WAZIRI BASHUNGWA AWACHUKULIA HATUA WEKAHAZINA WA HALMASHAURI

OR- TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Innocent Bashungwa amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Vitengo vya Fedha wa Halmashauri (Wekahazina) kwa kuwabadilishia vituo Wakuu wa Vitengo hivyo 109, kuwabadilishi majukumu Wakuu wa Vitengo vya Fedha 16 huku 72 wakiendelea kubaki kwenye Vituo vyao vya awali na 3 wakibaki kwenye vituo vyao vya awali kwa matazamio.

Waziri Bashungwa ameyasema hayo wakati alitoa taarifa ya mapato na matumizi ya Halmashauri kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa Fedha 2021/22.

Taarifa hiyo ameitoa mapema leo Jijini Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *