MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI UCHAGUZI WA CCM KIGOMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM) Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amewaasa wananchi wa Kijiji
cha Kasumo na Mkoa wa Kigoma kwa ujumla kutumia fursa za miradi
inayopelekwa na serikali katika mkoa huo kikamilifu ili kujiletea
maendeleo.
Makamu wa Rais amesema hayo wakati akizungumza na wananchi wa
mkoa wa Kigoma katika Kijiji cha Kasumo wilaya ya Buhigwe mara
baada ya kumaliza zoezi la upigaji kura katika uchaguzi wa mwenyekiti
na wajumbe wa CCM wa shina namba 5 kitongoji cha Kihanga.
Amesema serikali inatekeleza miradi mbalimbali katika mkoa huo
ikiwemo madaraja, barabara na ile ya elimu na kuwaasa wazazi
kuhakikisha wanawapeleka watoto wao kupata elimu inayotolewa bila
malipo na serikali.
Aidha amewapongeza wananchi wa Buhigwe kwa kukubali kutoa eneo la
hekari 149.9 kwaajili ya ujenzi wa Chuo cha Tehama kinachotarajiwa
kujengwa katika Kijiji cha songambele mkoani Kigoma. Makamu wa
Rais amesema serikali itaendelea kutatua changamoto mbalimbali
zinazowakabili wananchi wa mkoa huo katika masuala ya miundombinu
pamoja na mawasiliano.
Katika hatua nyingine Makamu wa Rais amewaasa viongozi wa shina
namba 5 wa kitongoji cha kihanga kuongoza kwa weledi ili kuimarisha
chama katika ngazi hiyo. Amesema viongozi hao wa CCM wanapaswa
kufanya vikao mara kwa mara ili kutatua changamoto mbalimbali
ikiwemo migogoro ya wananchi katika maeneo yao. Amesema ni
muhimu viongozi wa CCM kuwa mstari wa mbele katika kuimarisha
umoja, upendo na ushirikiano katika jamii ikiwemo kuhamasisha uanglizi
wa kila mmoja utakaoondoa uhalifu na matendo ya ukatili. Pia Makamu
wa Rais amewahimiza wanachama wa Chama Cha Mapinduzi
kuhakikisha wanalipa ada za uanachama zitakazorahisha uendeshaji wa Chama hicho

MATUKIO KATIKA PICHA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM) Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akipiga kura katika uchaguzi wa
mwenyekiti na wajumbe wa CCM wa shina namba 5 kitongoji cha
Kihanga Kijiji cha Kasumo Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM) Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizungumza na wananchi wa
Buhigwe mara baada ya kumaliza zoezi la uchaguzi wa mwenyekiti na
wajumbe wa CCM wa shina namba 5 kitongoji cha Kihanga Kijiji cha
Kasumo Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM) Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akisikiliza sera za wagombea wa
nafasi ya mwenyekiti wa CCM wa shina namba 5 kitongoji cha Kihanga
Kijiji cha Kasumo Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma kabla ya zoezi la
upigaji kura katika uchaguzi huo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *