NAIBU KATIBU MKUU DKT. GRACE ATOA MAAGIZO HALMASHAURI YA MUSOMA UKAMILISHAJI WA MIUNDOMBINU YA AFYA

OR-TAMISEMI

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya Dkt. Grace Magembe ameelekeza Uongozi wa Halmashauri ya Musoma kuhakikisha wanakamikisha ujenzi wa kituo cha Afya Makojo kilichopokea Fedha tangu mwezi September, mwaka 2021 ambacho hadi leo hakijaisha.


Aidha, ameelekeza Halmashauri kuhakikisha wanashirikisha jamii katika ujenzi wa miundombinu ya Afya katika Halmashauri yao ili ku8ngeza uwazi na uwajibikaji wa pamoja.

Dkt. Grace ametoa maelekezo hayo mapema jana Tarehe 21.04.2022 wakati wa ziara yake kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Musoma na Manispaa ya Musoma wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa vituo vya kutolea huduma sambamba na upatikanaji wa huduma bora za Afya kwa wananchi.

Amesema nimefanya ukaguzi wa ujenzi kituo cha afya Makojo, Halmashauri ya Wilaya ya Musoma hauridhishi, natoa wiki mbili kazi zote ziwe zimekwisha, kinyume na hapo Mhandisi na Mganga Mkuu wa Wilaya tutawachukulia hatua kali.


‘Utekelezaji wa ujenzi hauridhishi, usimamizi wa Mhandisi kutoka Halmashauri sio mzuri, ushiriki wa wananchi ni uko chini sana, naelekeza kasi ya ujenzi iongezwe, mhandisi asimamie mradi badala ya kuwaachia kamati peke yao ambao si wataalamu na hivyo kusababisha maamuzi kutofanyika kwa wakati au kufanyika kwa makosa na pia Wananchi wamenieleza kuna ukiukwaji wa taratibu katika manunuzi ya vifaa, hili tutalichunguza.

Dkt. Grace pia alikagua ujenzi wa jengo la wagonjwa wa dharura Hospitali ya Wilaya ya Suguti. Ujenzi huo hadi sasa uko takribani asilimia 30. Wakati wa ukaguzi kulijitokeza mapungufu machache ya kiufundi na hivyo alitoa maagizo Mhandisi kuongeza usimamizi na kasi ya ujenzi huku wakizingatia ubora.

Katika kituo cha Afya Lwamrimi kilichopo Manispaa ya Musoma, Dr Grace amepongeza kazi nzuri iliyofanyika, ushirikiano mkubwa kati watendaji na usimamizi mzuri wa Mwenyekiti wa Halmashauri na baraza lake.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa Dr. Juma Mfanga alisema Manispaa hiyo ya Musoma ni kati ya Halmashauri zinazofanya vizuri katika utekelezaji wa miradi. Walipata fedha milioni 250 mwezi Desemba 2021, wamemaliza ujenzi wa jengo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *