JOHN BOCCO AWATAKA WANASIMBA KUTOKUINAMISHA VICHWA CHINI

Na Emmanuel Charles

Nahodha wa Timu ya Simba Sc John Bocco amesema hawana sababu ya kuinamisha Vichwa chini baada ya kutolewa kwenye Michuano ya Kimataifa dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini

Kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram John Bocco ameeleza kuwa pamoja na kwamba hawajafikia malengo lakini wanapaswa kuinua vichwa juu na kusonga mbele

“Haikuwa rahisi kufika hapa tulipoishia ilihitaji nguvu pamoja na umoja🦁hatukufikia malengo kama yalivyokuwa ila hatuna sababu yakuweka vichwa chini bali tuinue vichwa vyetu juu na kusonga mbele,🦁tunaamini katika kutimiza malengo yetu bila kujali tunaanguka na kusimama marangapi, kwa pamoja twendeni tukaumalize kwa nguvu zaidi msimu kwa mashindano yaliobaki.Pongezi nyingi sana ziwaende wachezaji,benchi la ufundi,viongozi wetu, Wenyekiti wetu wote wawili pamoja na C.E.O wetu @bvrbvra kwa juhudi kubwa iliyofanyika @moodewji tunashukuru sana🙏🏿 hujawahi kutuacha peke yetu ukaribu wako umekua nguvu siku zote kwa wachezaji wako. Shukrani nyingi sana kwa mashabiki wetu inueni vichwa vyenu juu kabisa na mjivunie mafanikio ya club yenu mmekua chachu kubwa kwenye mafanikio yote kwa vipindi vyote,naamini nyie ni moja ya mashabiki bora kabisa kwa sasa ndani ya Afrika mlijitambulisha wenyewe na timu yenu ikawatambulisha pia kuweni wenye fahari kuwa mashabiki wa SIMBA.. twendeni tukamalize msimu kwa nguvu na umoja💪🏿 Nguvu moja🦁”

Simba walitolewa kwenye Michuano hiyo kwa Changamoto ya Mikwaju ya Penati 4-3 Ikiwa ni Baada ya Dakika 90 kumalizika kwa Simba kufungwa Bao 1-0 huku faida ya Goli moja katika mchezo wa Nyumbani ikiwafanya kuwa mzani sawa kwa 1-1

Simba inarejea Nchini kujiandaa na Mchezo wa Watani wa Jadi katika Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo watakuwa wageni wa Yanga April 30, 2022 katika Dimba la Benjamin Mkapa, Jijini Dar es salaam Majira ya 11:00 Jioni

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *