WILAYA YA SONGWE YAJIPANGA UPYA KUINGIA AWAMU YA PILI YA CHANJO YA POLIO

Taifa likiwa linasherehekea miaka 58 ya Muungano wa Tanzania leo Aprili 26,2022, Mkuu wa Wilaya ya Songwe Simon SIMALENGA @official_simalenga ametumia sikukuu hiyo kuendesha Kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi ya Wilaya (Primary Health Commitee) ili kufanya tathmini ya kwanza ya Chanjo ya Polio ambayo ilihusisha mikoa ya Songwe, Ruvuma, Njombe na Mbeya ambapo Halmashauri ya Wilaya Songwe iliibuka ya kwanza kwa kuvuka lengo la chanjo hiyo kwa kufikia %156. Pia kikao hiki kilijadili mikakati ya kuingia awamu ya pili ya campaign ya uchanjaji wa watoto kuanzia miezi 0 hadi miaka 5 zoezi ambalo litafanyika nchi nzima kuanzia Aprili 28,2022. Kikao hicho kilihusisha viongozi kutoka kwenye makundi mbalimbali ikiwemo Dini, Wazee wa Mila, Wanasiasa, Watumishi wa Sekta ya Afya na Idara za Halmashauri hiyo

Wengine pichani Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Mzee Abraham Sambila, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Ndugu Abdulkadir, kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya Bi. Lydia Kyumana na
Mwakilishi wa Wizara ya Afya Bi. Asteria Shirima

“Wilaya ya Songwe tumedhamiria kutoa Hamasa kwa Wananchi wetu ili watoto wote wapate chanjo dhidi ya Ugonjwa hatari wa Polio”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *