WIZARA YA MADINI YAENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU KUKIIMARISHA KITUO CHA JEMOLOJIA

Waziri wa Madini Mhe. Dkt. Dotto Biteko amesema katika kuhamasisha na kuhakikisha shughuli za uongezaji thamani madini nchini zinaimarika, Serikali imeendelea kukiimarisha Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) kwa kuongeza fedha katika Mwaka wa fedha 2022/23 kwa ajili ya kuboresha miundombinu na kununua vifaa vya kujifunzia. Kituo hicho kinatoa mafunzo ya uongezaji thamani madini ikiwemo utambuzi, ukataji, uchongaji, ung’arishaji madini ya vito na utengenezaji wa bidhaa za usonara katika ngazi ya Astashada na Stashahada. Lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa vijana wengi wanapata ujuzi katika nyanja hizo na kuwaongezea fursa za kupata ajira au kujiajiri.
“Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia STAMICO imejenga na kusimika miundombinu na mtambo wa kuzalisha makaa ya mawe kwa matumizi ya nyumbani (coal briquettes) katika eneo la TIRDO – Dar es Salaam. Uzalishaji wa majaribio ulifanyika kwa ufanisi. Aidha, Shirika limeagiza mitambo miwili (2)”


Ameongeza kuwa, Biashara ya madini nchini imeendelea kuimarika ambapo katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi 2022 jumla ya kilogramu 39,682.94 za dhahabu, kilogramu 7,102.96 za fedha, karati 155,117.10 za almasi, kilogramu 15,377.44 za Tanzanite ghafi, kilogramu 130,582.28 za Tanzanite za ubora wa chini (beads), karati 81,305.42 za tanzanite iliyokatwa na kusanifiwa, tani 19,355.13 za madini ya shaba na tani 322.49 za madini ya bati zilizalishwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *