SERIKALI ILIVYOJIPANGA KUBORESHA UTENDAJI WA TMA, YATOA WITO KWA WADAU KUTIMIZA TAKWA LA KISHERIA LA KUCHANGIA HUDUMA.

NA NOEL RUKANUGA,

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa (Mb) ametoa wito kwa wadau wanaotumia huduma za hali ya hewa kibiashara kuhakikisha wanatimiza takwa la kisheria la kuchangia huduma hizo.

Akizungumza jijini Dodoma hivi karibuni katika Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Profesa Mbarawa, amesema kuwa “Kuchangia huduma za hali ya hewa ni suala la kisheria, hivyo kila mdau hana budi kulitekeleza.

Prof. Mbarawa ameseama kuwa wakati serikali inatekeleza jukumu hilo, ametoa wito pia kwa wadau wanaotumia huduma hizo kibiashara kuhakikisha wanatimiza takwa hilo la kisheria la kuchangia huduma za hali ya hewa ili ziweze kuboreshwa zaidi.

Katika hatua nyingine Mhe. Prof. Mbarawa aliwapongeza wadau wote walio onesha ushirikiano kwa kujitokeza kusajili vituo vyao na kuchangia gharama za utoaji huduma mahususi zinazotolewa katika sekta zao na hivyo kukidhi matakwa ya Sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Na. 2 ya mwaka 2019 pamoja na kanuni zake.

Amewaelekeza TMA kuongeza juhudi na kuhakikisha sekta zote ambazo hawajaanza kuchangia huduma za hali ya hewa wanachangia kama sheria inavyoelekeza. Prof. Mbarawa aliwapongeza TMA kwa kuiwakilisha vyema nchi katika shughuli za hali ya hewa kimataifa na kuendelea kushikilia cheti cha ubora cha ISO 9001-2015.

Katika kutatua changamoto zinazoikabili TMA, Prof. Mbarawa aliahidi Wizara kuendelea kuiwezesha Mamlaka kupitia fedha za Miradi ya Maendeleo ili kuhakikisha miundo mbinu ya hali ya hewa inaboreshwa.

Ameongeza kuwa maslahi ya watumishi pia yataboreshwa, hivyo aliwataka wataalamu wa hali ya hewa kuendelea kufanya kazi kwa bidii wakati serikali inashughulikia uboreshaji wa maslahi.

Amesema kuwa amefurahi kusikia kwamba Baraza hilo lina wajumbe kutoka vituo vyote vya Hali ya Hewa Tanzania Bara na Zanzibar kwa kuzingatia muundo wa mkataba wa Baraza.

Ameeleza hilo inaonesha jinsi mawazo yao yapo  kwa pamoja yanavyotumika katika kuboresha huduma wanazotoa na kupelekea mafanikio makubwa ambayo mnaendelea kuyapata.

“Mmenifahamisha kuhusiana na changamoto mbalimbali zikiwemo zile za maslahi duni,  vifaa vya hali ya hewa na usafiri ili kuwezesha utekelezaji wa udhibiti na uratibu wa shughuli za hali ya hewa. Wizara itaendelea kuiwezesha Mamlaka kupitia fedha za Miradi ya Maendeleo ili kutatua changamoto hizo na hivyo kuwezesha utekelezaji wa majukumu yenu kwa ufanisi » amesema.

Imeelezwa kuwaMamlaka inaendelea na zoezi la kuimarisha mtandao wa Rada nchini, kwani ni jambo jema na ni vizuri likaendelea kufanyika kwa ufanisi wa hali ya juu sana.

Amesema kuwa TMA kulifanyia kazi Majadiliano yajikite kuwaelimisha wadau kuitekeleza Sheria na  kuchangia huduma kwani ni suala la kisheria hivyo kila mdau hana budi kulitekeleza.

Amebainisha kuwa ni vyema kuhakikisha wanaendelea kukusanya mapato kwenye maeneo yote yaliyoainishwa na sheria kwamba yanazitumia huduma za hali ya hewa kibiashara.

Ameeleza kwa serikali ni mdau mkubwa katika huduma zitolewazo kwa jamii (Public Good), wakati Serikali inatekeleza jukumu hilo wadau wanaotumia huduma kibiashara nao pia watekeleze wajibu wao wa kuchangia huduma ili huduma zote zitolewazo kwa jamii na kwa sekta za kiuchumi na kibiashara ziboreshwe.

Amesema kuwa Baraza liweke mkakati wa makusudi wa kukusanya mapato, uku akieleza kuwa kuhusu changamoto ya maslahi duni, Wizara yake kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais – UTUMISHI inalishughulikia na ninawaahidi taratibu zikikamilika maslahi ya watumishi ikiwemo mishahara itaboreshwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *