COSTECH YAJA NA MKAKATI MPYA WA MAWASILIANO.

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imeandaa Mkakati mpya wa Mawasiliano lengo likiwa ni kuchakata na kusambaza taarifa sahihi za Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kwa wadau wote  muhimu nchini huku COSTECH ikitoa rai kwa wadau na watumiaji wa taarifa za utafiti na ubunifu kutumia taarifa sahihi katika kupanga mipango ya maendeleo na kufanya mamuzi kwa kuzingatia taarifa  kutoka vyanzo sahihi kwa maendeleo endelevu. 

Hayo yalibainika wakati wa warsha uandaaji wa Mwongozo wa Utekelezaji Mkakati wa Mawasiliano, iliyofanyika kuanzia tarehe 19 –  23 Aprili 2022 na katika ukumbi Kituo cha Hisabati, uliopo Chuo cha Ualimu, Morogoro (MOTCO).

 Meneja Utunzaji Nyaraka na Machapisho kutoka COSTECH, Dkt. Bunini Manyilizu anafafanua kuwa katika warsha hiyo, kikosi kazi kilijadili Mwongozo huo na kuja na rasimu itakayohusianisha na Mpango wa Mawasaliano ambao umeandaliwa kwa kipindi cha miaka mitatu na inatarajiwa kutumika kuanzia mwaka 2023 -2026.

Dkt.Manyilizu amewataka wananchi na wadau mbalimbali wa mawasiliano kufuatilia taarifa za kielektroniki katika vyanzo vya kisayansi na kiteknolojia vinavotambulika.

Afisa Uhusiano kutoka COSTECH Bw. Faisal Abdul anafafanua zaidi. “Kupitia muongozo huu Tume itaongeza tija ya kujitangaza kwa kuwa karibu wadau muhimu kama vyombo vya habari ili kusaidia kufikia lengo na utekelezaji wa jukumu la taasisi katika kuhifadhi, kuchakata na kusambaza taarifa za Sayansi Teknolojia na Ubunifu nchini, alisema Bw. Abdul. 

Naye mratibu wa warsha hiyo Bi. Minza Charles alisema kuwa amejifunza mengi kupitia warsha hii na kupata uzoefu kutoka taasisi nyingine hapa nchini.

Washiriki wa Warsha ya uandaaji wa Mwongozo wa Utekelezaji Mkakati wa Mawasiliano uliofanyika kuanzia tarehe 19 – 23 aprili katika ukumbi wa Kituo cha Hisabati, uliopo Chuo cha Ualimu, Morogoro (MOTCO).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *