Na Regina Cheleso
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassani amesema Shirika la umoja wa
mataifa la elimu, sayansi na utamaduni {UNESCO} wametangaza Siku ya Wafanyabiashara {Sabasaba}
kuwa sikukuu ya Kiswahili Duniani kwa lengo la kueneza lugha ya Kiswahili.

Rais Samia ameyasema hayo alipozungumza na watanzania waishio Wishingston DC, Marekani amesema kila ifikapo tarehe 7 mwezi 7 Dunia nzima itasherehekea Siku ya Kiswahili Duniani.
Mhe.Rais Samia amesema UNESCO wamefanya jambo zuri la kutafuta namna nyingine ya kueneza
Kiswahili Duniani na amewaomba watanzania wote kuwa mstari wa mbele kusherehekea sikukuu hiyo
ya Kiswahili Duniani.
“Tumefanya juhudi za kukuza Kiswahili na ulimwengu unatupokea vizuri kwamba UNESCO sasa
wametangaza sikukuu ya sabasaba kuwa sikukuu ya Kiswahili ili kueneza lugha ya Kiswahili kwahiyo kila
ifikapo sabasaba Dunia nzima itasherehekea sikukuu ya Kiswahili”
