Na Mwandishi wetu,
Mbunge wa Jimbo la Ubungo Prof. Kitila Mkumbo ameitaka Serikali kutoa tamko la kutowasumbua Bodaboda kutokana na kundi hilo kutoa ajira nyingi hasa kwa kundi la vijana.
Akichangia bungeni leo jijini Dodoma Prof. Kitila amesema matamko yanayotolewa hivi sasa ya kuzuia pikipiki maarufu kama Bodaboda kwenda mjini yanakwenda kinyume na kipaumbele cha sita cha Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
“Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Innocent Bashungwa atoe tamko rasmi la kwamba bodaboda wasisumbuliwe tena, ilani ya CCM kipaumbele cha 6 ni kuajiri watu milioni 8 kutoka sekta rasmi na isiyo rasmi, bodaboda ni miongoni mwao tunapowasumbua hiyo idadi tutaitoa wapi?” Prof. Kitila Mkumbo.
Prof. Kitila Mkumbo amesema ajira nyingi zinatokana na biabida na kutolea mfano Jimbo la Ubungo ambalo lina Kata 8 na lina bodaboda zaidi ya 4891, na kwa Kata ya Ubungo pekee yake ina bodaboda 438 kati yao wanne wana Shahada ya Uzamili, bodaboda 21 wana Shahada ya kwanza na wanaosalia wengi wao wana elimu ya kidato cha nne.
Prof. Kitila Mkumbo amesema kundi hilo ni muhimu kwa Uchumi wa Dar es Salaam na kushauri wakuu wa mikoa wapewe maelekezo kuhusu kundi hilo.
“Sisi Dar es Salaam tulitoa ahadi kwamba bodaboda hawatasumbuliwa tena kwenda katikati ya jiji, tunaitaka Serikali itoe tamko rasmi na la mwisho kuhusu bodaboda kutosumbuliwa tena kwa maana hawa bodaboda ndiyo wenye uchumi” Prof. Kitila Mkumbo
Awali katika mchango wake Prof. Kitila Mkumbo amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuitangaza Tanzania kupitia filamu ya Royal Tour ambayo itasaidia kwa kiwango kikubwa kuinua uchumi wa Tanzania.
“Mipango yote ili iweze kutekelezwa kikamilifu inahitaji fedha, moja ya chanzo kikuu cha fedha katika nchi hii ni utalii, nimpongeze Sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa ubunifu wake wa kuja na Royal Tour, wataalamu wa utalii wanasema inaweza kuongeza idadi ya watalii mara 2 au 3” Prof. Kitila Mkumbo.
Kuhusiana na utumishi wa Umma Prof. Mkumbo amesema namna Tanzania inavyopambana kukabiliana na tatizo la uhaba wa watumishi wa umma, ambalo linatatuliwa
