ZITTO KABWE AOMBE RADHI AMEIKOSEA FAMILIA YA HAYATI MAGUFULI; MBUNGE LUSINDE

Na Regina Cheleso

Mbunge wa jimbo la Mvumi Mh Livingstone Joseph Lusinde amemwomba kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe kuiomba msamaha familia ya Aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Magufuli na watanzania kwa ujumla kwa kumsema vibaya Hayati huyo
Mbunge Lusinde ameyasema hayo leo april 22/2022 Bungeni Jijini Dodoma Wakati akichangia Hoja ya Bajeti ya Makadrio ya Mapato na Matumizi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Lusinde amesema kuwa kauli ya zitto ya kuwataka wanaompenda magufuli wakazikwe nae amewakosea watanzania na pia familia ya Hayati
Amesema nchi ili iendeleze utawala bora viongozi wote waliotangulia mbele za haki inatakiwa kushirikiana nao ikiwemo magufuri amefanya kazi kubwa sana na amemwomba Mh zitto kuchunga kauli yake na kumheshimu Hayati magufuri.
“Nataka niseme Hayati Magufuli aheshimiwe kwani katika suala la kufiwa ni suala kubwa sana suala la magufuli kusemwa vibaya mimi sitakaa kimya Zitto anataka tunaye mpenda magufuli tuzikwe nae,anatulazimisha sisi tumseme vibaya Magufuri hatuwezi aiombe msamaha familia ya magufuri na watanzania wote”
Mh Lusinde amesema kuwa dini inakataza pia kumsema vibaya marehemu na kueleza angemsema pale ambapo alikuwepo bado akiwa hai hivyo kumsema akiwa amekufa sio vizuri kwa ndugu jamaa na marafiki, inampasa akaiombe familia msamaha na watanzania wote kwa kosa alilolifanya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *