Na Regina Cheleso
Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Dkt. Tulia Acksoni ameahirishaVikao vya Bunge
kutokana na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Rukwa Mhe. Irene Alex Ndyamukama katika hospitali ya Tumbi Kibaha, Mkoani Pwani.
Hayo yamejiri Leo April 25, 2022 Bungeni Jijini Dodoma ambapo Spika amehairisha vikao vya
Bunge ili kuomboleza kifo cha Mbunge mwenzao.
Mhe. Spika amesema Ndyamkama aliugua ghafla akiwa safarini kuelekea Dar es salaam na akalazimika
kupelekwa Hospitalini kwaajili ya kupewa matibabu ya haraka ndipo umauti ulipomfika
“Waheshimiwa wabunge kwa mujibu wa kanuni na utaratibu wetu tunapofiwa na Mbunge mwenzetu
wakati wa mikutano ya Bunge siku ya kazi kunakuwa hakuna kikao cha Bunge ili kupata Fursa ya
kuombeleza msiba na kujiandaa kupokea mwili wa Mbunge mwenzetu”
Spika Dkt. Tulia amesema kufuatia msiba huo taarifa za awali ni kwamba mwili wa marehemu utapelekwa
Bungeni siku ya Jumatano April 27, 2022 kwaajili ya kuagwa na mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya
Ijumaa April 29, 2022 Mkoani Katavi.


