Timu ya Mpira wa Miguu kutoka Jijini Dodoma-Dodoma Jiji Fc imefanikiwa kuicharaza Timu ya Mbeya City Bao 2-1 Kwenye Mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara
Mchezo huo umepigwa katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma Majira ya Saa Tatu za Usiku, huku ikiwa ni mara ya kwanza kwa Timu hiyo kucheza ndani ya Huo muda tangu kufungwa kwa Taa uwanjani hapo
Katika Mchezo huo Dodoma Jiji walianza kupata bao la Mapema kabisa Dakika ya kwanza(02) kupitia kwa Mchezaji mahiri Augostino Nsata Kipindi cha kwanza cha Mchezo
Licha ya Timu ya Mbeya City kuonesha upinzani na kutafuta bao la kusawazisha lakini mambo yakazidi kuwa magumu kwao baada ya Mchezaji Seif Abdallah Karihe kuifungia Dodoma Jiji Fc Bao la Pili Dakika ya 25 ya mchezo.
Mbeya City nao waliendelea kupigana kutafuta matokeo ndipo Dakika ya 41 wakafanikiwa kupata Bao la 01 kupitia kwa mchezaji Madeleke Lifa
Kipindi cha pili kila Timu iliendelea kuonesha upinzani kwa mwenzake huku Mbeya City wakihitaji bao la kusawazisha, na Dodoma Jiji wakilinda au kuongeza ili kuondoka na alama 3
Hatimaye Dakika 90 zikaweza kumalizika na Dodoma Jiji Fc kufanikiwa kuondoka na alama tatu kwa matokeo ya Ushindi wa 2-1
Kwa Matokeo hayo sasa Dodoma Jiji Fc wanapaa hadi Nafasi ya 10 kwenye Msimamo wa Ligi wakiwa wamefikisha Alama 24, michezo 21.Kabla ya hapo walikuwa nafasi ya 14 na Alama 21.
Kwa upande wao Mbeya City FC Wanasalia nafasi ya 7 wakiwa wamecheza michezo 20 wakikusanya Alama 25.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA






BAADHI YA MASHABIKI WALIOJITOKEZA WAKIWA WANAFUATILIA MCHEZO





