NAIBU WAZIRI MAVUNDE AAGIZA CHAMA CHA WAKULIMA WA ZABIBU KUWALIPA WAKULIMA FEDHA ZAO

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Anthony Mavunde amekiagiza Chama cha Msingi cha Wakulima wa Zabibu (UWAZAMAM), kuhakikisha wanawalipa wakulima fedha wanazodai chama hicho bila ya kuwaathiriwa na taratibu za kitaasisi kati ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo TADB na uongozi wa chama hicho.

Mhe. Mavunde ametoa maelekezo hayo Jijini Dodoma baada ya kikao chake na wakulima wa zabibu, uongozi wa UWAZAMAM pamoja na Benki ya Maendeleo ya Kilimo TADB.

Amesema washirikiane na Benki ya Maendeleo ya Kilimo TADB kwa kuhakikisha kuwa wakulima wanapata fedha zao kwa utarabu wa kukusanya fedha moja kwa moja mara mkulima anapouza mvinyo ghafi kwani utarejesha matumaini ya wakulima na Benki haitapata hasara.

Pia aliwataka TADB kutoweka masharti magumu katika kuwawezesha wakulima kwani kutapeleke wakulima kutokopesheka.

Aidha Mhe. Mavunde ameipongeza TADB kwa kutambua hati za kimila kama dhamana za mikopo jambo ambalo amelitaja kama nia ya dhati ya kuwainua wakulima na sekta ya Kilimo kwa ujumla.

Aidha Mhe. Mavunde ameendelea kuwatia moyo wakulima wa zabibu kwa kuwahikishia kuwa Wizara iko bega kwa bega katika kuunga mkono juhudi zao na kuwakumbusha kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ni miongoni mwa viongozi wanaotaka kilimo cha zabibu kikue na wakulima waondokane na umasikini.

” Tanzania imebarikiwa; Dodoma ni kati ya maeneo machache duniani yanayovuna zabibu mara mbili kwa mwaka hivyo, hakuna sababu ya wakulima wetu kuendelea kuwa masikini” Amesema Mhe. Mavunde.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika cha UWAZAMAM Bw. Daud Nghawas, amemshukuru Mhe. Mavunde kwa kusikiliza malalamiko ya wakulima na kutafuta ufumbuzi utakaopelekea wakulima kupata fedha zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *