Serikali ina matarajio makubwa ya utekelezaji wa Miradi ya Kilimo cha
Umwagiliaji kutokana na ongezeko kubwa la Bajeti ya fedha za miradi ya
Maendeleo kwa Mwaka wa fedha 2022 – 2023, hatua hii ya Serikali ina lenga
kuongeza uzalishaji wa Mazao ya chakula na Biashara kutokana na kilimo cha
Umwagiliaji.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw.
REYMOND MNDOLWA alipokuwa akizungumza na watumishi wa Tume ya Taifa
ya Umwagiliaji Makao Makuu jijini Dodoma.
Kufuatia hatua hiyo ya Serikali kuongeza kiasi hicho cha fedha Shillingi Bilioni
146.5 Katika Sekta ya Kilimo cha Umwagiliaji Bw. Mndolwa ametumia fursa hiyo
kuwaasa watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kupendana kushirikiana,
kufanyakazi kwa pamoja (time work) kwa kuzingatia weledi katika maeneo yao ya
kazi.
Amesisitiza kuwa suala la kupendana na kuheshimiana katika Utumishi
linaongeza ufanisi katika utendaji kazi na kuleta amani.
“Tuheshimu kila mmoja aliyepo hapa, wote thamani yetu ni mmoja kwasababu
wote tunaitumikia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.” Alisisitiza
Bw. Mndolwa ameongeza kwa kusema kuwa watumishi wanao wajibu wa
kuhakikisha wanatunza mali zote za Tume akitolea mfano magari na Mitambo
inayotumika katika shughuli za ujenzi wa miradi ya Umwagiliaji.
“Nataka kila mtu ahakikishe anatunza mali ile aliyokuwa nayo” ili
iwezekutusaidia kwa muda mrefu zaidi, itunze ione ni mali yako wewe, usione
ni mali ya umma au serikali, sababu serikali ni mimi na wewe “kwahiyo naomba
wale wanaoendesha vyombo vya Mamlaka na wale wanaovipanda wavitunze.”
Kikao hicho cha Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ni cha kwanza
mara baada ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan mapema
Mwezi huu.
PICHA:
Bw, Reymond Mndolwa.
Mkurugenzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.

Baadhi ya Watumishi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wakimsikiliza kwa makini
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw, Reymond Mndolwa
