipwa katika kipindi hicho, riba ya kibishara itatozwa katika kipindi kisichozidi miaka miwili, na baada ya kipindi hicho uthamini huo unakosa uhalali wa kisheria na unapaswa kufanywa upya. Hivyo, katika hali hiyo, ulipaji wa fidia utafanyika baada ya kukamilika kwa tathmini mpya. Aidha, Majadiliano na Mwekezaji anayetarajiwa kutekeleza Mradi wa Chuma cha Maganga Matitu ulio karibu na eneo la Mchuchuma na Liganga yamekamilika. Maandalizi ya Mkataba wa Ubia yako kwenye hatua za mwisho ambapo yakikamilika ulipaji wa fidia utafanyika na utekelezaji wa Mradi utaanza mara moja. Mradi wa Chuma cha Maganga Matitu utakuwa ni awamu ya kwanza ya Mradi wa uzalishaji wa chuma nchini ukifuatiwa na utekelezaji wa Mradi wa Chuma wa Liganga.
  2. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia NDC imefanya utafiti wa Mradi wa Magadi Soda-Engaruka ambapo Upembuzi Yakinifu (Techno-Economic Study) umekamilika kwa asilimia 100. Kazi nyingine zilizokamilika ni pamoja na kufanya tathmini ya Athari za Kimazingira (Environmental Impact Assessment – EIA) iliyochangia upatikanaji wa Cheti chaMazingira na utafiti wa masoko ya Magadi Soda; Uthamini na uhakiki wa ardhi na mali za wananchi watakaopisha Mradi; Maombi ya leseni 29 kwa ajili ya uchimbaji (Mining Licence) yenye gharama ya Dola za Marekani 58,000; na maandalizi ya kutafuta mwekezaji wa kujenga kiwanda yameanza kwa kuandaa na kukamilisha nyaraka muhimu za kutangaza zabuni.
  3. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia NDC, inaendelea na ufuatiliaji wa madeni ya wakopaji wa Matrekta ya URSUS na kuendelea kutoa huduma za kiufundi kwa wateja wa matrekta hayo. Aidha, Timu za Majadiliano za Serikali ya Tanzania na Serikali ya Poland pamoja na Kampuni ya URSUS zinaendelea kufanya majadiliano ili kutafuta ufumbuzi wa changamoto na kupata hatma ya Mradi huo. Changamoto zinazotafutiwa ufumbuzi ni pamoja na changamoto za kiteknolojia, kisheria na kibiashara.
  4. Mheshimiwa Spika, Kutokana na kukua kwa Jiji la Arusha, sehemu ya eneo linalozunguka Kiwanda cha Matairi Arusha kwa sasa linatumika kwa shughuli za maendeleo ya kijamii ambazo zimeashiria haja ya kutafakari upya juu ya matumizi yanayozingatia mazingira ya sasa. Kimsingi, Wizara kupitia NDC inakusudia kubadili matumizi ya eneo hilo kuwa
    Kongani la Viwanda vya Kati (light industries). Hivyo, Upembuzi Yakinifu utafanywa ili kubaini aina ya viwanda vinavyofaa kusimikwa kwenye eneo hilo.
  5. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia NDC imeanza maandalizi ya awali kwa ajili ya kuzalisha mbolea zisizo na kemikali (Bio-fertilizer) kwenye Kiwanda cha Tanzania Bio-tech Product kilichopo Kibaha, Mkoa wa Pwani. Hii ni pamoja na kufanya stadi ya kiufundi ili kujua mahitaji halisi ya mashine zilizopo na gharama za kuzalisha mbolea hiyo. Aidha, Kiwanda cha Tanzania Bio-tech Product kinakamilisha taratibu za kufanya majaribio ya pili ya viuatilifu (Bio pesticides), usajili pamoja na kupata vibali vya uzalishaji wa kibiashara. Majaribio hayo ya pili ni katika kuendana na taratibu za Afrika Mashariki zinazotaka majaribio hayo yafanyake mara mbili. Majaribio ya awali yalifanyika kwenye pamba, mahindi na mbogamboga ambapo viuatilifu hivyo vilionesha ufanisi mkubwa. Uzalishaji wa Viuatilifu utatumia mashine zilizopo kiwandani za kuzalisha viuadudu na kuongeza ufanisi na tija kwenye Kiwanda cha TBPL.
  6. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TIRDO, imeendelea kufanya kazi ya kupima ubora wa makaa ya mawe kutoka kwenye Shirika la STAMICO na kutoka kwa Kampuni mbalimbali zinazochimba makaa ya mawe yakiwemo Magamba Coal, TANCOAL, Amil Coal Company, Kamba‟s Group of Companies, Kiasi Ltd na Edenville International. Upimaji huo ulionesha kuwa makaa ya mawe yanayochimbwa hapa nchini yana ubora wa hali ya juu na yanaweza kutumika katika miradi ya chuma, viwanda vya saruji na kufua umeme. Hii imeondoa uhitaji wa kuagiza makaa ya mawe kutoka nje ya nchi. Matokeo ya utafiti pia yamesaidia kuongeza usafirishaji wa makaa ya mawe kutoka Tanzania na kuuzwa nje ya nchi kama Rwanda na kuongeza kuchangia katika Pato la Taifa.

B. Mwongozo wa Mitaa ya Viwanda na Kanzidata ya Viwanda

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara imeandaa rasimu ya Andiko la Mwongozo wa Mitaa ya Viwanda na Mgawanyo wa Viwanda nchini (Guideline for Industrial Parks Development and Management in Tanzania and Classification of Industries). Andiko hilo litaweka utaratibu maalum wa kuwasaidia wawekezaji katika sekta mbalimbali. Wizara pia imeandaa Kanzidata ya Viwanda ambapo mapitio ya awali yamefanyika. Aidha, Wizara imeandaa miongozo mbalimbali ya Sekta ya Viwanda kama Mwongozo wa Viwanda ikiwemo pamoja na Mgawanyo wa Viwanda. Vilevile, Wizara imeendelea kuhamasisha utengaji na uendelezaji wa maeneo ya uwekezaji viwanda kwenye kila Mkoa na Halmashauri.
    C. Tathmini ya Uzalishaji na Mahitaji ya Bidhaa
    Viwandani
  2. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali za Serikali zikiwemo Wizara ya Fedha na Mipango na Bodi ya Sukari Tanzania ilifanya tathmini ya uzalishaji wa baadhi ya bidhaa za viwandani zikiwemo mafuta ya kula, sukari, vifaa vya ujenzi, vinywaji na taulo za kike. Lengo ni kujua hali halisi ya uzalishaji wa bidhaa hizo ili kufanya maamuzi sahihi yatakayowezesha upatikanaji wake katika soko na kwa bei stahiki. Kwa upande wa mafuta ya kula, tathmini imeonesha kuwa Tanzania ina changamoto ya kujitosheleza kutokana na uhaba wa malighafi kwa ajili ya kuzalisha mafuta hapa nchini. Katika kukabiliana na changamoto hiyo, Serikali inaendelea kuhamasisha uzalishaji wa alizeti na michikichi kwa kutumia teknolojia za kisasa. Aidha, tathmini ya uzalishaji wa dawa za binadamu ilifanyika sambamba na uandaaji wa Mkakati wa Kuendeleza Sekta ya Viwanda vya Dawa, Vifaa na Vifaa Tiba Nchini. Tathmini hiyo ilibainisha kuwa Tanzania inatumia fedha nyingi kuagiza dawa kwa kuwa viwanda vya ndani vinatosheleza kwa asilimia 11 tu ya mahitaji ya nchi. Hivyo, Mkakati huo wa kuendeleza Sekta ya Viwanda vya Dawa, Vifaa na Vifaa Tiba Nchini umeainisha njia na mazingira bora ambayo Serikali na Sekta Binafsi inatakiwa kuchukua ili kuwekeza kwenye sekta hiyo muhimu.

D.Kuhamasisha Uongezaji wa Thamani Mazao ya Kilimo

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara imeshiriki katika maandalizi ya Mradi wa kuanzisha Maeneo Maalum ya Viwanda vya Kusindika Mazao ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi yaani ―Special Agro-Processing Zone (SAPZ). Aidha, tarehe 4 hadi 10 Agosti 2021, Timu ya Wataalam kutoka Wizara za: Kilimo; Uwekezaji,
    Viwanda na Biashara; Mifugo; Uvuvi na Ofisi ya Waziri Mkuu; UNIDO na AfDB ilitembelea maeneo yenye ng’ombe wengi katika Mikoa ya Mwanza – Misungwi na Igunga – Tabora (Ibologero) ambako Vituo vya Uchakataji wa Awali – Agricultural Transformation Centre (ATCs) vitaanzishwa. Lengo lilikuwa ni kujiridhisha na uwepo wa maeneo yaliyopendekezwa kwa ajili ya ATCs pamoja na kukusanya taarifa za awali za maeneo hayo zitakazojumuishwa katika Andiko la Mradi. Ziara kama hiyo ilifanyika tarehe 26 Septemba hadi 4 Oktoba 2021, katika Mikoa ya Geita, Kagera, Mara, Mwanza, Simiyu, Singida, Shinyanga na Tabora ambako Vituo vya Ukusanyaji wa Mazao (Aggregation Centres – ACs) vitaanzishwa.
  2. Mheshimiwa Spika, Hadi kufikia mwezi Machi, 2022 umefanyika uhakiki wa taarifa za maeneo ya utekelezaji wa mradi zilizowasilishwa katika kipindi cha maandalizi ya mradi ikiwemo taarifa ya upembuzi yakinifu, kufanya majadiliano na wadau, kutathmini mahitaji muhimu ya utekelezaji wa mradi na kujadili mfumo wa utekelezaji pamoja na kutoa maoni na mapendekezo kabla ya kuidhinishwa kwa mradi. Vilevile, Wizara imeendelea na utengaji wa maeneo ya kongani yakiwemo Eneo la Kongani ya Korosho -Mtwara, Pamba – Kishapu na Kahama pamoja na Mchikichi – Kigoma.
  3. Mheshimiwa Spika, Kiwanda cha Sukari cha Bagamoyo (Bagamoyo Sugar Limited) kilichopo katika Wilaya ya Bagamoyo, kinamilikiwa na Bakhresa Group of Companies kina eneo kwa ajili ya Kiwanda na mashamba lenye ukubwa wa takriban ekari 10,000. Kiwanda hicho ambacho ujenzi wake umeanza kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 35,000 za sukari kwa mwaka. Aidha, Kiwanda kinatarajia kuanza uzalishaji wa sukari mwezi Julai 2022, ambapo uzalishaji unatarajia kuanza kwa kuzalisha tani 30,000 kwa mwaka na kuajiri wafanyakazi 600 inayojumuisha wafanyakazi 250 wa kudumu na vibarua 350. Aidha, Kiwanda kitakapokamilika msimu wa mwaka 2024/2025 kinatarajia kuzalisha sukari tani
    70,000 kwa mwaka na kutoa jumla ya ajira 1,000.
  4. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia CAMARTEC imebuni na kuunda Mashine za kupura mtama, maharage na alizeti; Mashine za kubangua Korosho; Mtambo wa kuzalisha mvuke wa kuchemshia
    Korosho; Jiko sanifu la kuni la kuchemshia Korosho;
    na Mashine za kukaushia mbogamboga, matunda na mazao mengine. Teknolojia hizo zinalenga kuongeza tija katika shughuli za kilimo nchini. Aidha, teknolojia hizo zinaundwa kwa kuzingatia matokeo ya utafiti wa uhitaji wa zana za kilimo na teknolojia za vijijini uliofanywa na CAMARTEC katika maeneo mbalimbali nchini.
  5. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TEMDO imekamilisha usanifu wa mtambo wa kukausha muhogo na utengenezaji wa Parts za mtambo huo zinaendelea. Ili kukamilisha chasili cha mtambo huo TEMDO imenunua mashine mbili (2) muambato (Grating and hydraulic pressing machines) kutoka Kampuni ya Kitanzania ya Intermech Engineering Company Ltd, sambamba na utengenezaji wa mtambo huo. Utengenezaji wa sehemu ya kuzalisha joto la kukaushia uko katika hatua ya mwisho kukamilishwa. Mtambo huo utakuwa na uwezo wa kukausha tani 12 za muhogo mbichi kwa saa 10 na kutoa tani tatu (3) za unga wa muhogo. Usanifu wa mtambo huo umekamilika kwa asilimia 100 na utengenezaji wa mtambo huo upo asilimia 85, na unategemea kukamilika kwa kwa asilimia 100 ifikapo mwezi Juni, 2022 ili uweze kupelekwa kwenye kikundi cha wakulima Handeni. Vilevile, TEMDO imekamilisha usanifu na michoro ya mtambo wa kukausha korosho.
  6. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TEMDO pia imekamilisha usanifu na michoro ya mtambo mdogo wa kutengeneza sukari kwa ajili ya wajasiriamali wadogo na utengenezaji (fabrications and manufacture) umeanza. Baadhi ya mashine zinazotengenezwa ni cane crusher, sugar cane juice heaters, sugar cane juice clarifier, vacuum pan evaporator, sugar crystallizer, rotary dryer, na mini boiler. Pia, usanifu wa mashine ya kuandaa mbegu za miwa ili zisishambuliwe na magonjwa (Hot water seed treatment plant) umekamilika na utengenezaji wake unaendelea. Mtambo huo mdogo wa sukari utakuwa na uwezo wa kuchakata tani 10 ya miwa (10 TCH), na kutoa tani moja (1) ya sukari kwa saa moja.
  7. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TEMDO limekamilisha pia usanifu wa teknolojia ya kuhifadhi mazao ya matunda na mbogamboga (Cold rooms), na uundaji wa mtambo unaendelea. TEMDO tayari ina makubaliano (MoU) na TAHA kwa ajili ya kuwatengenezea mitambo yenye teknolojia bora ya kuhifadhia mazao ya mbogamboga. Aidha, usanifu wa chasili cha mtambo wa kusindika mafuta ya kula yatokanayo na Zao la Chikichi umekamilika na utengenezaji unaendelea.
  8. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TEMDO imekamilisha utengenezji wa mashine ndogo ya kuchakata mkonge (Raspador) ili kutoa nyuzi zake. Mashine hiyo imefanyiwa majaribio ya awali katika karakana ya taasisi na imeonesha matokeo mazuri ya kutoa nyuzi. Mashine hiyo inategemewa kupelekwa kwa wadau wachakataji wa mkonge ili kuweza kubaini kama kuna maboresho yatakayohitajika kufanyika. Pia, mtambo wa ukubwa wa kati (Korona) umesanifiwa baada ya TEMDO na Bodi ya Mkonge Tanzania kushirikiana na kuonekana uhitaji huo upo na utawawezesha wachakataji wa viwanda vya kati kupata teknolojia hiyo.
  9. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TIRDO imesimamia ufufuaji wa Kiwanda cha Chai Mponde kilichopo chini ya umiliki wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (PSSSF na WCF). Tayari baadhi ya vifaa vinavyohitajika ikiwemo vya umeme na mechanical kwa ajili ya maboresho vimenunuliwa na ufungaji wa vifaa hivyo umefanyika.
  10. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TIRDO imekuwa msimamizi mkuu katika uanzishwaji na usimamizi wa ujenzi wa viwanda nchini kama vile Kiwanda cha Kukoboa Mpunga cha Mkuyuni Mwanza chenye uwezo wa kukoboa tani 96 kwa siku ambacho kinamilikiwa na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB). Hadi Mwezi Machi, 2022 Kiwanda kimekamilika na kimeanza uzalishaji na msimamizi (TIRDO) ipo katika hatua ya kipindi cha uangalizi. Shirika pia linasimamia uanzishwaji wa Kiwanda cha Kutengeneza Viatu cha Kilimanjaro International Leather Industries Company Limited kinachomilikiwa kwa ubia kati ya PSSSF na Jeshi la Magereza. Kiwanda hicho kimekamilika kwa zaidi ya asilimia 90 na uzalishaji wa viatu na bidhaa nyingine za ngozi umeanza.

E. Utekelezaji wa Mikakati ya Pamba, Nguo na Mavazi, Ngozi na Bidhaa za Ngozi na Mafuta ya Alizeti

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imekuwa ikitekeleza Mikakati ya Kuendeleza Sekta ya Nguo na Mavazi; Ngozi na Bidhaa za Ngozi na Mkakati wa Kuendeleza Sekta ya Mafuta ya Alizeti. Mikakati hiyo ambayo imefikia ukomo mwaka 2020 na sasa Wizara inaendelea na mapitio ya Mikakati hiyo.

i. Mkakati wa Ngozi na Bidhaa za Ngozi

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TIRDO inaendelea kusimamia ujenzi wa Kiwanda cha Kutengeneza Viatu vya Ngozi cha Kilimanjaro International Leather Industries Company Limited kinachomilikiwa kwa ubia kati ya PSSSF na Jeshi la Magereza. Sehemu ya kwanza ambayo ni Kiwanda cha Kuzalisha Viatu kimekamilika kwa asilimia 100. Sehemu ya pili ambayo ni ujenzi wa Kiwanda cha Kuchakata Ngozi umekamilika kwa asilimia 90 na Uzalishaji wa
    Viatu na Bidhaa nyingine za ngozi umeanza. Kwa sasa Kiwanda kina uwezo wa kuzalisha jozi 500 za viatu kwa siku.
  2. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TIRDO kwa ushirikiano na REPOA imetoa mafunzo ya kitaalam kwa wadau wa ngozi 407 wa mnyororo wa thamani ikijumuisha wafugaji 270, wachunaji ngozi 75, wafanyabiashara wa ngozi 25 na wasindikaji ngozi 10 na watengeneza bidhaa za ngozi 27. Mafunzo hayo yamefanyika katika Mikoa 11 nchini kwa kuzingatia ile yenye mifugo mingi, machinjio ya kimkakati na viwanda vingi vya ngozi ambayo ni Arusha, Dar es Salaam, Geita, Iringa, Kagera, Kilimanjaro, Manyara, Morogoro, Pwani, Shinyanga na Tabora. Aidha, TIRDO kwa kushirikiana na REPOA imefanya tathmini ya hali ya sasa ya Sekta ya Ngozi ya Tanzania na kuandaa taarifa na andiko la kitaalam ambalo litasaidia kuandaa mkakati na utafutaji ufadhili.
  3. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TIRDO kwa kushirikiana na REPOA imeandaa miongozo minne (4) ya mafunzo kwa kila sehemu ya mnyororo wa thamani wa Zao la Ngozi na kuisambaza kwa wahusika kwa ajili ya mafunzo zaidi na rejea. Pia, policy brief mbili (2) za uboreshaji wa Sekta ya Ngozi zimeandaliwa na zinapatikana kupitia https://www.repoa.or.tz/wp- content/uploads/2021/06/Leather-PB.pdf na pia udhibiti wa matumizi ya madawa ya kusindika ngozi yenye kemikali sumu ipo katika hatua ya ukamilishwaji.

ii. Mkakati wa Mafuta ya Alizeti

  1. Mheshimiwa Spika, Mwezi Septemba, 2021
    Wizara kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, pamoja na Sekta Binafsi ilifanya tathmini ndogo ya Sekta ya Mafuta ya Alizeti katika mikoa ya Dar es Salaam, Manyara, Morogoro na Singida. Tathmini hiyo ilifanywa chini ya Mradi wa TRF unaofadhiliwa na EU kupitia SADC ili kuangalia kipengele cha ushindani katika sekta hiyo. Utafiti huo umebaini kwamba bado kuna changamoto ya uzalishaji mbegu za kutosha za Alizeti kwa ajili ya viwanda. Aidha, Viwanda vingi vidogo na vya kati vina changamoto ya kiteknolojia ya kuchakata mafuta ya kula hadi hatua ya mwisho. Wizara kwa kushirikiana na Sekta Binafsi imeanza taratibu za kuandaa Mkakati mpya wa kukuza tasnia ya alizeti.
  2. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TIRDO pia imekamilisha utafiti wa soko, taarifa za uzalishaji wa Zao la Chikichi na kupata taarifa za awali za teknolojia. Pia, ukamilishaji wa taarifa ya upembuzi yakinifu kwa ajili ya uanzishwaji wa Kiwanda cha Mafuta ya Mawese unaendelea ili kuweza kutoa ushauri wenye tija juu ya uanzishwaji wa Kiwanda hicho katika Mkoa wa Kigoma. Kiwanda hicho kitakuwa soko kwa wakulima wa Zao la Chikichi, kitatoa ajira za moja kwa moja zaidi ya 300 (100 wakiwa ni waajiriwa wa kudumu, 200 wakiwa waajiriwa wa mkataba) na ajira zisizo za moja kwa moja zaidi ya
    50,000.
  3. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TEMDO imekamilisha usanifu na michoro ya mtambo wa kusindika Mafuta ya Kula ya Alizeti na utengenezaji wa mtambo huo unaendelea kufanyika (Fabrication and manufacture). Mitambo ina uwezo wa kukamua, kusafisha na kuweka virutubisho (seed cleaning, pressing, filtration, refining and fortification). Mitambo itakuwa na uwezo wa kusafisha tani moja (1) ya mafuta kwa siku (Lita 1,000) na kutoa ajira 15 za moja kwa moja na ajira zaidi ya 100 zisizo za moja kwa moja.

F. Kueneza Dhana ya KAIZEN Nchini

  1. Mheshimiwa Spika, KAIZEN ni falsafa inayoweka kanuni na taratibu ambazo zinahitaji mwendelezo katika uboreshaji wa mfumo wa uzalishaji unaozingatia ubora wa bidhaa, uwezo wa uzalishaji, mawasiliano, matumizi ya nafasi na kuwa na uwezo wa kuwatunza wateja na wafanyakazi. Wizara kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) inatekeleza Mradi wa KAIZEN ambao hapa nchini ulianza kutekelezwa mwaka 2013. Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022, Mradi wa KAIZEN umefanya uhamasishaji wa dhana ya KAIZEN upande wa Pemba ambapo wanufaika 80 walishiriki na upande wa Unguja ambapo wanufaika 20 walipata mafunzo hayo. Aidha, Wizara imefanya tathmini katika Mikoa sita (6) ambayo inatekeleza KAIZEN. Vilevile, Wizara ilishiriki kwenye Maonesho ya Viwanda Kitaifa yaliyofanyika Zanzibar na Maonesho ya Tamasha la JUAKALI la Afrika Mashariki yaliyofanyika Jijini Mwanza. Kushiriki kwenye maonesho hayo kuliwezesha kutangaza falsafa KAIZEN na kuhamasisha kuhusu umuhimu wa kutumia falsafa na hivyo kufanya watu wengi kuhitaji huduma hiyo.
  2. Mheshimiwa Spika, Wizara ilitoa mafunzo ya KAIZEN kwa nadharia na vitendo katika Mikoa ya Kagera, Mtwara, Pwani na Tanga ambapo takriban viwanda 20 vimenufaika na mafunzo hayo na wakufunzi 36 wamepatiwa mafunzo hayo. Vilevile, Wizara kwa kushirikiana na CTI iliandaa semina ya wadau iliyofanyika Dar es Salaam iliyowalenga wenye viwanda. Washiriki 18 walinufaika ambapo asilimia 50 kati yao walionesha nia ya kutaka kupatiwa mafunzo kwa kina. Vilevile, Wizara ilifanya mafunzo kazini (Intensive on the Job Training – OJT Program for Advanced KAIZEN Trainers) yaliyofanyika Dar es Salaam kwa muda wa wiki nane (8) na kuhusisha wabobezi wa Mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Kagera, Kilimanjaro, Manyara,
    Mbeya na Morogoro. Jumla ya Washiriki 14 wamenufaika na mafunzo hayo ambayo yalivifikia jumla ya viwanda vinne (4).

G. Uendelezaji na Uzalishaji wa Bidhaa kwa ajili ya Mauzo Nje ya Nchi

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia EPZA kwa kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022 imeendelea kuhamasisha uwekezaji katika Maeneo Maalum ya Kiuchumi – SEZ. Kutokana na uhamasishaji huo, Makampuni mapya 15 yamesajiliwa kufikia Mwezi Machi, 2022. Kampuni hizo ni Kriishi Green Limited, Green Bridge Commodities Limited, Diamond Foods Limited, NB Industries Limited, Coastal nuts Tanzania Limited, Tanzania Huafeng Agriculture Development Limited, East Africa zhenyuan Group Company Ltd, Apeck Export Group Limited, Unicarb Minerals Limited, Tanite
    Minerals Limited, Octavian Mshiu Trust Company Limited, Future Agro Pro Limited, Akofa East Africa Limited, Tanso Investment Limited na Polytex Africa Limited. Uwekezaji wa Kampuni hizo kwa ujumla utaleta jumla ya ajira za moja kwa moja 7,918, Mtaji unaokadiriwa kufikia Dola za Marekani milioni 62.8 na mauzo nje yanayokadiriwa kufikia Dola za Marekani milioni 94.85 (Jedwali Na.
    17).
  2. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia EPZA imeendelea kuboresha mifumo ya utoaji huduma kwa kutumia TEHAMA. Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022 EPZA kwa kushirikiana na taasisi ya Trade Mark East Africa (TMEA) imefikia hatua ya Tathmini (Evaluation) ya nyaraka za zabuni ili kumpata mkandarasi atakayetengeneza mfumo unaolenga kuboresha huduma za uwekezaji zinazotolewa na Mamlaka kwa kutumia TEHAMA. Mradi huo unahusisha utengenezaji na utekelezaji wa Mfumo wa kielektroniki wa huduma za pamoja (One Stop Service Centre) ambao utaunganishwa na mifumo mingine ya wadau muhimu katika kuboresha huduma za Uwekezaji. Aidha, Mamlaka kwa kushirikiana na Wakala wa Serikali Mtandao (eGA) imetengeneza tovuti mpya ya Taasisi na tayari imekwishasimikwa kwa ajili ya matumizi.

H. Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TIRDO kwa kushirikiana na Shirika la Madini Tanzania (STAMICO) wanazalisha teknolojia ya utengenezaji wa mkaa mbadala (Briketi) wenye nguvu, usiovunjika, usiotoa majivu mengi na kutokuwa na moshi mwingi ambao ni rafiki kwa mazingira kwa kutumia makaa ya mawe. Aidha, Shirika limefanikiwa kuandaa programu za mafunzo ya namna ya kutengeneza mkaa mbadala ulio katika ubora unaotakiwa kwa matumizi ya majumbani kwa wajasiriamali mbalimbali. Vilevile, TIRDO imenunua mtambo wa kati wa kuzalisha tofali ndogo, wenye uwezo wa kuzalisha tani mbili (2) kwa saa na umesimikwa kwa majaribio katika jengo lililopo TIRDO.
  2. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TIRDO imefanya kaguzi katika viwanda mbalimbali ili kuona uwezekano wa kuvirudisha katika hali ya uzalishaji au kushauri matumizi mbadala yenye tija kwa uchumi wa Taifa. Viwanda hivyo ni Mwanza Tannery Ltd, Buhongwa Industrial Area na Nyanza Glass Work Ltd. Pia, Shirika limefanya ukaguzi wa matumizi bora ya nishati katika viwanda vidogo vilivyopo Mkoa wa Dodoma, Singida na Shinyanga ambavyo ni Kibaigwa Flour Supplies Ltd (Dodoma), Musoma Food Co. Ltd (Shinyanga) na Mwenge Sunflower Oil Mills Company Ltd (Singida). Taarifa ya ukaguzi huo itawasilishwa kwenye taasisi zinazohusika.
  3. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TIRDO imefunga mtambo mdogo wa kupima ubora wa majiko yanayotumika kupikia majumbani, ikiwa ni sambamba na upimaji wa hewa/gesi zilizopo katika nishati mbalimbali (kuni, mkaa, mkaa mbadala) za kupikia majumbani ambapo zaidi ya sampuli 15 zimefanyiwa vipimo katika mtambo huo. Mtambo huo umefungwa katika ofisi za TIRDO Dar es Salaam ambapo watengenezaji mbalimbali wa majiko hayo kama vile TATEDO na watu binafsi wanashauriwa kurekebisha majiko yao endapo hayakidhi ubora unaotakiwa.
  4. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TIRDO imeendelea kutoa huduma za kitaalam viwandani na kwa taasisi mbalimbali. Huduma zilizotolewa ni za upimaji wa kiwango cha uchafuzi wa mazingira kutokana na shughuli za uzalishaji viwandani. Viwanda na taasisi zilizopata huduma hizo ni pamoja na Kilimanjaro Biochem Ltd, Tanzania Cigarette Public Ltd Company, Serengeti Breweries Ltd Dar es Salaam, TANESCO – Nyumba ya Mungu Power Plant na Kiwanda cha Mabati cha ALAF. Katika kulinda mazingira, Shirika limetoa huduma za namna hiyo kwa miradi ya kimkakati kama Mradi wa Reli ya Kisasa (Standard Gauge Railway) katika kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro na Morogoro hadi Makutupora.
  5. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TIRDO kwa kushirikiana na COSTECH imefanya utafiti wa matumizi ya pumba na mapapai katika uchakataji ngozi zikiwa kemikali mbadala na mwongozo umeandaliwa tayari kwa matumizi katika Kongani la Ngozi la Kiwango lililopo SIDO Usangi lenye wanakongani 15. Pia, TIRDO kwa kushirikiana na COSTECH na SIDO imewajengea miundombinu ya kusindika ngozi ya Kongani ya Ngozi ya Kiwango. Miundombinu hiyo itatumiwa na vikundi vingine vitano (5) vya vijana vya usindikaji na kutengeneza bidhaa za ngozi vilivyoanzishwa.
  6. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TIRDO kwa kushirikiana na COSTECH imebuni na kutengeneza chujio maalum la kuchuja tanini kutoka kwenye magome ya miti kwa ajili ya kusindika ngozi ikiwa ni mbadala wa kemikali sumu ya kromiam. Chujio hilo limekabidhiwa kwa Kongani la Kiwango kwa matumizi ya uchujaji dawa kwa ajili ya kusindika ngozi. Aidha, TIRDO imefanikiwa kupata ruzuku ya kukamilisha mtambo wa kuongeza thamani ya taka ngumu za ngozi kwa kutengeneza leather board na kwamba mchakato wa kufunga mtambo unaendelea. Shirika limefanya manunuzi ya vifaa kama vile Photometer itakayowezesha kitengo kuendelea na mchakato wa kuhakiki maabara ya mazingira. Vilevile, maabara imeshiriki katika upimaji wa sampuli za uthibitisho wa njia za upimaji wa BOD, COD, Turbidity na TSS ikiwa ni kigezo kimojawapo katika uhakiki wa maabara. Maabara pia imefanya ukarabati wa baadhi ya vifaa kama vile vya kupimia vumbi.
  7. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TIRDO imeweza kufanya upimaji wa sampuli za chakula na maji katika harakati za kujiandaa na mahitaji ya kupata ithibati (Accreditation) ya maabara hiyo. Maabara ya Chakula imeweza kuhakiki jumla ya sampuli 98 kwa ajili ya bidhaa za viwandani na hotelini kwa ajili ya kukidhi ubora unaohitajika. Wateja wakubwa wa maabara hiyo ni viwanda, hoteli na Taasisi za Serikali na Sekta Binafsi. 122. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TIRDO imefanya mashindano ya kimaabara kwa sampuli za unga lishe, karanga, chai, chumvi na pilipili. Maabara hiyo imeweza kuhakiki sampuli tisa (9) kwa wateja wanne (4). Katika jitihada za kuhakiki maabara hizo (Accreditation), wafanyakazi wapatao 27 wa maabara wamepatiwa mafunzo ya mfumo wa uhakiki wa maabara ISO17025/IEC 2017.
  8. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TIRDO kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imeendeleza Mradi wa Teknolojia ya Kuzalisha Mwani na mazao yake yenye ubora kupitia ufadhili kutoka TEA. Aidha Mradi huo unaendelea kutekelezwa katika Wilaya ya Kaskazini Pemba, Zanzibar ambapo TIRDO imefunga mtambo wenye teknolojia ya kukausha Mwani kwa kutumia nishati ya jua na biomass katika kijiji cha Makangalae. Kupitia Mradi huo wajasiriamali wamenunuliwa mashine ya kusagia Mwani baada ya kuukausha. Pia, TIRDO imetoa elimu ya uzalishaji na usindikaji wa Mwani kwa wajasiriamali 300 katika Kisiwa cha Pemba. Lengo ni kuwafundisha wajasiriamali 400, ambapo wajasiriamali
    100 watatoka Kisiwani Unguja.
  9. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia CAMARTEC imebuni na kuanza kutengeneza tela la kupakia mashine ambayo ilinunuliwa kwa lengo la kurahisisha kazi ya kuvuna Chikichi kwa kumpandisha mvunaji juu na kumshusha akiwa na matunda yaliyovunwa. Pia, Kituo kimehuisha mashine iliyoingizwa kutoka nje ya nchi mahsusi kwa ajili ya kutenganisha ―makademia nuts‖ na maganda yake ili kuihuisha ifae kutenganisha viini vya chikichi na maganda yake baada ya kubanguliwa. Mashine imefanyiwa majaribio ya awali (on-station testing) CAMARTEC, kisha kupelekwa mkoani Kigoma ambako imefanyiwa majaribio ya kina ya utendaji wake (performance testing). Pia, CAMARTEC imebuni na kuunda kipandio cha kupanda mbegu za mafuta (ufuta, alizeti, pamba na karanga) ili kuchangia kuongeza uzalishaji wa mazao yenye kutoa mafuta ya kula nchini.
  10. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia CAMARTEC inaendelea na matengenezo ya teknolojia za kulima, kupanda na kuchakata mazao mbalimbali. Teknolojia hizo ni trekta dogo aina ya ―CAMARTECFastTrucktor – CFT‖, vipandio vya mbegu; mashine za kubangua Korosho; jiko sanifu la kuni la kuchemshia Korosho; mashine za kupura mazao; na mashine za kuchakata na kufunga malisho ya mifugo.
  11. Mheshimiwa Spika, Ili kusogeza huduma kwa wadau na kuongeza matumizi ya teknolojia katika uzalishaji vijijini, Wizara kupitia CAMARTEC inaanzisha Kitovu cha Teknolojia za Kihandisi (Engineering Technology Hub-ETH) katika Kijiji cha Mwandete kilichoko Wilaya ya Maswa katika Mkoa wa Simiyu. Teknolojia zinazohitajika kwa matumizi ya ―Hub‖ hiyo zinaendelea kuandaliwa.
  12. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia CAMARTEC ilitoa mafunzo kwa wajasiriamali na kuwawezesha kutengeneza teknolojia zilizothibitishwa na zinazohitajika na wadau. Wajasiramali waliofundishwa na kuwezeshwa ni pamoja na Sumary Engineering Works – Kutengeneza mashine za kukatakata malisho ya mifugo (Forage chopper) na mashine ya kufunga majani kwa ajili ya mifugo (Baler); na Jowog Enterprise – Kutengeneza mashine ya kupura mtama na uwele inayokokotwa na Wanyamakazi. CAMARTEC pia iliwatembelea wadau wa korosho katika Wilaya ya Manyoni katika Mkoa wa Singida ili kuona uwezekano wa kusambaza mashine za kubangua korosho baada ya kutoa mafunzo, ambapo ilibainika kuwa uhitaji wa mashine hizo ni mkubwa sana. Vilevile, Kituo kilitembelea vikundi vya wadau wanaofuga ng’ombe wa maziwa na kuyasindika katika Wilaya ya Hai katika Mkoa wa Kilimanjaro kwa lengo la kuhawilisha teknolojia za kukatakata na kufunga malisho ya mifugo ili kupunguza upotevu wa majani na hatimaye kuongeza uzalishaji wa maziwa.
  13. Mheshimiwa Spika, Kwa mujibu wa Bodi ya Dawa (MSD) asilimia 90 ya vifaa tiba vinaingizwa na Serikali kutoka nje ya nchi (MSD, 2022). Ili kuweza kutoa suluhisho la changamoto hiyo, TEMDO imekamilisha ujenzi wa eneo maalum la karakana litakalokidhi ubora wa viwango vya kutengeneza na kuhifadhi vifaa tiba. Ununuzi wa mashine mbalimbali za aina tano (5) kwa ajili ya mradi upo kwenye hatua za mwisho. TEMDO imetengeneza vifaa vya Hospitali ambavyo ni vitanda vya kujifungulia (delivery beds), vitanda vya kawaida (normal hospital beds), drip stand, vitanda vya uchunguzi (examination tables) na kabati ndogo za wodini zenye gurudumu na zisizo na gurudumu. Vifaa hivyo vimekaguliwa na vimepitishwa na Mamlaka husika ya TMDA na MSD na TEMDO imepewa Ithibati inayoruhusu kuendelea kutengeneza vifaa tiba na kuvisambaza kwenye Hospitali mbalimbali hapa nchini. TEMDO tayari imepokea maombi ya kutengeneza vifaa tiba 150 vinavyojumuisha vitanda vya kawaida, vitanda vya kujifungulia na vitanda vya uchunguzi. TEMDO ina lengo la kujiimarisha zaidi kwenye uzalishaji wa aina mbalimbali za vifaa tiba vinavyohitajika nchini ili kuisaidia Serikali kupunguza gharama na matumizi ya fedha za kigeni. TEMDO inaendelea na usanifu wa vifaa vingine vya hospitali ambavyo ni gynecologic examination bed, cardiac table, office table for food serving, vitanda machela (stretchers), skirini za kukunja (folding screen) na majokofu ya kuhifadhia miili (mortuary cabinets) ya ngazi 3, 6 na 12. Aidha, kutokana na mahitaji ya soko la teknolojia ya vichomea taka (incinerators), TEMDO inaendelea na usanifu wa kutengeneza mtambo (incinarators) wenye uwezo wa kuteketeza dawa za hospitali zilizoharibika (one tonne per batch), nyama za mifugo zisizofaa kwa matumizi ya binadamu na uteketezaji wa damu isiyo salama.

5.2.4 Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo

A. Ujenzi wa Miundombinu ya Mitaa ya Viwanda ya SIDO

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia SIDO katika mwaka 2021/2022 ilipanga kujenga majengo ya viwanda (Industrial sheds) kwa ajili ya viwanda kwenye mnyororo wa thamani wa mazao ya pamba, korosho na mbegu za mafuta ya kula katika Mikoa ya Shinyanga (Kahama), Mtwara, Singida (Manyoni) na Tanga (Lushoto). Hadi Mwezi Machi, 2022 upembuzi yakinifu umefanyika, michoro ya kihandisi (architectural drawings) imeandaliwa na gharama zimeainishwa. Aidha, ujenzi wa majengo matano (5) yanayojumuisha Mikoa ya Mwanza (1), Katavi (2) na Morogoro (2) pamoja na ujenzi wa miundombinu ya mitaa ya viwanda katika Mikoa ya Kagera (uzio na mtaro), Kigoma (barabara na mitaro) na Chato – Geita (uzio, barabara na mitaro) umekamilika.
    B. Uzalishaji Teknolojia kwa Matumizi ya Viwanda Vidogo na vya Kati
  2. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia SIDO inaendelea kuboresha Vituo vya Kuendeleza Teknolojia (TDC), ambapo katika kipindi cha Mwaka 2021/2022, Vituo viwili (2) vilivyopo katika Mikoa ya Kilimanjaro na Mbeya vinaendelea kufanyiwa maboresho. Kwa sasa gharama za mahitaji ya mashine na vipimo (specifications) zimeainishwa, taratibu za manunuzi zimefanyika na mzabuni amepatikana. Aidha, pamoja na maboresho yanayoendelea, Vituo saba (7) vya SIDO vya kuendeleza teknolojia (TDCs) vilivyopo katika Mikoa ya Arusha, Iringa, Kilimanjaro, Kigoma, Mbeya, Lindi na Shinyanga kwa mwaka 2021/2022, vimeweza kuzalisha mashine 313 na vipuri 1,014 ambavyo viliuzwa kwa wajasiriamali. Vituo hivyo pia vinajihusisha na uendelezaji wa teknolojia na kutoa huduma za kiufundi kwa viwanda vidogo na vya kati mjini na vijijini katika mikoa husika kwa kuzingatia Mkakati wa Wilaya Moja Bidhaa Moja (ODOP) na fursa za kimasoko zinazojitokeza.
  3. Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022 Wizara kupitia SIDO imeweza kutoa mafunzo na ushauri mbalimbali kwa wajasiriamali wahitaji 26,800 katika maeneo ya uendelezaji wa biashara na shughuli za uzalishaji viwandani ambapo wajasiriamali 15,176 walipata mafunzo na wajasiriamali 11,624 walipata huduma ya ushauri. Aidha, mafunzo na huduma za ushauri wa kibiashara na ufundi kwa wajasiriamali hutolewa katika nyanja za ufundi, uchumi, uongozi, masoko, ubora wa bidhaa, teknolojia, ubunifu, usanifu na uandaaji wa chambuzi yakinifu za miradi ya viwanda na biashara na kwa vikundi/vyama vya wajasiriamali kwa lengo la kuviimarisha na kuviwezesha kujenga msingi wa kujitegemea katika Sekta ya Viwanda na Biashara Ndogo na za Kati.

C. Kuongeza Fursa za Upatikanaji wa Masoko kwa
Wajasirimali

  1. Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka 2021/2022, Wizara kupitia SIDO iliandaa Maonesho ya SIDO Kitaifa Wilayani Kasulu, Mkoani Kigoma na kushiriki Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF). Jumla ya Wajasiriamali 935 na Taasisi 38 zilishiriki katika Maonesho ya SIDO Kitaifa yaliyofanyika Mkoani Kigoma. Aidha, Mauzo yenye thamani ya Shilingi milioni 796.9 yakiwemo ya fedha taslimu na miadi yalifanyika katika maonesho hayo.
  2. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia SIDO imeendelea kuhamasisha utumiaji wa bidhaa za wajasiriamali kupitia mitandao ya kijamii, radio, luninga, machapisho na mitandao ya kidijitali ya SIDO Apps na web portal. Aidha, matukio 128 na bidhaa

109 yalirushwa na kuwafikia watu 11,700. Pia, Shirika liliweza kusambaza majarida 1,500 kwa wadau na kupitia vituo vilivyopo ofisi za Mikoa. Vilevile, imeweza kutangaza bidhaa za wajasiriamali na kurusha makala kupitia TBC1 kwa muda wa miezi miwili (2) mfululizo kwenye kipindi cha ―SIDO Fahari Yetu‖.

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia SIDO ilipanga kuunganisha Ofisi za Mikoa za Shirika katika Mkongo wa Taifa pamoja na mtandao wa makao makuu ya Shirika, kukamilisha kazi ya kusimika mfumo wa huduma za Masijara na kusanifu pamoja na kuunda mitandao ya ndani ya ofisi za Shirika hilo. Hadi kufikia Mwezi Machi, 2022 Mikoa 13 ilikuwa tayari imeunganishwa katika Mkongo wa Taifa. Kukamilika kwa kazi hiyo kunafanya jumla ya ofisi za Mikoa za SIDO zilizounganishwa kwenye Mkongo wa Taifa kufikia 21. Pia, Mikoa 13 tayari imeunganishwa kwenye Mtandao wa Shirika, na kufanya jumla ya Mikoa iliyounganishwa kwenye mtandao wa Shirika kufikia 21.
  2. Mheshimiwa Spika, Katika kutatua changamoto ya vifungashio kwa wajasiriamali, Wizara kupitia SIDO imeendelea kununua vifungashio kwa wingi kupitia kituo chake kilichopo katika Mtaa wa Viwanda wa Vingunguti, Jijini Dar es Salaam na kuvisambaza kwa wajasiriamali waliopo mikoani kupitia Ofisi za SIDO mikoani. Katika kipindi cha Mwaka 2021/2022, watengenezaji na wasambazaji wa vifungashio 20 walitambuliwa na kuunganishwa na wajasiriamali kupitia ofisi za SIDO Mikoani.
    1. Mheshimiwa Spika, K w a
      upande wa Mikopo kwa wajasiriamali, katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022, Wizara kupitia Shirika la SIDO ilikuwa imepokea maombi ya mikopo 3,832 yenye thamani ya Shilingi bilioni 8.327, ambapo jumla ya mikopo 2,166 yenye thamani Shilingi bilioni 4.651 ilitolewa. Kati ya mikopo hiyo asilimia 47 ilitolewa kwa wanawake na kutengeneza ajira 5,321 kati ya ajira hizo 2,714 zilienda kwa wanawake. Aidha, Wizara kupitia SIDO imekuwa ikiwaunganisha wajasiriamali na taasisi za fedha kupata mitaji mikubwa kwa ajili ya shughuli zao za kiuchumi. Vilevile, kupitia Mfuko wa Dhamana kwa Wajasiriamali (SIDO SME – CGS), mikopo yenye jumla ya thamani ya Shilingi milioni 110 ilitolewa katika Mikoa ya Singida na Kigoma (Jedwali Na. 18).

5.2.5 Sekta ya Mtangamano wa Biashara

A. Majadiliano ya Biashara Kati ya Nchi na Nchi

  1. Mheshimiwa Spika, Katika kukuza na kuimarisha biashara na uwekezaji baina ya Tanzania na Kenya, Wizara iliandaa na kushiriki kwenye Mkutano wa
    Saba (7) wa Kamati ya Pamoja ya Biashara (Joint Trade Committee – JTC) kati ya Tanzania na Kenya uliofanyika tarehe 9 – 12 Machi, 2022 Zanzibar ulijadili masuala mbalimbali ya Sekta za Biashara, Kilimo, Forodha, Uhamiaji na Usafirishaji. Jumla ya vikwazo 30 vilijadiliwa ambapo kati ya hivyo vikwazo 10 vilipatiwa ufumbuzi na kuondolewa, vikwazo vitano (5) vilifutwa kwa sababu ya kukosa taarifa za kutosha kuweza kujadiliwa, vikwazo 14 viliwekewa ukomo wa kuvitatua hadi tarehe 30 Juni, 2022 na Kikwazo kimoja kiliibuliwa. Vilevile, Vikwazo sita (6) vilivyowasilishwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vilisuluhishwa na kuondolewa katika orodha. Vikwazo hivyo ni: Ucheleweshaji wakati wa kupitisha mizigo mpakani kwa sababu ya taratibu za kiforodha; Ucheleweshaji wa utoaji wa vibali vya kuagiza bidhaa za maziwa nje ya nchi; Ugumu wa taratibu za Mamlaka ya Mapato Kenya; Ugumu unaoipata Kampuni ya Taifa Gas katika kuwekeza nchini Kenya; Changamoto za kupata vibali vya kufanyakazi kwa wataalam wa Tanzania; na kuhitajika kwa cheti cha UVIKO -19 kwa raia wa Tanzania wanaosafiri kwenda Kenya.
  2. Mheshimiwa Spika, Kwa upande wa Jamhuri ya Kenya masuala manne (4) yaliyowasilishwa na kupatiwa ufumbuzi ni: kuondolewa kwa ucheleweshaji wa vibali vya huduma za ndege kwenye Mamlaka za Anga za Tanzania; kuzuiwa kwa kampuni ya ndege ya Jambojet ya Kenya kuendesha huduma za ndege za abiria Tanzania; Kuzuiwa kwa wahandisi wa Kenya kuingia Tanzania; na kuwepo kwa tozo ya Shilingi 5,000 kwa magari ya watalii yanayosafirisha watalii kutoka Kenya kuingia Tanzania katika mpaka wa Namanga.
  3. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TANTRADE kwa kushirikiana na TPSF Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Ubalozi wa Uingereza nchini, iliratibu maandalizi ya Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Uingereza (Tanzania – UK Business and Investment Forum). Kaulimbiu ya Kongamano hilo ilikuwa ni ―Kuimarisha Ustawi Endelevu wa Kiuchumi wa Pamoja‖. Kutokana na Kongamano hilo ushirikiano wa biashara kati ya Tanzania na Uingereza umeimarishwa ambapo pande zote mbili (2) zilisaini makubaliano ya kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji.

B. Majadiliano ya Kikanda

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara ilishiriki Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika tarehe 17 – 18 Agosti, 2021 chini ya Kaulimbiu inayosema: ―Bolstering Productive Capacities in the Face of COVID – 19 Pandemic for Inclusive, Sustainable Economic and Industrial Transformation”. Mkutano huo pamoja na mambo mengine ulipokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa mkakati wa viwanda wa SADC kwa mwaka 2020/21 ambapo ilitolewa taarifa kuwa kati ya Nchi Wanachama 16, ni nchi tatu (3) ambazo zimeridhia Itifaki ya Viwanda. Tanzania ikiwa ni nchi mojawapo ambayo haijaridhia, inaendelea na taratibu za kuridhiwa Itifaki hiyo. Aidha, Nchi Wanachama ambazo bado hazijasaini Itifaki hiyo zilihimizwa kufanya hivyo. Kupitia Mkutano huo, Tanzania imenufaika kwa kuidhinishiwa ombi lake la kuwa Mwenyeji wa Kituo cha Kudhibiti Ugaidi katika Kanda, Aidha, Kituo husika tayari kimeshazinduliwa ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji wa Kituo hicho kwa muda wa miaka mitatu; na kuidhinishwa kwa Dola za Marekani 73,518.20 kwa ajili ya kuanza kutafsiri nyaraka za msingi za Jumuiya katika Lugha ya Kiswahili. Hatua hiyo ni muhimu na inatoa fursa kwa Tanzania kuendelea kukuza na kuimarisha Lugha ya Kiswahili.
  2. Mheshimiwa Spika, Wizara ilishiriki Mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Biashara, na Kikosi Kazi cha Mawaziri wanaohusika na Mtangamano wa Kiuchumi wa Kikanda, uliofanyika tarehe 26 – 30 Julai, 2021 kwa njia ya Mtandao. Mkutano ulikuwa chini ya Uenyekiti wa Serikali ya Jamhuri ya Msumbiji na kuongozwa na Mwenyekiti Mheshimiwa Carlos Alberto Fortes Mesquita, Waziri wa Viwanda na Biashara kutoka nchini humo. Pamoja na masuala mengine muhimu, Tanzania ilifanikiwa katika maeneo yafuatayo: Kuongezewa muda wa kuendelea kutoza Ushuru wa Forodha katika bidhaa ya Sukari kutoka nchi za SADC kwa kipindi kingine cha miaka mitatu (3) kuanzia Septemba, 2020 hadi Septemba, 2023. Katika Mkutano huo, Tanzania iliahidi kuendelea kutimiza masharti yanayoendana na utekelezaji wa Upendeleo Maalum wa Kiushuru (Tariff Dispensation) na iliomba kuruhusiwa kutoa taarifa pale ambapo patakuwa na changamoto ya utekelezaji wake.
  3. Mheshimiwa Spika, Wizara ilishiriki katika Kikao Kazi cha waratibu wa masuala ya Jumuiya ya Nchi zilizopo kwenye Mwambao wa Bahari ya Hindi (Indian Ocean Ream Association-IORA) tarehe 13 – 16 Septemba 2021, Zanzibar. Lengo kuu la kikao hicho lilikuwa ni kujipanga na kuimarisha ushiriki wa Tanzania katika majadiliano mbalimbali katika Jumuiya ya IORA. Hivyo, katika kikao hicho ilisisitizwa kuwa ni wakati muafaka sasa wa Tanzania kuona umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika Jumuiya ili kuchangamkia fursa mbalimbali zitokanazo na Uchumi wa Buluu na pia kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika jumuiya hiyo.
  4. Mheshimiwa Spika, Kikao kazi kilipanga vikundi kazi nane (8) vya ndani kulingana na uendeshaji wa Jumuiya.Vikundi kazi hivyo ni:- Masuala ya Ulinzi na Usalama wa Bahari; Masuala ya Sayansi; Teknolojia na Ubunifu; Biashara na Uwekezaji; Masuala ya Utalii na Utamaduni; Masuala ya Kupambana na Maafa, Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi; Masuala ya Uvuvi; na Uchumi wa Bluu. Aidha, Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara ni Mratibu na Kiongozi wa kikundi kazi cha Biashara na Uwekezaji na mratibu msaidizi ni Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda – Zanzibar. Vilevile, vikundi kazi vyote vya kitaifa vilivyoundwa viliombwa kufanya kazi sambamba na vikundi kazi vya IORA ili kuboresha ushiriki wa Tanzania katika Jumuiya hiyo.
  5. Mheshimiwa Spika, Wizara iliandaa kikao cha wataalam wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wa Biashara ya Huduma kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya Biashara ya Huduma ya Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA) kuanzia tarehe 13 – 17Desemba, 2021 mjini Moshi, Kilimanjaro. Mkutano huo ulipitia masuala mbalimbali yanayoendelea katika majadiliano ya Biashara ya Huduma ya Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA). Masuala yaliyojadiliwa ni pamoja na GATS PLUS na GATS Minus in respect to Trade in services Offers, Kanuni ya Reciprocity dhidi ya kanuni ya Most Favored Nation, uthibitishaji wa offer za biashara ya Huduma, njia ya kuthibitisha offer (Comments on the Verification methodology), na kupitia offer ya Jumuiya ya Afrika Mashariki dhidi ya maombi mbalimbali. Masuala hayo yaliyojadiliwa katika hatua hizo za majadiliano ya utekelezaji wa Mkataba wa Uanzishwaji kwa Eneo Huru la Biashara ni muhimu kwa kuwa yanatoa picha namna nchi itavyonufaika na AfCFTA.
  6. Mheshimiwa Spika, Wizara ilishiriki katika Kikao cha Kamati ya Biashara ya Huduma ya Eneo
    Huru la Biashara la Afrika kilichofanyika mjini Accra- Ghana kuanzia tarehe 01 – 05 Novemba 2021. Masuala yaliyojitokeza na kujadiliwa ni pamoja na kupitia mwongozo wa kupitisha offer za nchi wanachama, kuangalia namna ya kuanza kwa Biashara ya Huduma kwa nchi wanachama na taarifa za offer zilizofanyiwa maboresho na nchi wanachama. Vilevile, Wizara inashiriki katika maandalizi ya Itifaki ya Uwekezaji ya Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA Investment Protocol) na rasimu ya itifaki hiyo imeendelea kujadiliwa katika ngazi ya Wataalam wa Nchi Wanachama kwa lengo la kuhakikisha Nchi Wanachama wanavutia na kukuza uwekezaji wenye tija na endelevu.
  7. Mheshimiwa Spika, Wizara ilishiriki Mkutano wa kupitia Kanuni na Sheria ya Soko la Pamoja la Biashara ya Huduma ya Afrika Mashariki uliofanyika tarehe 23 – 25 Oktoba, 2021 Jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine, kikao kilijadili kwa kina kuhusu uhuru wa watu kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine kwa mujibu wa Itifaki ya Soko la Pamoja la Jumuiya na kuona kuwa kuna umuhimu wa kuboresha eneo hilo kwa kuwa litarahisisha utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja.
    C. Majadiliano ya Kimataifa
  8. Mheshimiwa Spika, Wizara ilishiriki kikamilifu katika Mkutano wa Mawaziri wa G33 ndani ya WTO tarehe 16 Septemba, 2021 kwa njia ya mtandao. Kundi hilo linajumuisha nchi zenye maslahi yanayofanana katika eneo la Kilimo. Lengo la Mkutano huo lilikuwa ni kujadili namna ya kuboresha Sekta ya Kilimo kwa kuzingatia madhara ya mlipuko wa UVIKO-19 duniani pamoja na kuwa na azimio la pamoja katika suala hilo katika Mkutano wa 12 wa Mawaziri wa WTO. Baadhi ya masuala ya msingi yaliyotetewa na Tanzania na baadaye kupitishwa katika azimio la pamoja ni: Nchi kuendelea kupata ridhaa ya kuwa na mpango wa kuhifadhi chakula kwa ajili ya usalama wa watu wake (food stockpiling program); na ruzuku kwa Sekta ya Kilimo ili kuendelea kuhamasisha uzalishaji.
  9. Mheshimiwa Spika, Wizara ilishiriki katika Mkutano wa 15 wa Mawaziri uliozikutanisha nchi wanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo (UNCTAD) uliofanyika tarehe 3 hadi 7 Oktoba, 2021 kwa njia ya mtandao. Mkutano huo pamoja na mambo mengine ulifanya maamuzi muhimu yatakayoongoza uendeshaji wa Shirika hilo kwa kipindi cha miaka minne ijayo kuanzia mwaka 2022 ambapo kwa kushirikiana na mashirika mengine litaweza kuzisaidia nchi zinazoendelea kurejea katika hali zao za kawaida kiuchumi kufuatia janga la UVIKO-19. Katika Mkutano huo, Tanzania ilizitaka Jumuiya za Kimataifa kuruhusu uzalishaji wa dawa pamoja na chanjo dhidi ya UVIKO-19 kwa nchi zinazoendelea katika masharti nafuu. Aidha, Tanzania ilipendekeza Shirika la UNCTAD kwa kushirikiana na mashirika mengine kuendelea kutoa misaada ya kiufundi na kifedha katika Sekta ya Uzalishaji hususan kilimo ambayo imeathirika zaidi kutokana na UVIKO-19. Masuala hayo pamoja na mengine yalipitishwa katika azimio la pamoja la Mawaziri ambalo lilipangwa kuwasilishwa katika Mkutano wa Mawaziri wa Shirika la Biashara la Dunia (WTO) uliopangwa kufanyika Disemba, 2021 lakini ukaahirishwa kutokana na mlipuko wa virusi vipya vya UVIKO-19.

D. Mkataba wa Uwezeshaji Biashara wa Shirika la
Biashara Duniani

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Kamati ya Kitaifa ya Uwezeshaji Biashara (National Committee on Trade Facilitation – NCTF) inaendelea na hatua za utekelezaji wa Mkataba wa Uwezeshaji Biashara wa Shirika la Biashara Duniani kwa kuendelea kuandaa miradi ya kutekeleza maeneo ambayo Serikali ilihitaji muda na msaada wa kifedha na kiufundi katika kuyatekeleza. Aidha, kupitia Kamati hiyo, Wizara inaendelea na utaratibu wa kupunguza taratibu zinazotakiwa katika kuingiza na kuuza bidhaa ndani na nje ya nchi kupitia mfumo wake wa utoaji taarifa za biashara kwa njia ya mtandao (Tanzania Trade Portal). Mfumo huo unawasaidia wafanyabiashara kufanya maamuzi yenye tija baada ya kupata taarifa sahihi.

5.2.6 Sekta ya Maendeleo ya Biashara

A. Kuwezesha Upatikanaji wa Fursa za Masoko

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara iliratibu na kushiriki Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF) yaliyofanyika tarehe 28 Juni hadi 13 Julai, 2021, Jijini Dar es Salaam na Maonesho ya Sita (6) ya Bidhaa za Viwanda yaliyofanyika tarehe 3 hadi 9 Desemba, 2021 katika Viwanja vya Maisara Zanzibar. Lengo la Maonesho hayo ni kutoa fursa kwa wadau mbalimbali wa Sekta ya Biashara kujitangaza na kuonesha bidhaa na huduma mbalimbali zikiwemo kilimo, elimu, fedha, nishati, maji, bidhaa za viwandani, usafirishaji, afya, ujenzi, mawasiliano, madini, ardhi na makazi, burudani na michezo. Mafanikio yaliyopatikana kutokana na maonesho hayo ni: Jumla ya Kampuni 3,002 zilishiriki katika Maonesho ya 45 ya DITF ambapo, kati ya hizo kampuni 2,926 ni za nchini na 76 kutoka nchi 16 na watembeleaji 177,390; Kampuni na Taasisi 113 zilishiriki Maonesho ya Sita (6) ya Bidhaa za viwanda Zanzibar. Hati za makubaliano kwa ajili ya mauzo ya bidhaa na mazao mbalimbali yenye thamani ya Shilingi bilioni 13.3 zilisainiwa kupitia mikutano ya Kibiashara (B2B) iliyoratibiwa kwa njia ya Mtandao na kuwashirikisha jumla ya wafanyabiashara 167 kutoka ndani na nje ya nchi; na Shughuli mbalimbali wakati wa maonesho zilitoa fursa za ajira za muda zipatazo 1,200.
  2. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TANTRADE iliratibu ushiriki katika maonesho na misafara ya kibiashara ambapo jumla ya Kampuni 382 zimefanikiwa kushiriki katika Misafara, Makongamano na Maonesho yaliyoratibiwa katika nchi za Afrika Kusini, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Uturuki na Uingereza. Kupitia ushiriki huo, Kampuni hizo zimefanikiwa kujitangaza, kujifunza na kutafuta masoko ya bidhaa zao. Makubaliano yafuatayo yalifikiwa:-

i. Kuingia Mkataba wa Makubaliano kati ya Sekta Binafsi ya Tanzania na Chemba ya Burundi ya kuendesha masoko ya pamoja mipakani (Kigoma Business Hub). Utekelezaji wa mkataba huo utawezesha kuimarisha biashara katika nchi hizi mbili (2);

ii. Kampuni ya Wadi Degla Holding iliyopo nchini Misri inayojishughulisha na ujenzi wa viwanja vya michezo, hoteli, migahawa na maeneo maalum ya viwanda imeingia makubaliano na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa ajili ya kuwekeza nchini;

iii. Kampuni tano (5) za Kitanzania zinazojihusisha na kilimo, viwanda na huduma zilisaini Mkataba wa Ushirikiano na wafanyabiashara wa Burundi na kubaini fursa za uwekezaji katika Ziwa Tanganyika;

iv. Kujenga uhusiano na wamiliki wa viwanda utakaowawezesha kununua teknolojia ya uzalishaji bidhaa mbalimbali kwa bei nafuu zaidi hivyo kuepukana na udalali ya biashara ya teknolojia ya kilimo, madini, vipuri vya mashine na magari;

v. Majadiliano na Wamiliki wa Viwanda vinavyozalisha Mashine za Vipuri vya aina mbalimbali katika Sekta ya Kilimo yanaendelea ili kuwezesha kampuni za nchini Uturuki kufungua matawi ya viwanda vyao nchini Tanzania; na

vi. Kampuni ya UK DIT Agri Tech imeonesha nia ya kuwekeza katika Sekta ya Kilimo. Vilevile, Kampuni ya Perry Engineering imetaka kuwekeza katika mashine za kilimo. Jumla ya wafanyabiashara saba (7) wa Alizeti walishiriki katika msafara wa biashara kwenye nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambao walipata fursa ya kutafuta masoko ya bidhaa katika nchi hiyo.

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TANTRADE imeratibu ushiriki wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Maonesho ya Expo 2020 Dubai yaliyoanza tarehe 1 Oktoba, 2021 na kumalizika rasmi tarehe 31 Machi, 2022, ambapo Tanzania ni miongoni mwa nchi 192 zilizoshiriki. Kupitia Maonesho hayo, Tanzania imetangaza Miradi ya Kimkakati ya ujenzi wa miundombinu ya TEHAMA, Nishati, Reli, Barabara, Bandari, Madaraja, Viwanja vya Ndege, Kilimo, Uvuvi, Mifugo na vivutio vya Utalii. Lengo ni kuvutia na kuhamasisha Wawekezaji kuwekeza na kutangaza fursa za kibiashara, kuvutia watalii na kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia.
  2. Mheshimiwa Spika, Mafanikio yaliyopatikana kutokana na Maonesho hayo ni pamoja na:-

i. Kusainiwa kwa Hati za Makubaliano 37 zenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 8.5 sawa na Shilingi trilioni 18.5 ambapo Hati 12 ni baina ya Serikali ya Tanzania kupitia Wizara na Taasisi za Umma na Sekta Binafsi, Hati 23 ni baina ya kampuni binafsi kutoka Tanzania na kampuni nyingine zenye nia ya kushirikiana katika sekta za kiuchumi, Hati moja (1) ni baina ya Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar na Wawekezaji kwenye Sekta ya Utalii. Aidha, sekta zinazotarajiwa kunufaika na makubaliano hayo ni pamoja na nishati, kilimo, utalii, miundombinu, usafiri na teknolojia. Idadi ya ajira zaidi ya 200,000 zinatarajiwa kupatikana kutokana na makubaliano yaliyofikiwa;

ii. Kampuni na Taasisi za Sekta Binafsi 640 kutoka Tanzania na Jumuiya ya Watanzania waishio nje ya nchi zilishiriki kwa nyakati tofauti katika kipindi cha miezi sita (6) kwa lengo la kujitangaza na kukutana na Wabia wa kibiashara katika Sekta mbalimbali. Aidha, mikutano 101 ilifanyika ndani ya banda la Tanzania kati ya Taasisi hizo na wawekezaji na wafanyabiashara mbalimbali; na Programu 11 za kutangaza sekta za kilimo, madini, utalii, afya, ujenzi, miundombinu, usafirishaji, mifugo, uvuvi, nishati, maji, sanaa na utamaduni ziliratibiwa kwa lengo la kutangaza fursa zilizopo katika sekta hizo. Kadhalika, makongamano matatu (3) ya utalii, uwekezaji na kilimo yaliratibiwa;

iii. Bidhaa za Kahawa, Chai, Korosho, Vito vya Tanzanite, Essential oils za Shirika la Biashara Zanzibar (ZSTC), vipodozi vya asili (nazi, mwani na viungo), ngozi, mkonge, sanaa za mikono na ubunifu zilifanikiwa kuuzwa katika mfumo wa soko la kimtandao la Expo

2020 Dubai uiitwao World Souq; na

iv. Jumla ya watembeleaji 928,469 kutoka mataifa mbalimbali wametembelea Banda la Tanzania kwa lengo la kuona fursa za utalii, uwekezaji na biashara zilizotangazwa. Aidha, watembeleaji hao

pia walipata fursa ya kujifunza mila, desturi na tamaduni za Watanzania; na kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia.

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara iliratibu Kongamano la Wadau wa Alizeti, Maonesho pamoja na
    Mikutano ya kibiashara (B2B) kuanzia tarehe 10 – 15
    Agosti, 2021 Mkoani Singida ambapo jumla ya wadau 364 wa Alizeti walishiriki. Mafanikio yaliyopatikana kutokana na uratibu wa matukio hayo ni pamoja na: Jumla ya wasindikaji wa Alizeti 16 kutoka mikoa mbalimbali waliingia mikataba ya Kilimo cha Mkataba na wakulima zaidi ya 32,000 ndani ya nchi chini ya Wizara ya Kilimo. Aidha, Kampuni saba (7) ambazo ni wajumbe wa Umoja wa Wasindikaji wa Mafuta ya Alizeti Nchini (TASUPA) waliratibiwa kwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa ajili ya mikutano ya kibiashara na makampuni yanayosambaza mafuta ya kula na bidhaa za walaji nchini humo, pamoja na kuangalia fursa za kibiashara kwa bidhaa zitokanazo na mbegu za alizeti, kama vile mafuta, mashudu, vipodozi, sabuni, na nta ya alizeti. Lengo ni kuwezesha Sekta Binafsi kuwa na fursa pana ya masoko ya bidhaa wanazozalisha kwa nchi za EAC na SADC.
  2. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TANTRADE imefanya majadiliano na wanunuzi mbalimbali kwa kushirikiana na Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nje ya nchi, ambapo fursa za masoko ya bidhaa zifuatazo zilipatikana: Kampuni ya DLYLK For Food Trade ya Qatar imeingia mkataba na Kampuni ya Borema Affairs ya nchini Tanzania wa kupeleka nyama ya mbuzi na kondoo tani 120 kwa mwezi. Aidha, machinjio matatu (3) yanayomilikiwa na Kampuni za: TanChoice – Kibaha, Eliya Food Industries-Arusha na Alpha Choice yamekidhi vigezo na Kampuni hizo zipo tayari kuanza mazungumzo ya uuzaji wa tani 100 za nyama ya ng’ombe kila mwezi kwa Kampuni ya Panda kutoka Saudi Arabia.
  3. Mheshimiwa Spika, Pia, Wizara imefanikisha Kampuni tisa (9) kutoka Tanzania kupata nafasi ya kushiriki Maonesho ya Saba ya Kahawa na Chokoleti yaliyofanyika nchini Saudi Arabia kuanzia tarehe 8 hadi 12 Desemba, 2021. Kampuni hizo ziliweza kutangaza bidhaa wanazozalisha kama vile kahawa, chai, korosho, kashata na viungo na kuingia makubaliano na wanunuzi; na Kuratibu zoezi la ukaguzi wa ubora na usalama wa asali kwa Kampuni 22 kwa Mamlaka ya Chakula na Dawa ya nchini Saudi Arabia. Kampuni zitakazokidhi viwango vya ubora unaohitajika zitaunganishwa na wanunuzi wa Saudi Arabia ambao wapo tayari kununua asali kutoka Tanzania. Vilevile, Wizara imefanikisha upatikanaji wa Soko la Asali nchini Saudi Arabia ambapo kampuni 22 zinakamilisha taratibu za ukaguzi wa ubora unafanywa na Mamlaka ya Chakula na Dawa ya nchini Saudi Arabia. Mara baada ya kukamilika zoezi hilo, Kampuni hizo zitaunganishwa na wanunuzi wa asali waliopo nchini Saudi Arabia.
  4. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TANTRADE kwa kushirikiana na Kituo cha Biashara ya Kimataifa (ITC) pamoja na Umoja wa Wadau wa Viungo nchini (TASPA) chini ya ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU) imefanikisha uzinduzi wa Nembo ya Viungo vya Tanzania (Tanzania Spice Label) katika Maonesho ya 45 ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF) tarehe 9 Julai, 2021. Nembo hiyo itawasaidia wazalishaji wa viungo wa Tanzania kuweza kupata masoko na kuongeza ushindani wa bidhaa hizo katika soko la ndani na la kimataifa ambapo jumla ya Kampuni 10 zimekidhi vigezo vya kutumia Nembo hiyo.
  5. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na Shirika la Posta ilizindua uendeshaji wa Duka Mtandao lijulikanalo kama Posta e-Shop kwa lengo la kupanua fursa za masoko kwa wazalishaji wa bidhaa nchini. Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Februari, 2022 duka mtandao lina wafanyabiashara 800. Elimu zaidi inatolewa ili kuwafahamisha wafanyabiashara nchini kutumia fursa hiyo ya duka mtandao. Sambamba na hilo, Mamlaka inakamilisha taratibu za kutoa huduma saidizi za kibiashara kupitia Mfumo wa eTradeDesks ambao utarahisisha kutoa huduma kwa kampuni zinazofanya biashara kwa njia ya mtandao. Mamlaka pia imefanikiwa kuratibu kampuni za Kitanzania 58 na Mtandao wa JD World Wide wa nchini China kwa lengo la kupanua wigo wa masoko wa bidhaa za Tanzania.
  6. Mheshimiwa Spika, Vilevile, Wizara kupitia TANTRADE imepata fursa ya kutangaza bidhaa za Tanzania katika mtandao maarufu unaojulikana kama JD.com kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini China. Ili kuhakikisha kampuni za Kitanzania zinatumia fursa hiyo ipasavyo, TANTRADE imefanya uchambuzi wa Kampuni za Kitanzania ili kutambua bidhaa zilizokidhi vigezo vya kuunganishwa na mtandao huo. Hadi kufikia, Mwezi Machi, 2022 jumla ya Kampuni 58 za Kitanzania zilipatikana na kuunganishwa na mtandao huo.
  7. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TANTRADE kwa kushirikiana na Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) na Taasisi inayosimamia Kongani ya Mwani Zanzibar Seawead Cluster Initiative (ZASCI) ilifanya tathmini mbili (2) za biashara ikihusisha wafanyabiashara wa mchele kutoka Tanzania Bara na vikundi 28 vya wakulima, wasindikaji na wafanyabiashara wa zao la Mwani Unguja na Pemba ili kutambua changamoto zinazowakabili na kuzipatia ufumbuzi. Mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na: –

i. Wafanyabiashara wa mchele kuunganishwa na masoko ya uhakika kwa upande wa Zanzibar;
ii. Kuwezesha maandalizi ya ujenzi wa mtambo wa kukaushia Mwani kwa kutumia jua; na

iii. Kuwezesha fursa za ununuzi wa mashine ya kusaga Mwani kupitia Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) ili kuongeza thamani na kukidhi mahitaji ya soko.

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TANTRADE iliratibu majadiliano ya Kibiashara ya wanunuzi kutoka nchi mbalimbali kama vile China, Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa lengo la kufungua fursa ya kuuza mazao mbalimbali ikiwemo nafaka, karafuu, mchele, muhogo, soya na bidhaa nyingine. Mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na: Soko la karafuu tani 2,000 kwa mwezi kutoka Zanzibar (ZSTC) kuuzwa katika Falme za Kiarabu (Dubai); Soko la mchele tani 60 kwa wiki kwenda nchini Kenya unauzwa na kampuni nne (4) za G2L Limited, Katani Rice, Tarmo Rice na Ruaha Milling; Bodi ya Nafaka kufungua ofisi ya bidhaa za Nafaka nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (Lubumbashi) na Kenya; Kampuni ya Quality Pulse Exporters (QPE) iliingia makubaliano ya kuuza soya tani 2,000 kwa Kampuni ya China ambapo biashara inatarajiwa kufanyika kuanzia msimu wa Mwezi Mei hadi Septemba, 2022. Pia, Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro kilifanikiwa kuuza jumla ya jozi
    450 za viatu kupitia Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF); Soko la muhogo tani 600 ambapo wakulima kutoka Mkuranga walifanikisha kuiuzia Kampuni ya Dar – Canton na Dalyon. Aidha, Bodi ya Nafaka ilinunua tani 100,000 kutoka kwa Wakulima wa Mikoa ya Dodoma na Singida.
  2. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TANTRADE ilifanya tafiti kuhusu biashara kati ya Tanzania na nchi jirani za ukanda wa Afrika Mashariki zikiwemo Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya na Uganda kwa lengo la kubaini fursa, vikwazo na changamoto za kibiashara zilizopo. TANTRADE imefanikiwa kutambua mazao na bidhaa mbalimbali zinazohitajika kwa wingi katika nchi hizo ambazo ni pamoja na nafaka, madini (chuma na dhahabu), mazao ya mbogamboga na matunda. Taarifa za fursa zimesambazwa kwa Wizara na Sekta za uzalishaji za Kilimo, Uvuvi, na Mifugo.
  3. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TANTRADE inasimamia uanzishwaji wa Mradi wa Uongezaji Thamani wa Zao la Dagaa wenye thamani ya Dola za Marekani 1,855,925 utakaotekelezwa kwa muda wa miaka mitano (5) chini ya ufadhili wa Benki ya Afrika. Matokeo tarajiwa ya Mradi huo ni pamoja na kuongeza mauzo ya dagaa katika soko la ndani na nje ya nchi pamoja na kutoa fursa ya ajira na kipato kwa wananchi wapatao 4,550 wanaojishughulisha na mnyororo wa thamani wa zao la dagaa.

B. Kuimarisha Mifumo ya Ukusanyaji wa Taarifa za Biashara na Masoko

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TANTRADE imesambaza taarifa za fursa za masoko ya mazao ya Korosho, Viungo, Viazi, Nyama, Vitunguu, Asali, Nafaka na Bidhaa za Ngozi kwa wadau kutoka Umoja wa Ulaya, Falme za Kiarabu, Uganda, Misri, Malawi, Ghana na Kenya. TANTRADE pia imepokea na kujibu maulizo 251 yaliyowasilishwa na wafanyabiashara kuhusu taratibu za kusafirisha bidhaa nje ya nchi. Vilevile, takwimu za biashara kati ya Tanzania na soko la Afrika Kusini, China, Indonesia, Rwanda, Singapore, Tunisia, Ubelgiji, Uingereza, Ujerumani, Urusi, Uturuki na Visiwa vya Komoro zimeandaliwa ili kutambua fursa zilizopo kibiashara katika masoko hayo. Vilevile, TANTRADE imesambaza bei za wastani za wiki za mazao ya kilimo na mifugo katika masoko ya Dar es Salaam na Dodoma na kuhuisha taarifa za Kampuni 1,315 kwenye Kanzidata ya Wafanyabiashara.
  2. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na Tume ya Ushindani (FCC) imefanya zoezi la ufuatiliaji na tathmini ya mwenendo wa usambazaji wa bei ya vifaa vya ujenzi Tanzania Bara katika Mikoa

ya Arusha, Dar es Salaam, Mbeya, Dodoma, Kilimanjaro, Ruvuma, Pwani, Singida Shinyanga na Mwanza. Zoezi hilo lilitokana na changamoto ya uhaba na upandaji wa bei holela kwa vifaa vya ujenzi uliojitokeza kwa kipindi cha Mwezi Septemba, 2021 hadi Novemba 2021. Tathmini iliyofanyika ilibaini kuwa upandaji wa bei unatokana na uhaba wa saruji; mifumo duni ya usambazaji bidhaa hii kuwafikia watumiaji wa mwisho na ucheleweshaji wa upatikanaji wa saruji kutoka kiwandani. Aidha, Wizara imeendelea kukusanya taarifa za bidhaa sokoni ikiwa ni pamoja na bei za mazao makuu ya chakula, mafuta ya kula, vifaa vya ujenzi (saruji, nondo na Bati) katika masoko mbalimbali hapa nchini kwa lengo la kuwafahamisha wananchi na wadau wengine kuhusu mwenendo wa bei za bidhaa mbalimbali.

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TANTRADE imezindua Mfumo wa Kuwezesha Upatikanaji wa Taarifa za Taratibu za Kufuata Kupata Leseni na Vibali mbalimbali vya Biashara za Kimataifa. Mfumo huo ulizinduliwa kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Biashara Duniani (UNCTAD), Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Taasisi ya TradeMark East Africa. Aidha, Mfumo huo una watumiaji 30,203 na watembeleaji 88,890 kutoka ndani ya nchi na kwenye nchi za Afika Kusini, Marekani, Zimbabwe, Uganda, India, Kenya, China, Malawi, Zambia na Uingereza.
    Bidhaa zilizopata maulizo kwa wingi ni pamoja na korosho, pamba, Sanaa za mikono na magari.
  2. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TANTRADE imeweka mfumo wa kuhakikisha mazao na bidhaa mbalimbali zinazozalishwa nchini zinapata masoko endelevu ambapo inashirikiana na wazalishaji katika kuunda na kuimarisha vikundi vya wazalishaji ili kutatua changamoto wanazokumbana nazo katika kuyafikia masoko yenye tija. Vikundi vilivyoimarishwa na idadi ya wananchama wake ni umoja wa wadau wa Muhogo (318), Umoja wa Wadau wa Viungo (150), Wazalishaji wa bidhaa za ngozi (160) na Umoja wa Wazalishaji wa embe (150).

C. Kuendelea Kuboresha Mazingira ya Biashara

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia BRELA imeendelea kuimarisha na kuboresha Mifumo yake ya Online Registration System (ORS) na Tanzania National Business Portal (TNBP) ambayo hutumika kutoa huduma za kusajili Kampuni, Majina ya Biashara, Alama za Biashara na Huduma, Hataza na Leseni za
    Viwanda na Biashara. Hadi kufikia Mwezi Machi, 2022 BRELA imesajili jumla ya kampuni 7,842 kati ya 11,100 yaliyokusudiwa sawa na asilimia 71. Pia, imesajili Majina ya Biashara 15,034 kati ya 19,500 yaliyopangwa, sawa na asilimia 77 na Alama za Biashara na Huduma 2,872 kati ya 4,500 zilizokuwa zimepangwa, sawa na asilimia 64. Vilevile, BRELA imefanikiwa kutoa Hataza 23 kati ya 35 zilizokuwa zimepangwa, sawa na asilimia 66, leseni za Viwanda 96 kati ya 244 zilizokuwa zimepangwa, sawa na asilimia 39 na leseni za Biashara 8,901 kati ya 13,200 zilizokuwa zimepangwa sawa na asilimia 67.
  2. Mheshimiwa Spika, Pamoja na kukamilika kwa mifumo hiyo, BRELA inaendelea kufanya maboresho zaidi katika mifumo ili kuwa rafiki zaidi kwa watumiaji ambapo hadi kufikia Machi, 2022 kazi ya kufanya maboresho kwenye mfumo imekamilika na mifumo ipo kwenye hatua ya majaribio kwa Watumiaji wa ndani (User Acceptance Test – UAT).
  3. Mheshimiwa Spika, Mafanikio hayo yametokana na juhudi za Serikali katika kuendelea kuboresha mazingira kwa kuweka mifumo ya kielekitroniki ya utoaji wa leseni na usajili kwa njia ya mtandao na utoaji wa elimu kwa umma kwa njia mbalimbali. Ongezeko hilo pia linatokana na uimara wa Serikali katika kusimamia na kudhibiti taratibu za ufanyaji wa biashara unaozingatia sheria na kanuni zilizopo. Maboresho yanaendelea kufanyika katika mifumo ili kuwa rafiki kwa watumiaji. Mifumo iliyokamilika kufanyiwa maboresho ipo kwenye hatua ya majaribio kwa Watumiaji wa ndani (User Acceptance Test – UAT).
  4. Mheshimiwa Spika, Katika kuimarisha biashara nchini, jumla ya wadau wa biashara 257 katika Mikoa ya Dar es Salaam, Geita na Kigoma walipatiwa huduma ya utatuzi wa changamoto katika Kliniki ya Biashara inayoratibiwa na TANTRADE kwa kushirikiana na Taasisi Wezeshi za Biashara zipatazo 28. Lengo la Kliniki hiyo ni kusogeza huduma karibu na maeneo ya wananchi. Aidha, jumla ya changamoto 479 zinazowakabili wafanyabiashara zilitatuliwa.
  5. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TANTRADE ilishirikiana na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kuandaa Mwongozo wa Usimamizi wa Biashara na Huduma Ndogo Zisizo Rasmi (Wamachinga) katika maeneo mbalimbali nchini. Lengo la Mwongozo huo ni kuwa na usimamizi na uratibu wa uendeshaji wa biashara ndogo na zisizo rasmi nchini unaotambulika kitaifa ili kukabiliana na changamoto za ufanyaji biashara katika maeneo hatarishi katika maeneo mbalimbali mijini. Vilevile, Wizara kupitia TEMDO imekamilisha usanifu wa vibanda bora vya biashara vitakavyowezesha wajasiriamali wadogo kufanya biashara kwenye maeneo maalum yaliyotengwa kwa mpangilio. Vilevile, TEMDO ilifanya mkutano na wadau wa biashara ndogo ndogo Jijini Dodoma na Dar es Salaam Mwezi Novemba, 2021 na Januari, 2022 na kupokea maoni yao kwa ajili ya uboreshaji wa usanifu na michoro ya vibanda hivyo na utengenezaji wa chasili kwa vibanda hivyo unafanyika.
    Utekelezaji wa mradi huo unafanyika kwa kushirikiana na wataalam wa dhana ya biashara ndogo ndogo kutoka Chuo cha Elimu ya Biashara, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Ofisi ya Rais – TAMISEMI.
  6. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TANTRADE imetembelea Taasisi zinazotoa Huduma ya Uwezeshaji Biashara (Cross Border Trade Facilitation) na Kamati za Pamoja Mipakani Kukuza Biashara za Mpakani katika Vituo vya Forodha vya Rusumo kwenye mpaka wa Tanzania na Rwanda; na Mtukula kwenye mpaka wa Tanzania na Uganda. Lengo kuu la ziara hiyo ilikuwa kujadili fursa na changamoto za biashara kupitia vituo hivyo ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha wafanyabiashara 215 kuhusu fursa zinazotokana na matumizi ya Utaratibu wa Kiforodha Uliorahisishwa ndani ya Jumuiya Kadhalika, ziara hiyo ililenga kuwezesha wafanyabiashara nchini kuchangamkia fursa za biashara katika nchi jirani na hivyo kuongeza mauzo ya bidhaa na huduma zinazozalishwa nchini.

D. Kutoa Elimu kwa Wafanyabiashara

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TANTRADE imetoa mafunzo kwa wadau 134 ili kuwajengea uwezo wa taratibu za kuuza bidhaa nje ya nchi hususan katika soko la Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) na kufahamu fursa za kibiashara zilizopo katika nchi hizo. Kupitia mafunzo hayo wafanyabiashara walifundishwa mbinu za kiushindani za kutafuta masoko na kufahamu mifumo saidizi ya biashara ya kielektroniki ya kuwawezesha kupata taarifa mbalimbali za masoko na taratibu za kufanya biashara. Mifumo hiyo ni e-Malalamiko, e-Shop, Market Access na Trade Information Portal. Vilevile, Wizara kupitia TANTRADE ilishirikiana na UNCTAD kuratibu mafunzo kwa wafanyabiashara wadogo wanawake 65 katika mipaka ya Mikoa ya Kilimanjaro (Holili/Taveta), Mbeya (Kasumulu) na Songwe (Tunduma/Nakonde). Kupitia mafunzo hayo, vikundi hivyo vilipata taarifa kuhusu taratibu za kufanya biashara kupitia mipaka halali.
  2. Mheshimiwa Spika, Ili kuimarisha mahusiano na Halmashauri kwa lengo la kufikisha huduma kwa umma, BRELA imeanzisha Mkakati wa kutoa elimu kwa Maafisa Biashara na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri na Mikoa nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo ili waweze kuwasaidia wafanyabiashara wa maeneo yao kupata huduma za Wakala. Mpaka kufikia Mwezi Machi, 2022, Mafunzo kwa Maafisa Biashara yamefanyika katika Mikoa 14 ambayo ni: Dodoma, Geita, Iringa, Kagera, Mara, Mbeya, Mwanza, Morogoro, Njombe, Rukwa, Ruvuma, Singida, Simiyu na
    Songwe. Jumla ya Maafisa Biashara na Maafisa Sheria
    172 walipatiwa mafunzo juu ya Sheria ya Leseni za
    Biashara Sura 208 na utekelezaji wake. Lengo ni kuweza kuwajengea uwezo Maafisa Biashara kuwahudumia wafanyabiashara kwa weledi na kwa haraka ili kuboresha na kurahisisha uanzishwaji na ufanyaji wa biashara nchini. Aidha, mafunzo hayo yanaendelea kufanyika katika Mikoa mingine na uhusiano kati ya BRELA na Mamlaka za Serikali za Mitaa umeendelea kuimarika.
  3. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia FCC ilitoa elimu ya uelewa kuhusu masuala ya ushindani wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Ushindani Duniani yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 3 hadi 06 Desemba, 2021. Kupitia Kliniki ya Ushindani pamoja na kongamano lililofanyika Siku ya Kilele cha Ushindani Duniani, watu 187 walihudhuria na kupatiwa elimu kuhusu Sheria ya Ushindani ya Mwaka 2003 na kutolewa ufafanuzi wa masuala mbalimbali hivyo kuongeza uelewa dhidi ya bidhaa bandia na kuwashauri kutoa taarifa FCC mara wanapobaini viashiria vya vitendo vinavyokiuka Sheria.
  4. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TBS imetoa mafunzo na semina 54 kuhusu viwango na udhibiti wa ubora ikiwa ni sawa na asilimia 36 ya lengo la kufanya semina 150 kwa mwaka. Aidha, jumla ya wadau 2,433 wa sekta mbalimbali ikiwemo sekta za korosho na bidhaa za korosho, mafuta ya kupikia, maziwa na bidhaa za maziwa, zabibu, wafanyabiashara na taasisi mbalimbali walipewa mafunzo juu ya masuala ya viwango.
  5. Mheshimiwa Spika, FCT imeendelea kujitangaza kwa njia mbalimbali ili kuongeza uelewa katika masuala yanayohusu ushindani wa kibiashara na udhibiti wa Soko. Hii ikiwa ni pamoja na kupitia Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Dares Salaam (SabaSaba) ambapo zaidi ya washiriki 800 walitembelea banda la Baraza. Pia, elimu ya huduma za Baraza ilitolewa kwa zaidi ya washiriki 400 waliotembelea banda la Baraza wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square, Dodoma kuanzia tarehe 23-29 Januari, 2022. Katika Maonesho hayo taarifa fupi mbalimbali zilitolewa kwa ajili ya wadau na wananchi, elimu kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu shughuli za Baraza, elimu kuhusu umuhimu wa ushindani katika maendeleo ya uchumi wa viwanda Tanzania na ushiriki wa wadau katika kuimarisha ushindani katika maeneo wanayoyasimamia ilitolewa, maswali yaliulizwa na ushauri pia ulitolewa na Wadau na Wananchi Aidha, vyombo vya habari mbalimbali vilishiriki katika kutangaza shughuli za Baraza wakati wa Maonesho hayo.
  6. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia BRELA imeendelea kutoa elimu kwa njia mbalimbali zikiwemo vyombo vya habari, maonesho na mikutano. Msisitizo ukiwekwa katika usajili, urasimishaji wa biashara, pamoja na mabadiliko ya sheria zinazosimamiwa na BRELA kama vile kuanzishwa kwa Daftari la kuwatambua Wamiliki Manufaa wa Makampuni (Beneficial Ownership Register). Hadi kufikia Mwezi Februari, 2022, vipindi 45 vilirushwa kupitia vyombo vya habari mbalimbali ikiwemo runinga, redio, magazeti na mitandao ya kijamii. Kupitia vyombo hivyo uelewa wa wananchi kuhusu majukumu ya BRELA umeongezeka. Vilevile, hadi kufikia Februari 2022 BRELA imeshiriki katika maonesho 10 yakiwemo:
  • Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), Maonesho ya Madini- Geita, Maonesho ya Jumuiya ya Afrika Mashariki- Mwanza, Maonesho ya Utalii-Geita, Maonesho ya SIDO- Kigoma, Maonesho ya siku ya Posta Duniani-Dodoma na Maonesho ya Karibu Dodoma Festival—Dodoma na Maonesho ya Bidhaa za Viwanda Tanzania-Zanzibar. Lengo la kushiriki maonesho hayo ni kufikisha huduma za usajili, utoaji wa leseni na kutoa elimu ya biashara kwa wananchi.
  1. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia WRRB ilitoa mafunzo na kufanya uhamasishaji kuhusu manufaa ya matumizi ya Mfumo wa Stakabadhi za Ghala katika Mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Mkoa wa Geita, Lindi, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza, Njombe, Pwani, Ruvuma, Shinyanga, Simiyu, Singida na Songwe kwenye mazao ya Korosho, Ufuta, Kahawa, Dengu, Choroko, Soya, Kokoa na Mpunga.
  2. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia WMA imetoa elimu kwa umma kuhusu matumizi sahihi ya vipimo kwa kushiriki kwenye Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), Tamasha la Biashara Chato, Teknolojia ya Madini Geita, SIDO Kitaifa Kigoma, Maonesho ya Uhuru Singida, Tabora na Mapinduzi Zanzibar, Maonesho ya Wajasiriamali Iringa na Maonesho ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania. Wakala iliandaa na kurusha vipindi 13 vya TV na vipindi saba (7) vya redio pamoja na kutoa taarifa 50 kwenye magazeti mbalimbali. Pia, Wakala ilitoa elimu kwa Wafanyabiashara na Wakulima wa Viazi Mviringo na Parachichi Wilaya za Njombe Mjini, Makete, Wanging’ombe na kwenye Baraza la Madiwani Mpwapwa, Dodoma kuhusu umuhimu wa kutumia vipimo sahihi.

E. Kuimarisha Matumizi ya Mfumo wa Stakabadhi za Ghala

  1. Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2021/2022, Wizara kupitia WRRB imewezesha Mfumo wa Stakabadhi za Ghala kuanza kutumika katika Mkoa wa Morogoro kwenye zao la kakao. Wakulima wa kakao katika Mkoa wa Morogoro kwa mara ya kwanza waliuza zao hilo kwa bei ya wastani ya Shilingi 4,892.50 kwa kilo kutoka kipindi cha nyuma walichokuwa wakiuza kwa bei ya wastani ya Shilingi 2,000 kwa kilo, ikiwa ni zaidi ya mara mbili ya bei ya awali. Aidha, Bodi imewezesha

wakulima wa zao la ufuta Mkoa wa Songwe kuuza tani 348.850 zilizokuwa na thamani ya Shilingi milioni 772.8. Mfumo wa Stakabadhi uliwawezesha wakulima wa ufuta Mkoa wa Songwe kuuza zao hilo kwa wastani wa bei ya Shilingi 2,221.53 ukilinganisha na wastani wa Shilingi 1,200 hadi Shilingi 1,700 kwa wakulima waliokuwa wameuza nje ya Mfumo wa Stakabadhi za Ghala.

F. Kushughulikia Mashauri ya Uvunjifu wa Sheria ya Ushindani

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara pamoja na mambo mengine ina jukumu la kulinda ushindani wa haki na kumlinda mlaji dhidi ya tabia hadaifu katika soko ili kuepusha athari za kiuchumi. Katika kusimamia hilo, Wizara kupitia FCT imepokea mashauri mapya 22 na kufanya kuwa na jumla ya mashauri 68 kwa kujumlisha mashauri 46 yaliyokuwa hayajaamuliwa katika kipindi cha 2020/2021. Aidha, mashauri 28 yameshughulikiwa kwa kusikilizwa na kutolewa maamuzi. Mashauri 40 yanaendelea kusikilizwa katika hatua mbalimbali.
  2. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia FCC imeendelea kufanyia kazi jumla ya mashauri 15 yanayohusu ukiukaji wa Sheria ya Ushindani ya Mwaka 2003 ambayo ni: Mashauri matano (5) ya Ukiukwaji wa Sheria ya miungano ya Kampuni bila kuiarifu FCC; Mashauri Matano (5) ya kupanga bei kiholela; na Mashauri matano (5) ya matumizi mabaya ya nguvu za soko (5). Katika mashauri matano (5) yanayohusu miungano ya Kampuni yaliyofanyika bila kuitaarifu FCC, wadaiwa katika mashauri manne (4) waliomba kuyamaliza kwa njia ya suluhu na shauri moja (1) lililobaki lipo katika hatua za awali za uchunguzi. Katika mashauri yanayohusu kupanga bei, wadaiwa katika shauri moja (1) waliiomba FCC kufanya majadiliano kwa lengo la kumaliza shauri hilo kwa njia ya suluhu na mashauri mengine manne (4) yapo katika hatua mbalimbali za uchunguzi. Aidha, katika mashauri yanayohusu matumizi mabaya ya nguvu ya soko, FCC imekamilisha uchunguzi kwenye shauri moja (1) na inaendelea na uchunguzi katika mashauri mengine manne (4).
  3. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia FCC ilifanya chunguzi katika masoko mbalimbali ili kubaini mienendo kandamizi na hadaifu. Hivyo, mikataba
    264 iliyoandaliwa na upande mmoja (Standard Form
    Consumer Contracts) ilipitiwa. Kati ya hiyo, mikataba 134 ilipokelewa katika kipindi kilichopita. Mikataba hiyo ilitoka katika Sekta Ndogo za Benki na Fedha. Mapitio ya mikataba hiyo yaliwezesha usajili wa jumla ya mikataba ya watumiaji 35. Jumla ya maombi 229 yanaendelea kushughulikiwa na yapo katika hatua mbalimbali za kupata maamuzi.
  4. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia FCC, ilichambua na kupitisha maombi 37 ya miungano ya Kampuni sawa na asilimia 64 ya maombi yaliyoshughulikiwa. Katika maombi yaliyoidhinishwa, maombi 36 yaliidhinishwa bila masharti na ombi moja (1) liliidhinishwa kwa masharti yenye lengo la kulinda ushindani, kukuza uchumi pamoja na kulinda maslahi ya umma katika soko husika. Maombi yaliyoidhinishwa yalilenga kuwezesha kampuni husika kuongeza mitaji kama ilivyofanyika katika Sekta Ndogo ya Benki iliyowezesha benki zilizoungana kukidhi matakwa ya kiasi cha mtaji kinachoelekezwa na Mdhibiti ambaye ni Benki Kuu ya Tanzania; Kuongezeka uzalishaji katika Sekta ya Madini na kuwezesha kampuni husika kuongeza kiasi cha uchimbaji na kuanza kuchimba madini ya aina nyingine tofauti na ya awali mfano machimbo ya Nickel, Mkoani Kagera; Kukuza uchumi wa ndani katika Sekta ya Bima iliyowezesha Watanzania kuwa na hisa katika kampuni husika (local content); na Kuongezeka kwa ufanisi katika uzalishaji katika Sekta ya Kilimo iliyowezesha kampuni husika kupata zana za kisasa katika kilimo.
  5. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia FCC ilikamilisha utafiti wa ushindani katika soko la dawa za saratani nchini. Utafiti ulibainisha changamoto mbalimbali za kiushindani katika soko la dawa za saratani ikiwemo uwepo wa miungano ya Kampuni iliyofanyika pasipo kuwa na baraka za Tume, uwepo wa mikataba baina ya viwanda vya uzalishaji dawa za saratani na waingizaji wa dawa hizo nchini kinyume cha Sheria ya Ushindani ya Mwaka 2003 na uwepo wa viashiria vya matumizi mabaya ya nguvu za soko. Pia, utafiti ulibainisha uwepo wa mikataba inayofifisha ushindani baina ya viwanda vya utengenezaji wa mashine za utambuzi na hospitali nchini kwa kupewa mashine bure kwa sharti la kununua reagents zinazozalishwa na watengenezaji wa mashine hizo. Hali hiyo inazuia hospitali kununua reagents kutoka kwa wasambazaji wengine wenye bei nafuu. Kutokana na matokeo ya utafiti huo, FCC imeanza utekelezaji wa mapendekezo ya utafiti huo kwa masuala yanayoangukia katika mamlaka yake hususan suala la miungano ya kampuni isiyotolewa taarifa kwa FCC. Aidha, FCC inatarajia kuwasilisha masuala yaliyo nje ya mamlaka yake kwa wadau wengine ikiwemo Wizara ya Afya kwa ajili ya hatua stahiki.
  6. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia FCC ilipokea na kushughulikia malalamiko 17 kutoka kwa watumiaji wa bidhaa au huduma zisizokidhi matarajio yao. Malalamiko 11 sawa na asilimia 65 yalitokana na bidhaa na malalamiko sita (6) sawa na asilimia 35 yalitokana na kuwepo kwa vipengele kandamizi katika mikataba iliyoandaliwa upande mmoja ambayo haijasajiliwa na FCC. Vilevile, FCC ilipitia mikataba iliyoandaliwa upande mmoja (Standard Form Consumer Contracts) 264. Kati ya hiyo, mikataba 134 ilipokelewa katika kipindi kilichopita. Mikataba iliyopokelewa hadi kufikia Mwezi Februari, 2022 ilitoka katika Sekta Ndogo za Benki na Fedha. Ushughulikiwaji wa mikataba hiyo ulisababisha usajili wa mikataba 46. Mikataba iliyosalia ipo katika hatua mbalimbali za ushughulikiwaji ikiwemo ufuatiliaji wa taarifa zaidi kutoka kwa waombaji pamoja na kusubiri malipo ya ada ya usajili.
  7. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TBS imekamilisha maandalizi ya viwango katika bidhaa za kilimo, chakula, uhandisi na vifungashio mbalimbali. Hadi mwezi Machi, 2022 jumla ya viwango 160 sawa na asilimia 27.6 ya lengo la kutayarisha viwango 580 kwa mwaka vilikamilika. Aidha, kati ya viwango 160 vilivyokamilika, viwango 43 ni katika bidhaa za kemikali, 32 ni za uhandisi umeme, 28 ni za mazingira, 16 ni za ujenzi na 41 ni za kilimo na chakula.
  8. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TBS imetoa leseni 512 za nembo ya ubora ya TBS ambayo ni sawa na asilimia 85.3 ya lengo la kutoa leseni 600 kwa mwaka 2021/2022. Miongoni mwa leseni hizo, leseni250 zilitolewa kwa wajasiriamali wadogo wanaozalisha mafuta ya kupaka, chaki, mchele, korosho, unga wa mahindi, sabuni za aina mbalimbali, viungo, mafuta ya nazi, keki, pombe za nafaka, mkate, pombe isiyotokana na nafaka, pombe kali, mvinyo, nyama za kuku, na nyama za kusindika. TBS imetoa mafunzo kwa wajasiriamali (SMEs) na wadau mbalimbali katika dhana nzima za kuzingatia mifumo ya ubora ili kuzalisha bidhaa zenye ubora. Vilevile, TBS imesajili majengo, maeneo ya uzalishaji, uuzaji na usambazaji wa bidhaa za chakula na vipodozi 6,372 ambavyo ni sawa na asilimia 32.6 ya lengo la kusajili na kutoa vibali 19,530 kwa mwaka. Pia, Shirika lilisajili bidhaa za chakula na vipodozi 1,290 ambavyo ni sawa na asilimia 21.4 ya lengo la kusajili na kutoa vibali 6,040 kwa mwaka.
  9. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TBS limetoa vyeti vya ubora 60,412 kwa shehena za bidhaa zitokazo nje ya nchi; sawa na asilimia 88.8 ya matarajio ya kutoa vyeti vya ubora wa bidhaa 68,000 kwa mwaka 2021/2022. Aidha, TBS kupitia Programu ya Ukaguzi wa Magari hapa Nchini (Destination Inspection) imekagua magari 31,231 yaliyotumika nje ya nchi sawa na asilimia 69.4 ya lengo la kukagua magari 45,000 kwa mwaka. Vilevile, TBS imetoa taarifa 157 za kitaalam kwa wasafirishaji wa bidhaa nje ya nchi zilitolewa sawa na asilimia 130.6 ya lengo la kutoa ripoti za kitaalam 170 kwa mwaka.
  10. Mheshimiwa Spika, Sampuli 24,087 zilipimwa katika maabara mbalimbali za TBS kwa lengo la kuhakiki ubora wake, sawa na asilimia 46.3 ya lengo la kupima sampuli 52,000 kwa Mwaka 2021/2022.

Jumla ya vifaa 7,880 vilifanyiwa Ugezi sawa na asilimia 78.8 ya lengo la kufanyia ugezi vifaa 10,000 kwa kipindi cha mwaka 2021/2022. TBS imepata mkandarasi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa jengo la TBS Jijini Dodoma (Viwango House). Kwa sasa TBS lipo katika hatua ya kusaini mkataba pamoja na kukabidhi eneo kwa ajili ya kuanza ujenzi.

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TBS ina wajibu wa kuthibitisha mifumo ya ubora wa usimamizi (Management Systems Certification) katika taasisi na makampuni nchini. Hadi sasa, TBS imethibitisha na kutoa vyeti 13 vya usimamizi wa ubora wa mifumo kwa viwango vya kimataifa yaani ISO 9001 Quality Management Systems, ISO 22000 Food Safety
    Management Systems pamoja na Hazard Analysis and Critical Control Point (HACCP). Kati ya hivyo, vyeti nane (8) vinahusu mifumo ya usalama wa chakula. Kampuni zilizothibitishwa na TBS zimewezeshwa kuuza bidhaa zao za vyakula nje ya nchi. Aidha, TBS imefanikiwa kupata cheti cha ithibati kutoka Taasisi ya Utoaji wa Ithibati ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Africa yaani Southern Africa Development Community Accreditation Systems (SADCAS). Huu ni uthibitisho wa umahiri wa Shirika letu la TBS katika kutekeleza jukumu la kuthibitisha mifumo ya ubora kimataifa. 194. Mheshimiwa Spika, Mazao yanayohifadhiwa katika ghala chini ya Mfumo wa Stakabadhi za Ghala yanakuwa na ubora ambapo wanunuzi wa mazao/ bidhaa wanatakiwa kununua kutoka kwenye ghala zilizosajiliwa. Aidha, WRRB imeendelea kuhamasisha wanunuzi wa mazao kununua bidhaa kupitia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala ili kuwa uhakika wa upatikanaji wa mazao yenye ubora. Kwa Mwaka 2021/2022 katika Sekta Ndogo ya Korosho kilogramu 2,116,600 zilinunuliwa na wanunuzi wa ndani kupitia Mfumo huo.
    1. Mheshimiwa Spika, Katika
      Mwaka 2021/2022, WRRB kwa kushirikiana na Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC) na Soko la Bidhaa Tanzania (TMX) imeandaa miongozo ifuatayo: –

i. Mwongozo Na.1 wa Usimamizi wa Masoko na Mauzo ya Korosho Ghafi wa Mwaka 2021/2022 Toleo la Kwanza; na

ii. Mwongozo wa Biashara kwa Kutumia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala uliotolewa chini ya TCDC, WRRB na TMX wa Mwaka 2021 kwa mazao ya
Choroko, Ufuta, Soya na Mbaazi.

  1. Mheshimiwa Spika, Matumizi ya miongozo ya pamoja yamepunguza migongano baina ya Taasisi za Umma katika utekelezaji wa majukumu wakati wa misimu ya mazao. Aidha, ufumbuzi wa changamoto wakati wa utekelezaji wa majukumu ya taasisi hizo umerahisishwa kupitia kuunda timu ya pamoja. Aidha, Bodi imeandaa rasimu za Mwongozo wa Usimamizi wa Masoko na Mauzo ya Wanyama Hai (Mbuzi, Kondoo na
    Ng’ombe) na Mwongozo wa Usimamizi wa Masoko na Mauzo ya viazi mviringo, pilipili manga na vitunguu maji ili kuongeza wigo wa matumizi ya mfumo.
  2. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia WRRRB ina jukumu la kufanya uhamasishaji wa ujenzi wa miundombinu bora ya uhifadhi wa bidhaa kwa wadau mbalimbali wa maendeleo, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Taasisi za Serikali na Sekta Binafsi. Katika kuendeleza jitihada hizo Bodi imejenga ghala mpya zifuatazo: Ghala la MAMCU – Nanyamba; Ghala Mohamed Kossa –
    Mangaka; Ghala la Liwale ―B‖ – Liwale; na Ghala la RUNALI – Ruangwa. Pia, Bodi imefanya marekebisho ya Ghala la
    Mhonda – Mvomero na Ghala la Ikungi – Singida.
  3. Mheshimiwa Spika, Ili kuwezesha utoaji wa elimu ya Biashara, Wizara kupitia CBE iliwezesha Uwekaji wa jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Kampasi ya Mbeya uliofanywa na Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 30 Novemba, 2021. Kazi zilizofanyika ni pamoja na upauaji wa majengo yote 11 ikiwemo kumbi mbili (2) za mihadhara, madarasa manne (4), jengo moja (1) la maktaba, ofisi tatu (3) na maabara moja (1) ya kompyuta. Aidha, kazi zinazoendelea ni za umaliziaji wa majengo hayo ikiwemo; kuweka vigae kwenye sakafu pamoja na kutandaza mifumo ya umeme, maji na ya mawasiliano (ICT).
  4. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Chuo kimepata ithibati ya mitaala ya programu mpya saba (7) za masomo kwa ngazi ya cheti hadi shahada ya awali kwenye; Uendeshaji wa Biashara katika Utunzaji wa Kumbukumbu (Business Administration in Records and Archives Management), Uendeshaji wa Biashara katika Usimamizi wa Rasilimali Watu (Business Administration in Human Resources Management) Masoko na Utalii (Marketing and Tourism), Masoko ya Kimtandao (Digital Marketing), Uhasibu na Fedha (Accounting and Finance), Uhasibu na Kodi (Accounting and Taxation) pamoja na Huduma za Kibenki na Fedha (Banking and Finance). Aidha, Chuo kimekamilisha mtaala mpya wa masuala ya Ubunifu na Ujasiriamali (Innovation and Entrepreneurship). Mtaala huo utafundishwa kwa wanafunzi wa Shahada ya Uzamili (Masters’ Degree) baada ya kupitishwa na NACTVET. Pia, Chuo kinaendelea na uandaaji wa mitaala mingine minne (4) na kimeshawasilisha mitaala mingine minne
    (4) NACTVET kwa ajili ya kuomba ithibati.

G. Kufanya Kaguzi za Biashara

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TBS imezuia bidhaa zisizokidhi viwango kutoka nje ya nchi kuingia sokoni shehena 1,517 na limeteketeza bidhaa zisizo kidhi ubora zenye thamani ya Shilingi 6,737,453,243.31. Sehemu kubwa ya bidhaa zilizozuiwa na zilizoondolewa kutoka sokoni zilikuwa ni bidhaa za chakula na vipodozi. Hatua stahiki zimechukuliwa kwa mujibu wa Sheria ikiwemo kuelimisha Umma na bidhaa husika kuharibiwa.
  2. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia BRELA imefanya ukaguzi elimishi katika viwanda mbalimbali nchini katika Mikoa ya Lindi na Mtwara. Jumla ya viwanda 97 vilikaguliwa na kupewa elimu kuhusu huduma zinazotolewa na BRELA na namna ya kupata leseni za viwanda. Pamoja na ukaguzi wa Leseni za Biashara uliofanyika katika Mikoa ya Lindi na Mtwara tarehe 28 Juni, hadi 11 Julai, 2021, Shinyanga tarehe 22 Agosti hadi 05 Septemba, 2021 na Tanga tarehe
    27 Septemba hadi 11 Oktoba, 2021. Pia, ukaguzi wa Makampuni 16 ulifanyika katika Jiji la Dar es Salaam mwezi Novemba na Desemba, 2021.
  3. Mheshimiwa Spika, Hadi kufikia Februari, 2022 WMA imekagua na kuhakiki vipimo 619,731 sawa na asilimia 74.98 ya lengo la kukagua vipimo 826,541 vilivyokadiriwa. Kati ya vipimo vilivyokaguliwa na kuhakikiwa Vipimo 18,648 vilirekebishwa na 489 vilikataliwa. Pia, Wakala ilifanya zoezi la ukaguzi wa kawaida na wa kushtukiza wa vipimo mbalimbali vitumikavyo kwenye biashara, afya, usalama na mazingira. Vipimo vilivyokaguliwa kwa wingi ni mizani, pampu za kuuzia mafuta, dira za maji, malori ya kubebea mchanga/kokoto na magari ya kubebea mafuta.
  4. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia WMA iliendelea na ukaguzi wa bidhaa zilizofungashwa (prepacked goods) toka nje ya nchi na zile zinazozalishwa hapa nchini. Mipaka iliyokaguliwa kupitia vituo vya ukaguzi ilikuwa ni Sirari (Mara), Mtukula (Kagera), Namanga (Arusha), Holili (Kilimanjaro), Tunduma (Songwe), Tarakea (Kilimanjaro), Horohoro (Tanga), Kasumulu (Mbeya), Kasesya (Rukwa). Aidha, hadi kufikia Mwezi Februari, 2022 Vituo vipya viwili (2) vilifunguliwa Manyovu (Kigoma) na Mbweni (Dar es Salaam) na asilimia 80 ya bidhaa zilizopita mipakani zimekaguliwa. Pia, WMA ilipima vipimo 204 vilivyoingizwa nchini na kutoa idhini kwa vipimo 150 ili viweze kutumika hapa nchini na vilivyokataliwa ni vipimo 54.
  5. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia WRRB imeratibu kaguzi kwenye ghala 43, zilizopo katika Wilaya 21 za Mikoa saba (7) ya Lindi, Manyara, Mtwara, Pwani,
    Morogoro, Ruvuma na Mbeya Kaguzi hizo zilihusu ukaguzi kabla ya utoaji Leseni na ukaguzi wakati Mfumo ukiendelea. Pia, leseni 38 zimetolewa kwenye mazao manne (4) ambayo ni korosho (33), kahawa (2), Dengu (2) na Kakao (1). Aidha, Kampuni 30 za waendesha ghala na moja (1) ya Mameneja Dhamana (Collateral Managers) walipewa leseni za kuendesha ghala. Tani 236,793.361 za mazao yakiwemo korosho tani 225,314.368, Mbaazi tani 6,944.897, Soya tani 1,002.916 na kokoa tani 3,531.180 zimekusanywa na kuhifadhiwa katika ghala kuu.
  6. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia WRRB ilifanya kaguzi za aina tatu katika msimu wa bidhaa husika, zikiwemo kaguzi kabla ya leseni kutolewa, kaguzi za kushtukiza na kaguzi baada ya msimu wa bidhaa kuisha. Hadi kufikia Mwezi Desemba 2021/2022, zaidi ya ghala 50 zilikaguliwa na kusajili kampuni 32 za waendesha ghala na kutoa leseni 41 katika mazao ya Korosho, Kahawa, Dengu na Kakao. Aidha, jumla ya kilo 242,914,484.50 zinazojumuisha mazao ya Korosho, Kokoa, Kahawa na Dengu zilihifadhiwa kwenye ghala katika Mfumo wa Stakabadhi za Ghala kwa mwaka
    2021/2022.
  7. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia FCC ilifanya ukaguzi wa mikataba katika Kanda ya Kusini (Lindi na Mtwara), Kanda ya Ziwa (Mara na Mwanza),
    Kanda ya Mashariki (Dar es Salaam na Morogoro) na Kanda ya Kati (Tabora na Dodoma) ili kubaini taasisi zinazotumia mikataba isiyosajiliwa na FCC. Katika zoezi hilo, asilimia 40 ya taasisi katika Sekta Ndogo ya Huduma Ndogo za Kifedha (Microfinance) zinatumia mikataba iliyoandaliwa na upande mmoja ambayo haijasajiliwa na FCC. Pia, ilibainika kuwa baadhi ya taasisi hutumia mikataba tofauti na iliyosajiliwa na FCC nyingine zikitumia mikataba iliyorejeshwa na FCC ili ifanyiwe marekebisho kabla ya kusajiliwa na FCC. Kwa upande mwingine, ilibainika kuwa asilimia 90 ya benki zinatumia mikataba iliyosajiliwa na FCC.
  8. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia FCC ilifanya ukaguzi katika Bandari ya Dar es Salaam na Bandari Kavu (ICDs) ambapo jumla ya makasha (containers) 2,831 yalikaguliwa. Kati ya hayo, makasha
    58 yalikamatwa kwa kukiuka Sheria ya Alama za Bidhaa (MMA) ya Mwaka 2003 Bidhaa zilizokamatwa ni pamoja na bidhaa za matumizi ya nyumbani, vifaa vya ujenzi, vipuri vya pikipiki na magari, shajala pamoja na vifaa vya kielekroniki. Pia, kaguzi za kushtukiza 20 zilifanyika katika Mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Kilimanjaro, Mwanza na Morogoro. Katika kaguzi hizo, bidhaa bandia zikiwemo simu za mikononi, betri za simu, vifaa vya umeme, dawa za kuua wadudu, kahawa, wino wa printer, udi, viatu na charger za simu zilikamatwa kwa MMA.
    5.2.7 Masuala Mtambuka

A. Kuwezesha Utoaji wa Huduma

  1. Mheshimiwa Spika, Ili kuwezesha utoaji wa huduma, Wizara imepokea watumishi 14 katika kada mbalimbali ambao wamehamia na kupunguza uhitaji katika idara na vitengo. Mchanganuo wa watumishi hao na kada zao ni kama ifuatavyo: Afisa Usafirishaji (1), Afisa Tawala (2), Afisa Utumishi (1), Dereva (3), Mchumi
    (1) Afisa Biashara (3), Afisa Sheria (2) na Afisa Ugavi (1). Wizara iliandaa Mpango wa Mafunzo wa mwaka mmoja ambao ndiyo dira ya kuongoza mafunzo kwa lengo la kuwajengea uwezo watumishi na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao. Wizara imewawezesha watumishi tisa (9) kuhudhuria mafunzo ya muda mrefu na watumishi 11 wamewezeshwa kuhudhuria mafunzo ya muda mfupi katika kozi mbalimbali. Aidha, Wizara imewawezesha Watumishi saba (7) wanaostaafu katika mwaka huo wa fedha kuhudhuria mafunzo ya ujasiriamali mahsusi katika kuwaandaa na maisha baada ya kustaafu.

B. Kupambana na Rushwa

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea na jitihada za kupambana na kudhibiti rushwa kwa kutoa elimu kupitia vikao vya watumishi, Baraza la Wafanyakazi, na Menejimenti na kusisitizwa uadilifu katika utekelezaji wa majukumu. Wizara ilifanya semina kwa wajumbe wa Kamati ya Wizara ya Uadilifu mwezi Agosti, 2021. Wizara imeendeleza jitihada za kuboresha utendaji katika Dawati la Malalamiko kwa kupokea na kufanyia kazi malalamiko kwa wakati. Aidha, Wizara imeanza kufanya mapitio ya Mkataba wa Huduma kwa Mteja ili uweze kujumuisha majukumu yote ambayo imekabidhiwa baada ya kuundwa kwa Wizara mpya

C. Janga la UKIMWI na UVIKO – 19

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kushiriki katika mapambano dhidi ya UKIMWI kwa kuwahudumia watumishi wanne (4) walioathirika kwa kuwapa posho ya lishe na nauli. Wizara inaendelea na utoaji wa vifaa kinga (kondomu) kwa watumishi wa Wizara ili kuendelea kuwasisitiza umuhimu wa kutunza afya zao kwa kuepuka ngono zembe. Aidha, Wizara imewezesha maafisa wanaosimamia masuala ya mapambano dhidi ya UKIMWI/VVU kuhudhuria semina elekezi kuhusu upangaji wa mikakati ya kuhudumia watumishi waathirika pamoja na kuhudhuria maadhimisho ya kitaifa ya siku ya UKIMWI duniani.
  2. Mheshimiwa Spika, Wizara na taasisi zake imeendelea kupambana na maambukizi ya UVIKO-19 kwa kutoa elimu ya kujikinga na virusi vya korona na kuweka vipukusi maeneo ya ofisi. Aidha, katika mapambano hayo, Wizara imeunda kikosi kazi ambacho kinaratibu masuala ya UVIKO-19 ambapo taarifa za Wizara na Taasisi huwasilishwa Wizara ya Afya.

5.2.8 Mawasiliano Serikalini

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 20021 / 2022 Wizara imeendelea kutoa elimu na kuhabarisha umma kuhusu utekelezaji wa sera, mikakati na programu mbalimbali za kuendeleza Sekta ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kupitia vyombo vya habari ikiwemo radio, runinga, magazeti, majarida, mitandao ya kijamii na maonesho ya biashara yanayofanyika nchini.
  2. Mheshimiwa Spika, Wizara imekamilisha uandaaji wa Mkakati wa Mawasiliano (MIIT Communication Strategy) unaotumika kama mwongozo wa uandaaji na usambazaji taarifa za Wizara kwa Umma na kuendelea na maboresho ya Tovuti ya Wizara www. mit.go.tz ili iendane na mahitaji halisi ya habari na teknolojia ya kisasa. Vilevile, Wizara imeanzisha kurasa maalum za mitandao ya kijamii, Youtube, Twitter, Instagram na Facebook inayopatikana kwa jina la uwekezajiviwandabiashara.
  3. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) inaandaa na kutangaza kipindi cha ―Wekeza‖ kinachorushwa mara moja kwa wiki katika chaneli ya TBC1. Vilevile, Wizara inaandaa programu za runinga, na video fupi zinazohusu matukio mbalimbali yanayorushwa moja kwa moja kupitia ukurasa wa Wizara wa Youtube unaopatikana kwa jina la uwekezajiviwandabiashara. Wizara imeanzisha jarida la mtandao linalotoa taarifa za kazi zilizotekelezwa na Wizara kila mwezi. Pia, Wizara huandaa mabango ya mtandaoni yanayolenga kuhabarisha na kuelimisha Umma kuhusu shughuli zote za maendeleo ya Sekta ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara na matukio mbalimbali ya kitaifa.

5.2.9 Usimamizi wa Fedha na Ununuzi

  1. Mheshimiwa spika, Wizara imeendelea kuimarisha udhibiti wa matumizi ya fedha za umma kwa kuboresha usimamizi wa rasilimali fedha ikiwemo uzingatiaji wa sheria na kanuni za fedha na manunuzi ya umma. Aidha, katika kutekeleza masuala ya uwazi na uwajibikaji katika matumizi ya fedha za umma, Wizara imekuwa ikiandaa taarifa za fedha zinazokidhi viwango vya kimataifa katika uandaaji wa taarifa za fedha kwa taasisi za umma (International Public Sector Accounting Standards – IPSAs) na miongozo mbalimbali iinayotolewa na Wizara ya Fedha na Mipango. Kutokana na taarifa zinazokidhi viwango vya kimataifa na miongozo mbalimbaliya Serikali, Wizara kwa miaka mingi imekuwa ikipata Hati Safi za Ukaguzi kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ikiwemo ya Mwaka 2020/2021.
    1. Mheshimiwa Spika, Katika
      mwaka 2021/2022, Wizara imeendelea kutekeleza majukumu kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo inayotolewa na Serikali mara kwa mara. Katika kuhakikisha kuwa kunakuwepo na matumizi sahihi ya rasilimali za Serikali, Wizara imefanya ukaguzi wa fedha, rasilimali watu na ununuzi na kuhakikisha kwamba sheria, kanuni na taratibu zinafuatwa.
  2. Mheshimiwa Spika, Wizara iliandaa Mpango wa Ununuzi wa mwaka 2021/2022, taarifa za ununuzi za kila mwezi, robo mwaka pamoja na taarifa ya mwaka mzima na kuziwasilisha Mamlaka ya Udhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA). Wizara ilitumia Mfumo wa Ununuzi kwa Njia ya Mtandao (TANePS), kuratibu vikao vya Bodi ya Zabuni kwa kuzingatia Sheria ya Manunuzi Na.7 na Kanuni zake za mwaka 2013 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2016. Pia, Wizara imeboresha Daftari la Mali la Wizara (Non-Current Fixed Asset Register) kwa kuzingatia Mwongozo wa Mali za Serikali wa mwaka 2019 pamoja na Sheria ya Fedha ya Mwaka 2001 na Kanuni zake GN 132 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2004.
    5.2.10 TEHAMA na Takwimu
    1. Mheshimiwa Spika, Katika mwaka
      2021/2022, Wizara imetengeneza Mfumo wa Ghala la Kuhifadhia Taarifa za Wizara na Taasisi zake ambao umekamilika kwa asilimia 50 na Kutengeneza Kanzidata ya Taifa ya Viwanda ambayo kazi hii imekamilika kwa zaidi ya asilimia 70. Mfumo wa Ghala la Kuhifadhia Taarifa kwa sehemu iliyobaki ni kuunganisha mifumo ya Taasisi katika Ghala hilo ili mifumo hiyo iweze kuwasiliana na kubadilishana taarifa.

6 MWELEKEO WA SEKTA YA UWEKEZAJI, VIWANDA
NA BIASHARA

  1. Mheshimiwa Spika, Mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Sita unalenga kuongeza uwekezaji, kukuza Sekta Binafsi na kujenga uchumi shindani wa viwanda utakaowawezesha Watanzania kufikia na kunufaika na uchumi wa kati ifikapo 2025. Kufanya hivyo kutawezesha Watanzania kutumia fursa za kiuchumi na kijamii katika mifumo iliyoboreshwa na inayozingatia haki na utawala bora. Ni nia thabiti ya nchi yetu kumfanya kila Mtanzania kuwa na maisha bora na kunufaika na rasilimali na fursa zilizopo na zinazojitokeza. Hivyo, ni jukumu letu sote kuwaandaa na kuwawezesha Watanzania kuchangamkia fursa zilizopo ipasavyo.

A. Kuimarisha Taasisi za Utafiti na Maendeleo ya Teknolojia na Uwekezaji

  1. Mheshimiwa Spika, Katika kuendeleza
    uchumi wa viwanda, Serikali inaimarisha taasisi zake ili kukidhi mahitaji ya maendeleo na ujenzi wa viwanda nchini. Wizara inaziimarisha Taasisi za Utafiti na Maendeleo ya Teknolojia yaani TIRDO, TEMDO na CAMARTEC, kwa kupitia upya na kwa kina majukumu na miundo ya kisheria ya taasisi hizo. Lengo ni kuzifanyia maboresho mahsusi ili ziweze kuwa na tija na ufanisi katika kuleta mwendelezo wa mafanikio ya taasisi hizo na pia kuongeza nguvu katika kuendeleza viwanda nchini.
  2. Mheshimiwa Spika, Serikali itajielekeza katika kuimarisha taasisi za uwekezaji nchini hususan TIC, EPZA na NDC ili ziwe mihimili na nguzo za uwekezaji katika viwanda ambavyo ni muhimu katika kujenga uchumi wa Taifa. Msukumo ukiwa ni kujenga viwanda mama, viwanda vya kimkakati na viwanda ambavyo kutokana na umuhimu wake ni vyema Serikali ikashiriki.

B. Kuimarisha taasisi za uwezeshaji Kiuchumi

  1. Mheshimiwa Spika, Kwa kutambua umuhimu na mchango wa uwezeshaji wananchi katika uchumi na hususan ujenzi wa viwanda vidogo na vya kati, Serikali itachukua hatua za makusudi kuimarisha Mifuko na Programu za Uwezeshaji ili kukuza ujasiriamali nchini. Kipaumbele kitakuwa katika kuimarisha taasisi ya NEEC na SIDO ili ziweze kutoa mikopo kwa wanaviwanda na wafanyabiashara hasa wadogo ili kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja.
  2. Mheshimiwa Spika, Kwa kutambua umuhimu huo, Serikali itaongeza unafuu wa mikopo inayotolewa na Mfuko wa NEDF. Hivyo, kuanzia tarehe 1 Julai, 2022 riba za mikopo zitahuishwa ili ziwe chini ya riba za mabenki ya biashara. Viwango vya riba ya mikopo ya uzalishaji itapungua kutoka asilimia 18 hadi asilimia 9. Aidha, riba ya mikopo ya biashara na huduma itapungua kutoka asilimia 22 hadi asilimia 12.

C. Utoaji Huduma kwa Kulenga Wateja

  1. Mheshimiwa Spika, Utoaji huduma bora kwa wananchi kwa kiwango kinachoridhisha ni lengo kuu la mabadiliko ya kiutendaji ambayo Serikali ya Awamu ya Sita inayapa kipaumbele. Hivyo, mwelekeo wetu ni kuhakikisha kuwa taasisi za kisekta tukianzia na TIC, TBS, WMA na BRELA zinajielekeza katika kutoa huduma kwa kiwango kinachokidhi matarajio ya wananchi. Wizara yangu na taasisi zake itaongeza ubunifu katika utendaji kazi kwa tija na kutoa huduma kwa weledi ili kuchochea ufanisi katika Sekta ya
    Uwekezaji, Viwanda na Biashara na hatimaye kuongeza Pato la Taifa.

D. Kukuza Maendeleo ya Sekta Binafsi

  1. Mheshimiwa Spika, Mtazamo wa Sera za Taifa zinatambua nafasi ya Sekta Binafsi kama injini ya kukuza uchumi. Katika kukuza Sekta Binafsi hasa wajasiriamali wadogo na wa kati, Serikali itaweka mazingira wezeshi na rafiki kupitia upatikanaji wa mitaji, teknolojia rahisi na rafiki, masoko ya uhakika na huduma muhimu zinazolenga kuongeza tija na ufanisi katika uzalishaji ni suala lisilohitaji mjadala. Hivyo, katika kukuza Sekta Binafsi nchini, Serikali itaimarisha majadiliano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi pamoja na kuweka mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji.
  2. Mheshimiwa Spika, Kupitia Bunge lako Tukufu, natoa rai kwa Sekta Binafsi kutumia fursa ya uwepo wa mahitaji makubwa ya ngano, mafuta ya kula na sukari kushiriki katika uzalishaji na uchakataji wa mazao hayo nchini ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi.

E: Kuboresha Mazingira ya Biashara Nchini

  1. Mheshimiwa Spika, Ujenzi wa mazingira bora na endelevu ya biashara ni kichocheo kikubwa na muhimu katika kuvutia wawekezaji wa ndani na nje. Hivyo, Serikali kupitia Wizara yangu itahakikisha kuwa inaendelea kuboresha mazingira ya biashara nchini. Maboresho hayo yatavutia wawekezaji wa ndani na nje katika viwanda na biashara na hivyo kuwezesha kutumia fursa mbalimbali za ndani na nje ya nchi kadri zinavyojitokeza. Misingi ya maboresho ya mazingira ya kibiashara itawekewa nguvu ya kisheria na utaratibu wenye ushirikishaji mpana zaidi wa wadau. Aidha, katika kuhakikisha uendelevu na uhakika wa kuvutia wawekezaji na upatikanaji wa soko kwa bidhaa zetu nje ya nchi, Wizara kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeendelea kutumia Ofisi za Balozi zetu nje ya nchi kutangaza bidhaa zetu ikiwa ni pamoja na kuzishirikisha katika maonesho ya Kimataifa ambayo nchi inashiriki.

E. Ujenzi wa Miundombinu kwa ajili ya Uwekezaji wa Viwanda

  1. Mheshimiwa Spika, Kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu ya msingi na wezeshi kwa ajili ya ujenzi wa viwanda na ufanyaji biashara ni suala la msingi. Uendelezaji wa miundombinu hiyo kwa kushirikiana na sekta binafsi utapewa msukumo zaidi ili kuleta tija na mvuto kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi. Jitihada za kushirikisha Mamlaka ya Serikali za Mitaa katika kumiliki, kuendeleza na kusimamia Maeneo Maalum ya Uwekezaji nazo zitapewa kipaumbele kabla ya kukimbilia kutafuta wawekezaji wa nje.
  2. Mheshimiwa Spika, Katika kujengea uwezo na kuendeleza uwekezaji wa wajasiriamali wadogo na wa kati nchini, mwelekeo wa Wizara ni kuhakikisha kuwa ujenzi wa Industrial Shades unafanywa katika mikoa yote nchini. Pia, msukumo ukitakiwa katika kukamilisha miradi iliyoanza kwa kufungamanisha maboresho ya vituo vya biashara za mipakani na viwanda katika maeneo hayo.
  3. Mheshimiwa Spika, Maendeleo ya Sekta za Uwekezaji, Viwanda na Biashara Nchini hutegemea uwepo wa maeneo yaliyo na miundombinu stahiki kwa ajili ya uwekezaji ikiwemo nishati ya umeme na gesi asilia, maji, usafiri wa reli pamoja na barabara. Hivyo, Wizara yangu itaendelea kushirikiana na Wizara nyingine kuhakikisha kunakuwa na maeneo ya uwekezaji yenye miundombinu stahiki. Vilevile, Wizara yangu itahakikisha tunapunguza gharama za kuendesha biashara hasa katika utaratibu wa upatikanaji wa leseni na vibali mbalimbali vya biashara, ili kwa pamoja tuweze kuvutia wawekezaji na kukuza Sekta ya Viwanda kwa kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda vya kuongeza thamani mazao ya kilimo pamoja na malighafi nyingine ikiwemo madini na mazao ya misitu hivyo kupunguza uuzaji wa mazao na bidhaa ghafi nje ya nchi. Kwa kufanya hivi, Sekta ya Viwanda itaweza kuongeza ajira zitokanazo na uzalishaji viwandani.

F. Kukuza Masoko ya Bidhaa na Huduma zinazozalishwa Nchini

  1. Mheshimiwa Spika, Kuthamini rasilimali na bidhaa za ndani ni ukombozi muhimu wa kiuchumi kwa Taifa lolote kwa kuwa, nchi ni soko la kwanza kabla ya kutafuta soko lingine. Suala la msingi ni wananchi kujenga imani na kupata thamani na ubora wanaouhitaji katika bidhaa na huduma za ndani ya nchi. Kwa msingi huo, Wizara itaendelea kuhamasisha uimarishaji wa ubora na matumizi ya bidhaa za ndani, nguvukazi na malighafi za ndani ili kuleta ufungamanisho wa sekta katika kujenga uchumi na kuleta maendeleo kwa wananchi wake. Aidha, Wizara kupitia TANTRADE inaendelea kuhamasisha wananchi kutumia bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya ndani kupitia kaulimbiu ya ―Nunua Bidhaa za Tanzania‖, Jenga Tanzania Kaulimbiu hiyo ni muhimu sana katika kipindi hiki cha ujenzi wa uchumi wa viwanda ili kuimarisha viwanda vya ndani kwa kutegemea soko la uhakika la ndani ya nchi. Hii itajumuisha kusimamia matumizi ya bidhaa, mazao na nguvukazi ya ndani katika miradi ya kimkakati na uwekezaji unaofanyika nchini ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa dhana ya ushiriki wa Watanzania.
  2. Mheshimiwa Spika, Wizara pia itaendelea kuhimiza na kuhamasisha wawekezaji kuwekeza katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu. Jitihada zitaelekezwa katika kuhakikisha kuwa mipango na shauku ya wawekezaji kuwekeza Tanzania zinatimia kwa kushughulikia vikwazo, kuondoa usumbufu na urasimu na kuongeza bidii ya kuwashawishi wawekezaji wa ndani na wa nje kuwekeza hapa nchini. Vilevile, Wizara itaweka msukumo mkubwa katika kuendeleza kwanza:
    Viwanda ambavyo sehemu kubwa ya malighafi yake itatoka ndani, hususan kwenye sekta za kilimo, mifugo, uvuvi, madini na maliasili zilizopo nchini. Viwanda vya aina hiyo vitatupa fursa ya kujenga mfumo wa uzalishaji ndani ya nchi uliofungamana na kushikamana. Pili: Viwanda vya kuzalisha bidhaa ambazo zinatumiwa na watu wengi humu nchini yaani bidhaa kama vile nguo, viatu, mafuta ya kupikia, n.k. Kwa hiyo, viwanda hivyo vitakuwa na uhakika wa soko la ndani kabla ya kufikiria soko la nje. Viwanda hivyo vitatarajiwa kuzalisha ziada kwa ajili ya masoko ya nje na hivyo kutuongezea akiba ya fedha za kigeni.

G. Kujenga Sekta Binafsi

  1. Mheshimiwa Spika, Katika kufanikisha na kuimarisha soko la ndani, tunahitaji kuwa na Sekta Binafsi imara ambayo inaakisi utashi wa kisera na malengo ya kitaifa. Hivyo, pamoja na haki ambayo Sekta Binafsi inastahili, ina wajibu wa kutekeleza majukumu ambayo yana tija na kuweza kuendeshwa kibiashara ikiwemo kulipa kodi na ada stahiki za Serikali. Kwa upande wa wawekezaji kutoka nje, ni jukumu na wajibu wao kuhakikisha kuwa wanazingatia mikataba na masharti ya uwekezaji ikiwemo kuwajibika kulipa kodi na ada zinazostahiki kwa Serikali, kulipia michango ya wajibu kwa nchi, kujenga mahusiano mema katika maeneo ya uwekezaji na kuzingatia ushiriki wa Watanzania (matumizi ya bidhaa, wafanyakazi, malighafi, huduma za ndani, nk).
  2. Mheshimiwa Spika, Kwa upande mwingine, wawekezaji wa ndani wanakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo ukosefu wa mitaji, matumizi ya teknolojia duni, upatikanaji wa ardhi, upatikanaji wa masoko na ujuzi stahiki katika shughuli za uzalishaji viwandani na kuendesha biashara. Kimsingi, Sekta hiyo inahitaji kulindwa kwani viwanda vingi ni vidogo na vichanga kukabiliana na ushindani wa nguvu za soko na viwanda ambavyo tayari vimelindwa vya kutosha na kujijengea uwezo mkubwa wa ushindani. Ulinzi huo tunaozungumzia kwa viwanda vyetu pia ulikuwa ukifanywa na nchi zilizoendelea kiuchumi zikiwemo China na India kwani biashara na uwekezaji katika eneo hilo la wazalishaji, wafanyabiashara na wawekezaji kwa sehemu kubwa ni wadogowadogo. Azma ya Serikali sio kulinda shughuli za uzalishaji zisizo za tija bali ni kuhakikisha shughuli zenye tija zinaimarika na kuweza kushindana kimataifa.
    7 VIPAUMBELE KWA BAJETI YA MWAKA 2022/2023
    1. Mheshimiwa Spika, Katika Mwaka
      2022/2023, Vipaumbele vikuu vya Wizara ni: –

i. Miradi ya kipaumbele iliyopo katika Mipango na Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 inaanza utekelezaji;

ii. Uwekezaji katika Kongani na maendelezo kwenye SEZ, EPZA, Kongani za viwanda Mfano – Kongani ya Kigamboni, Kwala na Kitaraka;

iii. Usimamizi na udhibiti wa masoko;

iv. Ushiriki katika shughuli za Kikanda EAC, SADC, AfCFTA na Kimataifa;

v. Kuondoa urasimu katika kuhudumia wawekezaji na wafanyabiashara; na

vi. Kuimarisha ushiriki wa Sekta Binafsi moja kwa moja katika uchumi na uwezeshaji wa wananchi.

  1. Mheshimiwa Spika, Vipaumbele mahsusi ni vifuatavyo: –

i. Kuendelea kuratibu programu za uhamasishaji wa uwekezaji ndani na nje ya nchi;

ii. Kuratibu masuala ya uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi;

iii. Kuratibu ufanikishaji wa uwekezaji ikiwemo kuongeza ufanisi wa miradi ya uwekezaji kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC);

iv. Kuratibu uanzishaji na uendelezaji wa miradi mikubwa ya uwekezaji yenye manufaa mapana kwa
Taifa;

v. Kuimarisha mifumo ya kushughulikia changamoto za uwekezaji;

vi. Kuboresha mazingira wezeshi ya kuendeleza viwanda na biashara kwa kupitia na kutunga sheria, sera na mikakati ya kuvutia uwekezaji;

vii. Kuimarisha na kuhamasisha uwekezaji wa Sekta Binafsi katika Maeneo Maalum ya Kiuchumi (SEZ) na Maeneo Maalum ya Uwekezaji kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa zitakazouzwa nje (EPZ);

viii. Kuimarisha taasisi za utafiti na kufanya tafiti kwa ajili ya maendeleo ya viwanda;

ix. Kuhamasisha uwekezaji wa viwanda vinavyotumia malighafi zinazopatikana kwa wingi nchini na bidhaa zinazotumiwa kwa wingi nchini kama vile nguo, mafuta na sukari;

x. Kuendeleza viwanda vya usindikaji vinavyozalisha bidhaa za petroli (Petro-gas), kemikali, uzalishaji wa dawa za binadamu na vifaa vya ujenzi;

xi. Kuratibu programu za kuimarisha Mifumo ya Udhibiti wa Biashara inayolenga katika kupunguza gharama za uwekezaji na kufanya biashara;

xii. Kuimarisha mifumo ya uratibu na usimamizi wa masuala ya uwekezaji kitaifa;

xiii. Kushughulikia masuala ya ubora na viwango nchini;

xiv. Kuendelea kuwajengea uwezo watumishi; na

xv. Kutafuta fursa za masoko na kuwaunganisha na wajasiriamali wa ndani.  
8 MALENGO YA MWAKA 2022/2023

8.1 IDARA NA VITENGO VYA WIZARA

8.1.1 Maendeleo ya Uwekezaji

237.    Mheshimiwa  Spika,  Katika  Mwaka 

2022/2023, Sekta ya Maendeleo ya Uwekezaji imepanga kutekeleza malengo yafuatayo: –

i. Kukamilisha maandalizi ya Sera, Mkakati na Sheria ya Uwekezaji na kuanza utekelezaji wake;

ii. Kuratibu uanzishaji na uendelezaji wa miradi mikubwa ya uwekezaji yenye manufaa mapana kwa Taifa;

iii. Kuendelea kuratibu programu za uhamasishaji wa uwekezaji ndani na nje ya nchi;

iv. Kuimarisha mifumo ya kushughulikia changamoto za uwekezaji;

v. Kuratibu programu za kuimarisha Mifumo ya Udhibiti wa Biashara inayolenga katika kupunguza gharama za uwekezaji na kufanya biashara;

vi. Kuimarisha ushiriki na maslahi ya nchi katika masuala ya uwekezaji kwenye ushirikiano wa
kikanda na kimataifa;
vii. Kuimarisha uhamasishaji wa fursa za uwekezaji na kuboresha Mfumo wa Kanzidata ya Takwimu za Uwekezaji na Kanzidata ya Benki ya Ardhi kwa ajili ya Uwekezaji; na

viii.Kuimarisha mifumo ya uratibu na usimamizi wa masuala ya uwekezaji kitaifa.

8.1.2 Uwezeshaji Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta
Binafsi

  1. Mheshimiwa Spika, Katika Mwaka 2022/2023, Sekta ya Uwezeshaji Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta
    Binafsi imepanga kutekeleza malengo yafuatayo: –

i. Kufanya tathmini ya utendaji wa Sekta Binafsi katika uchumi wa nchi;

ii. Kuandaa Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Sekta
Binafsi na Mkakati wake;

iii. Kuandaa taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Mikutano ya Taifa ya Baraza la Biashara Tanzania (TNBC);

iv. Kuandaa Kanzidata ya Sekta Binafsi Nchini;

v. Kuandaa Dirisha kwa ajili ya kushughulikia malalamiko ya Sekta Binafsi;
vi. Kufanya mapitio ya Mwongozo ya Majadiliano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika ngazi za mikoa na wilaya;

vii. Kutoa mafunzo katika Mikoa mitano (5) kuhusu majadiliano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika ngazi ya mikoa na wilaya;

viii. Kuandaa Sera ya Taifa ya Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati na Uwekezaji nchini;

ix. Kufanya Mapitio ya Sheria ya Taifa ya Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi ya Mwaka 2004; na

x. Kujenga Vituo vipya vya Uwezeshaji Wananchi katika baadhi ya mikoa na wilaya ambayo haijajenga.

8.1.3 Maendeleo ya Viwanda

239.    Mheshimiwa  Spika,  Katika  Mwaka 

2022/2023, Sekta ya Viwanda imepanga kutekeleza malengo yafuatayo:-

i. Kuhamasisha uongezaji thamani wa mazao ya kilimo ili kuongeza ushindani;

ii. Kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa Miradi ya
Kimkakati;

iii. Kufanya tathmini katika sekta za kipaumbele (Nguo na mavazi, Ngozi na bidhaa za Ngozi, Korosho na
Mafuta ya kula);
iv. Kuendelea kueneza dhana ya KAIZEN nchini;
v. Kuwezesha utekelezaji wa Programu ya PCP; vi. Kuainisha mahitaji ya ujuzi viwandani; vii. Kukamilisha marejeo ya Sera ya Viwanda (SIDP) na
Mkakati wake (IIDS);

viii.Kuandaa mikakati ya Pamba, Nguo na Mavazi, Ngozi na Bidhaa za Ngozi na Mafuta ya Alizeti; na

ix. Kufanya tathmini ya hali halisi ya uzalishaji na mahitaji ya sabuni, mboga na matunda na dawa za binadamu.

8.1.4 Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo

  1. Mheshimiwa Spika, Katika Mwaka 2022/2023, Wizara kupitia Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo imepanga kutekeleza malengo yafuatayo: –

i. Kuhamasisha na kufuatilia utekelezaji wa utengaji na uendelezaji wa maeneo kwa ajili ya shughuli za wajasiriamali wadogo na wa kati kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa;

ii. Kukamilisha marejeo ya Sera ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo (2003) pamoja na Mkakati wa Utekelezaji wake; na

iii. Kuhamasisha urasimishaji wa shughuli za wajasiriamali wadogo na wa kati ikiwa ni pamoja na kuelimisha faida za urasimishaji.
8.1.5 Mtangamano wa Biashara

241.    Mheshimiwa  Spika,  Katika  Mwaka 

2022/2023, Wizara kupitia Sekta ya Mtangamano wa
Biashara imepanga kutekeleza malengo yafuatayo: –

i. Kuendeleza majadiliano ya kibiashara kati ya Nchi na Nchi (Bilateral), Kikanda (Regional) na Kimataifa (Multilateral) kwa ajili ya kupanua fursa za masoko na uwekezaji ili kuvutia uwekezaji nchini;

ii. Kuendelea na majadiliano ya utekelezaji wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara kwa Nchi za Afrika
(Continental Free Trade Area – CFTA);

iii. Kukamilisha majadiliano ya kuanzisha Eneo Huru la Biashara la Utatu (Tripartite) linalojumuisha Kanda za COMESA, EAC na SADC;

iv. Kukamilisha majadiliano ya Biashara ya Huduma kwa sekta sita (6) za kipaumbele katika nchi wanachama wa SADC;

v. Kutekeleza Itifaki ya Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenye masuala ya Biashara ya Bidhaa na Huduma;

vi. Kuratibu na kushiriki kwenye majadiliano ya biashara ya kimataifa na utekelezaji wake katika mashirika yaliyo chini ya Umoja wa Mataifa na mengineyo ikiwemo WTO, UNCTAD, CFC na ITC;
vii. Kukamilisha utungaji wa Sheria ya Ahueni ya Kibiashara (Anti-dumping and Countervailing Measures);

viii.Kukamilisha mapitio na kuanza utekelezaji wa Sera mpya ya Taifa ya Biashara; na

ix. Kuimarisha Kamati za Kitaifa za Kusimamia
Urahisishaji wa Biashara Nchini.

8.1.6 Maendeleo ya Biashara

242.    Mheshimiwa  Spika,  Katika  Mwaka 

2022/2023, Wizara kupitia Sekta ya Maendeleo ya
Biashara imepanga kutekeleza malengo yafuatayo: –

i. Kuendelea kuboresha mazingira ya biashara nchini;

ii. Kuhamasisha Jumuiya ya Wafanyabiashara kuhusu fursa za masoko ya upendeleo yatakonayo na majadiliano ya Nchi na Nchi, Kikanda na Kimataifa;

iii. Uratibu wa kazi za Mafisa Biashara Nchini;

iv. Uratibu na uendelezaji wa miundombinu ya masoko;

v. Kuratibu majukwaa ya masoko nchini; vi. Kuendelea kuboresha mazingira ya biashara nchini; vii. Kuhamasisha na kurahisisha biashara mipakani; viii.Kuhamasisha na kuwezesha utangazaji wa bidhaa na huduma za Tanzania; na
ix. Kuandaa na kupitia Sera, Sheria na Kanuni mbalimbali.

8.1.7 Maendeleo ya Rasilimali Watu na Utoaji wa
Huduma

  1. Mheshimiwa Spika, Katika Mwaka 2022/2023, Wizara itatekeleza malengo yafuatayo kwenye eneo la Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu:-

i. Kuajiri watumishi 38 wa kada mbalimbali kwa lengo la kuwezesha Idara na Vitengo kutekeleza majukumu yake ipasavyo;

ii. Kupandisha vyeo watumishi 57 wa kada mbalimbali;

iii. Kutoa mafunzo elekezi kwa waajiriwa wapya 38, kuwapeleka katika mafunzo ya muda mrefu watumishi 26, kuwawezesha watumishi 41 kuhudhuria mafunzo ya muda mfupi katika vyuo mbalimbali nchini ili kuboresha utendaji kazi, kukidhi mahitaji ya Muundo na kutoa mafunzo ya kujiandaa kustaafu kwa watumishi sita (6); na

iv. Kutekeleza Mfumo wa Wazi wa Mapitio ya Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS) kwa Watumishi 231.
8.2 TAASISI ZILIZOPO CHINI YA WIZARA

8.2.1 Kituo cha Uwekezaji Tanzania

  1. Mheshimiwa Spika, Katika Mwaka 2022/2023, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimepanga kutekeleza malengo yafuatayo:-

i. Kuendelea kuboresha mifumo ya kusajili ili kuongeza idadi ya miradi ya uwekezaji inayosajiliwa na Kituo;

ii. Kuendelea kuboresha na kuimarisha huduma zitolewazo katika Kituo cha Huduma za Mahali Pamoja (One Stop Facilitation Centre) ili kufanikisha uwekezaji;

iii. Kuendelea na mkakati wa kufuatilia na kutathmini miradi ya uwekezaji iliyosajiliwa (Project Monitoring
& Evaluation);

iv. Kuendelea na kutafuta ardhi kwa ajili ya uwekezaji;

v. Kuendelea kuhamasisha uwekezaji ndani na nje ya nchi kupitia makongamano na semina;

vi. Kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya masuala mbalimbali ya uwekezaji nchini kupitia vyombo vya habari na mitandao;

vii. Kuendelea kutatua migogoro na changamoto za uwekezaji;

viii.Kufanya tafiti mbalimbali ikiwa ni pamoja na tafiti za kuibua fursa za uwekezaji nchini, tafiti za kuboresha mazingira ya uwekezaji, tafiti za kuibua maeneo yenye fursa za uwekezaji kwa ajili ya wajasiramali wa kati na wadogo;

ix. Kuendelea kushirikiana na Balozi za Tanzania katika kuitangaza Tanzania ili kuvutia uwekezaji kutoka nchi zilipo balozi hizo; na

x. Kuwajengea uwezo wafanyakazi wa Kituo ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

8.2.2 Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi

245.    Mheshimiwa  Spika,  Katika  Mwaka 

2022/2023, Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) limepanga kutekeleza malengo yafuatayo:-

i. Kuratibu utekelezaji wa Mpango wa Kuendeleza Viwanda Vidogo na vya Kati (SANVN viwanda scheme);

ii. Kuratibu masuala yanayolenga kuwawezesha wananchi kiuchumi ili wanufaike na fursa zilizopo na kushiriki kikamilifu katika shughuli za uchumi;

iii. Kuhamasisha wananchi kuanzisha na kujiunga na vikundi vya uzalishaji mali, vyama vya kuweka akiba na kukopa (SACCOS), benki za jamiii vijijini
(VICOBA) na vikundi vingine vya kiuchumi;

iv. Kuimarisha uratibu wa utendaji wa Mifuko na
Programu za Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi;

v. Kuratibu upatikanaji wa elimu ya biashara, fedha, masoko, ithibati na ujasiriamali kwa vijana, vyama vya ushirika na vikundi vya kiuchumi; na

vi. Kuratibu ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya Kimkakati na uwekezaji hasa katika Sekta za vipaumbele kama vile mafuta na gesi asilia; kilimo, mifugo na uvuvi; ujenzi; viwanda; utalii na Sekta mtambuka.

8.2.3 Shirika la Taifa la Maendeleo

246.    Mheshimiwa  S p i k a ,  K a t ik a 

Mwaka 2022/2023, Shirika la Taifa la Maendeleo
(NDC) limepanga kutekeleza malengo yafuatayo:-

i. Kuendelea na utekelezaji wa Miradi ya Kimkakati, na kukamilisha taratibu za ulipaji wa fidia na majadiliano katika miradi ya Mchuchuma na Liganga na Makaa ya Mawe Katewaka;

ii. Kukamilisha majadiliano ya Mradi wa Matrekta ya
URSUS;

iii. Kuendelea na ukarabati wa Kiwanda cha KMTC katika Mkoa wa Kilimanjaro ;
iv. Kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya msingi katika Kongani ya Viwanda – TAMCO na kufanya usanifu wa miundombinu ya msingi katika Kongani za Nyanza, KMTC na Kange;

v. Kufanya tafiti ya matumizi sahihi ya eneo la Kiwanda cha Matairi Arusha;

vi. Kufanya maandalizi ya uchimbaji wa chuma ghafi (iron ore) Maganga Matitu na utafiti wa Makaa ya Mawe Mhukuru;

vii. Kuboresha Maktaba kwenda kwenye mfumo wa kidigitali; na viii.Kuendelea na uzalishaji wa viuadudu wa mbu waenezao malaria na kufanya majaribio ya pili ya viuatilifu pamoja na kukamilisha usajili na kupata vibali vya uzalishaji katika Kiwanda cha Viuadudu (TBPL).

8.2.4 Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji
kwa Mauzo Nje ya Nchi

247.    Mheshimiwa  Spika,  Katika  Mwaka 

2022/2023, Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa Mauzo Nje ya Nchi (EPZA) imepanga kutekeleza malengo yafuatayo:-

i. Kuendelea na utekelezaji wa Mradi wa Eneo Maalum la Kiuchumi Bagamoyo (Bagamoyo SEZ);
ii. Kukamilisha malipo ya fidia pamoja na kuendeleza miundombinu ya msingi katika Eneo Maalum la Kiuchumi Nala (Nala SEZ) Dodoma;

iii. Kuhamasisha Sekta Binafsi pamoja na Serikali za Mikoa kuwekeza katika kuendeleza Maeneo Maalum ya Kiuchumi – SEZ;

iv. Kufanya uratibu, tafiti, ufuatiliaji na tathmini ya miradi inayotekelezwa na Mamlaka ya EPZ;

v. Kuboresha mifumo ya utoaji huduma kwa kutumia
TEHAMA; na

vi. Kuimarisha Rasilimaliwatu katika Mamlaka ya EPZ.

8.2.5 Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda
Tanzania

  1. Mheshimiwa Spika, Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) limepanga kutekeleza malengo yafuatayo kwa Mwaka 2022/2023;

i. Kuendelea kuimarisha Idara ya Uhandisi kwa kuongeza wataalam na vifaa hasa katika shughuli za upimaji ubora (Non Destructive Testing) wa mabomba ya mafuta na gesi ili kuendelea kukidhi viwango vya Kimataifa;

ii. Kuendelea na kukamilisha mchakato wa ithibati (Accreditation) na kuboresha maabara ya mazingira, kemia, makaa ya mawe, mafuta na gesi na vifaa ili ziweze kufikia viwango vya kimataifa na kuweza kutoa huduma bora kwa wazalishaji viwandani;

iii. Kuendelea kufanya utafiti katika kanda saba (7) nchini ili kubaini fursa za uwekezaji na maeneo yenye viwanda na rasilimali zilizopo (Industrial Mapping) ili kutumia kikamilifu rasilimali zilizopo na kuongeza uwekezaji Nchini;

iv. Kuendelea na ukamilishaji wa Jengo la Utawala ili kuongeza nafasi za maabara, viatamizi na Kituo cha Ubashiri wa Teknolojia na taarifa za maendeleo ya viwanda;

v. Kuendelea na ununuzi wa vitendea kazi ikiwemo magari ikiwa ni nyenzo muhimu katika utekelezaji wa majukumu ya Shirika;

vi. Kuendelea kutoa huduma za kitaalam viwandani zenye lengo la kuongeza uzalishaji wa bidhaa bora bila kuchafua mazingira pia zinazolenga matumizi bora ya nishati;

vii. Kuendelea na mchakato wa kufanya utafiti na kutoa mafunzo kwa wadau 400 wa Sekta ya Ngozi kuhusu namna bora ya kuongeza thamani ya ngozi zinazozalishwa Nchini na Kuimarisha Maabara ya Ngozi ili kutoa huduma kwa wadau wa viwanda vidogo na vikubwa vya kuchakata ngozi;

viii.Kuandaa kanzidata ya viwanda vya nguo na ngozi nchini na kufanya tathmini ya viwanda vya nguo

na ngozi ili kubaini changamoto na kuainisha mapendekezo ya utatuzi wa changamoto; na

ix. Kuendelea kukamilisha mchakato wa mapitio ya Sheria ya Bunge Na. 5 ya Mwaka 1979 iliyoanzisha TIRDO.

8.2.6 Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini

249.    Mheshimiwa  Spika,  Katika  Mwaka 

2022/2023, Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) kimepanga kutekeleza malengo yafuatayo:-

i. Kuendeleza utafiti na uendelezaji wa teknolojia kwa kuanzisha Kiwanda Darasa cha Kubangua Korosho katika Wilaya ya Manyoni katika mkoa wa Singida; na Kufanya kazi za utafiti kwa kushirikiana na Taasisi nyingine za utafiti ikiwa ni pamoja na kubaini mahitaji ya zana za kilimo, mifugo, uvuvi na teknolojia za vijijini kwa wakulima katika Wilaya za Momba Mkoa wa Songwe, na Chemba katika Mkoa wa Dodoma;

ii. Kuendeleza mafunzo na kuhawilisha zana za kilimo kwa kuanzisha Kitovu cha Teknolojia za Kihandisi (Engineering Technology Hub – ETH) katika Wilaya ya Karatu katika mkoa wa Arusha, Kujenga ufahamu wa zana za kilimo na teknolojia za vijijini kwa wadau, kuanzisha maktaba ya kisasa kwa ajili ya utafiti na uendelezaji wa teknolojia;

iii. Kufanya ukaguzi wa zana za kilimo na teknolojia za vijijini kwenye maeneo ya mipakani; na

iv. Kufanya ufuatiliaji, tathmini na ukaguzi wa miradi.

8.3 Shirika la Uhandisi na Usanifu wa Mitambo
Tanzania

250.    Mheshimiwa  Spika,  Katika  Mwaka 

2022/2023, Shirika la Uhandisi na Usanifu wa Mitambo Tanzania (TEMDO) limepanga kutekeleza malengo yafuatayo: –

i. Kuendeleza ubunifu na utengenezaji wa chasili cha mtambo mdogo wa kuchakata miwa na kutengeneza sukari (sugar mini-processing plant) kwa ajili ya wajasiriamali wadogo ili kutoa ujuzi na ajira na kupunguza upungufu wa sukari nchini;

ii. Kusanifu na kuendeleza utengenezaji wa vifaa tiba vya hospitali kwa awamu ya II (Wheel chairs, 6-body Mortuary cabinets, stretchers, theatre trolleys, Autoclave, and Laundry machines) ili kuisaidia Serikali kutoagiza vifaa tiba kutoka nje ya nchi na kupunguza matumizi ya fedha za kigeni;

iii. Kubuni na kuendeleza mtambo wa kuchakata mkonge ili kupata nyuzi bora (export quality sisal fibres) na kuwezesha ukuaji wa viwandana ongezeko la ajira;

iv. Kubuni na kuendeleza teknolojia ya kutengeneza matofali yanayostahimili joto kali (Refractory bricks) hapa nchini;

v. Kubuni na kuendeleza mtambo wa kuteketeza taka ngumu za hospitali mahsusi kwa kuchomea damu isiyofaa, mabaki ya wanyama na dawa zilizoharibika na kupitwa na muda (incinerating carcass from livestock/cattle abattoir, biomedical waste blood and expired drugs) katika Sekta ya Afya;

vi. Kusanifu na kuendeleza teknolojia ya kuhifadhi maziwa wakati wa kukusanya na kusafirisha ili yasiharibike mapema;

vii. Kuendeleza na kuunda kibiashara teknolojia ya kuhifadhi mazao ya mbogamboga kwenye ubaridi (Coldrooms for smallholder horticulture farmers) ili kuepusha mazao kuharibika haraka;

viii.Kuboresha Karakana kwa kusimika mashine na vifaa vya kisasa (Heavy duty 6-axes CNC Machines) na miundombinu, pamoja na kuanzisha ujenzi wa Karakana ya Useremala kwa ajili ya kuwezesha utengenezaji wa vifaa tiba nchini ili kuzalisha bidhaa kwa wingi;

ix. Kubuni na kuendeleza chasili cha mtambo wa kukausha mazao ya kilimo (Korosho) ili kuongeza thamani, na kubuni, kusanifu na kuendeleza teknolojia ya mtambo wa kuchakata chikichi ili kuongeza thamani;

x. Kufanya ufuatiliaji na tathmini wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo;

xi. Kutangaza huduma za Shirika ili kujenga uelewa kwa umma kwa kushiriki kwenye maonesho ya teknolojia/biashara, pamoja na kufanya ziara za kitaalam kwenye viwanda mbalimbali na kutatua changamoto za kihandisi;

xii.Kujenga uwezo wa Taasisi kwa kuwapatia wafanyakazi mafunzo mbalimbali ya muda mrefu na mfupi katika nyanja za usanifu, uendelezaji wa teknolojia mpya na kujua matumizi ya teknolojia mpya; na

xiii.Kuendelea na uboreshaji wa miundombinu ya karakananaofisiyausanifupamojanamiundombinu ya Taasisi kwa ujumla.

8.3.1 Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo

  1. Mheshimiwa Spika, Katika Mwaka
    2022/2023, Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo
    (SIDO) limepanga kutekeleza malengo yafuatayo: –

i. Kuendeleza Mitaa ya Viwanda ya SIDO kwa kuweka miundombinu wezeshi na kukamilisha kutengeneza Mfumo Unganishi wa TEHAMA wa Shirika;

ii. Kuhawilisha teknolojia kwa kuimarisha Vituo vya Uendelezaji Teknolojia (TDCs) na Vituo vya Mafunzo na Uzalishaji (TPC) vya SIDO;

iii. Kuimarisha Mfuko wa Wafanyabiashara Wananchi
(NEDF);

iv. Kutangaza Shirika na bidhaa za viwanda vidogo;

v. Kuongeza wigo wa huduma za SIDO kwa wajasiriamali; na

vi. Kuimarisha utendaji kazi wa Shirika.

8.3.2 Shirika la Viwango Tanzania (TBS)

  1. Mheshimiwa Spika, Katika Mwaka 2022/2023, Shirika la Viwango Tanzania (TBS) litatekeleza malengo yafuatayo: –

i. Kutayarisha viwango 630 vya kitaifa katika sekta/ nyanja mbalimbali ikiwemo nyanja za uhandisi mitambo, kemikali, uhandisi umeme, nguo na ngozi, madini, kilimo na chakula, mazingira pamoja na Sekta mtambuka;

ii. Kutoa leseni ya ubora kwa bidhaa 650 kutoka katika sekta mbalimbali zikiwemo bidhaa za wajasiriamali wadogo (SMEs);

iii. Kusajili majengo, maeneo ya uzalishaji, uuzaji na usambazaji wa bidhaa za chakula na vipodozi 10,000;

iv. Kusajili bidhaa za chakula na vipodozi 2,700;

v. Kukagua na kutoa vibali 100,000 kwa bidhaa zitokazo nje ya nchi;

vi. Kufanya ukaguzi wa ubora na kutoa vyeti vya ukaguzi 50,000 wa magari yaliyotumika yanayoingizwa nchini kwa utaratibu wa kukagua magari kabla ya kusafirishwa kuja nchini yaani Pre-Shipment Verification of Conformity to Standards (PVoC) Programme na kwa utaratibu wa kukagua magari baada ya kufika nchini ikiwa waagizaji watakuwa hawajakagua nje ya nchi;

vii. Kutoa mafunzo na kuendesha semina kuhusu viwango na udhibiti ubora kwa wadau 1,200 wa Sekta ndogo tatu (3) ambazo ni mchele, muhogo na viungo;

viii.Kuthibitisha kampuni 12 chini ya mifumo ya ubora
(management systems);

ix. Kupima sampuli 40,000 za bidhaa mbalimbali;

x. Kufanya ugezi kwa vifaa/mashine mbalimbali vipatavyo 12,000;

xi. Kuendelea na ujenzi wa Viwango House Dodoma; na

xii.Ujenzi wa maabara na ofisi katika Kanda ya Ziwa (Mwanza).

8.3.3 Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni
(BRELA)

253.    Mheshimiwa  Spika,  Katika  Mwaka 

2022/2023, Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni
(BRELA) itatekeleza malengo yafuatayo: –

i. Kuendelea kuelimisha umma juu ya utekelezaji wa sheria na umuhimu na faida za kufanya sajili mbalimbali za kibiashara zinazofanywa na BRELA;

ii. Kuendelea kufanya mapitio ya sheria mbalimbali za usajili na utoaji Leseni;

iii. Kuendelea kusimamia hitaji la taarifa za Wamiliki Manufaa na zoezi la uhuishaji wa taarifa za Makampuni na Majina ya Biashara;

iv. Kuendelea kuboresha mifumo-mtandao ya usajili na utoaji leseni na kuimarisha miundombinu ya TEHAMA;

v. Kuendelea kuimarisha mahusiano kati ya BRELA na uongozi wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri na Maafisa Biashara kwa lengo la kufikisha karibu huduma kwa umma katika maeneo yao;

vi. Kukamilisha maandalizi ya nyaraka zote muhimu zinazohusiana na maslahi ya Watumishi pia miongozo ya kiutendaji na utoaji maamuzi; na

vii. Kuendelea kuboresha mazingira ya kazi ikiwemo vitendea kazi na kutoa mafunzo kwa Watumishi kwa lengo la kuongeza tija na ufanisi katika utoaji wa huduma.

8.3.4 Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala

254.    Mheshimiwa  Spika,  Katika  Mwaka 

2022/2023, Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala
(WRRB) imepanga kutekeleza malengo yafuatayo: –

i. Kusimamia utekelezaji wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala kwa kutoa leseni kwa waendesha ghala, kuanisha ghala na kufanya ukaguzi wa ghala, kusimamia upokeaji na utoaji wa bidhaa ghala kuu pamoja na uandaaji wa miongozo ya bidhaa zinazotumia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala nchini;

ii. Kuhamasisha matumizi ya Mfumo wa Stakabadhi za Ghala;

iii. Kuainisha viwanda vinavyoongeza thamani mazao yaliyo katika Mfumo wa Stakabadhi za Ghala na kuwaunganisha na fursa mbalimbali;

iv. Kutoa elimu na kuhamasisha matumizi ya Mfumo wa Stakabadhi za Ghala kwa wadau mbalimbali katika maeneo yanayotekeleza Mfumo, na maeneo mapya;

v. Kufanya mapitio ya utekelezaji wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala kwa lengo la kuboresha utendaji na ufanisi;

vi. Kuendelea kupanua wigo na kuimarisha utekelezaji wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala katika maeneo mapya na yale yanayotumia Mfumo kwa sasa;

vii. Kutengeneza Mkakati mahsusi kwa ajili ya kutangaza Mfumo wa Stakabadhi za Ghala;

viii.Kuweka Mifumo mipya na kuimarisha Mifumo ya TEHAMA iliyopo ikiwemo ile ya maombi ya Leseni, upokeaji na utoaji wa bidhaa ghala kuu, mfumo wa utendaji kazi za kila za siku (e-office), mfumo wa ukaguzi wa ghala, mfumo wa usajili wa ghala nchini, mfumo wa ukusanyaji wa takwimu na taarifa mbalimbali pamoja na kuhuisha nyaraka mbalimbali za WRRB ili ziendane na Mifumo ya ICT

iliyopo;

ix. Kushirikiana na Halmashauri za Wilaya, Vyama vya Ushirika na Taasisi nyingine kuzitambua ghala zote nchini kwa lengo la kufanikisha ukarabati na ujenzi wa ghala za kuhifadhia mazao ya wakulima katika maeneo mbalimbali nchini pamoja na udarajishaji wa ghala zote; na

x. Kukagua na kuangalia utekelezaji wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala katika maeneo mbalimbali na kufanya tathmini ya utekelezaji wa Mfumo.

8.3.5 Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania

255.    Mheshimiwa  Spika,  Katika  Mwaka 

2022/2023, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) imepanga kutekeleza malengo yafuatayo: –

i. Kuimarisha ushindani wa kibiashara nchini;

ii. Kuanzisha na kusimamia mifumo ya ufanyaji
Biashara;

iii. Kutafuta masoko ya bidhaa za Tanzania;

iv. Kuboresha utoaji wa huduma kwa wafanyabiashara nchini; na

v. Kuimarisha uwezo wa Taasisi.

8.3.6 Wakala wa Vipimo

  1. Mheshimiwa Spika, Katika Mwaka 2022/2023, Wakala wa Vipimo (WMA) imepanga kutekeleza malengo yafuatayo:-

i. Kusimamia, kuhakiki na kukagua vipimo vyote vitumikavyo nchini kwa lengo la kumlinda mlaji;

ii. Kuendelea na ukaguzi wa bidhaa zilizofungashwa kwenye maeneo ya mipakani, bandarini na viwandani kwa lengo la kuhakiki usahihi wa kiasi/ idadi iliyotamkwa (decraled quantity);
iii. Kununua vitendea kazi ikiwemo vitendea kazi vya kitaalam na magari manne (4);

iv. Kuongeza idadi ya watumishi ikiwemo Maafisa Vipimo 150, Maafisa Vipimo Wasaidizi 50 na Madereva 50;

v. Kutoa elimu kwa umma kuhusu matumizi sahihi ya vipimo; na

vi. Kuendelea na ujenzi wa Ofisi ya Makao Makuu ya
Wakala wa Vipimo Mkoa wa Dodoma.

8.3.7 Tume ya Ushindani

  1. Mheshimiwa Spika, Katika Mwaka 2022/2023, Tume ya Ushindani (FCC) itatekeleza malengo yafuatayo: –

i. Kuboresha hali ya ushindani katika soko;

ii. Kumlinda mtumiaji kutokana na vitendo hadaifu na kandamizi katika soko;

iii. Kuongeza mapambano dhidi ya bidhaa bandia na pia kuhakikisha kiwango cha bidhaa hizo kinapungua katika soko; na

iv. Kuongeza ufanisi katika kutoa huduma kwa kuboresha afya za watumishi, kuongeza idadi ya wafanyakazi pamoja na kuwezesha mifumo ya kielekroniki ya utoaji huduma.
8.3.8 Baraza la Ushindani

258.    Mheshimiwa  Spika,  Katika  Mwaka 

2022/2023, Baraza la Ushindani (FCT) litatekeleza malengo yafuatayo: –

i. Kushughulikia mashauri ya rufaa yanayowasilishwa katika Baraza ili kutoa maamuzi ya mashauri 70;

ii. Kuimarisha uwezo wa kutekeleza majukumu ya Baraza ili kuongeza kasi ya usikilizaji wa mashauri yanayowasilishwa katika Baraza ikiwa ni pamoja na: kuboresha mifumo ya Baraza; kutoa mafunzo mbalimbali kwa Watumishi na kuboresha vitendea kazi;

iii. Kufanya utafiti wa kisheria na kiuchumi kuhusu ushindani kwa ajili ya kuongeza ufanisi katika uendeshaji wa mashauri ya Baraza;

iv. Kuongeza uelewa kwa wadau wengi zaidi na jamii kwa ujumla kuhusu shughuli za Baraza na haki katika ushindani wa soko; na

v. Kushughulikia masuala mtambuka.

8.3.9 Chuo Cha Elimu ya Biashara

  1. Mheshimiwa Spika, Katika Mwaka 2022/2023, Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE)kimepanga kutekeleza malengo yafuatayo: –
    i. Kuimarisha na kuendeleza rasilimaliwatu katika hatua za Shahada ya Uzamivu (PhD) na Shahada ya Uzamili (Masters’ Degree);

ii. Kujenga jengo jipya la Vipimo na Viwango katika
Kampasi Kuu ya Dar es Salaam;

iii. Kujenga jengo jipya katika Kampasi ya Dodoma ili kuongeza miundombinu ya kufundishia na kujifunzia;

iv. Kuandaa Mpango Kabambe katika eneo la Nzuguni
Kampasi ya Dodoma;

v. Kumalizia ujenzi wa ukumbi wa mihadhara katika Kampasi ya Mwanza ili kupunguza uhaba wa miundombinu ya kufundishia na kujifunzia;

vi. Kujenga mabweni ya wanafunzi eneo la Iganzo
Kampasi ya Mbeya; na

vii. Kuanza ujenzi wa Kampasi mpya ya Zanzibar.
9 MAOMBI YA FEDHA KWA MWAKA 2022/2023

9.1 Makisio ya Maduhuli kwa Mwaka 2022/2023

260. Mheshimiwa     Spika,  Katika Mwaka 

2022/2023, Wizara inatarajia kukusanya maduhuli ya Shilingi 6,000,000 kutokana na uuzaji wa nyaraka za zabuni na makusanyo mengine.

9.2 Maombi ya Fedha kwa Mwaka 2022/2023

261. Mheshimiwa     Spika,  Katika Mwaka 

2022/2023, Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara inaomba kutengewa jumla ya Shilingi 99,105,506,000 katika Fungu 44. Kati ya fedha hizo, Wizara inaomba kutengewa Shilingi 68,308,687,000 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi 30,796,819,000 za Matumizi ya Maendeleo. Fedha za Matumizi ya Kawaida zinajumuisha Shilingi 8,728,788,000 za Matumizi Mengineyo (OC) na Shilingi 59,579,899,000 za Mishahara. Aidha, Fedha za Matumizi ya Maendeleo zinajumuisha Shilingi 30,346,819,000 fedha za ndani na Shilingi 450,000,000 fedha za nje.
9.3 HITIMISHO

  1. Mheshimiwa Spika, Naomba nichukua fursa hii kuwashukuru tena Watanzania wote na hasa Wazalendo wa Nchi hii kwa kuendelea kutuunga mkono katika jitihada zetu za kuendeleza Sekta ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara. Katika kipindi kilicho mbele yetu, tutaendeleza jitihada za kujenga na kuimarisha misingi thabiti ya uchumi kwa kuvutia wawekezaji na ujenzi wa viwanda kama ilivyobainishwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025. Ni jukumu kubwa ambalo linapaswa kuendelea kuungwa mkono na wapenda maendeleo wote na hasa Watanzania na wazalendo wote. Tunahitaji kila Mtanzania popote alipo kutimiza wajibu wake, kujituma, kubadilisha mtizamo na kuwa mstari wa mbele kulinda na kutetea jitihada na kuendeleza uwekezaji, viwanda na biashara kwa maslahi ya nchi yetu. Inawezekana, tutimize wajibu wetu.
  2. Mheshimiwa Spika, Hotuba hii pia inapatikana katika Tovuti ya Wizara www.mit.go.tz.
  3. Mheshimiwa Spika, Naomba kutoa hoja.

VIAMBATISHO
17

Jedwali Na. 1: Biashara kati ya Tanzania na China kwa Mwaka 2013 – 2021 (Dola za Marekani „000,000‟)

Mwaka
2013
2014
2015
2016
2017
2018
2019
2020
2021
Bidhaa zilizouzwa 307.8 683.9 645.9 355.9 142.3 143.0 233.7 238.9 273.1
Bidhaa zilizoagizwa 1,444.2 1,571.1 2,147.6 1,630.2 1,408.1 1,762.0 1,987.7 1,940.3 2,696.2
Jumla 1,752 2,255 2,793.5 1,986.1 1,550.4 1,905.00 2,221.40 2,179.20 2,969.30
Chanzo: Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA)

Jedwali Na. 2: Biashara kati ya Tanzania na India kwa mwaka 2013-2021 (Dola za Marekani „000,000‟)

Mwaka
2013
2014
2015
2016
2017
2018
2019
2020
2021
Bidhaa zilizouzwa
748.2
1,254.5
1,320.3
706.4
977.6
727.1
867.8
528.7
1,008.7
Bidhaa zilizoagizwa
2,088.2
1,848.6
1,458.3
1,421.6
1,077.6
1,762.0
1,987.7
1,940.3
2,696.2
Jumla 2836.4 3103.1 2778.6 2,128 2,055.2 3,704.90 3,704.90 3,704.90 3,704.90
Chanzo: Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

Jedwali Na. 3: Biashara kati ya Tanzania na Japani kwa mwaka 2013-2021 (Dola za Marekani „000,000‟)

Mwaka 2013 2014 2015 2016 2017 2018 2019 2020 2021
Bidhaa zilizouzwa 220 247.8 263.4 139.2 75.7 66.0 64.2 55.8 67.5
Bidhaa zilizoagizwa 466.7 559.3 458.6 369.2 365.2 398.0 485.2 338.4 469
Jumla 686.7 807.1 722 508.4 440.9 464 549.4 394.2 536.5

Chanzo: Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  

Jedwali Na. 4: Biashara kati ya Tanzania na Jumuiya ya Ulaya kwa mwaka 2013-2021 (Dola za Marekani „000,000‟)

Mwaka
2013
2014
2015
2016
2017
2018
2019
2020
2021

Bidhaa zilizouzwa
898.4
791.7
708.7
236.5
441.4
657.3
725.9
1,475.9
857.1

Bidhaa zilizoagizwa
2,759.4
2,895
1,159.8
557.7
936.1
982.4
1,069.9
1,072.0
1,003.7

Jumla
3,657.8
3,686.7
1,868.5
794.2
1,377.5
1,639.70
1,795.80
2,547.90
1,860.80
Chanzo: Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

Jedwali Na. 5: Biashara ya Bidhaa kati ya Tanzania na Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa mwaka 2013 – 2021 (Dola za Marekani “000,000”)

Mwaka 2013 2014 2015 2016 2017 2018 2019 2020 2021
Bidhaa zilizouzwa
419.1
598.1
1,062.4
437.7
349.6
444.3
674.4
807.9
1,161.2
Bidhaa zilizoagizwa
394.7
706.4
322.8
298.9
220.4
302.8
329.2
324.3
523.4
Jumla 813.8 1,304.5 1,385.2 736.6 570 747.1 1003.6 1132.2 1684.6
Chanzo: Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

Jedwali Na. 6: Biashara kati ya Tanzania na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za
Kusini mwa Afrika (SADC) kwa mwaka 2013 – 2021 (Dola za Marekani „000,000‟)

Mwaka 2013 2014 2015 2016 2017 2018 2019 2020 2021
Bidhaa zilizouzwa
1,243.55
1,235.9
1,357.7
1,017.9
877.8
993.6
1,350.9
1,458.3
1,311.5
Bidhaa zilizoagizwa
835.9
773
771.2
612.4
1,7781.4
604.2
594.0
492.4
232.5
Jumla 2079.45 2008.9 2128.9 1630.3 18659.2 1,597.8 1,944.9 1,950.7 1,544

Chanzo: Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  

Jedwali Na. 7: Mwenendo wa Bei ya Nondo

JIJI/
NONDO 8mm (TZS/PC) NONDO 10mm (TZS/ PC)
NONDO 12mm(TZS/PC)
NONDO 16mm (TZS/PC)

MJI Machi, 2021 Machi, 2022 Badi- liko % Machi, 2021 Machi, 2022 Badi-
liko Machi, 2021 Machi, 2022 Badi- liko % Machi, 2021 Machi, 2022 Badi- liko %
Mtwara 11,750 15,500 31.9 17,000 19,000 11.8 21,500 27,250 26.7 42,500 47,500 11.8
Dar es Salaam
11,500
15,000
30.4
16,000
18,000
12.5
20,500
26,000
26.8
34,000
45,000
32.4
Musoma 11,000 16,000 45.5 15,500 19,000 22.6 21,000 27,000 28.6 34,000 44,000 29.4
Mwanza 15,000 16,500 10.0 16,000 19,000 18.8 19,500 26,500 35.9 35,000 48,000 37.1
Tanga 12,000 15,500 29.2 15,000 18,000 20.0 17,000 26,000 52.9 32,000 45,000 40.6
Arusha 13,500 15,000 11.1 16,000 18,500 15.6 20,000 26,500 32.5 32,000 46,000 43.8
Rukwa 14,000 16,000 14.3 17,000 20,000 17.6 22,000 26,500 20.5 36,000 45,000 25.0
Morogoro 12,000 15,500 29.2 15,500 19,200 23.9 20,000 26,500 32.5 35,000 46,000 31.4
Lindi 10,500 15,500 47.6 14,000 20,000 42.9 22,000 27,500 25.0 39,500 48,000 21.5
Kigoma 12,000 17,000 41.7 15,000 20,000 33.3 19,000 28,000 47.4 37,500 52,000 38.7
Moshi 11,000 15,000 36.4 15,000 18,500 23.3 19,000 27,000 42.1 37,500 46,000 22.7
Bukoba 12,000 17,000 41.7 17,000 20,000 17.6 21,000 27,500 31.0 37,000 48,000 29.7
Songea 13,000 15,500 19.2 16,000 19,000 18.8 21,500 27,000 25.6 36,500 46,000 26.0
Dodoma 11,000 15,500 40.9 17,000 20,000 17.6 21,500 27,000 25.6 36,000 46,000 27.8
Iringa 12,000 1,550 -87.1 15,500 20,000 29.0 20,000 27,000 35.0 35,000 45,000 28.6
Wastani 12,161 15,750 29.5 15,857 19,157 20.8 20,393 26,875 31.8 36,036 46,607 29.3
Chanzo: Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara

Jedwali Na. 8: Mwenendo wa Bei ya Bati

 BATI 32G (TZS/PC)   BATI  30G (TZS/PC)  BATI 28G (TZS/PC) 

JIJI MJI Machi, 2021 Machi, 2022 Badiliko % Machi, 2021 Machi, 2022 Badiliko % Machi, 2021 Machi, 2022 Badiliko %
Mtwara 16,000 16,000 0.0 20,000 28,000 40.0 28,000 37,000 32.1
Dar es Salaam 17,000 17,000 0.0 22,000 27,000 22.7 27,500 35,000 27.3
Musoma 16,000 16,000 0.0 22,000 28,000 27.3 26,000 40,000 53.8
Mwanza 15,000 22,000 46.7 20,000 27,000 35.0 28,000 37,000 32.1
Tanga 16,000 16,000 0.0 20,000 28,000 40.0 26,000 35,000 34.6
Arusha 16,000 22,000 37.5 20,500 28,000 36.6 26,500 37,000 39.6
Rukwa 15,500 15,500 0.0 21,000 28,000 33.3 26,500 40,000 50.9
Morogoro 16,000 21,500 34.4 22,000 28,000 27.3 27,000 37,000 37.0
Lindi 16,000 16,000 0.0 20,000 27,000 35.0 29,500 37,000 25.4
Kigoma 16,000 23,000 43.8 19,000 28,500 50.0 27,500 40,000 45.5
Moshi 16,000 16,000 0.0 20,000 27,000 35.0 27,000 37,000 37.0
Bukoba 17,000 17,000 0.0 21,000 28,000 33.3 28,000 38,000 35.7
Songea 17,000 21,500 26.5 21,500 28,500 32.6 30,000 40,000 33.3
Dodoma 17,000 22,000 29.4 22,000 27,000 22.7 28,000 35,000 25.0
Iringa 16,000 16,000 0.0 22,000 27,500 25.0 27,000 37,000 37.0
Wastani 16,179 18,679 15.5 20,786 27,714 33.3 27,536 37,500 36.2
Chanzo: Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara

Jedwali Na. 9: Mwenendo wa Bei ya Saruji

JIJI/MJI BEI YA MFUKO MMOJA WA SARUJI WA KILO 50 (SH.)
Machi, 2021 Machi, 2022 Badiliko %
Mtwara 15,400 15,500 0.6
Dar es Salaam 15,550 16,000 2.9
Musoma 21,900 22,500 2.7
Mwanza 19,250 19,500 1.3
Tanga 14,000 15,000 7.1
Arusha 17,594 18,000 2.3
Rukwa 20,000 22,000 10.0
Morogoro 15,750 16,750 6.3
Lindi 16,000 16,500 3.1
Kigoma 21,375 22,000 2.9
Moshi 15,333 16,000 4.4
Bukoba 21,375 22,000 2.9
Songea 16,222 17,000 4.8
Dodoma 17,800 18,000 1.1
Iringa 17,375 17,500 0.7
Wastani 17,662 18,283 3.5

Chanzo: Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara

Jedwali Na. 10: Uwezo wa Uzalishaji wa Viwanda vya Saruji

Na.
Jina la Kiwanda
Kiwanda Kilipo
Jina la Bidhaa inayozalishwa Uwezo
Uliosimikwa
(Tani) Tones)
Uwezo wa Uzalishaji
Unaotumika (Tani)

1
Tanzania Portland
Cement Co Ltd
Tegeta- Wazohill Twiga Cement (Twiga Ordinary, Twiga Plus+, and Twiga Extra)

2,000,000

1,400,000

2
Tanga Cement Co. Ltd
Pongwe-Tanga Simba Cement
1,250,000
1,000,000

3
Mbeya Cement Co Ltd Mbeya Vijijini Tembo Cement
400,000
350,000
4
Lake Cement
Kigamboni
(Kimbiji)-DSM
Nyati
Cement
500,000
MT/annum
83% (415,000)

5
Lee Building Materials
Company Limited
Kilwa Masoko

  • Lindi
    Kilwa
    Cement

300,000

240,000

6 ARM Cement Co Ltd/
Maweni
Limestone
Company
Mkuranga – Coast Region
Rhino
Cement

750,000
Around
50% (375,000)

Na.
Jina la Kiwanda
Kiwanda Kilipo
Jina la Bidhaa inayozalishwa Uwezo
Uliosimikwa
(Tani) Tones)
Uwezo wa Uzalishaji
Unaotumika (Tani)

7
Camel Cement Ltd Mbagala – DSM Camel Cement
150,000
150,000
8
Dangote Cement
Industry
Mikindani,
Mtwara
Dangote
Cement
3,000,000
2,250,000

9 Moshi Cement Holili, Kili-
manjaro Moshi Cement
2,100,000
900,000

10 Kisarawe Cement Company Coast Lucky Cement 400 MT/ DAY (120,000) 150 MT/ DAY (45,000)

11
Fortune Cement Co Ltd Mkuranga-
Coast Region Diamond Cement 300 tonnes/ Day (90,000)

12 Chang Jiang Mikindani, Mtwara Mtwara Cement
150,000
100,000

13
Arusha Cement Co Ltd Arusha-
Ngaramtoni Zaidi Cement 500 MT/Day (150,000) 250 tonnes/ day (75,000)

14
Kilimanjaro Cement Co
Tanga
Kilimanjaro Cement
108,000
43,200
JUMLA 10,978,000 7,433,200

Chanzo: Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara

Jedwali Na. 11: Mwenendo wa Bei za Mafuta ya Kula (2019 – 2022)

Bidhaa Machi, 2019 Machi, 2020 Machi, 2021 Machi, 2022
Bei ya
Dunia
($/mt)
Nchini
(Sh./ Ltr) Bei ya
Dunia
($/mt)
Nchini
(Sh./ Ltr) Bei ya
Dunia
($/mt) Nchini
(Sh./ Ltr) Bei ya
Dunia
($/mt) Nchini
(Sh./ Ltr)

Mafuta ya
Alizeti
711.71
4,176.92
730.00
5,216.46
1,611.11
5,512.50
1,491.30
7,625.00
Mafuta asili ya Mawese
573.02
3,359.09
636.25
3,475.00
1,030.48
4,987.50
1,776.96
5,685.71

Chanzo: Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara

12: Mwenendo wa Wastani wa Bei za Mazao Makuu ya Chakula Tanzania Bara (Gunia La Kilo 100)

Bidhaa 2015 2016 2017 2018 2019 2020 2021 2022*
Maharage 159,452 159,306 175,103 165,589 172,170 198,231 176,202 185,786
Uwele 76,609 91,014 107,781 79,056 90,524 109,704 109,598 114,093
Ulezi 111,786 112,546 150,316 140,728 133,203 128,488 151,480 168,354
Viazi Mviringo
76,031
83,174
76,786
77,235
72,647
77,778
68,838
79,742
Mahindi 50,844 63,190 78,059 43,862 65,481 62,849 47,713 62,684
Mchele 161,609 158,059 177,463 169,128 170,049 159,198 141,251 184,348
Mtama 71,635 93,590 100,422 78,632 85,740 103,589 99,304 116,839
Ngano 117,413 124,096 124,736 116,242 124,598 122,293 122,098 149,940
Angalizo: Mwaka 2022* ni kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2022

Chanzo: Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara
13: Mwenendo wa Mchango wa Sekta ya Viwanda katika Pato la Taifa

Mwaka 2015 2016 2017 2018 2019 2020 2021
Asilimia 7.86 7.81 7.67 8.05 8.5 8.4 8.0
Chanzo: Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
Jedwali 14: Ukuaji wa Sekta ya Viwanda
Mwaka 2015 2016 2017 2018 2019 2020 2021
Asilimia 7.1 10.8 8.2 8.3 5.8 4.5 5.1

Chanzo: Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)

Jedwali Na. 15: Idadi ya Ajira katika Sekta ya Viwanda 2013 – 2021

Miaka 2013 2014 2015 2016 2017 2018 2019 2020 2021
Ajira 231,098 242,654 254,786 267,524 280,899 306,180 336,797 370,485 345,615

Chanzo: Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
16: Usajili wa Miradi ya Uwekezaji Katika Kituo cha Uwekezaji Tanzania
kwa Kipindi cha Julai 2021 hadi Machi 2022

Sekta
Idadi ya
Miradi
Miradi ya
Watanzania
Miradi ya Wageni
Miradi ya
Ubia

Ajira
Mtaji
(USD Mil)
% sekta katika Miradi %
sekta
katika
Mtaji
Kilimo 20 7 7 6 2,751 244.0 9.7 13.1
Majengo ya Biashara
17
9
4
4
2,647
302.0
8.3
16.2
Miundombinu 1 0 1 0 10,000 50.5 0.5 2.7
Nishati 1 0 1 0 3 100.0 0.5 5.4
Taasisi za Fedha
2
0
0
0
2,744
72.7
1.0
3.9
Raslimali watu 9 3 0 6 804 15.9 4.4 0.9
Uzalishaji Viwandani
99
28
43
29
12,135
498.0
48.1
26.8
Huduma 15 4 5 6 1,133 65.6 7.3 3.5
Mawasiliano 2 0 2 0 85 177.0 1.0 9.5
Utalii 17 6 6 6 866 55.7 8.3 3.0
Usafirishaji 23 13 3 7 4,283 278.0 11.2 15.0
206 70 72 64 37,451 1,859.4 100.0 100.0
Chanzo: Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC

17: Usajili wa Miradi ya Uwekezaji EPZA Julai 2021 hadi Machi, 2022

Na.

Jina la
Kampuni
Mtaji utakaowekezwa
(USD Milioni) Makadirio ya
Mauzo Nje kwa mwaka (USD
Milioni) 2021
/ 2022

Ajira

Sekta

Hatua iliyofikiwa
Nchi walikotoka
Wawekezaji

  1. Kriishi Green
    Limited
    4.56
    1.2

120
K I L I M O Kuchakata mazao ya jamii ya kunde.

Uendelezaji
unaendelea
India na
China
(Hongkong)

  1. Green Bridge
    Commodities
    Limited

3.4

2.5

90 K I L I M O – K u c h a k a t a mazao ya jamii ya Kunde na
Karanga.

Uendelezaji unaendelea

Tanzania na
India


  1. Coastal Nuts
    Tanzania
    Limited

2.5

4.5

900 KILIMO K u c h a k a t a Korosho
Uendelezaji
(Development)

Tanzania

  1. NB Industries
    Limited
    5.3
    16.5
    30 K I L I M O
    K u t e n g e n e z a
    vifungashio –
    Uendelezaji unaendelea
    India
  2. Diamond
    Foods
    Limited
    0.8
    1.46
    40 K I L I M O
    K u t e n g e n e z a
    vyakula –
    Kimeanza Kazi

India

Na.

Jina la
Kampuni
Mtaji utakaowekezwa
(USD Milioni) Makadirio ya
Mauzo Nje kwa mwaka (USD
Milioni) 2021
/ 2022

Ajira

Sekta

Hatua iliyofikiwa
Nchi walikotoka
Wawekezaji


  1. Tanzania
    Huafeng
    Agriculture
    Development
    Limited

4.56

1.2

120 K I L I M O –
Kuchakata mihogo
(chips) kwa ajili ya chakula na unga wa stachi kwa matumizi ya viwandani

Uendelezaji
unaendelea

China

  1. East Africa zhenyuan Group
    Company Ltd

10

5.5

1000
K I L I M O Kuchakata mazao
ya misitu (mbao)
Uendelezaji unaendelea

China


  1. Apeck Export
    Group
    Limited

3.18

0.9

180 K u c h a k a t a bidhaa za mazao yanayotokana na mikunde kunde
(Pulse)

Uendelezaji
unaendelea

Tanzania,
India na
UAE


  1. Unicarb Minerals
    Limited

2.13

6.4

43 Kuchenjua na kuchakata madini ya Bunyu na
Shaba
Uendelezaji unaendelea
Tanzania na India

  1. Tanite Minerals
    Limited
    1.49
    0.814
    55 Kuchenjua na kuchakata madini
    ya grafiti
    Uendelezaji unaendelea Tanzania,
    India na
    UAE

Na.

Jina la
Kampuni
Mtaji utakaowekezwa
(USD Milioni) Makadirio ya
Mauzo Nje kwa mwaka (USD
Milioni) 2021
/ 2022

Ajira

Sekta

Hatua iliyofikiwa
Nchi walikotoka
Wawekezaji

  1. Polytex Africa
    Limited
    14.5
    40.13
    4500 K u t e n g e n e z a
    Mablanketi na mashuka
    Uendelezaji unaendelea
    Tanzania
  2. Future Agro
    Pro Limited

1.0

1.0

60 K u c h a k a t a korosho, mazao jamii ya kunde na nafaka
Uendelezaji unaendelea

Tanzania

  1. Octavian Mshiu Trust
    Limited
    0.52
    0
    30 K u e n d e l e z a
    Ukanda Maalum wa Kiuchumi
    Uendelezaji unaendelea
    Tanzania
  2. Akofa East
    Africa
    Limited
    8.0
    10.2
    500
    K u c h a k a t a korosho
    Uendelezaji unaendelea
    Tanzania
  3. Tanso
    Investment
    Company
    Limited

0.858

2.75

250
Kuchakata madini
ya Vito
Uendelezaji unaendelea

Tanzania na China
JUMLA 62.8 94.85 7918

Chanzo: Mamlaka ya Maeneo Huru ya Uzalishaji wa Bidhaa kwa ajili ya Mauzo Nje ya Nchi (EPZA)

Jedwali Na. 18: Mchanganuo wa Mikopo Iliyotolewa kupitia Mfuko wa NEDF Kimkoa kwa Kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022

MIKOPO ILIYOTOLEWA WANUFAIKA
Na. MKOA (SHS) JUMLA WANAWAKE WANAUME
1 Dar es Salaam 65,345,138,917.60 429,311 287,590 141,721
2 Mbeya 52,680,428,537.23 346,107 237,666 108,441
3 Iringa 50,493,487,438.39 331,739 229,042 102,697
4 Njombe 49,849,605,700.78 327,511 226,508 101,003
5 Ruvuma 46,763,667,282.63 307,237 214,341 92,896
6 Kilimnanjaro 46,196,715,386.49 303,510 182,105 121,405
7 Arusha 45,592,245,167.28 299,541 179,726 119,815
8 Lindi 39,129,853,001.90 257,084 154,249 102,835
9 Tanga 38,931,818,761.55 255,782 158,469 97,313
10 Mwanza 37,715,726,251.92 247,788 158,675 89,113
11 Manyara 37,309,019,816.59 245,121 147,070 98,051
12 Mtwara 37,132,787,373.11 243,963 146,375 97,588
13 Morogoro 35,943,319,800.80 236,147 146,690 89,457

MIKOPO ILIYOTOLEWA WANUFAIKA
Na. MKOA (SHS) JUMLA WANAWAKE WANAUME
14 Rukwa 34,943,577,444.96 229,575 137,745 91,830
15 Mara 32,121,604,545.35 211,039 126,622 84,417
16 Pwani 29,951,597,026.84 196,781 118,067 78,714
17 Songwe 29,585,278,758.28 194,372 116,626 77,746
18 Shinyanga 27,973,763,858.42 183,785 110,272 73,513
19 Tabora 25,059,415,047.61 164,637 98,785 65,852
20 Dodoma 22,849,364,945.60 150,121 98,048 52,073
21 Singida 22,540,894,311.74 148,093 88,854 59,239
22 Kigoma 20,807,403,542.14 136,701 82,022 54,679
23 Kagera 20,333,473,647.67 133,592 80,155 53,437
24 Katavi 18,706,783,134.56 122,901 73,741 49,160
25 Simiyu 18,300,076,699.22 120,232 72,137 48,095
26 Geita 16,742,953,601.34 109,998 66,001 43,997
Jumla 903,000,000,000.00 5,932,668 3,737,581 2,195,087
Chanzo: Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *