TARATIBU ZA MAZISHI YA ALIYEKUWA MBUNGE
WA VITI MAALUM MKOA WA RUKWA, MHE. IRENE ALEX NYAMKAMA

Kikao cha pamoja baina ya Tume ya Utumishi wa Bunge na Kamati ya Uongozi
ya Bunge kimefanyika na kukubaliana kuwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa
Viti Maalum Mkoa wa Rukwa, Marehemu Irene Alex Ndyamkama utaletwa
Bungeni Jijini Dodoma siku ya Jumatano tarehe 27 Aprili 2022 kwa ajili ya Ibada
Maalum na Waheshimiwa Wabunge kutoa heshima zao za mwisho.

Uamuzi huo umefikiwa baada ya Uongozi wa Bunge kushauriana na
kukubaliana na familia.
Baada ya Waheshimiwa Wabunge kutoa heshima zao za mwisho, mwili wa
wa marehemu utapelekwa Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa ajili ya
kuhifadhiwa.

Siku ya Alhamisi tarehe 28 Aprili 2022 utasafirishwa kuelekea
Sumbawanga, Mkoani Rukwa ambapo kutakuwa na shughuli ya kuaga mwili
wa marehemu kwa utaratibu utakaoandaliwa na uongozi wa Serikali na
Chama cha Mapinduzi Mkoani hapo.

Mheshimiwa Irene Alex Ndyamkama aliyefariki siku ya Jumapili tarehe 24 Aprili
2022 katika Hospitali ya Tumbi Mkoani Pwani anatarajiwa kuzikwa tarehe 29
Aprili 2022 Mpanda, Mkoani Katavi.
Ofisi ya Bunge inaendelea kuratibu taratibu za mazishi kwa kushirikiana na
familia ya Marehemu, taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema peponi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *