Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi Mhe. Innocent Bashungwa amemsimamisha Kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mvomero Mkoani Morogoro Bw.Hassan Njama Hassan Kuanzia leo Tarehe 20, April 2022 Ili kupisha uchunguzi
Waziri Bashubngwa amechukua Hatua hiyo baada ya Mkurugenzi huyo kushindwa kutekeleza maagizo aliyoyatoa wakati wa Ziara yake ya Kikazi aliyoifanya 10.03.2022 kwenye Halmashauri hiyo.
Wakati wa Ziara hiyo, Bashungwa alibaini upotevu wa Fedha za Miradi na matumizi yasiyo sahihi ya Kiasi cha Shilingi Milioni 281.84 katika ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kumbukumbu ya Moringe Sokoine zilizotolewa kwaajili ya Ujenzi wa bwalo la chakula, Jiko na bweni na kumuagiza Mkurugenzi huyo kuwachukulia hatua za kiutumishi Wakuu wote wa Idara na watumishi waliohusika na ukiukwaji wa taratibu za manunuzi katika mradi huo.
Hadi kufikia leo hii hakuna Mkuu wa Idara yeyote ama Mtumishi aliyechukuliwa Hatua kufuatia agizo hilo.
Aidha, Waziri Bashungwa ameendelea kuwataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuendelea kusimamia Miradi ya Maendeleo kikamilifu na kuchukua hatua za haraka pale wanapobaini ubadhilifu wa fedha za Umma
