“MASKINI WANAKOSA AJIRA, MTANDAO UNAWAKWEPA”MBUNGE LUSINDE

Na Regina Cheleso

Mbunge wa jimbo la Mvumi Mh Livingstone Joseph Lusinde ameiomba serikali itoe ajira Kiwilaya au kimajimbo na sio kimtanda huku akisema mtandao unakwepa watu maskini “
Mh Lusinde ameyasema hayo leo april 22/ 2022 Bungeni jijini Dodoma Wakati akichangia Bajeti ya Makadrio ya mapato na Matumizi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Amesema Ajira zinazotolewa kwa njia ya mtandao zinakwepa wale ambao nimaskini na kuiomba serikali itoe ajira kimajimbo au kiwilaya.
Amesisitiza kuwa, endapo serikali itatoa ajira kwa njia ya kiwilaya au kimajimbo itasadia wabunge kujua namna ya ajira hizo kuwagawia watu wao bila kupendelea maskini wala tajili lakini ikitumia mtandao itakwepa maskini”
“Mgao wa ajira kwa njia ya mtandao unakwepa maskini hili la ajira tukisema tuliombe online kuna vijana wa familia za maskini hawatakaa wapate,mimi nashauri Mh Mwenyekiti kwasabababu taifa hili tunafahamiana hizi ajira zitolewe kwa njia ya majimbo au kiwilaya itasaidia sana”
Pia amesema kuwa kipaumbele cha ajira kitolewe kwa watu wanaojitolea kwenye idala mbalambali wengine wana miaka mitano kumi kumi na tano wajitolea basi ajira hizo zipewe kipaumbele kwa wale wanaojitolea
“Watu wamejitolea mda mlefu sana na wengine wamekata hadi tamaa wengine naomba serikali itoe kipaumbele kwa watu hao ili wapate ajira “

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *