
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Dkt. Philip Mpango leo tarehe 29 Aprili 2022 akiwasili katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta uliopo Nairobi nchini Kenya
alipoenda kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya kitaifa ya aliyekuwa
Rais wa Tatu wa Jamhuri ya Kenya ,Hayati Mwai Kibaki. Makamu wa
Rais ameongozana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi(CCM-Bara) Komredi Abdulrahman Kinana

