HOTUBA YA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI MHANDISI HAMAD MASAUNI AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI MWAKA WA FEDHA 2022/2023

HOTUBA YA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI

MHE. MHANDISI HAMAD YUSSUF MASAUNI (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA              

MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA                            

MWAKA 2022/2023

Mhe. Hamad Y. Masauni (Mb.),

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi

Mhe. Jumanne A. Sagini (Mb.),

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi

  Ndugu Christopher D. Kadio                       Ndugu Ramadhan K. Kailima

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo            Naibu Katibu Mkuu Wizara ya           ya Ndani ya Nchi                         Mambo ya Ndani ya Nchi

ORODHA YA VIFUPISHO

ACPAssistant Commissioner of Police 
Cap.Chapter 
CCISClearance Certificate Information System 
CCMChama cha Mapinduzi 
CCTVClosed-Circuit Television
CPCommissioner of Police
DAWASADar es Salaam Water and Sewerage Authority
Dkt.Daktari 
DPADar es Salaam Police Academy 
DPPDirector of Public Prosecution 
DRCDanish Refugee Council
EARPCCO  Eastern Africa Regional Police Chiefs Cooperation
EMLExtra Mural Labour 
EUEuropean Union
GCFGreen Climate Fund
GePGGovernment Electronic Payment Gateway
IOMInternational Organisation for Migration 
JKTJeshi la Kujenga Taifa 
JKUJeshi la Kujenga Uchumi 
Mb.               Mbunge 
MONUSCOUnited Nations Organization Stabilization Mission in the Democratic Republic of Congo
NIDANational Identification Authority 
NINNational Identification Number
NUUKamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama
OPDOutpatient Department 
PGISPolice Gazzette Information System 
POSPoint of Sale
RECSARegional Cooperation for Small Arms
RPCRegional Police Commander 
RSMISRegistration of Societies Management Information System
SACCOSSavings and Credit Co-operative Society
SARSemi-Automatic Rifle
SARPCCOSouthern Africa Regional Police Chiefs Cooperation Organisation
SGRStandard Gauge Railway 
SHIMAShirika la Magereza
SMGSub Machine Gun
TAKUKURUTaasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa 
TAMFITanzania Association of Microfinance Institutions 
TANESCOTanzania Electricity Supply Company Limited
TARITanzania Agriculture Research Institute 
TATCTanzania Automotive Technology Centre 
TAZARATanzania Zambia Railway Authority
TBATanzania Building Agency 
TBSTanzania Bureau of Standards 
TEHAMATeknolojia ya Habari na Mawasiliano
TIRATanzania Insurance Regulatory Authority
UNUnited Nations  
UNDPUnited Nations Development Programme
UNFPAUnited Nations Population Fund
UNHCR United Nations High Commissioner for Refugees
UNICEFUnited Nations Children’s Fund
UNISFAUnited Nations Interim Security Force for Abyei
UNMISSUnited Nations Mission in South Sudan
UVIKO–19Ugonjwa wa Virusi vya Korona–19 
VTSVehicle Tracking System
WFPWorld Food Programme

HOTUBA YA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI MHE. MHANDISI HAMAD YUSSUF MASAUNI (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA                 MWAKA 2022/2023 A. UTANGULIZI

  1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba, Bunge lako sasa lipokee na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Mwaka 2021/2022 na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka 2022/2023. 
  2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia uhai na kuniwezesha kuwasilisha Hotuba hii nikiwa na afya njema. Kwa dhati kabisa, naomba kutumia nafasi hii kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuniamini na kuniteua kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi tangu tarehe 08 Januari, 2022.
  3. Mheshimiwa Spika, pamoja na kumshukuru Mhe. Rais, nampongeza kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya ya kuleta mageuzi makubwa ya maendeleo ya nchi yetu katika maeneo yote ikiwemo masuala ya usalama kwa ujumla wake. Pia, ninamshukuru kwa dhati kwa kutoa kipaumbele katika kushughulikia changamoto za Vyombo vya Usalama zilizodumu kwa muda mrefu ikiwemo masuala ya ajira, upandishwaji vyeo, stahiki, ulipaji wa madeni, ujenzi wa miundombinu na ununuzi wa vitendea kazi.
  4. Mheshimiwa Spika, mbali ya kazi kubwa ya kuzitatua changamoto za vyombo vyetu vya usalama nilizozitaja kwa kipindi kifupi tangu ameingia madarakani, naomba pia nimshukuru Mhe. Rais kwa kuendelea kuleta mapinduzi makubwa ya kibajeti kwenye vyombo vya usalama, kwa kuwezesha ongezeko la fedha kwa mafungu yote yaliyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka 2022/2023. Ni dhahiri kabisa, hali hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha utendaji kazi wa Vyombo vya Usalama na Wizara kwa ujumla wake katika kutoa huduma kwa wananchi.
  5. Mheshimiwa Spika, pongezi zangu pia nazitoa kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdori Mpango, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), kwa kumsaidia Mhe. Rais katika kuliongoza Taifa letu, kutoa ushauri na maelekezo mbalimbali ambayo yamewezesha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kutekeleza wajibu wake kwa ufanisi.
  6. Mheshimiwa Spika, vilevile, nakupongeza wewe binafsi Dkt. Tulia Ackson Mwansasu (Mb.) kwa kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia 100. Aidha, ninampongeza Mhe. Mussa Azan Zungu (Mb.) kwa kuchaguliwa kwa asilimia 98.3 kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Asilimia ya kura za ndiyo mlizozipata ndani ya Bunge hili ni ishara tosha kwamba sisi Wabunge wenzenu tunawaamini, tunawakubali na tupo tayari kufanya kazi ndani ya Bunge kwa usimamizi wenu. HONGERENI SANA.
  7. Mheshimiwa Spika, kwa namna ya kipekee nawapongeza na kuwashukuru Waheshimiwa Wajumbe Makini wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) chini ya uongozi wa Mhe. Vita Rashid Kawawa Mbunge wa Jimbo la Namtumbo akisaidiwa na Makamu Mwenyekiti Mhe. Vincent Paul Mbogo Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kusini. 
  8. Mheshimiwa Spika, Kamati hii imekuwa na msaada mkubwa katika utekelezaji wa kazi na majukumu ya Wizara kupitia maoni, ushauri na maelekezo ambayo imekuwa ikitoa pamoja na ushirikiano wa dhati katika masuala yanayohusu Wizara. Aidha, Kamati imepitia kwa kina bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Mwaka 2022/2023 na kutoa ushauri na mapendekezo ambayo yamesaidia kuboresha bajeti hii na mwelekeo wa Wizara kwa mwaka wa fedha

2022/2023.   

  • Mheshimiwa Spika, tarehe 24 Aprili, 2022 kwa masikitiko makubwa tulimpoteza Mbunge mwenzetu Mhe. Irene Alex Ndyamkama, aliyekuwa mbunge wa viti maalum akiwakilisha Mkoa wa Rukwa. Msiba huu ni pigo kubwa kwetu wote, hivyo naomba nichukue fursa hii kutoa pole kwako Mhe. Spika, Waheshimiwa Wabunge wenzangu wote, familia yake, Chama Cha Mapinduzi pamoja na wananchi wa Mkoa wa Rukwa kwa kuondokewa na mpendwa wetu. Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani, Amina.

B. TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI        KWA      MWAKA       2021/2022    NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2022/2023 Mapitio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2021/2022 

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/2022 Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi iliidhinishiwa bajeti ya jumla ya Shilingi 939,089,045,000. Kati ya fedha hizo Shilingi 521,868,651,000 ni kwa ajili ya Mishahara, Shilingi 389,750,394,000 ni za Matumizi Mengineyo na Shilingi 27,470,000,000 ni za Miradi ya Maendeleo.    
  2. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi, 2022 jumla ya Shilingi 674,519,036,551.66 zilipokelewa na Wizara. Kati ya fedha hizo, Shilingi 382,195,444,973.08 zilikuwa ni za Mishahara, Shilingi 274,300,902,961.37 kwa ajili ya Matumizi Mengineyo na Shilingi 18,022,688,617.21 ni za Miradi ya Maendeleo. Fedha zilizopokelewa ni sawa na asilimia 71.83 ya bajeti yote iliyoidhinishwa na Bunge. 
  3. Mheshimiwa Spika, Wizara pia ilipokea jumla ya Shilingi 55,155,537,101.29 kwa ajili ya kulipa madeni ya watumishi, wakandarasi, wazabuni na watoa huduma. Kati ya fedha hizo, Shilingi 50,611,293,832.21 ni kwa ajili ya Jeshi la Polisi, Shilingi 4,516,792,092.86 Jeshi la Magereza na Shilingi 27,451,176.22 Jeshi la Zimamoto na

Uokoaji. 

Makusanyo ya Maduhuli

13. Mheshimiwa Spika, malengo ya ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali yaliyowekwa kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ni jumla ya Shilingi

374,975,034,000. Kwa kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022 jumla ya Shilingi 195,464,755,316 zilikusanywa sawa na asilimia 78.47 ya lengo la kukusanya Shilingi 249,085,706,938.39. Ukusanyaji wa maduhuli umepungua kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo: baadhi ya ofisi za wilaya za uhamiaji (70) kutokuunganishwa na mfumo wa hati dharura za kielektroniki, kutokuunganishwa na huduma za kimtandao katika ofisi za Jeshi la Zimamoto na Uokoji za wilaya, upungufu na uchakavu wa vifaa vya TEHAMA kwa ajili ya kuunganishwa na mifumo ya kielektroniki ya ukusanyaji maduhuli na upungufu wa magari ya ufuatiliaji wa ukusanyaji maduhuli.

Mafanikio     Yaliyopatikana   katika    Mwaka 2021/2022

  1. Mheshimiwa Spika, kupitia utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya mwaka 2021/2022 Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imepata mafanikio mbalimbali yakiwemo: kukamilika kwa nyumba 119 za maafisa na askari wa Jeshi la Magereza katika maeneo mbalimbali nchini; kukamilika kwa ujenzi wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Singida; kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Wilayani Chamwino – Dodoma; na ukamilishaji wa kituo cha Polisi Daraja C Mtambaswala – Mtwara.
  2. Mheshimiwa Spika, mafanikio mengine ni kukamilika kwa Kiwanda cha Maziwa katika Gereza Kingolwira – Morogoro, kukamilika kwa majengo ya kiwanda cha kuchakata na kupakia chumvi katika Gereza Lilungu – Mtwara, kukamilika kwa ujenzi wa Zahanati ya Polisi Wilaya ya Bariadi; kuanzishwa kwa Kambi ya Mafunzo ya Idara ya Uhamiaji katika eneo la Bomakichakamiba mkoani Tanga na kukamilisha ufungaji wa Mfumo wa Ki-elektroniki wa Usajili na Usimamizi wa Jumuiya (Registration of Societies Management Information System – RSMIS).
  3. Mheshimiwa Spika, Wizara imefanikiwa kununua magari 19 kwa ajili ya kusindikiza misafara ya Viongozi Wakuu wa Kitaifa; kununua magari 25 ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa ajili ya shughuli za utawala na ukaguzi na boti mbili (2) za uokoaji. Aidha, Serikali imelipatia Jeshi la Polisi Helikopta moja (1).
  4. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita Wizara imefanya mabadiliko ya kisheria na kimuundo. Kupitia mabadiliko ya Sheria ya Uhamiaji, Sura 54 Rejeo la mwaka 2016, Idara ya Uhamiaji imeanza kupata stahiki zote kama majeshi mengine yaliyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Sheria ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Sura ya 427 ilifanyiwa marekebisho kwa lengo la kuimarisha utendaji na ufanisi katika kuwahudumia wananchi.

Marekebisho haya yamesaidia kuleta mabadiliko makubwa ikiwemo kuviongezea nguvu na ufanisi vyombo hivyo pamoja kuboresha maslahi kwa watendaji wake.  

  1. Mheshimiwa Spika, Sheria ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu, Sura 432 imefanyiwa marekebisho madogo ambayo yanahusisha utolewaji wa rufaa kwa wahanga ili kuwawezesha kupata huduma muhimu kwa haraka kama matibabu na hifadhi. Aidha, Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu imejumuishwa rasmi katika muundo wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  2. Mheshimiwa Spika, mafanikio mengine nikuajiri askari 6,023; kupandisha vyeo maafisa na askari 34,986; kuwaokoa wahanga 171 wa biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu; na kuwarejesha kwa hiari yao wakimbizi 10,866 nchini Burundi kutokana na kuimarika kwa hali ya usalama katika nchi hiyo.  
  3. Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) chini ya uongozi wa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria kwa dhati kupunguza changamoto ya upungufu wa askari kwa Vyombo vya Usalama vilivyo chini ya Wizara. Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022 jumla ya askari 6,023 wameajiriwa. 
  4. Mheshimiwa Spika, miongoni mwa askari hao 4,103 ni wa Jeshi la Polisi, 700 wa Jeshi la Magereza, 400 wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na 820 ni kwa ajili ya Idara ya Uhamiaji. Kwa sasa askari hao wapo katika mafunzo ya awali kwenye vyuo husika vya kijeshi na watamaliza mafunzo hayo kwa awamu kabla ya Oktoba, 2022. Ajira hizi zitasaidia kuboresha utendaji wa majeshi haya na kuendelea kudumisha amani na usalama nchini. 

MAENEO YALIYOPEWA KIPAUMBELE KATIKA BAJETI YA MWAKA 2022/2023 Mafunzo kwa Askari

  • Mheshimiwa Spika, kwa muda mrefu maafisa na askari wa majeshi yote yaliyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi walikuwa wakichangia gharama wanapohudhuria mafunzo. Hivyo, kuathiri hali za maisha ya familia zao na askari wetu wanapokuwepo mafunzoni. Ninayo furaha kulitangazia Bunge lako kuwa katika mwaka 2022/2023, jumla ya Shilingi 16,603,650,000 zimetengwa kwa ajili ya kugharamia mafunzo ya maafisa, wakaguzi na askari. Kati ya fedha hizo Shilingi 11,648,650,000 ni kwa ajili ya Jeshi la Polisi, Shilingi 3,500,000,000 za Jeshi la Magereza, Shilingi 555,000,000 kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Shilingi 900,000,000 kwa ajili ya Idara ya Uhamiaji.
  • Mheshimiwa Spika, bajeti iliyotengwa kwa mafunzo ya askari, inadhihirisha nia thabiti ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya kuendelea kuboresha maslahi ya askari wetu kwa vitendo. Hivyo, kuanzia sasa ni marufuku kwa afisa, askari ama mkaguzi yoyote wa chombo chochote cha usalama kilichopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kujigharamia kwa kutumia posho yake ya aina yoyote kwa ajili ya mafunzo ya upandishwaji vyeo na utayari ndani ya nchi.  Ununuzi wa Sare za Askari
  • Mheshimiwa Spika, kwa muda mrefu kumekuwa na changamoto ya upungufu wa sare za askari. Mheshimiwa Rais, Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuimaliza changamoto hii kwa askari wetu. Kwa kuanzia jumla ya Shilingi 18,154,000,000 zimetengwa kwenye bajeti ya mwaka 2022/2023 kwa ajili ya ununuzi wa sare. Kati ya fedha hizo Shilingi 11,727,000,000 ni kwa ajili ya Jeshi la Polisi, Shilingi 4,127,000,000 za Jeshi la Magereza, Shilingi 1,000,000,000 kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Shilingi

1,300,000,000 kwa ajili ya Idara ya Uhamiaji.  

  • Mheshimiwa Spika, Natumia fursa hii kuyaelekeza Mashirika ya Uzalishaji Mali ya Jeshi la Polisi na Magereza kuanza mchakato wa kushiriki zabuni kwa ajili ya ununuzi wa sare

za vyombo vyote vya usalama vilivyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ili kutimiza matakwa ya Amiri Jeshi Mkuu ya kuyawezesha mashirika hayo kujiimarisha kiuchumi pamoja na kuhakikisha vyombo vya usalama vinanunua sare zenye ubora, viwango na kwa gharama nafuu.

Mpango Maalumu wa Ujenzi wa Makazi ya

Askari, Vituo na Ofisi

  • Mheshimiwa Spika, itakumbukwa kuwa, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi iliahidi kuandaa Mpango Kabambe wa Ujenzi wa Nyumba za Askari, Ofisi na Vituo kwa Vyombo vya Usalama vilivyo chini yake. Napenda kutoa taarifa kuwa Rasimu ya Mpango husika imekamilika na utekelezaji wake utaanza mwaka 2022/2023 – 2031/2032. Mpango huo wa miaka 10 utahusisha ujenzi wa nyumba 51,780 za askari, ofisi 44 za Makamanda wa Mikoa, ofisi 12 za Wakuu wa Vikosi vya Kutuliza Ghasia, ofisi 135 za Makamanda wa Wilaya, zahanati nane (8) na vituo vya ofisi 582.
  • Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza Mpango huo, kwa mwaka 2022/2023 Jeshi la Polisi litajenga vituo vya polisi 18. Kati ya hivyo, Vituo vya Daraja A ni nane (8), Daraja B vitano (5) na Daraja C vitano

(5). Jeshi la Magereza litajenga magereza sita (6), Jeshi la Zimamoto na Uokoaji litajenga vituo saba (7) na Idara ya Uhamiaji itajenga ofisi tano (5). 

  • Mheshimiwa Spika, vilevile, kupitia bajeti hii jumla ya nyumba 79 za makazi ya familia 216 za maafisa na askari zitajengwa. Kati ya hizo, nyumba 15 ni za Jeshi la Polisi za kuishi familia 51, nyumba 30 za Jeshi la Magereza za kuishi familia 60. Pia, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji litakamilisha ujenzi wa majengo nane (8) ya ghorofa ya kuishi familia za askari 80. Kwa upande wa Idara ya Uhamiaji itanunua nyumba 12 eneo la Msamala – Ruvuma na kujenga nyumba 14. 

Kushirikisha Sekta Binafsi katika Miradi

  • Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza maagizo ya Mhe. Rais na Amiri Jeshi Mkuu ya kuhakikisha Mashirika ya Uzalishaji Mali yanajiendesha kibiashara pamoja na ushirikishwaji wa sekta binafsi kwenye shughuli za uendeshaji wa miradi ya uzalishaji mali, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inaendelea kufanya maboresho (reforms) katika muundo na mfumo wa uendeshaji na usimamizi wa Mashirika ya Uzalishaji Mali ya Jeshi la Polisi na

Magereza. Maboresho hayo ya kimkakati yatasaidia mashirika haya kujiendesha kibiashara; kuimarisha usimamizi wa mapato na matumizi; na kusimamia miradi ikiwemo ya ubia na sekta binafsi. 

Lengo ni kuhakikisha vyombo vya usalama vilivyopo chini ya Wizara vinajielekeza katika majukumu yake ya msingi na mashirika ya uzalishaji mali yanatimiza malengo ya kuundwa kwake.

  • Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Jeshi la Magereza, Maandiko ya Miradi na Hadidu za Rejea za kuwapata washauri elekezi watakaofanya upembuzi yakinifu wa miradi itakayotekelezwa kwa ubia na sekta binafsi zimekamilika. Kwa kuwa Shirika la Magereza limepewa dhamana ya kufanya uzalishaji kibiashara, ndilo litakaloingia ubia na sekta binafsi kwa niaba ya Jeshi la Magereza. Miradi inayopendekezwa kwa upande wa Jeshi la Magereza ni ya kilimo, mifugo, viwanda na uchimbaji madini.

JESHI LA POLISI Hali ya Usalama Nchini

  • Mheshimiwa Spika, amani, utulivu na usalama ni muhimu katika maendeleo ya nchi yetu kiuchumi, kijamii na kisiasa. Kwa kutambua umuhimu huo, Jeshi la Polisi limeendelea kuchukua hatua kubaini, kuzuia na kudhibiti uhalifu wa aina zote ili kuwawezesha wananchi kuendelea kushiriki katika shughuli za kiuchumi na kijamii katika hali ya amani na utulivu.
  • Mheshimiwa Spika, pamoja na kuwepo hali ya amani na utulivu nchini, baadhi ya matukio ya uhalifu yaliendelea kujitokeza kama vile, makosa dhidi ya binadamu, maadili ya jamii na kuwania mali. Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022 makosa makubwa yaliyoripotiwa katika Vituo vya Polisi ni 39,182 ikilinganishwa na makosa 37,250 yaliyoripotiwa katika kipindi kama hicho mwaka 2020/2021. Hili ni ongezeko la makosa 1,932 sawa na asilimia 5.2.  
  • Mheshimiwa Spika, kati ya makosa yaliyoripotiwa, upelelezi wa kesi 15,339 ulikamilika na watuhumiwa 16,514 walifikishwa mahakamani. Kati ya kesi hizo 2,673 zilishinda, kesi 388 zilishindwa na kesi 12,278 zinaendelea kusikilizwa mahakamani. Katika mwaka 2022/2023 Jeshi la Polisi litahakikisha kuwa kesi zote zinapelelezwa kwa haraka ili wahusika waweze kufikishwa mahakamani. Aidha, Jeshi hilo litaendelea kuboresha utendaji kazi wa maafisa, wakaguzi na askari kwa kutoa mafunzo na kutumia vifaa vya kisasa pamoja na kusimamia nidhamu na uwajibikaji ndani ya Jeshi la Polisi. Nitumie nafasi hii kuwasisitiza wananchi kutii sheria bila shuruti na kuzingatia maadili ya jamii
  • Mheshimiwa Spika, ili kuharakisha upelelezi wa kesi, Jeshi la Polisi litaendelea kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashitaka (DPP) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Mamlaka hizo hufanya ufuatiliaji na tathmini ya kesi zilizo chini ya upelelezi katika ofisi husika zenye mahabusu magerezani na zile zinazosubiri vikao vya Mahakama Kuu. Hatua hiyo itasaidia kuharakisha upelelezi na kupunguza msongamano wa mahabusu magerezani. Katika mwaka wa fedha 2022/2023, Wizara kupitia Jeshi la Polisi itaendelea kuimarisha ushirikiano na wadau wa Haki Jinai katika kushughulikia mashauri ya jinai.  Hali ya Usalama Barabarani

  • Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022 jumla ya matukio makubwa ya ajali 1,594 ya usalama barabarani yaliripotiwa katika Vituo vya Polisi ikilinganishwa na matukio 1,228 yaliyoripotiwa katika kipindi kama hicho mwaka wa fedha 2020/2021. Takwimu zinaonesha kuwa matukio 366 ya usalama barabarani yameongezeka sawa na asilimia 29.8. 
  • Mheshimiwa Spika, kati ya matukio hayo ya ajali, 874 yalisababisha watu 1,191 kupoteza maisha na 2,139 kujeruhiwa. Takwimu hizo zimeongezeka ikilinganishwa na matukio 756 ya ajali yaliyosababisha vifo vya watu 999 na majeruhi

1,589 katika kipindi kama hicho mwaka 2020/2021.

Kwa ujumla ajali nyingi kati ya hizo zimesababishwa na madereva kutozingatia sheria za usalama barabarani, ubovu wa magari na miundombinu ya barabara. Aidha, ajali 300 zimesababishwa na madereva wa pikipiki za biashara (bodaboda) kutofuata sheria zinazosimamia matumizi salama ya barabara, hivyo kuongeza ajali za barabarani.

  • Mheshimiwa Spika, Jeshi la Polisi liliwafikisha mahakamani madereva wa magari 852 na madereva wa pikipiki 583 kwa kukiuka sheria za usalama barabarani. Aidha, madereva 141 walifungiwa leseni kwa kipindi maalum na wengine 87 waliosababisha ajali kubwa walifutiwa leseni zao.  
  • Mheshimiwa Spika, sambamba na kusimamia sheria za usalama barabarani, elimu kwa jamii kuhusu matumizi salama ya barabara inaendelea kutolewa. Katika kipindi husika, elimu hiyo ilitolewa kupitia vipindi 477 vya luninga na 2,211 vya redio. Elimu hiyo pia imetolewa kwa wanafunzi 408,021 wa shule za msingi, abiria 196,714 na kwa madereva wa bodaboda 19,792.
  • Mheshimiwa Spika, kutokana na ongezeko la matukio ya ajali, tarehe 30 Machi, 2022 nilitoa maelekezo kwa Jeshi la Polisi kuchukua hatua mahsusi za kudhibiti ajali barabarani. Miongoni wa hatua zilizochukuliwa ni kuanza kwa operesheni maalum na doria nchi nzima ili kudhibiti matukio ya ajali barabarani, kuwachukulia hatua stahiki wamiliki na madereva wa magari ya abiria wasiotumia vifaa vya kufuatilia mwendokasi (VTS) na kusimamia matumizi ya vidhibiti mwendo (speed governor) kwenye mabasi ya abiria. Operesheni hizo zitaendelea katika mwaka 2022/2023 ili kuhakikisha matumizi salama ya barabara na kupunguza ajali.

Operesheni za Kupambana na Uhalifu

  • Mheshimiwa Spika, Jeshi la Polisi limefanya misako, doria na operesheni za kupambana na uhalifu. Mafanikio ya operesheni hizo ni kukamatwa kwa risasi 1,858 na silaha 104 zikiwemo Mark IV moja (1), AK47 nne (4), mabomu ya kutupwa kwa mkono manne (4), rifle sita (6), shortgun 10, bastola 11 na magobore 68. Jumla ya watuhumiwa 117 walikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa makosa ya kupatikana na risasi pamoja na silaha na kesi zao zinaendelea. 
  • Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022 jumla ya silaha haramu 5,230 ziliteketezwa kwa moto. Silaha hizo zilikuwa zinamilikiwa na majangili pamoja na baadhi ya wananchi. Silaha zilizoteketezwa ni pamoja na magobore 3,724, shotgun 789, rifles 573, AK47 111, bastola 20, mabomu saba (7), SAR tano (5) na G3 moja (1). 
  • Spika, Serikali ilitoa Tangazo Na.

474 la mwaka 2021 ambalo liliwataka wananchi kusalimisha silaha kwa hiari. Kupitia tangazo hilo, jumla ya silaha 228 zilizokuwa zinamilikiwa na wananchi kinyume na sheria zilisalimishwa. Silaha zilizosalimishwa ni pamoja na  magobore 174, shotgun 38, rifle 10, bastola tano (5) na AK47 moja

(1). 

  • Mheshimiwa Spika, katika kudhibiti umiliki wa silaha kinyume cha sheria, Jeshi la Polisi limeweka alama silaha 221 zikiwemo bastola 182, shotguns 20, rifles 18 na airgun moja (1). Aidha, silaha 183 zilisajiliwa zikiwemo bastola 121, shotguns 50 na rifle 12. Vilevile, Jeshi limefuta vibali vya wamiliki wanne kutokana na matumizi mabaya ya silaha. Katika mwaka 2022/2023, Jeshi la Polisi litaendelea kutoa vibali vya kumiliki silaha kwa waombaji wenye sifa na kufuta vibali kwa wamiliki watakaozitumia vibaya. Aidha, ninasisitiza wamiliki wa silaha kulipa ada za umiliki wa silaha kwa wakati na kuwa waangalifu katika kuhifadhi na kutumia silaha wanazomiliki kihalali.
  • Mheshimiwa Spika, ushirikiano wa Jeshi la Polisi na Mamlaka nyingine za Serikali katika kufanya operesheni ulifanikisha kukamata Nyara za Serikali 1,190 zenye uzito wa kilo 10,310 na gramu 423 zikiwa na thamani ya Shilingi 3,920,554,596.

Watuhumiwa 699 (wanaume 657 na wanawake 42) walifikishwa mahakamani na kesi zao zinaendelea. 

  • Mheshimiwa Spika, operesheni za kuzuia wizi wa mifugo, doria na ukaguzi wa minada na machinjio ya mifugo zimefanyika katika mikoa mbalimbali nchini, ambapo ng’ombe 986, mbuzi 539, kondoo 90 na punda 20 walioibwa walipatikana. Watuhumiwa 97 wa wizi wa mifugo hiyo walikamatwa na kufikishwa mahakamani. 
  • Mheshimiwa Spika, operesheni za kudhibiti uvuvi haramu, uporaji, magendo na bidhaa bandia zimefanyika katika Ziwa Victoria, Nyasa, Tanganyika na mwambao wa Bahari ya Hindi. Katika operesheni hizo watuhumiwa 135 walikamatwa wakiwa na bidhaa mbalimbali zikiwemo injini za boti 58, mitumbwi isiyosajiliwa 14, samaki wachanga kilo 313, nyavu haramu 892, makokoro 203. Aidha, watuhumiwa nane (8) waliokutwa na bidhaa 4,741 zikiwa na nembo bandia za makampuni tofauti zenye thamani ya Shilingi 58,937,200 walikamatwa. 
  • Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Jeshi litaendeleza operesheni za pamoja kwa lengo la kudhibiti wizi wa Nyara za Serikali na mifugo, biashara ya dawa za kulevya, uvuvi haramu, uporaji, magendo na bidhaa bandia.
  • Spika, katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022 Serikali imelipa fidia ya Shilingi 1,000,782,500 kwa askari walioumia na kwa familia za askari waliopoteza maisha wakati wakitekeleza majukumu yao. Kati ya fedha hizo, Shilingi 685,782,500 zimelipwa kwa askari 171 walioumia na Shilingi 315,000,000 zimelipwa kwa wasimamizi wa mirathi kwa familia za askari 21 waliopoteza maisha. Mwenyezi Mungu azipumzishe roho za mashujaa wetu mahali pema peponi, Amina.  

Kushiriki katika Kuimarisha Ulinzi wa Amani Kikanda na Kimataifa

  • Mheshimiwa Spika, Jeshi la Polisi ni mwanachama wa Jumuiya ya Wakuu wa Polisi

Kanda ya Afrika Mashariki (Eastern Africa Regional Police Chiefs Cooperation – EARPCCO) na Jumuiya ya Wakuu wa Polisi Kanda ya Kusini mwa Afrika (Southern Africa Regional Police Chiefs Cooperation Organisation – SARPCCO). Ushirikiano huo umesaidia kuongeza wigo wa kuzuia, kudhibiti na kupambana na makosa yanayovuka mipaka.

  • Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza makubaliano ya kikanda na kimataifa ya ulinzi wa amani wa pamoja, watendaji 42 wa Jeshi la Polisi wanaendelea kushiriki katika ulinzi wa amani kwenye nchi mbalimbali. Watendaji 25 wapo Sudani Kusini (United Nations Mission in South Sudan – UNMISS); wawili (2) Sudani – Abyei (United Nations Interim Security Force for Abyei – UNISFA) na12 wapo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (United Nations Organization Stabilization Mission in the Democratic Republic of Congo – MONUSCO). Pia, Maafisa watatu (3) wanafanya kazi kwa muda maalum (Secondment) katika Ofisi za Umoja wa Mataifa, wawili (2) nchini Sudani – Abyei na mmoja (1) yupo Ethiopia. Ushiriki huo unawezesha watendaji hao kupata uzoefu na mbinu za kisasa za ulinzi wa amani.

Ajira, Mafunzo na Upandishwaji Vyeo katika Jeshi la Polisi

  • Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na changamoto ya upungufu wa askari, Serikali ilitoa kibali kwa Jeshi la Polisi kuajiri askari wapya 4,103 waliomaliza kidato cha nne, kidato cha sita, stashahada na shahada waliopitia mafunzo ya

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU). Askari haowanaendelea na mafunzo ya awali yaliyoanza tarehe 01 Desemba, 2021 katika Shule ya Polisi Moshi. Katika mwaka 2022/2023, Jeshi la Polisi linatarajia kuajiri askari wapya 3,000 na watumishi raia 220.

  • Spika, katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022 jumla ya watumishi 23,453 walipata mafunzo ya fani mbalimbali.  Kati ya hao, watendaji 22,752 walipata mafunzo ya upandishwaji vyeo kupitia Vyuo vya Polisi na Shule ya Polisi Moshi, 472 wanaendelea na masomo ya Astashahada ya Sheria, Astashahada ya Upelelezi, Astashahada ya Mawasiliano ya Polisi, Stashahada ya Upelelezi na Stashahada ya Polisi Sayansi kupitia vyuo vya Jeshi la Polisi. 
  • Mheshimiwa Spika, watendaji 229 walipata mafunzo ambapo 204 wanasoma fani mbalimbali nje ya Vyuo vya Polisi, 10 walipata mafunzo nje ya nchi na watumishi raia 15 walipata mafunzo ndani ya nchi. Katika mwaka 2022/2023 Jeshi la Polisi litaendelea kuwapatia mafunzo ya kuwajengea uwezo kiutendaji watumishi wake. Mafunzo hayo yatawawezesha kukabiliana na uhalifu wa aina zote. 
  • Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi, 2022 maafisa, wakaguzi na askari 24,151 wamepandishwa vyeo. Mapendekezo ya upandishwaji yamezingatia uwepo wa nafasi, bajeti, utendaji wa ziada wa mtu binafsi, uzoefu na elimu kama kigezo cha ziada. Watendaji waliopandishwa vyeo ni kama ifuatavyo: Makamishna Wasaidizi 118, Warakibu Waandamizi 120, Warakibu 258, Warakibu Wasaidizi 749, Wakaguzi 904, Wakaguzi Wasaidizi 3,984, Sajini Meja 41, Stesheni Sajini 610, Sajini 5,824 na Koplo 11,543. 
  • Mheshimiwa Spika, watendaji hao walipandishwa vyeo baada ya kuhitimu mafunzo ya upandishwaji vyeo kutoka Vyuo vya Polisi na Shule ya Polisi Moshi. Pia, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan alimpandisha cheo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Awadhi Juma Awadhi kuwa Kamishna wa Polisi (CP) na kumteua kuwa Kamishna wa

Polisi Zanzibar.

Upatikanaji wa Vitendea Kazi

  • Mheshimiwa Spika, ili Jeshi la Polisi liweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi linahitaji vitendea kazi vya kisasa na vya kutosha. Taratibu za ununuzi wa magari 25 ya kusindikiza misafara ya Viongozi Wakuu wa Serikali na Viongozi Wakuu Waandamizi zimekamilika. Magari hayo yamenunuliwa kwa gharama ya Shilingi

5,717,242,846.88 zilizotolewa na Serikali mwaka 2021/2022. Magari 19 yamepokelewa na yanatumika na magari sita (6) yatapokelewa Oktoba, 2022. 

  • Mheshimiwa Spika, vilevile, Jeshi limepata msaada wa magari 16 na pikipiki 32 kutoka kwa wadau. Magari mawili (2) yametolewa na Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi, 14 Mgodi wa Dhahabu wa

North Mara, pikipiki 10 zimetolewa na United Nations Population Fund (UNFPA) na pikipiki 22 zimetolewa na Tanzania Insurance Regulatory

Authority (TIRA). 

  • Mheshimiwa Spika, Jeshi la Polisi linatarajia kupokea magari 369 ifikapo Septemba, 2022 ikiwa ni utekelezaji wa mkataba kati ya Serikali na Kampuni ya Ashok Leyland ya nchini India. Magari 78 yanatarajiwa kupokelewa mwezi Mei, 2022. Magari hayo yatakapofika yatapelekwa katika Vituo vya Polisi vyenye uhitaji mkubwa.  
  • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/2022, Serikali imeliongezea Jeshi la Polisi jumla ya Shilingi 10,481,856,816.25 nje ya bajeti ya Matumizi Mengineyo. Kati ya fedha hizo, Shilingi 2,075,730,790.25 zimetumika kulipa wastaafu 1,372 kwa ajili ya kusafirisha mizigo. Shilingi 7,693,791,026 zimetumika kugharamia mafunzo kwa askari wapya 4,103 na Shilingi 470,662,500 zimetumika kulipa stahiki za maafisa, wakaguzi na askari 128 waliopo kwenye operesheni maalum. 
  • Mheshimiwa Spika, Shilingi 102,380,000 zimetumika kwa ajili ya upembuzi yakinifu wa mradi wa ukaguzi wa magari na miji salama, Shilingi 83,000,000 kwa ajili ya maandalizi ya sherehe ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara na Shilingi 56,292,500 kwa ajili ya gwaride la sherehe ya miaka 58 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Miradi ya Ujenzi wa Makazi, Vituo vya Polisi na Ofisi

  • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/2022 Wizara imekamilisha ujenzi na ukarabati wa vituo vifuatavyo: Kituo cha Polisi Daraja “B’’ Mkokotoni – Zanzibar kwa gharama ya Shilingi 340,106,750; Kituo cha Polisi Daraja “C’’ na nyumba ya kuishi

Mkuu wa Kituo katika eneo la uwanja wa ndege

                Jijini     Dodoma     kwa     gharama     ya     Shilingi

115,000,000; Kituo cha Polisi Daraja “C’’ Mbande Wilaya ya Kongwa; na ukarabati wa Ofisi ya Kamanda wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia – Dar es Salaam kwa gharama ya Shilingi 93,973,600. 

  • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/2022 Jeshi la Polisi lilitengewa jumla ya Shilingi 2,000,000,000 kutekeleza miradi nane (8) ya maendeleo. Hadi kufikia Machi, 2022 Jeshi la Polisi limepokea Shilingi 1,850,000,000 za kutekeleza miradi ifuatayo: Shilingi 200,000,000 kwa ajili ya kukamilisha mradi wa ujenzi wa nyumba 14 za makazi ya Askari – Kusini Pemba ambao umefikia asilimia 80; Shilingi 150,000,000 kwa ajili ya kukamilisha mradi wa ujenzi wa nyumba 12 za makazi ya Askari – Kaskazini Pemba na umefikia asilimia 75; naShilingi 450,000,000 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa jengo la Ofisi ya Kamanda wa Polisi – Mara umefikia asilimia 60.
  • Mheshimiwa Spika, miradi mingine inayoendelea kutekelezwa kupitia fedha hizo na mchanganuo wake ni kama ifuatavyo: Shilingi 250,000,000 kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Polisi Daraja “A” Lushoto – Tanga na umefikia asilimia 40; Shilingi 300,000,000 ujenzi wa Kituo cha Polisi Daraja “C” Ludewa – Njombe; Shilingi 220,000,000 kukarabati Jengo la Ofisi ya Kikosi cha Polisi Anga – Dar es Salaam kwa kutumia Mkandarasi Aluminium Africa; na Shilingi 280,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za makazi ya Askari Ludewa – Njombe. 
  • Mheshimiwa Spika, Jeshi la Polisi linatarajia kupokea Shilingi 150,000,000 kabla ya Juni, 2022. Kati ya fedha hizo, Shilingi 70,000,000 zitatumika kumalizia ujenzi wa nyumba sita (6) za makazi ya Askari Wilaya ya Ludewa na Shilingi 80,000,000 kuanza ujenzi wa Kituo cha Polisi Daraja “C” Nyakanazi mkoani Kagera. 

Miradi inayotekelezwa kupitia Mfuko wa Tuzo na Tozo wa Jeshi la Polisi

  • Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Jeshi la Polisi pia imeendelea kutekeleza miradi ya ujenzi kwa kutumia fedha za Mfuko wa Tuzo na Tozo. Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa Kituo cha Polisi Daraja “A’’ Wanging’ombe – Njombe ambapo Shilingi 948,384,951 zimetolewa na ujenzi umefikia asilimia 60, ujenzi wa Kituo cha PolisiDaraja “C” Chang’ombe – Dodoma Shilingi 176,000,000 umefikia asilimia 42, ujenzi wa jengo la Polisi Afya Kuu – Dar es Salaam awamu ya kwanza ghorofa mbili (2) kwa gharama ya Shilingi 800,000,000 upo katika hatua ya msingi, ujenzi wa madarasa katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA) kwa gharama ya Shilingi 698,285,000 umefikia asilimia 60. Ujenzi wa Jengo la ghorofa nne (4) kwa ajili ya mabweni katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam kwa gharama ya Shilingi 777,025,000 umefikia asilimia 70.
  • Mheshimiwa Spika, miradi mingine iliyotekelezwa kwa kutumia Mfuko wa Tuzo na Tozo ni ujenzi wa jengo la Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) wa Katavi, ambapo Shilingi 800,000,000 zimetolewa na upo asilimia 30; ujenzi wa jengo la Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe zimetolewa Shilingi 800,000,000 na umefikia asilimia 40, mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara zimetolewa Shilingi 800,000,000 na umefikia asilimia 50; mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya umepewa Shilingi 1,564,953,000 upo asilimia 70 na ujenzi wa nyumba 3 za kuishi Makamishna wa Jeshi la Polisi

– Jijini Dodoma zimetolewa Shilingi 1,050,000,000 na umefikia asilimia 40. 

  • Mheshimiwa Spika, ujenzi wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja na Mkoa wa Kaskazini Unguja umeanza.  Kiasi cha Shilingi 1,650,724,400 kimetolewa mwezi Januari, 2022 kwa kila ofisi.Aidha, ujenzi wa nyumba ya makazi ya Kamanda ya Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba umeanza na kiasi cha Shilingi 266,465,544 kimetolewa mwezi Machi, 2022.

Miradi inayotekelezwa kutoka Vyanzo Vingine

  • Mheshimiwa Spika, Jeshi la Polisi linatekeleza ujenzi wa majengo mawili (2) ya ghorofa nne (4) kwa ajili ya mabweni katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam. Gharama za ujenzi huo ni Shilingi 1,000,000,000 na umefikia asilimia 70.

Vilevile, ujenzi wa Kituo cha Polisi Daraja “A’’

Gezaulole Kigamboni – Dar es Salaam unaokadiriwa kugharimu Shilingi 899,481,533 umefikia asilimia 50. Miradi hii miwili inatekelezwa kwa fedha zilizotolewa na Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli. 

  • Mheshimiwa Spika, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.) aliweka Jiwe la msingi la ujenzi wa Kituo cha Polisi Daraja “A’’ katika Mji wa Serikali Mtumba Dodoma tarehe 02 Desemba, 2021. Kituo hicho kitagharimu Shilingi 948,384,951

na kinatarajiwa kukamilika Juni, 2022. Fedha za mradi huo zinaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu na ujenzi umefikia asilimia 65

  • Mheshimiwa Spika, wananchi na wadau wengine wamekuwa wakijitokeza kusaidia juhudi za Serikali katika ujenzi wa vituo vya polisi na makazi ya askari. Miradi inayoendelea kutekelezwa kwa fedha zilizotolewa na wadau hao ni: ujenzi wa Kituo cha

Polisi Daraja “B’’ Ruangwa – Lindi ambao umefikia asilimia 60 ambapo Shilingi 302,000,000 zimetolewa; ujenzi wa Kituo cha Polisi Daraja “B’’ Chemba – Dodoma umefikia asilimia 32 kwa kutumia Shilingi 170,000,000; na ujenzi wa Kituo cha Polisi Daraja “B’’ Siha – Kilimanjaro umefikia asilimia 60 ambapo Shilingi 190,000,000 zimetolewa.

  • Mheshimiwa Spika, miradi mingine iliyotekelezwa kwa michango ya wadau ni: ujenzi wa Kituo cha Polisi Daraja “C’’ Kizimkazi – Kusini Unguja pamoja na nyumba ya makazi ya familia mbili kwa gharama ya Shilingi 198,934,750 ambao umefikia asilimia 80; na ujenzi wa Kituo cha Polisi Daraja “C’’ Chang’ombe – Dodoma umefikia asilimia 42 na hadi sasaShilingi 176,000,000 zimetolewa. 
  • Mheshimiwa Spika, Jeshi limepokea Shilingi 207,404,000 kutoka UNICEF nje ya bajeti ya Maendeleo kwa ajili ya kutekeleza mradi wa Mpango   wa Ulinzi       wa Haki za Mtoto na

Ushirikishwaji Jamii. Kazi zitakazofanyika ni kupitia upya mitaala ya kufundishia udhibiti wa uhalifu mtandao, makosa ya ukatili wa kijinsia na watoto, kutoa mafunzo kwa wakufunzi wa udhibiti wa uhalifu wa mtandao na kupitia mitaala ya Vyuo vya Polisi ili kujumuisha masuala yanayohusu ulinzi wa haki za wanawake na watoto. 

Miradi ya Kipaumbele ya Jeshi la Polisi katika Mwaka 2022/2023

  • Mheshimiwa Spika, Serikali imedhamiria kuongeza kasi ya ujenzi wa Vituo vya Polisi na makazi ya askari, ambapo katika mwaka 2022/2023 imetenga Shilingi 12,500,000,000. Fedha hizo zitatekeleza miradi ya kipaumbele ifuatayo: kukamilisha ujenzi wa jengo la ghorofa tatu la kuishi familia 12 za askari, Buyekera Mkoa wa Kagera kwa gharama ya Shilingi 1,700,000,000; kukamilisha ujenzi wa majengo ya Vituo vya Polisi Daraja “A” Mkalama kwa Shilingi 967,148,000 na Ikungi kwa Shilingi 1,107,875,000 vilivyopo Mkoa wa Singida; kukamilisha ujenzi wa Vituo vya Polisi Daraja “B” Mkuranga Mkoa wa Kipolisi Rufiji kwa

Shilingi 400,000,000, Bariadi Mkoa wa Simiyu kwa Shilingi 320,000,000 na Ruangwa mkoani Lindi kwa Shilingi 140,000,000. 

  • Spika, miradi mingine ni kuanza ujenzi wa jengo la Ofisi ya Kamanda wa Polisi

                Mkoa     wa     Mtwara     utakaogharimu      Shilingi

1,300,000,000; ujenzi wa Vituo vya Polisi Daraja

“B” Sikonge mkoani Tabora Shilingi 700,000,000; Namtumbo mkoani Ruvuma Shilingi 700,000,000; na Shilingi 600,000,000 kwa ajili ya kulipia fidia ya ardhi maeneo mbalimbali yanayomilikiwa na Jeshi la Polisi. 

  • Mheshimiwa Spika, Jeshi pia litafanya ununuzi wa vifaa vya uendeshaji wa Maabara ya Uchunguzi wa Sayansi ya Jinai kwa Shilingi 700,196,450, kuanzisha mfumo wa hati ya tabia njema na Gazeti la Polisi la Kidijitali kwa ajili ya utoaji taarifa za Polisi kwa Umma, ambapo Shilingi 160,000,000 zimetengwa. Vilevile, Shilingi 750,000,000 zimetengwa kwa ajili ya kuanza awamu ya kwanza ya ujenzi wa ofisi ya TEHAMA Makao Makuu ya Polisi Dodoma na Shilingi 328,950,000 zitatumika kuboresha mifumo ya TEHAMA inayounganisha Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na Mikoa, Vikosi, Vitengo na Vituo vya Polisi. 
  • Mheshimiwa Spika, Jeshi litaanzisha mfumo wa pamoja wa ukusanyaji wa taarifa za Intelijensia na upelelezi ambapo Shilingi 122,500,000 zimetengwa. Aidha, Shilingi 63,300,000 zitatumika kuanzisha Mfumo wa Kielektroniki wa Malipo ya Mfuko wa Tuzo na Tozo.
  • Spika, miradi mingine ya kipaumbele kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ni pamoja na: kumalizia ujenzi wa Kituo cha Polisi Daraja “C” Maungani Kombeni Mjini Unguja – Zanzibar kwa gharama ya Shilingi 60,000,000; kuanza  awamu ya pili ya ujenzi wa majengo saba (7) ya familia 14 za makazi ya Askari Mfikiwa Kusini Pemba – Zanzibar ambapo Shilingi 350,000,000 zitatumika; kuanza awamu ya pili ya ujenzi wa majengo matatu (3) ya familia 12 za Makazi ya Askari Finya Kaskazini  Pemba – Zanzibar Shilingi 200,000,000; na kiasi cha Shilingi 48,000,000 kitatumika kumalizia ujenzi wa Kituo cha Polisi Daraja  “C”  Dunga Mitini Kusini Unguja – Zanzibar. 
  • Mheshimiwa Spika, bajeti ya maendeleo kwa mwaka 2022/2022 pia itahusisha ukarabati katika maeneo yafuatayo: jengo la ghorofa la makazi ya Askari la Kilimanjaro Ziwani Magharibi Unguja – Zanzibar Shilingi 60,000,000; jengo la ghorofa la makazi ya Askari Kilimanjaro Wete Kaskazini Pemba – Zanzibar gharama ya Shilingi 100,000,000; bweni eneo la Bububu Mjini Magharibi – Zanzibar Shilingi 47,976,000; nyumba za makazi ya Askari eneo la Mwera Unguja Magharibi Shilingi 105,000,000 na jengo la Makao Makuu ya Polisi Zanzibar Mjini Magharibi ambapo Shilingi 40,753,800 zitatumika. 
  • Spika, katika mwaka 2022/2023

Jeshi la Polisi litaendelea kutekeleza miradi ya kipaumbele kwa kumalizia ujenzi wa Kituo cha Polisi Chukwani Mjini Magharibi – Zanzibar kwa kiasi cha Shilingi 60,000,000, ujenzi wa Hanga la kuishi Askari la Mkokotoni Kaskazini Unguja kwa Shilingi 130,103,000, ujenzi wa ukumbi wa mikutano katika Chuo cha Polisi Mjini Magharibi Zanzibar Shilingi 40,000,000, kuanza ujenzi wa

Kituo cha Polisi Daraja “ B’’ Makunduchi Kusini Unguja Shilingi 110,000,000 na kukarabati Kituo cha Polisi Malindi kilichopo Mji Mkongwe Mjini Magharibi – Zanzibar Shilingi 126,887,750. 

  • Mheshimiwa Spika, Maafisa wa Polisi Kata na Shehia watajengewa uwezo katika kutekeleza muundo wa ushirikishwaji wa jamii kwa gharama ya Shilingi 117,670,000. Pia, Shilingi 78,000,000 zimetengwa kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa Maafisa wa Polisi Kitengo cha Habari ili kuboresha utoaji wa taarifa za kazi za Polisi, kutoa mafunzo kwa Maafisa wa Polisi Dawati la Ukatili wa Jinsia na Watoto kwa kiasi cha Shilingi 115,640,000. Aidha,

Washirika wa Maendeleo EU na UNICEF wameahidi kutoa Shilingi 500,000,000 kwa ajili ya kuimarisha Dawati la Jinsia na Watoto Tanzania.

Nishani kwa Maafisa na Askari wa Jeshi la Polisi

81. Mheshimiwa Spika, watendaji 123 walitunukiwa nishani na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kati ya hao, watano (5) walitunukiwa nishani ya miaka 60 ya uhuru, 58 nishani ya utumishi uliotukuka na 60 nishani ya utumishi wa muda mrefu na tabia njema. Katika mwaka 2022/2023, Jeshi la Polisi litaendelea kusimamia nidhamu kwa watendaji wake ili waendelee kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi mkubwa.

SHIRIKA LA UZALISHAJI MALI LA JESHI LA POLISI

  • Mheshimiwa Spika, Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi limetoa mafunzo ya kuzuia na kupambana na uhalifu wa kimtandao na utakatishaji fedha. Mafunzo hayo yametolewa kwa watumishi 188 wa taasisi za umma na binafsi. Aidha, Shirika limeingia makubaliano na Shirikisho la Watoa

Huduma Wadogo wa Fedha Tanzania (Tanzania

Association of Microfinance Institutions – TAMFI) ili kuwajengea uwezo wa kukabiliana na matukio ya wizi wa kimtandao na utakatishaji fedha. Pia, Shirika limetoa mafunzo ya umahiri wa matumizi ya silaha za moto kwa wamiliki na watumiaji wa silaha 1,004. Kupitia mafunzo hayo, jumla ya Shilingi 179,410,000 zilikusanywa.  

  • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2022/2023 Shirika litaendelea kutoa mafunzo kwa mujibu wa Sheria ya Udhibiti wa Silaha za Moto Na. 2 ya 2015. Nitumie fursa hii kuzitaka taasisi, kampuni za ulinzi na wamiliki binafsi wa silaha za moto kuhudhuria mafunzo yanayoendelea nchini. Hatua za kisheria zitachukuliwa kwa watakaokiuka taratibu za umiliki wa silaha.
  • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2022/2023

Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi litaanza miradi mengine itakayotekelezwa kwa njia ya ubia na sekta binafsi. Miradi hiyo ni pamoja na Ukaguzi wa Vyombo vya Moto wa Lazima (Mandatory Vehicle Inspection) kwa vyombo vyote nchini kwa mujibu wa sheria ili kukabiliana na ajali za barabarani na Mradi wa Miji salama ‘safer cities’ wa kuimarisha usalama kwa kutumia teknolojia kupitia mifumo ya kamera zitakazofungwa maeneo mbalimbali. Upembuzi yakinifu wa miradi hii utakamilika mwezi Juni, 2022 na utekelezaji wa miradi utaanza mwaka 2022/2023.

  • Mheshimiwa Spika, kupitia fursa hizi za Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi, Serikali itaweza kujiongezea mapato kwa kiwango kikubwa yatakayosaidia kumaliza changamoto nyingi za Jeshi la Polisi. Changamoto hizo ni pamoja na makazi ya askari, ununuzi vifaa na zana za kisasa za kufanyia kazi, vyombo vya usafiri na ofisi ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na Waheshimiwa Wabunge na wananchi kwa ujumla. Aidha, ni matarajio yetu kuwa miradi hii itakapoanza itawezesha Shirika lijiendeshe kibiashara na kusaidia kuimarisha hali ya usalama nchini.

JESHI LA MAGEREZA Hali ya Ulinzi na Usalama Magerezani

86. Mheshimiwa Spika, hali ya ulinzi na usalama katika magereza yote nchini ni salama na tulivu. Jeshi la Magereza limeendelea kuwapokea, kuwahifadhi na kuwapatia huduma muhimu wahalifu wanaopelekwa magerezani kwa mujibu wa sheria. Hadi kufikia Machi, 2022 jumla ya wafungwa na mahabusu 32,671 walikuwepo katika magereza yote nchini sawa na asilimia 9.2 zaidi ya uwezo wa magereza wa kuwahifadhi wafungwa na mahabusu 29,902. Kati ya wafungwa hao, 16,883 wamehukumiwa kutumikia adhabu mbalimbali gerezani na 15,788 ni mahabusu ambao wanaendelea kusikiliza kesi zao mahakamani.

Hatua za Kupunguza Msongamano Magerezani

  • Mheshimiwa Spika, katika jitihada za kupunguza msongamano wa wafungwa magerezani, Serikali inatumia utaratibu wa kifungo cha nje (EML), parole, huduma kwa jamii na huduma za uangalizi kutoa wafungwa wenye viashiria vya kurekebika tabia. Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022 jumla ya wafungwa 4,106 walitolewa magerezani. Kati ya hao, wafungwa 955 walitolewa kwa utaratibu wa kifungo cha nje na wafungwa 3,151 walihukumiwa kutumikia adhabu chini ya programu ya huduma kwa jamii na huduma za uangalizi. Kwa upande wa parole, hakuna wafungwa walionufaika kwa kipindi hicho kutokana na bodi za mikoa kumaliza muda wake. Bodi hizo zimezinduliwa mwezi Machi, 2022.
  • Mheshimiwa Spika, wafungwa 9,530 walinufaika na Msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa

Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu

Hassan. Kati ya hao, wafungwa 5,704 walisamehewa siku ya Maadhimisho ya Sherehe za Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika tarehe 9 Desemba, 2021 na wafungwa 3,826 walisamehewa siku ya maadhimisho ya miaka 58 ya Muungano wa Tanzania yaliyofanyika tarehe 26 Aprili, 2022.

  • Mheshimiwa Spika, hatua nyingine iliyochukuliwa na Wizara katika kupunguza msongamano wa wafungwa ni ujenzi wa magereza katika baadhi ya wilaya. Ujenzi wa Gereza la Wilaya la Kilosa upo hatua ya msingi na Gereza Karatu ujenzi wake umefikia kwenye lenta. Kiasi cha Shilingi 702,000,000 kimetumika katika ujenzi huo.
  • Mheshimiwa Spika, Jeshi la Magereza pia limefanya ukarabati wa mabweni 12 ya wafungwa, ujenzi wa jengo la utawala na ukuta wa ngome ya Gereza Mkono wa Mara mkoani Morogoro, ambapo ujenzi huo upo katika hatua za umaliziaji. Kukamilika kwa Gereza Mkono wa Mara kutasaidia kupunguza msongamano uliopo katika Gereza la Mahabusu Morogoro. Aidha, wafungwa na mahabusu 200 watahamishwa kutoka Gereza la Mahabusu Morogoro kwenda Gereza Mkono wa Mara. Jumla ya Shilingi 238,032,411 zimetumika katika ukarabati na ujenzi huo. 
  • Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi, 2022 kulikuwa na wafungwa (wahamiaji haramu) 5,679 kutoka mataifa mbalimbali walioingia nchini kinyume cha sheria. Kati ya hao, 582 ni mahabusu, 2,822 wanaendelea kutumikia kifungo, 2,275 wamemaliza vifungo vyao na wanasubiri kurejeshwa katika nchi zao. Uwepo wa wafungwa hao magerezani unaigharimu Serikali takribani Shilingi 5,182,087,500 kwa mwaka kwa chakula (wastani wa matumizi ya Shilingi 2,500 kwa mfungwa mmoja kwa siku). Pia, zipo gharama nyingine kama matibabu na mavazi ambazo

Serikali inagharamia. 

  • Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na changamoto ya wahamiaji haramu waliopo magerezani, Idara ya Uhamiaji kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) inaratibu utaratibu utakaowezesha wafungwa 500 waliomaliza kifungo kurejeshwa nchini kwao.
  • Mheshimiwa Spika, hatua nyingine zilizopangwa zitakazochukuliwa kukabiliana na msongamano wa wafungwa na mahabusu katika mwaka 2022/2023 ni: kuendelea kutumia utaratibu wa kifungo cha nje, parole pamoja na huduma kwa jamii na huduma za uangalizi kupitia sheria husika. Aidha, Bodi za Parole za Mikoa zitaendelea kufanya kazi zake ipasavyo, ambapo jumla ya Shilingi 329,688,000 zimetengwa.
  • Mheshimiwa Spika, Serikali imetenga Shilingi

4,569,600,000 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa Magereza ya Wilaya ya Karatu na Kilosa. Sambamba na magereza hayo mawili (2), Jeshi la Magereza litaanza ujenzi wa magereza mengine manne (4) ya Wilaya ya Kakonko – Kigoma, Wilaya ya Kaliua – Tabora, Wilaya ya Gairo – Morogoro na Msalato – Dodoma.

Kuimarisha Ulinzi na Usalama Magerezani

  • Mheshimiwa Spika, Jeshi limekamilisha ujenzi wa ukuta wa ngome wa Gereza Rombo – Kilimanjaro.

Aidha, ujenzi wa kuta za ngome unaendelea katika Magereza ya Mbigiri na Idete – Morogoro pamoja na Kwitanga – Kigoma. Ujenzi huo utakamilika mwaka 2022/2023.  

  • Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali itaendelea kuimarisha mifumo ya ulinzi na usalama kwa kufunga mitambo na vifaa maalum vya kiusalama katika magereza makuu 12. Vifaa hivyo ni pamoja na CCTV Camera, Metal Detector na Walk through Scanner. Mifumo hii itaondoa matumizi ya njia za kizamani za upekuzi na ulinzi wa wafungwa magerezani. Jumla ya Shilingi 5,000,000,000 zimetengwa kwa ajili ya kununua na kufunga mitambo hiyo. Hii ni hatua muhimu kwa Serikali ya Awamu Sita ambayo imejipambanua kwa dhamira na vitendo katika kutokomeza viashiria vyote vya uvunjifu wa haki za binadamu.  
  • Mheshimiwa Spika, kwa kutambua upungufu wa vitendea kazi, Serikali imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa magari ya Jeshi la Magereza. Katika mwaka 2021/2022 jumla ya Shilingi 4,661,416,000 zilitengwa kwa ajili ya ununuzi wa magari 26 ya shughuli za utawala, ufuatiliaji na utekelezaji wa miradi. Taratibu za ununuzi wa magari hayo zimekamilika.  
  • Mheshimiwa Spika, katika bajeti ya mwaka 2022/2023 Jeshi la Magereza limetenga Shilingi 5,700,000,000 za ununuzi wa magari 32. Kati ya magari hayo, 22 ni kwa ajili ya shughuli za utawala na 10 ni kwa ajili ya usafirishaji wa mahabusu. Upimaji wa Maeneo ya Jeshi la Magereza
  • Mheshimiwa Spika, Jeshi la Magereza linakabiliwa na migogoro ya ardhi katika baadhi ya maeneo yake. Maeneo ya Jeshi la Magereza yaliyopimwa ni 74 na yenye hati ni 13. Aidha, Jeshi linakamilisha taratibu za upatikanaji wa hati kwa viwanja 61. Katika mwaka 2022/2023 Shilingi 2,800,000,000 zimetengwa kwa ajili ya kupima maeneo 55 na kulipa fidia. Upimaji wa maeneo hayo utaliwezesha Jeshi la Magereza kuondokana na migogoro ya mipaka na hivyo kuyatumia kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo kwa ajili ya kujitosheleza kwa chakula na uwekezaji.  Upimaji wa maeneo hayo utafanyika kwa kushirikisha viongozi wa kijamii ili kuepuka malalamiko kutoka kwa wananchi.

Ununuzi wa Sare kwa Maafisa na Askari wa Jeshi la Magereza

100. Mheshimiwa Spika, Serikali imetenga Shilingi 4,127,000,000 kwa ajili ya ununuzi wa sare kwa maafisa na askari wa Jeshi la Magereza. Ununuzi wa sare hizo utasaidia kuondoa tatizo la sare kwa maafisa na askari wa Jeshi la Magereza. Serikali itaendelea kuongeza fedha za sare na vifaa vingine muhimu vya kijeshi kwa kadiri uwezo wa kifedha utakavyokuwa unaimarika.

Mafunzo na Ajira kwa Watumishi

  1. Mheshimiwa Spika, changamoto ya muda mrefu ya maafisa na askari ya kutopandishwa vyeo imepatiwa ufumbuzi kwa maafisa na askari 8,736 kupandishwa vyeo. Vilevile, maafisa na askari 6,582 walipatiwa mafunzo ya uongozi kama sharti la kupandishwa vyeo kwa mujibu wa Sheria za Jeshi la Magereza. Kupandisha vyeo watumishi kunawaongezea ari ya kufanya kazi na kuimarisha utendaji wa Jeshi.  
  2. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/2022 Jeshi la Magereza lilipewa kibali cha kuajiri askari wapya 700 ambao wapo mafunzoni katika Chuo cha Magereza Kiwira – Mbeya. Askari hao watahitimu mafunzo Julai, 2022. Kuajiriwa kwa askari hao kutapunguza changamoto ya upungufu wa watumishi ambayo imetokana na kustaafu, kuacha kazi, kufukuzwa kazi na vifo.
  3. Mheshimiwa Spika, watumishi 570 wanaendelea na mafunzo ya taaluma mbalimbali katika vyuo vya ndani na nje ya Jeshi. Miongoni mwao, 450 wanapata mafunzo ya Astashahada na

Stashahada, 41 Shahada, saba (7) Stashahada ya Uzamili, nane (8) Shahada ya Uzamili na wawili (2) Shahada ya Uzamivu. Aidha, 62 wanahudhuria mafunzo ya Astashahada na Stashahada ya Sayansi ya Urekebishaji kwenye Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Ukonga. 

  1. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza maagizo ya Mhe. Rais kuhusu Jeshi la Magereza kutimiza majukumu yake ya msingi ya urekebu wa wafungwa, Wizara itafanya yafuatayo: kupitia na kuboresha mitaala ya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji kilichopo Ukonga; kuwa na mpango mahsusi wa kupeleka maafisa na askari kujiendeleza katika fani ya taaluma ya urekebishaji; na kuandaa utaratibu na ubadilishanaji wa uzoefu ndani na nje ya nchi kwa walimu wanaotoa mafunzo ya urekebishaji.
  2. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2022/2023 watumishi 2,390 wa Magereza wanatarajiwa kupandishwa vyeo katika ngazi mbalimbali za uongozi. Kiasi cha Shilingi 3,500,000,000 kimetengwa kwa ajili ya kugharamia mafunzo ya maafisa na askari. Mafunzo hayo ni kwa watumishi 3,435 wanaohitajika kupitia mafunzo maalum ya uongozi ili kupandishwa vyeo.  

Kuimarisha Kikosi cha Ujenzi cha Magereza  

106. Mheshimiwa Spika, Jeshi la Magereza linaendelea kuimarisha kikosi chake cha ujenzi. Katika mwaka 2021/2022 Jeshi limenunua malori matano (5) ya tani 10 yanayotumika katika miradi ya ujenzi, ambayo yamegharimu Shilingi 550,000,000. Jeshi la Magereza linaendelea na taratibu za kununua mitambo ya ujenzi ambayo ni excavator moja (1), backhoe loader moja (1), gari la kuchimba visima moja (1), compactors tatu (3) na concrete mixers nne (4) kwa gharama ya Shilingi 2,079,000,000. 

Uboreshaji wa Makazi ya Watumishi

  1. Mheshimiwa Spika, kwa miaka mitatu (3) mfululizo Serikali imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za makazi ya watumishi wa Jeshi la Magereza. Katika mwaka 2021/2022 Jeshi la Magereza limekamilisha ujenzi wa nyumba za makazi 119 katika vituo mbalimbali nchini. Nyumba zilizokamilika zina uwezo wa kuhudumia familia 210. Kati ya hizo, nyumba 58 zimejengwa Msalato – Dodoma na zilizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 25 Machi, 2022. Aidha, nyumba nyingine 34 zinaendelea kujengwa katika magereza tofauti nchini. Gharama za ujenzi wa nyumba zote ni Shilingi 7,280,000,000. 
  2. Mheshimiwa Spika, Jeshi pia linaendelea na ujenzi wa nyumba 120 za kuishi familia 240 katika magereza mbalimbali nchini kwa kutumia rasilimali zinazopatikana katika maeneo ya magereza hayo.

Katika mwaka wa fedha 2022/2023, Jeshi la Magereza linatarajia kuendelea kuboresha makazi ya watumishi wake.  

  1. Mheshimiwa Spika, sambamba na ujenzi wa nyumba za maafisa na askari, Jeshi la Magereza pia linatarajia kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji safi katika vituo vyake. Katika mwaka wa fedha 2022/2023, Jeshi limetenga Shilingi 1,700,000,000 kwa ajili ya uchimbaji wa visima 34 vya vituo vya magereza na ujenzi wa miundombinu ya usambazaji. Fedha zilizotengwa zitatumika pia kugharamia usafirishaji wa mitambo.

Huduma za Afya Magerezani

  1. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Jeshi la Magereza imeanza ujenzi wa Hospitali ya Makao Makuu ya Jeshi hilo Msalato Jijini Dodoma.

Hospitali hiyo iliwekewa jiwe la msingi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 25 Machi, 2022. Awamu ya kwanza itahusisha ujenzi wa majengo ya huduma za matibabu ya wagonjwa wa nje (OPD), jengo la upasuaji, maabara, jengo la utawala, jengo la XRay, jengo la huduma ya mama na mtoto na jengo la kufulia nguo za hospitali. Katika mwaka 2022/2023 Jeshi la Magereza limetenga Shilingi 1,000,000,000 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi huo. Hospitali hii itakapokamilika itahudumia jamii ya magereza iliyopo eneo la Msalato pamoja na wananchi wanaoishi maeneo ya Msalato, Veyula na Makutopora.

  1. Mheshimiwa Spika, Jeshi la Magereza limepokea jumla ya mifuko 1,000 ya saruji kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika Hospitali ya Makao Makuu Msalato Jijini Dodoma. Saruji hiyo imetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. Hatuna budi kumshukuru Mhe. Rais kwa mchango huo mkubwa ambao utasaidia mradi kutekelezwa kwa kasi zaidi. Aidha, tunawashukuru na kuwapongeza maafisa na askari wanawake wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza kwa kuchangia mifuko 1,000 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo.

Kuboresha Uzalishaji wa Bidhaa za Viwandani

112. Mheshimiwa Spika, katika kuendeleza sera ya uchumi wa viwanda, Jeshi la Magereza limekamilisha ujenzi wa Kiwanda cha Samani Msalato na ununuzi wa mashine za kiwanda ambazo zimeshafungwa na kuanza kazi. Kiwanda hicho kilizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 25 Machi, 2022. Ujenzi wa kiwanda na ununuzi wa mashine umegharimu Shilingi 2,000,000,000. Ni imani yetu kuwa kukamilika kwa kiwanda hicho kutaleta manufaa makubwa kwa Jeshi la Magereza na Taifa kwa ujumla wake. Hivyo, naomba kutoa wito kwa wananchi, taasisi binafsi na za umma kununua bidhaa za samani zenye ubora wa kiwango cha juu kutoka Kiwanda cha Samani Msalato.

Kuboresha Uzalishaji wa Mazao ya Kilimo na Mifugo

  1. Mheshimiwa Spika, Jeshi la Magereza limekamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi wa mradi wa umwagiliaji Gereza Idete uliokuwa umesimama kwa muda mrefu. Shilingi 2,100,000,000 zimetumika kukamilisha ujenzi wa mfereji mkuu wa kutoa maji mtoni hadi shambani. Aidha, ujenzi wa ghala lenye uwezo wa kuhifadhi tani 600 za mazao unaendelea. 
  2. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali imetenga Shilingi 2,800,000,000 ili kuanza awamu ya pili ya Mradi wa Idete. Fedha hizo zitatumika kujenga miundombinu ya kusambaza maji shambani ili kuongeza uzalishaji wa mpunga. Ujenzi huu utawezesha umwagiliaji kufanyika katika ekari 1,000 na utakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 975 kwa mwaka.
  3. Mheshimiwa Spika, Serikali pia imetenga Shilingi 2,500,000,000 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji katika mashamba ya magereza ya Ushora – Singida, Kitete – Rukwa na Kalilankulukulu – Katavi. Ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji katika mashamba hayo utaongeza uzalishaji wa mahindi, alizeti na maharage yanayolimwa katika magereza hayo.
  4. Mheshimiwa Spika, kwa lengo la kufufua na kuendeleza zao la michikichi nchini, Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Mazao ya Kilimo (TARI – Kihinga)limezalisha miche 120,000 ya mbegu bora za michikichi na kufanikiwa kusambaza miche 54,000 kwa wananchi na wadau. Vilevile, miche 62,000 bado ipo kwenye vitalu. Pia, ekari 250 zimelimwa katika Gereza Kwitanga – Kigoma, ambapo ekari 57 zimepandwa miche 3,249 inayotokana na mbegu mpya za michikichi aina ya tenera. Kwa ujumla mpaka sasa katika shamba la Kwitanga zimepandwa ekari 532 za michikichi ya kisasa yenye jumla ya miche 26,999.
  5. Mheshimiwa Spika, Jeshi la Magereza limeendelea kuhudumia mifugo iliyopo katika magereza mbalimbali nchini kwa kuipatia malisho, chanjo, matibabu na kuboresha kosafu (breed) kwa njia ya uhamilishaji. Hadi kufikia Machi, 2022 jumla ya mifugo 25,371 ilikuwa inatunzwa na Jeshi la Magereza kwa mchanganuo ufuatao: ngombe

9,664 (ng’ombe wa nyama 7,637 na wa maziwa 2,027), mbuzi 4,004, kondoo 718, nguruwe 287 na kuku 10,698.

  1. Mheshimiwa Spika, Jeshi la Magereza limefanikiwa kuvuna jumla ya ng’ombe 1,329, mbuzi 538, kondoo 37 na nguruwe 60 wenye thamani ya Shilingi 769,970,500. Aidha, kwa kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022 Jeshi limefanikiwa kuzalisha lita 77,567 za maziwa zenye thamani ya Shilingi 62,053,600. 
  2. Mheshimiwa Spika, mwezi Aprili, 2022 Jeshi la Magereza limepokea Shilingi 7,439,000,000 za miradi ya maendeleo. Kati ya fedha hizo, Shilingi 1,000,000,000 ni kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kuoneshea bidhaa (show room) zinazozalishwa na

                Kiwanda    cha    Samani    Msalato    na     Shilingi

840,000,000 ni kwa ajili ya ukarabati wa Magereza ya Isanga na Kondoa – Dodoma, Mkuza – Pwani, Lindi – Lindi, Maweni – Tanga, Mbozi – Songwe, Mpanda – Katavi na Songwe – Mbeya.

  1. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa utekelezaji wa Mkakati wa Kilimo, Shilingi 4,249,000,000 ni za ununuzi wa matrekta na mitambo ya kilimo, Shilingi 1,190,000,000 za ujenzi wa maghala na nane (8) na Shilingi 160,000,000 za ujenzi wa Karakana nane (8). Ujenzi wa karakana na maghala utafanyika katika Magereza ya Arusha – Arusha, Kitai – Ruvuma, Kitengule – Kagera, Mollo – Rukwa, Pawaga – Iringa, Songwe – Mbeya, Ubena – Pwani na Ushora – Singida. Ujenzi utakamilika mwaka 2022/2023.

SHIRIKA LA MAGEREZA (SHIMA)

  1. Mheshimiwa Spika,mbali ya hatua mbalimbali ambazo Serikali imeshanza kuzichukua kwa lengo kuhakikisha mashirika yake uzalishaji mali ya vyombo vya usalama yanajiendesha kibiashara pamoja na kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi kwenye miradi inayosimamiwa na mashirika hayo, bado Serikali ya awamu ya sita inaendelea kuwekeza kwa nguvu kwenye miradi kwa kuitengea bajeti ya kuridhisha. Ni imani yetu kuwa hatua hiyo itasaidia kuongezea thamani na tija ya miradi pamoja na mashirika yake kwa ujumla wake.
  2. Mheshimiwa Spika, katika kuongeza thamani ya mazao ya mifugo, Shirika la Magereza limekamilisha ujenzi wa Kiwanda cha Maziwa katika Shamba la Kingolwira. Kiwanda kilizinduliwa rasmi tarehe 15 Oktoba, 2021 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi. Kiwanda hicho kinachangia kutoa ajira na soko kwa wazalishaji wa maziwa wanaozunguka eneo la kiwanda. Ujenzi wa kiwanda umegharimu Shilingi 451,000,000 na kinatengeneza siagi, mtindi na jibini na kina uwezo wa kuchakata lita 1,000 za maziwa kwa siku.
  3. Mheshimiwa Spika, Shirika la Magereza kwa kushirikiana na mamlaka za tafiti za kilimo linaendelea na jitihada za uzalishaji wa mbegu bora za kilimo. Mpaka kufikia Machi, 2022 jumla ya ekari 560 zimelimwa na kupandwa mbegu bora za mazao ya mahindi (UH 615), mpunga (TXD 88), alizeti (Record), ufuta (Lindi 2002), mihogo (Vipando) na maharage (Jesca). Eneo lililopandwa mazao ya mbegu bora ni ongezeko la ekari 360 kutoka ekari 200 zilizolimwa msimu wa mwaka 2020/2021. 
  4. Mheshimiwa Spika, kutokana na kilimo hicho, Jeshi la Magereza linatarajia kupata mbegu bora tani 183.6 za mahindi, 120 za mpunga, 25.2 za alizeti, 17.5 za ufuta, 48 za maharage na vipando 400,000 vya mihogo. Mbegu hizo zitatumika katika mashamba ya magereza na hivyo kupunguza gharama za ununuzi wa mbegu.
  5. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/2022 Shirika la Magereza limekamilisha ujenzi wa majengo ya Kiwanda cha Kuchakata na Kupakia Chumvi katika Gereza Lilungu mkoani Mtwara. Pia, limenunua na kufunga mitambo mitatu (3) ya kukausha, kusaga na kufungasha chumvi. Mitambo hiyo ina uwezo wa kuchakata na kupakia tani tatu (3) za chumvi kwa siku. Shilingi 82,500,000 zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa majengo na kununua mitambo ya kuchakata na kufungasha chumvi. 
  6. Mheshimiwa Spika, kuimarika kwa kiwanda hiki kumeongeza ubora wa chumvi inayozalishwa na hivyo kuongeza kipato cha Shirika kutoka mauzo ya Shilingi 80,000 hadi Shilingi 160,000 kwa tani. Kiwanda hicho kimepata cheti cha ubora kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Kiwanda kitanunua chumvi kutoka kwa wazalishaji wadogo wa maeneo ya jirani kwa madhumuni ya kuongeza ubora wa chumvi hiyo, ajira na kipato kwa wananchi.
  7. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Shirika la Magereza litaboresha miundombinu ya uzalishaji kwa kukarabati mabirika 10 ya kuzalishia chumvi. Mabirika hayo yaliyopo Gereza Lilungu – Mtwara yatakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 900 za chumvi ghafi kwa mwaka. Kazi nyingine zitakazofanyika ni ujenzi wa ghala kwa ajili ya kuhifadhia chumvi ghafi na chumvi iliyochakatwa. Kazi zote zitagharimu takribani Shilingi 100,000,000. Sambamba na shughuli hizo, kiwanda kinatarajia kuanza kufungasha chumvi katika vipimo vidogo vya gramu 300 na 500 ifikapo mwezi Julai, 2022. Lengo ni kuuza katika soko la watumiaji wadogo na kuongeza mapato.
  8. Mheshimiwa Spika, Shirika la Magereza limeanza ujenzi wa kiwanda cha kuchakata mahindi katika Gereza Kitai mkoani Ruvuma. Ujenzi huo unatarajiwa kugharimu Shilingi 180,000,000 na umeanza kwa kujenga jengo la kiwanda ambalo limefikia asilimia 70
  9. Mheshimiwa Spika, kiwanda kitakapokamilika kitakuwa na uwezo wa kuchakata wastani wa tani 6,240 za mahindi kwa mwaka. Aidha, Shirika limepanga kununua mashine za kuchakata na kusindika mazao ya mahindi ili kiwanda kianze uzalishaji. Kiwanda kitasaidia kuongeza thamani ya mahindi na kuongeza wigo wa mapato kwa kuuza unga na vyakula vya mifugo vinavyotokana na mabaki ya mazao ya mahindi. 

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

  1. Mheshimiwa Spika, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linaendelea kutekeleza majukumu yake na hadi kufikia Machi, 2022 limezima moto na kufanya uokoaji katika matukio 2,036. Pia, ukaguzi wa kinga na tahadhari ya moto umefanyika kwenye maeneo 33,160 kati ya 52,500 sawa na asilimia 63.2 ya lengo la kipindi husika. Shilingi 5,957,310,000 zilikusanywa kutokana na ukaguzi huo. 
  2. Mheshimiwa Spika, ukaguzi wa kinga na tahadhari dhidi ya moto huenda sambamba na ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali. Wizara kupitia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika kudhibiti upotevu wa maduhuli itaimarisha mfumo wa kieletroniki (Fire Safety Inspection Revenue Management System).

Uimarishaji huo utahusisha ununuzi wa vifaa vya TEHAMA, kuhuisha kanzi data ya maeneo ya ukaguzi na kutengeneza miundombinu kwa ajili ya kuunganisha huduma za kimtandao katika ofisi za zimamoto na uokoaji za wilaya.    

  1. Mheshimiwa Spika, kutokana na kuongezeka kwa matukio ya moto katika masoko, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linaendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara na kutoa elimu zaidi kuhusu namna ya kudhibiti matukio hayo. Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022 masoko 228 nchini yalifanyiwa ukaguzi wa kinga na tahadhari ya moto.
  2. Mheshimiwa Spika, sambamba na utoaji wa elimu kwenye shule na masoko, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji litaendelea kushirikiana na mamlaka nyingine ikiwemo Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi, Kamati za Usalama katika maeneo husika ili kuimarisha usimamizi wa sheria.     
  3. Mheshimiwa Spika, ninatoa rai kwa wafanyabiashara na watumiaji wa masoko yote nchini kuzingatia elimu ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto inayotolewa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili kuepuka matukio ya moto ambayo yamekuwa yakisababisha hasara kwao na kwa Taifa kwa ujumla.
  4. Mheshimiwa Spika, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pia linashiriki kutoa ushauri wa kitaalam kuhusu kinga na tahadhari ya moto kwenye miradi ya kitaifa ya kimkakati. Katika ushiriki huo kwa sasa Gari la kuzima moto na askari 20 wamepelekwa katika mradi wa Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere. Aidha, ushauri wa kitaalam umetolewa katika miradi ya ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) na Bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania). 

Sare na Vitendea Kazi kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/2022 Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lilitenga Shilingi 1,000,000,000 kwa ajili ya ununuzi wa sare kwa maafisa na askari. Taratibu zinaendelea ili kukamilisha ununuzi wa sare hizo ambapo maafisa na askari 2,006 watapatiwa sare. Pia, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Jeshi limetengewa Shilingi 1,000,000,000 kwa ajili ya sare za maafisa na askari 2,006.
  2. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/2022 Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limekamilisha ununuzi wa magari 25 yenye thamani ya Shilingi 2,721,826,135.80. Magari hayo yatatumika katika shughuli za utawala na ukaguzi wa kinga na tahadhari ya moto. Aidha, katika mwaka 2022/2023 Shilingi 1,960,000,000 zimetengwa kwa ajili ya ununuzi wa magari 19 ya utawala na shughuli za ukaguzi. 
  3. Mheshimiwa Spika, mwezi Mei, 2022 Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linatarajia kupokea magari matatu (3) ya kuzima moto kutoka Shirika la Nyumbu (TATC). Magari hayo yatagharimu Shilingi 2,997,500,000 na kiasi cha Shilingi 2,233,125,000 sawa na asilimia 75 kimeshalipwa.
  4. Mheshimiwa Spika, vilevile, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limekamilisha malipo ya Shilingi

634,976,928 kwa ajili ya ununuzi wa boti mbili (2) za uokoaji. Boti hizo zinatengenezwa na Kampuni ya Songoro Marine Transport Limited ya Tanzania na zitagharimu Shilingi 705,529,920. Boti husika zinatarajiwa kukabidhiwa mwezi Mei, 2022.  

Ajira, Upandishwaji Vyeo na Mafunzo kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji

  1. Mheshimiwa Spika, katika kuboresha utendaji, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limepatiwa kibali cha kuajiri Askari wapya 400.  Askari hao wanaendelea na mafunzo ya awali katika Chuo cha Zimamoto na Uokoaji kilichopo Chogo – Handeni Mkoani Tanga. Pia, maafisa, askari na watumishi raia 918 wamepandishwa vyeo katika ngazi mbalimbali.
  2. Mheshimiwa Spika, kwa lengo la kuongeza ufanisi,maafisa na askari 796 wamepata mafunzo ndani ya nchi na maafisa wawili (2) wamepata mafunzo nje ya nchi. Katika mwaka wa fedha 2022/2023 Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limepanga kuwapatia mafunzo na kuwapandisha vyeo maafisa na askari 700.

Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji 

142. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/2022 Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linatekeleza miradi ya ukarabati na ujenzi wa vituo vya zimamoto na uokoaji pamoja na makazi ya maafisa na askari kwa utaratibu wa nguvu kazi (force account). Utekelezaji wa miradi hiyo ni kama ifuatavyo: 

(a) Ukarabati wa Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Ilala – Dar es Salaam

143. Mheshimiwa Spika, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limetenga Shilingi 273,746,089 kwa ajili ya ukarabati wa Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Ilala – Dar es Salaam. Ukarabati wa kituo hicho unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2022.

(b) Ujenzi wa Nyumba za Makazi ya Askari katika eneo la Kikombo – Dodoma

144. Mheshimiwa Spika, ujenzi wa nyumba za makazi ya askari Kikombo – Dodoma ulianza kutekelezwa Julai, 2020 na unatarajiwa kugharimu Shilingi 7,391,068,800 hadi kukamilika kwake. Kupitia fedha hizo, majengo nane (8) ya ghorofa yanatarajiwa kujengwa kwa ajili ya familia 80 za askari. Hadi kufikia Machi, 2022 ujenzi umefikia asilimia 65

(c) Ujenzi wa Kituo cha Zimamoto na Uokoaji cha Wilaya ya  Chamwino – Dodoma

145. Mheshimiwa Spika, mradi wa ujenzi wa Kituo cha Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Chamwino – Dodoma ambao ulianza tarehe 15 Agosti, 2020 umekamilika. Mradi umegharimu Shilingi

1,193,000,000 zilizotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Mfuko wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Jiji la Dodoma. Ujenzi umejumuisha majengo ya utawala, bwalo la chakula, eneo la kuegeshea magari ya zimamoto na jengo la kufanyia mazoezi ya kuzima moto na uokoaji.

(d) Ujenzi wa Kituo cha Zimamoto na Uokoaji katika eneo la Nzuguni – Dodoma

146. Mheshimiwa Spika, ujenzi wa Kituo cha Zimamoto na Uokoaji katika eneo la Nzuguni – Dodoma kilianza kujengwa tarehe 14 Aprili, 2021 na umefikia asilimia 80. Ujenzi utagharimu Shilingi 1,248,050,000. Kazi zinazoendelea ni za umaliziaji ikiwemo kuweka mifumo ya umeme, maji safi na maji taka pamoja na kazi za usanifu wa mazingira. Mradi utakamilika mwezi Juni, 2022.

(e) Umaliziaji wa Ujenzi wa Kituo Kikuu cha Zimamoto na Uokoaji katika eneo la TAZARA – Mchicha (Dar es Salaam)

147. Mheshimiwa Spika, umaliziaji wa ujenzi wa Kituo Kikuu cha Zimamoto na Uokoaji katika eneo la

TAZARA – Mchicha, Dar es Salaam ulianza tarehe 6 Julai, 2021 na unajumuisha ujenzi wa jengo la utawala, truck bay, hose tower na tenki la kuhifadhia maji. Ujenzi huo utagharimu Shilingi 2,397,178,675 na umefikia asilimia 90. Mradi utakamilika mwezi Mei, 2022.  

Miradi ya Kipaumbele ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika Mwaka 2022/2023

  1. Mheshimiwa Spika, kwa madhumuni ya kuendelea kuboresha huduma za zimamoto na uokoaji nchini, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limetenga Shilingi 9,930,000,000 za utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Fedha hizo zitatumika kwa ajili ya ukarabati wa vituo vinne (4) vya zimamoto na uokoaji katika Mikoa ya Kilimanjaro, Morogoro, Mwanza na Ruvuma pamoja na ujenzi wa vituo saba (7) vya zimamoto na uokoaji katika Mikoa ya Geita, Kagera, Katavi, Manyara, Njombe, Simiyu na Songwe.  
  2. Mheshimiwa Spika, miradi mingine iliyopangwa kutekelezwa ni kukamilisha ujenzi wa nyumba za makazi ya askari Kikombo – Dodoma; uendelezaji wa Chuo cha Zimamoto na Uokoaji Chogo – Handeni Mkoani Tanga na ujenzi wa vyumba vya kuhifadhia silaha katika mikoa tisa (9) ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Morogoro, Mwanza, Ruvuma, Simiyu, Songwe na Tanga.  

IDARA YA UHAMIAJI

150. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitiaIdara ya Uhamiaji inaendelea kutoa huduma zake kupitia mfumo wa kielektroniki (e-immigration). Katika kuboresha mifumo ya utoaji huduma, ufungaji wa mfumo wa usimamizi na udhibiti wa mipaka (eborder management system) umekamilika katika Ofisi za Uhamiaji za Mikoa 22 na vituo 25. Kupita mfumo huo, usalama wa nchi unazidi kuimarika kwa kuhakikisha wageni na raia wanaoingia au kutoka nchini ni wale wanaostahili. 

Udhibiti wa Uingiaji, Ukaaji na Utokaji wa Wageni Nchini

  1. Mheshimiwa Spika, Idara ya Uhamiaji inaendelea kusimamia na kutoa huduma za kuwawezesha raia wa Tanzania na wageni kutoka na kuingia nchini. Katika kipindi cha kuanzia Julai, 2021 hadi Machi, 2022 jumla ya wageni 958,007 waliingia nchini ikilinganishwa na wageni 511,243 waliongia katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2020/2021. Aidha, jumla ya wageni 882,579 walitoka nchini ikilinganishwa wageni 421,687 waliotoka katika mwaka wa fedha 2020/2021. 
  2. Mheshimiwa Spika, idadi ya wageni walioingia na kutoka nchini imeongezeka kutokana na nchi mbalimbali kuondoa zuio la watu kusafiri baada ya maambukizi ya UVIKO–19 kupungua. Aidha, hadi kufikia Machi, 2022 wageni 430 walizuiwa kuingia nchini kutokana na sababu za kiusalama au kutokidhi vigezo vya uhamiaji. 
  3. Mheshimiwa Spika, vilevile, vibali vya ukaazi kwa wageni wanaoingia, kuishi na kufanya kazi hapa nchini vinaendelea kutolewa. Kwa kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022, jumla ya vibali vya ukaazi 15,143 (Daraja A 1,855; Daraja B 10,479; na Daraja C 2,809) vilitolewa. Vibali 2,467 vimeongezeka ikilinganishwa na vibali 12,676

(Daraja A 2,353; Daraja B 7,007; na Daraja C 3,316) vilivyotolewa kipindi kama hiki mwaka 2020/2021.

  1. Mheshimiwa Spika, jumla ya Hati za Mfuasi 2,274 zilitolewa ikilinganishwa na Hati 2,694 zilizotolewa katika kipindi kama hiki mwaka 2020/2021. Vilevile, Hati za Msamaha 808 zilitolewa ikilinganishwa na Hati 1,299 zilizotolewa katika kipindi kama hiki mwaka 2020/2021. Aidha, visa 314,635 zilitolewa kwa wageni walioomba kuingia nchini kwa shughuli mbalimbali. Katika mwaka wa fedha 2022/2023 Idara itaendelea kutoa vibali vya ukaazi na hati nyingine za kuingia hapa nchini kwa wageni wenye tija kwa Taifa.

Misako, Doria na Ukaguzi

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Idara ya Uhamiaji imeendelea kufanya misako, doria na ukaguzi katika maeneo mbalimbali. Lengo ni kuwabaini, kuwakamata na kuwadhibiti wahamiaji haramu wanaoingia nchini. Hadi kufikia Machi, 2022 jumla ya watuhumiwa 14,728 wa uhamiaji haramu walikamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.  
  2. Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na changamoto ya wahamiaji haramu ikiwemo wa kutoka Ethiopia, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imeshakamilisha rasimu ya mkakati wa namna bora ya kulipatia ufumbuzi wa kudumu suala hili, na mapendekezo yake yapo katika hatua mbalimbali za majadiliano. Hatua hiyo itasaidia kudhibiti wahamiaji haramu kuingia nchini na hatimaye kuteketeza mtandao wake wote unaojihusisha na biashara hiyo uliopo nchini, jambo ambalo pia litasaidia kupunguza gharama za kuwahudumia wanapokuwa mahabusu katika vituo vya polisi na magerezani.
  3. Mheshimiwa Spika, Watanzania 322 walirejeshwa nchini kwa sababu ya kumaliza vifungo na kutokukidhi vigezo vya uhamiaji katika nchi husika. Katika mwaka wa fedha 2022/2023 Idara ya Uhamiaji itaendelea kufanya misako, doria na ukaguzi ili kudhibiti wahamiaji haramu na kuhakikisha watu wote wanaoingia na kutoka nchini wanatumia njia zilizo rasmi.

Pasipoti na Hati Nyingine za Safari

158. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022 jumla ya Pasipoti 57,206 zilitolewa kwa Watanzania ikilinganishwa na Pasipoti 54,072 zilitolewa kipindi kama hicho mwaka 2020/2021.  Pasipoti 690 zilikuwa za

Kibalozi, Pasipoti za Kiutumishi ni 49 na Pasipoti za Kawaida ni 56,467. Aidha, Hati za Safari za Dharura 210,779 zilitolewa ikilinganishwa na Hati za Safari za Dharura 164,506 kwa mwaka 2020/2021. Katika mwaka wa fedha 2022/2023, Idara ya Uhamiaji itaendelea kutoa Pasipoti na hati nyingine za safari kwa raia wa Tanzania ili kuwawezesha kusafiri nje ya nchi kwa shughuli halali. 

Wageni Waliopewa Uraia wa Tanzania

159. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi, 2022 jumla ya wageni 85 walipewa uraia wa Tanzania ikilinganishwa na wageni 52 ambao walipewa uraia katika kipindi kama hiki kwa mwaka 2020/21. Wageni hao wanatoka mataifa ya Burundi (2), Brazil (1), DRC (1), Guinea (1), Hispania (2), India

(44), Kenya (9), Lebanon (6), Pakistani (2), Rwanda (3), Somalia (2), Sudani (1), Uganda (3), Ufaransa

(1), Uingereza (1), Yemen (4) na Zimbabwe (2).

Watanzania Waliopatiwa Uraia wa       Mataifa Mengine

160. Mheshimiwa Spika, hadi Machi, 2022 Watanzania 38 waliukana uraia na kupata uraia wa mataifa mengine kama ifuatavyo: Australia (1), Botswana (1), China (1), India (2), Kenya (1), Marekani (7), Namibia (2), Singapore (1), Uganda (1), Uingereza (3) na Ujerumani (18). Katika kipindi kama hiki kwa mwaka wa fedha 2020/2021 Watanzania 57 waliukana Uraia wa Tanzania.

Mafunzo na Ajira katika Idara ya Uhamiaji

  1. Mheshimiwa Spika, Idara ya Uhamiaji imewapatia mafunzo maafisa, wakaguzi na askari 269 pamoja na watumishi raia 21 ndani na nje ya nchi. Maafisa na askari 679 walihitimu mafunzo ya uongozi katika Kambi ya Mafunzo ya Uhamiaji Boma Kichakamiba – Tanga. Aidha, askari wawili (2) wanashiriki katika ulinzi wa amani nchini Lebanon.
  2. Mheshimiwa Spika, askari wapya 820 wameajiriwa na wanapatiwa mafunzo ya awali katika Kambi ya Boma Kichakamiba Mkoani Tanga. Askari hao watahitimu mafunzo husika Septemba, 2022. Vilevile, askari 1,181 walipandishwa vyeo katika ngazi mbalimbali. Katika mwaka wa fedha 2022/2023, Idara ya Uhamiaji itaendelea kutoa mafunzo kwa maafisa, wakaguzi, askari na watumishi raia ili kuwaongezea ujuzi na weledi katika utendaji wa kazi.

Vitendea Kazi, Majengo ya Ofisi na Makazi ya Askari wa Uhamiaji

  1. Mheshimiwa Spika, Idara ya Uhamiaji imepata kibali cha kununua magari sita (6) na hatua za ununuzi zimekamilika. Upatikanaji wa magari hayo utasaidia katika shughuli za misako, doria, ukaguzi pamoja na shughuli za utawala. Aidha, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Idara ya Uhamiaji imetenga Shilingi 5,605,200,000 kwa ajili ya kununua magari 30. 
  2. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023 mfumo wa kutolea Hati za Dharura utafungwa katika wilaya 70. Mfumo huo utaimarisha ukusanyaji wa mapato yanayotokana na huduma ya hati za dharura. Ufungaji wa mfumo huo utagharimu Shilingi 830,000,000.
  3. Mheshimiwa Spika, Serikali imetoa Shilingi 2,213,811,336.37 kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya Ofisi za Uhamiaji katika mikoa mbalimbali. Mchanganuo wa fedha hizo na hatua za utekelezaji wa miradi hiyo ni kama ifuatavyo: Shilingi 420,797,376.87 zimetolewa kwa ajili ya Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Geita na utekelezaji umefikia asilimia 75, Shilingi 401,119,203.76 zimetolewa kwa Ofisi ya Uhamiaji ya Mkoa wa Mtwara na utekelezaji wake umefikia asilimia 55, Shilingi 137,908,605.74 zimetolewa kwa Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Lindi na utekelezaji umefikia asilimia 80. Aidha, Shilingi 353,986,150 zimetolewa kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Manyara.
  4. Mheshimiwa Spika, ujenzi wa Kambi ya Mafunzo Boma Kichakamiba katika Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga unaendelea. Mradi huo unahusisha ujenzi wa zahanati, mabweni matano (5), madarasa matatu (3) na uwanja wa gwaride, ambapo Shilingi 900,000,000 zimetolewa. Aidha, mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Uhamiaji Makao Makuu Jijini Dodoma umefikia asilimia 58.
  5. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Wizara kupitia Idara ya Uhamiaji imepanga kukamilisha miradi ya ujenzi wa ofisi ya Uhamiaji katika Mikoa ya Geita, Lindi na Mtwara. Vilevile, itaendelea na ujenzi wa Ofisi ya Uhamiaji Makao Makuu Jijini Dodoma na Kambi ya Mafunzo ya Uhamiaji ya Boma Kichakamiba – Tanga kwa kujenga nyumba 12 za makazi ya wakufunzi. 
  6. Mheshimiwa Spika, miradi mingine iliyopangwa kutekelezwa ni ujenzi wa Ofisi za Uhamiaji za Wilaya ya Butiama – Mara na Mlele – Katavi; na ukarabati wa Ofisi za Uhamiaji za Mikoa ya Mara, Morogoro na Kurasini – Dar es Salaam. Aidha, nyumba 12 za Wakala wa Ujenzi Tanzania (TBA) zilizopo eneo la Msamala Mkoa wa Ruvuma zinazokodishwa kwa Idara ya Uhamiaji zitanunuliwa kwa ajili ya makazi ya askari. 
  7. Mheshimiwa Spika, kazi nyingine ni kukarabati nyumba 10 za makazi ya askari – Tabora na nyumba sita (6) – Pwani na ujenzi wa nyumba mbili (2) za makazi ya Makamishna wa Uhamiaji – Dodoma. Miradi yote ya ujenzi, ununuzi wa magari

na vifaa maalum vya usalama imepangwa kutekelezwa kwa jumla ya Shilingi 12,235,200,000. 

MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA –

NIDA  Hali ya Usajili na Utambuzi wa Watu Nchini 

  1. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022 NIDA imesajili watu 380,688 hivyo kufikia jumla ya watu 22,917,859 waliosajiliwa ikiwa ni asilimia 90.8 ya lengo la kusajili watu 25,237,954. Jumla ya wageni wakaazi 34,776 na wakimbizi 236,792 wamesajiliwa. Pia, Namba za Utambulisho (NIN) 19,313,358 zimezalishwa na kugawiwa kwa wananchi hadi kufikia Machi, 2022.
  2. Mheshimiwa Spika, NIDA imezalisha vitambulisho 2,621,644 na kufanya jumla ya vitambulisho 10,761,886 vilivyozalishwa hadi Machi, 2022. Pia, NIDA imefanikiwa kusambaza vitambulisho 2,535,520 hivyo kufanya vitambulisho vilivyosambazwa kwa wananchi kuwa 10,011,679. Pamoja na Serikali kusogeza huduma za ugawaji wa vitambulisho karibu na wananchi, bado kuna vitambulisho 750,207katika ofisi za wilaya za NIDA, Ofisi za Kata, Shehia, Vijiji na Mitaa ambavyo havijachukuliwa na wananchi. Ninatoa wito kwa wananchi wote waliopewa taarifa ya kwenda kuchukua vitambulisho vyao wafanye hivyo.  
  3. Mheshimiwa Spika, ilitarajiwa kuwa watu wote wenye Namba za Utambulisho wangepata vitambulisho. Matarajio hayo hayakufikiwa kutokana na changamoto za mkataba kati ya NIDA na Mkandarasi wa mradi. Katika kutatua changamoto hiyo, mwezi Machi, 2022 NIDA imesaini mkataba na Kampuni ya IRIS CORPORATION BERHAD ya nchini Malaysia. Mkataba huo wa miezi 18 unahusisha ununuzi wa kadi ghafi na vifaa vya TEHAMA, matengenezo ya Kituo cha Kuchakata Taarifa na Kituo cha Uokozi wakati wa Majanga, pamoja na mafunzo.

Utekelezaji wa mkataba utaiwezesha NIDA kutumia Shilingi 9,000,000,000 zilizotengwa mwaka 2021/2022 kuzalisha vitambulisho 1,960,000 ifikapo Juni, 2022.

  1. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha

2022/2023 Wizara kupitia NIDA itaendelea na zoezi la usajili na utambuzi wa watu. Jumla ya watu

1,200,000 wanatarajiwa kutambuliwa na kusajiliwa. Aidha, kiasi cha Shilingi 42,500,000,000 kimetengwa kwa ajili ya kununua kadi ghafi toleo la pili 8,500,000 ili kuendelea na uzalishaji wa vitambulisho. Pia, NIDA imetenga Shilingi 1,225,000,000 kwa ajili ya kununua magari sita (6) yatakayosaidia shughuli za usajili.  

Uunganishaji wa Mfumo wa NIDA na Mifumo ya Taasisi Nyingine

  1. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi, 2022, jumla ya taasisi 59 zimeunganishwa katika Mfumo wa Usajili na Utambuzi, ambapo taasisi za umma ni 25 na binafsi ni 34. Lengo ni kurahisisha utoaji huduma na utambuzi wa wananchi wanaopata huduma katika Taasisi hizo. Aidha, watu wenye Namba za Utambulisho wa Taifa wanaweza kutumia namba hizo kupata huduma mbalimbali.
  2. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Mamlaka imepanga kuwafikia watoa huduma wengi zaidi ikiwemo taasisi za fedha na vyama vya ushirika ili kuziunganisha na Kanzidata ya NIDA. Aidha, elimu itatolewa juu ya matumizi ya Mfumo wa Utambulisho wa Taifa (National ID System) kwa ajili ya uhakiki wa taarifa za watu kabla ya kutoa huduma. Lengo ni kuongeza uelewa kwa taasisi hizo na wananchi kuhusu umuhimu wa usajili.

Kuboresha Huduma za NIDA katika Ofisi za Wilaya 

  1. Mheshimiwa Spika, NIDA inaendelea kuunganisha mfumo wa usajili katika wilaya tano (5) za Gairo, Malinyi, Mbogwe, Ngorongoro na Ulanga zilizofikiwa na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano. Aidha, njia mbadala ya mawasiliano ya kuunganisha mfumo wa usajili inatumika kwa wilaya ambazo hazijafikiwa na Mkongo wa Taifa wa

Mawasiliano. Serikali imetenga Shilingi 1,932,900,000 kwa ajili ya gharama ya mifumo ya mawasiliano ya taarifa za usajili kutoka ofisi za wilaya kwenda katika kituo cha uchakataji wa taarifa.

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali imetenga Shilingi 2,960,863,840 kwa ajili ya uendeshaji wa ofisi za wilaya, kituo cha kuchakata taarifa na kituo cha uokozi wa taarifa wakati wa majanga. Pia, Shilingi 1,637,766,600 zimetengwa kwa ajili ya matengenezo ya mifumo ya umeme katika kituo cha kuchakata taarifa na ukarabati wa ofisi za usajili za wilaya nchini.

Mpango wa Mamlaka Kujitegemea katika Kuendesha Mfumo wa Vitambulisho vya Taifa

  1. Mheshimiwa Spika, kwa kutumia wataalamu wa ndani NIDA imefanikiwa kujenga mifumo 13 kati ya 16 iliyopangwa. Mifumo hiyo imesaidia kutumia wataalamu wa ndani na kupunguza utegemezi wa mkandarasi. Katika mwaka wa fedha 2022/2023 NIDA imetenga Shilingi 226,680,000 ili kuboresha na kukamilisha mifumo mbalimbali inayotumika katika shughuli za usajili na utambuzi. Shilingi 1,155,965,000 zimetengwa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa na mifumo ya kiusalama ya TEHAMA katika mfumo wa usajili.
  2. Mheshimiwa Spika, awamu ya pili ya utekelezaji wa mradi wa vitambulisho inatarajiwa kuanza Julai, 2022 na kukamilika ifikapo Juni, 2025. Mradi huo utahusisha ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya NIDA, ghala la kuhifadhia na kufanyia matengenezo ya vifaa vya TEHAMA pamoja na ujenzi wa ofisi 31 za wilaya. Jumla ya Shilingi 8,060,734,560 zimetengwa, ambapo Shilingi 1,282,634,560 ni fedha za ndani na Shilingi 6,778,100,000 ni fedha za nje.
  3. Mheshimiwa Spika, kutokana na uwekezaji utakaofanyika, ni dhahiri kuwa Serikali ya Awamu ya Sita itaondoa malalamiko ya wananchi ya kuchelewa kupata vitambulisho vyao vya Taifa. 

PROGRAMU YA HUDUMA KWA JAMII NA

UANGALIZI

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imeendelea kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Huduma kwa Jamii, Sura 291 ya mwaka 2002 na Sheria ya Uangalizi, Sura 247, Rejeo la mwaka 2002. Sheria hizo zinalenga kupunguza msongamano wa wafungwa magerezani na kuipunguzia Serikali gharama za kuendesha magereza. Aidha, utekelezaji wa sheria husika huwaepusha wafungwa wasio wazoefu kuiga tabia

za kihalifu kutoka kwa wafungwa sugu na kuzipatia taasisi za umma nguvu kazi ya wafungwa badala ya kuajiri vibarua. 

  1. Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa Sheria ya Huduma kwa Jamii, na Sheria ya Uangalizi hutoa fursa ya kuwarekebisha wafungwa wakiwa ndani ya jamii. Aidha, husaidia kuzuia familia na ndoa za wafungwa kusambaratika kutokana na mzazi, mwenza au mlezi kufungwa gerezani.
  2. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi, 2022 jumla ya Taarifa za Uchunguzi wa Kijamii (Social Enquiry Reports) 3,743 ziliwasilishwa Mahakamani kwa ajili ya kuziwezesha Mahakama kutoa maamuzi ya kuwaweka wafungwa kwenye vifungo vya nje. Kupitia taarifa hizo jumla ya wafungwa 3,151 (wanaume 2,444 na wanawake 707) walihukumiwa kutumikia adhabu zao kwenye jamii. Wafungwa 2,863 walimaliza kutumikia vifungo vyao na kurudishwa kwenye jamii kuungana na familia zao, ambapo wanaume walikuwa 2,147 na wanawake

716. 

  1. Mheshimiwa Spika, Serikali imeweza kuokoa Shilingi 2,875,287,500 kutokana na wafungwa kutekeleza adhabu zao nje ya magereza. Fedha hizo zingetumika kuwalisha wafungwa kama wangeendelea kukaa gerezani (kwa wastani wa Shilingi 2,500 kwa mfungwa kwa siku moja kwa chakula). Vilevile, Serikali imeokoa jumla ya Shilingi 3,024,960,000 ambazo zingetumika kuwalipa vibarua kwa kufanya kazi kwenye taasisi za umma baada ya kazi hizo kufanywa na wafungwa wa vifungo vya nje (kwa wastani wa malipo ya Shilingi 4,000 kwa kibarua kwa siku). 
  2. Mheshimiwa Spika, kazi zilizofanywa na wafungwa wa vifungo vya nje zinajumuisha utunzaji wa mazingira ikiwemo upandaji miti, utunzaji wa bustani katika taasisi za umma na usafishaji wa mabwawa ya majitaka katika Mkoa wa Dar es Salaam. Kazi nyingine zilizofanyika ni kushiriki katika ujenzi wa Ofisi ya Hakimu Mkoani Mara, madarasa mawili (2) katika Shule ya Sekondari Changarawe na nyumba moja (1) ya mwalimu katika Shule ya Sekondari Malangali Wilayani Mufindi Mkoani Iringa.
  3. Mheshimiwa Spika, wafungwa wenye taaluma ya ualimu wanaotumikia vifungo vya nje walishiriki kufundisha wanafunzi kwenye Shule ya Sekondari Mdandamo Kata ya Mletele Mkoani Ruvuma. Wengine wameshiriki katika uzalishaji wa mbegu za viazi, Kata ya Bushushu Mkoani Shinyanga. 
  4. Mheshimiwa Spika, programu za urekebishaji kwa wafungwa wa adhabu mbadala zilifanyika kwa kuzingatia mahitaji ya kila mfungwa. Kupitia programu hizo, wafungwa 500 walifundishwa stadi

za kazi na maisha, wafungwa 2,620 walipewa ushauri nasaha ili kuwasaidia kuishi maisha yasiyotegemea uhalifu na wafungwa 31 waathirika wa dawa za kulevya waliunganishwa na taasisi zinazotoa huduma za ushauri nasaha na matibabu. 

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara imetoa mafunzo ya utekelezaji wa adhabu mbadala kwa Waheshimiwa Majaji saba (7), Mahakimu 130, Wakuu wa Magereza 13 na Waendesha Mashtaka 12 katika Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tabora. Aidha, elimu kwa umma ilitolewa kupitia vyombo vya habari, ambapo vipindi vya redio vilikuwa 45, vipindi vya runinga nane (8), mitandao ya kijamii nane (8) na magazeti manne (4). Wizara pia imeshiriki Maadhimisho ya wiki ya Sheria katika mikoa yote ya Tanzania Bara, na kutumia maadhimisho hayo kutoa elimu kwa wadau na wananchi.
  2. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Wizara itawasimamia na kuwafuatilia wafungwa 5,000 wanaotegemewa kutumikia adhabu chini ya Programu ya Huduma kwa Jamii na Huduma za Uangalizi. Ili kufikia lengo hilo Wizara itaendelea kutoa mafunzo ya utekelezaji wa adhabu mbadala kwa wadau wa haki jinai na maafisa wasimamizi wa wafungwa. 
  3. Mheshimiwa Spika, zoezi la kutembelea Mahakama na Magereza litafanyika kwa lengo la kusaili wafungwa wenye sifa za kutumikia adhabu chini ya Programu ya Huduma kwa Jamii na Huduma za Uangalizi. Zoezi hilo litahusisha kufanya uchunguzi wa kijamii, kuandaa taarifa, kutekeleza programu za urekebishaji na kukagua taasisi zinazotoa kazi kwa wafungwa. 
  4. Mheshimiwa Spika, kazi nyingine zitakazofanyika ni kutengeneza Kanuni za Huduma za Utangamanisho, Usimamizi na Ufuatiliaji wa wafungwa wanaomaliza vifungo (Aftercare Services Regulations). Kanuni hizo zitasaidia kudhibiti wimbi la wafungwa wanaoachiwa magerezani au vifungo vya nje kurudia kutenda vitendo vya kihalifu. 
  5. Mheshimiwa Spika, Wizara inatarajia kuanzisha kanzidata ya wafungwa wa vifungo vya nje (Offenders’ Database Information System) na kutoa elimu kuhusu matumizi ya mfumo huo kwa wadau 1,000. Katika kutekeleza na kufanikisha kazi za huduma kwa jamii na huduma za uangalizi Shilingi 1,900,339,000 zitatumika.

USAJILI NA USIMAMIZI WA JUMUIYA ZA KIDINI NA ZISIZO ZA KIDINI 

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Ofisi ya Msajili wa Jumuiya imeendelea kusajili na kusimamia Jumuiya za Kidini

na zisizo za Kidini. Lengo ni kuhakikisha kuwa jumuiya hizo zinajiendesha kwa kufuata Sheria ya Jumuiya, Sura 337 na hivyo kudumisha amani na utulivu katika Taifa letu. 

  1. Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi, 2022 jumla ya maombi ya usajili wa jumuiya 356 yalipokelewa. Kati ya hayo, 224 ni ya Jumuiya za Kidini na 132 ni Jumuiya zisizo za Kidini. Jumla ya jumuiya 268 zilisajiliwa, kati ya jumuiya hizo 169 ni za kidini na 99 zisizo za kidini. Pia, maombi 88 yanaendelea kufanyiwa kazi. Aidha, migogoro mitano (5) ya Jumuiya za Kidini nammoja (1) wa Jumuiya isiyo ya Kidini imesuluhishwa na kuleta utulivu ndani ya jumuiya husika. Natoa wito kwa Viongozi wa Jumuiya za Kidini na Zisizo za Kidini kuzingatia sheria na katiba za jumuiya hizo ili kuepusha migogoro.
  2. Mheshimiwa Spika, katika kipindi husika Wizara imekamilisha ufungaji wa Mfumo wa Ki-elektroniki wa Usajili na Usimamizi wa Jumuiya (Registration of Societies Management Information System – RSMIS). Mfumo husika upo katika hatua ya majaribio na utaanza kutumika Julai, 2022. Pamoja na mambo mengine, mfumo huo utawezesha jumuiya kuwasilisha maombi ya usajili na kuambatisha nyaraka zinazohitajika; Viongozi wa Jumuiya kulipa tozo na ada kwa kutumia mfumo; wadau kupata taarifa za Jumuiya zilizosajiliwa.

Mfumo umeunganishwa na mifumo mingine ya Serikali ya GePG na NIDA.

  1. Mheshimiwa Spika, ufuatiliaji wa uendeshaji wa jumuiya zilizosajiliwa umefanyika katika Mikoa yote ya Tanzania Bara. Katika kutekeleza jukumu hili, Wizara imefanikiwa kukamilisha zoezi la uhakiki wa jumuiya 395. Kupitia zoezi hilo, elimu ilitolewa kuhusu taratibu za usajili na kazi zinazofanywa na Ofisi ya Msajili wa Jumuiya. Aidha, elimu kuhusu usajili na usimamizi wa Jumuiya ilitolewa kwa Wakuu wa Wilaya 59 kwa lengo la kuimarisha utaratibu na mifumo ya usajili na usimamizi wa jumuiya nchini. 
  2. Mheshimiwa Spika, elimu imeendelea kutolewa kwa vikundi vya kiuchumi, wajasiriamali, vijana na wanawake juu ya umuhimu wa kusajiliwa. Hii ni pamoja na kuviwezesha vikundi hivyo kuingia katika mfumo rasmi utakaorahisisha kufikiwa na programu za maendeleo, kupatiwa mafunzo na kunufaika na mikopo yenye riba nafuu kutoka katika taasisi za fedha na wadau wa maendeleo. 
  3. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Wizara itaendelea kusajili, kuhakiki na kukagua jumuiya kwa mujibu wa sheria ili kuhakikisha zinajiendesha kulingana na malengo ya kuanzishwa kwake. Pia, itafanya kampeni za usajili na kutoa elimu sambamba na kushiriki katika maonesho mbalimbali ya kitaifa. Wizara imetenga jumla ya Shilingi 667,910,000 kwa ajili ya kuwezesha shughuli za Ofisi ya Msajili wa Jumuiya.  

UDHIBITI WA USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Kuzuia Usafirishaji haramu wa Binadamu, Sura 432. Hadi kufikia Machi, 2022 Wizara imewaokoa wahanga 182 wa usafirishaji haramu wa binadamu waliokuwa wakitumikishwa kuomba mitaani, kufanya kazi za ndani, kufanya kazi ngumu na kutumikishwa kingono. Kati yao, wahanga 171 waliokolewa hapa nchini, wahanga wawili (2) waliokolewa Kurdistan – Iraq na wahanga tisa (9) waliokolewa nchini Kenya. Aidha, wahanga 153 ni watoto wenye umri chini ya miaka 18 na wahanga 29 wana umri wa zaidi ya miaka 18. 
  2. Mheshimiwa Spika, katika kipindi hicho, kesi 11 za usafirishaji haramu wa binadamu zilizohusisha wahalifu 33 zilifunguliwa. Kati ya kesi hizo, kesi sita

(6) zimeshatolewa uamuzi na wahalifu 13 kuhukumiwa. Vilevile, Wizara kwa kushirikiana na wadau ilitoa huduma muhimu kwa Wahanga 171 waliookolewa. Huduma zilizotolewa ni pamoja na malazi, chakula, matibabu, msaada wa kisheria, msaada wa kisaikolojia, ushauri nasaha, elimu ya ujasiriamali,   stadi       za   maisha   pamoja   na

reintegration package”. Pia, Wizara iliratibu zoezi la kutambua familia za wahanga 102 na kufanikiwa kuwaunganisha wahanga 70 na familia zao.

  • Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022 wadau 543 wakiwemo Mahakimu, Waendesha Mashtaka, Polisi, Maafisa Kazi, Maafisa Uhamiaji, Maafisa Ustawi wa Jamii na watoa huduma kutoka taasisi zisizo za Serikali wamepewa mafunzo ya kupambana na usafirishaji haramu wa binadamu. Mafunzo hayo yalilenga kuboresha mbinu za utambuzi na usimamizi wa wahanga, upelelezi na uendeshaji wa mashtaka yanayohusiana na makosa ya usafirishaji haramu wa binadamu. Mikoa iliyonufaika na mafunzo hayo ni Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Kagera, Kaskazini Unguja, Kigoma, Kilimanjaro, Kusini Unguja, Lindi, Mbeya, Mjini Magharibi, Mtwara, Mwanza, Njombe, Ruvuma na Shinyanga. 
  • Mheshimiwa Spika, udhibiti wa usafirishaji haramu wa binadamu unaenda sambamba na kutoa elimu kwa umma. Elimu hiyo imetolewa kupitia makongamano 9 yaliyofanyika katika Mikoa ya Kagera, Kigoma, Shinyanga na Simiyu.

                Makongamano      hayo     yalihusisha      Madiwani,

Watendaji wa Kata na Vijiji, Wenyeviti wa Vijiji, Wajumbe wa Halmashauri za Vijiji, Viongozi wa

Dini, Wajumbe wa Kamati za Kupinga Ukatili dhidi

ya Wanawake na Watoto, walimu na jamii kwa ujumla. Vilevile, elimu kwa umma imetolewa kupitia vyombo vya habari, semina na maadhimisho ya Siku ya Kupinga Usafirishaji Haramu wa Binadamu Duniani ambayo hufanyika tarehe 30 Julai kila mwaka. 

  • Mheshimiwa Spika, Wizara imefanikiwa kuandaa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kuzuia na Kupambana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu (2021 – 2024) na kufanya marekebisho madogo ya Sheria ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu, Sura 432. Aidha, Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu imejumuishwa rasmi katika muundo wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Pia, maandalizi ya utaratibu wa kitaifa wa kutoa rufaa kwa wahanga (National Referral Mechanism) yanaendelea. Utaratibu huo utaanza kutumika Mei, 2022. Rufaa hiyo itasaidia wahanga kupatiwa huduma muhimu kwa haraka kama matibabu, hifadhi na ushauri nasaha.
  • Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na taasisi nyingine za Serikali, ipo kwenye hatua za kuanzisha majukwaa ya ushirikiano na nchi jirani za Malawi na Msumbiji kwa ajili ya kupambana na usafirishaji haramu wa binadamu. Pia, Wizara kwa kushirikiana na Serikali ya Kenya na Botswana inafanya utaratibu wa kuwarejesha nchini wahanga 5 Raia wa Tanzania waliookolewa katika nchi hizo. 
  • Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Wizara itaanzisha Ofisi ya Sekretarieti Zanzibar na kujenga nyumba salama tatu (3) kwa ajili ya wahanga (Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar). Vilevile, itaendelea kutoa mafunzo kwa wadau na elimu kwa umma; kufanya uchunguzi na operesheni za kubaini mitandao ya biashara haramu ya binadamu na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, kikanda na kijumuiya katika kupambana na usafirishaji haramu wa binadamu. Fedha zilizotengwa kwa mwaka 2022/2023 kwa ajili ya utekelezaji wa kazi hizo ni Shilingi 1,763,867,000. 

HUDUMA KWA WAKIMBIZI

  • Mheshimiwa Spika, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ina jukumu la kusimamia ulinzi na usalama katika kambi na makazi ya wakimbizi, kusimamia utoaji wa huduma muhimu kwa wakimbizi, kuwatafutia wakimbizi suluhisho la kudumu kupitia urejeaji au uhamiaji nchi ya tatu, kupokea maombi ya hifadhi na kuyafanyia maamuzi kupitia Kamati ya Kitaifa ya Maombi ya Hifadhi.
  • Mheshimiwa Spika, Wizara inasimamia na kuratibu shughuli zote zinazohusu wakimbizi nchini kwa mujibu wa Sheria ya Wakimbizi Na. 9 ya mwaka 1998, Sera ya Taifa ya Wakimbizi ya mwaka 2003 pamoja na Mikataba ya Kimataifa na Kikanda ambayo Tanzania imeridhia na ni mwanachama.
  • Mheshimiwa Spika, kwa sasa zipo kambi mbili (2) na makazi matatu (3) ya wakimbizi. Kambi hizo ni Nyarugusu na Nduta zilizopo katika Wilaya za Kasulu na Kibondo mkoani Kigoma. Katika upande wa makazi, kuna makazi ya Katumba na Mishamo yaliyopo Mkoa wa Katavi na makazi ya Ulyankulu mkoani Tabora. Aidha, kuna wakimbizi wanaoishi katika baadhi ya vijiji vya Mkoa wa Kigoma na wengine katika maeneo ya miji kwa vibali na sababu maalum kama vile masomo na matibabu.
  • Mheshimiwa Spika, hadi kufikia tarehe 31 Machi, 2022 Tanzania ilikuwa na jumla ya wakimbizi na waomba hifadhi 257,267. Kati ya hao, wakimbizi wanaoishi katika makambi ni 207,676 na waliopo kwenye makazi ni 27,726. Vilevile, wakimbizi 21,508 wanaishi kwenye baadhi ya vijiji vya Mkoa wa Kigoma, 150 wapo eneo la Chogo mkoani Tanga na 207 wapo katika maeneo ya mijini kwa vibali maalum.

Maombi ya Hifadhi na Suluhisho la Kudumu kwa Wakimbizi

  • Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Machi, 2022 Wizara imepokea maombi ya hifadhi 82. Maombi hayo ni kutoka nchi za Afghanistani (1), Bahrain (1), Burundi (3), Comoro (1), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (2), Ethiopia (2), Kenya (1), Liberia (1), Marekani (1), Somalia (2), Sudani Kusini (2), Syria (4), Uingereza (1), Uganda (50) na Yemeni (10). Waombaji hao wanasubiri kujadiliwa na Kamati ya Kitaifa ya Ustahiki (National Eligilibity Committee) ambayo itakaa mwezi Juni, 2022.
  • Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanzia tarehe 1 Julai, 2021 hadi tarehe 31 Machi, 2022 Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) imefanikiwa kuwarejesha wakimbizi 10,866 wenye asili ya Burundi kwa hiari yao. Aidha, Wizara kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) imewahamishia katika nchi ya tatu (Resettlement) wakimbizi 1,733. Wakimbizi hao wamehamishiwa katika nchi za Australia, Canada, Marekani, Ubelgiji, Ufaransa na Uingereza. 
  • Mheshimiwa Spika, mwezi Desemba, 2021 Wizara imekamilisha zoezi la kuwahamisha wakimbizi 21,240 waliokuwa katika Kambi ya Mtendeli kwenda Kambi ya Nduta. Kwa sasa Kambi ya Mtendeli iliyopo Wilaya ya Kakonko imefungwa.  Utunzaji Mazingira
  • Mheshimiwa Spika, katika jitihada za utunzaji wa mazingira kwenye kambi za wakimbizi na maeneo yanayozunguka kambi hizo jumla ya miti 1,061,732 imepandwa. Hatua hiyo ni utekelezaji wa awali wa mradi unaofadhiliwa na Shirika la Danish Refugee Council (DRC) na kuratibiwa na Mkoa wa Kigoma pamoja na UNHCR.
  • Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi itaongeza jitihada za kuwatafutia wakimbizi suluhisho la kudumu. Jitihada hizo zitaendelea kufanyika kupitia urejeaji wa hiyari na uhamiaji katika nchi ya tatu. Ili kutekeleza shughuli za huduma kwa wakimbizi, Wizara imetenga jumla ya Shilingi 1,031,219,000.

C. SHUKRANI   

  • Mheshimiwa Spika, naomba nitumie nafasi hii kukushukuru wewe binafsi, Naibu Spika, Wenyeviti wa Bunge na Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge kwa kusimamia vema shughuli za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.  
  • Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee natoa shukrani zangu za dhati kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Jumanne A. Sagini na Mbunge wa Jimbo la Butiama kwa kunisaidia kusimamia majukumu ya Wizara. Aidha, ninawashukuru Katibu Mkuu Ndugu Christopher D. Kadio na Naibu Katibu Mkuu Ndugu Kailima Ramadhani kwa kusimamia vema utekelezaji wa kazi za Wizara. 
  • Mheshimiwa Spika, natoa shukrani kwa Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambao ni:

Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Simon N. Sirro; Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Meja Jenerali Suleiman M. Mzee; Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, John W. Masunga; Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna P. Makakala; na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa, Ndugu Ismail H. Rumatila. Viongozi hao kwa kusaidiana na watumishi waliopo chini yao wamesaidia kuendelea kuwepo kwa amani na utulivu nchini na kuwezesha kupatikana kwa mafanikio mbalimbali katika Wizara.

  • Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii pia kuwashukuru wenyeviti wa Bodi wa Mashirika ya Uzalishaji Mali yaliyopo chini ya Wizara. Wenyeviti hao ni Prof. Suffian H. Bukurura wa Shirika la

Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi na Meja Jenerali Mstaafu Raphael M. Muhuga wa Shirika la Magereza. Wenyeviti hao pamoja na wajumbe wa bodi wamekuwa na mchango mkubwa katika kutoa ushauri wa kuboresha utendaji na usimamizi wa mashirika hayo ambayo yameanza kuimarika.

  • Mheshimiwa Spika, nawashukuru Wakurugenzi, Wakurugenzi Wasaidizi, Makamishna, Makamishna Wasaidizi, Wakuu wa Vitengo, Maafisa, Askari na watumishi wote wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kuendelea kutekeleza majukumu ya Wizara. Pia, ninazishukuru Jumuiya za Kidini na zisizo za Kidini, Vyombo vya Habari na wananchi kwa ujumla. 
  • Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, natoa shukrani kwa nchi za Austria, Ujerumani, Jamhuri ya Korea Kusini, Visiwa Vya Shelisheli pamoja na Kampuni na Mashirika ya IOM, UNDP, UNHCR, UNICEF, UNFPA, EU, UN – Women, WFP, TIRA, Buzwagi Gold Mine, North Mara Gold Mine, RECSA kwa kuendelea kutoa misaada ya kifedha, kijamii na kiufundi kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
  • Mheshimiwa Spika, mwisho lakini siyo kwa umuhimu, namshukuru mke wangu na familia yangu kwa ujumla wake, ndugu na jamaa kwa ushirikiano mkubwa wanaonipa katika kutekeleza majukumu yangu. Aidha, ninawashukuru wananchi wa Jimbo la Kikwajuni kwa kuniunga mkono katika kuchangia maendeleo ya jimbo letu.

D. HITIMISHO

222. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2022/2023 Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi itaendelea kuimarisha hali ya amani, usalama na utulivu ili kuwawezesha wananchi kutekeleza shughuli za kijamii na kiuchumi kwa maendeleo ya nchi yetu.

Makadirio ya Ukusanyaji wa Mapato kwa Mwaka 2022/2023

223. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Wizara imewekewa lengo la kukusanya jumla ya Shilingi 407,600,000,000 kutoka kwenye vyanzo mbalimbali. Mikakati iliyowekwa ya ukusanyaji wa mapato ni pamoja na: kufanya uhakiki, ufuatiliaji na ukaguzi wa jumuiya zilizosajiliwa; kununua vitendea kazi ikiwemo magari; kuimarisha mfumo wa kielektroniki unaotumika katika ukusanyaji wa maduhuli; kuendelea kutoka elimu kwa umma; kuhakikisha mashine za kukusanyia mapato (POS) zinatumika katika vituo vyote ambavyo havijaunganishwa na huduma za kibenki pamoja kusimamia maadili nidhamu na uwajibikaji.

Maombi ya Fedha kwa Mwaka 2022/2023

  • Mheshimiwa Spika, kwa heshima na taadhima, naomba sasa Bunge lako liidhinishe Bajeti ya jumla ya Shilingi 1,211,881,077,000 kwa ajili ya Wizara

ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka 2022/2023. Kati ya fedha hizo, Shilingi 471,249,055,000 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo, Shilingi 600,219,122,000 ni Mishahara na Shilingi 140,412,900,000 ni fedha za Miradi ya Maendeleo. Kati ya fedha za maendeleo, Shilingi 133,134,800,000 ni fedha za ndani na Shilingi 7,278,100,000 ni fedha za nje.

  • Mheshimiwa Spika, hotuba hii inapatikana pia kwenye tovuti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambayo ni www.moha.go.tz.  
  • Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

Jedwali Na. 1: Muhtasari wa Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Mwaka 2022/2023

FUNGUJINA LA FUNGUMISHAHARAMATUMIZI MENGINEYOMAENDELEOJUMLA
FEDHA ZA NDANIFEDHA ZA NJE
14Jeshi la Zimamoto na Uokoaji19,363,712,00023,179,623,0009,930,000,000052,473,335,000
28Jeshi la Polisi404,839,753,000296,514,612,00032,000,000,000500,000,000 733,854,365,000
29Jeshi la Magereza116,030,662,00099,253,884,00021,369,600,0000236,654,146,000
51Makao Makuu ya Wizara4,143,623,00011,095,630,0001,200,000,000016,439,253,000
NIDA10,224,764,0005,400,000,00056,400,000,0006,778,100,00078,802,864,000
Jumla Ndogo14,368,387,00016,495,630,00057,600,000,0006,778,100,00095,242,117,000
93Idara ya Uhamiaji45,616,608,00035,805,306,00012,235,200,000093,657,114,000
JUMLA KUU600,219,122,000471,249,055,000133,134,800,0007,278,100,0001,211,881,077,000

90

Jedwali Na. 2:  Malengo ya Ukusanyaji wa Mapato ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa   Mwaka 2022/2023

FUNGUJINA LA FUNGULENGOASILIMIA
14Jeshi la Zimamoto na Uokoaji11,000,000,0002.70
28Jeshi la Polisi94,500,000,00023.18
29Jeshi la Magereza1,500,000,0000.37
51Makao Makuu ya Wizara500,000,0000.12
93Idara ya Uhamiaji300,100,000,00073.63
JUMLA KUU407,600,000,000100.00

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *