WATU SITA WAFA KWENYE AJALI ARUSHA

Watu sita (06) wamefariki dunia na wengine wanne wamejeruhiwa katika ajali baada ya gari aina ya Toyota Noah kugongana na lori aina ya scania katika eneo la ALKATANI kata ya Sepeko tarafa ya Kisongo wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha katika barabara ya Arusha Babati.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo ameseama ajaili hiyo imetokea jana Aprili 19, 2022 majira ya saa nne usiku na kuyataja magari hayo kuwa ni Toyota Noah yenye namba za usajili T.189 DFY likitokea Arusha mjini kwenda Karatu na lori lenye namba za usajili T.250 CAA ambapo lori hilo lilikuwa linatokea makuyuni kwenda Arusha mjini.

ACP Masejo amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva amabapo alishindwa kulimudu gari hilo na kuhamia upande mwingine wa Barabara na kusabisha kugonga gari hilo aina ya toyota Noah hiyo.Kamanda Masejo amesema kuwa Jeshi hilo linamshikilia dereva wa roli aliyesababisha ajali hiyo.

Cc-wasafifm

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *