TUENDELEE KUIMARISHA UPENDO, UMOJA NA MSHIKAMANO NDANI YA CCM: BASHUNGWA

Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Ndugu Innocent Bashungwa ametoa wito kwa Wanachama wa Chama cha Mapinduzi kuendelea kuimarisha Upendo, Umoja na Mshikamano ndani ya Chama kwa kuanzia ngazi ya Shina.

Bashungwa ametoa wito huo leo tarehe 27 Aprili, 2022 katika Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Shina na Wajumbe wanne wa Kamati ya Shina namba 14 (Maya) Tawi la la Ahakishaka Kata Nyabiyonza, wilaya Wilaya Karagwe, Mkoani Kagera.“Chama Cha Mapinduzi kinaongea kwa vitendo zaidi kuliko maneno katika jitihada za kutekeleza Ilani ya Chama, hiyo ndiyo kiu ya Watanzania ambayo inadhihirishwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anavyopambana kuleta Maendeleo Kwa Watanzania” amesema Bashungwa


Bashungwa ametoa wito kwa Wanachama wa CCM kuendelea kusemea kazi nzuri inayofanywa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kupitia miradi ya maendeleo inayoendelea kuletwa katika maeneo yao.Katika uchaguzi huo, Mwenyekiti wa Shina Ndugu Modest Ntele ameibuka kidedea kwa ushindi wa kura 36 kati ya kura 48, Katibu wa Shina Januaria Mwesiga na wajumbe wa Kamati ya Shina ambao ni Evalista Fideli, Shelia Mujebe na Godfrey Kamafa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *