
1
HOTUBA YA WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA, MHESHIMIWA. DKT.
DAMAS DANIEL NDUMBARO (MB), WAKATI AKIWASILISHA
BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA
MWAKA WA FEDHA 2022/2023
A. UTANGULIZI
- Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa zilizowasilishwa leo katika
Bunge lako na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na
Sheria na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, naomba
kutoa hoja kwamba Bunge lako sasa likubali kupokea, kujadili na kupitisha
Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya
Katiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023.
Salamu za Pongezi, Shukrani na Pole - Mheshimiwa Spika, awali ya yote nimshukuru Mwenyezi Mungu
mwingi wa rehema kwa kutujalia afya njema na kutuwezesha kukutana
hapa leo kwa ajili ya kujadili taarifa ya mapitio ya utekelezaji wa mpango na
bajeti kwa mwaka wa fedha 2021/2022 na mwelekeo wa mpango na bajeti
ya Wizara na Taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2022/2023. Aidha,
ninaomba kuwatakia heri ya Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani
kwa Waislamu wote. Vilevile, nitumie fursa hii kuwatakia wananchi wote
kheri ya sikukuu ya Eid. - Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee naomba nichukue fursa hii
kumpongeza Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, kwa kutimiza mwaka
mmoja tangu ashike nafasi ya kuongoza nchi yetu akiwa Rais wa Awamu
ya Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika kipindi hicho,
2
tumeshuhudia mafanikio makubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta
ya sheria. Naomba niungane na Waheshimiwa Wabunge na Wananchi
wenzangu kuendelea kumuombea Rais wetu kwa Mwenyezi Mungu
amjaalie kila la kheri katika kuliongoza Taifa letu la Tanzania. - Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii pia kuwapongeza Mheshimiwa
Dkt. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Mheshimiwa Kassim Majaliwa
Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa
uongozi wao mahiri katika kulitumikia Taifa letu. - Mheshimiwa Spika, naomba nichukue nafasi hii kukupongeza wewe
binafsi Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kwa kuchaguliwa kwako na Bunge na kwa kupata ushindi wa kishindo.
Kuchaguliwa kwako kunaonesha imani kubwa waliyonayo Wabunge ya
kuliongoza Bunge hili kwa umahiri mkubwa. Aidha, nimpongeze
Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu (Mb.), kwa kuchaguliwa kuwa Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Vilevile,
niwapongeze Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na
Sheria Mheshimiwa Dkt. Joseph Kizito Mhagama, Mbunge wa Madaba na
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mheshimiwa Sillo
Daniel Baran, Mbunge wa Babati Vijijini, Makamu Wenyeviti pamoja na
Wajumbe wa Kamati hizo mbili kwa ushauri na maelekezo ambayo
yamewezesha Wizara na Taasisi zake kutekeleza majukumu yake kwa
ufanisi.
3 - Mheshimiwa Spika, Nitumie fursa hii kuwapongeza Mheshimiwa
Emmanuel Lekishon Shangai (Mb.) kwa kuchaguliwa kuwa Mbunge wa
Jimbo la Ngorongoro na Mheshimiwa Shamsi Vuai Nahodha (Mb.) kwa
kuteuliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ni matumaini yangu kuwa Wabunge hao watashirikiana na Wabunge
wengine katika kutekeleza majukumu yao. - Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee, nichukue fursa hii
kumshukuru Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuniamini na kuniteua kuiongoza
Wizara hii ya Katiba na Sheria. Ninaahidi kuendelea kuitumikia nafasi hii
kwa uaminifu na uadilifu ili kuwaletea maendeleo wananchi na Taifa kwa
ujumla. Aidha, namshukuru na kumpongeza kwa dhati mtangulizi wangu
Mheshimiwa George Boniface Simbachawene, Mbunge wa Kibakwe na
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) kwa
kuingoza Wizara hii kwa umahiri. Vilevile, nimpongeze Mheshimiwa Balozi
Dkt. Pindi Hazara Chana (Mb.), kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na
Utalii. - Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/2022 Bunge lako
lilipoteza Waheshimiwa Wabunge ambao tulikuwa nao katika Bunge hili.
Wabunge hao ni Mheshimiwa William Tate Olenasha, aliyekuwa Mbunge
wa Ngorongoro na Mheshimiwa Irene Alex Ndyamkama, aliyekuwa
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Rukwa. Hivyo, naomba nitumie
fursa hii kutuma salamu zangu za pole kwako wewe binafsi Mheshimiwa
Spika, Bunge lako kwa ujumla, ndugu na wananchi wa majimbo husika
waliopoteza wapendwa wao. Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu
hao mahala pema peponi. Amina.
4
B. DIRA NA DHIMA - Mheshimiwa Spika, Wizara ya Katiba na Sheria inaongozwa na Dira
ambayo ni Katiba na Sheria wezeshi kwa maendeleo ya Taifa. Dira
inalenga kuweka mazingira rafiki ya kisera na ya kisheria ya kuwezesha
utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Taifa, kudumisha hali ya amani,
utulivu na utangamano wa kitaifa ambazo ni nguzo muhimu kwa mstakabali
wa Taifa letu. Aidha, Dhima ya Wizara ni Kuwa na mfumo madhubuti wa
Kikatiba na Sheria wenye kufanikisha utekelezaji wa sera na mipango kwa
maendeleo ya Taifa. Dhima hii inahimiza ubunifu katika kujenga mazingira
wezeshi ya upatikanaji haki na huduma bora za kisheria kwa wananchi.
Aidha, Dira na Dhima hii imeakisiwa katika Dira na Dhima za Taasisi.
C. MUUNDO NA MAJUKUMU YA WIZARA - Mheshimiwa Spika, Wizara ya Katiba na Sheria inajumuisha Mhimili
wa Mahakama ya Tanzania, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi
ya Taifa ya Mashtaka, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Wakala wa Usajili
Ufilisi na Udhamini, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tume ya
Kurekebisha Sheria Tanzania, Tume ya Utumishi wa Mahakama, Taasisi
ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania na Chuo cha Uongozi
wa Mahakama-Lushoto. Katika kutekeleza majukumu yake ya kuhakikisha
kuwa nchi inaongozwa kwa kuzingatia Katiba, sheria, Kanuni na taratibu
zilizowekwa na vyombo halali vya maamuzi, Wizara imeendelea kutekeleza
majukumu yake kama yalivyoainishwa katika Hati ya Mgawanyo wa
Majukumu kwa Mawaziri, kupitia Tangazo la Serikali Na. 534/2021
majukumu hayo ni: –
5
(i.) Kutunga Sera zinazohusu masuala ya kisheria na kusimamia
utekelezaji wake;
(ii.) Kushughulikia mambo ya kikatiba;
(iii.) Kusimamia mfumo wa haki na utoaji haki;
(iv.) Uandishi wa sheria;
(v.) Kuendesha mashtaka ya jinai;
(vi.) Kushughulikia uendeshaji wa mashauri ya madai na
usuluhishi;
(vii.) Usuluhishi wa migogoro ya kibiashara, Sheria za kimataifa na
Mikataba;
(viii.) Kuratibu masuala ya haki za binadamu na utoaji wa huduma
ya msaada wa kisheria;
(ix.) Kuratibu shughuli za usajili wa matukio muhimu ya binadamu,
ufilisi na udhamini;
(x.) Kuratibu tathmini na maboresho ya Sheria;
(xi.) Kuratibu ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa Sheria za
Utajiri na Maliasilia za nchi;
(xii.) Kushughulikia urejeshwaji wa wahalifu na masuala ya
ushirikiano wa kimataifa kwenye makosa ya jinai;
(xiii.) Kuboresha utendaji na maendeleo ya rasilimali watu iliyo chini
ya Wizara; na
(xiv.) Kuratibu shughuli za taasisi, mipango na miradi chini ya
Wizara.
6
D. UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA WA
FEDHA 2021/2022 - Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara kwa
mwaka wa fedha 2021/2022 umezingatia miongozo mbalimbali ya kisera
ya Kitaifa, kikanda na kimataifa. Miongozo hiyo ni pamoja na Dira ya
Maendeleo ya Taifa ya Mwaka 2025; Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa
Taifa wa miaka Mitano 2021/22- 2025/26 ambao unalenga kujenga uchumi
shindani na viwanda kwa maendeleo ya watu; Ilani ya Uchaguzi ya Chama
cha Mapinduzi ya mwaka 2020 hadi 2025; Maelekezo ya Mheshimiwa
Samia Suluhu Hassan, Rais wa Awamu ya Sita wa Jamhuri wa Muungano
wa Tanzania aliyoyatoa wakati akihutubia Bunge la 12 la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania mwezi Aprili, 2021 pamoja na maelekezo ya
viongozi wakuu wa Serikali. Aidha, Wizara inazingatia Malengo ya
Maendeleo Endelevu ya Dunia 2030; Ajenda ya Maendeleo ya Afrika 2063;
Mpango Mkakati wa SADC wa Maendeleo 2020-2030; Mpango Mkakati wa
Jumuia ya Afrika Mashariki wa Maendeleo 2021/2022 – 2025/2026; pamoja
na Mpango Mkakati wa Wizara wa mwaka 2021/22-2025/26. - Mheshimiwa Spika, kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa
Fedha 2021/2022, Wizara na Taasisi zake ilibainisha masuala mahsusi
ya kipaumbele kuwa msingi wa kutekeleza majukumu yake. Utekelezaji
wa majukumu ya Wizara ni kama ifuatavyo:-
7
I. Kushughulikia Masuala ya Kisera ya Sekta ya Sheria na Kusimamia
Utekelezaji wake - Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuratibu masuala ya kisera
na kikatiba ili kuhakikisha kuwa haki inafikiwa na inapatikana kwa wakati na
gharama nafuu. Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022 Wizara
iliendelea kuimarisha, kusimamia na kuratibu mfumo wa utatuzi wa
migogoro kwa njia mbadala ndani na nje ya mfumo wa Mahakama. Wizara
ilisimamia kutungwa kwa Sheria ya Usuluhishi, Sura ya 15 na Marekebisho
ya Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Daawa, Sura ya 33. Sheria hizi
zinaweka misingi ya utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi,
upatanishi, majadiliano na maridhiano. Aidha, Waziri mwenye dhamana na
masuala ya Sheria alitengeneza Kanuni za Sheria hizo ili kuwezesha utoaji
haki kwa wakati, kupunguza gharama za uendeshaji mashauri, mlundikano
wa mashauri na kurahisisha ufikiaji wa haki. Kanuni hizo zimeweka misingi
ya ithibati ya watoa huduma za utatuzi wa migogoro na utambuzi wao.
Vilevile, Wizara imefanikisha kuweka mfumo wa usajili wa Watatuzi wa
migogoro kwa njia mbadala ambapo, jumla ya Wasuluhishi 192,
Wapatanishi 106, Waendesha majadiliano 37 na Waendesha
Maridhiano 23, walisajiliwa na kupatiwa vyeti. - Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na Wadau wa Sekta
imeratibu zoezi la maandalizi ya Sera ya Taifa ya Mashtaka ambapo
Andiko la Mapendekezo ya kutunga sera hiyo limekamilika. Sera hiyo
inalenga kuimarisha huduma za uendeshaji wa Mashtaka ya jinai nchini ili
kuhakikisha Serikali inaimarisha hali ya amani na usalama katika jamii.
Vilevile, Wizara iliandaa rasimu ya Kanuni za Sheria ya Kuwalinda
Mashahidi na Watoa Taarifa za Uhalifu (Sura 446).
8 - Mheshimiwa Spika, Kuhusu masuala ya ufuatiliaji haki, Wizara
imeendelea kuratibu masuala ya kisera yanayohusu utoaji haki kwa
kutembelea na kukagua maeneo ya vizuizi ikiwemo Magereza, Mahabusu
za watoto na vituo vya Polisi. Aidha, Wizara ilitembelea Mahakama Kuu,
Mahakama za Wilaya na Mahakama za Mwanzo pamoja na vituo jumuishi
vya utoaji haki vya Mahakama. Lengo la kaguzi hizi ni kufuatilia utekelezaji
wa haki, kuainisha changamoto za kiutendaji na kiupelelezi na kutoa
maelekezo stahiki ya kutatua changamoto hizo. Wizara ilikagua utendaji
kazi wa Taasisi hizo ili kubaini endapo unazingatia misingi ya Utawala
Bora, Utawala wa Sheria na utoaji haki kwa wananchi. Katika kipindi cha
Julai, 2021 hadi Machi, 2022 jumla ya magereza 129 yalikaguliwa
ikilinganishwa na magereza 64 yaliyokaguliwa kipindi cha Julai, 2020 hadi
Machi, 2021. Aidha, vituo vya polisi 391 vilikaguliwa ikilinganishwa na vituo
vya polisi 180 vilivyokaguliwa katika kipindi cha Julai, 2020 hadi Machi, - Zoezi hilo la ukaguzi wa maeneo ya vizuizi umewezesha kupunguza
mlundikano wa Mahabusi kwa kuwaachia huru jumla ya Mahabusi 809.
Kwa upande wa Zanzibar vyuo vya mafunzo tisa (9) na vituo vya polisi 17
vilikaguliwa katika mikoa yote ya Zanzibar. Orodha ya vituo vya Polisi na
Magereza vilivyokaguliwa na idadi ya Mahabusi walioachiwa huru kwa kila
Mkoa imeoneshwa katika Kiambatisho A. - Mheshimiwa Spika, Matokeo ya ukaguzi yalionesha kuwa hali ya
magereza na vyuo vya mafunzo inaendelea kuboreshwa kwa kuzingatia
vigezo vya haki za binadamu ikilinganishwa na kaguzi zilizopita. Maeneo
yaliyoboreshwa ni pamoja na haki ya kupata chakula, malazi, afya na haki
ya kupata habari. Aidha, kutokana na mapendekezo ya taarifa ya tathmini
jitihada zinaendelea kufanyika ili kuboresha hali ya uzingatiwaji wa haki za
9
binadamu katika maeneo hayo.
II. Kusimamia mfumo wa haki na utoaji haki
(a) Usikilizwaji wa Mashauri - Mheshimiwa Spika, kwa muda mrefu suala la kupunguza
mlundikano wa mashauri mahakamani limekuwa ni moja ya vipaumbele
muhimu vya Serikali katika kuhakikisha kuwa wananchi wote wanapata
haki sawa na kwa wakati. Kwa kipindi cha kuanzia Mwezi Julai 2021-
Machi, 2022 kulikuwa na Jumla ya mashauri 241,793. Kati ya mashauri
hayo mashauri 178,877 (sawa na asilimia 74) yalisikilizwa na kuhitimishwa.
Mahakama inendelea na mipango ya kuboresha matumizi ya TEHAMA ili
kuongeza kasi ya kuhitimisha usikilizwaji wa mashauri.
(b) Kuboresha Miundombinu ya Utoaji Haki - Mheshimiwa Spika, Mahakama imeendelea na utekelezaji wa
Mpango wa Miaka Mitano (2021/22 – 2025/26) wa Ujenzi na Ukarabati wa
Miundombinu ya Mahakama, ambapo katika mwaka 2021/2022 miradi 37
ilitekelezwa katika ngazi mbalimbali za Mahakama. Hadi kufikia Machi,
2022 miradi imefikia katika hatua mbalimbali za utekelezaji kama ifuatavyo:
i. Miradi iliyokamilika; Ujenzi wa vituo Jumuishi sita (6) vya kutoa haki
(IJCs) katika mikoa ya Dar es salaam (Kinondoni na Temeke),
Dodoma, Morogoro, Mwanza na Arusha; Ujenzi wa Mahakama za
Hakimu Mkazi mbili (2) katika Mikoa ya Katavi na Lindi; ujenzi wa
Mahakama za Wilaya nne (4) katika wilaya za Bahi, Chemba, Rungwe
na Bunda; ujenzi wa Mahakama za mwanzo tatu (3) za Matiri
(Mbinga), Hydom (Mbulu), na Kibaigwa (Kongwa) na ujenzi wa Jengo
10
la Kuhifadhia Kumbukumbu – Tanga.
ii. Miradi inayoendelea; ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Mahakama
Dodoma ambapo ujenzi wa boma (structure) umekamilika kwa asilimia
100; Ukarabati na upanuzi wa Mahakama Kuu Tabora; ujenzi wa
Mahakama za Hakimu Mkazi katika Mikoa ya Songwe na Tabora;
Ujenzi wa Mahakama za Wilaya za Nanyumbu, Namtumbo, Same,
Tandahimba, Kilindi, Sikonge, Mwanga, Kakonko, Buhigwe, Uvinza,
Butiama, Rorya, Itilima, Busega, Songwe, Mbogwe, Nyang’wale,
Kyerwa, Misenyi, Gairo, Mvomero, Kilombero, Mkinga, Tanganyika na
Kaliua. Miradi mingine inayoendelea ni ujenzi wa Mahakama za
mwanzo Mang’ula na Mlimba (Morogoro), Nyakibimbili (Bukoba),
Kabanga (Ngara), Chanika (DSM), na Kimbe (Kilindi); na Ujenzi wa
bweni la wavulana katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama – Lushoto. - Mheshimiwa Spika, Mahakama imeendelea kuanzisha na
kuboresha mifumo ya utoaji haki kwa kutumia TEHAMA. Hadi kufikia Machi
2022, Mahakama imeanzisha mfumo wa ‘SEMA NA MAHAKAMA’ wenye
lengo la kupata mrejesho wa huduma zitolewazo, malalamiko na
mapendekezo. Aidha, Mfumo wa Madalali wa Mahakama umeanzishwa
wenye lengo la kuwasajili, kuwasimamia na kuwatambua. Vilevile,
Mahakama imefanya maboresho mbalimbali katika mifumo ifuatayo:
Mfumo wa kielektroniki wa usimamizi na uendeshaji wa mashauri (Judicial
Statistical Dashboard System – JSDS II); Mfumo wa Mkutano Mtandao
(Video Conferencing) unaowezesha kuendesha mashauri kwa njia ya
mtandao; Mfumo wa kielektroniki wa kusajili na kuwatambua mawakili (eWakili); Mfumo wa kutambua Viwanja na Majengo ya Mahakama (JMap)
wenye lengo la kutambua hali halisi ya majengo na viwanja vya mahakama
11
ili kuwezesha uandaaji wa mpango wa ujenzi na ukarabati wa majengo ya
mahakama nchi nzima; na Mfumo wa kuratibu na kuhifadhi taarifa za mali
na vitendea kazi Mahakamani.
III. Uandishi, Urekebu na Ufasiri wa Sheria - Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali imeendelea kuhakikisha kuwa sheria za nchi zinakwenda na wakati
na zinaakisi sera na vipaumbele vya Serikali katika nyanja za kisiasa,
kiuchumi, kijamii, kiutamaduni, mazingira na teknolojia. Katika kipindi cha
Julai 2021, hadi Machi, 2022, miswada ya sheria 11 iliandaliwa
ikilinganishwa na Miswada mitatu (3) iliyoandaliwa katika kipindi cha Julai,
2020 hadi Machi, 2021 sawa na ongezeko la asilimia 267. Miswada
iliyoandaliwa ni kama ilivyooneshwa kwenye Kiambatisho Na. B. Aidha,
Miswada hiyo 11 iliwasilishwa Bungeni na kusomwa kwa mara ya pili na ya
tatu. Kati ya Miswada hiyo, tisa (9) imesainiwa na Mhe. Rais kuwa sheria
na kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali kama inavyoonekana kwenye
Kiambatisho C. Aidha, Sheria Ndogo 542 ziliandaliwa na kuchapishwa
katika Gazeti la Serikali au kutumika kama ilivyokusudiwa ikilinganishwa na
sheria ndogo 807 zilizoandaliwa katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi,
2022 sawa na upungufu wa asilimia 33. Upungufu huo ulitokana na
kupungua kwa maombi yaliyopokelewa ya kuandaa Sheria ndogo. - Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na Wadau imeendelea
na zoezi la kutafsiri sheria kutoka Lugha ya Kingereza kwenda Lugha ya
Kiswahili. Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022 kupitia zoezi hili
jumla ya Sheria Kuu 214 zilitafsiriwa kwa hatua ya rasimu ya kwanza.
Sheria kuu zilizofanyiwa ufasiri zimeoneshwa kwenye Kiambatisho Na. D.
Ongezeko hili limetokana na kutekeleza maagizo ya Serikali kuwa
12
Mahakama zote nchini ziendeshe mashauri na kutoa hukumu katika lugha
ya Kiswahili. Aidha, katika kipindi hicho, Wizara kupitia Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ilifanya urekebu wa Sheria Kuu 46 kama
inavyoonekana kwenye Kiambatisho E.
IV. Usimamizi wa Masuala ya Mikataba - Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, imeendelea kushiriki na kutoa ushauri wa kisheria katika
majadiliano mbalimbali ya Mikataba ya kibishara, mikutano ya kitaifa,
kikanda na kimataifa. Katika kipindi cha Julai, 2021, hadi Machi, 2022 jumla
ya Mikataba 1,171 ilifanyiwa upekuzi ikilinganishwa na Mikataba 713 katika
kipindi cha Julai, 2020 hadi Machi, 2021 sawa na ongezeko la asilimia 64.
Ongezo hili linatokana na ongezeko la miradi inayotekelezwa na Serikali.
Mikataba hiyo ilihusisha masuala ya ununuzi, ujenzi na ukarabati wa
majengo, utoaji wa huduma za jamii kama vile ujenzi wa shule, hospitali na
barabara. Kati ya mikataba hiyo 1,171 mikataba 511 ilithaminishwa katika
sarafu mbalimbali katika mchanganuo ufuatao: Mikataba 407 ilikuwa na
thamani ya Shilingi Trilioni 116.69; Mikataba 88 ilikuwa na thamani ya
Dola za Marekani 3,254,993,763.98 sawa na Shilingi Trilioni 7.44; na
Mikataba 16 ilikuwa na thamani ya fedha ya Jumuiya ya Ulaya (Euro)
360,569,062.16 sawa na Shilingi Trilioni 0.92.
V. Utoaji wa Ushauri wa Kisheria - Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali ina jukumu la kutoa ushauri wa kisheria kwa Wizara, Idara
zinazojitegemea, Mashirika ya Umma, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa na kwa wananchi. Lengo ni kuhakikisha ushauri unaotolewa
unazingatia maslahi ya umma na kusaidia Serikali kutoingia kwenye
13
migogoro kwa kuhakikisha sheria, kanuni na taratibu za nchi zinafuatwa.
Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022 jumla ya maombi ya
ushauri wa kisheria 1,129 yalipokelewa na kufanyiwa kazi ikilinganishwa na
maombi 768 katika kipindi cha Julai, 2020 hadi Machi, 2021 sawa na
ongezeko la asilimia 47. Kati ya maombi 1,129, maombi 472 yalihusu
maombi ya wananchi 657 yanatoka katika Wizara, Idara zinazojitegemea,
Mashirika ya Umma, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa. Kuongezeka kwa
maombi ya watu binafsi kunatokana na mwamko wa wananchi wanaoupata
katika maadhimisho mbalimbali ikiwemo Wiki ya Sheria, Wiki ya Msaada
wa Kisheria pamoja na makongamano mengine ya kisheria. - Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali ilishiriki katika mikutano 402 ya ndani ya nchi ikilinganishwa na
mikutano 149 katika kipindi cha Julai, 2020 hadi Machi, 2021 sawa na
ongezeko la asilimia 170. Aidha, Ofisi ilishiriki katika mikutano 57
inayohusu masuala ya Kikanda na Kimataifa ikiwemo mikutano ya Jumuiya
ya Maendeleo ya Nchi zilizopo Kusini mwa Afrika (SADC), Jumuiya ya
Afrika Mashariki (EAC) na Umoja wa Mataifa (UN).
VI. Kuendesha Mashtaka ya Jinai - Mheshimiwa Spika, Katika kulinda misingi ya utawala wa sheria
ambayo ni nguzo muhimu ya kudumisha amani, utulivu na umoja wa
kitaifa, Wizara kupitia Ofisi ya Taifa ya Mashtaka iliendelea kuratibu
shughuli za upelelezi wa makosa ya jinai, kufungua na kuendesha
mashauri ya jinai mahakamani. Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi,
2022 Wizara kupitia Ofisi ya Taifa ya Mashtaka iliendesha mashauri ya jinai
katika Mahakama za Wilaya, Hakimu Mkazi, Mahakama Kuu na
Mahakama ya Rufani ambapo Jumla ya mashauri ya jinai 42,138
14
yaliendeshwa ikilinganishwa na mashauri 26,993 yaliyoendeshwa katika
kipindi cha Julai, 2020 hadi Machi, 2021. Katika kipindi hiki, mashauri
11,676 sawa na asilimia 28 yalihitimishwa ikilinganishwa na mashauri
12,745 sawa na asilimia 47 ya mashauri yaliyohitimishwa katika kipindi cha
Julai, 2020 hadi Machi, 2021. Kati ya mashauri yaliyohitimishwa, 7,117
yalihitimishwa kwa washtakiwa kutiwa hatiani sawa na asilimia 61
ikilinganishwa na mashauri 6,558 sawa na asilimia 52 zilizohitimishwa kwa
kipindi cha kuanzia Julai, 2020 hadi Machi, 2021 na mashauri 30,462 sawa
na asilimia 72 ya mashauri yaliyoendeshwa, yalikuwa yanaendelea
mahakamani katika hatua mbalimbali ikilinganishwa na mashauri 14,248
sawa na asilimia 53 ya mashauri yaliyoendeshwa, yaliyokuwa
yanaendelea katika kipindi cha Julai, 2020 hadi Machi, 2021. Katika kipindi
cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022, Ofisi iliendesha jumla ya mashauri 871
katika Mahakama za watoto (Juvenile Courts) ambapo mashauri 315
yalihitimishwa na mashauri 556 yapo katika hatua mbalimbali mahakamani. - Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Ofisi ya Taifa ya Mashtaka pia
imeendelea kushughulikia masuala ya rushwa kwa kushirikiana na Taasisi
ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU). Katika kipindi husika
Ofisi ilifanya kikao na vyombo vya upelelezi ambavyo ni TAKUKURU na
Jeshi la Polisi ambapo majalada 28 ya mashauri za rushwa yalifanyiwa
mapitio na majalada 14 yaliandaliwa Hati za Mashtaka, majalada sita (6)
yalirudishwa kwa ajili ya upelelezi zaidi katika maeneo yaliyobainika kuwa
na mapungufu, jalada moja (1) lilifungwa kwa kukosa ushahidi na majalada
mengine saba (7) yanaendelea kufanyiwa kazi. Washtakiwa waliotiwa
hatiani walipewa adhabu mbalimbali zikiwemo vifungo, faini na mali
mbalimbali zilitaifishwa. Kiasi cha Shilingi 1,262,893,030.09 kililipwa
15
mahakamani kama faini katika mashauri 3,895 ikilinganishwa na Shilingi
1,025,498,746.00 zilizolipwa kwenye mashauri 4,211 katika kipindi cha
Julai, 2020 hadi Machi, 2021. Aidha, mali mbalimbali zilitaifishwa na
Serikali ikiwa ni pamoja na fedha taslim kiasi cha Shilingi 321,068,400,
Dola za Marekani 5,000, nyumba tatu (3), matrekta 24, magari 11, pikipiki
tano (5), ng’ombe 25, sukari kilo 238, madini aina ya Almasi Karati 11 na
vitendea kazi mbalimbali. - Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Ofisi ya Taifa ya Mashtaka
imeendelea kutekeleza Progamu ya kutenganisha shughuli za upelelezi na
uendeshaji mashtaka kwa kusogeza huduma za mashtaka karibu na
wananchi katika ngazi za Mikoa na Wilaya. Katika kipindi cha Julai, 2021
hadi Machi, 2022 Ofisi za Mikoa Mitatu (3) ya kimashtaka ya Kinondoni,
Temeke na Ilala (Kinyerezi) zilifunguliwa. Vilevile uzinduzi wa jengo la Ofisi
la Wilaya ya Serengeti mkoa wa Mara na hivyo kufanya jumla ya Ofisi za
Mikoa ya kimashtaka kuwa 29 na Ofisi za Wilaya zilizofunguliwa kuwa 14.
VII. Kushughulikia Uendeshaji wa Mashauri ya Madai na Usuluhishi - Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali
imeendelea kuiwakilisha Serikali na Taasisi zake kwenye mashauri ya
Madai na Usuluhishi yaliyofunguliwa na au dhidi ya Serikali kwenye
Mahakama na Mabaraza mbalimbali ya usuluhishi ndani na nje ya nchi.
Katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022 Wizara kupitia Ofisi ya
Wakili Mkuu wa Serikali iliendesha mashauri 701 ambapo mashauri ya
madai 590 na mashauri ya usuluhishi 111 ikilinganishwa na Mashauri 543
yaliyoendeshwa katika kipindi cha kuanzia Julai 2020 hadi kufikia Machi
2021 sawa na ongezeko la asilimia 29. Kati ya mashauri 701
yaliyoendeshwa, mashauri 247 yalihitimishwa ambapo Serikali ilishinda
16
mashauri 221 na kuokoa Shilingi Bilioni 236.6.
VIII. Kuratibu Masuala ya Haki za Binadamu na Utoaji wa huduma ya
msaada wa kisheria
(a) Kuratibu Masuala ya Haki za Binadamu na Haki za Watu - Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuratibu masuala ya kisera
yanayohusu, kukuza, kulinda na kuhifadhi misingi ya haki za binadamu.
Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022, Wizara iliwasilisha Taarifa
ya nchi chini ya Mfumo wa Mapitio katika kipindi Maalum ambapo kila nchi
mwanachama anafanyiwa tathmini ya hali ya haki za binadamu kila baada
ya miaka minne. Taarifa ya Nchi ilijadiliwa katika Kikao cha Baraza la Haki
za Binadamu la Umoja wa Mataifa kilichofanyika Geneva, Novemba, 2021.
Katika kikao hicho Wizara ilitoa taarifa kuhusu jitihada za Serikali katika
kukuza, kuheshimu na kulinda haki za kisiasa, kiraia, kiuchumi,
kiutamaduni na kijamii kama ifuatavyo: –
i. Kuhusu Haki ya Kisiasa, taarifa ilibainisha kuwa uchaguzi mkuu wa
Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2020 ulifanyika kwa amani na
utulivu,
ii. Kuhusu haki za kiraia Serikali ilieleza kwamba ilifanya majadiliano na
vyombo vya Habari ili kuimarisha haki ya uhuru wa kujieleza kwa
kuboresha kanuni za Maudhui ya Mawasiliano ya Kielektroniki na
Posta, 2020.
iii. Kwa upande haki za kiuchumi, Serikali ilibainisha hatua ambazo
zimechukuliwa kuboresha ukusanyaji wa mapato ya Serikali. Hatua
hizo ni pamoja na kuanzisha mfumo wa malipo kwa kielektroniki wa
Ankara za malipo ya kodi za ardhi na kuharakisha usuluhishi wa
17
migogoro ya ardhi. Hatua nyingine iliyobainishwa ni Serikali kuboresha
upatikanaji wa maji vijijini kutoka asilimia 47 mwaka 2015 hadi
asilimia 70.1 mwaka 2020 kwa vijijini na kwa mijini kutoka asilimia 74
mwaka 2015 hadi asilimia 84 mwaka 2020.
iv. Kwa upande wa haki za kijamii Serikali ilianzisha mfumo wa kuwalea
Watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika mikoa minne
ambayo ni Mwanza, Dar es Salaam, Arusha na Iringa. - Mheshimiwa Spika, Katika majadiliano hayo Serikali ilipokea
mapendekezo 252 kutoka nchi wanachama yenye malengo ya kukuza na
kulinda haki za binadamu na haki za watu. Aidha, Wizara iliratibu
upatikanaji wa maoni juu ya mapendekezo hayo na kuwasilisha msimamo
wa Serikali kutekeleza mapendekezo 187 kati ya mapendekezo
yalipokelewa kwenye kikao cha Baraza la Haki za Binadamu mwezi Machi, - Mapendekezo hayo yatakayotekelezwa yanahusu masuala ya Haki
za binadamu, sera, sheria, kanuni, mikakati na mipango ya maendeleo ya
nchi, mila, desturi na utamaduni wa watanzania. Hivyo, Serikali iliweza
kutimiza wajibu wake kama nchi mwanachama wa umoja wa mataifa
kwenye Baraza la Haki za Binadamu pamoja na kuahidi kutekeleza
mapendekezo ambayo yamelenga kukuza na kulinda haki za kisiasa,
kiraia, kiuchumi, kiutamaduni na kijamii kwa maendeleo ya watanzania. - Mheshimiwa Spika, Katika kuimarisha utoaji wa elimu kwa umma
kuhusu hatua za kulinda na kuhifadhi haki za binadamu, Wizara katika
kuadhimisha Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania bara ilishirikiana na Asasi za
Kiraia kuandaa Kongamano la Haki za Binadamu na Miaka 60 ya Uhuru.
Lengo la Kongamano hilo lilikuwa ni kujadili mafanikio ya Serikali katika
kukuza na kulinda haki za binadamu tangu tulipopata uhuru miaka 60
18
iliyopita. Katika kongamano hilo Wizara na wadau walieleza mafanikio ya
sekta kuhusu haki za binadamu ambayo ni pamoja na kuanzishwa kwa
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inayosimamia masuala ya
haki za binadamu, Kuanzisha Idara mahususi inayoshughulikia masuala ya
kisera kuhusu Haki za Binadamu kwenye muundo wa Wizara ya Katiba na
Sheria.
(b)Elimu kwa Umma - Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Tume ya Haki za Binadamu na
Utawala Bora ilitoa mafunzo kuhusu ukatili wa kijinsia kwa Madiwani na
Masheha 243 (wanaume 145, wanawake 88) katika Mikoa mitatu (3) ya
Tanzania bara ambayo ni Tabora, Iringa na Dodoma na Mikoa mitatu (3) ya
Zanzibar ambayo ni Kaskazini Unguja, Kusini Unguja na Kaskazini Pemba.
Mafunzo hayo yaliwajengea uwezo wa namna ya kutatua kero za wananchi
kwa kuzingatia haki za binadamu na utawala bora. Vilevile, katika mikoa
miwili ya Zanzibar, mafunzo yalifanyika kwa wananchi katika Wilaya nne
(4) ambazo ni Magharibi A, Magharibi B, Wete na Chakechake ambapo
jumla ya washiriki 509 (231 Unguja na 278 Pemba) walipata mafunzo hayo. - Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Tume ya Haki za Binadamu na
Utawala Bora imeandaa na kurusha hewani vipindi kumi na tano (15) vya
Radio na vipindi sita (6) vya runinga kuhusu Haki za Binadamu na Utawala
Bora na majukumu ya Tume. Katika hatua nyingine, Tume ilitumia njia
mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii kama facebook, twitter na
instagram kuhamasisha jamii katika kukabiliana na vitendo vya udhalilishaji
dhidi ya wanawake na watoto.
19
(c) Kushughulikia Malalamiko ya Uvunjifu wa Haki za Binadamu na
Utawala Bora. - Mheshimiwa Spika, Katika kusimamia hifadhi ya Haki za Binadamu
na ukiukwaji wa misingi ya Utawala Bora nchini, katika kipindi cha kuanzia
Julai, 2021 hadi Machi, 2022 Tume ilifanya ufuatiliaji wa Malalamiko 569
katika Halmashauri za Wilaya 53 zilizopo katika Mikoa 20 ya Tanzania
Bara ambayo ni Arusha, Dodoma, Dar es salaam, Geita, Iringa, Kagera,
Kigoma, Kilimanjaro, Lindi, Mara, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Mwanza,
Ruvuma, Singida, Songwe, Tabora na Tanga na mikoa mitano (5) ya
Zanzibar ambayo ni Mjini Magharibi, Kaskazini Unguja, Kusini Unguja
Kaskazini Pemba na Kusini Pemba. Katika Malalamiko 569 yaliyofuatiliwa,
Malalamiko 337 yalihusu uvunjifu wa Haki za Binadamu na Malalamiko 232
yalihusu ukiukwaji wa misingi ya Utawala Bora. Katika ufuatiliaji huo,
Malalamiko 253 sawa na asilimia 45 ya Malalamiko yaliyofuatiliwa
yalifanyiwa kazi. - Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Tume ya Haki za Binadamu na
Utawala Bora ilifanya chunguzi maalumu 16 katika maeneo yaliyohusu
migogoro ya ardhi, madai ya fidia na matibabu, matumizi mabaya ya
madaraka, kuchukua sheria mkononi na uharibifu wa mazingira. Chunguzi
zilifanyika katika Mikoa 11 ya Tanzania Bara ambayo ni Dodoma, Manyara,
Kigoma, Njombe, Kilimanjaro, Morogoro, Tabora, Shinyanga, Tanga, Dar
es salaam, Mtwara na Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar. Kupitia chunguzi
hizi Tume imesaidia wananchi kutatua kero zinazowakabili na kuzishauri
mamlaka za Serikali namna ya kuzingatia masuala ya haki za binadamu na
misingi ya utawala bora.
20
(d)Kuimarisha Utoaji wa Huduma za Msaada wa Kisheria - Mheshimiwa Spika, Wizara inatekeleza jukumu la kuimarisha
usimamizi na uratibu wa huduma ya msaada wa kisheria nchini. Katika
kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022 Wizara imesajili Watoa huduma ya
msaada wa kisheria 15 na wasaidizi wa kisheria 56 kwa ajili ya kutoa
huduma ya msaada wa kisheria kwa wananchi. Idadi hii inafanya jumla ya
Watoa huduma ya msaada wa kisheria waliosajiliwa kufikia 202 na
Wasaidizi wa Kisheria 763. Aidha, katika kipindi husika jumla ya wananchi
1,455,566 (wanawake 529,079, wanaume 514,051 na watoto 412,436)
walipatiwa msaada wa kisheria. Hii ni ongezeko la wanufaika 1,133,124.00
sawa na asilima 351 ikilinganishwa na idadi ya wananchi 322,442
waliopatiwa huduma ya msaada wa kisheria katika kipindi cha Julai, 2020
hadi Machi, 2021. - Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha Julai 2021 hadi Machi, 2022
Wizara kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania ilianzisha madawati ya
msaada wa kisheria katika vituo jumuishi vya utoaji haki sita (6) katika
Mikoa ya Dar es salaam (Kinondoni na Temeke), Arusha, Dodoma,
Morogoro na Mwanza. Lengo la kuanzisha madawati hayo ni kurahisisha
upatikanaji wa huduma ya msaada wa kisheria mahakamani kwa wananchi
wenye uhitaji. Pamoja na kuanzisha madawati hayo, Wizara iliwapatia
mafunzo wanasheria na mawakili wanaotoa huduma ya msaada wa
kisheria katika vituo jumuishi vya utoaji haki. Aidha, Wizara iliwajengea
uwezo Watumishi wa Mahakama wakiwemo Maafisa Utumishi na Watunza
Kumbukumbu katika vituo jumuishi vya utoaji haki ili kurahisisha utoaji wa
huduma ya msaada wa kisheria.
21 - Mheshimiwa Spika, Katika kipindi hicho, Wizara iliwezesha
kufanyika kwa vikao viwili (2) vya Bodi ya Taifa ya Ushauri wa Msaada wa
Kisheria ambapo bodi ilipendekeza kuimarisha uratibu wa msaada wa
kisheria ambapo pendekezo hili lilifanyiwa kazi na Wizara imefanikiwa
kupata kibali cha kuanzisha Kitengo cha Msaada wa Kisheria katika mwaka
wa fedha 2021/2022. Aidha, mapendekezo mengine yaliyotolewa na bodi
yanaendelea kufanyiwa kazi. - Mheshimiwa Spika, Katika kuimarisha huduma za msaada wa
kisheria, Wizara iliwezesha Wasajili Wasaidizi kukagua utendaji wa Watoa
huduma za msaada wa kisheria katika mikoa 26 Tanzania Bara, lengo ni
kuhakiki ubora wa utendaji wa watoa huduma hao. Zoezi hili limewezesha
kutambua watoa huduma ya msaada wa kisheria waliopo katika kila
Halmashauri na utendaji kazi wake ikiwemo kutoa huduma kwa kuzingatia
matakwa ya sheria.
IX. Kuratibu shughuli za Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu,
Ufilisi na Udhamini; - Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022,
Wizara kupitia Ofisi ya Kabidhi Wasii Mkuu iliimarisha shughuli za usajili wa
vizazi, vifo, ndoa, talaka na watoto wa kuasili ikiwa ni haki ya msingi ya
utambuzi na upatikanaji wa takwimu kwa ajili ya maendeleo ya Taifa. Ofisi
ilitekeleza Mpango Wa Usajili wa Watoto wa Umri Chini ya Miaka Mitano
katika Mikoa ya Mwanza, Rukwa na Katavi pamoja na Mpango wa Usajili
wa Watoto wenye Umri wa Miaka 5 Hadi 17 walio Shuleni katika wilaya za
Mlele, Arumeru, Kahama, Arusha na Misungwi. Hadi kufikia Machi, 2022
jumla ya vizazi 1,173,752 vilisajiliwa.
22 - Mheshimiwa Spika, maboresho ya Mfumo wa Usajili wa Matukio ya
Vifo yenye lengo la kuhakikisha kila tukio la kifo linasajiliwa mara tu
linapotokea, kumpunguzia mwananchi gharama za kupata huduma hiyo
pamoja na kupata takwimu za sababu za vifo ili kuweka afua katika
huduma za afya, yalifanyika katika Mkoa wa Songwe katika ngazi ya Vituo
vya Afya na Ofisi za Kata. Hadi kufikia Machi, 2022 vituo vya usajili
vimeongekeza kutoka vituo vinne (4) ambavyo ni wilaya hadi kufikia vituo
130 ambavyo ni Ofisi za Kata 93 na Vituo vya Afya 37 katika Mkoa huo.
Jitihada hizo zimewezesha kusajili jumla ya vifo 25,743 katika kipindi cha
Julai, 2021 hadi Machi, 2022. - Mheshimiwa Spika, Katika cha kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi,
2022,Ofisi ya Kabidhi Wasii Mkuu ilisajili ndoa 26,303 na talaka 303. Katika
jitihada za kuboresha usajili wa matukio hayo, Mfumo wa Usajili wa Ndoa
na Talaka kielektroniki umeanzishwa kwa lengo la kurahisisha usajili na
upatikanaji wa taarifa hizo nchini. Aidha, mfumo huo umeunganishwa na
mfumo wa kielektroniki wa Mashauri wa Mahakama ili kurahisisha
upatikanaji na uhakiki wa amri za mahakama kuhusu mashauri
yanayohusu talaka. Sambamba na maboresho hayo ya kimfumo, mafunzo
kuhusu ufungishaji ndoa yalitolewa kwa Viongozi wa Dini na Serikali katika
Mikoa ya Pwani, Kilimanjaro, Iringa, Rukwa na Katavi. - Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022
hati za kuasili watoto 24 zilisajiliwa pamoja na wosia 127 zilitayarishwa na
kuhifadhiwa. Elimu kuhusu uandikaji na uhifadhi wa wosia ilitolewa Mkoani
Dar es Salaam, Kilimanjaro, Rukwa na Katavi kwa Viongozi wa dini na
Serikali. Aidha, elimu ilitolewa kwa wananchi katika maadhimisho ya Wiki
ya Wajane mkoani Kagera na Dar es Salaam; na Mkoani Mbeya katika
23
maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa Kisheria. - Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Ofisi ya Kabidhi Wasii Mkuu
katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022 imesajili Bodi za Wadhamini - Ili kuboresha huduma na upatikanaji wa taarifa za Bodi za Wadhamini,
Ofisi imeanzisha Mfumo wa kieletroniki wa Usajili wa Bodi za Wadhamini
ambao unasaidia upatikanaji na uhakiki wa taarifa za Bodi za Wadhamini
kwa wakati pamoja na utoaji vibali vya umiliki ardhi hivyo kurahisisha utoaji
huduma na kuongeza maduhuli ya Serikali.
X. Kuratibu Tathmini na Maboresho ya Sheria - Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022
Wizara kupitia Tume ya Kurekebisha Sheria ilihakikisha sheria za nchi
zinafanyiwa mapitio na maboresho ili ziendane na wakati kwa kuzingatia
mabadiliko ya maendeleo katika nyanja za kijamii, kiuchumi, kisiasa na
kiutamaduni. Katika kipindi husika Tume ya Kurekebisha Sheria
imekamilisha Taarifa kuhusu Mapitio ya Mfumo wa Sheria zinazosimamia
Masoko ya Mazao ya Kilimo Tanzania ambapo utafiti ulifanyika katika
Mikoa tisa (9) ya Dodoma, Morogoro, Dar es Salaam, Mtwara, Arusha,
Kilimanjaro, Mwanza, Iringa na Njombe. Lengo la utafiti huo lilikuwa kubaini
changamoto za mfumo wa masoko ya mazao ya kilimo Tanzania na kutoa
mapendekezo yatakayohakikisha kunakuwepo mfumo thabiti na endelevu
wa masoko ya mazao ya kilimo nchini. - Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Tume ya Kurekebisha Sheria
ilifanya Mapitio ya Mfumo wa Sheria unaosimamia Vyama vya Kijamii
ambapo utafiti ulifanyika katika Mikoa saba (7) ya Dar es Salaam,
Dodoma, Iringa, Mbeya, Morogoro, Mwanza na Shinyanga. Lengo la utafiti
24
huo ni kubaini changamoto za Mfumo wa Sheria unaosimamia vyama vya
kijamii na kutoa mapendekezo yatakayohakikisha kunakuwepo na mfumo
thabiti wenye uwazi na uwajibikaji. - Mheshimiwa Spika, Kuhusu tathmini ya utekelezaji wa sheria,
Wizara kupitia Tume ya Kurekebisha Sheria ilikamilisha Taarifa nne (04) za
tathmini ya utekelezaji wa sheria ambazo zinahusu mifumo ya Adhabu
Mbadala; Sekta ya Utalii, Sekta ya Mifugo na Sekta ya Uvuvi. Kwa upande
wa Adhabu Mbadala, sheria zilizofanyiwa tathmini ni pamoja na Sheria ya
Magereza, Sura 58; Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Sura 20;
Sheria ya Makosa ya Uhujumu Uchumi, Sura 200, Sheria ya Huduma za
Jamii, Sura 291; Sheria ya Bodi ya Msamaha, Sura ya 400 na Sheria
Ukomo wa Adhabu, Sura 90. Lengo la tathmini ni kupima endapo malengo
ya sheria husika yamefikiwa ikiwemo kupunguza msongamano wa
Wafungwa Magerezani, kupunguza adha ya kupata magonjwa ya
kuambukiza kwa Wafungwa na kuipunguzia Serikali gharama za
kuendesha magereza. - Mheshimiwa Spika, Katika Sekta ya Utalii, sheria zilizofanyiwa
tathmini ni pamoja na Sheria ya Utalii, Sura 65; Sheria ya Wanyamapori,
Sura 283; Sheria ya Mbuga za Wanyama, Sura 282; Sheria ya
Makumbusho ya Taifa, Sura 281; Sheria ya Hifadhi ya Eneo la Mamlaka ya
Ngorogoro, Sura 284; na Sheria ya Malikale, Sura 333. Tathmini katika
Sekta ya Utalii ililenga kubaini endapo madhumuni yaliyokusudiwa na
Sheria hizo yamefikiwa katika kuboresha na kukuza vivutio vya utalii,
kuboresha kipato cha wananchi, kuongeza fedha za kigeni na kuongeza
pato la Taifa. Aidha, Tume ilifanya tathmini ya utekelezaji wa sheria katika
Sekta ya Mifugo. Sheria zilizofanyiwa tathmini ni pamoja na Sheria ya
25
magonjwa ya Mifugo, Sura 156; Sheria ya Madaktari wa Mifugo, Sura 319;
Sheria ya Nyama, Sura 421; Sheria ya Maziwa, Sura 262; Sheria ya
Biashara ya ngozi, Sura 120; Sheria ya Ustawi wa Wanyama, Sura 120;
Sheria ya Utambulisho, Usajili na Ufuatiliaji wa Wanyama, Sura 184; Sheria
ya Matumizi ya Ardhi, Sura 116 na Sheria ya Nyanda za Malisho na
Rasilimali za Vyakula vya Mifugo, Sura 180. Dhumuni la tathmini ya sheria
zinazosimamia sekta ya mifugo ni kupima endapo malengo yaliyokusudiwa
katika sheria hizo yamefikiwa katika kuhakikisha ufugaji unakuwa wa
kibiashara na wenye tija kwa wafugaji na Taifa kwa ujumla. - Mheshimiwa Spika, Kuhusu tathmini ya utekelezaji wa Sheria
zinazosimamia Sekta ya Uvuvi Tanzania, Sheria zilizofanyiwa tathmini ni
pamoja na Sheria ya Uvuvi, Sura 279; Sheria ya Usimamizi na Maendeleo
ya Uvuvi wa Bahari kuu, Sura 388; Sheria ya Hifadhi za Bahari na maeneo
Tengefu, Sura 146; na Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania,
Sura 280. Dhumuni la tathmini ya sheria zinazosimamia Sekta ya Uvuvi
Tanzania ni kupima kufikiwa kwa malengo ya sheria hizo ya kuhakikisha
kuwa Sekta ya Uvuvi inakuwa ya kibiashara na kuchangia katika ukuaji wa
uchumi wa buluu wenye kuboresha maisha ya wananchi na kukuza Pato la
Taifa. - Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Tume ya Kurekebisha Sheria
iilitoa elimu ya sheria kwa umma kupitia vipindi vya radio, runinga,
vipeperushi, maonesho ya wiki ya sheria, na mikutano mbalimbali. Lengo
lilikuwa kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu Sheria ya Mtoto; Sheria ya
Ajira; Sheria ya utatuzi wa Migogoro ya Ardhi; Sheria ya Haki za Walaji na
nafasi ya Tume katika maboresho ya sheria nchini. Taarifa za tathmini hizo
zitawasilishwa kwenye mamlaka husika kwa hatua zaidi.
26
XI. Kuratibu ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa Sheria za Utajiri
na Maliasilia za nchi - Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuimarisha mifumo ya
ufuatiliaji na tathmini ya shughuli za utajiri asilia na maliasilia za nchi kwa
kuandaa Mfumo wa Kielektroniki utakaowezesha; kukusanya taarifa
zinazobainisha sehemu zenye utajiri na Maliasili za Nchi na aina ya
uwekezaji unaofanyika, kusajili mikataba ya utajiri na Maliasilia za Nchi
iliyoingiwa na Wizara, Idara na Taasisi kwa niaba ya Serikali na kupata
taarifa za utekelezaji wa Sheria ya Mamlaka ya Nchi na Umiliki wa Utajiri
na Maliasilia za Nchi Sura 449 na Sheria ya Mapitio na Majadiliano Kuhusu
Mikataba yenye Masharti Hasi Sura 450 kutoka kwa Wizara, Idara na
Taasisi zinazosimamia utajiri asilia na maliasilia za nchi. Aidha, Wizara
imeshiriki katika kutoa mafunzo na elimu kwa wadau mbalimbali
wanaohusika na masuala ya utajiri asilia na maliasilia za nchi kwa Maafisa
wa Serikali 260 kuhusu Sheria ya Mamlaka ya Nchi na Umiliki wa Utajiri na
Maliasilia za Nchi Sura 449 na Sheria ya Mapitio na Majadiliano Kuhusu
Mikataba yenye Masharti Hasi Sura 450 na nafasi ya maafisa wanyamapori
katika kulinda na kuhifadhi wanyamapori kwa mujibu wa sheria hizo.
Wizara imesimamia jukumu la kufanya marekebisho ya Kanuni za ushiriki
wa Serikali katika shughuli za uchimbaji wa madini nchini kwa mujibu wa
kifungu cha 10 cha Sheria ya Madini, 2010. Wizara imeshiriki katika
majadiliano na makampuni ya uchimbaji wa madini za Nyanzaga. - Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kushiriki kuweka mifumo
mbalimbali ili kuhakikisha kwamba utajiri na maliasilia za nchi unasaidia
kuinua uchumi wa nchi na wananchi kwa ujumla. Wizara inashirikiana na
Wizara mbalimbali kuandaa sera na miongozo mbalimbali ambapo katika
27
kipindi husika imeshirikiana na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara
kuandaa Sera ya ushiriki wa wananchi katika miradi ya kimkakati (Local
Content) pamoja na Sera ya uwekezaji.
XII. Kuboresha Utendaji na Maendeleo ya Rasilimali Watu iliyo chini ya
Wizara - Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022,
Wizara imeendelea kusimamia na kuboresha maslahi ya watumishi na
utendaji kazi katika kutekeleza majukumu yake. Katika kipindi hicho Wizara
ya Katiba na Sheria iliajiri mtumishi mpya mmoja (1) na watumishi wawili
(2) walipandishwa vyeo. Aidha, kwa upande wa Taasisi zilizo chini ya
Wizara, zimeendelea kusimamia maendeleo ya rasilimaliwatu kama
ifuatavyo: –
i. Tume ya Utumishi wa Mahakama iliajiri jumla ya watumishi 45 wa
kada mbalimbali kwa kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022
ikilinganishwa na idadi ya ajira ya watumishi 239 wa kada
mbalimbali kwa kipindi cha Julai, 2020 hadi Machi, 2021. Vilevile,
vikao vinne (4) vilifanyika kushughulikia masuala mbalimbali
ikiwemo Uteuzi wa Naibu Wasajili 25 wa Mahakama Kuu ya
Tanzania kwa ajili ya kuimarisha utendaji wa Mahakama;
Kushughulikia mashauri 21 ya kinidhamu ambapo Mahakimu saba
(7) walistaafishwa kwa manufaa ya umma; watumishi watano (5)
wasio Mahakimu walifukuzwa kazi na Mahakimu tisa (9)
walirejeshwa kazini. Aidha, mtumishi mmoja (1) wa Sekretarieti ya
Tume alipandishwa cheo na mtumishi mmoja (1) aliteuliwa kuwa
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu;
28
ii. Ofisi ya Taifa ya mashtaka iliajiri watumishi wapya wanne (4),
mtumishi mmoja (1) alithibitishwa kazini na watumishi 19
walipandishwa vyeo;
iii. Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliajiri watumishi wapya
wawili (2), watumishi wawili (2) walithibitishwa kazini, mtumishi
mmoja (1) alipandishwa cheo;
iv. Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali iliajiri watumishi wapya 23,
watumishi 8 walithibitishwa cheo na mtumishi mmoja (1)
alipandishwa cheo;
v. Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora iliajiri watumishi
wapya watano (5), watumishi wawili (2) walithibitishwa vyeo na
watumishi wawili (2) walipata uteuzi kuwa Katibu Mtendaji na
Naibu Katibu Mtendaji;
vi. Chuo cha uongozi wa Mahakama Lushoto kiliajiri watumishi wapya
wawili (2), mtumishi mmoja (1) alithibitishwa cheo na mtumishi
mmoja (1) alipata uteuzi kuwa Mkuu wa Idara ya Mafunzo ya
Sheria;
vii. Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania
kilipandisha cheo watumishi tisa (9); na
viii. Ofisi ya Kabidhi Wasii Mkuu iliwathibitisha vyeo watumishi sitini na
saba (67), watumishi watatu (3) walipandishwa vyeo, watumishi
wawili (2) walisimamishwa kazi na watumishi watatu (3)
waliteuliwa katika nyadhifa za Kabidhi Wasii Mkuu, Naibu Kabidhi
Wasii Mkuu na Meneja wa Usajili.
29 - Mheshimiwa Spika, jumla ya watumishi 1,579 kwa Wizara na
Taasisi zake walipatiwa mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi. Maelezo
ya kina kuhusu maendeleo ya Rasilimaliwatu yameoneshwa katika
Kiambatisho F.
XIII. Kushughulikia urejeshwaji wa wahalifu na masuala ya ushirikiano
wa kimataifa kwenye makosa ya jinai - Mheshimiwa Spika, Tanzania imeendelea kushirikiana na mataifa
mengine katika kupambana na kusimamia kurejeshwa kwa watuhumiwa
wa uhalifu katika nchi walikofanya kosa. Wizara kwa kushirikiana na wadau
imeandaa mkataba wa urejeshwaji wa Wahalifu na ushirikiano katika
masuala ya mashauri ya jinai baina ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na Kenya. Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022, Wizara ilipokea
na kushughulikia maombi matano (5) ya kuwarejesha wahalifu wa makosa
ya jinai waliokimbilia nchini kutoka katika mataifa ya Zimbabwe (2), Malawi
(1), Uturuki (1) na Kenya (1). Lengo la kurejesha waharifu hao ni
kuimarisha ushirikiano wa kisheria na mataifa mengine katika masuala ya
jinai na kudhibiti watuhumiwa wa uhalifu kukimbilia katika mataifa mengine.
XIV. Kuratibu shughuli za Taasisi, Mipango na Miradi chini ya Wizara
(a)Kuimarisha Uendeshaji wa Mafunzo Endelevu na Elekezi ya
Kimahakama na Kisheria - Mheshimiwa Spika, Katika kuhakikisha watumishi wa Mahakama na
wa sekta ya sheria wanakuwa na ujuzi na weledi wa kutosha katika
kutimiza wajibu wao kwa ufanisi, Wizara kupitia Chuo cha Uongozi wa
Mahakama, Lushoto imeendelea kuratibu na kutoa mafunzo endelevu na
30
elekezi ya Kimahakama kwa watumishi wa Mahakama na wadau wa sekta
ya sheria nchini. Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022 Chuo
kimeratibu mafunzo yafuatayo;
(i) Mafunzo endelevu: Wizara kupitia Chuo cha Uongozi wa
Mahakama Lushoto imeendelea kuwajengea uwezo jumla ya
wasaidizi wa sheria wa Majaji 84 kwenye eneo la kufanya utafiti wa
kisheria ili waweze kuwasaidia majaji ipasavyo katika kutoa haki.
Vilevile, jumla ya Mahakimu 200 walipatiwa mafunzo kuhusu
uendeshaji wa mashauri ya rushwa na urejeshaji mali zilizopatikana
kwa njia ya uhalifu na Mahakimu 36 walipatiwa mafunzo kuhusu
uendeshaji wa mashauri yanayohusu ukatili wa kijinsia, na
usafirishaji haramu wa binadamu. Chuo kwa kushirikiana na
Mahakama kimekuwa kikiendesha mafunzo kwa njia ya mtandao
kwa lengo la kuwafikia watumishi wengi na kutoa fursa ya
kubadilishana uzoefu. Katika kipindi husika jumla ya Mahakimu 100
waliokasimiwa mamlaka ya ziada na Jaji Mkuu ya kusikiliza
mashauri ambayo yanaangukia kwenye mamlaka ya Mahakama
Kuu ya Tanzania walipatiwa mafunzo endelevu na kupata fursa ya
kubadilishana uzoefu wa namna mamlaka hayo yanavyotumika
pamoja na kujadili changamoto na namna ya kuboresha usikilizaji
wa mashauri. Aidha, Chuo kiliratibu mafunzo kwa njia ya mtandao
kwa majaji, wasajili na Mahakimu wengine wa ngazi mbalimbali
wapatao 150 yaliyolenga utekelezaji wa sheria ya wosia na
usimamizi wa mirathi pamoja na kubadilishana uzoefu.
(ii)Mafunzo elekezi: Wizara kupitia Chuo cha Uongozi wa Mahakama
Lushoto iliendelea kutoa mafunzo elekezi kwa Mahakimu wapya 35,
31
Manaibu Wasajili wapya 25, Watendaji wa Mahakama wa kanda na
mikoa wapya 11 pamoja na Wakurugenzi wasaidizi watatu 3,
mafunzo ya udalali wa mahakama kwa washiriki 30 na wasambazaji
nyaraka za Mahakama 16. Katika kipindi husika chuo kwa
kushirikina na Mahakama ya Tanzania kupitia ufadhili wa Shirika la
UNICEF kiliendesha Mafunzo kwa Wadau wa Haki Mtoto Kanda ya
Kigoma wapatao 40 waliojumuisha Mahakimu 15 kutoka Mahakama
Kuu Kanda ya Kigoma, Mahakimu 15 kutoka kanda ya Tabora,
Maafisa Ustawi wa Jamii watano (5), Waendesha Mashtaka watatu
(3) kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Waendesha Mashtaka
wawili (2) kutoka jeshi la Polisi. Mahakimu walioshiriki ni wale
wenye mamlaka ya kusikiliza mashauri ya mtoto kutoka Mahakama
za wilaya na baadhi ya mahakimu wa Mahakama za mwanzo
kutoka kanda zilizotajwa. - Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha Julai, 2021 mpaka Machi,
2022, Wizara kupitia Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto imeratibu
ushiriki wa maafisa mbalimbali kutoka Mahakama ya Tanzania na Chuo
kwenye vikao na mafunzo yaliyoendeshwa na wadau kama ifuatavyo:-
(i).Mkutano wa wadau (High Level symposium) wa utoaji haki jinai na
ulinzi kwa mashahidi, wahanga na washtakiwa ulioendeshwa na
Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Mahakama ya
Uingereza kupitia Taasisi ya Majaji Wastaafu iitwayo Slynn
Foundation chini ya ufadhili wa Programu ya Kitaifa ya Kuzijengea
Uwezo Taasisi zinazohusika na Kupambana na Rushwa (BSAAT).
(ii).Mafunzo juu ya Uelewa wa utendaji kazi wa Mahakama ya Haki ya
Afrika Mashariki, Utawala wa sheria na Utawala bora. Mafunzo haya
32
yaliendeshwa na Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki kwa
kushirikiana na Centre for Public Interest Law na Ford Foundation
kwa majaji wa mahakama ya Rufani watatu (3), majaji wa
mahakama kuu watatu (3) na Naibu Wasajili saba (7). - Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka wa masomo 2021/22 Chuo
kimedahili wanafunzi wapya 870 wa Astashahada na Stashahada ya sheria
(wanawake 412 na wanaume 458). Kwa upande wa Astashahada ya sheria
waliodahiliwa ni 492 (wanawake 224 na wanaume 268) na Stashahada ya
sheria mwaka wa kwanza ni 378 (wanawake 188 na wanaume 190). Aidha,
wanachuo wanaoendelea na Stashahada mwaka wa pili ni 231 (wanawake
137 na wanaume 94). Jumla ya wanafunzi wote wa Chuo waliodahiliwa
katika Astashahada na Stashahada ya sheria kwa mwaka wa masomo
2021/2022 ni 1,101 (wanawake 549 na wanaume 552) ikilinganishwa na
udahili wa jumla ya wanafunzi 944 (wanaume 420 na wanawake 524)
katika mwaka wa masomo 2020/2021 sawa na ongezo la asilimia 17. - Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Chuo cha Uongozi wa
Mahakama Lushoto imeendelea kusimamia haki za mtoto kwa kuandaa na
kuzindua Kitabu cha Mkusanyiko wa Mashauri ya Watoto na Taarifa ya
Tathmini ya Mafunzo ya Haki za Watoto kwa wadau wa haki za Watoto
kwa ajili ya kurahisha rejea kuhusu mwenendo wa mashauri ya watoto.
(b)Kuimarisha Uendeshaji na Usimamizi wa Utoaji wa Mafunzo ya
Uanasheria kwa Vitendo - Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Taasisi ya Mafunzo ya
Uanasheria kwa Vitendo Tanzania imeendelea kutekeleza jukumu lake la
msingi la kutoa mafunzo ya uanasheria kwa vitendo. Katika kipindi cha
33
Julai, 2021 hadi Machi, 2022, Taasisi imedahili jumla ya wanafunzi 1,507
sawa na ongezeko la asilimia 0.5 ya lengo la udahili wa wanafunzi 1,500.
Aidha, katika kipindi husika, Taasisi imetunuku vyeti kwa wahitimu 293
wanaostahili kusajiliwa kuwa mawakili na kufanya idadi ya wahitimu
waliopata mafunzo kupitia Taasisi hiyo tangu kuanzishwa kwake mwaka
2007 kufikia 7,561.
(c) Miradi ya Maendeleo Inayotekelezwa na Wizara - Mheshimiwa Spika, Wizara na Taasisi zake imeendelea kubuni na
kutekeleza miradi ya maendeleo ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu
yake. Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022 Wizara na Taasisi
zake imeendelea kutekeleza miradi ifuatayo:
i. Mradi wa Kujenga Mfumo Endelevu wa Kupambana na Rushwa.
Mradi huu una lengo la kupunguza athari za rushwa ambazo ni
kikwazo cha maendeleo na kupambana na umaskini nchini. Mradi
huu unatekelezwa na Wizara ya katiba na Sheria, Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mahakama ya Tanzania na Ofisi ya
Taifa ya Mashtaka. Kazi zilizofanyika katika kipindi hicho ni pamoja
na kutoa mafunzo kwa Mahakimu Wakazi 200 kuhusu uendeshaji wa
mashauri ya rushwa na urejeshwaji mali; kuandaa Rasimu ya
Mwongozo wa Upelelezi na Uendeshaji wa Mashauri ya Rushwa na
mashauri mengine (Standard Operating Procedures – SOPs);
kufanya mapitio ya majalada 55 ya mashauri ya rushwa kwa Wakuu
wa Mashitaka wa Mikoa mitano (5) ya Dar es Salaam, Dodoma,
Arusha, Mbeya na Mwanza kwa lengo la kuwajengea uwezo kwa
vitendo na kuimarisha mifumo ya kupambana na rushwa; na kufanya
34
ufuatiliaji na tathmini za Programu ya Kujenga Mfumo Endelevu wa
Kupambana na Rushwa Tanzania.
ii. Mradi wa Haki Mtandao (e-Justice).
Mradi huu unalenga kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika utoaji
wa huduma za kisheria na upatikanaji haki. Aidha, mradi huu
unalenga kuunganisha mifumo ya taasisi za utoaji haki kwa njia za
kielektroniki ili kuongeza ufanisi, kuharakisha upatinaji wa haki na
kupunguza gharama za upatikanaji wa huduma hizo. Katika kipindi
cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022 mradi umetekeleza kazi ya usanifu
wa mfumo wa kielektroniki wa uangalizi na usimamizi wa utajiri wa
maliasilia za nchi. Mfumo huu utawezesha usajili wa Mikataba
iliyoingiwa na taasisi za Serikali, utambuzi wa maliasilia zote nchini
na uwekezaji uliofanyika.
iii. Mradi wa Kuboresha Uwajibikaji wa Kitaasisi katika kupambana
na Rushwa na kuongeza Wigo wa Kuifikia Haki.
Lengo la mradi huu ni kuimarisha mazingira ya wananchi kuifikia haki
hususan wanawake na watoto pamoja na kuimarisha mapambano
dhidi ya rushwa. Kazi zilizofanyika katika kipindi cha Julai 2021 hadi
Machi, 2022 ni pamoja na: Kuwezesha utoaji wa huduma ya Msaada
wa kisheria ambapo katika maadhimisho ya Wiki ya Msaada wa
Kisheria yaliyofanyika nchi nzima jumla ya wananchi 1,455,566
(wanawake 529,079, wanaume 514,051 na watoto 412,436)
walipatiwa huduma ya msaada wa kisheria.
35
iv. Mradi wa kisekta unaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la
Kuhudumia Watoto.
Mradi huu unatekeleza Mkakati wa Haki Mtoto wa mwaka 2020/2021
- 2024/2025 pamoja na kuimarisha usajili wa matukio Muhimu ya
Binadamu na Takwimu, hususan usajili wa vizazi. Kazi zilizofanyika ni
pamoja na Kusajili Vizazi kwa jumla ya watoto 573,888 kupitia
Mpango wa Usajili wa Watoto wa Umri Chini ya Miaka Mitano, katika
Mikoa ya Mwanza, Rukwa na Katavi na usajili wa vifo 480 katika
Mkoa wa Songwe.
v. Mradi wa Uimarishaji wa Upatikanaji Haki za Kisheria Ulinzi wa
Haki za Binadamu Tanzania.
Mradi huu unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa
(UNDP). Mradi huu unalenga kuimarisha uwezo wa taasisi za Umma
na Asasi za Kiraia (AZAKI) katika kulinda na kutetea haki za
binadamu. Kupitia mradi huu Katika eneo la uchunguzi, Tume ilifanya
chunguzi maalum tano (5) kuhusu migogoro wa ardhi, matumizi
mabaya ya madaraka na mazingira mkoani Dodoma, Morogoro,
Tabora, Shinyanga na Manyara. Uchunguzi wa malalamiko haya
unaendelea. Kupitia chunguzi hizi, Tume imeweza kusaidia wananchi
kutatua kero zinazowakabili na kuzishauri mamlaka za Serikali
namna ya kuzingatia masuala ya utawala bora.
vi. Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Taasisi zilizokuwa Chini ya Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Katika kipindi husika, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
imekamilisha taratibu za awali za ujenzi wa Ofisi Jumuishi katika
mkoa wa Mwanza, ambapo mkandarasi ameshapatikana na ujenzi
unatarajiwa kuanza mwezi Juni 2022.
36
- Mheshimiwa Spika, Mchanganuo wa fedha za Miradi ya Maendeleo
zilizopitishwa katika mwaka wa fedha 2021/2022 na kupokelewa na Wizara
na Taasisi katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022 umeambatishwa
kwenye KIAMBATISHO G.
E. UTEKELEZAJI WA ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI YA MWAKA
2020 HADI MWAKA 2025 - Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kutekeleza azma ya Serikali
ya Awamu ya sita ya kuhakikisha kwamba inawajibika ipasavyo kwa
wananchi kupitia utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, ahadi na
maelekezo mbalimbali ya viongozi wa kitaifa. Miongoni mwa ahadi hizo ni
pamoja na kuendeleza vita dhidi ya rushwa na ubadhirifu wa mali ya
umma; kukuza, kulinda na kuhifadhi haki za binadamu na kuendeleza
utawala wa sheria; na kuimarisha mfumo wa utoaji haki. Katika kipindi cha
Julai 2021 hadi Machi, 2022 Wizara katika utekelezaji wa majukumu yake
imetekeleza maelekezo mbalimbali ya Ilani ikiwa ni pamoja na yafuatayo:
I. Kuendeleza Mapambano Dhidi ya Rushwa na Ubadhirifu wa Mali
ya Umma - Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022,
Wizara imechukua hatua mbalimbali za kuimarisha mapambano dhidi ya
rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma. Hatua hizo ni pamoja na
kuimarisha uwezo wa Mahakama ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu
Uchumi kusikiliza mashauri yanayohusu makosa hayo. Kwa kipindi cha
Julai 2021- Machi, 2022 kulikuwa na Jumla ya mashauri 46. Kati ya
mashauri hayo, 21 yalikuwepo mwanzoni mwa Julai 2021 na mashauri
mapya 25 yalifunguliwa katika mahakama hiyo. Hadi Machi, 2022 mashauri
37
20 yamehitimishwa na mashauri 26 yanaendelea kusikilizwa.
II. Kuchukua Hatua za Kupunguza Mlundikano wa Mashauri
Mahakamani - Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi kufikia Machi,
2022, Mlundikano wa mashauri umepungua kwa asilimia 26 kutoka
mashauri 9,399 mwezi Machi 2021 hadi Mashauri 6,994 mwezi Machi, - Hatua zilizochukuliwa ili kupunguza mlundikano wa mashauri ni
pamoja na kufuta mashauri yasiyokuwa na ushahidi; kutumia mfumo wa
kumaliza mashauri kwa njia ya makubaliano na majadiliano (plea
bargaining); kuimarisha mfumo wa ufifishaji wa makosa; kutumia
mahakama zinazotembea na mikutano mtandao (video conference) katika
kuendesha mashauri; na kutekeleza mkakati wa kumaliza mashauri ya
muda mrefu.
III. Kuhakikisha Huduma Bora za Sheria Zinapatikana Kwa Wakati
na Gharama Nafuu kwa Kuongeza Wataalam, Miundombinu,
Vitendea Kazi na Kusogeza Huduma Karibu na Wananchi - Mheshimiwa Spika, Jumla ya Mahakama za Mwanzo tatu (3)
zilikamilika katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai, 2021 hadi Machi, 2022
ambazo ni za matiri (Mbinga), Hydom (Mbulu) na Kibaigwa (Kongwa).
Vilevile, mahakama inaendelea na ujenzi wa mahakama za mwanzo katika
maeneo ya Mlimba na Mang’ula (Morogoro) Chanika (Dar es Salaam),
Kabanga (Ngara), Nyakibimbiri (Bukoba) na Kimbe (Kilindi). Mahakama
inaendelea na Mpango wa ujenzi wa Mahakama za Mwanzo 60 katika Kata
ambazo zipo Makao Makuu ya Tarafa ili kusogeza huduma ya utoaji haki
karibu na Wananchi.
38
IV. Kuimarisha Mfumo wa Wasajili Wasaidizi Katika Halmashauri
zote Ili Kuwezesha Uratibu na Utoaji wa Msaada wa Kisheria Kwa
Wananchi, Ikiwemo Msaada Wa Huduma za Kisheria Katika
Masuala ya Mirathi na Ndoa. - Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022
Wizara imezindua Kamati za Uratibu wa Wadau wa Msaada wa Kisheria
katika mikoa ya Katavi, Mtwara, Dar es Salaam, Mara, Mbeya, Ruvuma,
Lindi, Manyara, Mwanza na Mbeya na hivyo kufanya jumla ya mikoa 18
kuwa na kamati za uratibu wa masuala ya huduma za msaada wa kisheria.
Kamati hizi zinarahisisha upatikanaji wa watoa huduma kwani wadau wote
wa msaada wa kisheria wanakutana na hivyo kuimarisha ushirikiano katia
kutekleza majukumu yao.
V. Kuimarisha Matumizi ya Lugha ya Kiswahili Katika Kutoa
Huduma za Kimahakama na Kwenye Uandishi wa Nyaraka za
Kisheria - Mheshimiwa Spika, Idadi ya Sheria kuu zilizokamilika kutafsiriwa
kutoka lugha ya Kiingereza kuwa Kiswahili hadi kufikia Machi, 2022 ni 212
ambazo zilitafsiriwa kupata Rasimu ya Kwanza. Aidha, kupitia wasaidizi wa
kisheria na watoa huduma za msaada wa kisheria, elimu kwa jamii kwa
lugha ya Kiswahili na lugha za maeneo mahsusi imeendelea kutolewa kwa
lengo la kujenga uelewa zaidi kwa jamii katika masuala mbalimbali ya
kisheria. Lengo ni kuwezesha wananchi kusimamia na kulinda haki zao
kwa kufahamu sheria.
39
VI. Kujenga Mifumo ya TEHAMA ya Kuendelea Kuhimiza Matumizi
yake Katika Utoaji Haki - Mheshimiwa Spika, Wizara pamoja na taasisi sita (6) ambazo ni
(Mahakama, Ofisi ya Kabidhi Wasii Mkuu), Tume ya Utumishi wa
Mahakama, Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo, Tume ya Haki
za Binadamu na Utawala Bora na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali)
kati ya Taasisi 10 vimeimarisha matumizi ya TEHAMA katika utoaji haki
ikiwemo wananchi kuweza kufungua na kufuatilia malalamiko; kuwasilisha
maombi ya nyongeza ya muda, usajili wa waendesha maridhiano,
majadiliano, usuluhishi na upatanishi; kuwezesha kufungua mashauri kwa
njia ya kielektroniki; kusajili vizazi, vifo na bodi za wadhamini kielektroniki;
kusajili, kutambua na kusimamia madalali wa Mahakama na kutoa
mrejesho wa huduma zitolewazo na Mahakama kupitia simu janja.
F. MWENENDO WA BAJETI NA FEDHA ZILIZOPOKELEWA NA
WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2021/2022
(i) Makusanyo ya Maduhuli - Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022
Wizara ilipanga kukusanya maduhuli ya jumla ya Shilingi
12,672,599,000.00 kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vya mapato
ambavyo ni pamoja na; ada za watoa huduma ya utatuzi wa migogoro kwa
njia ya majadiliano, maridhiano, upatanishi na usuluhishi; ada za watoa
huduma ya msaada wa kisheria; ada za kusajili mashauri, ada za mawakili
na faini zinazotokana na mashauri mbalimbali pamoja na pango la ofisi.
Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022 Wizara ilikusanya jumla ya
Shilingi 6,018,450,524.81 sawa na asilimia 47 ya lengo la makusanyo
40
yaliyopangwa. Mchanganuo wa maduhuli kwa kila Fungu ni kama
unavyoonekana kwenye Jedwali Na. 1.
JEDWALI Na. 1 Mchanganuo wa maduhuli yaliyokusanywa kwa kila
Fungu kwa kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022
Mafungu
KIASI
KILICHOIDHINISHWA
(SH)
KIASI
KILICHOKUSANYWA
JULAI 2021-MACHI 2022
(SH)
Fungu 12 – –
Fungu 16 – –
Fungu 19 – –
Fungu 35 56,400,000.00 56,400,000.00
Fungu 40 12,571,199,000.00 5,921,836,129.00
Fungu 41 45,000,000.00 40,214,395.81
Fungu 55 – –
Fungu 59 – –
JUMLA 12,672,599,000.00 6,018,450,524.81
(ii) Bajeti Iliyoidhinishwa - Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha 2021/2022 Wizara ya
Katiba na Sheria iliidhinishiwa na Bunge jumla ya Shilingi
231,693,745,000 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Miradi ya maendeleo.
Kati ya hizo Shilingi 79,599,030,000 ni kwa ajili ya mishahara ya
Watumishi, Shilingi 99,178,885,000 ni kwa ajili ya matumizi mengineyo na
Shilingi 52,915,830,000 ni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Kati ya fedha za Maendeleo jumla ya Shilingi 44,100,000,000 ni fedha za
ndani na Shilingi 8,815,830,000 fedha za nje.
41
(iii) Fedha zilizopokelewa na Wizara na Taasisi - Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022
Wizara ilipokea jumla ya Shilingi 194,115,559,872.30 sawa na asilimia
84 ya Shilingi 231,693,745,000 zilizoidhinishwa katika mwaka wa fedha
2021/2022. Kati ya hizo Shilingi 63,868,833,607.27 ni mishahara na
Shilingi 81,691,778,331.58 ni matumizi mengineyo. Fedha za maendeleo
zilizopokelewa ni Shilingi 49,616,082,804.44 ambazo zinajumuisha
Shilingi 22,135,756,234.90 fedha za ndani na Shilingi 27,480,326,569.54
ni fedha za nje. Ongezeko la fedha za nje zilizopokelewa limetokana na
Mfuko wa Mahakama kupokea kiasi cha Shilingi 22,901,711,761.54
ambazo zilitokana na Mkataba wa Benki ya Dunia na Serikali ambapo kiasi
hicho cha fedha kiliongezeka wakati wa utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa
fedha 2021/22. Muhtasari wa mchanganuo wa Bajeti iliyoidhinishwa
umeoneshwa kwenye Jedwali Na. 2 na kiasi cha fedha zilizopokelewa na
Wizara na Taasisi hadi Machi, 2022 zimeoneshwa kwenye KIAMBATISHO
H.
42
JEDWALI: Na. 2: Muhtasari wa Bajeti na Fedha zilizopokelewa kwa
Wizara na Taasis kwa Kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi 2022
Na. Matumizi Bajeti
iliyoidhinishwa
Kiasi
kilichopokelewa
Hadi Machi,
2022
Asilimia ya
kiasi
kilichopokelewa
hadi kufikia
Machi, 2022
Mishahara
ya
watumishi
79,599,030,000 63,129,965,237 79%- Matumizi
mengineyo 99,178,885,000 81,369,511,831 82%
Miradi ya
Maendeleo
(Ndani)
44,100,000,000 22,135,756,235 50%
Miradi ya
Maendeleo
(Nje)
8,815,830,000 27,480,326,570 312%
JUMLA 231,693,745,000 194,115,559,872 84%
G. MAFANIKIO YALIYOPATIKANA- Mheshimiwa Spika, Utekelezaji wa majukumu ya Wizara katika
kipindi cha Julai 2021 hadi Machi 2022 ulikuwa na mafanikio yafuatayo:-
i. Kuimarisha mfumo wa utoaji haki nchini kwa kuanza kutumia
lugha ya Kiswahili katika uandishi wa sheria na shughuli za utoaji
haki mahakamani;
ii. Kuongezeka kwa wigo wa mfumo wa utoaji haki kwa
kuwawezesha Mawakili kuanza kutoa huduma za uwakili katika
Mahakama za Mwanzo;
iii. Kuimarisha mfumo wa utatuzi wa migogoro nje ya mahakama kwa
43
kutumia njia mbadala ambazo ni; majadiliano, maridhiano,
upatanishi na usuluhishi;
iv. Uteuzi wa Majaji tisa (9) wa Mahakama ya Rufani na Majaji 21 wa
Mahakama Kuu na kufanya jumla ya idadi ya Majaji wa Mahakama
ya Rufani kufikia 24 na Majaji wa Mahakama Kuu kufikia 82 na
Mahakimu 245;
v. Uteuzi wa Kabidhi Wasii Mkuu na Naibu Kabidhi Wasii Mkuu na
hivyo kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya
Kabidhi Wasii Mkuu;
vi. Kuendelea na matumizi ya lugha ya Kiswahili katika Shughuli za
mahakama na uandishi wa nyaraka za Kisheria ambao
umeongeza uelewa wa sheria kwa wananchi na hivyo kurahisisha
upatikanaji wa haki kwa wakati na kwa gharama nafuu;
vii. Kuunganishwa kwa Mfumo wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na
Udhamini na Mahakama ambapo imerahisisha upatikanaji wa
taarifa za talaka na watoto wa kuasili kwa njia ya mtandao;
viii. Tanzania kupitia Ofisi ya Kabidhi Wasii Mkuu kuwa kinara wa
Usajili wa matukio muhimu ya binadamu katika ukanda wa Afrika
kupitia tangazo la Umoja wa Afrika mwaka 2021;
ix. Kuimarika na kuboreshwa kwa utoaji wa mafunzo ya uanasheria
kwa vitendo nchini na mafunzo ya uongozi wa mahakama;
x. Kuendelea kuimarika kwa matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa
huduma;
xi. Kuiwakilisha Serikali katika mashauri ya madai na usuluhishi
kulikowezesha kuokoa kiasi cha Shilingi bilioni 236.6; na
xii. Kutoa taarifa kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na
Ulimwengu kwa ujumla kuhusu jitihada za Serikali ya Jamhuri ya
44
Muungano wa Tanzania katika kukuza, kuheshimu na kulinda haki
za kisiasa, kiraia, kiuchumi, kiutamaduni na kijamii.
H. CHANGAMOTO ZILIZOJITOKEZA - Mheshimiwa Spika, Pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika
utekelezaji wa majukumu, Wizara ilikabiliwa na changamoto mbalimbali
kama ifuatavyo: –
i. Kukosekana kwa ulinzi na usalama kwa watoa taarifa na
mashahidi. Hali hii inasababisha watoa taarifa na mashahidi kusita
au kutokutoa ushirikiano unaohitajika kwa vyombo vya haki jinai
katika kutoa taarifa za uhalifu kwa kuhofia usalama wao;
ii. Kuongezeka kwa uhitaji wa Wananchi kuelewa wajibu wao katika
kudai haki zao za kijamii na kiraia ikilinganishwa na uwezo uliopo;
iii. Mirathi kuchukua muda mrefu kufungwa kutokana na wanufaika
kuendeleza migogoro hata baada ya Mahakama kumteua Kabidhi
Wasii Mkuu kuwa msimamizi wa mirathi;
iv. Kuwepo kwa migogoro ndani ya Bodi za Wadhamini za Taasisi
zisizo za Serikali zilizosajiliwa na Ofisi ya Kabidhi Wasii Mkuu
inayotokana na kugombania madaraka, maslahi binafsi na
ubadhilifu wa mali; na
v. Kutofungamanishwa kwa mfumo wa utoaji haki kunakoathiri
upatikanaji wa haki, uendeshaji na usimamizi wa vyombo vingine
vya utoaji haki.
45
I. MIKAKATI YA KUTATUA CHANGAMOTO - Mheshimiwa Spika, ili kutatua changamoto zilizotajwa hapo juu
Wizara imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na:
(i) Wizara inaratibu maandalizi ya kanuni za kutekeleza Sheria ya
Kuwalinda mashahidi na Watoa taarifa za Uhalifu nchini;
(ii)Kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu katiba na Sheria kupitia
vyombo mbalimbali vya habari ikiwa ni pamoja kushirikisha Asasi za
Kiraia ili kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu haki na wajibu wao
katika kupata haki zao.
(iii) Kutoa elimu kwa wanufaika kuhusu taratibu za usimamizi na ufungaji
ili mirathi iweze kufungwa kwa wakati na warithi kupata haki zao.
(iv)Kuendelea kuhakikisha taasisi zilizosajiliwa zinaweka vipengele
bayana katika katiba zake vitakavyotoa miongozo ya kuepusha
migogoro katika Bodi za Wadhamini na kuendelea kutoa elimu
kuhusu majukumu na wajibu wa Bodi za Wadhamini; na
(v) Kuendelea kuboresha na kufungamanisha mifumo ya utoaji haki kwa
vyombo vya utoaji haki nchini. - Mheshimiwa Spika, mafanikio yaliyopatikana ni juhudi za pamoja
kati ya Wizara, Idara, Taasisi na wadau wa Sekta ya Sheria wakiwemo
washirika wa maendeleo. Hivyo, nitumie fursa hii kutoa shukrani zangu za
dhati kwa ushirikiano mzuri uliopo kati yetu na Washirika wa Maendeleo
ikiwa ni pamoja na Benki ya Dunia, Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP), Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto
46
(UNICEF), Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UNWOMEN), Umoja
wa Ulaya (EU), Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Uingereza (FCDO),
Mahakama ya Uingereza, Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki. Wadau
wengine walioshiriki katika kuleta mafanikio ya Wizara ni pamoja na;
Kampuni ya Simu ya TIGO ambayo imeipatia Ofisi ya Kabidhi Wasii Mkuu
simu janja 1,046 kwa ajili ya usajili wa watoto chini ya umri wa miaka
mitano (5) katika mikoa mitatu (3) ya Mwanza, Rukwa na Katavi na hivyo
kufanya jumla ya mikoa iliyopokea simu janja kwa ajili ya shughuli za usajili
kufikia 22. Ni matumaini yangu kuwa, Kampuni hiyo itaendelea kuipatia
simu janja mikoa minne (4) iliyobaki ya Tabora, Kigoma, Kagera na Dar es
Salaam kufanikisha usajili wa watoto. Wizara inatambua na kuthamini
uhusiano mzuri uliopo kati ya Serikali na wadau hao, na tutahakikisha kuwa
ushirikiano huo unaimarishwa kwa maendeleo ya sekta ya sheria na taifa
kwa ujumla.
J. MPANGO NA BAJETI YA WIZARA NA TAASISI ZAKE KWA
MWAKA WA FEDHA 2022/2023 - Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha 2022/2023 Wizara na
Taasisi zake itaendelea kuboresha utoaji wa huduma kwa umma ili
kuendana na Dhima yake. Ili kufikia azma hiyo Wizara na Taasisi zake
zimeainisha maeneo mahsusi ya kipaumbele na kuyawekea malengo na
shabaha kwa ajili ya utekelezaji.
(a) Vipaumbele vya Wizara na Taasisi zake - Mheshimiwa Spika, Maeneo ya vipaumbele muhimu ambavyo
Wizara na taasisi zake itakavyovitekeleza kwa mwaka wa fedha 2022/2023
ni ifuatavyo: –
47
i. Kuendelea na kuanza kujenga vituo jumuishi vya Taasisi za Sheria
Nchini;
ii. Kuendelea na kuanza kujenga majengo ya Makao Makuu ya Wizara na
taasisi zake katika mji wa Dodoma;
iii. Kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala ya kikatiba na
utawala wa sheria;
iv. Kuendelea kuhuisha sheria mbalimbali ili kuimarisha uhuru na wajibu wa
wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo na kukuza demokrasia
na utawala wa Sheria;
v. Kuimarisha mifumo ya uangalizi wa matumizi ya utajiri na maliasilia za
nchi ili kuleta manufaa kwa wananchi na maendeleo ya Taifa kwa
ujumla;
vi. Kuendelea kuhamasisha matumizi ya njia mbadala za utatuzi wa
migogoro ambazo ni usuluhishi, upatanishi, maridhiano na majadiliano ili
kurahisisha na kuharakisha upatikanaji wa haki nchini;
vii. Kuimarisha mifumo ya kuhamasisha, kuzingatia na kulinda haki za watu
na haki za binadamu;
viii. Kuendelea kuimarisha mifumo ya utoaji Haki nchini na kuhimiza
matumizi ya TEHAMA katika Sekta ya Sheria;
ix. Kuimarisha mifumo ya upatikanaji wa Huduma ya Msaada wa Kisheria
nchini;
x. Kutekeleza Programu ya Kutumia Lugha ya Kiswahili katika utoaji Haki
Nchini;
xi. Kuendelea na utekelezaji wa Mkakati wa Pili wa Taifa wa Haki Mtoto
2020/2021-2024/2025;
xii. Kuendelea kuimarisha Usajili wa matukio muhimu ya binadamu na
takwimu pamoja na shughuli za ufilisi na udhamini;
48
xiii. Kuharakisha utatuzi wa mashauri ya kawaida na mkakati wa kumaliza
mashauri ya muda mrefu (Backlog);
xiv. Kuimarisha uwezo katika ukaguzi na usimamizi wa shughuli za
Mahakama;
xv. Kuendelea kutekeleza mpango wa ujenzi na ukarabati wa Majengo ya
Mahakama katika ngazi mbalimbali;
xvi. Kuendelea na ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya
Tanzania ili kuhamia Dodoma;
xvii. Kuimarisha maendeleo ya rasilimali watu, ikiwa ni pamoja na mafunzo,
na nidhamu ya watumishi;
xviii. Kuongeza ushirikiano na wadau wa haki jinai ili kuharakisha huduma ya
utoaji haki;
xix. Kuendesha vikao vya kisheria vya Tume na mchakato wa Ajira ya
watumishi wa Mahakama;
xx. Kutoa Elimu kwa Umma kuhusu majukumu ya Tume na Kamati za
Maadili ya Maafisa wa Mahakama ngazi ya Mikoa na Wilaya
xxi. Kufanya Tafsiri, Uandishi na Urekebu wa sheria;
xxii. Kutoa ushauri wa kisheria na kufanya Upekuzi na Marejeo ya Mikataba;
xxiii. Kuimarisha uendeshaji mashtaka na usimamizi wa mashauri ya jinai;
xxiv. Kuimarisha uratibu na usimamizi wa upelelezi wa makosa ya jinai;
xxv. Kuimarisha mfumo wa utaifishaji mali, usimamizi na urejeshwaji wa mali
zinazohusiana na uhalifu;
xxvi. Kuimarisha utekelezaji wa programu ya kutenganisha shughuli za
Mashtaka na Upelelezi;
xxvii. Kuratibu, kusimamia na Kuiwakilisha Serikali na Taasisi zake katika
kuendesha mashauri ya madai na usuluhishi yaliyofunguliwa na au dhidi
49
ya Serikali katika mahakama na mabaraza mbalimbali ndani na nje ya
nchi;
xxviii. Kufanya uchunguzi kuhusu masuala ya haki za binadamu na utawala
bora;
xxix. Kutoa elimu kwa Umma kuhusu masuala ya haki za binadamu na
utawala bora;
xxx. Kuimarisha mahusiano na Taasisi za Kitaifa, Kikanda na Kimataifa;
xxxi. Kufanya tafiti kuhusu masuala ya haki za binadamu na utawala bora
xxxii. Kufanya Tathmini ya utekelezaji wa sheria za Kudhibiti na Kupambana
na Dawa za Kulevya; na Mfumo wa Sheria unaosimamia Usafiri Majini.
xxxiii. Kufanya Mapitio ya mifumo ya sheria za Usimamizi wa haki katika
Mahakama za Mwanzo; Makosa ya uhujumu uchumi; na Usajili wa
wadhamini.
xxxiv. Kuimarisha maendeleo ya rasilimali watu na vitendea kazi.
(b)Makusanyo ya Maduhuli ya Serikali - Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha 2022/2023 Wizara
inatarajia kukusanya kiasi cha Shilingi 12,676,201,000.00 ikiwa ni
maduhuli ya Serikali, kama inavyoonekana kwenye Jedwali Na. 3:-
Jedwali Na. 3: Makadirio ya Maduhuli ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha
2022/2023
Fungu 12 – Sh. 0.00
Fungu 16 – Sh. 0.00
Fungu 19 – Sh. 0.00
Fungu 35 – Sh. 60,000,000.00
50
Fungu 40 – Sh. 12,571,199,000.00
Fungu 41 – Sh. 45,000,000.00
Fungu 55 – Sh. 2,000.00
Fungu 59 – Sh. 0.00
JUMLA Sh. 12,676,201,000.00
(c) Makadirio ya Fedha kwa ajili ya Kutekeleza Mpango na Bajeti kwa
Mwaka wa Fedha 2022/2023
- Mheshimiwa Spika, Ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu yake,
Wizara inaomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi 272,768,278,800.00 kwa
ajili ya matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha
2022/2023. Kati ya Fedha hizo, Shilingi 207,703,708,800.00 ni kwa ajili ya
matumizi ya kawaida na Shilingi 65,064,570,000.00 ni kwa ajili ya
matumizi ya miradi ya maendeleo. Mchanganuo wa makadirio ya bajeti
kwa mafungu nane (8) ya Wizara na taasisi zake ni kama ilivyooneshwa
kwenye Jedwali Na. 4: –
Jedwali Na. 4: Mchanganuo wa Makadirio ya Bajeti kwa Wizara ya
Katiba na Sheria na Mafungu yake kwa mwaka wa fedha, 2022/2023
Na. Fungu la Matumizi Bajeti 2022/23 - Mishahara ya watumishi 95,356,423,800.00
- Matumizi mengineyo 112,347,285,000.00
- Miradi ya Maendeleo 65,064,570,000.00
JUMLA 272,768,278,800.00
51 - Mheshimiwa Spika, Kiasi hicho cha fedha kinaombwa kupitia
mafungu ya bajeti yaliyo chini ya Wizara yafuatavyo: –
(i) Fungu 12: Tume ya Utumishi wa Mahakama
Matumizi ya Mishahara – Sh. 461,127,800.00
Matumizi Mengineyo – Sh. 2,700,000,000.00
Matumizi ya Maendeleo (Ndani) – Sh. 0
Matumizi ya Maendeleo (Nje) – Sh. 0
Jumla – Sh. 3,161,127,800.00
(ii) Fungu 16: Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Matumizi ya Mishahara – Sh. 2,928,360,000.00
Matumizi Mengineyo – Sh. 6,942,981,000.00
Matumizi ya Maendeleo (Ndani) – Sh. 4,000,000,000.00
Matumizi ya Maendeleo (Nje) – Sh. 500,000,000.00
Jumla – Sh. 14,371,341,000.00
(iii) Fungu 19: Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali
Matumizi ya Mishahara – Sh. 3,339,798,000.00
Matumizi Mengineyo – Sh. 9,473,018,000.00
Matumizi ya Maendeleo (Ndani) – Sh. 0
Matumizi ya Maendeleo (Nje) – Sh. 0
Jumla – Sh. 12,812,816,000.00
(iv) Fungu 35: Ofisi ya Taifa ya Mashtaka
Matumizi ya Mishahara – Sh. 14,548,751,000.00
Matumizi Mengineyo – Sh. 22,068,944,000.00
Matumizi ya Maendeleo (Ndani) – Sh. 8,000,000,000.00
Matumizi ya Maendeleo (Nje) – Sh. 630,000,000.00
Jumla – Sh. 45,247,695,000.00
(v) Fungu 40: Mfuko wa Mahakama
Matumizi ya Mishahara – Sh. 63,408,443,000.00
Matumizi Mengineyo – Sh. 57,774,382,000.00
Matumizi ya Maendeleo (Ndani) – Sh. 36,002,000,000.00
Matumizi ya Maendeleo (Nje) – Sh. 3,091,000,000.00
Jumla – Sh. 160,275,825,000.00
52
(vi) Fungu 41: Wizara ya Katiba na Sheria
Matumizi ya Mishahara – Sh. 7,647,528,000.00
Matumizi Mengineyo – Sh. 6,865,271,000.00
Matumizi ya Maendeleo (Ndani) – Sh. 5,110,800,000.00
Matumizi ya Maendeleo (Nje) – Sh. 7,615,770,000.00
Jumla – Sh. 27,239,369,000.00
(vii) Fungu 55: Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
Matumizi ya Mishahara – Sh. 2,292,096,000.00
Matumizi Mengineyo – Sh. 4,098,680,000.00
Matumizi ya Maendeleo (Ndani) – Sh. 0
Matumizi ya Maendeleo (Nje) – Sh. 115,000,000.00
Jumla – Sh. 6,505,776,000.00
(viii) Fungu 59: Tume ya Kurekebisha Sheria
Matumizi ya Mishahara – Sh. 730,320,000.00
Matumizi Mengineyo – Sh. 2,424,009,000.00
Matumizi ya Maendeleo (Ndani) – Sh. 0
Matumizi ya Maendeleo (Nje) – Sh. 0
Jumla – Sh. 3,154,329,000.00
JUMLA KUU SH. 272,768,278,800.00 - Mheshimiwa Spika, maelezo ya kina na mchanganuo wa maombi ya
fedha za bajeti ya kila Fungu umeainishwa kwenye vitabu vya Randama za
mafungu husika ambavyo vimegawanywa kwa Waheshimiwa Wabunge
kupitia Mfumo wa Kielektroniki wa Bunge. - Mheshimiwa Spika, kabla ya kuhitimisha hotuba yangu, naomba
nitumie fursa hii kuwashukuru viongozi na watendaji wa Wizara na Taasisi
zake kwa ushirikiano mkubwa wanaonipatia katika utekelezaji wa
majukumu ya kila siku ya uwaziri. Hakika, ni kutokana na ushirikiano huo
nimeweza kusimama leo hii mbele ya Bunge lako kueleza mafanikio,
53
mipango na mikakati tuliyonayo katika kuwahudumia wananchi. Hivyo,
kipekee nimshukuru Mhe. Geophrey Mizengo Pinda (Mb.) Naibu Waziri wa
Katiba na Sheria; Bi. Mary Gasper Makondo, Katibu Mkuu; Dkt. Khatibu
Malimi Kazungu, Naibu Katibu Mkuu; Mhe. Prof. Ibrahimu Hamisi Juma,
Jaji Mkuu wa Tanzania na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa
Mahakama; Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi (Mb.), Mwanasheria Mkuu
wa Serikali; Mhe. Mustapher Mohamed Siyani, Jaji Kiongozi wa Mahakama
Kuu ya Tanzania; Prof. Elisante Ole Gabriel, Mtendaji Mkuu wa Mahakama
ya Tanzania na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama; Mhe. Wilbert
Martin Chuma, Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania; Bw. Sylvester
Anthony Mwakitalu, Mkurugenzi wa Mashtaka; Bw. Gabriel Pascal Malata,
Wakili Mkuu wa Serikali; Bi. Angela Kemanzi Anatory, Kabidhi Wasii Mkuu
na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini; Mhe. Jaji
Mstaafu wa Mahakama ya Rufani January Henry Msoffe, Mwenyekiti wa
Tume ya Kurekebisha Sheria; Bw. Casmir Sumba Kyuki, Katibu Mtendaji
wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania; Mhe. Jaji Mstaafu wa
Mahakama Kuu ya Tanzania Mathew Mhina Mwaimu, Mwenyekiti Tume ya
Haki za Binadamu na Utawala Bora; Bw. Patience Kilanga Ntwina, Katibu
Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora; Mhe. Jaji wa
Mahakama ya Rufani Dkt. Paul Faustin Kihwelo, Mkuu wa Chuo cha
Uongozi wa Mahakama Lushoto; Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu Dkt. Benhajj
Shaaban Masoud, Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa
Vitendo Tanzania; Wakurugenzi na Watumishi wote wa Wizara na Taasisi
zake. Aidha, nawashukuru familia yangu ikiwa ni pamoja na mke wangu
Bibi. Flora Ndumbaro na watoto wangu kwa ushirikiano wanaoendelea
kunipatia kwa kunivumilia na kunitia moyo wakati ninapokuwa natekeleza
majukumu yangu ya kulitumikia Taifa. Mwisho lakini sio mwisho kwa
54
umuhimu, naomba nichukue fursa hii kwa namna ya kipekee kabisa
kuwashukuru Wapiga kura wa Jimbo langu la Songea Mjini kwa kuendelea
kunipa ushirikiano katika shughuli za kuleta maendeleo ya jimbo letu. - Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.
55
KIAMBATISHO A
ORODHA YA MAGEREZA NA VITUO VYA POLISI VILIVYOKAGULIWA
KUANZIA JULAI, 2021 HADI MACHI, 2022
NA. MKOA MAGEREZA
YALIYOKAGULIWA
VITUO VYA POLISI
VILIYOKAGULIWA
IDADI YA MAHABUSI
WALIOACHIWA
HURU
1 Arusha 2 5 2
2 Dodoma 6 11 37
3 Dar es Salaam 16 79 35
4 Geita 4 40 24
5 Iringa 5 15 70
6 Kagera 9 18 48
7 Katavi 3 20 24
8 Kigoma 3 10 5
9 Kilimanjaro 4 11 0
10 Lindi 8 5 2
11 Manyara 3 7 3
12 Mara 7 13 15
13 Mbeya 4 5 10
14 Morogoro 2 15 120
15 Mtwara 5 9 10
16 Mwanza 5 22 20
17 Njombe 3 15 5
18 Pwani 8 18 3
19 Rukwa 3 9 52
20 Ruvuma 3 8 5
21 Shinyanga 4 19 1
22 Simiyu 6 7 21
23 Singida 3 5 10
24 Songwe 2 3 61
25 Tabora 4 8 205
26 Tanga 7 14 21
JUMLA 129 391 809
56
KIAMBATISHO B
MISWADA ILIYOANDALIWA KWA KIPINDI CHA JULAI, 2021 HADI
MACHI, 2022
- Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na 3) ya mwaka 2021
(The Written Laws Miscellaneous Amendment (No. 3) Act, 2021); - Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na 4) ya mwaka 2021
(The Written Laws Miscellaneous Amendment (No. 4) Act, 2021); - Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
(The Fire and Rescue Force (Amendment) Act 2021); - Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na 5) ya mwaka 2021
(The Written Laws Miscellaneous Amendment (No. 5) Act, 2021); - Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na 6) ya mwaka 2021
(The Written Laws Miscellaneous Amendment (No. 6) Act, 2021); - Sheria ya Ahueni za Biashara (The Trade Remedies Act);
- Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na 7) ya mwaka 2021
(The Written Laws Miscellaneous Amendment (No. 7) Act, 2021) - Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Usalama Barabarani (The Road
Traffic (Amendment) Act 2021; - Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa, 2022;
10.Muswada wa marekebisho ya Sheria ya Kudhibiti Utakatishaji Fedha
Haramu (The Anti Money Laundering Amendment Act); na
11.Muswada wa Nyongeza ya Matumizi (The Appropriation Supplement
Act)
57
KIAMBATISHO C
MISWADA ILIYOPITISHWA KUWA SHERIA NA KUSAINIWA NA MHE.
RAIS KUWA SHERIA NA KUTANGAZWA KWENYE GAZETI LA
SERIKALI
1.Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na 3) ya mwaka 2021
(The Written Laws Miscellaneous Amendment (No. 3) Act, 2021);
2.Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na 4) ya mwaka 2021
(The Written Laws Miscellaneous Amendment (No. 4) Act, 2021);
3.Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Usajili wa Wahasibu na
Wakaguzi ya mwaka 2021 (The Accountants and Auditors
Registration (Amendment) Act, 2021);
4.Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
(The Fire and Rescue Force (Amendment) Act 2021);
5.Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na 5) ya mwaka 2021
(The Written Laws Miscellaneous Amendment (No. 5) Act, 2021);
6.Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na 6) ya mwaka 2021
(The Written Laws Miscellaneous Amendment (No. 6) Act, 2021);
7.Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na 7) ya mwaka 2021
(The Written Laws Miscellaneous Amendment (No. 7) Act, 2021);
8.Muswada wa marekebisho ya Sheria ya Kudhibiti Utakatishaji Fedha
Haramu (The Anti Money Laundering Amendment Act);
9.Muswada wa Nyongeza ya Matumizi (The Appropriation Supplement
Act)
58
KIAMBATISHO D
ORODHA YA SHERIA ZILIZOTAFSIRIWA KWA HATUA YA RASIMU YA
KWANZA KUTOKA LUGHA YA KINGEREZA KUWA LUGHA YA
KISWAHILI HADI KUFIKIA MACHI, 2022
Na. Jina la Sheria Sura Na.
- Sheria ya Adhabu ya Viboko 17
- Sheria ya Ardhi 113
- Sheria ya Ardhi ya Vijiji 114
- Sheria ya Barabara 167
- Sheria ya Baraza la Kiswahili la Taifa 52
- Sheria ya Baraza la Michezo la Taifa 49
- Sheria ya Baraza la Sanaa la Taifa 204
- Sheria ya Baraza la Taifa la Mitihani Tanzania 107
- Sheria ya Baraza la Taifa la Ujenzi 162
- Sheria ya Benki Kuu 197
- Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha 342
- Sheria ya Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza 230
- Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu 178
- Sheria ya Bodi ya Utalii Tanzania 364
- Sheria ya Bodi za Paroli 200
- Sheria ya Chama cha Mawakili Tanganyika 307
- Sheria ya Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania 66
- Sheria ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere 93
- Sheria ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama – Lushoto 405
- Sheria ya Dawa na Vifaa Tiba 219
- Sheria ya Elimu 353
- Sheria ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (VETA) 82
- Sheria ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro 284
- Sheria ya Fedha za Kigeni 271
- Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa 290
- Sheria ya Fedha za Umma 348
- Sheria ya Gharama za Uchaguzi 278
- Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki 218
- Sheria ya Hati za Makubaliano 26
- Sheria ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu, 146
- Sheria ya Hospitali ya Benjamini Mkapa
- Sheria ya Huduma kwa Jamii 291
59 - Sheria ya Huduma za Habari 229
- Sheria ya Jeshi la Polisi na Polisi Wasaidizi 322
- Sheria ya Jeshi la zimamoto na Uokoaji 427
- Sheria ya Jumuiya 337
- Sheria ya Kamisheni za Uchunguzi 32
- Sheria ya Kanuni ya Adhabu 16
- Sheria ya Karadha 14
- Sheria ya Kinga na Upendeleo wa Kidiplomasia na
Kikonseli
356 - Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge 296
- Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya 95
- Sheria ya Kudhibiti Vinasaba vya Binadamu 73
- Sheria ya Kulinda Watoa Taarifa na Mashahidi 446
- Sheria ya Kuongeza Hukumu 7
- Sheria ya Kuratibu Usajili na Usimamizi wa Maabara
Binafsi za Afya
136 - Sheria ya Kuzuia na Kuthibiti VVU na Ukimwi 431
- Sheria ya Kuzuia Ugaidi 19
- Sheria ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu, 432
- Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma 398
- Sheria ya Mabaraza Maalumu 126
- Sheria ya Madaktari wa Mifugo 319
- Sheria ya Madaktari, Madaktari wa Meno na Wataalam wa
Afya Shirikishi
152 - Sheria ya Madini 123
- Sheria ya Maeneo na Sehemu Zinazolindwa 74
- Sheria ya Mafao ya Hitimisho la Kazi 225
- Sheria ya Mafao ya Viongozi wa Kisiasa 255
- Sheria ya Magereza 58
- Sheria ya Magonjwa ya Wanyama 156
- Sheria ya Mahakama na Matumizi ya Sheria 358
- Sheria ya Mahakama za Mahakimu 11
- Sheria ya Mahakama za Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi, 216
- Sheria ya Majadiliano ya Pamoja Katika Utumishi wa
Umma
105 - Sheria ya Maji na Usafi wa Mazingira 272
- Sheria ya Makumbusho ya Taifa 281
- Sheria ya Mamlaka na Majukumu ya Kabidhi Wasii Mkuu 27
- Sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania 157
60 - Sheria ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa
Serikali
177 - Sheria ya Mamlaka ya Nchi ya Utajiri Asili na Mali Asilia za
nchi
449 - Sheria ya Mapato ya Uhalifu 256
- Sheria ya Mapitio na Majadiliano ya Masharti Hasi Katika
Mikataba ya Utajiri Asili na Mali Asilia
450 - Sheria ya Mashirika ya Maendeleo ya Wilaya 382
- Sheria ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali 56
- Sheria ya Masoko la Mitaji na Dhamana 79
- Sheria ya Masuala ya Ofisi ya Rais 9
- Sheria ya Matamko ya Sheria za Kiislamu 375
- Sheria ya Mawakili 341
- Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta 306
- Sheria ya Mawaziri ya Utekelezaji wa Majukumu ya
Uwaziri,
299 - Sheria ya Mazishi ya Viongozi wa Kitaifa 419
- Sheria ya Mfuko wa Elimu 412
- Sheria ya Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Majimbo 96
- Sheria ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) 422
- Sheria ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya 395
- Sheria ya Michezo ya Kubahatisha 41
- Sheria ya Mipango Miji 355
- Sheria ya Mirathi (Kwa Waasia) Wasio Wakristo 28
- Sheria ya Mishahara na Mafao ya Majaji 424
- Sheria ya Misitu 323
- Sheria ya Msaada wa Kisheria 21
- Sheria ya Mtoto 13
- Sheria ya Mwenendo wa Madai ya Serikali 5
- Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Madai 33
- Sheria ya Ndoa 29
- Sheria ya Optmetria 23
- Sheria ya Pasipoti na Hati za Kusafiria 42
- Sheria ya Petroli 392
- Sheria ya Probesheni 247
- Sheria ya Reli ya Tanzania na Zambia 143
- Sheria ya Serikali Mtandao 273
- Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) 288
- Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka Za Wilaya) 287
61 - Sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzania 304
- Sheria ya Shirika la Nyumba la Taifa 295
- Sheria ya Shirika la Posta 303
- Sheria ya Shule za Udereva wa Vyombo vya Moto (Usajili) 163
- Sheria ya Sikukuu za Kitaifa 35
- Sheria ya Taasisi ya Bahari Dar es Salaam 253
- Sheria ya Taasisi ya Elimu Tanzania 142
- Sheria ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima 139
- Sheria ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo
Tanzania
425 - Sheria ya Taasisi ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR) 59
- Sheria ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)
- Sheria ya Taasisi ya Saratani 86
- Sheria ya Taasisi ya Taifa ya Usafirishaji 187
- Sheria ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam 144
- Sheria ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii 110
- Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania 280
- Sheria ya Tafsiri ya Alama za Taifa 10
- Sheria ya Tafsiri ya Sheria 1
- Sheria ya Taifa ya Mashtaka 430
- Sheria ya Taifa ya Uchaguzi 343
- Sheria ya Takwimu 351
- Sheria ya Taratibu za Uanzishaji wa Mikoa na Wilaya 397
- Sheria ya Tasnia ya Mifugo 262
- Sheria ya Tasnia ya Mkonge 30
- Sheria ya Tawala za Mikoa 97
- Sheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala 244
- Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora 391
- Sheria ya Tume ya Jeshi la Polisi na Magereza 241
- Sheria ya Tume ya Kurekebisha Sheria 171
- Sheria ya Tume ya Sayansi na Teknolojia 266
- Sheria ya Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania 226
- Sheria ya Tume ya Taifa ya UNESCO 433
- Sheria ya Tume ya Ukimwi Tanzania 379
- Sheria ya Tume ya Vyuo Vikuu 346
- Sheria ya Tume za Uchunguzi, 32
- Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa 292
- Sheria ya Uchawi 18
- Sheria ya Uchunguzi wa Kifo 24
62 - Sheria ya Udhamini wa Umma na (Mamlaka na Majukumu) 31
- Sheria ya Uendeshaji wa Bunge 115
- Sheria ya Ufilisi 25
- Sheria ya Ufuatiliaji Wahalifu Watoro 57
- Sheria ya Uhamiaji 54
- Sheria ya Uhamisho wa Mali zinazohamishika 210
- Sheria ya Uhamisho wa wafungwa 387
- Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori 283
- Sheria ya Uhujumu Uchumi 200
- Sheria ya Ukaguzi wa Umma 418
- Sheria ya Ukomo 89
- Sheria ya Umiliki wa Sehemu ya Jengo 416
- Sheria ya Ununuzi wa Umma 410
- Sheria ya Upangaji wa Matumizi ya Ardhi 116
- Sheria ya Upatikanaji wa Taarifa 149
- Sheria ya Upimaji Ardhi 324
- Sheria ya Uraia 357
- Sheria ya Urejeshaji wahalifu 368
- Sheria ya Urekebu wa Sheria 4
- Sheria ya Usafiri Majini 165
- Sheria ya Usafiri wa Anga 80
- Sheria ya Usafirishaji wa Bidhaa kwa Njia ya Bahari 164
- Sheria ya Usajili na Utambuzi wa Watu 36
- Sheria ya Usajili wa Ardhi 334
- Sheria ya Usajili wa Makandarasi 235
- Sheria ya Usajili wa Nyaraka 117
- Sheria ya Usajili wa Rehani zinazohamishika
- Sheria ya Usajili wa Vizazi na Vifo 108
- Sheria ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji
Majenzi
269 - Sheria ya Usajili wa Wahandisi 63
- Sheria ya Usajili wa Wataalam wa Afya ya Mazingira 428
- Sheria ya Usajili wa Wataalamu wa Mipango Miji 426
- Sheria ya Usajili Wataalamu wa Upimaji 270
- Sheria ya Usalama Barabarani 168
- Sheria ya Usambazaji Maji Safi na Usafi wa Mazingira 272
- Sheria ya Ushahidi 6
- Sheria ya Ushirikiano katika Makosa ya Jinai 254
- Sheria ya usimamizi Hospitali za watu Binafsi 151
63 - Sheria ya Usimamizi na Uendelezaji wa Uvuvi wa Bahari
Kuu
388 - Sheria ya Usimamizi wa Kumbukumbu na Nyaraka 309
- Sheria ya Usimamizi wa Maafa. 242
- Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji 331
- Sheria ya Usimamizi wa Uthibiti wa Silaha na Risasi 223
- Sheria ya Usimamizi ya Waasibu na Wakaguzi 286
- Sheria ya Ustawi wa Wanyama 154
- Sheria ya Usuluhishi 15
- Sheria ya Utafiri wa Wanyamapori Tanzania 260
- Sheria ya Utalii 65
- Sheria ya Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji wa Mifugo 184
- Sheria ya Utaratibu wa Heshima kwa Waasisi wa Taifa 194
- Sheria ya Utawala wa Mahakama 237
- Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Msingi na Wajibu 3
- Sheria ya Utekelezaji wa Hukumu ya Kigeni 8
- Sheria ya Utekelezaji wa Hukumu za Nchi Jirani 7
- Sheria ya Utekelezaji wa Majukumu ya Mwanasheria Mkuu
wa Serikali
268 - Sheria ya Uthamini na Usajili wa Wathamini 138
- Sheria ya Uthibiti wa Bidhaa za Tumbaku 121
- Sheria ya Uthibitisho na Usimamizi wa Mirathi 352
- Sheria ya Utumishi wa Umma 298
- Sheria ya Utwaaji Ardhi 118
- Sheria ya Utwaaji na Urejeshaji wa Mashamba Vijijini 22
- Sheria ya Uvuvi 279
- Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania 415
- Sheria ya Uwekezaji wa Wadhamini 53
- Sheria ya Viapo na Matamko ya Kisheria 34
- Sheria ya Vivuko 173
- Sheria ya Vyama vya Siasa 258
- Sheria ya Vyuo Vikuu 346
- Sheria ya Waasisi wa Taifa 195
- Sheria ya Wakala wa Serikali 245
- Sheria ya Wakimbizi 37
- Sheria ya Wanataaluma wa Kemia 160
- Sheria ya Wataalamu wa Maabara ya Afya 48
- Sheria ya ya Utekelezaji wa Wito wa Mashahidi wa kigeni 67
64
KIAMBATISHO E
ORODHA YA SHERIA ZILIZOFANYIWA UREKEBU KWA HATUA YA
USOMAJI WA AWALI KUANZIA JULAI, 2021 HADI MACHI, 2022
S/N CHAPTER NAME - 416 The Unit Titles Act
- 420 The Special Economic Zones Act
- 421 The meat Industry Act
- 422 The Universal Communications Services Access Act.
- 423 The Anti-money Laundering Act
- 425 The Law School of Tanzania Act
- 427 The Fire and Rescue Force Act
- 428 The Environmental Health Practitioners (Registration)
Act. - 429 The Medical Radiology and Imaging Professionals Act
- 430 The National Prosecutions Service Act
- 431 The HIV and AIDS (Prevention and control) Act
- 432 The Anti-Trafficking in persons Act
- 433 The UNESCO National Commission Act.
- 434 The Tanzania Livestock Research Institute Act
- 435 The National Irrigation Act
- 436 The Non-citizens (Employment Regulation Act
- 437 The National Payment System Act
- 438 Tax Administration Act
- 439 The Budget Act
- 440 The Referendum Act
- 441 The National Youth Council Act
- 442 The Electronic Transactions Act
- 443 The Cybercrimes Act
- 444 The One Stop Border Posts Act
- 445 The Commodity Exchange Act
- 446 The Whistleblower and Witness Protection Act
- 447 The Tanzania Extractive Industries (Transparency and
Accountability) Act - 448 The Teacher s’ Service Commission Act
- 449 The Natural Wealth and Resources (Permanent
Sovereignty) Act
65
KIAMBATISHO E
ORODHA YA SHERIA ZILIZOFANYIWA UREKEBU KWA HATUA YA
USOMAJI WA AWALI KUANZIA JULAI, 2021 HADI MACHI, 2022
S/N CHAPTER NAME
- 450 The Natural Wealth and Resources Contracts (Review
and Re-negotiation of Unconscionable Terms) Act - 82 The Vocational Education and Training Act
- 93 The Mwalimu Nyerere Memorial Academy Act
- 102 The Tanzania Library Services Act
- 107 The National Examinations Council of Tanzania Act
- 129 The National Council for Technical Education Act
- 139 The Institute of Adult Education Act
- 142 The Tanzania Institute of Education Act
- 144 The Dar- Es –Salaam Institute of Technology Act
- 178 The Higher Education Students Loans Board Act
- 188 The Atomic Energy Act
- 226 The Tanzania Commissioner for Science and
Technology Act - 314 The Tanzania Teachers’ Professional Board Act
- 346 The Universities Act
- 352 The Education Act
- 412 The Education Fund Act
- 433 The UNESCO National Commission Act.
66
KIAMBATISHO NA. F
MAENDELEO YA RASILIMALIWATU 2021/2022
FUNG
U
TAASI
SI
AJIR
A
MPY
A
KUTHIBITI
SHWA
KAZINI
KUPAND
ISHWA
CHEO
UTEU
ZI
MAFUNZ
O
KUSIMAMI
SHWA
KAZI
KUACHIS
HWA
KAZI
KUACH
A KAZI
KUREJ
ESHWA
KAZINI
KUSTA
AFISH
WA
KWA
MASLA
HI YA
UMMA
12 0 0 1 1 10 0 0 0 0 0
16 21 2 0 1 19 0 0 0 0 0
19 23 8 0 0 13 0 0 0 0 0
35 4 1 19 0 258 0 0 0 0 0
40 45 199 0 25 1099 3 5 3 9 7
41 1 0 2 2 0 0 0 0 0 0
55 5 0 0 1 23 0 0 0 0 0
59 0 0 0 0 20 0 0 0 0 0
IJA 2 1 36 1 70 0 0 0 0 0
LST 0 0 9 0 20 0 0 0 0 0
RITA 0 67 3 3 47 2 0 0 2 0
JUML
A KUU 101 278 70 34 1579 5 5 3 11 7
67
KIAMBATISHO G
MCHANGANUO WA BAJETI NA FEDHA ZILIZOPOKELEWA ZA MIRADI YA MAENDELEO KUANZIA
JULAI, 2021 HADI MACHI 2022
Fungu
Bajeti iliyoidhinishwa kwa Mwaka wa Fedha
2021/2022 Fedha zilizopokelewa hadi Machi, 2022
Miradi ya Maendeleo Jumla Miradi ya Maendeleo Jumla Ndani Nje Ndani Nje
16-Ofisi ya
Mwanasheria
Mkuu wa Serikali 1,000,000,000 – 1,000,000,000 – – –
35-Ofisi ya Taifa
ya Mashtaka 3,000,000,000 993,616,000 3,993,616,000 214,155,912.00 84,000,000.00 298,155,912.00
40-Mfuko wa
Mahakama 39,100,000,000 1,090,000,000 40,190,000,000 21,492,475,322.90 23,133,893,261.54 44,626,368,584.44
41-Wizara ya
Katiba na Sheria 1,000,000,000 6,358,598,000 7,358,598,000 429,125,000.00 4,002,354,217.00 4,431,479,217.00
55-Tume ya Haki
za Binadamu na
Utawala Bora
- 373,616,000 373,616,000 – 260,079,091.00 260,079,091.00
Jumla 44,100,000,000 8,815,830,000 52,915,830,000 22,135,756,234.90 27,480,326,569.54 49,616,082,804.44
68
KIAMBATISHO H
MCHANGANUO WA BAJETI ILIYOIDHINISHWA NA KIASI CHA FEDHA ZILIZOPOKELEWA NA
WIZARA NA TAASISI HADI MACHI, 2022
Ndani Nje Ndani Nje
12-Tume ya Utumishi
wa Mahakama 420,191,000.00 2,700,000,000.00 – – 3,120,191,000.00 297,394,730.26 1,925,392,500.00 – – 2,222,787,230.26
16-Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa
Serikali
2,650,210,000.00 5,022,981,000.00 1,000,000,000.00 – 8,673,191,000.00 1,933,307,000.00 3,324,786,212.44 – – 5,258,093,212.44
19-Ofisi ya Wakili
Mkuu wa Serikali 2,658,329,000.00 9,473,018,000.00 – – 12,131,347,000.00 1,410,702,307.65 7,205,068,823.98 – – 8,615,771,131.63
35-Ofisi ya Taifa ya
Mashtaka 9,199,868,000.00 12,068,944,000.00 3,000,000,000.00 993,616,000.00 25,262,428,000.00 7,446,962,412.20 15,568,101,031.00 214,155,912.00 84,000,000.00 23,313,219,355.20
40-Mfuko wa
Mahakama 55,264,477,000.00 57,774,382,000.00 39,100,000,000.00 1,090,000,000.00 153,228,859,000.00 45,246,273,055.13 43,754,226,949.97 21,492,475,322.90 23,133,893,261.54 133,626,868,589.54
41-Wizara ya Katiba
na Sheria 6,089,479,000.00 5,865,271,000.00 1,000,000,000.00 6,358,598,000.00 19,313,348,000.00 4,491,024,764.03 4,875,315,587.41 429,125,000.00 4,002,354,217.00 13,797,819,568.44
55-Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala
Bora
2,495,556,000.00 3,850,280,000.00 – 373,616,000.00 6,719,452,000.00 1,762,074,968.00 2,829,482,951.00 – 260,079,091.00 4,851,637,010.00
59-Tume ya
Kurekebisha Sheria 820,920,000.00 2,424,009,000.00 – – 3,244,929,000.00 542,226,000.00 1,887,137,774.79 – – 2,429,363,774.79
Jumla 79,599,030,000.00 99,178,885,000.00 44,100,000,000.00 8,815,830,000.00 231,693,745,000.00 63,129,965,237.27 81,369,511,830.59 22,135,756,234.90 27,480,326,569.54 194,115,559,872.30
MCHANGANUO WA BAJETI ILIYOIDHINISHWA NA KIASI CHA FEDHA ZILIZOPOKELEWA NA WIZARA NA TAASISI HADI MACHI, 2022
Miradi ya Maendeleo Mishahara Matumizi Mengineyo Fungu
Bajeti iliyoidhinishwa kwa Mwaka 2021/2022
Jumla
Fedha zilizopokelewa hadi Machi, 2022
Mishahara Matumizi Mengineyo Miradi ya Maendeleo Jumla
